Istilahi ya Saumu ya Wajibu

Egypt's Dar Al-Ifta

Istilahi ya Saumu ya Wajibu

Question

 Je, kuna tofauti baina ya Saumu ya Wajibu na Saumu ya Ramadhani? Kwani nasikia baadhi ya wanazuoni wakizungumzia Saumu ya Wajibu, na siyakuti hayo katika vitabu ambavyo ninavimiliki, na kama ikiwa ipo istilahi kama hiyo; basi dalili yake nini, kama ikiwezekana?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Basi ipo tofauti baina ya Saumu ya Ramadhani ni Saumu ya wajibu; kwani aina ya Saumu ya wajibu ni pana zaidi kuliko Saumu ya Ramadhani. Na Saumu ya wajibu ni kwa ujumla lakini Saumu ya Ramadhani inahusiana na siku maalumu; siku hizo ni mwezi wa Ramadhani. Maana ya hayo ni kwamba Saumu ya Ramadhani yote ni Saumu wajibu, lakini siyo kila Saumu ya wajibu ni Saumu ya Ramadhani.
Hakika kwamba Saumu ya Ramadhani imejulikana kwa Saumu ya Wajibu kwa wasio wanazuoni tu, kwani Ramadhan ni Saumu ya Wajibu ya kwanza juu ya Muislamu baleghi kwa masharti yake, na hiyo miongoni mwa nguzo za Uislamu, na uwajibu wa Saumu yake ni yanayojulika katika dini kwa dharura. Ama Saumu nyingine haipo ila kwa sababu inaambatana na mwanadamu mwenyewe, au kwa sababu ya kisheria kama vile, kafara kwa dhambi hasa iliyofanywa na mwanadamu huyo. Na hiyo ni tofauti baina ya Saumu ya Wajibu na Samu ya Ramadhani.
Ama aina za Saumu za wajibu katika Sharia na dalili zake ni:
Hakika kuwa Saumu ya faradhi katika sharia ni Saumu ya Ramadhani tu. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akaagiza katika Qur’ani tukufu: {Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge}. [AL-BAQARAH 185]. Na Mtume S.A.W. akasema: “Uislamu umejingwa kwa nguzo tano … miongoni mwa Saumu ya Ramadhani”. Na kutoka kwa Twalha Bin Ubaid Alaah alisema: “Hakika kuwa mtu alikuja kwa Mtume S.A.W., na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niambie Mwenyezi Mungu Mtukufu Amenifaradhishia nini kutokana na Saumu, Mtume S.A.W. akasema: mwezi wa Ramadhani, akasema: je, nimefaradhishiwa Saumu nyingine? Mtume S.A.W. akasema: Hapana, isipokuwa Sunna ya Saumu”. [Hadithi mbili zimetolewa na Bukhari na Muslim]
Na waislamu wote wanakubaliana kwa uwajibu wa mwezi wa Ramadhani, na ambaye hakufunga basi anawajibika kukidhi saumu hiyo, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyngine} [AL BAQARA 185], isipokuwa ikiwa mtu huyo alikuwa hawezi kufunga kamwe basi huwajibika fidia.
Na zipo hali mbalimbali zinazolazimisha Saumu kwa sababu:
Miongoni mwazo ni Saumu ya kafara ya kumwingilia mke katika mchana wa Ramadhani, basi kutoka kwa Abi Huraira R.A., alisema: “Mtu maalumu alikuja kwa Mtume S.A.W., na akasema: mimi nimeangamia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume S.A.W., akasema: mambo gani? Mtu akasema: nilimwingilia mke wangu katika mchana wa Ramadhani, Mtume S.A.W., akasema: unaweza kumkomboa mtumwa? akasema: hapana, Mtume S.A.W., akasema: unaweza kufunga miezi miwili ya kufuatana, akasema: hapana, Mtume S.A.W., akasema: basi, unaweza kuwalisha masikini sitini? akasema: hapana. Basi mtu mmoja mingoni mwa Maansari alikuja na kipapa cha matende, Mtume S.A.W., akasema:: chukua kipapa hicho na ukitoe kama Sadaka! akasema: kuna mwenye haja zaidi kuliko mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Naapa kwa Aliyekutuma kwa haki, hamna katika Madina watu wenye haja zaidi kuliko watu wa nyumba yetu. Mtume S.A.W., akasema: basi nenda na uilishe familia yako! [Imetolewa na Bukhari na Muslim].
Na miongoni mwayo ni Saumu ya kafara ya kujitenga wanawake wao, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda. (3) Na asiye pata mtumwa kumkomboa, basi na afunge miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiyeweza hayo basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na kwa makafiri ikoadhabu chungu. [AL MUJAADILAH 3, 4]
Na miongoni mwayo ni Saumu ya kafara ya kuua kwa kosa; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea.Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Naakiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini,basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima}. [AN NISAA 92]
Na miongoni mwa ni Saumu ya kafara ya kiapo; kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahalizenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ilimpate kushukuru}. [AL MAIDAH 89]
Na miongoni mwake ni Saumu ya nadhiri; na Aya tukufu zikaitaja hiyo, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale}. [AL HAJ 29], na miongoni mwao Alizozisemea Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhusu watu bora: {Wanatimiza ahadi, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana}, [AL INSAAN 7]. Na kutoka kwa Aisha R.A., kwamba Mtume S.A.W., alisema: “Mtu aliye weka nadhiri ya kumtii Mwenyezi Mungu, basi amtii, na aliye weka nadhiri ya kumuasi Mwenyezi Mungu basi asimuasi” [metolewa na Bukhari]. Na kutoka kwa Ibn Omar R.A. kwamba Mtume S.A.W., limsemea Omar: (uondoe nadhiri yako) [Bukhari na Muslim].
Na Ibn Qodamah alisema: Waislamu wamekubaliana usahihi wa nadhiri kwa kiujumla na ulazima wa kuitekeleza. [Al Mughiy 3/10, Ch. Maktabat Al Qahira].
Na miongoni mwao ni Saumu ya kafara ya Nadhiri; basi kutoka kwa Ibn Abbas (Hadithi ina hukumu ya marfua), Mtu akiweka nadhiri na hakuiitaja aina yake, basi kafara yake ni kafara ya kiapo [Isnadi yake ni sahihi, lakini wahifadhi walielekea kuizuia, kama alivyosema Al Hafedh Ibn Asaker katika kitabu cha: Bulugha Al Maram].
Na kutoka kwa Oqbah Bin Amer kutoka kwa Mtume S.A.W., alisema: “Kafara ya nadhiri ni kafara hiyohiyo ya kiapo”. [Muslim na At-Tarmiziy waliitoa, na akaisahihisha kwa tamko la: ““Kafara ya nadhiri kama haikutajwa ni kafara hiyohiyo ya kiapo”.
Na wanafiqhi wana fafanua katika baadhi ya hayo, lakini hakika tulitaka kujumuisha mlango wote. Ama kuhusu suala kutokuwepo (Saumu ya Wajibu) katika baadhi ya vitabu:
Basi jawabu ni kwamba kutosoma si dalili ya kutokukuta Saumu ya wajibu, lakini sababu ya hayo kwa kiujumla inarejea kwa kuvitumia vitabu vinavyo fupisha matini, halafu kuvisoma vitabu vya wanazuoni kwa haraka. Basi mtafiti hutazama katika kitabu cha Saumu basi akamkuta mtunzi anaongea Saumu ya Ramadhani basi akatosheka na mtazamo huo. Au pengine anapitia pasipo kutazamia yaliyopo baina ya mistari na mapindo ya maneno kama hayakuwa kwa maneno yanayohifadhiwa kwa akili ya mtafiti, na hayo pia yanalengana na mtifiti ambaye anatafiti katika vitabu vya kielektroniki.
Lakini katika uhalisi, hakika mwanachuoni wa fiqhi anataja Saumu ya Ramadhani kwa urefishu, kwani Saumu ya Ramadhani ni ya asili kama tulivyosema hapo juu, na anaashiria Saumu zote nyingine ishara nyepesi. Kwani ufafanuzi wa kila aina huja katika mlango wale, na hiyo ni mfano kwa huo katika kitabu cha: [Al-Mughniy], ambapo alitaja mwanzoni mwa kitabu cha Saumu kuongea katika Saumu ya Ramadhani, kisha akataja baada ya hayo kuongea juu ya Saumu ya Wajibu katika kuongea kwa Nia.
Ibn Qodamah akasema: (Kitabu cha Saumu) Saumu katika lugha maana yake ni mfungo (kujinyima- mwiko), inasemwa mchana umefunga, maani yake Jua likisimama kutembelea, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema katika habari za Maryam: {Napindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu}. [MARYAM 26] yaani kunyamaza, kwani ni mfungo kutokuongea.
Na Saumu kisheria maana yake ni: mfungo au kujinyima kwa vitu maalumu katika wakati maalumu, sharehe yake itakuja baadaye. Na Saumu ya Ramadhani ni Wajibu, na dalili yake ni Qur’ani na Sunna na makubaliano ya wanazuoni na Umma. [Al-Mughniy 104/3].
Halafu Ibn Qodamah akasema: Suala: akasema: “Haimtoshi Saumu ya Faradhi hadi aweke nia wakati wowote katika usiku”. Na ujumla wake ni kwamba haisihi Saumu ila kwa nia, kwa makubaliano, kwa faradhi au Sunna , kwani Saumu ni ibada halisi, basi inahitajika nia, kama mfano wa Swala, kisha kama ilikuwa faradhi kama mfano wa Saumu ya Ramadhani katika kuitendea au kuikidhi, na Saumu ya Nadhiri au Kafara; imeshurutishwa nia kutoka usiku kama walivyosema imamu wetu, licha ya Malik na Shafi. [Al-Mughniy 109/3]
Na pamoja ya hayo yupo aliyeboresha katika mgao, na akataja yanayotakiwa katika ufafanuzi wake, kama alivyofanya Ibn Rushd katika kitabu chake bora cha: [Bidayatu Al-Mujtahed].
Na Ibn Rushd amesema: Basi tuanze kwa sehemu ya kwanza ya kitabu hicho, na kwa sentensi yake ya kwanza, sentensi hiyo ni maarifa ya aina za Saumu basi tuseme: kwamba Saumu ya kisheria; miongoni mwake ni Saumu ya faradhi na Saumu ya Sunna na Saumu ya Wajibu ni vigawanyo vitatu; miongoni mwake ni ambayo inawajibika kwa wakati wenyewe, na hiyo ni Saumu ya mwezi wa Ramadhani wenyewe, na miongoni mwake ni ambayo inawajibika kwa sababu, na hiyo ni Saumu ya kafara, na miongoni mwake ni ambayo mtu anafaradhisha juu ya nafsi yake, na hiyo ni Saumu ya Nadhiri. Na kitabu hicho kinaambatana na ufafanuzi wa Saumu ya Ramadhani tu miongoni mwa Saumu za Wajibu, na ama Saumu ya kafara basi hutajwa katika mambo yanayowajibika kafara, na kadhalika Saumu ya Nadhiri hutajwa katika kitabu cha Nadhiri. [Bidayatu Al-Mujtahed na Nihayatu Al-Moqtswed 42/2, Ch. Dar Al-Hadiith]
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia: Hakika ni kwamba Istilahi ya Saumu ya Wajibu inakusudiwa kwake Saumu ya Ramadhani na nyinginezo, na kutokuwepo katika baadhi ya vitabu haimaanishi kutokuwepo katika baadhi ya vitabu vingine.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas