Kutenguka Udhu Wakati wa Kuitekelez...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutenguka Udhu Wakati wa Kuitekeleza Ibada ya Tawafu.

Question

 Ni nini anachofanya mwenye kutengukwa na Udhu wake wakati wa Kutufu? Je, akamilishe Tawafu yake au aanze tawafu upya?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Jamhuri ya wanazuoni wa Fiqhi, miongoni mwa madhehebu ya Imamu Malik, Shafi, na Hanbali, wanaona kuwa kujitwaharisha kutokana na haja ndogo, kubwa, janaba, na kutokana na najisi ni sharti la kusihi Ibada ya kutufu kwa uwazi, ikiwa Tawafu hii ni ya baada tu ya Kuwasili Makkah, Ziara, au ya Kuaga, kwa hiyo mtu akianza Tawafu bila ya twahara, basi Tawafu yake ni batili na haizingatiwi kabisa. [Rejea: Ash-Sharh Al-Kabiir, na Ad-Dardiir; 2/32, Ch. ya Dar Al-Fikr; Nihayat Al-Muhtaaj, na Ar-Ramliy; 3/279, Ch. ya Dar Al-Fikr; Mughniy Al-Muhtaaj, na Al-Khatiib Ash-Shirbiniy; 2/244, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah; Al-Inswaaf, na Al-Mardawiy; 4/17, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy].
Wafuasi wa madhehebu ya Hanafi walielekea kuwa twahara si sharti la usahihi wa Tawafu, ingawa ni wajibu kwake, kwa hiyo aliyetufu bila ya twahara basi Tawafu yake ni sahihi, lakini ni wajibu kwake kuifanya tena, muda wa kuwa yuko Makkah, na kama si hivyo analazimika kutoa fidia. [Rejea: Badaiu’ As-Sanaii’: 2/129, Ch. Ya dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Na maana ya kuifanya tena, kwa rai ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafi, ni kuifanya tena Tawafu kwa ukamilifu wake; ama akitengukwa na udhu wakati wa kuitekeleza Tawafu, basi inajuzu kukamilisha Tawafu yake, na ataelezwa (hukumu yake) kama yule aliyeanza Tawafu yake bila ya twahara kabisa, au atatawadha upya na kukamalisha Tawafu yake bila ya kuianza upya.
Imamu Muhammad Ibn Al-Hasan katika kitabu chake [Al-Hujjah Ala Ahl Al-Madinah] amenukulu kutoka kwa Imamu Abu Hanifa kuwa: “Anayepatwa na kitu cha kuutengua udhu wake wakati wa kutufu Kaaba, au wakati wa kufanya Saiyu kati ya Safwa na Marwa, au katikati ya hivi, hapo akipatwana jambo hili wakati akitekeleza sehemu ya Tawafu au Tawafu yote na bado hajarukuu rakaa mbili za Tawafu, hapo atatawadha na kukamilisha Tawafu, kisha ataswali rakaa mbili; yaani katika hali ya kutenguka udhu atatawadha kisha atakamilisha Tawafu”. [2/281, Ch. Ya Alam Al-Kutub].
Al-Kasaniy katika [Al-Badaii’] anasema: “Kuhusu twahara kutokana na haja ndogo, kubwa, janaba, hedhi, na nifasi sio sharti la kujuzu Tawafu, na sio fardhi kwa rai yetu, bali ni wajibu hata inajuzu kuitekeleza Tawafu bila twahara. Na kwa rai ya Imamu Shafi ni faradhi na Tawafu haisihi bila twahara. Na hoja yake ni ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa amesema : “Tawafu ni Swala, lakini Mwenyezi Mungu ameruhusu kutamka maneno ndani yake”, na ikiwa ni Swala basi Swala haijuzu bila ya twahara.
Na hoja yetu ni kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na waizunguke Nyumba ya Kale, (Nyumba kongwe – AlKaaba)}. [Al Haj: 29], hapa aliamuru kuitekeleza Tawafu kwa uwazi na mbali na sharti la twahara, na haijuzu kuzuia (tamko la) uwazi wa Qur`ani kwa habari ya mpokeaji mmoja, kwa hiyo (Hadithi) inafasiriwa kwa maana ya tashbihi (kufafanisha), kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na wakeze ni mama zao}. [Al Ahzab: 6], yaani wakeze ni kama mama zao, yaani Tawafu ni kama Swala, ama katika thawabu au kutokana na asili ya faradhi ya Tawafu ya ziara; kwa sababu maneno ya tashbihi hayana uwazi, kwa hiyo inafahamika kwa maana ya ulinganiaji katika baadhi ya sifa, kwa mujibu wa Qur`ani na Sunna.
Au tunaweza kusema: Tawafu inafanana na Swala lakini siyo Swala kwa hakika, na kwa njia ya kuwa siyo swala kwa hakika basi twahara haiwi faradhi kwake, na kwa njia ya kuwa inafanana na Swala basi twahara kwake ni wajibu, kwa mujibu wa dalili mbili kwa kadiri iwezekanavyo.
Na kama twahara ni miongoni mwa wajibu wa Tawafu, na kama mtu akitufu bila ya twahara wakati bado yuko Makkah, atawajibika kutufu upya; kwa sababu kutufu upya ni mbadala wake kwa mithili yake, na mbadala kwa mithili ni bora zaidi; kwa sababu maana ya mbadala ni kusahihisha kosa, nayo inatakiwa. Na kama akitufu upya wakati wa Siku za kuchinja basi hana kosa, lakini akiahirisha mbadala basi analazimika na damu, kwa mujibu wa kauli ya Imamu Abu Hanifa”. [2/129].
Kuhusu rai ya wengi wa wanachuoni kuwa: Akitengukwa udhu wakati wa Tawafu atakwenda kutawadha; kwa sababu twahara ni sharti la kuifanya Tawafu, lakini kuna hitilafu kuhusu kukamilisha Tawafu au kuifanya upya.
Rai sahihi ya wafuasi wa madhehebu ya Shafi kuwa: atakamilisha Tawafu yake bila ya kuifanya upya, yaani kuanzia kwenye mahali alipotenguka udhu, na hafanyi tena safari (sehemu alipoanza) aliyotenguka udhu ndani yake.
Imamu Ash-Shirbiniy katika [Mughniy Al-Muhtaj: 2/244] anasema: “… akitengukwa udhu wake kwa makusudi atatawadha, na ni bora zaidi ajitakase ili ikusanye kuosha; na ataanza Tawafu kwa mahali alipotengukwa udhu wake, akiwa kwenye pembe ya jiwe jeusi (Rukn) au siyo; na kwa rai nyingine: ataanza upya Tawafu, kulingana na Swala, na tofauti hapa kuwa: inajuzu katika Tawafu ile isivyojuzu katika Swala, na kama akipatwa kwa haja basi inatofautiana na makusudi kuhusu kukamilisha Tawafu hali ya muda wa kuacha Tawafu ni mfupi, na hata muda ukiwa ni mrefu kwa rai sahihi zaidi.
Na kama nguo yake, mwili wake au mahala pake pa kutufu kumepatwana najisi isiyosameheka kwake, au sehemu ya uchi wake imefichuka, kama vile: nywele za mwanamke huru au kucha za mguu wake zimefichuka basi haisihi ilivyofanywa baada ya hayo, na kama sababu imekwisha basi atakamilisha Tawafu, kulingana na mwenye kutenguka udhu, na ikiwa muda wa kuacha Tawafu ni mrefu au mfupi kama ilivyopita hapo juu, kwa sababu kutoshurutishwa kudumu kama vile katika udhu; na kwa sababu Udhu na Tawafu zote ni ibada, na inajuzu kuziingiza ndani yake kitu kisichoambatana nazo, na kinyume cha Swala; lakini ni bora kutokana na Sunna kuanza upya Tawafu, kujiepusha kwa hitilafu kwa rai ya aliyeiwajibisha”.
Ash-Sharwaniy anaeleza katika Hashiya zake katika At-Tuhfa katika kauli ya mtungaji wa Al-Minhaaj: (aliunda), akisema: “(aliunda) kinyume na kuzimia, wazimu, ataanza upya kwa sababu ya kutoka kwake kwa ibada. Al-Adhri’i anasema: kuhusu aliyetoka kwa ibada kwa sababu ya kuzimia: Imamu Shafi aliamua kuwa ataanza upya udhu na Tawafu ikiwa ni karibu au mbali, na tofauti hapa ni kutokuwa na jukumu, kinyume na mwenye kutenguka udhu. Na inafahamiwa kuwa wazimu ni mfano wa kuzimia, vile vile mwenye kulewa, akiwa mwenye kusudi au la”. [4/75, Ch. Ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy].
Wafuasi wa madhehebu ya Malik na Hanbal walisema: aliyetengukwa udhu wakati wa kuifanya Tawafu ataianza upya, na hairundi ilivyokwishafanywa. Katika [Ash-Sharh Al-Kabiir] na Ad-Dardiir kwenye maneno ya Tawafu: “… uundaji kwa Tawafu (ulivunjika kwa haja) iliyofanyika hata kwa kusahau; na kama kujengea ulitenguka basi kuanza upya ni wajibu ikiwa Tawafu ni wajibu, au siyo wajibu pamoja na kufanya haja kwa makusudi”. [2/31, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Al-Kharshiy anasema: “kujengea ulitenguka kwa haja, yaani haja ikifanywa wakati wa kuifanya Tawafu kwa kusudi au kwa husahau, yaani kusahau kuwa anafanya Tawafu, au anapatwa kwa haja, hapo Tawafu inabatilika na kuzuia ujengaji kwa ilivyofanywa kwa safari za Tawafu, na hayo kwa rai mashuhuri, na ikiwa Tawafu ni wajibu au siyo; na ataanza wajibu baada ya twahara, kinyume na isiyo wajibu, ila katika hali ya kuifanya haja kwa makusudi; hapo akijengea basi yeye ni kama vile asiyetufu kabisa, kwa rai ya Ibn Al-Qasim, kinyume na rai ya Ibn Habiib”. [Sharh Mukhtasar Khalil: 2/314, Ch. Ya Dar Al-Fikr].
Wafuasi wa madhehebu ya Malik walivua sura miongoni mwa uwajibikaji wa kuanza upya, nayo ni: damu ikitoka kwenye pua yake, hapoatjenea baada ya kuosha damu, kwa sharti la kutopita mahali karibu, mfano wa Swala; na mahali pasipo mbali sana, na hakanyagi unajisi. [Rejea: Ash-Sharh Al-Kabiir: 2/32].
Al-Bahutiy katika [Sharh Al-Muntahaa] anasema: “(ataanza Tawafu kwa haja) iliyo makusudi au siyo, baada ya kupata twahara,mfano wa Swala”. [1/574, Ch. Ya A’alam Al-Kutub].
Katika [Al-Insaaf] na Al-Mardawiy: “akitenguka udhu wakati wa Tawafu, au akiikata kwa muda mrefu ataianza) na hii bila shaka ni madhehebu sahihi; kwa sababu kudumu ni sharti”. [4/17].
Kwa mujibu wa yaliyotangulia: akitenguka udhu wake wakati wa Tawafuatajengea kwa aliyotufu, na hataanza upya kwa kauli ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafi na Shafi, kwa rai inayotambuliwa; na ataanza upya kwa kauli ya wafuasi wa madhehebu ya Malik na Hanbal.
Na asili ya hitilafu kati ya kujengea na kuanza upya ni kushurutishwa kudumu kwa safari za tawafu; hapo wanaokushurutisha kama vile wa Malik na wa Hanbal wakisema: ataanza upya akivunjwa udhu wake; kwa kuwa kuvunjwa udhu na udhu mpya ni kukata kudumu; na wale wasioshurutisha kudumu kama vile wa Hanafi na wa Shafi walijuzisha kujengea kwa safari zilizofanywa kwa Tawafu.
Na dalili za kila upande ni nguvu; kwa hiyo inajuzu kufuata upande wowote, hasa suala hili ni la jitihada, na hakuna matini maalumu yenye nguvu zaidi.
Na wanaoshurutisha kudumu walitoa dalili ya kauli yake Mtume S.A.W: “Tawafu kuzunguka Nyumba ni Swala”, [wameipokea Ahmad na An-Nasaii, na kudumu kunashurutishwa katika Swala, na Tawafu ni ibada inayoambatana na Nyumba, kwa hiyo kudumu ni sharti lake kama swala. Na dalili ya wasioshurutisha kudumu ni kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na waizunguke Nyumba ya Kale, (Nyumba kongwe – AlKaaba)}. [AL HAJ: 29], ambapo Mwenyezi Mungu aliamuru kwa Tawafu na hakushurutisha kudumu, na hii ni dalili ya usahihi wake pamoja na kukata hata ikiwa kwingi, na pia ni ibada inayosihi pamoja na baadhi ya kukata, basi inasihi kwa kukata kwingi kama vile matendo yote ya Hija.
Hivyo kila upande ulitoa dalili ya jumla ya Athari zilizopokelewa na Masahaba, na dalili zao zote zinazingatiwa.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: aliyetengukwa na udhu wake wakati wa Tawafu, analazimika atawadhe kisha aendelee na Tawafu yake pale alipoishia bila ya kuanza upya, ingawa ni bora zaidi aanze upya kwa ajili ya kutoka kwenye hitilafu. Kuhusu aliyeanza kabisa tawafu hali ya kuwa na twahara kisha akatenguka udhu wakati wa Tawafu, na akakamilisha Tawafu yake hali hakuwa na twahara, kisha akarudi nyumbani kwake, na hakuweza kufanya upya tawafu yake, basi Tawafu yake ni sahihi; kwa kuwafuata wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi wanaoona uwepo wa uwajibu wa twahara kwa mwenye kutufu bila ya kuwepo sharti, kwa kujua kuwa: wanazuoni wote wanakubaliana kutojuzu kuanza kabisa Tawafu bila ya twahara.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas