Kuuza Paka

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuuza Paka

Question

 Nimenunua paka kwa ajili ya pambo kwa thamani ya juu lengo ni kumfuga, na jambo hili ni la muda mrefu, lakini hivi sasa nataka kumuuza kutokana na kazi nyingi na kushindwa kumhudumia vizuri, lakini hata hivyo baadhi ya marafiki zangu wenye kufuata dini wameniambia kuwa kuna katazo kisharia kuhusu kuuza paka, na kuchukua pesa ya mauzo ya paka ni haramu, wakanipa nasaha ya kumtoa zawadi kwa yule mwenye kuweza kumfuga. Je hii ndiyo hukumu sahihi ya kisharia kwenye hali kama hii?

Answer

 Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Sala na Salamu ziwe kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, pamoja na Masahaba zake na wale waliomfuata. Baada ya utangulizi huu.
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba} [AL BAQARAH 275].
Mwenyezi Mungu amebainisha kuwa kuuza kwa ujumla wake ni halali, amesema Imamu Al-Qurtubiy katika tafsiri yake [3/356, chapa ya Dar Al-Shaab] kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kuiharamisha riba} haya ni katika ujumla wa Qur`ani.
`Na uhalali huu unaendana na kila aina za mauzo isipokuwa biashara ambayo ina tamko la kisharia juu ya uharamu wake na kuiondoa hukumu ya asili, kwa hali hiyo ni kama biashara iliyo na riba ndani yake au mambo mengine yaliyoharamishwa, Shaukaniy anasema katika kitabu cha: [Fat-h Al-Qadir 1/339, chapa ya Dar Al-Kalam Al-Tayyib- huko Beirut] {Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kuiharamisha riba} kwa maana: hakika Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara, na akaharamisha aina katika aina zake, nazo ni uuzaji wenye kukusanya vitendo vya riba.
Uasili wa hali ya uuzaji unaungwa mkono na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini! msiliane mali yenu kwa dhuluma, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe} [AN NISAA 29].
Amesema Imamu Shafi R.A. katika kitabu cha: [Al-Umm, 3/3, chapa ya Dar Al-Maarifa]: asili ya kuuza ni halali pale inapokuwa kuuza huko ni kwa kuridhiana wanaouziana isipokuwa yale aliyoyakataza Mtume S.A.W. katika hayo, na yale yatakayo kuwa na maana iliyokatazwa na Mtume S.A.W., ni haramu kwa ruhusa yake ndani ya maana iliyokatazwa, na yaliyotofautiana na hayo tumeyahalalisha kwa kile tulichokielezea katika halali ya kuuza ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kusudio la kuuza kwa upande wa lugha ni: ubadilishanaji wa kitu kwa kitu kwa njia ya kulipia, na katika maana ya kisharia: ubadilishanaji wa mali kwa njia maalumu. Au yenye makubaliano ya kulipia mali inayopelekea umiliki wa kitu au manufaa kwa njia ya moja kwa moja na wala siyo kwa njia ya ukaribu [Kitabu cha Asnaa Al-Matalib, 2/2, chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy. Na kitabu cha Hashiyat Al-Qalyubiy na Umaira sherh Al-Mahliy, 2/152 chapa cha Issa Al-Halabiy).
Na katika yale yanayokuwa na sharti la kufaa katika makubaliano ya biashara ni kukamilika katika mauzo masharti matano, nayo ni: Kinachouzwa kiwe ni chenye kufahamika, kisafi, chenye manufaa, kinamilikiwa na mwenye kuingia makubaliano, awe na uwezo wa kukikabidhi. [Al-Wajiz kwa sherehe yake ya Fat-h Al-Aziz, 8/112, chapa ya Dar Al-Fikr]. Lazima kinachouzwa kiwe ni chenye manufaa kisharia, kuuza kitu kisicho na manufaa kuuza kwake kunakuwa ni batili ni sawa sawa kwa asili hakina manufaa au kina manufaa lakini si yenye kuzingatiwa kisharia, kwa sababu wakati huo haitazingatiwa kuwa ni mali, na hilo ni kama sharia ilivyoondoa thamani ya pombe hata ikiwa inaweza kuwa na manufaa kwa baadhi ya pande zengine, lakini madhara yake yamekuwa ni makubwa kuliko manufaa yake, basi thamani yake inaondoshwa kisharia. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake} [AL BAQARAH, 219].
Kanuni ya kifiqhi katika hilo ni kuwa hukumu inakuwa kwa jambo lenye kushinda, (kuwa na sifa ya ziada) kwa sababu lile lenye kushindwa linakuwa ni lenye kutumika mbadala wa lenye kushinda, chenye kutumika katika hukumu ni chenye kukosekana [Kitabu cha Almabsuut, cha Al-Sarkhassiy, 1/196 chapa ya Dar Al-Maarifa], basi kuchukua mali kwa mbadala wa kitu kisicho na manufaa kisharia inakuwa ni haramu, ikiwa ni kukataza upotevu wa mali, ni sawa sawa mali yake mtu binafsi au mali ya mtu mwingine, kwa sababu hilo lipo karibu na kitendo cha kula mali za watu kwa batili. [Asnaa Al-Matwalib, 2/9, Fat-h Al-Aziz, 8/118].
Asili katika wanyama wasafi wenye manufaa ni kwamba inafaa kunufaika nao na kuwazungusha kwa makubaliano ya kuuza na kununua na mfano wa hayo, na hilo ni kuwa kwake katika baadhi ya vile vilivyodhalilishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya manufaa ya mwanadamu na kumhudumia pamoja na kumneemesha. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mwenyezi Mungu amevifanya vikutumikieni viliomo mbinguni na kwenye ardhi, na akakujalizieni neema zake, za dhahiri na za siri?} [LUQMAAN, 20]. Na Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri} [AJ JAATHIYAH, 13].
Kunufaika na wanyama kama inavyokuwa kwenye kula kunywa maziwa kuwapanda na kazi za kilimo, pia inakuwa kwa uzuri wa sauti yake kama vile ilivyo kwa ndege aina ya kasuku, na uzuri wa umbile lake na rangi yake kama vile ilivyo kwa ndege aina ya tausi, kunufaika na mfano wa hivi inazingatiwa ni katika mambo ya upendezeshaji yaliyo halali, ni aina ya kunufaika na neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni mlango wa kuzingatia utukufu wa alama zake Mwenyezi Mungu Mtukufu katika uzuri wa kuumba na umakini wa kutengeneza. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyoonekana na yanayoonekana. Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo} [AS SAJDAH, 6: 7]. Na Akasema: {Ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu} [AN NAML, 88].
Imekuja katika Aya za Qur`ani Takatifu yanaoonesha kufaa kufuga wanyama na wengineo kwa lengo la kunufaika na uzuri wao na kujipamba nao ikiwa ni kutafuta furaha ya nafsi, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na farasi, na nyumbu, na punda ili muwapande, na kuwa ni pambo. Na ataumba msivyovijua} [AN NAHL, 08]. Na Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye aliyeifanya bahari ikutumikieni, ili kutokana na humo mpate kula nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayoyavaa} [AN NAHL, 14].
Anasema Imamu Al-Rafii katika kitabu cha: [Fathul aziiz 8/118 – 119) “Fahamu kuwa wanyama walio wasafi ni aina mbili, ya kwanza, ni wale wenye manufaa, kwa hivyo basi inafaa kuwauza kama vile mbuzi, nyumbu na punda, na wanaowindwa ni kama vile paa na swala, na wale wenye kujeruhi ni kama kipanga na chui, na katika aina za ndege ni kama njiwa, ndege wadogo wadogo n.k. Katika hao wapo ambao watu wananufaika na rangi zao au sauti zao kama vile tausi na kwezi, na vile vile tembo na paka pamoja na nyani au ngedere, ambapo wanyama hawa wanafundishwa vitu na kufahamu. Na (aina ya pili) ni wale wasio kuwa na manufaa ambapo haifai kuwauza.
Imepokelewa na Imamu Bukhariy na Muslim katika vitabu vyao kuwa Sahaba Anas Ibn Malik R.A. alikuwa ana ndugu yake mdogo anaitwa Abu Umair, na alikuwa na ndege mdogo akicheza naye anayefanana na kitonombe na ana kucha nyekundu, kauli nyingine: inasema kuwa ni ndege aina ya kasuku Mtume S.A.W, alikuwa pindi anapokuja basi humwona Abu Umair mpole sana akamuuliza: “Abu Umair amefanya nini huyu kasuku”. Katika Hadithi hii kuna dalili ya wazi ya kuwa inafaa kwa mtoto kucheza na ndege, na inafaa kwa wazazi kumuacha mtoto wao mdogo acheze michezo iliyohalali kwake, na inafaa kuvinunua kwa fedha katika vile vitakavyomfurahisha mtoto miongoni mwa vitu halali, na inafaa pia kumfuga ndege kwenye kitundu na mfano wake lakini pia kumpunguza manyoya ya mbawa zake ambapo ndege wa Abu Umair hakukosa kuwa na moja ya sifa hizi mbili, na sifa yoyote katika sifa hizi mbili zilizokuwepo inakutana na sifa nyingine kwa upande wa hukumu. [Fat-h Al-Bary cha Ibn Hajar, 10/584, chapa ya Dar Al-Maarifa – Beirut].
Paka wafugwao na watu, yanakubaliana kwake yale yaliyotangulia utajo wake kwa asili ya hukumu, ambapo mwenye huyo paka ni mnyama twahara inafaa kumfuga pamoja na kummiliki, na anaweza kufuata maelekezo na kufahamika hali yake na sifa zake, kama vile ana manufaa kwa uzuri wa umbile lake na kupata hali ya utulivu, na vile vile ana manufaa katika huduma kwa sababu mwenyewe huwa anawinda panya wale wenye kukera. [Al-Bahri Al-Raiq sherehe ya kitabu cha Kanz Al-Daqaaiq, 6/187, chapa ya Daru Al-Kitab Al-Islamiy].
Na katika yanaonesha utwahara wa paka ni yale yaliyopokelewa na wenye vitabu vinne: kutoka kwa Kabsha bint Kaab Ibn Malik, na alikuwa kwa mtoto wa Abi Qatada, ambapo Abu Qatada aliingia, akasema: nikamjazia maji ya kutawadha. Amesema: mara akaja paka na kuanza kunywa yale maji, na akayamaliza yale maji yote, Kabsha akasema: akanionesha ili niangalie, akasema: unafurahi ewe binti ya ndugu yangu? Nikasema: ndiyo, akasema: Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amesema kuwa: “Paka si najisi, kwa hakika ni miongoni mwa wahudumu kwenu”. Amesema Imamu Tirmidhiy: “Hadithi hii ni nzuri, nayo ni kauli ya wanachuoni wengi miongoni mwa Masahaba wa Mtume S.A.W. pamoja na wale waliofuata na baada ya hao kama vile wakina Imamu Shafi, Ahmad, Is-haqa, ambapo hawajaona ubaya wa paka, na hili ni jambo zuri zaidi katika mlango huu”. Kauli yake Mtume S.A.W, pale aliposema kuwa: “Paka si najisi” ni wazi katika kuthibitisha utwahara wa paka.
Na inaonesha uhalali wa kummiliki paka ni pamoja na Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari na Muslim na tamko kutoka kwa Abu Huraira R.A, toka kwa Mtume S.A.W, amesema: “Mwanamke ameingia motoni kutokana na kumtesa paka wake – alimfungia bila ya kumpatia chakula, wala hata kumuachia huru akale wadudu wa ardhini mpaka paka yule akafa”.
Imebainika kutokana na Hadithi hii kuingia mwanamke motoni hakukuwa kwa sababu ya kumfuga paka na kummiliki, ambapo kwenye huku kufuga hakuna mateso yaliyokuwa haramu kwa dalili ile ya kufaa kufuga ndege na kumuweka kwenye tundu, lakini kilicho muingiza huyu mwanamke motoni ni kule kumnyima chakula na wala hakumuacha mwenyewe akawa anajitafutia wadudu wadogo wadogo ardhini akawa anakula.
Ameelezea Ibn Mundhir kauli ya wanachuoni juu ya kufaa kufuga paka, na jopo la wanachuoni limekubaliana juu ya kufaa kumuuza paka, na katika hili amepitisha Ibn Abbas, Ibn Syreen, Hakamu, Hamada, Malik, Thauriy, Shafiy, Ahmad, Is-Haq, Abu Hanifa na wengine wenye mitazamo. Na wakajenga hoja kuwa paka ni mnyama mwenye twahara na mwenye manufaa, na kuna masharti yote ya kuuza kwa hiyari, na kwa hiyo inafaa kumuuza kama vile wanavyouzwa punda na nyumbu. [Kitabu Al-Majmuu 9/274, chapa ya Matba Al-Muniriya]
Na kwa vile kuuza kumewekewa utaratibu wa kufikia katika kukidhi haja na kunufaika na manufaa yaliyo halali, ili kila mmoja ayapate manufaa ya kile kilichokuwa mkononi mwa mwenzake katika vile vilivyokuwa halali kunufaika navyo. Na paka ni halali kunufaika naye, hivyo inapaswa kuwa ni sharia kumuuza kwake, (Kitabu Al-Mughniy, 4/175, chapa ya Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy). Na vile vile kuuza kukiendana na manufaa ya kweli halali moja kwa moja kunufaika nayo inakuwa imekidhi hitajio la sharia, kwa sababu uhalali wake unakuwa ni sababu na njia ya kuhusisha kuondoa moja kwa moja mivutano, na kuondoa mivutano ni muhimu, ambapo mivutano hiyo ndicho chanzo kikuu cha uharibifu, na kwa hili imekuwa ni lazima kwa Waislamu kuangalia umuhimu huo, [Kitabu Badaai As-Sanaii, 5/143, 7/2, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Amesema mwanachuoni Al-Qurafiy katika kitabu cha [Al-Furuq” 3/290, chapa ya Alam Al-Kutub]: na hii hapa kanuni, Kinachotakiwa na mtu wa sharia mafanikio binafsi na kuondoa mada ya uharibifu na fitina mpaka akaifikia katika hilo kauli ya Mtume S.A.W. aliposema: “Hamtaingia peponi mpaka mpendane”.
Vile vile katika yaliyochukuliwa na Jamhuri ya wanachuoni kuwa ni dalili ni kuwa kwa umiliki kama ni sababu ya matumizi, na manufaa halali yanahalalisha kunufaika nayo, basi inafaa kwake kuchukua malipo, na halali kwa mwingine kutumia mali yake katika hilo, hali ya kuifikia na kukidhi haja yake katika hilo, na kama vitu vingine vilivyo halali kuuza, kila chenye kumilikiwa halali kunufaika nacho inafaa kukiuza isipokuwa katika vile vilivyoondolewa na sheria [Kitabu Al-Mughniy, 4/174].
Kuna kundi la wanachuoni wamesema kuwa kuuza paka ni jambo linalochukiza, na katika hilo amesema Abu Haraira R.A. na Mujahid pamoja na Taus na Jabiri Ibn Zeid [Al-Majimuu, 9/2], nao ni mapokezi ya Ahmad yaliyopitishwa na Abu Bakr [Al-Mughniy, 4/175]. Na wakasema baadhi ya wafuasi wa Imamu Malik kuwa kuuza paka kwa lengo lengine lisilokuwa kuichukua ngozi, haifai kutokana na uharamu wa kumla mnyama huyu, na kauli ya kuchukiza kumla inapelekea pia kuchukiza kumuuza.
Amepitisha Imamu Al-Juziy kuwa inachukiza kuuza paka, katika [Kitabu Mawahib Al-Jalil, 4/268, chapa Dar Al-Fikr], lakini usahihi katika madhehebu ya Imamu Malik ni kauli yake kuwa inafaa kuuza paka ili kunufaika naye akiwa hai na hata ngozi yake pia, haya yanaonesha uwazi wa yale yaliyokuja katika kitabu cha: [Hashiyat Al-Dusuqiy ya sherehe ya Kitab Al-Kabir, 3/11, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]. Na katika wanayoshikamana nayo wale waliosema kuwa inachukiza ni Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim katika kitabu chake toka kwa Abu Zubeir amesema: “Nilimwuliza Jabir, kuhusu thamani ya mbwa na wanaotumia meno kama silaha. Akasema amekemea Mtume S.A.W. wanyama hao” miongoni mwa wanyama wenye sifa hiyo ni pamoja na paka.
Na kuchukua uwazi wa Hadithi lakini wamechukua kama ni dalili ya uharamu wa kuuza paka, kwa dalili ya kuwepo neno hili "kukemea", ambapo kukemea ni katika aina ya ukatazaji mkali, na vile vile Hadithi iliyopokelewa na Jabir Ibn Abdillah kuwa inachukiza kuuza mbwa na wanyama wanaotumia meno kama silaha. Wakasema: hii ni Fatwa ya Jabir kwa kile kilichopokelewa wala hatufahamu Sahaba aliyetofauti na hilo [Kitabu Al-Mahaly cha Ibn Hazm, 7/498, chapa ya Dar Al-Fikr].
Jopo la wanachuoni limezijibu hoja za wenye kupinga kwa kutumia Hadithi hizi ni kuwa, kusudio la paka lililopo hapa ni wale paka shume na ni kwa sababu ya kutokuwa na manufaa tofauti na hawa paka wanaofugwa na watu. Vile vile wamejibu kuwa katazo lililopo katika Hadithi si katazo la uharamu, lengo la Hadithi hii ni kuruhusu kuenea paka wa kufugwa na kuazimwa kwake gharama ya kifedha kama ilivyo kawaida [Al-Majmuu 9/274]. Na katika majibu ni kuwa katazo linafungamana na paka wasiomilikiwa kwa kuuzwa, au wasio na manufaa kwa mnunuzi [Kitabu cha Al-Mughniy, 4/175].
Ama kwa upande wa Hadithi ameweka wazi Ibn Abdulbarr kuwa, haifai katika mlango wa Hadithi [Angalia: Kitabu cha Tamheed, 8/2403, chapa ya Wizara ya Waqfu – Morocco] na akaashiria Ibn Rajab Al-Hanbaliy sababu ya upokezi huu [Angalia: Kitabu jaamii Al-Ulum wa Al-Hikam 2/451, chapa ya Taasisi ya Risala].
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia na katika swali lenyewe: Ni kuwa inafaa kwako wewe muulizaji na kwa wengine kumuuza paka wako, na ni halali kwako kunufaika na thamani yake kwa mujibu wa makubaliano jopo la wanachuoni, ikiwa huhitaji thamani ya pesa ya paka badala yake ukamzawadia mmoja wa marafiki zako ili kujitofautisha kati ya wale walio haramisha thamani ya paka na wale waliosema kuwa inachukiza miongoni mwa watu wa elimu, basi huo unakuwa ni utumiaji unaopendeza, na una malipo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas