Adhana ya Pili katika Swala ya Al-F...

Egypt's Dar Al-Ifta

Adhana ya Pili katika Swala ya Al-Fajiri.

Question

 Katika kijiji chetu ulizuka mgogoro kwa sababu ya adhana ya Al-Fajiri, Je Swala ya Al-Fajiri ina adhana moja au adhana mbili? Ni ipi hukumu ya adhana mbili kwa Swala ya Al-Fajiri? Na ni ipi njia sahihi; kuadhiniwa adhana moja au kuadhiniwa adhana mbili?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Masuala haya yanahusiana na hukumu ya adhana, na kuihusisha adhana ya swala ya asubuhi kwa adhana ya kwanza kabla ya kuingia wakati wa swala ya Al-Fajiri, na masuala katika swali la muuliziji hapa ni kuitekeleza Sunna hii inapelekea kutokea fitina miongoni mwa watu kwani hawajazoea juu ya jambo hili. Na pia kuna jambo jingine halikutajwa katika swali moja kwa moja, swali hili ni kwamba ikiwa tutatekeleza Sunna hii na kuadhini adhana ya kwanza, labda itasababisha kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwa kati ya watu wanapomsikia muadhini, je ni adhana ya kwanza au ya pili? Na hasa hasa kwa kuwa adhana kupelekea Swala kusimamishwa na pia wanaofunga huanza kujizuia kula vyakula vya kufuturisha.
Ama hukumu ya masuala haya ni kwamba asili katika adhana ni kuingia wakati wa Swala ya faradhi kama ni sharti lake, ni kama ilivyokuja katika vitabu vya sahihi mbili kutoka kwa Malik bin Al-Huwairith kwamba Mtume (S.A.W) Alisema: “Inapo wadia swala basi na aadhini na akimu mmoja wenu na awe Imamu aliye mkubwa kati yenu”. Na kwa sababu adhana ni kwa ajili ya kuwaarifu watu kuingia wakati wa swala na hii ni kwa lengo la kuwahimiza watu kwa kusimamisha swala kwani swala haisihi ila ndani ya wakati wake.
Lakini katika swala ya asubuhi inajuzu kuadhini kwake kabla ya wakati wake kwa mujibu ya yaliyopokewa katika vitabu vya sahihi mbili kutoka kwa bin Umar R.A., alisema: “Mtume S.A.W, alikuwa ana waadhini wawili; Bilal na Ibn Umm Maktum aliyekuwa kibofu. Mtume S.A.W alisema: Hakika Bilali huadhini wakati wa usiku, basi kuleni na kunyweni mpaka akiadhini Ibn Umm Maktum”.
Al-Nawawiy alisema katika maelezo yake juu ya Muslim [7\202, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Na ndani ya maelezo haya ni kupendelea uwepo wa adhana mbili kwa swala ya asubuhi mmoja wao kabla ya wakati wa swala ya Al-Fajiri na nyingine baada ya kuchomoza kwa mwangaza wa Al-Fajiri yaani mwanzo wake”. A.H.
Na Mtume S.A.W., ametanabahisha juu ya kwamba adhana ya kwanza haimzuii mtu kula daku, na kuwa na muadhini mwingine kunaitofautisha sauti yake na ya muadhini wa kwanza badala ya kuwa na muadhini moja tu, ni dalili ya wazi juu ya kuepusha watu kuchanganyikiwa na inatakiwa hivyo kisheria, na Sunna hii ikipingana na msingi wa sheria basi ni lazima jambo hili liondolewe kwa lengo la kuhakikisha maslahi na kuzuia ufisadi; kwa hivyo athari ya hayo ilidhihirika katika maneno ya wanazuoni kwa ajili ya masilahi ya watu mbali ya kuchanganyikiwa.
Al-Bahutiy Al-Hambaliy alisema: “Inapendelewa kwa anayeadhini adhana ya kabla ya Swala ya Al-Fajiri aadhini adhana yake ndani ya wakati mmoja wa usiku wa kila siku, haitangulii wala kuchelewa ili watu wasichanganyikiwe (Na yapasa awepo muadhini mwingine anayeadhini katika wakati wa adhana, iwe ni kawaida juu ya jambo hili ili watu wasipate kuchanganyikiwa na kuchukia) adhana (katika Ramadhani kabla wakati wa Al-Fajiri ya pili tu) yaani adhana kabla ya Al-Fajiri. (ama wakiwa na muadhini mwingine katika wakati wa kwanza basi sio makruhu kwa kauli ya Mtume S.A.W aliposema: Hakika Bilali huadhini wakati wa usiku, basi kuleni na kunyweni mpaka anapoadhini Ibn Umm Maktum)” Bukhari na Muslim. [Kashashaf Al-Qinaa 1\241, Ch. Dar Al-Fikr].
Na Al-Kasaniy Al-Hanafiy: “Adhana kabla ya Al-Fajiri inasababisha madhara kwa watu; kwani wakati huu ni wakati wa kulala kwao hususan kwa wanaoswali swala ya Tahajud katika nusu ya kwanza ya usiku, na labda huenda wakachanganyikiwa, na hiyo ni makruhu”. [Badaea As-Swanaea 1\154 Ch. Al-Maktaba Al-Elmiyah].
Na kujiepusha na shaka kuna thibitika kwa sura mbali mbali:
Ni bora kutofanya hivyo isipokuwa wakiwepo waadhini wawili katika Msikiti mmoja ili watu wapate kupambanua kati ya adhana mbili kwa ajili ya kutofautisha kati ya sauti za waadhini hao wawili. Na katika suala hili Al-Eraqiy alisema: “Ibn Al-Munzer na wengine walisimulia katika masuala haya rai tatu kutoka katika kundi moja miongoni mwa wanachuoni wa Hadithi walisema kwamba wakiwepo waadhini wawili katika Msikiti mmoja basi mmoja wao ataadhini kabla ya kuchomoza kwa Al-Fajiri na muadhini mwingine ataadhini baada ya kuchomoza kwa Al-Fajiri, kwa maana kuadhiniwa kwa Swala ya asubuhi, na Ibn Hazm Al-Dhahitiy aliisema pia rai hii: inajuzu kuadhini kabla ya kuchomoza Al-Fajiri ya pili kwa kiasi cha kutimiza muadhini wa kwanza adhani yake na kushuka chini au kwa kiasi cha kupanda juu kwa muadhini mwingine, na kuchomoza kwa Al-Fajiri kabla ya kuanza kwa muadhini wa pili katika adhana”. [Twarih Al-Tathreeb 2\206, Ch. Dar Ihiyaa At-Tutath Al-arabiy].
Na anaweza kuacha adhana ya kwanza ikiwa itasababisha watu kuchanganyikiwa, na hii ni kwa mujibu wa kanuni ya Fiqhi inayosema: Kuepusha madhara kunatangulizwa mbele ya kuleta maslahi na kanuni hii ya Kifiqhi inathibitisha hivyo kupitia baadhi ya maandiko kama yalivyotajwa katika kitabu cha sahihi mbili kutoka kwa Aisha R.A. alisema: “Nilimuuliza Mtume S.A.W, Ukuta unaofuatia Hijr Ismail ni katika sehemu ya Nyumba Tukufu? Akasema: Naam “Nikasema: Wana nini hata wasiutie katika Nyumba Tukufu. Akasema: "Hakika kaumu yako walipungukiwa na pesa” Nikasema: Kwa nini mlango wake uko juu? Mtume S.A.W akasema: "Walifanya hivyo kaumu yako ili wamuingize wanaye mtaka na wamzuwie wasiye mtaka. Na lau ingelikuwa kaumu yako karibuni tu wametoka katika ujahili na kwamba mimi ningechelea zisiingie chuki nyoyo zao ningeliuingiza ukuta huo katika Nyumba Tukufu na ningeuteremsha mlango na kuuambatisha na ardhi). Na hasa kwa kuwa adhana moja tu yaweza kutosha, An-Nawawiy alisema: “Masahaba zetu walisema: kuadhini asubuhi mara mbili ni Sunna, moja kati ya adhana hizo ni kabla ya Swala ya Al-Fajiri, na ya pili ni baada ya kuchomoza kwake; kwa kauli ya Mtume S.A.W alisema:Hakika Bilal huadhini wakati wa usiku ,basi kuleni na kunyweni mpaka akiadhini Ibn Umm Maktum”. Na ni bora wakiwa waadhini wawili, mmoja wao anaadhini kabla ya Al-Fajiri na mwingine anaadhini baada ya Al-Fajiri. Na ikiwa ni adhana moja tu, yaweza kujuzu kuwa kabla ya Al-Fajiri au baada yake, na yajuzu pia kufanya hivyo kwa kuwepo baadhi ya maneno kabla Al-Fajiri au baada yake, na ikiwa adhana moja tu itatosheleza, basi ni bora iwe baada ya Al-Fajiri kama katika Swala nyingine, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi [Rejelea: Al-Majmou 3\87, Ch. Dar Al-Fikr].
Kwa upande mwingine, anaweza kusema baadhi ya dhikri badala ya adhana ya kwanza kwa ajili ya kutanabahisha wafungaji na wenye kuswali na wenye kulala, na na hayo yalitajwa katika Sahihi mbili kutoka kwa Abdullahi Ibn Masoud, kutoka kwa Mtume S.A.W alisema: “Hakuziwiini nyinyi au mmoja kati yenu- kutikana na kula daku yake adhana ya Bilali, kwani yeye huadhini-au hunadi swala wakati wa usiku-ili aliye kaa macho kwa ajili ya ibada apate kwenda kupumzika kidogo kabla ya kuingia Al-Fajiri na apate kuwahi kula daku, na aliyelala apate kuamka ajiweke tayari kwa ajili ya sala ya Al-Fajiri”.
An-Nawawiy alisema katika maelezo yake juu ya kitabu cha: ]Muslim 7\204]: “Kurejea anayeswali ili kulala baadhi ya wakati kwa kuchukua raha yake na kumuamsha aaliyelala kati yenu ili awe tayari kwa Swala ya asubuhi na kuweza kufanya anayetaka kutoka katika Swala ya Tahajudi au Swala ya Witri au kuchukua chakula cha daku au kuosha na kadhalika”.
Ikiwa mambo hayo yote ni kwa sababu ya adhana ya kwanza –na ni wazi kutokana na matini – basi panaweza kufanywa mengine ili kuepusha mchanganyiko, kwa njia ya kuinua sauti ya muadhini katika adhana yake ya kwanza kwa kusema baadhi ya dhikri ili kuyapata maslahi na kuepusha madhara ya mchanganyiko, na maneno haya yanaweza kuchukuliwa kutoka katika maneno ya Ibn Rajabu Al-Hhambaliy katika maelezo yake kwa Hadithi ya Ibn Masoud katika kauli yake: “Kuna faida mbili kwa adhana yake kabla ya Al-Fajiri: ya kwanza ni: Kumjulisha anayeswali kwamba wakati ya Swala ya Al-Fajiri umekaribia, na hii ni dalili juu ya kuwa adhana ilikuwa wakati wake ni karibu na swala ya Al-Fajiri, na tuliutaja mlango uliyopita, kwamba iliadhiniwa wakati wa kupambazuka kwa Al-Fajiri ya kwanza. Na faida ya pili ni: Kuamka aliye lala, ili kuwa tayari kwa ajili ya Swala na kwa kujitwaharisha; ili kuidiriki Jamaa ya Swala ya Al-Fajiri katika wakati wake wa mwanzo; na pia ili kudiriki Swala ya Witri au sehemu ya Swala ya Tahajudi kabla ya wakati wa Al-Fajiri, au pengine kula chakula cha daku kwa anayetaka kufunga. Pia alisema: “Hakuziwiliini nyinyi kutokana na kula daku yake adhana ya Bilal)). Na hii ni dalili juu ya fadhila ya kuwaamsha waliolala katika wakati wa mwisho wa usiku kwa adhana au dhikri. Na katika jambo hili, At-Tirmidhiy alisimulia kutoka kwa Abdullahi Ibn Muhamamd Bin Aqiil, kutoka kwa At-Twofiil Ibn Ubay Ibn Kaab kutoka kwa baba yake alisema kwamba: Mtume S.A.W, alikuwa akienda katika theluthi ya usiku akaswali swala ya Qiyam, na alisema: “Enyi watu, mtajeni Mwenyezi Mungu, siku ya Kiama iko karibu kuja, kifo kitakuja, kifo kitakuja kwa kila kilicho ndani yake”. Na alisema kuwa Hadithi hii ina hukumu ya Hasan. Na ina dalili juu ya kuwa dhikri na Tasbihi kwa sauti mwishoni mwa usiku ni sawa na si kosa, kwa ajili ya kuwaamsha watu waliolala. Na kwa upande mwingine kuna kikundi miongoni mwa Wanazuoni ambao wao wanakanusha jambo hili na wanasema kuwa ni uzushi. Miongoni mwao ni Abu Al-Faraj Ibn Al-Juziy. Na katika tuliyotaja kuna dalili juu ya jambo hili ya kwamba si uzushi. [Fat-h Al-Bariy 5\332, Ch. Maktabat Al-Ghurabaa Al-Athariyah - Al-Madinah Al-Monawarah].
Na rai hii ilikuwa ni rai inayofanyiwa kazi katika zama za mwishoni, na Ibn Hajar Al-Asqalaniy alisema: “Baadhi ya wafuasi wa Al-Hanafiyah walidai kwamba mwito wa swala kabla ya Al-Fajiri haukuwa kwa lafudhi ya adhana bali ulikuwa ni dhikri au kwa ajili ya daku kama katika hali ya siku hizi”. [Fat-h Al-Bariy 2\104, CH. Dar Al-Maarifah].
Na kwa upande mwingine Ibn Hajar aliyarudi maneno haya, lakini ushahidi katika haya ni kwamba watu walilifanya jambo hili katika zama za mwishoni.
Na kutokana na yaliyotangulia ni wazi kwamba kutoa adhana mbili katika sala ya Al-Fajiri inajuzu. Na pakiwepo mchanganyiko kati ya watu basi yaweza kubadilishwa adhana kwa kitu kingine kama dhikri au Dua kwa ajili ya kuwazindua watu ili waamke kwa ajili ya swala.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas