Uimamu wa Mtu Mwovu

Egypt's Dar Al-Ifta

Uimamu wa Mtu Mwovu

Question

Je, nini hukumu ya uimamu wa mtu mwovu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu.
Uovu katika lugha maana yake ni kutomtii Mwenyezi Mungu, kupotoka kutoka katika dini, na kutoka katika hali ya usawa.
Asili ya Uovu ni kutoka kitu nje ya kitu kingine kwa njia ya mbaya. [Rejea kidahizo: ufuska katika Lisan Al-Arab 10/308, Dar Sader, na Al-Misbah Al-Muniir kwa Al-Fayoumi uk. 473, Al-Maktabah Al-Ilmiyah].
Ufuska unakuwa kwa kutenda dhambi kubwa au kuendeleza dhambi ndogo na wala hauzidi utiifu juu ya makosa [Rejea: Mughni Al-Muhtaj 4/257, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Ama kwa mtu mwovu anayewasalisha watu kama Imamu: inapaswa kujua kwamba swala ni uhusiano kati ya mja na Mola wake, nayo ni ibada tofauti na ibada nyingine, ina masharti na nguzo zake, kama masharti na nguzo zinapatikana basi swala ni sahihi, lakini kama hazipatikani, basi swala si sahihi na aliyeswali anatakiwa kuswali tena, na siyo miongoni mwa masharti yake au nguzo zake kuwa hana dhambi yoyote ili swala yake iwe sahihi, lakini inatosha kutekeleza nguzo na masharti ili swala iwe sahihi. Hali kadhalika kuhusu Imamu, anayeswali na swala yake ni sahihi kwa nafsi yake, basi ni sahihi kwa wengine, yaani kama swala yake ni sahihi, basi swala yake pamoja na wengine ni sahihi pia, kutokana na hivyo sala nyuma ya Imamu mwenye tabia ya ufuska ni sahihi, nao ni mtazamo wa wengi wa Wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, Imamu Ahmad Ibn Malik, na Imamu Al-Shafii, ingawa Wanavyuoni wote wanachukizwa na hali hii.
Al-Sharnbalali Al-Hanafi alisema katika kitabu cha: [Maraqi Al-Falah, Sharh Noor Al-Idhah Uk. 115, Al-Maktaba Al-Asriyah]: “(Na) Kwa hiyo inachukiza kusali nyuma ya Imamu ambaye ni (mwovu) mwenye elimu kwa ajili ya kutojali kwake mambo ya dini, basi ni ni lazima akosolewe kufautana na Sheria, kwa hivyo hairuhusiwi kuswalisha kama Imamu, na kama haiwezekani kumzuia kuswalisha kama Imamu inaruhusiwa kwenda kuswali sala ya Ijumaa katika msikiti mwingine, kama haiwezekani inaruhusiwa kuswali pamoja naye”.
Sheikh Ad-Dardeer wa Kimalikiy alisema katika kitabu cha: [Al-Sharhul Kabiir Limukhtasar Khalil] katika maneno yake kuhusu masharti ya kuswalisha kwa Imamu [1/326, Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah]: “Rai iliyochaguliwa ni kwamba anayewaswalisha watu kama Imamu hahitaji kuwa sawa kwa maadili yake, na kwa hivyo basi swala ya mwovu ni sahihi kama huo ufuska wake hauhisiani na swala”.
Al-Mawardi alisema katika kitabu cha: [Al-Hawi Al-Kabiir 2/328, Darul Kutub Al-Elmiyah]: “Suala: Shafiy alisema: inachukiza kuswali nyuma ya Imamu ambaye ni mwovu na mwenye kuonesha uzushi, na aliyeswali nyuma yake hahitaji kuirejea swala yake, Al-Mawardi alisema hivyo: na mtazamo huu ni sahihi.
Sheikh Zakaria Al-Answariy Ashafiy alisema katika maelezo ya kitabu cha: [Rawdh Al-Talib 1/219, Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: “(Sura: anatangulia) katika Uimamu (aliye mwadilifu zaidi kuliko mwovu, hata kama mwovu akiwa na maarifa na elimu zaidi ya aliye mwadilifu), kwa sababu mwovu haaminiki (lakini inachukiza) kusala (nyuma ya mwovu) kwa sababu ile ile, ila kusali nyuma yake ni sahihi kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Maimamu wawili kwamba Ibn Umar alikuwa anasali nyuma ya Al-Hajjaj, Al-Shafii alisema: Na mtu huyu (Al-Hajjaj) anatosha kuwa mwovu”.
Ashafiy alichukua dalili kutoka katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W amesema: “Wanaokusalisheni wakisibu basi thawabu ni zenu nyote, nyinyi na wao. Na wakikosea basi thawabu ni zenu na makosa ni yao”.
Na kauli yake: (wakifanya makosa), yaani: wakifanya madhambi, na kauli hii inaruhusu kuwa Imamu mtu mwema na mtu mwovu. [Fath Al-Bari 2/188, Dar Al-Maarifa].
Vile vile Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Bukhari kutoka kwa Ubaidullah Ibn Adiy bin Khiyaar kwamba aliingia kwa Othman Ibn Affaan R.A., huku amehusuriwa (yaani amezungukwa na maadui zake nyumbani kwake) na akasema: Hakika wewe ndiye Imamu wa umma wote, na wewe yamekufika haya tunayoyaona (yaani huku kuzungukwa) na anatusalisha Imamu ambaye ni mtu wa fitina (yaani mkubwa wa fitina) nasi tunaona dhiki na tuna khofu kuingia katika dhambi. Akasema (Othman): Swala ndiyo ibada bora kuliko yote wanayoyatenda kwa watu. Watu wakifanya mazuri nanyi fanyeni mazuri na wakifanya maovu basi jiepusheni na maovu yao.
Imamu Bukhariy ameweka Hadithi hii katika Mlango wa kuwa Imamu mtu wa fitina na mtu wa bidaa, kisha akataja kauli yake Al-Hassan aliposema: basi sali wewe na dhambi ya bidaa yake ni juu yake tu. Kisha akataja hadithi hii, na baadhi ya Wanavyuoni waliichukua hadithi hii kama dalili kwamba inaruhusiwa kuswali nyuma ya Imamu ambaye ni mwovu [Rejea: Fath Al-Bari 2/189].
Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawood na Ad-Daaraqutni kutoka kwa Abu Hurayrah, R.A. alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W alisema: “Jihad ni wajibu kwenu pamoja na kila Amir, akiwa ni mwema au ni mwovu, na swala ni wajibu juu yenu nyuma ya kila Muislamu, akiwa ni mwema au mwovu, hata akifanya madhambi makubwa”, na Hadithi hii ni wazi kuhusu kuruhusiwa kuswali nyuma ya Imamu ambaye ni mwovu.
Na imepokelewa kutoka kwa Ad-Daaraqutni kutoka katika Hadithi ya Abdullah Ibn Omar, R.A.: “Salini nyuma ya anayesema hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na salini mbele anayesema hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu”.
Imepokelewa kutoka kwa Imamu Bukhariy kuwa Abdullah Ibn Omar alikuwa akiswali nyuma ya Al-Hajjaj Ibn Yusuf Athaqafiy, na Abdullah Ibn Masuod R.A aliswali nyuma ya Al-Walid Ibn Uqbah Ibn Abu Muayit ambaye alikuwa anakunywa pombe, na mara moja aliwasalisha Al-Fajiri watu rakaa nne, Othman Ibn Affaan R.A. akamwadhibu. Pia alisema kuwa Sheikh Ibn Taymiyah aliruhusu kuswali nyuma ya maimamu waovu na swala hairudiwi tena. [Al-Fatwa Al-Kubra 2/308, Darul Kutub Al-Ilmiyah].
Ibn Abi Shaybah pia alitaja katika kitabu chake sura ya swala nyuma ya wakuu, na alitaja swala ya Ibn Umar nyuma ya Al-Hajjaj wakati wa kuzingirwa kwa Ibn Al-Zubayr, na swala ya Al-Hassan na Al-Hussein nyuma ya Marwan, alitaja mapokezo mengi kutoka kwa Maulamaa waliotangulia yanayothibitisha usahihi wa swala na kutorudia tena swala kwa mara nyingine.
Baadhi ya Wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Maalik na Imamu Ahmad Ibn Hanbal wamesema kuwa sio sahihi kuswali nyuma ya mwovu.
Sheikh Khalil ibn Ishaq Al-Maliki alisema katika Muhtasari wake [2/22 pamoja na maelezo ya Al-Kharshi, Dar Al-Fikr]: “Imebatilika swala ya mwenye kuswali nyuma ya mwovu”, lakini Wananvyuoni wa madhehebu ya Imamu Malik hawakuupitisha mtazamo huu; Al-Adawi alisema katika kitabu chake Sharhu Ar-Resalah [1/300, Dar al-Fikr]: “Na mtazamo wa Al-Khalil aliosema kuhusu ubatili wa swala nyuma ya mwovu ni mtazamo dhaifu.
Al-Bahoutiy Al-Hanbaliy alisema katika ufafanuzi wa [Muntaha Al-Iradaat 1/272, Alam Al-Kutub]: “Uimamu wa mwovu sio sahihi wakati wote, akiwa ni mwovu kwa itikadi, au vitendo vya haramu, ikiwa alitangaza uovu wake au la, na mwenye kuswali nyuma ya mwovu anatakiwa kuziswali tena swala zake zote”.
Na waliosema kwamba kusali nyuma ya mwovu si sahihi walithibitisha kauli yao kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Maajah kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah, R.A, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alisema: “Mwanamke hamsalishi mwanamume, wala Bedui hamsalishi mhamiaji, wala mwenye uasherati hamsalishi Mwaminifu, isipokuwa atakayenyanyaswa na mtawala ambaye anaogopa upanga wake na mjeledi wake.”
Katika Hadithi hii yupo Al-Walid Ibn Bakir, Abdullah bin Mohammed Al-Adawi, ambaye alituhumiwa na Wakii kuwa ni mwongo, na yupo Ali Ibn Zaid bin Jad'aan, naye ni dhaifu.
Pia wamethibitisha mtazamo wao kwa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ad-Daraqwutniy na Salam Ibn Suleiman, alituambia Umar, kutoka kwa Mohammed Ibn Wasii kutoka kwa Said Ibn Jubair kutoka kwa Ibn Umar amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alisema: “Chagueni wabora wenu kuwa maimau wenu kwani wao ni kiungo baina yenu na Mwenyezi Mungu”.
Ibn Abd Al-Hadi alisema katika kitabu cha: [Tanqiih Al-Tahqiiq 2/468, Adhwaa As-Salaf]: “Hadithi hii ni Munkar, na kama ni sahihi inabebwa juu ya umuhimu, na Salam Ibn Suleiman ndiye ni Abu Abbas Al-Madaini ambaye ni kipofu, alituhumiwa na Abu Hatem, Aqeeli, na Ibn Adiy ... nk. Al-Bayhaqi ameidhoofisha Hadithi hii katika Sunan yake .
Hiyo lazima kuzingatia kuwa hukumu ya uovu haikuwa katika kuacha mamabo amabyo ni wajibu au kufanya mambo yaliyokatazwa, lakini ni lazima kuwa mambo ambayo yaliyoachwa ni wajibu. Wanavyuoni wamekubalina kuwa ni wajibu, au ni wajibu katika akida ya mwenye mchamungu, pia mambo yaliyokatazwa yanakubaliwa kuwa ni haramu, au Hiyo ni haramu kwa akida ya mwenye kuyatenda, kwa kuwa hakuna kukataa mambo yenye shaka, bali inakataliwa mambo yaliyokubaliwa na Wanavyuoni wote. [Rejea: Al-Ashbah wal Nadhair kwa As-Suyuuti uk. 158, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Ibn Hajar Al-Haythami alisema katika kitabu cha: Tuhfatul Muhtaj 3/244, Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi]: “Hairuhusiwi kwa mfuasi wa madhehebu ya Imamu Al-Shafii kucheza Chesi pamoja na mfuasi wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, kwa sababu ni usaidizi wa kufanya dhambi kwa mujibu wa akida ya mfuasi wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, kwani kucheza haramu hakuwi isipokuwa kwa usaidizi wa huyo mfuasi wa madhehebu ya Imamu Ashafiy”.
Kutokana na yaliyotangulia hapo juu: swala ya faradhi au Sunna ni sahihi nyuma ya Imamu ambaye ni mwovu kama walivyosema Wanavyuoni wa umma pamoja na kukubaliana kwao kuwa swala ni sahihi lakini inachukiza, isipokuwa ni bora zaidi kujiepusha na tofauti ya Wanavyuoni.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

  

Share this:

Related Fatwas