Kunyonya kwa Mtu Mzima.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kunyonya kwa Mtu Mzima.

Question

Je Mwanamke anapomnyonyesha mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili, uharamisho wa kunyonya unathibiti kwa unyonyeshaji huo? Na ni upi umri wa unyonyonyeshaji unaoharamisha? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Wanachuoni wa Fiqhi wa madhehebu manne wameafikiana kuwa Kunyonya ambako kunasababisha uharamu ni kwa utotoni na wala sio ukubwani. Na kiwango tenganishi baina ya ukubwa na udogo kina hitilafu za wanazuoni. Kwa hivyo basi wanazuoni wa Madhehebu ya Shafi, na wa Hambali na wanazuoni wetu wawili wa Madhehebu ya Hanafi wanaona kwamba mpaka wa udogo ni miaka miwili, lakini wanazuoni wa Madhehebu ya Maliki wanaona kuwa nyongeza inayokaribiana na miaka miwili huingia katika uharamu huo, na kiwango chake ni mwezi au miezi miwili kwa kauli inayotegemewa kwao. Lakini Imamu Abu Hanifah ameelekea katika rai ya kwamba mpaka wa udogo ni miezi thalathini, yaani miaka miwili na nusu. Na Zafar Bin Al Hazeel –miongoni mwa wanazuoni wa Madhehebu ya Haanafi, akasema kuwa mpaka wa udogo ni miaka mitatu. Rejea vitabu vya: [Badai' Aswanai' kwa Al Kasaaniy 5, 6/4, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah, na Sharhu Mukhtasari Khalil kwa Al Kharashiy 178/4, Ch. Dar Al Fikr, na Esniy Al Matwalib kwa Sheikh Zakariyah Al Nswariy 416/3, Ch. Dar Al Kitab Al Islamiy, na Mughniy Al Muhataj kwa Al Khatweeb Asherbiniy 126. 127 /5, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na kauli ya wanazuoni wa madhehebu manne ya Fiqhi ni kwamba kunyonya kunakosababisha uharamu ni kwa udogoni na sio ukubwani, na hii ni kauli ya wengi miongoni mwa wanachuoni, na ndiyo inayotegemewa katika Fatwa. Na yamepokelewa kama hayo kutoka kwa Omar, Ali, Ibn Omar, Ibn Masoud, Ibn Abbas, Abi Hurairah na wakeze wa Mtume S.A.W. isipokuwa Bibi Aisha, na kwa maoni haya, Wanazuoni hawa; As-Sha'abiy, Ibn Shabramah, Al Awzaa'iy, na Is-haq na Abu Thaur wameifuata Rai hii. [Al Mughniy kwa Ibn Qudamah 142/8, Ch. Dar Al Fikr].
Na Jamhuru ya Wanazuoni imetoa dalili mbali mbali za wale wanaoona kuwa kunyonya kunakosababisha uharamu ni kwa udogoni na sio ukubwani, kama mfano kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha} [AL BAQARAH 233]. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akajaalia utimizaji wa unyonyeshaji katika miaka miwili kamili, na yeye anafahamisha kwamba hukumu baada ya hayo ni tofauti, na aya tukufu hiyo pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini} [AL AHQAAF 15], alisema muda mfupi zaidi wa mimba na utimizi wa muda wa unyonyeshaji.
Na miongoni mwao yaliyotolewa na Masheikhe wawili: "Kutoka kwa Aisha R.A., kwamba Mtume S.A.W., Aliingia ndani kwake akiwa na mwanamume, na ikawa kama vile uso wake ulibadilika, kama mtu aliyechukizwa na tukio hilo, akasema yule Mwanamke: Hakika mambo yalivyo huyu ni kaka yangu, na akasema: "Tazameni ni nani katika ndugu zenu kwani hakika kunyonya husababishwa na njaa". Basi Mtume S.A.W., aliashiria kuwa kunyonya utotoni ndiko kunakosababisha uharamu; kwani ni hali ya kuhitajia chakula na maziwa, na hicho ndicho kinachoisukuma njaa. Ama kwa upande wa njaa ya mtu mzima haipeleki kunyonya. Rejea kitabu cha: [Badai' Aswanai' kwa Al Kassaniy 5/4, na Sharhu Al Muntaha kwa Al Bahutiy 315/3, Ch. Alam Al Kitab] Na hadithi ianaafikiana nayo.
Na miongoni mwao ni Hadithi ya Ummu Salamah alisema: Mtume S.A.W. akasema: "Hakuharamishwi kwa kunyonya isipokuwa kwa yule ambaye utumbo wake hutanuliwa kwa maziwa ya kunyonya na akiwa bado mchanga". Imepokelewa na At Termiziy. Na kunyonya kwa mtoto mdogo ni kule kunakoutanua utumbo na wala sio kunyonya kwa mtu mzima kwa sababu utumbo wa mtoto mchanga huwa unakuwa umebana na hautanuliwi isipokuwa kwa maziwa ya kunyonya kwa kuwa maziwa ni chakula chepesi kuliko chochote. Ama utumbo wa mtu mzima umetanuka na wala hauhitaji maziwa kutanuliwa.
Na miongoni mwa ni Hadithi ya: "Hakukubaliki kunyonya isipokuwa ndani ya miaka miwili". Imepokelewa na Ad Darqutwniy na Al Baihaqiy katika kitabu cha: [Al Fatawa Al Kubra].
Na miongoni mwao yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., aliposema: "Kunyonya ni kule kunakootesha nyama na kuimarisha mifupa", imepokelewa na Ab Dawud na Al Baihaqiy kwatika Kitabu cha: [Al Fatawa Al Kubra]. Na huo ni unyonyeshaji wa mtoto mchanga sio mkubwa, kwani unyonyeshaji wake hauitoa nyama na wala hauiamirishia mifupa. Na athari hiyo imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masuod, na hiyo ni kwamba: "Kwamba mtu mmoja miongoni mwa watu wa majangwani mke wake alijifungua mtoto wa kiume kisha mtoto wake akafa na maziwa yake yakavimba, mwanaume akawa anayanyonya na kuyatema kisha funda moja likaingia kooni mwake, na akamuuliza Abu Musa Ash-ariy R.A, akasema: kwa hakika amekuharamikia Mwanamke huyo. Kisha akaja kwa Abdullahi Bin Masoud R.A. na akaulizia, basi akasema je, ulimwulizia mtu yeyote? Basi akasema Ndiyo, nimemuuliza Abi Musa Al Asha'riy basi akasema "kwa hakika amekuharamikia Mwanamke huyo". Basi Ibn Masuod akaja kwa Abi Musa Al Asha'riy R.A. wote wawili, na akasema: Kwani hukuwa ukijua kwamba hakika mambo yalivyo inakuwa haramu kwa kunyonya kinachokuza nyama za mwili, akasema Abu Musa: Msiniulize kuhusu jambo wakati mwanachuoni huyu mko naye. Imepokelewa na Ad Darqutwniy na Al Baihaqiy.
Na miongoni mwao iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., kwamba akasema: "Hakuna kunyonya baada ya miaka miwili". Imepokelewa na At Twabraniy katika kitabu cha: "As Swagheer.
Na miongoni mwao iliyopokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar R.A. wote wawili, kwamba mwanamume mmoja akaja kwa Omar R.A., na akasema: "Mimi nilikuwa na kijakazi nikimwingilia, na mke wangu akampa maziwa yake na akayanyonya kisha nikaja kumwingilia basi mke wangu akasema: mimi nimemnyonyesha na Omar akasema: endelea kumwingilia huyo ni kijakazi wako, hakika kunyonya kunakoharamisha ni kwa utotoni tu". Imepokelewa na Al Baihaqiy na Malik katika kitabu cha: [Al Muwatwa'].
Na Ibn Hazm akaenda kinyume cha Jamhuri ya Wanachuoni wa Fiqhi katika suala hilo, na akasema: hakika kunyonya kwa mkubwa na mdogo kunakoharamisha. [Kitabu cha Al Mahaliy 205/10, Ch. Dar Al Kutub Al Elimiyah] na hiyo ilinasabishwa kwa Bibi Aisha, Al Imam Ali, Atwaa na Al Laith, kitabu cha: [Al Mughniy 142/8]. Na amepokea dalili nyingi kuhusu hilo na akatafuta tatizo katika dalili za Jamhuri ya Wanazuoni kwa yale yasiyokuwa na faida yoyote, na katika kutoa dalili ya Madhehebu yake athari moja inapokelewa kutoka kwa Salem Bin Abi Aj Ja'ad –Maula wa Al Ashja'iy- akamwambia kuwamba babake akamwambia kwamba akamwuliza Ali Bin Abi Twaleb basi akasema: "Mimi nilitaka kumwoa mwanamke na alikuwa amewahi kuninyanyowesha maziwa yake hali ya kuwa mimi ni mkubwa, je, nimeharamikiwa kwa kufanya hivyo? Ali R.A akamwambia: Usimuoe. Na akamzuia kufanya hivyo.
Na hiyo ni athari dhaifu, imepokelewa na Abdulraziq katika kitabu chake cha: [Al Muswanaf 461/7, Ch. Al Maktabu Al Islamiy], na ndani yake Abdulkareem Ibn Abi Al Makhariq, na huyo ni dhaifu kama alivyotaja Al Hafedh katika kitabu cha: [At Taqreeb Uk. 361, Ch. Dar Ar Rasheed]. Na pia hadithi ya Salem Maula Bin Abi Al Ja'ad kutoka kwa Ali R.A., ni hadithi yenye hukumu ya Mursal kama alivyotaja Abu Hatem kutoka kwa Abi Zara'ah [Tahdheedu At Tahdheeb 432/4, Ch. Matwba'at Daierat Al Maaref An Niedhamiya, India]. Basi nasaba hiyo kwa Imamu Ali haisihi, kama alivyotaja Ibn Abdul Bar na Abu Zar'ah Al Iraqiy [At Tamheed 256/8, Ch. Wizara ya Wadfu ya Moroko, Al Istinkaar 255/6, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah na Twarhu At Tathreeb 135/7, Ch. Dar Al Fikr]. Na pia Abdulraziq akapokelea katika kitabu chake cha: [Al Muswanaf] kinyume cha madhehebu hiyo kutoka kwa Imamu Ali [461/7].
Na Ibn Hazm pia akatoa dalili kwa iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Shehaab kwamba aliuliziwa katika kunyonya kwa mtu mzima? Basi akasema: "Urwah Bin Az Zubair aliniambia kwa Hadithi ya amuru ya Mtume S.A.W., kwa Sahlah Bint Sohail kumnyanyoa Salem Maula (mtumwa aliyeachwa huru) Abi Hudhaifah mara tano na yeye alikuwa mkubwa, na Sahlah akafanya hayo, basi akamwona Salim kama mwanae". Urwah akasema: Na Bi Aisha Mama wa Waumini R.A, akachukulia hivyo kwa wale ambao alikuwa akipendelea waingie nyumbani kwake katika wanaume, na akawa anamuamrisha dada yake Ummu Kulthuum na mabinti wa kaka yake, wawanyonyeshe wanaopendezwa nao waingie ndani kwake miongoni mwa wanaume. Na kwa iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Juraij akasema: "Nimesikia Atwaa Bin Abi Rabaah alimwulizia mwanamume mmoja basi akasema: mwanamke amewahi kuninywesha maziwa yake hali ya kuwa mimi ni mkubwa, basi naweza kumwoa? Atwaa akasema: La, Ibn Jareer akasema: basi nilimsemea: na hilo ni oni lako? Akasema: Naam, Aisha alikuwa akiwaamirisha mabinti wa ndugu yake.
Na hizi ni dalili mbili ambazo hazifai kuthibitisha Madai haya; kwani dalili hizi mbili hazihesabiwi kwa kuwa kwake ni maelezo ya rai ya wenyewe katika jambo hili, na ndani yake hakuna kitu chochote kinachonasibishwa moja kwa moja na Mtume S.A.W.
Na vile vile akatoa dalili kwa Hadithi: "Hakika kunyonya hutokana na njaa". Akasema: Mtu mzima kwa kunyonya kwake huiondosha njaa kama afanya you mtoto mchanga, hali hii ni ya wote wanaonyonya kama kunyonya huko kutafikia mara tano kama alivyoamuru Mtume S.A.W.
Na anazungumzia jambo hili kuwa tafsiri ya Hadithi kwa yale yaliyotajwa yako mbali na Tamko lenyewe, na wala fahamu za wanaosemeshwa haziwezi kulikimbilia, bali hiyo kauli katika maana yake ni yaliyotaja Abu Ubaid: "Hakika yule ambaye anapokuwa na njaa chakula chake cha kumshibisha kikawa ni maziwa, basi huyo atakuwa mtoto mchanga, na ama kuhusu yule aliyeyashiba na njaa kwa chakula, basi kunyonya hakuzingatiwi kuwa ni kunyonya. Kama ambavyo hawezi kuzoea kamwe mtu mwenye ndevu akashibishwa na kwa kunyonyeshwa na Mwanamke na kuiondosha njaa yake, kinyume na mtoto mchanga, kwa hakika hali ilivyo hana chochote kinachoweza kuchukua nafasi ya maziwa, hayo maziwa humuondoshea yeye njaa yake na Mtu mzima kiasili hana njaa ya kuondoshwa kwa maziwa. Na iliyoelezea hayo kwamba Mtume S.A.W. Haikupokelewa uhalisia wa njaa isipokuwa kilichokusudiwa ni dhana na muda wake, na hakuna shaka yoyote kwamba huo ni utotoni. Na tukienda pamoja na udhairi wa matni, ni lazimisho kuwa kumnyonyisha mtu mzima hakuharamishi ispokuwa akinyonya na hali alikuwa na njaa, na akinyonya na hali alikuwa akisheba basi haipo athari yoyote, na haifichiwi ya ndani yake kutoka ukereketwa [Zad Al Mia'ad kwa Ibn Al Qaim 522/5, Ch. Mua'sasat Ar Resalah].
Pia Ibn Hazm akatoa dalili kwa hadithi ambayo Muslim akatolea katika Sahihi yake, kutoka kwa Mama wa waanaimani Bibi Aisha R.A., akasema: "Sahlah Bin Sohail akaja kwa Mtume S.A.W., basi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mini naona katika uso wa Abi Huzaifah kwa sababu ya kuingia kwa Salem -na yeye ni rafiki yake-, basi Mtume S.A.W. akasema: Mnyonyeshe! Basi akasema: vipi nimnyony3eya na yeye ni mtu mzima! Basi Mtume S.A.W. akatabasamu kisha akasema: wewe ulijua kwamba yeye ni mtu mzima. Na katika kauli kwa Bibi Aisha mama wa wanaimani R.A. " Hakika Salem muachwa huru na Abu Hudhaifah alikuwa pamoja na Abu Hudhaifah na jamaa zake nyumbani kwao, mtoto wa Suhail akamwendea Mtume S.A.W, na akasema: Hakika Salem amefikiwa kiwango wanachokifikia wanaume na akawa na akili kama wao na kwamba yeye anaingia kwetu na mimi ninadhani kuwa katika ndani ya nafsi ya Abu Hudhaifah kuna kitu kuhusu jambo hilo. Mtume S.A.W akamwambia: Mnyonyeshe na utakuwa haramu kwake na kilichoko kwenye nafsi ya Abu Hudhaifah kitatoweka".
Ibn Hazm akasema: "Na Hadithi hizi zinaondosha matatizo na kubainisha lengo la Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aya zilizotajwa ya kwamba kunyonya kunakotimia kwa miaka miwili au kwa kuridhiana wazazi wawili kabla ya kumalizika kwa miaka miwili, ikiwa wao wataona katika kufanya hivyo kuna uzuri wowote kwa mtoto". [Al Mahaliy 210/10
Na inajibiwa kwa hayo kwamba hadithi ya Sahla na Salem ni hasa kwao, na tukio lao ni tukio hasa pekee na silo kwa watu wote, na hilo ni jibu moja miongoni mwa majibu ya jamhuri wa wanazuoni kwa hadithi hiyo, indapo wakasema: ama hadithi ya Salem basi ina jawabu katika pamde mbili:
Moja lao ni: ilipokelewa kutoka kwa Mama wa wanaimani Salmah mke wa Mtume S.A.W., kwamba alikuwa akisema: Wakeze wote wa Mtume S.A.W walikataa mtu yoyote kuingia makwao kwa kunyonya huko - kwa maana ya kunyonya ukubwani - na wakamwambia Bi Aisha R.A: "Kwa kweli sisi hatuoni katika jambo hili isipokuwa ni ruhusa aliyoitoa Mtume S.A.W kwa Saalima peke yake, basi hakutuingia mtu yeyote kwetu kwa kunyonya huko na wala hatukumwona. Imepokelewa na Muslim. Na hii inamaanisha kwamba Saalim alikuwa maalumu katika jambo hili, na kinachokuwa katika mambo maalumu ya baadhi ya watu kwa maana isiyokubalika kiakili, hakuna uwezekano wowote wa kukitumia kama Kipimo, na wala hatuachi uasili wake uliopitishwa katika Sheria ya Uislamu.
Na la Pili: ni kwamba hiyo hukumu imefutwa. Kwa maana kuwa kunyonya kwa mtu mzima kulikuwa kunaharamisha kisha kukafutwa kutokana na Hadithi zilizotangulia. [Bada'i Aswana'i 4,5/4, na Ithni Al Matwalib kwa Sheikh Zakariya Al Answariy 416/3, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy, na Mughniy Al Muhtaaj kwa Al Khatweeb As Sherbiniy 159/5, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah, na Kashaaf Al Qenaa' 445/5, Ch. Dar Al Fikr]
Al Haafedh Ibn Hajar akasema: "Na wakajibu kuhusu kisa cha Salem kwa majibu ambayo miongoni mwayo ni kuwa: hiyo ni hukumu iliyofutwa, na hivyo ndivyo alivyoelekea Muhibbu Twabrii katika kitabu chake cha: [Al Ahkaamu], na baadhi yao wakaamua kuwa kisa cha Salem kilitokea mwanzoni mwa Hijrah (kuhama kwa Mtume), na Hadithi zinazotoa dalili ya miaka miwili ni katika simulizi za matukio ya Maswahaba, na kwa hiyo ikawa inamaanisha kuchelewa kwake, nayo ni Musnad Dhaifu". Kwani hailazimu kuchelewa kusilimu kwa Msimuliaji wala udogo wake na kwamba kile alichokipokea kisiwe kimemtangulia vile vile, na katika matni ya kisa cha Salem kuna yanayohisisha kutangulia kwa hukumu kwa kuzingatia miaka miwili. Kwa kauli ya mke wa Abi Hudhaifah katika baadhi ya simulizi zake, indapo Mtume S.A.W. akamwambia: "Mnyonyeshe! Basi akasema: vipi ninamnyonyesha na yeye ni mtu mzima! Basi Mtume S.A.W. akatabasamu kisha akasema: wewe ulijua kwamba yeye ni mtu mzima". Na katika simulizi ya Muslim akasema: "hakika yeye ana ndevu, basi Mtume S.A.W., akasema: Mnyonyeshe!"
Na hili linahisisha kuwa yeye alikuwa anajua kwamba utoto unazingatiwa katika kunyonya kunakoharamisha. Na miongoni mwake ni wito maalumu kwa Salem na Mwanamke wa Abu Hudhaifah, na asili ndani yake ni kauli ya Ummu Salamah na wakeze Mtume S.A.W: Haulioni hili isipokuwa ni ruhusa maalumu aliyoitoa Mtume S.A.W kwa Salem kwa yale yaliyotokea kwa kumchukua na kumlea kama mwanae ambapo jambo hili likapelekea kuchanganyika kwa Salem na Sahla. Na ilipoteremshwa amri ya kuvaa hijabu wakazuiwa waislamu kuchukua watoto wakufikia na kuwalea jambo hili lilikuwa gumu sana kwa Sahla, hapo ikatokea ruhusa kwa Sahla katika jambo hili ili aondoshewe uzito. na kuna mtazamo katika hili; kwa kuwa linapelekea kumweka mwenye uzito kama wa Sahla katika hali kama hiyo na kulitumia kama hoja na hivyo kuukanusha umaalumu na kuthibitika kwa madhehebu yanayokwenda kinyume na hayo, lakini yanaonesha kulitumia hili kama hoja.
Na wengine wameamua: kwamba asili ni kuwa kumyonyesha huko hakuharamishi, na baada ya kuthibitika hivyo utotoni asili ikaendewa kinyume na kikabaki katika asili kisichokuwa hicho. Na kisa cha Salem ni tukio la kipekee lina njia ya uwezekano wa kuwa maalumu na kwa hiyo ni wajibu kuacha kukitumia kama hoja. [Fathu Al Baariy 149/9, Ch. Dar Al Maarifah]
Na Kasani alijibu kutokana na kazi ya Bi Aisha R.A kwa Hadithi ya Salem kwa kauli yake: "ama kwa kuhusu kazi ya Bi Aisha R.A, imepokelewa kwa hakika kutoka kwake kauli inayoonyesha kurejea maneno yake. Hakika mambo yalivyo imepokelewa kutoka kwake kuwa alisema: hakiharamishi kwa kunyonya isipokuwa kitakachootesha nyama nyama na damu.
Na ilipokelewa kwamba Bibi Aisha alikuwa akimwamirisha binti ya ndugu yake Abdulrahmaan Bin Abi Bakr R.A. wote wawili, Awanyonyeshe wavulana mpaka waingie ndani kwake watakapokuwa wakubwa na kwamba kazi yake hii inakwenda kinyume na kazi ya wakeze Mtume S.A.W, hakika wao walikuwa hawaoni kuwa inaruhusiwa mtu mzima yeyote kuingia ndani mwao kwa ajili ya kumnyonyesha, na mpingaji yoyote sio hoja. [Bada'i Aswana'i 6/4]
Na kinachoonekana ni kwamba yeye R.A ametofautisha baina ya kuwa kusudio ni kulisha chakula au kunyonyesha kwa ajili ya kuhitajia hivyo, na wakati wowote lengo linapokuwa kulisha haiwi haramu isipokuwa kitakachokuwa kabla ya kuacha kunyonya maziwa, na huu ndio unyonyeshaji wa watu wote. Na kuhusu ya pili inajuzu ikiwa patatolewa hoja ya kumfanya awe katika ndugu wa karibu na kwa sababu ya haja kinajuzu kwake kisichochuzu kwa mwanamke mwngine na hii ni jitahada ya Mama wa Waumini R.A - kwa maana kuwa jambo hili haliwi zaidi ya kuwa ni tofauti ya Kifiqhi na lilivyo ni kama yalivyo masuala mengine ya Kifiqhi ambayo wanazuoni wanahitilafiana ndani yake, anayepatia anapata malipo mawili na anayekosea hupata moja ya thawabu.
Na Ibnu Hazmi ameziandikia dalili za Jamhuri ya wanachuoni pingamizi nyingi zinazokusanyika kwa pamoja katika udhaifu wa Hadithi walizozitolea ushahidi wao. Kwani Hadithi ya Ummu Salamah: "Haiwi haramu kwa kunyonya..." Hadi mwisho wake, amesema kwamba Hadithi hiyo imekatika. Kwani Fatima Bint Al Mundher msimulizaji kutoka kwa Umm Salamah hakumsikilii, kwani alimuwa mkubwa Zaidi kuliko mume wake Hesham kwa miaka kumi na miwili, na kuzaliwa kwa Hesham kulikuwa mwaka wa 60 katika Hijra, basi kuzaliwa kwa Fatima kutokana na hiya na mwaka wa 48 katika Hjrah, na Umm Salamah alikufa katia mwaka wa 59 katika Hijra, na Fatima bado ni mdogo na hakumkutana naye, basi vipi Fatima anahifadhi kutoka kwa Umm Salamah? Na hakusikilii kitu cho chote kutoka kwa shangazi wa babake Bibi Aisha mama wa waumini R.A., -na yeye ni katika ulizi wake- na kwamba ni mbali zaidi kusikia kwake na kutoka nyanya yake Asmaa Bint Abi Bakr Swidiq R.A.
Na hutolewa jawabu kutokana na hili kuwa huu ni ukereketwa: kukatika kwa Hadithi hakuna ulazima wowote kwa kuwa Fatuma Binti Mundhir alikutana na Ummu Salamah mdogo; na kuna uwezekano mtoto mdogo mno akawa na akili za kutosha za kuyaelewa mambo na kuyahifadhi. Na hakika mlisema: Hakika wakati wa kifo cha Ummu Salamah, Fatumah alikuwa binti wa miaka kumi na moja. Na huu ni umri mzuri na hasa hasa kwa Mwanamke, kwani unafaa kwa ndoa. Na kwa yule aliyefikia kiwango cha ndoa, iweje isemwe kwamba: hakika mwanamke huyo hajapevuka akili, usikivu na utambuzi wa yanayomtokea mwanaume? Pamoja na kwamba Ummu Salamah alikuwa akiishi na Bibi yake Asmaa na makazi yao yalikuwa ya pamoja, na kwa hivyo Fatumah huyu akakulia mikononi mwa Bibi yake Asmaa pamoja na Shangazi wa Baba yake Aisha R.A. wote wawili, na Ummu Salamah. Na Aisha alikufa R.A. katika mwaka wa 57 katika Hijrah, inasemekana pia mwaka wa 58 katika Hijrah, na inawezekana kusikia kwa Fatima kutoka kwake, ama nyanya yake Asmaa alikufa katika mwaka wa 73 katika Hijra, na Fatima katika wakati huo alikuwa na umri wa miaka 25, kwa hiyo kusikia kwake kutoka Asmaa kulizidi. [Zad Al Mia'ad kwa Ibn Al Qaim 524/5].
Na akasema katika habari ya: "Isipokuwa kunyonya baada ya miaka miwili" yaani baada ya mtoto huachea maziwa ya mamake. Kunyonya huko kutoka usimulizi wa Mua'mar kutoka kwa Jubair, kutoka kwa Ad Dhahaak, kutoka kwa An Nizaal Bin Sabrah, kutoka kwa Ali kutoka kwa Mtume S.A.W., basi hii ni habari inayoanguka, kwani Jubair ni anaanguka, na Ad Dhahaak ni dhaifu, na hadithi ya " Isipokuwa kunyonya baada ya miaka miwili", kutoka usimulizi wa Mua'amar pia kutoka kwa Haraamu Bin Othmaan, kutoka kwa Abdulrahmaan na Muhammad wana wawili wa Jaber Bin Abdullahi kutoka kwa baba yao, kutoka kwa Mtume S.A.W., na huyo ni anaanguka pia, kwani Haraami bin Othmaan alikufa katik Muurah.
Na alichokisema hata kukiwa na mwelekeo wa kukubali isipokuwa hakizirudi dalili zote zilizobakia. Na kama ilivyosemwa: kuirudi dalili maalumu hakumaanishi kukirudi kitu maalumu kilichotolewa dalili.
Na labda inasemekana kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha} [AL BAQARAH 233]. Ni bayana ya muda wa kunyonya kunakowajibika kwa matumizi ya mwanamke anayenyonya, na haina uharamisho nayo baada ya hayo, wala uarahisho utaktika baada ya kutimiza kwa miaka miwili.
Na tungeweza kuacha hivyo lakini dalili ya kukatika uharamu kwa kutimia miaka miwili imechukuliwa kutoka katika Hadithi za Mtume S.A.W, na pia kutokana na walivyofanya akina mama wote wa Waislamu - isipokuwa Mama yetu Aisha - na kutokana na kauli za Maswaha R.A.
Na kutokana maelezo yaliyotangulia inaonekana wazi kwamba kunyonya kunakoharamisha ni kule kunakofanyika ndani ya miaka miwili, ama kinachozidi zaidi yake kama kunyonya kwa mtu mzima basi huko hakuleti uharamu. Na tukio la Suhla na Hudhaifah ni la mtu mmoja tu na wala sio la wote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas