Mfumo wa Riba kwa Mamlaka, Taasisi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mfumo wa Riba kwa Mamlaka, Taasisi na Makampuni.

Question

Je inazingatiwa kuwepo mfumo wa riba kati ya Mamlaka, Taasisi, Makampuni na mengineo? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Taasisi ya kutoa Fatwa ya Misri imetoa Fatwa kuhusu Mamlaka,Taasisi na Makampuni tarehe 18\5\2011, chini ya nambari 208 ya mwaka 2011, imebainisha maana ya istilahi ya (Mamlaka,Taasisi na Makampuni) katika vitabu vya fiqhi, na tofauti baina yake na istilahi ya (mtu wa kawaida), na iliambatana na baadhi ya hukumu za (Maamlaka,Taasisi na Makampuni), na mwisho wa yote haya Fatwa imesema kwamba: Mamlaka, Taasisi na Makampuni ni aina ya kikundi cha watu katika Taasisi na mali yenye mfumo wa wake unajitehemea, ina malengo maalumu na ina haki ya mtu wa kawaida kwa upande wa kanuni kuhusu jambo hilo.
Na makusudio ya mfumo wa dhati wa kujitegemea ni kukadiria majukumu na kuwepo utegemezi kwa mtu wa taasisi kutoka kwa watu wa kawaida wanaoshirikiana naye katika taasisi, na kwa sababu ya haki hii anaweza kufanya kila kitu kama mtu yeyote wa kawaida na anaweza kuishi maisha sawa ya kisheria, na anaweza kufanya maafikiano/mapatano pamoja na watu wengine wa kawaida na waasisi,na maana ya hayo mtu wa taasisi anaweza kufanya kila kitu na wengine yaani anajua haki yake na wajibu anaopaswa kufanya na wengine, na kadhalika kuna tofauti kati ya mtu wa kawaida na mtu wa taasisi,na tofauti hii baina ya hawa wawili ilikuwa na athari yake juu ya hukumu zilizohusiana nao wawili.
Na hukumu hizi zilikuwa maarufu katika Fiqhi ya kiislamu, na wanazuoni wa Fiqhi walitaja ufahamu wake bila ya kutaja jina lake moja kwa moja, kanuni ya Misri ya kiserikali kama kanuni zingine za nchi za warabu, na kupanga miamala na mapatano na mtu anayehusikia katika Taasisi.
Na Fatwa hii ilibainisha kupambanua baina ya mtu wa taasisi (Mamlaka, Taasisi na Makampuni) na mtu wa kawaida ya kuwa mtu wa taasisi ana mali yake mwenyewe mbali na mali ya waasisi, na kwa kutokana na hayo ana uhuru kamili wa kuutimiza mradi wake mwenyewe bila ya kuchukulia mali au deni kutoka mali ya waasisi wengeni; kwani jukumu au mali ya waasisi ni tofauti na mali ya mtu huyu wa taasisi.
Na jukumu hili lililoithibitishwa kwa mtu wa taasisi ni matokeo ya kufuata kanuni ya kuwa mtu huyu ana haki zote kwa mujibu wa kanuni, na maana ya hayo mtu huyu ana haki yake mwenyewe na wajibu juu yake; kwani lengo la hilo ni jukumu la mtu mwenyewe, na kutokana na kanuni iliyothibitihswa kwa mtu wa taasisi. Kwa hivyo jukumu na haki maalumu ya mtu wa taasisi ni msingi wa ujenzi wa mtu wa taasisi,na masuala ya kuithibitisha jukumu kwa mtu wa taasisi ni msingi wa ujenzi wa haki yake; kwani maana ya kulithibitisha jukumu la kifedha kwake hasa ni dalili ya kuzithibitisha haki zote na wajibu juu yake kama tulivyozitaja hapo juu katika Fatwa .
Tunaweza kusema kwamba: Kutokana ya kuthibitisha jukumu kwa mtu wa taasisi, basi anaweza kuitimiza kazi yoyote pamoja na mtu mwingine wa taasisi au wa kawaida; kwani tunasimama mbele ya haki mbili tofauti ya mtu wa kawaida na ya mtu wa taasisi, mmoja wao kwa mtu wa kawaida na nyingine kwa mtu wa taasisi, na kwa hivyo muamala wa kifedha umepitishwa baina ya watu hawa wawili wa kawaida na wa taasisi kuhusu kuipa mikopo ya benki baina ya watu wa kawaida, mfanyakazi wa benki hana haki ya kunufaika kutokana na faida ya benki kutoka kwa mteja wa benki, na ufumbuzi ni kwamba uharamu wa faida za benki katika sura hii msingi wake sio kutokana na muamala kati ya watu hawa wawili tu, bali kuna vipengele vingine vinavyoisababisha haramu ya sura hii, hakuna sababu za kueleza hapa kwa sasa, na kwa upande mwingine akili ya mfanyakazi wa kibenki inatoa tatuzi nyingi ili kutatua tatizo la mwenye kuhitaji pesa na kuziepushia mfumo wa riba. Na utatuzi huu ni kama ushirikiano wa upungufu unaoafikiana kati ya washiriki hawa wawili kwa kuacha hisa ya mmoja wao kwa mwingine kwa mpigo au sehemu sehemu kwa mujibu wa masharti waliyowekeana.
Ama utendaji wa kibiashara ukiwa baina ya wahusika badala (waasisi wa taasisi) kama katika taasisi kubwa ya kiuchumi inayokuwa na kikundi cha kitegauchumi na makampuni, na wanaofanya miamala mingi ya kibiashara kama mikopo na mategemeo ya kipesa na kadhalika, na mfano wa haya ni (mashirika ya muungano) yanayokuwa na idadi ya mashirika tanzu hata kama yasingekuwa katika uwanja wake ule ule. Na mashirika haya yanajengeka kwa msingi wa ushirikiano wa kweli katika rasilimali za mashirika hayo tanzu, na ushirikiano kati ya mashirika hayo.
Na kwa upande mwingine shirika kuu linaweza kuyapa mikopo mashirika tanzu, na linaweza kuwa ni tegemezi wakati wa deni la shirika tanzu la shirika kuu. Na kanuni zinaupangilia uhusiano huu baina ya shirika kuu na tanzu, na pengine (shirika kuu) linamiliki mashirika yote ya kikundi cha ushirikiano au linashiriki kwa sehemu katika kikundi cha ushirikiano huo.
Na matokeo ya muamala huu mbele ya wahusika badala ya waasisi wawili, kila mmoja wao ana jukumu la kifedha kujitegemea mbali na mwingine na pia mbali na waasisi wengine wa shirika kuu, na wakati huo huo, hatuweza kusahau kwamba katika muamala wa kifedha tunakuta kwamba shirika kuu ndilo mmiliki kamili au wa hisa ya mashirika mengine tanzu; katika hali hii mikopo kwa mashirika tanzu kutoka katika shirika kuu haitakuwa na tatizo lolote kwani hali hii ni mfano wa mtu anayechukuwa mkopo kutoka katika mali yake yeye mwenyewe. Na hali hii ni halali.
Kwa hivyo wanazuoni wa Fiqhi hawaharamishi riba baina ya mtumwa na bwana wake; kwani mtumwa na mali yake ni mali ya bwana wake huyo, yaani ni sawa sawa na mtu kujikopesha yeye mwenyewe kutoka katika mali yake mwenyewe.
Al-Sarkhasiy anasema katika kitabu cha Al-mabsout: "Mlango wa matumizi baina ya bwana na mtumwa wake: Alisema: hakuna riba baina ya bwana na mtumwa wake kutokana na kauli ya Mtume S.A.W.: "Hakuna riba baina ya mtumwa na bwana wake", kwani hali hii sio kuuza na kununua; kwani pato la mtumwa ni mali ya bwana wake, na uuzaji ni mbadilishano wa miliki kwa mmiliki mwingine, na kuiweka mali yake katika baadhi ya mali nyingine ambayo ni yake pia huko sio kuuza. lakini kama mtumwa alikuwa na deni kwake, basi hakuna riba baina yao, na bwana wake huyo analazimika kukirudishia alichokichukua kwa mtumwa wake; kwani chumo lake linahangaikia deni la wanaomdai kwa ajili ya uhuru wake, na wala asimkabishi isipokuwa baada ya kumaliza deni lake, kama ambavyo angelidhukua bila ya mkataba wowote, iwe alinunua kutoka kwake dirhamu kwa dirhamu au dirhamu mbili kwa dirhamu moja, kwani alichokitoa na kumpa mtu sio mbadala haya kama kilikuwa kichache, au zaidi , atalazimika kukirejesha kwa ajili ya haki ya wadai wa mtumwa" [Al-Mabsout 14\59, cha, Dar Al-Maarifah].
Al-Marduwy alisema: katika kitabu cha: [Al-inswaf)] "Faida: hakuna riba baina ya mtumwa na bwana wake, na Al-majdi alisisitizia jambo hilo kwenye mfumo wa riba baina yake na bwana wake tukisema kwa umiliki wake. Na alisema hilo katika kitabu cha Al-qawaed Alusuliah" [Al-Inswaf 5\53, cha, Dar Ihyaa At-Turath Al-arabiy].
Ama shirika kuu likiimiliki hisa moja katika hisa za mashirika tanzu, basi bila shaka mfumo wa riba unakuwa kati ya mashirika mawili, na shirika kuu likitoa mkopo kwa shirika tanzu, basi linaweza kufanya hivyo lakini bila ya kuchukua nyongeza ya aina yoyote; kwani nyongeza hiyo itakuwa ni riba. Na washirika wawili iwapo mmoja wao anahitaji kuuchukuwa mkopo kutoka katika shirika hawezi kuuchukuwa mkopo huo isipokuwa baada ya muwafaka wa mwingine kwa sharti la kuyalinda masilahi yao wote wawili.
Na kutokana na maeelezo yaliyotangulia, bila shaka muamala baina ya washirika wawili wa taasisi, unaweza kuwa muamala wenye riba ulio haramu baina yao kama katika muamala baina ya washirika wa taasisi na wa kawaida, au baina ya washirika wawili wa kawaida. Ama katika hali ya kuwa baina ya mshirika wa taasisi tanzu na mshirika wa taasisi inayomilikiwa na muhusika wa taasisi kuu, basi hakuna riba katika muamala baina yao kwa mujibu wa madhehebu ya Jamhuri ya wanazuoni.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas