Hukumu ya Kumwoa Mtoto wa Mkeo.

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kumwoa Mtoto wa Mkeo.

Question

 Mwanamume mmoja alimwoa mwanamke mwenye watoto wa kiume na wa kike, na baada ya kumpa talaka mke huyo, akataka kumwoa binti wa mtoto wa mke wake, Je ndoa hiyo ni Halali au Haramu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Vizuizi vya ndoa miongoni mwake huhusiana na ukoo au ukwe au kunyonya pamoja, na huenda vikawa vya kudumu au vya muda; Basi miongoni mwa vizuizi vya kudumu ni vile alivyo vitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat An Nisaa katika kauli yake: {na watoto wenu wa kambo walio katika ulinziwenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu}. [AN NISAA 23]
Rabiba ni neno la Kiarabu lenye maana ya mtoto wa kike wa Mkeo. Na neno hili linatokana na Rabu kwa maana ya kurekebisha: kwani mume wa mama yake anamfanyia mambo yake na kuirekebisha hali yake. Na mwanaume huitwa Rabiibu.
Na wanazuoni wamekubaliana kuwa iwapo mume atamwingilia mkewe basi ataharamishiwa kumwoa binti yake na binti wa mtoto wake wa kiume na mtoto wa binti yake na kushuka chini, kwa nasaba au kwa kunyonya, na uharamu huu ni uharamu wa kudumu. Ndoa haitasihi kwa mwanaume hata baada ya mwanaume huyo kumwacha mwanamke aliyemwingilia ambaye ndio sababu kuu ya uharamu huu. Na juu ya hayo ni madhehebu manne, na hizo ni matini zao ambazo zinabainishia hayo:
Ibn Al Hamam akasema baada ya kuutaja uharamu wa binti wa mwanamke aliyemwingilia: "Na katika hili suala, watoto wa mtoto wa kike au wa kiume wa mke pia wanaingia katika uharamu huu na kushuka chini, kwani jina hili linawakusanya wote kinyume na wale walio halali kwa watoto wenu wa kiume na wazazi wao kwa kuwa hili ni jina maalumu na kwa hivyo inajuzu kumwozesha mama wa mke wa mtoto wa kiume na mtoto wa kike pia, na inajuzu kwa mtoto wa kiume pia kumwoa mama wa mke wa baba na binti yake" [Fathu Al Qadeer 210/3, Ch. Dar Al Fikr].
Na Al Kassaniy akasema: "Binti wa mkwe anaharamishwa, na watoto wake wa kike, kike, na watoto wake wa kiume hata kama walishuka chini.
Ama binti wa mkwe anaharamishwa kwa matini ya Qur'ani tukufu, kama alikuwa amemwingilia mke wake, lakini kama hakumwingilia basi haharamishwi kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu}.
Ni sawa sawa iwe binti huyo wa mkewe yuko chini ya ulezi wake au hapana kwa mtazamo wa wengi wa wanazuoni. Na baadhi ya watu wanasema: hawi haramu kwake isipokuwa atakapokuwa chini ya malezi yake. Na sisi tunaona kuwa kuweka maandiko katika hukumu ya kinachopewa wasifu maalumu hakumaanishi kuwa hukumu yake katika kisichopewa wasifu huo ni tofauti nacho, kwani uwekaji wa maandiko haumaanishi umaalumu na kwa hivyo uharamu wa binti wa mke unathibiti kwa mwanaume aliyemwingilia mama wa binti huyo huku binti huyo akiwa chini ya malezi yake kwa Aya hiyo".
Na ikiwa hatakuwa chini ya ulezi wake basi atakuwa haramu kwake kwa kuthibiti dalili nyingine nayo ni kuwa kumwoa kutapelekea kuukata undugu iwe binti huyo yuko kwake kimalezi au hapana isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametaja Malezi kwa, mujibu wa kwamba mila na desturi za watu zinaona kuwa binti wa mke anakuwa chini ya Malezi ya Mume wa mama yake kwa kawaida, na kwa hivyo maneno yameuondosha upenyo wa mila na desturi.
Na kuhusu watoto wa kike wa mke na watoto wa kike wa binti yake mke kama wakishuka chini, uharamu wao unapatikana kwa makubaliano ya wanazuoni wote, na huwenda tukawa tumetaja maana inayokubalika kiakili sio kwa kuwepo maandiko , isipokuwa katika kauli ya anayeona kuwa kuna ukusanyaji baina ya uhalisia na uazimaji wa maana katika tamko moja panapowezekana kuzifanyia kazi rai zote mbili". [259/2, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Katika kitabu cha [Asharh Al Kabeer kwa Ad Dardere]: "Na imeharamika kwa mtu yeyote watoto wa kizazi cha mwanzo na ni haramu kufunga nao ndoa, na hata kama hajapata ladha yoyote kwa kizazi cha awali cha mke wake ambao ni mama mkwe na kuendelea juu, na hiyo ni maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mama wa wake wenu}.
Na imeharamishwa kwa kupata ladha kwa mke wake hata kama ni baada ya kifo chake, hata kwa kuangalia tu, na ikiwa itapatikana hata kama hakukusudia hivyo sio kama atakusudia tu vipambanuzi vyake nao ni kila yule ambaye ana yeye kwao uzazi wa moja kwa moja au kupitia mtoto wa kiume au wa kike. Na hiyo ni maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia} [251/2, Ch. Dar Al Fikr].
Basi Kauli yake: "Nao ni kila yule ambaye ana yeye kwao uzazi wa moja kwa moja au kupitia mtoto wa kiume au wa kike", hukumu hii inamwingiza binti, na binti wa mtoto wa kiume na kushuka chini katika nasaba, kwani yote hayo yanamuhusu yeye kwa wao katika uzazi.
Na Al Khatweb As Sherbiniy akasema: "Faida, Ar Rabibah ni binti wa mke, binti zake, na binti wa mtoto wa kiume wa mke, na binti zake. Al Mawardiy akaitaja katika tafsiri yake, Na kutokana na haya, unajuliwa uharamishaji wa binti mtoto wa Mke na mtoto wa binti huyo kwa kuwa yeye ni katika watoto wa kike wa watoto wa mke wake, na hili ni suala nyeti mno linaloulizwa mara kwa mara" [Al Iqnaa' 418/2, Ch. Dar Al Fikr].
Na katika kitabu cha: [Al Iswaaf kwa Al Mardawiy]: "Faida: Akamharamishia binti wa mtoto wa mke wake. Swaleh na wengineo wakainukulu, na Sheikh Taqiy Edeen (Mwenyezi Mungu amrehemu) akataja: "Kwamba yeye hajui kuwa uko upingano" [115/8, Ch. Dar Ihyaa At Turath Al Arabiy].
Na Al Bahuti akasema alipoongea waharamishwa: "(na) ya nne ni Ar Rabaib; na wao ni mabinti wa mke wake aliyemwingilia na kama walishuka chini" kutoka nasaba au kunyonya; kawa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia}. Au (walikuwa) ni Mabinti (wa mtoto wa mke au) walikuwa watoto wa kike wa (mtoto wa kiume wa mke), wawe wana undugu au hawana, warithi au hawarithi, wako chini ya malezi yake au hapana. [653/2, Ch. Alam Al Kutub]
Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Kimisri imetoa fatwa kadhaa kuhusu suala hilo, na miongoni mwa hayo: Fatwa ya Mheshimiwa Sheikh Ahmad Haridiy katika tarehe: 27/4/1968, Ambapo aliulizwa kuhusu: mwanamke aliyeolewa na ana mtoto wa kike wa mtoto wake wa kiume aliyefariki, na mwanamke huyo akawa anataka mume wake ampe talaka kwa kuwa hajajaaliwa kamwe kumzalia mtoto ili amwozeshe mtoto wa kike wa mwanae wa kiume aliyetajwa. Na mwenye suala anaomba fatwa ya kuwa; je, inajuzu kisheria kwamba mume huyo amwoe binti wa mtoto wa mke wake baada ya kumpa talaka ama hapana?
Basi akajibu: Qur'ani Tukufu imetaja kwamba mwanamume anaharamishiwa kumwoa binti wa mke wake aliyemwingilia, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na watoto wenu wa kambo walio katika ulinziwenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu} [AN NISAA 23]
Na wanazuoni wametoa kauli ya kuwa uharamishaji hauishii kwa mtoto wa kike wa mke aliyeingiliwa na mumewe, bali uharamishaji huo unakusanya matawi yote ya mke huyo, kama vile mtoto wa kike wa mwanaye wa kike na mtoto wa kike wa mtoto wake wa kiume na kushuka chini. Na uwazi wa swali hili ni kwamba mume anayetaka kumwoa mtoto wa kike wa mtoto wa kiume wa mkewe aliyekwishamwingilia, kwa hali hiyo inaharamishwa kwake kumwoa mtoto wa kike wa mtoto wa kiume wa mke wake, kwa uharamu wa kudumu, awe mume huyo amemwacha mke wake au bado yuko katika himaya yake, na kutoka hayo yaliyotajwa inajulikana jawabu la suala.
Na kutokana na maelezo yaliyotanguliza: basi kwamba haihalalishwi kwa mwamume kumwoa binti wa mtoto wa mke wake, baada ya kumpa talaka kama alikuwa amemwingilia, ama kama alikuwa hakumwingilia basi binti huyo ni halali kwake kwa ndoa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


Share this:

Related Fatwas