Talaka kwa Sababu ya Utasa wa Mume

Egypt's Dar Al-Ifta

Talaka kwa Sababu ya Utasa wa Mume

Question

 Mwanamke aligundua baada ya kipindi kirefu cha ndoa kupita bila ya kupata mimba kuwa mume wake alikuwa tasa, kwa mujibu wa kipimo cha matibabu kilichothibitisha hivyo. Je, atafanya dhambi kama akiomba talaka kwa sababu anahitaji kukidhi haja zao za ujauzito na hamu ya kuwa na watoto? Kama akiamua talaka, katika hali hii haki zake mke za kifedha zitaondolewa au atakuwa na haki ya kudai na kutosamehe haki hii?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Tasa: ni mwanamke asiyeweza kuzaa, [Al-Miswbah Al-Muniir kwa Al-Fayoumi 2/423, Al-Maktaba Al-Ilmiyah].
Katika istilahi ya wanavyuoni wa Fiqhi utasa una maana: kutokuwa na uwezo wa kuwa na watoto katika kipindi cha muda wa kawaida wa kupata uzazi kati ya wanandoa wasio na ugonjwa wowote, na hasa usalama wa sehemu za siri na ukamilifu na kuanzisha uwezekano wa ngono kama kawaida. Wanavyuoni wametofautisha katika maneno yao kati ya mtu asiyeweza kufanya ngono, aliyehasiwa, aliyekatwa uume wake na tasa, kuonesha kwamba mtu ambaye ni tasa katika desturi yao ni mtu kamili anayeweza kufanya ngono, hana tofauti na mtu wa kawaida isipokuwa hana uwezo wa kuzaa.
Wengi wa wanavyuoni wamesema kuwa utasa sio ugonjwa unaothibitisha chaguo la kuvunja mkataba wa ndoa. Hivyo kwa sababu ugonjwa unaothibitisha chaguo la kuvunja mkataba wa ndoa au ombi la talaka ni mmoja wa wanandoa kupatwa na mambo yanayosababisha madhara kwake au mambo yanayomzuia kustarehe au kufikia kilele cha kustarehe, hii ni kinyume na madhumuni ya awali ya ndoa, ambayo ni makazi, upendo na huruma kati ya mume na mke, kama ilivyoelezwa katika Aya hii: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu} [AR RUUM: 21].
Aliyehasiwa hakuweza kuzaa pamoja na ukosefu wa viungo vya mwili wake, hata hivyo, haithibitishwi kwa mke wake chaguo la kuvunja mkataba wa ndoa, basi katika nafasi ya kwanza ni tasa, ambaye hana kasoro katika viungo vya mwili wake.
Ingawa uzazi ni matunda miongoni mwa matunda muhimu ya ndoa na lengo muhimu pia, lakini kuchelewa kwa matunda haya au kutotokea kwake hakusababisha ndoa kubatilika, ndoa ina malengo mengi yasiyokuwa uzazi, kama vile; usafi wa moyo – nao ni muhimu zaidi – mshikamano, na kuimarisha uhusiano wa kijamii kati ya jamaa na wengine. Na kama kuna upinzani kati ya kutozaa na ndoa, basi hairuhusiwi kumwoa mwanamke ambaye ni tasa, au inampa mume chaguo wakati mkewe anapofikia umri wa kukatika hedhi, na hakuna yeyote aliyesema hivyo.
Mkuu wa maimamu Al-Sarkhasiy Al-Hanafiy alisema katika kitabu chake cha: [Al-Mabsoot 18/157, Dar Al-Maarifa]: “Mtoto ni matunda, basi hastahili kwa ndoa, na kwa hivyo, kama mke alikuwa mzee au ni tasa, mume hawi na chaguo”.
Al-Hatwab Al-Malikiy anasema katika kitabu cha: [Mawahib Al-Jaliil” 3/404, Dar Al-Fikr]: “Kuhusu utasa, inaonekana kwamba siyo lazima kumwambia kwa utasa huu; kwa sababu sio kasoro kujitakia”.
Al-Dasouqi alisema katika ufafanuzi wake juu ya “Al-Sharhul Kabiir” [2/278, Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiah]: “Kutozaa hakusababishi madhara kama vile; utasa”.
Imam Al-Shafiy R.A. anaamua kwamba kupoteza uwezo wa kuzaa hakumpi haki ya chaguo, hata ikifichwa hali hii mpaka kufunga ndoa, kinyume na uwezo wa kuwa na ngono, ambao unathibitisha chaguo. Imam Al-Shafiy R.A. alisema katika kitabu cha: [Al-Umm" 5/43, Dar Al-Maarifa] "Kama akimwoa, ambapo anasema: Mimi ni tasa, au hakusema hata akamwoa kisha akakiri kuwa ni tasa, mkewe hakuwa na chaguo , hivyo yeye hajui kuwa yeye ni tasa kamwe hata kufa kwake; basi hana chaguo katika kuzaa, lakini chaguo lake ni katika ngono siyo katika kuzaa mtoto”.
Al-Amrani Al-Shafiy anasema katika kitabu cha Al-Bayan [9/294, Dar Al-Menhaj- Jeddah] akisema: “Kama mke akiwa ni tasa hazai, au mume akiwa ni tasa hazai, basi hakuwi sababu ya kuwa na chaguo; kwa sababu hali hii haizuii starehe kamili”.
Na iliyotajwa kwa mujibu wa wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Ahamad Ibn Hanbali ni kwamba utasa hauleti haki ya chaguo. Al-Bahoutiy Al-Hanbaliy katika kitabu cha: [Ghatul Muntaha 5/146, pamoja na Sharhu Matalib Ulunuha, Al-Maktab Al-Islami] alisema: “Kama kwamba alikuwa ni tasa au alikuwa akifanya ngono pasipo na manii basi hana chaguo, kwa sababu hali yake katika ngono siyo katika manii”
Hasan Al-Basri miongoni mwa wanavyuoni wa Fiqhi baada ya Maswahaba (Tabiina) alisema kwamba utasa sio kasoro inaoleta haki ya chaguo, lakini hakufuatilia mtazamo wake huu; kwa sababu utasa sio kasoro ya wazi inayosababisha kuepukana au inayozuia kustarehe. Imamu Ibn Qudaamah Al-Hanbali anasema katika kitabu cha: [Al-Mughni 7/142, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy], baada ya kutaja dosari zinazothibitisha chaguo wa kuvunja ndoa hakutaja utasa miongoni mwa dosari hizi: “Isipokuwa katika dosari hizi hakuthibitishwi chaguo ... na hatujui hitilafu katika hali hii kati ya wanavyuoni, lakini Al-Hassan alisema: Kama mume au mke ni tasa wanachagua. Ahmad angependa kujua hali yake, akisema: Labda mke wake anataka kuzaa mtoto, na hali hii katika mwanzo wa ndoa, Lakini kuvunja ndoa hakuthibitishi kwake, hata kama ikithibitika katika hali hii inathibitika katika hali ya mke alikatika hedhi yake”.
Ingawa wengi wa wanavyuoni wameafikiana kwamba utasa sio kasoro kwa mume, lakini kama mwanamke ataathirika na ukosefu wa uwezo wa mume wake wa kutopata watoto pamoja na kuhakikisha kwamba mume ni sababu ya hivi, ana haki ya kuomba talaka na hana dhambi kwa kuiomba; kwa sababu ni kunyimwa mke kutokana na kustarehe kwa upendo wa umama na ni kumnyima kwake kutokana na hisia ya kimaumbile inayopanda mpaka kiwanngo cha mahitaji, yaani: yale ya msingi ni kwamba haja inakuwa kama dharura ikiwa ni ya umma au ni maalum [Rejea: Al-Ashbah wan Nadhair kwa As-Soyuti uk 88, Dar al-Kutub Al-Ilmiyah], ingawa uvumilivu kwa mke ni bora zaidi, na vile vile sayansi za dawa zinaendeleza siku baada ya siku, pengine Mwenyezi Mungu atawafanyia njia na atawaruzuku uzazi kwa upande wasioutazamia.
Kuhusu yaliyopokelewa kutoka kwa wenye Sunan kutoka kwa Thawbaan R.A kuwa Mtume, S.A.W., alisema: “Mwanamke yeyote ambaye anamuomba mume wake talaka pasipo na dharura basi harufu ya peponi ni haramu kwake”. Kitisho kilichomo katika Hadithi hii maana yake ni kwamba kama ombi la talaka halikuwa kwa sababu ya dharura au ya lazima inayohitajika. Imamu Al-Manaawi alisema katika kitabu cha: [Faidh Al-Qadiir 3/138, Al-Maktabah Al-Tujariyah Al-Kubra]: “Dharura ni: shida; yaani: katika hali isiyo ya shida inayomlazimisha kuomba talaka, kama akiogopa kutosimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu katika mambo yanayotakiwa kufanya kuhusu urafiki mzuri kwa sababu ya kumchukia mume au anamdhuru mpaka anajitenga naye”.
Kama mume ambaye ni tasa akijibu ombi la mkewe kuhusu talaka, na akamtaliki haki za mke za kifedha haziondolewi mara moja tu, isipokuwa mkewe akimsamehe tu, na ana haki ya kufikisha ombi la kujitenga mahakamani; kwa ajili ya kutazama ukweli wa madhara ambayo kwa ajili yake mke anaomba talaka. Kama madhara yakithibitishwa jaji atamwamuru mume kumtaliki au jaji mwenyewe anamwachanisha na kutokana na mumewe pasipo na kurejea na haki zake mkewe za kifedha haziondolewi, na kama madhara hayathibitishwi mke anaweza kusamehe katika haki zake za kifedha au baadhi yake na atajitenga kutokana na mumewe.
Kama ilivyoelezwa katika Ibara ya sita kutoka Sheria ya familia iliyorekebishwa na Sheria nambari ya 100 kwa mwaka wa 1985 kwamba: "Kama mke akidai kwamba mume anamdhuru kwa wasiyoweza kukaa pamoja anaweza kuomba kutoka kwa jaji kujitenga naye, katika hali hii jaji anaweza kumtaliki kutoka kwa mumewe pasipo na kurejea ikithibitishwa madhara na kukosekana uwezo wa kuwapatanisha, kama akikataa ombi, kisha malalamiko yanakariri mara kwa mara na madhara hayakuthibitishwa jaji atapeleka waamuzi wawili na atahukumu kwa mujibu wa ibara za (7, 8, 9, 10 na 11)”.
Katika ibara ya 10 ya Sheria ile ile inasema: "1. Kama ubaya wote ni kutoka kwa mume waamuzi wanaweza kupendekeza kumtaliki kwa talaka moja isiyorejewa pasipo na kuondolewa kwa haki za mke zinazotokana na ndoa na talaka 2. Kama ubaya wote ni kutoka kwa mke waamuzi wanaweza kupendekeza kutaliki mkabala wa pesa maalum ni lazima kulipwa na mke.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, inaonesha kuwa utasa wa mume sio kasoro inayosababisha kuvunja ndoa kwa mujibu wa mtazamo wa wanavyuoni wengi wa Fiqhi, na kwamba hakuna ubaya wowote kuwa mwanamke anaweza kuomba talaka kutoka kwa mumewe ambaye ni tasa, lakini uvumilivu kwake ni bora zaidi. Vile vile mke ana haki ya kufikisha ombi lake mahakamani kama hawakupatanishwa, katika upande wa haki zake za kifedha.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas