Hukumu ya Uvaaji wa Pete kwa Wanau...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Uvaaji wa Pete kwa Wanaume na Wanawake

Question

  Ni nini hukumu ya kisheria kwa uvaaji wa pete kwa mwanamume na mwanamke? Na kuifanya ikawa alama ya uchumba au ndoa?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa zote njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya utangulizi huo:
Inakubalika kisheria kwamba asili ya uvaaji wa pete ni kwamba inajuzu. Na Pete ina umbile la duara na iliyotengenezwa kwa madini ya fedha. [Al Muswbaahu Al Muneer Fii Ghareeb As-Sharhu Al Kabeer kwa Al Faiyumiy, Uk. 137, Kidahizo cha Khatama, Ch. Al Maktabah Al Elimiyah].
Na ya asili katika hukumu hiyo ni maelezo yaliyotajwa katika vitabu viwili Sahihi, kutoka kwa Ibn Omar R.A, kwamba Mtume S.A.W, alikuwa akiivaa pete ya fedha, iliyoandikwa Muhamad Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Lakini kujuzu huku kunaambatanishwa na hiyo Pete kutokuwa ya dhahabu, kwani inapokuwa hivyo huzuilika kwa wanaume kuivaa na huhalalika kwa wanawake kuivaa. Hukumu hii ni kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa na At Tirmiziy na akasema kwamba Hadithi hiyo ina hukumu ya ni Sahihi na Nzuri, kutoka kwa Abu Musa Al Asha'riy R.A. kwamba Mtume S.A.W. anasema: "Uvaaji wa Hariri na Dhahabu umeharishwa kwa wanaume wa Umma wangu na umehalalishwa kwa Wanawake wao".
Na kadhalika Hadithi iliyopokelewa na Abu Dawud kutoka kwa Amiri wa waumini Ali Bin Abi Twaleb R.A. kwamba Mtume S.A.W. Aliichukua Hariri na akaiweka kuliani kwake na akaichukua Dhahabu na kuiweka kushotoni kwake kisha akasema: "Hakika viwili hivi ni haramu kwa wanaume wa Umma wangu".
Ama kuhusu Pete basi ni: ile ya dhahabu au ya fedha bila ya jiwe lolote la thamani katikati yake na huvaliwa katika kidole. [Al Mu'jamu Al Waseetw 270/1, Baraza la Kiarabu katika Kairo, Ch. Dar Ad Da'wa kidahizo cha Dabal] Basi nayo iko katika maana ya Pete kwani hiyo ni Pete na zaidi ya Pete na inajuzu kuivaa kama pete kwa kuwa kwake tu sio ya dhahabu kwa wanaume.
Sheikh wa Uislamu Zakariyah Al Nswariy amesema katika kitabu cha: [Sharhu Al Manhaj 31/2, Ch. Al Halabiy]: "(Na akaharamisha katika kidole) Pete ya dhahabu au ya fedha na akaifanya (kuwa sunna Pete ya dhahabu) kwa mwanamke". Sheikh Al Bijirimiy akaeleza katika [Hashiya yake] kauli yake: (Na kuwa Sunn ya pete ya dhahabu) na akasema: "Na jino ni sehemu ya kishikizo cha vito katika Pete ambayo sio pete isiyokuwa na kito chochote ambapo huvaliwa kidoleni, kwani hiyo ni aina nyingine ya Pete na kwa hivyo inakuwa Haramu kwa dhahabu na inajuzu kwa fedha".
Imamu Ibn Hajar Al Haitamiy amesema katika kitabu cha: [Tuhafat Al Muhtaaj 276/3, Ch. Dar Ihuyaa At Turath Al Arabiy]: "Na (inamhalalikia) yaani kwa mwanaume, (Pete ya fedha) kwa kukubali wanachuoni wote bali inasuniwa hata katika mkono wa kushoto lakini katika mkono wa kulia ni bora zaidi, kwani huo uko kwa wingi katika Hadithi, na kwa kuwa kwake umekuwa ni alama ya Rawaafidh hakuna dalili yoyote ya Hadithi. Na inajuzu kuiwekea Kito cha thamani kinachotokana na dhahabu au kitu kingine au kilicho chini ya dhahabu, na kwa ajili hiyo unatambulika uhalali wa Pete kwani lengo lake ni Pete bila ya kuweka jiwe lolote la thamani".
Na hii ni katika mambo yanayofungamana na uvaaji wa pete kama ilivyo Pete, ama kwa upande wa uvaaji wa Pete yenye umbile maalumu linaloifanya iwe alama ya uchumba au ndoa basi hiyo haina ubaya wowote ule kwa kuwa kitendo hichi kinaingia chini ya desturi.
Mila na desturi hukusanya kila kinachokaririwa katika kauli na vitendo, na iwe vinatokana na mtu mmoja au wengi, na iwe vinatokea kimaumbile au kiakili au vinginevyo. [Rejea: Mila na Desturi kwa Dkt. Ahmad Fahmiy Abu Sinna, Uk. 10, Ch. Mtwuba'at Al Azhar 1947]
Na asili ya mila na desturi ni uhalali kwa kuendelea kuwa kwake hazipingani na Sheria na hivyo kuambatana na uhalali ndani yake.
Sheikh Taqiy Ad Deen Ibn Taimiah amesema katika kitabu cha: [Al Fatawa Al Kubra 31/4, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: Na mila na desturi asili iliyo ndani yake ni kusameheka, basi haizuiwa nazo isipokuwa yale aliyoyaharisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kama sio hivyo basi tutaingia katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Je! Mwaonaje zile riziki alizo kuteremshieni Mwenyezi Mungu, nanyi mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali. Sema: Je! Mwenyezi Mungu amekuruhusuni, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?} [YUNUS 59]
Na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasema vibaya washirikina ambao walianzisha sheria katika Dini yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuyaidhinisha, na wakaharamisha yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuyaharamisha kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Al Anaam: {Na wamemwekea sehemu Mwenyezi Mungu katika mimea na wanyama alio umba, nao husema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miungu yao havimfikii Mwenyezi Mungu, na vilivyo kuwa vya Mwenyezi Mungu huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu (136) Na kadhalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwaua watoto wao ili kuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na kama Mwenyezi Mungu angeli penda wasinge fanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua (137). [AL AN'AAM 137-137]
Na haisemwi kwamba; hakika kitendo hicho ni katika vitendo vya wasio waislamu na kwa hivyo kukifanya kunakuwa ni kujifananisha nao; kwani kama tungekubali hivyo basi mwisho wake ni kuwa katika mazoea, na kinachokuwa katika vilivyozoeleka na kusudio la kufananisha likatoweka hakiwi katika vinavyokatazwa. Basi Mtume S.A.W. ameswalia katika joho ya kishami kama ilivyopokelewa katika vitabu viwili sahihi katika Hadithi ya Al Mugherah Bin Sha'bah, na Imamu Bukhariy alitanguliza kwa mlango huo kwa kauli yake: "Mlango wa kuswalia katika Joho ya Kishami".
Na Al Hafedh Ibn Hajar alieleza hayo katika kitabu cha; [Fathu Al Baariy 473/1, Ch. Dar Al Maarifah] na akasema: "Tafsiri hii inafungamana na kujuzu swala kwa nguo ya makafiri kama hapatakuwepo uhakika wa kuwa kwake na najisi, hakika mambo yalivyo, ameeleza kwa njia ya Sham kwa ajili ya kuchunga tamko la Hadithi, na Sham ilikuwa wakati huo nyumba (nchi) ya Ukafiri".
Na Kadhalika Amiri wa wanaumini Omar Bin Al Khatwab R.A. akawalingania Waajemi katika kuanzisha madiwani na haikuwa kufanya hayo ni haramu. [Rejea: Al Ahkaam As Sultwania kwa Al Mawardiy Uk. 249 Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Waislamu kwa sasa wanavaa nguo ambazo asili yake zilivyo sio za Waislamu na kufanya hivyo hakujazingatiwa kuwa ni kujifananisha nao, kwani asili ya kujifananisha nao imekwishasahaulika na imekuwa sio alama yao tena na mfano wa hali hiyo ni hii Pete; basi panasemwa: ni Jambo lililozoeleka na kuenea baina ya watu, na asili yake imesahaulika - hata kama ilikuwa hiyo-.
Kisha kujifananisha hakuzingatiwi kuwa ni kujifananisha kwa sababu tu ya kuwepo kinachofananishwa bali hapana budi pawepo kusudio na mwelekeo huo ili kupatikane kujifananisha; kwani kujifananisha: ni kuathirika kivitendo, na maana hii inamaanisha kujengeka nia na kuelekea katika kukikusudia kitendo na yote yanayotokana nacho.
Asiyutwiy akasema katika kitabu cha: [Hame' Al Hawame' 305/3, Ch. Al Maktabah At Tawfiqiyqh]: "Na (unatenda) nako ni (kukitekeleza kitendo hicho) kama vile unaposema, "nimekivunja basi kikavunjika, au nimemfundisha basi akaelimika... Kwa hiyo basi, kujifananisha kunakokatazwa maana yake haipatikani isipokuwa kwa kukusudia mwenye kujifananisha na kufanya kwa makusudi; na inaashiria hayo pia Hadithi iliyopokelewa na Imam Muslim katika kitabu chake sahihi kutoka kwa Jabir R.A., amesema: "Mtume S.A.W. aliumwa basi tuliswali nyuma yake na hali alikuwa ameketi, basi akatutazama basi akatuona tukisimama basi akatuashiria tuketi, basi tuliketi, basi alipotoa salamu akasema: "Kama hapo kabla mlikuwa mkifanya kitendo cha Wafursi na Warumi wakiwasimamia wafalme wao na hali ya kuwa wao wameketi, msifanye hivyo, wafuateni Maimamu wenu. Wakiswali hali ya kuwa wamesimama basi nanyi swalini mkiwa mmesimama, na wakiswali hali ya kuwa wameketi basi nanyi mswali hali ya kuwa mmeketi".
Na imekaribia kumaanisha katika kuthibitisha hivyo kutokana na kuwa Wafursi na Warumi walifanya hivyo, na palitokea kweli lakini Maswahaba hawakukusudia kujifananisha huko, na wasifu huo ukawaondoka kisheria.
Na baadhi ya wanachuoni wa Fiqhi wameyataja hayo katika vitabu vyao, Ibn Najiim wa Kihanafiy akasema katika kitabu cha: [Sharhu Al Kanz 11/2, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy]: "Tambua kuwa kufanana na watu wa Kitabu haichukizi katika kila kitu na sisi tunakula na kunywa kama wafanyavyo wao, bali kilicho haramu ni kujifananisha nao kwa kile ambacho kimetajwa vibaya na katika vinavyokusudiwa kwavyo ufananishaji".
Na kwa kuyategemea yaliyotangulia: kuvaa Pete haikatazwi kisheria iwe kwa kutokuwapo sababu au kama alama ya uchumba au ndoa kwa sharti la kutokuwa dhahabu kwa wanaume, na atakayeivaa asiwe na itikadi kuwa yenyewe kama pete, inaathiri jinsi ya kuendelea kuwapo mapenzi baina ya wanandoa wawili na inaleta mkosi iwapo itavuliwa au sehemu yake katika vidole vya mkono ikibadilishwa.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas