Baina ya Waqfu na Sadaka Yenye Kuen...

Egypt's Dar Al-Ifta

Baina ya Waqfu na Sadaka Yenye Kuendelea.

Question

Kuna tofauti gani kati ya Waqfu na Sadaka yenye kuendelea? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Sifa zote njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya utangulizi huo:
Basi maana ya Sadaka katika lugha ni: Wanachopewa mafukara kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.Tazama: [Taj Al-Aros 26\12, Kidahizo cha: (S D Q) Ch. Dar Al-Hedayah]. Al-Ragheb Al-Asfahany katika kitabu cha: [Al-Mufradat 1\480, Ch. Dar Al-Qalam]: "Sadaka ni :Kinachotolewa na binadamu kutoka katika mali yake kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni kama Zaka, lakini Sadaka katika asili inasemwa kwa mtu anayejitolea katika mali yake, ama Zaka ni kwa lazima, yaani faradhi, na wakati mwingine Sadaka inasemwa wajibu au lazima ikiwa mtu anayetoa akithibitishia ukweli katika kufanya kwake".
Na maana ya Sadaka katika istilahi ni:Kutoa mali na kadhalika kwa makusudio ya kupata thawabu Akhera [Al-Majmuoa kwa Al-Nawawy 6\246, Ch. Al-Muneriyah], na hii kwa ujumla wake inajumuisha Sadaka ya mtu anayejitolea na Sadaka ya Faradhi yaani Zaka, lakini maana yake katika istilahi ya wanafiqhi kwa ujumla ni Sadaka ya kujitolea [Mughny Al-Muhtaji 4\194, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah], na hakuna hitilafu baina ya wanafiqhi katika kujuzu kwa kutoa Sadaka ya kujitolea kwa watu wasiyohitaji, na ilhali msimamo huu ni kinyume cha makusudio ya Swadaka na Swadaka ya wajibu ambayo ni Zaka, lakini kwa kumpa asiyehitaji hakuzingatiwi ni Sadaka ya kutaka kwake thawabu ya Akhera, na Imam Al-Nawawy alisema katika kitabu chake [Al-Majmoua 6\236]: ”Sadaka ya kujitolea waweza kuwapa matajiri bila hitilafu baina ya wanazuoni, basi waweza kuwapa na anayewapa ataatapata thawabu juu ya kitendo hiki, lakini kuwapa wanaohitaki ni afadhali”. Na Al-Khatweeb Al-Sherbeny alisema katika kitabu cha: [Mughny Al-Muhtaj 3\559]: Sadaka kwa matajiri inajuzu na anayeitoa atapata thawabu akikusudia uhusiano wa familia, kwa hivyo akatoka katika jambo hili, akitoa Sadaka kwa mtajiri bila ya kukusudia thawabu ya akhera “.
Na inasemwa Sadaka kwa majazi juu ya kila vitendo vya kheri kama katika kauli yake Mtume S.A.W., "Kila kitendo cha kheri ni Sadaka". Na Al-Imam Al-Nawawiy alisema katika kitabu cha: [Al-Majmuoa 6\246]: ”Kujua kwamba hakika ya Sadaka ni kumpa mali mtu mwingine kwa makusudio ya kipataa thawabu ya akhera na mengine pia”.
Na Sadaka ya kujitolea imegawanyika: (Sadaka ya kwisha) ni kama kupamiliki mahali maalumu na manufaa yake kwa kuchukua Sadaka, au kuruhusu manufaa yake kwa wakati maalumu, au kwa tukio maalumu linalosubiriwa kutokea na Sadaka itakwisha kwa kumalizika tukio hilo, na (Sadaka yenye kuendelea) thawabu za mwenye Sadaka zinaendelea katika maisha yake na baada ya kufa kwake; kwa sharti la kubaki asili ya Sadaka na kuzuia kuuzwa kwake na mfano wake, au kumilikisha na kubaki sehemu ya mwenye Sadaka na hii -ikiwa ni mtu mmoja au taasisi moja- muda wa kubaki mahali baada ya mwanzo wake (asili ya Sadaka) na kuitengeneza ili kuendelea na kutokatika; ni sawa ikiwa ilianza wakati wa maisha yake kama katika (Waqfu) au baada ya kufa kwake kama katika (Usia kwa kutumia manufaa daima).
Na asili ya kisharia ya Sadaka yenye kuendelea ni katika Hadithi ya Mtume S.A.W., iliyosimuliwa na Al-Bukhariy na Muslim (kutoka kwa Ibn Omar -Mwenyezi Mungu awe radhi juu yao- kwamba Omar Ibn Al-Khatwab alipata ardhi huko Khaibar, akamwendea Mtume S.A.W., akimuomba amri na ushauri katika ardhi hiyo. Akamwambia: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungiu nimepata ardhi Khaibar, sijawahi kupata mali ilio bora zaidi kwangu kuliko mali hiyo. Utaniamuru niifanyeje?)” Mtume S.A.W., akamwambia “Ukipenda, uitoe waqfu asili yake na utoe Sadaka manufaa yake, ”Omar akaitoa Sadaka isipokuwa asili yake haiuzwi wala hairithiwi wala haitolewi Hiba. ”Omar akalitoa sadaka kwa mafukara, watumwa walioandikiana katika njia ya Allah, mpita njia na mgeni. Hapana ubaya kwa anayelisimamia jambo hili ale ndani yake kwa wema au amlishe rafiki lakini asiifanye ni milki yake.”.
Na kadhalika Hadithi iliyosimuliwa na Bukhari kutoka kwa Ibn Omar -Mwenyezi Mungu Awe radhi juu yao-: Kwamba Omar alitoa mali zake Sadaka wakati wa Mtume S.A.W., na ilikuwa mitende, Omar alisema: Ewe Mtume S.A.W.! Nimenufaika na mali na nina nyingi, ninataka kutoa katika mali hizi, Mtume S.A.W., akasema: "zitoe Sadaka kwa asili yake, haiuzwi wala haitolewi Hiba lakini matunda yake hutolewa (kupewa watu)". ”Omar akalitoa sadaka kwa mafukara ambao ni jamaa zake wa karibu, watumwa walioandikiwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, msafiri na mgeni. Hapana ubaya kwa anayelisimamia jambo hili ale ndani yake kwa wema au amlishe rafiki lakini asiifanye ni milki yake”
Na kadhalika Hadithi iliyosimuliwa na Muslim kutoka kwa Abu-Huraira- Mwenyezi Mungu Awe radhi naye-amesema kwamba Mtume S.A.W., amesema: "Mwanadamu akifa amali yake hukatika ila kwa mambo matatu: Sadaka inayoendelea au elimu inayonufaisha au mtoto mwema anayemuombea dua".
Al-Ezz Ibn Abdussalam alisema katika kitabu cha: [Qawa'ed Al-Ahkam 1\136, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah:]: ”Sadaka inayoendelea inafaa katika waqfu na katika wasia kwa manufaa ya nyumba yake na matunda yake daima, na hili ni kutokana na chumo lake na kwa sababu yake katika mali hii, kwa hivyo atachukuwa thawabu yake”.
Na waqfu katika lugha ni: Kuzuia. na katika istilahi ni:Kuzuia mali inayoweza kunufaisha pamoja na kubakisha mahali palipotolewa na kuzitoa mali hizi katika njia ya Mwenyezi Mungu.Tazama kitabu cha: [Ghayat Al-Bayan maelezo ya Al-Zubad kwa Al-Ramliy Al Shafiy, Uk. 230, Ch. Dar Al-Maarifah]. Na katika kitabu cha: [Maelezo ya Al-Shalaby Al-Hanafiy juu ya uwazi wa ukweli /Ala Tabyiin Al-Hakaek 3\324, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: Alitoa dhana ya waqfu kisharia ni: ”Kuzuia mali ambayo watu watanufaika nayo pamoja na kubakia asili yake, kama vile mtu kutoa nyumba yake waqfu ili kodi yake ilipe mishahara ya walimu kadhalika waqfu ni kutoa manufaa yake kwa anayempenda -na hii ni rai ya Al-Imam Abu Hanifa- na kadhalika rai ya wanachuoni wawili Abu Yusuf na Muhammad -kwa maana hii hii-kuzuia kwa njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na pia waqfu unafaa kwa mmoja miongoni mwa matajiri bila ya kusudio la jamaa wa karibu.
Ama wasia kwa manufaa, maana ya wasia katika lugha ni: Kuusia kwa kitu kimoja, kwa maana, nimuusia kwa mali kwake, tazama:[Al-Mesbah Al-Munir kwa Al-Fayumiy 2\662, Ch. Al-Maktabah Al-Elmiyah], na maana ya wasia katika istilahi ni: Umiliki wa unaopatikana baada ya mauti kwa njia ya Hiba, ikiwa ni katika mali au manufaa. {Tazama kitabu cha: Tabyeen Al-Hakaek kwa Zaylaayy 6\182, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy], na [Al-Bahr Al-Raeq kwa Ibn Najeem 8\459, Ch. Dar Al-kitab Al-Islamiy]. Na Al-Manifia ni mwingi wa Manfaah na ni: Faida anayoipata kwa kuitumia mali, ni kama kodi ya nyumba na kodi ya kumtumia mnyama kwa kupanda kwake. Tazama: [Durar Al-Hukkam Sharhe Mejalat Al-Ahkam kwa Ali Hedar 1\115, Ch. Dar Al-Jeel ].
Na Jamhuri ya Waulamaa wamesema kuwa ni madhumuni ya Sadaka yenye kuendelea kama ilivyo katika Hadithi iliyotangulia ni waqfu peke yake bila ya amali ya kheri nyingine, ikiambatana naye maana ya Hadithi iliyo wazi kwa ujumla; ni kwa madhumuni ya ujumla yanayotakiwa katika umaalumu hasa, pamoja na waamuabatano wao kwamba kuna amali nyingine ya kheri na thawabu baada ya mauti kama vile wasia kwa manufaa kwa uchache wake, lakini walisema kwamba Sadaka yenye kuendelea ni waqfu, na waliepusha mbali juu ya maana ya wasia kwa manufaa kwa uchache wake, Al-Khatweeb Al-Sherbiny alisema katika kitabu cha: [Mughny Al-Muhtaj 3\523]: ”Maana ya Sadaka yenye kuendelea kwa wanazuoni ni waqfu kama alivyosema Al-Rafiey ni kitu kingine kisicho sadaka kisicho sadaka ya kuendelea,bali anayechukuwa sadaka anaweza kunufaika kwa manufaa yake, ama wasia kwa manufaa, na kwa upande mwingine maana ya sadaka inaweza kuwa waqfu pia”.
Lakini kwa upande mwingine Wanachuoni wa Shafiy waliokuja mwishoni hawaafiki rai ya hapo juu bali walipendelea kwamba Waqfu unaweza kuwa Sadaka yenye kuendelea na rai yao ni kutokana na Hadithi zingine za Mtume S.A.W., kama katika Hadithi ya Abu Huraira kwamba Mtume S.A.W., amesema: "Hakiia katika Matendo au mambo mazuri ambayo humwendea mja baada ya kufa kwake ni elimu aliyoifundisha na kuisambaza, mtoto mwema aliyemwacha, na Msahafu aliyourithisha au msikiti aliyoujenga au nyumba aliyoijenga kwa ajili ya wapita njia, au mto aliyoupitisha kwa watu, au Sadaka aliyoitoa kutoka katika mali yake, akiwa na afya na katika uhai wake, vyote hivyo vitamwendea baada ya kufa kwake".
kutoka kwa Anas-Mwenyezi Mungu Awe radhi naye- alisema :Mtume S.A.W., amesema: "Mambo saba ambayo malioo yake kwa mja huendelea kupatikana yeye akiwa kaburini baada ya kufa kwake: Mtu atakayeifundisha elimu yoyote, au akaupitisha mto, au aliyechimba kisima, au aliyeupanda mtende, au aliyejenga Msikiti, au aliyeurithisha Msahafu au aliyeacha mtoto anayemwombea baada ya kufa kwake." Hadithi hii Imesimuliwa na Al-Bazzar na Abu Naeem katika kitabu cha Helyah.
Hafedh Al-Menawiy alisema katika kitabu cha: [Faydhu L-Qadeer 4\87, Ch. Al-Maktabah Al-Tugariyah Al-Kubra]: ”(Au alilima mitende) kwa maana aliipa kama sadaka…. Al-Baihaqy alisema :Hadithi hii haina tofauti na Hadithi sahihi nyingine iliyosemwa: Mwanadamu akifa amali yake hukatika ila kwa mambo matatu, alisema ndani yake ila Sadaka inayoendelea na hii inakusanya yaliyo tajwa kutokana na ziada"; kwani kuipanda mitende kwa ajili ya kutoa Sadaka kwa matunda yake ni sura nyingine miongoni mwa sura za sadaka za kuendelea.
Al-Bejermy alisema katika kitabu chake: [Tuhfat Al-Habib Ala Sharh Al-Khatib 3\243, Ch. Dar Al-Fekr]: ”Tazama kinachohusisha Waqfu na ilhali ya Sadaka ya kuendelea ni yenye kujumuisha zaidi”
Na alisema katika [Kitabu chake juu ya maelezo ya mfumo wa wanafunzi 3\201, Ch. Dar Al-Fekr]; ”Kauli yake: (Wanazuoni walisema kuwa Sadaka ya kuendelea ni waqfu….). Kwa hivyo yaweza kuzingatiwa ni matendo ya kheri nyingine zilizotajwa kama Sadaka ya kuendelea ambayo matendo yake hayakatiki baada ya kufa kwake mwanadamu… Na ilisemwa yaweza kuwa kama: Wasia kwa manufaa yake na hii ni dalili juu ya rai hii lakini ni jambo la nadra ,kwa hivyo kuzingatiwa Sadaka ya kuendelea ni waqfu”. Na Al-Ezz Ibn Abdussalaam alisema kwa rai hii katika kitabu cha: [Kawaed Al-Ahkam 1\136]: ”Sadaka ya kuendelea inachukuwa juu ya waqfu na juu ya Wasia kwa manufaa ya nyumba yake na matunda ya bustani yake daima”.
Kutokana na yaliyotangulia ni wazi kwamba ufahamu wa Sadaka ya kuendelea una maana kamili ya kuambatana na kila matendo ya kheri zaidi kuliko ufahamu wa waqfu; kwani wasia kwa manufaa yaweza kuwa ni Sadaka ya kuendelea lakini ufahamu wake ni tofauti na maana ya waqfu, na wanazuoni walipohusisha ufahamu wa sadaka ya kuendelea juu ya waqfu katika Hadithi haiwajibishi kuwa Sadaka nyingine isiyokuwa Sadaka ya kuendelea bali kila matendo ya kheri yanaingia chini ya ufahamu wa sadaka ya kuendelea; kwa hivyo tunaweza kusema kwamba wasia ni kwa manufaa ya vitu vyovyote visivyo kuwa ni sadaka ya kuendelea na thawabu ya vitu hivi inaendelea kwa mwanadamu hata baada ya kufa kwake na ni sawa kama sadaka ya kuendelea, lakini waqfu ni afadhali kwani thawabu yake inaanza katika maisha ya mwanadamu na kuendelea baada ya kufa kwake, lakini thawabu ya wasia kwa manufaa inaanza baada ya mauti ya mwanadamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas