Hukumu ya Kichinjo cha Mwezi wa Raj...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kichinjo cha Mwezi wa Rajabu.

Question

Ni ipi hukumu ya kichinjo cha mwezi wa Rajabu, na hicho ambacho kinaitwa kwa Utairah? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Utairah ni kichinjo walichokuwa wakikichinja waarabu katika siku kumi za kwanza za mwezi wa Rajabu, na pia walikuwa wakikiita kwa jina la kichinjo cha mwezi wa Rajabu. Na Uislamu ulikuja na waarabu walikuwa wakichinja kichinjo hicho katika mwezi wa Rajabu, na walikiita Utairah au kichinjo cha mwezi wa Rajabu, na wakaendelea kufanya hivyo tangu mwanzo wa Uislamu, kwa kauli ya Mtume S.A.W, katika Hadithi yenye hukumu ya Nzuri (Hassan) iliyopokelewa na Tirmidhiy kutoka kwa Mukhanaf Bin Saleem: “Alisema: Tulikuwa tumesimama na Mtume S.A.W, eneo la Arafa, nikamsikia anasema: Enyi watu, hakika watu wa kila nyumba kila mwaka wana Kichinjo pamoja na Utairah. Je mnajua maana ya Utairah? Ni yule mnyama mnaemwita Kichinjo/mnyama wa Mwezi wa Rajabu”.
Lakini wanazuoni wa Fiqhi walihitilafiana baada ya hayo kuhusu kufutwa kwa hukumu hiyo, na Jamhuri ya wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafi, ya Maliki na ya Hanbali wanakubali kuwa kuomba Utairah kumefutwa, kwa dalili yao ya kauli ya Mtume S.A.W, katika Hadithi yenye hukumu ya Mutafaqu alaihi (wanazuoni wameafikiana), kutoka kwa Abu Hurairah R.A, kutoka kwa Mtume S.A.W, amesema: “(Sio mtoto wa mnyama wala Sio Utairah) Na tawi: zao la mwanzo la mifugo, walikuwa wanamchinja kwa ajili ya miungu yao ya kishetani, na Utairah ilikuwa katika mwezi wa Rajabu”.
Na wafuasi wa madhehebu ya Shafi wanaona kutofutwa kwa takwa la Utairah na wakasema kuwa inapendeza, na hiyo ni kauli ya Ibn Siriin.
Al Hafedh anasema katika kitabu cha: [Al Fatih] “Na anamuunga mkono kwa Hadithi iliyotolewa na Abu Dawud, na An Nassaiy, na Ibn Majah, na Al Haakem na Ibn Al Mundher wakaisahihisha kutoka kwa Nubaishah alisema: “Mtu mmoja alimwita Mtume S.A.W, kwa kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, akasema: sisi tulikuwa tukimzingatia mnyama wa Utairah kuwa ni wa mwezi wa Rajabu katika zama za ujahili (ujinga wa kabla ya Uislamu), Je wewe unatuamrisha tufanye nini? Akasema Mtume S.A.W: Chinjeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mwezi wowote, na mfanye wema kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na muwalishe watu”. Imepokelewa na Abu Dawud na wengineo kwa Isnadi nyingi sahihi. Ibn Al Mundher akasema: hiyo ni Hadithi sahihi, halafu akasema: Mtume S.A.W, hakubatilisha Utairah kutoka katika asili yake isipokuwa alibatilisha kuchinja maalumu kwa ajili ya mwezi wa Rajabu”. [Fathu Al Bariy kwa Ibn Hajar 597/9, Ch. Dar Al Maarifah].
Na An Nassaiy akatoa Hadithi kutoka kwa Al Harith Ibn Amru akasema: “Nilimwendea Mtume S.A.W, katika eneo la Arafaati au alisema katika eneo la Minah na akaulizwa na mtu mmoja kuhusu Utairah akajibu kwa kusema: atakayetaka atachinja kwa ajili ya mwezi wa Rajabu na asiyetaka asichinje, na atakayetaka atachinja mnyama wa mwanzo kuzaliwa na asiyetaka asifanye hivyo”.
Na pia An Nassaiy akapokea Hadithi kutoka kwa Razeen kwamba alisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakika sisi katika zama za ujahili tulikuwa tunachinja vichinjo kisha tunakula na kuwalisha watu wengine, Mtume S.A.W, akasema: Hakuna ubaya wowote kufanya hivyo”.
Na wanazuoni wa Sunnan (Hadithi) walitoa Hadithi kutoka kwa Mukhanaf Bin Saleem Al Ghamidiy R.A. alisema: “Tulikuwa umesimama na Mtume S.A.W: katika vilima vya Arafaat nikamsikia anasema: Enyi watu, kila nyumba katika kila mwaka inalazimika kuchinja mnyama na Utairah. Je unajua maana ya Utairah? Ni yule mnyama aitwaye Rajabiyah (ambaye huwa anachinjwa katika mwezi wa Rajabu)”.
Ashafiy akasema: “Na Utairah ndiye Rajabiyah, naye ni mnyama aliyekuwa akichinjwa enzi za Ujahili kwa ajili ya sadaka, na Mtume S.A.W, akasema: Hakuna ulazima wa (kuchinja) Utairah: Na kauli yake (Hakuna Utairah): maana yake sio wajibu, (chinjeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wowote mpendapo) kwa maana kuwa pale mnapotaka kufanya hivyo mchinje kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya mwezi wowote mtakao; kwani Utairah ilikuwa ndani ya mwezi wa Rajabu sio katika miezi mingine”. [Asunnan Al Mathura kwa Ashafiy Li Abi Ibrahiim Al Mazniy 341/1, Ch. Dar Al Maarifah.]
Imam An-Nawaiy anasema katika kitabu cha: [Al Majmou’] Na ilijibiwa kutokana na Hadithi: (Hakuna kuchinja Far-u ambaye ni mtoto wa kwanza wa mnyama, wala hakuna kuchinja Utairah) kwa njia tatu: ya kwanza yake: ni Jawabu la Imamu Shafi lililotangulia kwamba kinachokusudiwa ni ukanushaji wa uwajibu. Ya pili yake: kwamba kinachokusudiwa ni kukanusha walichokuwa wakikichinja kwa ajili ya masanamu yao. Na ya tatu: kwamba kilichopo ni kuwa wanyama hawa wa aina mbili sio kama sunna ilivyo katika vichinjo au thawabu za kumwaga damu yake, na kwamba kugawa nyama kwa masikini ni jambo jema na ni sadaka, na njia sahihi ni ile aliyoisema Imamu Shafi na ikaungwa mkono na Hadithi, kwamba ni Sunna inayopendeza na wala haichukizi. Na hayo ndio madhehebu yetu sisi. [Al Majmou’ kwa An Nawawiy 445/8, Ch. Dar Al Fikr]
Kutokana na yaliyotangulia; Kwa hakika sisi hatuoni ubaya wowote wa kuchinja mnyama aitwaye Utairah kama ilivyotangulia kusemwa, na kwamba maana huru ya kuchinja ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya mwezi wa Rajabu, hakuzuiwi kama ilivyo kawaida ya kuchinja katika miezi mingine yote
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas