Kushiriki kwa Wanawake katika Maand...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushiriki kwa Wanawake katika Maandamano na Kuweka Kambi.

Question

 Mwanamke kutoka nje ya nyumba wakati wa kutojiepusha na fitina ni jambo la kuzingatiwa katika Fiqhi ya kiislamu. Na hii inaambatana na safari au mfano wake, na miongoni mwa mambo lazima kuyajua kidini ni kuwa maandamano ya halaiki au kuweka kambi ikiwemo kama kulala kwa muda wa siku na nyusiku kadhaa, ambapo vinapelekea kutopatikana usalama dhidi ya fitina hata kidogo kwa mwanamke. Na mahali pa maandamano hapana heshima, vile vile waandamanaji sio wote waadilifu, na ilivyotokea ndiyo inahakikisha hivyo. Je, nini hukumu ya Sharia ya kutoka kwa wanawake sambamba na wanaume katika matukio mfano wa nilivyotaja hapo juu? Na je, kuna njia yenye usalama kwa mwanamke wakati anapotoka, ili asikatazwe kueleza maoni yake? Na nini hukumu ya mwanamke ambaye anajua hivyo, na kwa hivyo kushikilia msimamo wake kutoka, pamoja na kuwepo au kutokuwepo idhini ya walii wake?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Baadhi ya watu wanafanya maandamano, na hii inapelekea kuchanganyika wanawake na wanaume wenyewe kwa wenyewe, na huenda inapelekea kulala usingizi katika mahali wazi au ndani ya mahema, na huenda pia hema linakusanya wanaume na wanawake wasio jamaa. Na si daima kupatikana hivi vyote, lakini haya ni maelezo ya muhtasari wa swali. Je, nini hukumu ya Sharia katika hivi?
Matokeo kama hayo yakifanyika bila ya kuangalia vigezo vya Sharia, yataingia chini ya jina la :mchanganyiko mbaya.
Na hukumu ya kisharia ya suala hili, kutokana na swali, inagawanyika katika nukta kadhaa:
Kwanza: Kuhusu kutoka kwa mwanamke katika maandamano au kweka kambi: ikiwa sababu ya maandamano ni ya kisharia, na ya utulivu, na mbali na uhalifu wa Sheria, na kuzuia masilahi ya watu, tena mwanamke atapata idhini ya mwenye haki ya kutoa idhini ya kutoka, kama vile mume, basi hapo maandamano na kuweka kambi ni kujuzu kwa mtazamo wa asili yake.
Kadhalika wanawake wanaoshirikiana maandamano na kuweka kambi hawana sura moja, baadhi yao wanashirikiana wakati wa mchana, na si usiku, na wengine wanashirikiana pamoja na waume zao na jamaa zao, na wengine pamoja na wanawake wenzao waaminifu kama vile madaktari wanaouguza katika mahali pa maandamano, na baadhi yao huenda wakazuiwa katika mahali pa kambi au maandamano, na hawawezi kuondoka kutokana na mapigano kwa mfano, na baadhi yao wanakuwa katika viwanja mbele ya watu wote. Vile vile kuwepo makosa kwa baadhi ya wanawake hakumaanishi kuwa wote ni wenye makosa.
Na huenda kuna jambo la heri linaambatana na makosa ndani yake, lakini haisihi kuwa makosa yakazuia heri iliyopo, na dalili ya hayo ilivyopokelewa kutoka kwa Abdullah ibn Umar R.A, alisema: Mtume S.A.W, alimpeleka Khalid Ibn Al-Waliid kwa Bani Jadhima, akawalinganie Uislamu, na wao hawakuweza kutamka vizuri matamshi ya kusilimu, lakini wakasema: tumeacha Uislamu, tumeacha Uislamu, na Khalid aliendelea kuwaua na kuwateka, kisha akamkabidhi kila mtu kati yetu mateka wake, na siku moja Khalid aliamuru kila mtu amuue mateka wake, nikasema; Wallahi simuui mateka wangu, wala mtu miongoni mwa rafiki zangu amuue mateka wake; na tulipokuja mbele ya Mtume S.A.W, tulimwambia ilivyotokea, hapo Mtume S,A.W., aliinua mkono wake akisema: “Ewe Mola mimi ni mbali na alivyofanya Khalid, alisema hivi mara mbili”. [Ameipokea Bukhariy].
Upande wa dalili ya Hadithi hii kuwa Mtume S.A.W., hakujiepusha na jeshi lote wala Khalid, lakini alijiepusha na kitendo hicho hasa.
Pili: Kuhusu mwanamke kushikilia msimamo wake ili atoke, pamoja na kuhofia kukabiliwa na fitina na hatari, hakika hukumu inaweza kuwa makuruhu au haramu; kwa sababu, maudhui hii inaweza kuwa shaka au hakika, kutokana na tofauti kati ya hali na nyingine, kama tulivyoeleza. Kwa kuongeza aina za fitina ni mbali mbali; ikiwa makusuduo ya fitina hapa ni kuchanganyika na wanaume, atalazimika asichanganyike na yule atakayehofia fitina kwa upande wake, na asifanye matendo yanayopelekea fitina au matendo yenyewe ni haramu, kwa mfano kulala usingizi pamoja na asiye jamaa peke yao ndani ya hema moja kwa mfano. Na hakuna shaka kuwa dalili za jambo hili ni nyingi na mashuhuri kati ya watu wote, miongoni mwake ilivyotajwa na mwenye swali kuhusu kuzuia safari bila ya kuwepo jamaa, na inafahamika kuwa sababu ni kuhofia fitina, na sababu inaambatana na hukumu kuwepo au kutokuwepo, na kama sababu ikiwepo basi hukumu itakuwepo hivyo hivyo.
Na ikiwa fitina ni kupambana na Jeshi la Polisi naye, basi analazimika kutopambana nao, ili asipate aina yoyote ya adha.
Tatu: Kuhusu njia zinazopendekezwa kwa kueleza maoni, na kulinda kutoka kwake, ni kama ifuatazo:
• Kufungua milango ya vyombo mbali mbali vya habari mbele ya mwanamke, ili asije kushiriki katika ghasia ambazo huenda ndani yake kukawa na aina za kutumia nguvu au fitina yoyote.
• Kama mwanamke akishikilia msimamo wake kushirikiana, basi awe na baadhi ya jamaa zake, au ashiriki katika mahali mahsusi, ambapo awe mbali na vurugu na fitina, kama ilivyotangulia.
• Kujisitiri kwa kuvaa hijabu na kujiheshimu, kimaneno na kimatendo, na analazimika kuvaa nguo zitakazomkinga na kufunuka katika hali ya kwenda na kukimbia ambako hutokea mara nyingi katika matukio kama haya.
• Kutosheka kwa maandamano ya utulivu yaliyo mbali na vurugu, kama vile kueleza maoni yake kwa kuchukua bango lililoandikwa juu ya maoni yake anavyotaka, na bila ya madhara ya kimaneno, kwa sababu kutodhuru ni lengo la kisheria, na mwenendo huu unazuia yeyote atakaye kumuudhi kutokana na matendo yake.
• Kutolala usingizi nje ya nyumba, isipokuwa awe na jamaa zake au wanawake waaminifu, kama ilivyotangulia.
• Kuonya vijana kutokana na unyanyasaji wa kijinsia, au kumshawishi kwa makubaliano; kwa sababu Sharia hairuhusu hivyo, zaidi ya hayo, kuharibu sura ya wote. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na iogopeni adhabu ya (Mwenyezi Mungu ya hapa duniani) ambayo haitawasibu peke yao wale waliodhulumu nafsi zao miongoni mwenu (bali itawasibu hata walionyamaza wasiwakataze, bali na wengineo pia); na jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu}. [AL ANFAAL 25]. Na hili ni jukumu la wenye kuweka kambi na wengineo.
• Kuonya Jeshi la polisi kupambana naye kwa adha, na ni bora kumtendea kama jamaa, na kama mmoja kati yao atakapopatikana na uhalifu wa sheria, basi kumtendea kwa mujibu wa sheria, na kwa mujibu wa huruma na uungwana, na kwa kujua kuwa mwanamke ana hali maalumu mbali na mwanamume, na mwili wake ni uchi na ni lazima ujisitiriwe, na tena ni dhaifu, kwa hivyo hakabiliwi kwa ushupavu mfano wa mwanamume. Na Mtume S.A.W, alisema: “Wafanyieni heri wanawake”. [Muttafaq], na akasema pia: “Mbora zaidi kati yenu ni mbora kwa wanawake”. [Ameipokea Al-Hakim katika kitabu cha Al-Mustadrak], na miongoni mwa wasia wa mwisho wa Mtume S.A.W,: “Mcheni Mwenyezi Mungu kwa madhaifu wawili: mwanamke na yatima”. [Ameipokea Al-Baihaqiy katika Shua’ab Al-Iman].
Na kwa mujibu wa yaliyotangulia kuwa: Inajuzu kwa mwanamke kushiriki katika maandamano ya utulivu, akijikinga na fitina, na aina yoyote ya hatari, na kuangalia mambo yaliyotangulia kutajwa hapo juu. Na kwa ilivyotangulia, inafahamika jibu la swali.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas