Kusafisha Nguo kwa Mvuke

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusafisha Nguo kwa Mvuke

Question

Je, kufua nguo kwa mvuke, yaani (Dry cleaning) kunazitakatisha nguo zenye unajisi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni zake, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu..
Dini ya Uislamu inahimiza sana suala la usafi wa mwili na wa nafsi katika hukumu na kanuni zake zote, kwa mfano sala ambayo ni nguzo ya dini haiwi sahihi ila kwa kuwepo sharti la usafi ambalo lina sehemu mbili: kuwepo usafi, na la pili ni: kuondosha najisi kwenye mwili, nguo, na mahali pa kusalia.
Imamu Muslim amepokea kutoka kwa Abi Malik Al-Asha’riy R.A., kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Usafi ni nusu ya imani”, [Ameipokea Muslim}, na Masahaba watukufu walipomuuliza Mtume S.A.W.: je, anaweza kuwajua na kuwatambua wao kati ya watu wote wa Siku ya Kiyama? Mtume S.A.W., akasema: “Ndio, ninyi mna sura zilizo tofauti na sura za watu wengine wote, na mtanijia hali ya kuwa ni wenye nuru katika mapaji ya nyuso na miguu yenu, kutokana na athari ya udhu”. [Ameipokea Muslim kutoka kwa Abi Hurairah R.A,]. Kuhusu kusafisha nguo, Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: {Na nguo zako uzisafishe}. [AL MUDDATHIR: 4].
Mwenyezi Mungu ametuongoza kuwa maji ya mbingu ni maada iliyoumbwa kwa ajili ya kutaharisha na kusafisha, na anasema: {Na akakuteremshieni maji mawinguni ili kukutahirisheni kwayo}. [AL ANFAAL: 11], na mfano wa maji ya mbingu ni aina zote za maji ya asili yenye umbile safi na chimbuko lake ni maji ya mbingu kama vile: maji ya bahari, mito, chemchem, na visima, na Mwenyezi Mungu anasema: {Na tumeteremsha kutoka mawinguni maji kwa kiasi, na tukayatuliza ardhini, (tukayahifadhi ndani ya ardhi). Na bila shaka sisi ni wenye uweza wa kuyaondoa}. [AL MUMINUN: 18]. Na maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: {na tunayateremsha kutoka mawinguni maji safi (kabisa)}. [AL FURQAAN: 48], yaani: maji yenyewe ni safi, na husafisha vitu vingine. Imamu Abu Bakr Ibn Al-Arabiy katika kitabu cha [Ahkaam Al-Quran: 3/436, Ch. ya dar Al-Kutub Al-Ilimiyah] anasema: “wanazuoni wote walikubaliana kilugha na kisheria kuwa lafudhi (safi kabisa) linaambatana na maji tu, hata ikiwa vitu vingine vya majimaji ni safi pia, ili kuonyesha kuwa maji yanasafisha vitu vyote”. [Mwisho].
Katika Hadithi tukufu, kutoka kwa Asmaa Bint Abi Bakr RA, alisema: nilimsikia mwanamke anamuuliza Mtume S.A.W.: mwanamke miongoni mwetu anafanya nini kuhusu nguo yake baada ya kumaliza hedhi? je, anaweza kusali kwa nguo hiyo? Akasema: “akiona damu, basi aioshe kwa maji, na kupiga kwa maji asioiona, kisha asali kwayo”. [Ameipokea Abu Dawuud].
Hadithi hii ni dalili ya usahihi wa sala katika nguo yenye najisi kutokana na damu ya hedhi, baada ya kuisafisha kwa kuondoa asili ya unajisi na kuosha athari yake kwa maji, na kupiga kwa maji mahali penye dhana ya kuwepo unajisi kwapo kwa kutumia maji, na hayo yote huonyesha kuwa maji ni mada inayofaa kusafisha nguo.
Lakini wanazuoni wanahitilafiana kuhusu maada nyingine isipokuwa maji katika kusafisha ngu kwa ajili ya kuondosha najisi; wengi wa wanazuoni walielekea katika rai ya kuwa maji ni maada pekee ya kisheria inayotumika kusafishia nguo, na hakuna nyingine. Imamu An-Nawawiy Ash-Shafiy katika kitabu cha: [Al-Majmuu’: 1/ 139-124, Ch. ya Al-Muniriyah] anasema: “Hukumu ya suala hili ni kuwa; usafi kamili na kuondoa najisi hauijuzu isipokuiwa kwa maji safi kabisa, na hii ni kwa mujibu wa madhehebu yetu bila ya hitilafu kati yetu, pia ni kauli ya wengi wa Salaf (wema waliotangulia) na waliofuata, miongoni mwa Masahaba na waliofuata… na tumetaja kuwa kuondoa najisi hakujuzu, kwa mujibu wa kauli yetu na kauli ya wengi wa wanazuoni, isipokuwa kwa maji, kwa hiyo hakujuzu kwa siki wala mada nyingine ya majimaji.
Na miongoni mwa yalivyonukuliwa na: Malik, Muhammad Ibn Al-Hassan, Zufar, Is-Haq Ibn Rahawaih, na haya ni mapokezi sahihi kabisa kutoka kwa Ahmad”. [Mwisho].
Wanaelekeza dalili zao katika Hadithi iliyotajwa na Asmaa kuwa: “suala likiambatana na jambo lenyewe, basi kutekelezwa kunaambatana na jambo hilo, kunalikusanya jingine”. [Hashiyat Al-A’twar Ala sharh Jama’ Al-Jawamii’ na Al-Mahaliy: 1/334, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]; na Mtume wa Mwenyezi Mungu aliamuru kusafishwa nguo kwa ajili ya kuondosha damu ya hedhi kwa kutumia maji, ili sala katika nguo hizi iwe sahihi, na hukumu ya usahihi wa sala au kuivunja kwake hakika ni hukumu ya kisheria kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na Sharia ikiamuru kuuondoa najisi katika nguo kwa kutumia maji, inalazimika kutumia maada iliyoainishwa na Sharia, kwa kuitikia amri.
Ibn Al-Arabiy Al-Malikiy katika kitabu cha [Ahkaam Al-Qu'ran: 3/441-442, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] anasema: “Mwenyezi Mungu alipoeleza maji kuwa safi kabisa, na kufanya hisani kwa kuyateremsha kutoka mawinguni ili kutusafisha kwayo, kuna dalili ya sifa hii ya maji, na akasema kwa Asmaa Bint As-Swiddiq kuhusu damu ya hedhi inapodondokea katika nguo: “Isafishe sana kisha ioshe kwa maji”, kwa hiyo maada nyingine yoyote ya majimaji hailingani na maji kwa sababu mbili: Kwanza: kuondoa faida ya hisani ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Pili: Maada nyingine ya majimaji sio ya kusafishia, na dalili yake ni kuwa: haiondoshi janaba wala najisi.
Baadhi ya wanazuoni wetu na wa Iraqi wanasema kuwa: kila maada ya majimaji ni safi na huondoa najisi… na najisi si kitu dhahiri tu, ambacho huondoshwa kwa maada yoyote iwayo, bali ni hukumu ya kisheria, Mwenye Sharia aliainisha maada maalumu, ambayo ni maji. Kwa hiyo, haiwezi kuambatanishwa maada nyingine isiyokuwa mfano wake …”. [Mwisho].
Maimamu Abu Hanifa, Abu Yusuf, Dawuud Adh-Dhahiriy, na Imamu Ahmad katika mapokezi, na baadhi ya wanazuoni wa Madhehebu ya Malik, kama ilivyonukuliwa na Ibn Al-Arabiy, na Muhammad Ibn Abdur-Rahman Ibn Abi Laila, na Abu Bakr Al-Asamm, nayo ni kauli ya Sheikh Taqiy-Diin Ibn Taimiyah wa madhehebu ya Hanbal, walielekea kuwa: Kuanishwa maji katika Sharia kama maada ya kusafisha hakupingi uwepo wa maada nyingine inayofaa kusafishia, hali ya kuweza kuondosha najisi, mfano wa kila maada ya majimaji iliyo safi. [Taz.: Al-Majmuu’: 1/139-142; Al-Fatawa Al-Kubra; 1/428, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Miongoni mwa dalili ya wenye rai hii ni kuwa: kinachokusudiwa katika suala hili ni kuondoa najisi, na si matumizi ya maji, na dalili yake kuwa; inajuzu kukata sehemu ya unajisi kutoka kwa nguo, au kuichoma moto, na hapo nguo itakuwa tahiri, na kuwa maji ni mada inayofaa kuondoa unajisi ni hukumu ya kisheria sababu yake ni kuondosha, kwa hiyo inashirikiana na kila mada ya majimaji yenye sababu hiyo hiyo. [Hashiyat At-Talwiih Ala At-Tawdiih na As-Saa’d At-Taftazaniy: 2/124, Ch. ya Maktabat Subeih, Masr].
Imamu Ash-Shashiy Al-Hanafiy katika kitabu cha: [Al-Usuul; Uk. 177, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Arabiy] anasema: “kutegemea kauli ya Mtume S.A.W.,: “Isafishe sana kisha ioshe kwa maji” kwa kuthibitisha kuwa siki haiondoshi najisi ni kauli dhaifu; kwa sababu Hadithi hii inawajibisha uoshaji wa damu kwa maji, katika hali ya kuwepo damu mahali fulani, na hapo hakuna hitilafu, lakini hitilafu inapatikana katika usafi wa mahali baada ya kuodosha najisi kwa siki”. [Mwisho].
Al-Jassas katika kitabu cha: [Al-Fusuul: 1/53-54, Ch. ya Wizaarat Al-Awqaaf Al-kuwaitiyah] anasema: “ilivyokuja katika Hadithi hii ni amri ya kuosha damu ya hedhi kwa maji, na damu inapoondoshwa kwa siki au majimaji ya aina nyingine, basi haitabaki damu kutokana na maana ya Hadithi hii, hapo Hadithi hii haiambatani na suala la hitilafu”. [Mwisho].
Imamu Ibn Taimiyah anataja matini ya Sharia na maana yake, ni zile zinazozipa nguvu kauli za usahihi wa kusafisha kwa kutumia maada nyingine isipokuwa maji, amesema katika [Al-Fatawa Al-Kubra: 1/428, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “kauli yake katika Hadithi ya bedui aliyekojoa katika msikiti: “Mwagieni juu ya mkojo wake ndoo ya maji”, hapo aliamuru kuondosha kwa najisi kwa kutumia maji katika jambo maalumu, na hakuamuru hivyo kwa ujumla, yaani haimaanishi kuwa kila najisi lazima isafishwe kwa maji, kwa sababu aliruhusu kuuondosha najisi bila ya maji katika masuala kadhaa, miongoni mwayo; kutumia mawe katika kustanji, na kauli yake katika viatu: “avisugue kwa udongo, kwani udongo ni safi kabisa”, na kauli yake katika upembe wa nguo: “Asafishe kilichokuwa baada yake”, na pia: “Mbwa walikuwa wakitembea na kukojoa katika msikiti wa Mtume S.A.W., na kwa hivyo hawakuwa wakiosha hivyo”, na kauli yake katika paka: “paka ni miongoni mwa wanyama wafugwao kama mapambo kwenu siku zote”, na kwa hivyo kwa kawaida paka hula panya, na wakati huo hapakuwa na mfereji wa maji hata pasemwe kuwa kasafisha kinywa chake, isipokuwa kasafisha kwa mate yake tu.
Na miongoni mwa hayo pia: pombe ikigeuzwa ikawa siki itakuwa safi kwa kauli ya pamoja ya waislamu, kwa hiyo, kauli yenye nguvu juu ya suala hili ni kuwa: najisi ikiondoshwa kwa kutumia maada yo yote iwayo, basi hukumu yake itaondoshwa pia, kwani hukumu hiyo ilikuja kwa sababu ya kuwepo kwa najisi hiyo, itaondoshwa kwa kuondoshwa sababu hiyo. Na haijuzu kutumia vyakula na vinywaji katika kusafishia najisi bila ya haja, kwa sababu hii itakuwa ni kupoteza mali, na pia haijuzi kuvitumia vyakula na vinywaji hivyo katika kustanji. Na wale waliosema: unajisi hauondoshwi ila kwa kutumia maji kwa hoja ya kuwa: ni kiibada, lakini si hivyo, kwa sababu Mwenye Sharia aliamuru kutumiwa maji katika masuala maalum, na kuondosha kwa kutumia vimiminika ambavyo wanafaidika navyo waislamu ni uvunjaji wa sharia, na uondoshaji wake kwa kutumia madaa kama mawe ulikuwa udhuru”. [Mwisho].
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia, twasema kuwa: msingi katika kuondosha najisi ni kutumia maji, na kama ikiwa kuna shida ya kuyapata na kuyatumia, au matumizi ya maji hayo yataharibu nguo, hapo hakuna kosa lolote kwa kuifuata kauli ya kuwa: kusafisha nguo na mfano wake kwa kuondosha najisi ni hukumu ya kisheria sababu yake ni dhahania, yaani: kuondosha ile najisi yenyewe kikamili, na athari yake kwa kiasi kiwezekanavyo.
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: usafishaji kwa njia ya mvuke ambao ni: kazi ya teknolojia ya kisasa ya usafishaji, ambamo ndani yake hutumiwa madaa iitwayo kwa muhtasari wa (perc), pamoja na kutumia mvuke wa maji katika hatua fulani, na huu ni mbadala wa maji, kwa ajili ya kusafisha nguo na vitambaa ambavyo vinaharibika kwa kuvisafisha kwa njia ya maji, au mbinu za kienyeji za kusafisha, na hii ni njia inayofaa kusafisha nguo zenye najisi, na kwa kuangalia kuwa maada zenyewe zinazotumika katika kazi hii ni safi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas