Utiifu kwa Wazazi katika Suala la T...

Egypt's Dar Al-Ifta

Utiifu kwa Wazazi katika Suala la Talaka.

Question

Mimi nimemwoa mwanamke ambaye ninampenda na ananipenda na sisi tunafurahi, lakini baba yangu anataka nimuache, je, ni wajibu juu yangu kumwacha? Je, kukataa kwangu kumuacha mke wangu ni kutowatii wazazi au ni kutowafanyia wema?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Sifa zote njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya utangulizi huo:
Talaka katika lugha ni: kuacha. Neno talaka ni jina, na kitenzi chake ni kuacha. Maana yake Kisharia ni: kuvunja mkataba wa ndoa katika hali au mali kwa maneno maalumu au chochote kilicho sawa na maneno yale. [Al-Bahru Ar-Raa'iq kwa Ibn Najim 3/252, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy].
Wanavyuoni wametofautiana kuhusu hukumu ya talaka kama, inaruhusiwa au hapana, na pengine katika baadhi ya nyakati hairuhusiwi kama walivyosema wanavyuoni wa umma, au hukumu yake ni tahadhari au pengine katika baadhi ya nyakati hukumu hii huwa inabadilishwa? Katika hali yoyote ile, Sharia haioni talaka yenyewe kama ni jambo zuri, bali ni baya kama haina sababu za kukubalika. Imepokelewa kutoka kwa Hakim katika Al-Mustadrak na Hadithi hii imesahihishwa na Abdullah Ibn Omar R.A, anasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. amesema: "Mwenyezi Mungu hakuhalalisha kitu anachokichukia zaidi kuliko talaka". . Imepokelewa kutoka kwa Hakim katika kitabu cha: [Al-Mustadrak Juzu 2, Uk. 214], alisema Hadithi hii mapokezi yake ni sahihi, pia imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, akisema: "Katika halali inayochukiza mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni talaka”. Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud katika Sunan yake Juzu 2, Uk. 255].
Bali Mtume S.A.W., alitaja furaha ya shetani kwa kuwatenganisha wanandoa, na hadhani kama kuna jambo linalomfurahisha zaidi shetani na ni zuri katika nafsi yake, (kama talaka). Katika Sahihi ya Imamu Muslim Imepokelewa kutoka kwa Jaber, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., anasema: "Hakika Ibilisi atakiweka Kiti chake juu ya bahari kisha atatuma jeshi lake kwa watu. Mwenye cheo cha kuwa karibu naye zaidi, ni yule mwenye kuleta chokochoko zaidi na mwenye kufitinisha (watu) zaidi. Mmoja wao humjia akamwambia: Nilikuwa kwa fulani, sikumuacha ila baada ya yeye kusema maneno kadha wa kadha, Iblisi humwambia: “Laa! Hukufanya kitu chochote. Huja (Shetani) mwingine akasema: Nilimchimba fulani hadi nikawaachanisha kwa kuwatenganisha yeye na mkewe wakawa mbali mbali.
Ibilisi baada ya kumsikiliza huyu Shetani wake: Humvuta karibu yake na kumwambiya: “Ama wewe naam. (Umefanya jambo)". Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim. Imepokelewa kutoka kwa Al-Baihaqiy katika Sunan yake kutoka kwa Ali Ibn Abi Talib, R.A, alisema: “Talaka ni mbaya ninaichukia.”
Pamoja na kuwapo hatari ya talaka na maana zake za kujitenga na uharibifu wa familia, lakini Uislamu haukuiharamisha bali umeihalilisha, lakini haukuihalilisha kuwa ni jambo jema, bali Mwenyezi Mungu akairuhusu kwa ajili ya kuwafanyia wepesi Waislamu katika hali ya kutowezekana kuishi wanandoa pamoja, kuhalilisha kwake kuna kwenda sambamba na msingi unaosema “Dhara jepesi zaidi katika madhara mawili”, ambapo mtu ambaye amemchukia mwanamke na maisha yao kwa pamoja yamekuwa ni vigumu kwao pengine akaelekea kufanya jambo la haramu na pia mwanamke, na vile vile watoto watakuwa katika hatari kubwa ya kuishi pamoja na familia inayogombana, na kwa ukubwa wa uharibufu huu Mwenyezi Mungu ameruhusu talaka mpaka awatajirishe kwa fadhila yake.
Pengine mtu mmoja atasema: Kwa nini kila mmoja miongoni mwa wanandoa hamvumilii mwenzake? Hasa kwani Mwenyezi Mungu ametupendekezea uvumilivu, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimesema: {Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake} [AN NISAA: 19].
Jibu: ni kwamba uvumilivu kama huu ndio muhimu zaidi, lakini labda haupatikani kwa wanandoa au hawawezi kuutekeleza, pengine sababu za ugomvi zinapita uwezekano wao, au pengine wao wanakaa katika hali mbaya ya kisaikolojia ambayo haiwasaidii kuwa na subira, na katika hali hii: Sharia inaweza kuamuru kwa kudumisha ndoa pamoja na ugumvi ambao unaweza kuzidi na kusababisha fitina, au uhalifu, au kupunguza haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu, au angalau kukosa hekima ambayo kwa ajili yake Mwenyezi Mungu ameitunga sharia ya ndoa, nayo ni upendo na urafiki na kuzaa vizazi wema, au sharia inaweza kuruhusu talaka na kutengana, nayo ni njia ambayo inachaguliwa na sharia ya Kiislamu, na hivyo inafahamika kwamba talaka labda inachaguliwa kwa ajili ya kumaliza ugomvi kati ya wanandoa, ili waendelee baada yake maisha yao kila mmoja peke yake au kuhusishwa na mahusiano mengine ya ndoa, ambapo kila mmoja anaweza kupata anayempenda na kumvumilia, Mwenyezi Mungu anasema: {Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hekima.} [AN NISAA: 130], na kwa hivyo, wanavyuoni wa Fiqhi walisema kuwa, ni wajibu kutaliki katika hali maalumu, na inapendekezwa kutaliki katika hali nyingine -kama ilivyotangulia- pakiwa na madhara yake, hivyo kwa ajili ya kutangulia dhara jepesi zaidi katika madhara ambayo ni magumu zaidi.
Na maana ya wema katika lugha: Unaitwa kwa kheri, fadhila, utii na uzuri, na maana yake katika sharia kuhusu wazazi ni: kuwatendea wema kwa kusema nao kwa maneno mazuri ya heshima yanaoashiria wema na upendo, na kuepuka kauli chafu zinazo sababisha chuki, hivyo ni pamoja na huruma, wema, upendo, kuwatendea wema kifedha na vitendo vingine vya uadilifu.
Uislamu umefanya kuwatendea wema wazazi kuwa ni wajibu zaidi kuliko mambo mengine, na kufanya kutowatendea wema ni katika madhambi makubwa yaangamizayo, na Mwenyezi Mungu ameunganisha kati ya kumuabudu yeye na kuwatendea wema wazazi, anasema: {Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima} [AL ISRAA: 23].
Hadithi za Mtume zilithibitisha Aya hizi za Qur`ani katika kusisitiza utiifu kwa wazazi na kuwatendea wema. Imepokelewa kutoka kwa Imamu Bukhari katika kitabu cha: [Al-Adab Al-Mufra, Al-Baihaqiy katika kitabu cha: [Shuab Al-Iman] imepokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W.,: "Radhi za Allah ni katika radhi za wazazi wawili, na chuki ya Allah ni katika chuki yao". Imepokewa kutoka kwa Al-Baihaqiy katika kitabu cha: [Shuab Al-Iman 6/177].
Pengine inaweza kutokea tofauti kati ya wajibu wa kuwaheshimu wazazi, na muendelezo wa maisha ya ndoa na faida yake baadaye kwa mtu binafsi na jamii, na hali hii hutokea kama wazazi au mmoja wao aliweka masharti ya radhi zake juu ya mtoto wake kumwacha mkewe, na katika kwa huo ikatokea hali ya kuchanganyikiwa kwa mtoto na hajui atatanaguliza utii wa nani kati yao.
Hadithi nyingi zimelitaja suala hili miongoni mwa Hadithi hizo ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Hakim katika Al-Mustadrak na imesahihishwa na Hamza Ibn Abdullah Ibn Omar akisema: "Ibn Omar alikuwa na mke wake, na alikuwa anampenda lakini Omar hampendi, akamwambia: mwache mkeo, lakini yeye akakataa na akamwambia Mtume wa Allah S.A.W., Mtume S.A.W.. na Mtume S.A.W, akasema, mtii baba yako na mwache mkeo".
Imetajwa katika kitabu cha Ibn Abi Shaybah kutoka kwa Abu Twalha Al-Asadiy, amesema: nilikuwa nimeketi pamoja na Ibn Abbas mabedui wawili wakaja wakamzunguka, mmoja wao akasema: “Mimi nilikuwa nikitaka ngamia nikaenda kwa watu basi nikampenda msichana wao nikamwoa, wazazi wangu wakaapa kwamba ni lazima nimwache, vile vile mvulana mmoja aliapa akisema: akimwacha mkewe basi atalazimika kuwaacha huru watumwa elfu moja kama zawadi, na ngamia elfu moja, Ibn Abbas akasema: hairuhusiwi kukuamuru wewe umwache mkeo au kutowatii wazazi wako. Mvulana huyo akasema: nifanyaje kwa mwanamke huyu? Ibn Abbas akasema, watii wazazi wako”
Na katika Hadithi nyingine Abu Abdul Rahman alisema: “Mvulana mmoja alikuwa akikaa kitongojini katika nyumba ambayo mama yake alikuwa bado anaishi ndani yake mpaka alipomwoa binti wa mjomba wake akampenda sana, basi mama yake alimwambia: amwache mkewe, mvulana yule akasema: Siwezi, kwani ninampenda sana na kwa hivyo siwezi kumwacha, mama yake akasema: chakula chako na vinywaji vyako ni haramu kwangu mpaka umwache mkeo, mvulana huyo akaenda kwa Abu Ad-Dardaa huko Sham, akamwelezea hali yake hiyo, Abu Ad-Dardaa akasema: Siwezi kukuamuru umwache mke wako, na siwezi kukuamuru kutowatii wazazi wako”.
Kutajwa kwa Hadithi hizi kumesababisha utata unaotambuliwa na Imam At-Twahaawiy Al-Hanafiy, ambapo aliuweka katika kitabu chake kinachoitwa “Mushkil Al-Athaar” akathibitisha kwamba Abu Ad-Dardaa mwenyewe amechanganyikiwa katika suala hili, anasema: “Abu Jaafar akasema: maana hii imemchanganya Abu Ad-Dardaa R.A. mpaka akasema kuhusu hali hii kwa aliyemwuliza hilo swali aliyotuambia Ibrahim Ibn Marzouk, Thana Abu Huzaifa Musa Ibn Masoud, Thana Sufian Ath-Thawri alisema, ametusimulia Ataa akasema, naye ni Ibn As-Saa'ib alisema Abu Abdul Rahman As-Salmi alisema: "Mmoja wenu mama yake alimwamuru aoe, na alipooa mama yake alimwamuru amwache mkewe, akaendelea mpaka Abu Ad-Dardaa akaja kumuuliza kuhusu hilo, akasema: Siwezi kukuamuru umwache mke wako, na siwezi kukuamuru uendelee kuwa naye, nikasikia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., anasema: mama ni mlango wa katikati ya peponi, uulinde mlango huu au uukose" au kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. Abu Jaafar akasema:. Tulifahamu kuwa Abu Ad-Dardaa R.A, kwamba alichanganyikiwa na jibu alipouliza kuhusu Suala hili. jibu lake lilikuwa jibu ambalo hakuamua kuendelea kuwa na mke au kumwacha, tukaangalia je, imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., Hadithi yoyote ambayo inadhihirisha ukweli wa maana hii? [Mushkil Al-Athaar 1/419, Muasasatur Risalah].
Ashafiy amechagua kuchukiza kwa kuwatii wazazi katika suala la talaka kama kuna chuki. Sheikh Al-Islam Zakaria Al-Ansari alisema: “(Inaruhusiwa kuacha mke kama akiogopa kutokutekeleza haki) miongoni mwa haki ya mke au nyingine (au kwa ukosefu wa usafi wa mke) Ibn Ar-Rafa’ah akaambatanisha suala la kuacha mke na mtoto kama akiamuriwa na baba yake, jambo ambalo ni wazi kama akimwamuru sio kwa shida (na inachukiza wakati wa usalama wa hali) kwa mujibu wa Hadithi inayosema:. "Talaka ndio ni halali inachochukiwa zaidi na Mwenyezi Mungu." [Asna Al-Matwalib 3/264, Ch. Dar Al-Kutub Al-Islamiy].
Kwa Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad Ibn Hanbal: tunawakuta wanaichukia rai ya kutowatii kwa wazazi isipokuwa ikiwa baba aliyeamuru ni miongoni mwa watu wema na wacha Mungu, Ibn Taymiyah akasema maneno ya Imam Ahmad kuwa: “Maneno ya Ahmed kuhusu uwajibu wa kumwacha mke kutokana na amri ya baba yanaifungia hali ya wema wa baba.” [Al-Fatwa Al-Kubra kwa Ibn Taymiyah 5/491, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Ibn Taymiyah amechagua uharamu wa Mtoto kuwatii wazazi wake katika kumwacha mkewe, hasa kama akiwa na watoto aliyezaa na mke huyo, ambapo Ibn Taymiyah aliulizwa kuhusu mtu mmoja aliyeoa na ana watoto, na mama yake anamchukia mke wake na akamwambia amwache, je, ni halali kwake kumwacha?
Jibu: “Hairuhusiwi kwake kumwacha mkewe kutokana na kauli ya mama yake, lakini ni lazima kwake kumfanyia wema, na kumwacha mke sio kumfanyia mama wema, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi.” [Al-Fatawa Al-Kubra kwa Ibn Taimiyah, 3/331].
Ibn Mofleh katika kitabu cha Al-Furuu ametaja kwamba hairuhusiwi kuwatii wazazi katika suala la talaka, akisema kwamba: “Kama akimwamuru mama yake Ibn Mofleh akasema: sipendi talaka yake, na sheikh wetu akazuia hayo, na amesema pia: kama ukichelea basi atakuwa hana haki ya kufanya hivyo, vile vile akasema hivyo kama wazazi wakimzuia kuoa”. [Al-Furuu kwa Ibn Mofleh 5/363, Ch. Alam Al-Kutub].
Katika kitabu cha: [Al-Adab Al-Sharia] pia Ibn Taimiyah alisema kwamba: “Wazazi hawana haki ya kumlazimisha Mtoto wao kumwoa mke asiyemtaka, na kwamba kama akikataa hawi mwenye kuwatendea vibaya wazazi wake, kwa kuwa hairuhusiwi kwa yeyote kumlazimisha kula chakula asichopenda pamoja na uwezo wake wa kula kile ambacho anachotaka mwenyewe basi hali ile ile katika ndoa, kama akila asichopenda anaweza kuvumilia uchungu wake kidogo tu, lakini uchungu wa kumwoa asiyempenda unaendekea kumuudhi mwanandoa na hawezi kuachana nao.” [Al-Adab Al-Sharia kwa Ibn Mofleh 1/446, Ch. Alam Al-Kutub].
Vile vile Al-Bahwatiy alisisitiza hivyo akisema kuwa: “(Haipaswi kuwa) kwa Mtoto (kuwatii wazazi wake), hata kama wakiwa (waadilifu katika kumwacha) mke wake, kwani hivyo sio katika kuwafanyia wema (au) kwa maana ya: Haipaswi kwa Mtoto kuwatii wazazi wake katika (kumzuia kuoa)”. [Daqaiq Uli Al-Nuha kwa Al-Bahwatiy 3/74, Ch. Alam Al-Kutub].
Mwandishi wa kitabu cha Ghidhaul Albaab alisema kuwa: “... Alisema katika kitabu cha: [Al-Adabul Kubra]: Kama wazazi wake wakimwamuru amwache mkewe si lazima afanye hivyo. Wanavyuoni wengi wamesema hivyo hiyo. Mtu mmoja alimuuliza Imam Ali R.A. akisema kuwa hakika baba yangu aliniambia nimwache mke wangu, Imam Ali R.A. akasema: Usimwache mke wako. akasema: Omar hawezi kumwamuru mwanawe Abdullah amwache mkewe? Akasema: mpaka baba yako awe kama Omar R.A.” [Ghidhaul Albaab kwa Al-Safarini 1/447, Ch. Muasasatur Risalah].
Ibn Atfiish Al-Ibadi alisema katika kitabu cha [Sharhun Nili wa Shifaaul Aliili] kwamba Mtoto hatakiwi kumwacha mkewe kama akiombwa na wazazi wake afanye hivyo, au mmoja wao hapa atakaposema: “Kama akiweka nadhiri ya kumwacha mkewe au akiombwa afanye hivyo na wazazi wake si lazima kutimiza nadhiri hiyo, na halazimishwi kuwatii katika jambo hili”. [Sharhun Nili wa Shifaaul Aliili 5/22, Ch. Maktabatul Irshaad].
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotanguliwa hapo juu katika swali hili: kumwacha mke na kuuvunja unyumba sio katika kuwafanyia wema na kuwatii wazazi wawili, wala mtoto hatakiwi kuwatii wazazi wake katika suala hili, lakini ni lazima awatendee wema na asiwakemee, na wala asidanganye katika hali yake ya kuyafikia maslahi yake mwenyewe na ya familia yake, na wakati huo huo asiwakasirishe wazazi wake na asiwatendee ubaya wowote katika suala hili, kutowatii wao kuhusu suala hili sio kuwafanyia ubaya, na kuwafanyia vibaya kwao ni haramu kwa hali yoyote.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas