Hukumu ya Kuvaa Suruali kwa Wanawak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kuvaa Suruali kwa Wanawake.

Question

Ni ipi hukumu ya vazi la suruali kwa wanawake? 

Answer

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa Njema za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake, na Masahaba wake, na waliomfuata. Na baada ya hayo:
Suruali ni aina ya mavazi ambayo yanasitiri sehemu ya chini ya mwili wa binadamu, kuanzia kiunoni hadi chini ya miguu, pamoja na kuigawanya miguu miwili katika kuisitiri, maana kila mguu hufunikwa peke yake, bila ya kukutana pamoja katika nguo moja ambayo huizunguka. Nguo ya aina hii inaitwa suruali.
Rai iliyochaguliwa kutoa katika fatwa ni: Kuwa inajuzu kuvaa wanawake suruali, kwa sharti la kuwa: Kuhakikisha masharti ya kusitiri yanayotakiwa kisheria. Hakika mavazi anayoyavaa mwanamke yana masharti, ambayo wanazuoni wamekubali kuwa ni lazima kupatikana katika mavazi ya mwanamke Muislamu, nayo ni kuisitiri uchi na hayadhihirishi, na wala kuwa yamebana kufichua vilivyo chini yake.
Mipaka ya uchi ambayo mwanamke analazimika kuisitiri ndani au nje ya Swala ni mwili wake wote, isipokuwa uso na vitanga vyake viwili vya mikono, na haya ni madhehebu ya wengi wa wanazuoni, miongoni mwa madhehebu ya Hanafiy, Malikiy, na Shafiy, na pia ni madhehebu ya Al-Awzai’iy, Abu Thawr, miongoni mwa wenye jitihada wa Salafi, na kauli moja katika madhehebu ya Ahmad.
Kuhusu mwanamke, kuvaa mavazi yanayofichua yaliyo chini yake ni haramu; kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim katika kitabu chake, kutoka kwa Abu Huraira R.A., alisema: Mtume S.A.W., anasema: “Aina mbili za watu wa motoni ambao sikuwaona; wanaoshikilia mijeledi sawa na mikia ya ng’ombe, na wanawapigia watu; na wanawake wanaovaa mavazi, lakini wanaonekana kuwa uchi, wananyonga mabega, na kutembea wakichechemea, vichwa vyao vinaonekana kama nundu za ngamia zinazomili. Hawa hawataingia Peponi wala kupata harufu yake, na hakika harufu ya Pepo itapatikana kutoka umbali mkubwa kabisa”.
Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Sharh yake ya Sahih Muslim: 14/110, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy] anasema kuhusu kubainisha maana ya “Wanavaa mavazi, lakini wanaonekana kuwa uchi” kuwa: ni kuvaa nguo za kubana ambazo hufichua rangi ya mwili wake”. [Mwisho].
Na An-Nafarawiy mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha: [Sharh ya Risala ya Abu Zaid Al-Qairawaniy: 2/310, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Haijuzu maana yake na inaharamishwa wamawake kuvaa mavazi yaliyobana ambayo yanabainisha miili yao wanapotoka majumbani mwao, kwa muhtasari: Inaharamishwa kwa wanawake kuvaa mavazi yanayofichua yaliyomo miilini mwao wao kama vile: Matiti yao, makalio yao, kwa kumfanya mtu asiyeruhusiwa kuwatazama, atazame”. [Mwisho].
Na kuvaa suruali ambayo inahakikisha masharti ya kujisitiri inajuzu, kwa sababu ni msingi, maana suala la kuvaa kwa mwamamume au mwanamke ni halali, isipokuwa limekatazwa kwa mujibu wa dalili, au kuambatana na maana iliyopo katika Sharia; kama vile: Kuvaa Hariri kwa wanaume, au kuwa kwa lengo la kujiona au kiburi.
Na zimepokelewa Hadithi zinazothibitisha asili ya kujuzu; Al-Bazzar amepokea katika Musnad yake, kutoka kwa Ali, alisema; “Nilikuwa na Mtume S.A.W, kwenye Al-Baqii’- yaani: Baqii’ Al-Gharqad- katika siku yenye mvua, hapo mwanamke alipita akiwa juu ya punda, na alikuwa na mwenye punda, akapita juu ya shimo, akaanguka, na Mtume S.A.W, akauepusha uso wake, na watu wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Hakika yeye ni mwenye suruali, akasema Mtume: Ewe Mola! wasamehe wenye suruali wa Umma wangu”.
Na Al-Baihaqiy katika Shua’ab Al-Imaan, kutoka kwa Abu Huraira R.A, alisema: “Wakati Mtume S.A.W., alipokaa kwenye mlango wa msikiti, mwanamke alipita akiwa juu ya kipando, na alipokuwa karibu na Mtume S.A.W., kipando kikajikwaa, na Mtume S.A.W., akauepusha uso wake, na nguo za mwanamke zikafichuka, pakasemwa; Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Yeye ni mwenye suruali, akasema Mtume: Mwenyezi mungu! Warehemu wenye suruali”.
Hadithi hii kwa mapokezi yake kwa jumla inapanda kwenye daraja ya Hassan, kama alivyosema Imamu As-Sayutiy katika kitabu cha: [Al-Laali Al-Masnuua’ah; 2/223, Ch. ya dar Al-Kutub Al-ilmiyah], na Imamu Ash-Shwkaniy katika kitabu cha Al-Fawaid Al-Majmuu’ah, Uk. 189, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]
Hadithi hii ni dalili ya kujuzu kuvaa suruali ambazo sura yake ni sawa na suruali za siku hizi. Kuhusu kuvaa mavazi mengine juu yake ni suala lingine ambalo linarejea desturi.
Pia faidaya Hadithi hii: Kutoharamisha kwa lengo la kufanana na wanaume au wasio Waislamu. Hapa inaongezeka katika suala hili kuwa: Uhalisia unapingana na suala la kufanana na wanaume; maana kuna mavazi ya aina hii ambayo yanahusu wanaume, na mengine yanahusu wanawake.
Kuhusu kufanana na wasio Waislamu sio vibaya kwa uwazi, bali vibaya iliyokatazwa ni kujifananisha katika dini kwa makusudi, lakini kuhusu mambo ya kawaida na hayana lengo la kujifananisha basi hayakatazwi; na Mtume S.A.W., aliswali katika Juba la Sham, kama ilivyopokelewa katika Vitabu Sahihi vya Sunna, kutoka kwa Hadithi ya Al-Mughira Ibn Shuu’ba, na Imamu Bukhariy aliweka anwani ya mlango huu kwa kusema: Mlango wa Swala katika Juba la Sham.
Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Al-Fat-h: 1/473, Ch. ya Dar Al-Ma’arifah] alieleza hivyo akisema: “Anwani hii inaonesha kuwa: Inajuzu kuitekeleza Swala katika nguo za makafiri, zisizokuwa na najisi, na alitaja neno la Sham, kwa kuzingatia tamko la Hadithi hii, na wakati huo Sham ilikuwa nchi ya ukafiri”. [Mwisho].
Sharti la kusudio katika kufanana hasa si la wazi, kwa sababu kufanana ni kushirikiana katika tendo, na inamaanisha: Kufunga nia na kuelekea kulifanya tendo kwa makusudi na kulijaribu, na kwa kuzingatia kusudio la mtendaji ni miongoni mwa misingi ya Sharia. Dalili ya hayo pia, alivyoipokea Imamu Muslim katika kitabu chake sahihi , kutoka kwa Jaabir R.A., alisema: “Mtume S.A.W., aliugua, nasi tuliswali nyuma yake naye ameketi, akatutazama, akatuona tukisimama, akatuashiria tukaketi, na alipotoa salamu alisema: Ninyi mmekaribia kufanya kama Waajemi na Warumi, wakisimama mbele ya wafalme wao, na wafalme wakiwa wameketi, msifanye hivyo, fuateni Maimamu wenu, akiswali hali ya kusimama, basi swalini hali ya kusimama, na akiswali hali ya kuketi, swalini hali ya kuketi”.
Na kauli yake (mmekaribia) inaonesha kuwa kutokuwepo habari, lakini inakaribia kuwepo, na tendo la Waajemi na Warumi limekwisha fanywa, lakini Masahaba hawakukusudia kufanana nao, kwa hiyo sifa hii imeepushwa nao kisharia.
Na baadhi ya wanazuoni walieleza hivyo katika vitabu vyao; na Ibn Nujaim mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy katika kitabu cha: [Sharh Al-Kanz: 2/11, Ch. ya Dar Al-Kitaab Al-Islaamiy] anasema: “Jua kuwa kufanana na Watu wa Kitabu hakuchukuliwi katika kila kitu, na sisi tunakula na kunywa kama wanavyofanya sawasawa, lakini hakika haramu ni kujifananisha nao kwa vilivyo vibaya, na kwa nia ya kujifananisha”. [Mwisho].
Asili ya kusitiri uchi ni kusitiri rangi na sio ukubwa; kwa sababu ni vigumu kujiepusha nayo, na hii imenukuliwa na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Malik, Hanbal, na shafiy. Katika kitabu cha: [Ash-Sharh Al-Kabiir Li Mukhtasar Khaliil, na Sheikh Ad-Dardiir Bi-Hashiyat Ad-Disuuqiy, miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Malik: 1/217-218, Ch. ya Dar Ihiyaa Al-Kutub Al-Arabiyah]: “Na mavazi yanayouainisha uchi yanachukiza kwa sababu ya wepesi wake au kwa sababu nyingine kama vile mkanda wa nguo kwa kubana na kuzunguka kwake mwilini, kama vile suruali, hata kama ni nje ya swala kwani hilo sio vazi la wema waliotangulia, na sio ikiwa uainishaji huo upatikane kwa nguo kusukumwa na upepo au kuloana kwa maji haichukizi ”.
Sheikh Ad-Disuoqiy alieleza katika kitabu cha: [Al-Hashiyah yake] akisema: “Kauli yake: (mavazi yanayoainisha mwili yanachukiza) yaani inachukuza kuvaa mavazi yanayoainisha uchi, hata nje ya Swala, hakika tumekadiria vazi; kwa kuwa hukumu zinaambatana na matendo. Na kauli yake ( kwa wepesi wake) yaani kwa ajili ya wepesi wa nguo, maana yake ni kwamba na kilicho faradhi ni kutoonekana uchi wake hata kidogo, au kuonekana kwa kuangalia na kuzingatia, na kama imetangulia kuwa chukizo la kuvaa kwake hivyo ni kwa ajili ya kuzuia kama inavyofuatwa na wanazuoni na wala sio kuharamisha (kauli yake: kama mkanda) kwa maana ya juu ya nguo isiyo nyepesi, kwa kuwa nguo iliyotajwa ni maalumu kwa kuainisha utupu kwa sababu ya mkanda, lakini kuvaa mkanda juu ya Kanzu hakuainishi sehemu kuu au ndogo ya utupu, kama vile makalio ya mtu basi hapo mkanda wa kanzu unaofungwa katikati utakuwa unachukiza na sehemu inayochukiza ni kuufunga juu ya nguo kama kufanya hivyo sio kawaida ya watu au kufanya hivyo kwa ajili ya kazi maalumu, na kama sio hivyo basi hakuna chukizo lolote hata katika swala, kama kwa mfano alikuwa mtu ameuvaa mkanda huo kisha akahudhuria swala na hilo pia halichukizi katika swala yake hali ya kuwa ameuvaa mkanda huo, na sehemu ya chukizo haiuainishi utupu, kama hatakuwa ameuvaa mkanda juu yake kitu kama juba na kama sio hivyo basi hakuna chukizo. Na kauli yake (kama suruali) hivyo ndivyo inavyosikika kilugha kinyume na suruali, na imekwishaeleweka kuwa kuivaa suruali kunachukiza kama hakuna nguo yoyote inayovaliwa juu yake hata kama hali itazorota kwa nguo hiyo, na kama sio hivyo basi hakuna chukizo lolote.
Na mtu wa kwanza kuvaa suruali ni Bwana wetu Ibrahim A.S. Na Je, Mtume wetu S.A.W., alivaa au hakuvaa? Kuna kauli tofauti, lakini iliyo sahihi kuwa Yeye alizinunua nguo za aina hiyo, kama ilivyotajwa katika Vitabu vinne vya Sunna.
Kauli yake (kwa sababu siyo miongoni mwa mavazi ya Salaf) haya ni maelezo ya chuki kwa suruali, na siyo chukizo la linaloainisha kwa uwazi, maana sababu ya chukizo ni kwa uainishaji wa uchi wenyewe.
Kwa muhtasari: Sababu ya chukio la suruali ni mambo mawili: Uanishaji na sio miongoni mwa mavazi ya Salaf. Na ilikuwa bora kwa mwenye maelezo aseme katika ibara yake (na kwa sababu siyo miongoni mwa mavazi ya salaf)… yaani kwa kuongeza (na).
Na kuhusu chukio lililoainishwa na nyingine hivyo hivyo imejiainisha yenyewe; kwa hiyo, imesemwa kuchukia kuvaa nguo ya chini (Miizar) ingawa ni miongoni mwa mavazi ya Salaf. Na maana ya (Miizar) hapa ni kitambaa cha kuvaliwa katika kiuno kama vile: Taulo ya chooni, lakini ikiwa maana yake ni nguo inayofunika mwili wote kama vile; kanzu au juba, basi haichukiwi kabisa, kama alivyosema hivyo Ibn Al-Arabiy, kwa kuuepusha uainishaji, na kwa kuwa ni miongoni mwa mavazi ya Salaf.
Na kwa muhtasari, baadhi yao waliieleza (Miizar) kuwa nguo inayovaliwa juu ya mwili wote, mfano wa kauli ya Ibn Al-Arabiy, kwa hiyo alihukumu kuwa kutochukiwa, na wengine waliieleza kuwa nguo inayovaliwa juu ya kiuno, kwa hiyo walihukumu kuichukia”. [Mwisho].
Ibn Hajar Al-Haitamiy katika kitabu cha [Sharh Al-Muqadimah Al-Hadhramiyah, miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Shafiy, Uk. 115, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] anasema: “Sharti la kusitiri ni ndani na nje ya swala ni kufunika kusitiri kutokana na nguo au kingine, pamoja na kusitiri rangi ya ngozi, kwa hiyo inatosha iliyozuia kuona rangi ya ngozi, hata lau ikidhihirisha ukubwa, kama vile suruali nyembamba, lakini hii kwa mwanamke ni makuruhu, na kwa mwanamume ni kinyume’. [Mwisho].
Katika kitabu cha: [Ar-Rawdh Al-Murbii’, na Al-Bahuutiy mfuasi wa madhehebu ya Hanbal:, Uk. 72-73, Ch. ya Dar Al-Muayad, na Muassasat Ar-Risalah]: “(miongoni mwake) yaani miongoni mwa sharti la usahihi wa Swala (kusitiri uchi). Ibn Abdil Bar anasema: “Walikubali pamoja kuwa: ubatili wa swala ya aliyeacha nguo yake, hali ya kuwa anaweza kujisitiri nayo, na akaswali akiwa uchi.
(Katika lugha ya Kiarabu: Satr: maana yake kujisitiri, na Sitr: maana yake Kusitiri (Pazia), na A’awra: maana yake upungufu na kitu kibaya; A’awraa’: maana yake ubaya).
Na utupu katika Sharia ni: uchi wa mbele na wa nyuma, na kila kilichosababisha Haya kwa kuonwa kwake, kama tutakavyoeleza baadaye; (lazima) mtu ajisitiri hata anapokuwa peke yake, hali ya upweke, giza, na nje ya swala, (kwa kitu kisichoeleza ngozi yake) yaani rangi ya ngozi ya tupu, ama nyeupe au nyeusi; kwa sababu kujisitiri ndiyo iinapelekea njia hii, na haizingatiwi kuueleza ukubwa wa kiungo, kwa sababu haiwezekani kujiepusha nacho”.
Na mavazi yanayobana ya wanawake, miongoni mwake ni suruali zinazobana ambazo huchochea matamanio na hupelekea fitina, na mavazi hayo yamekatazwa kwa sababu hii. Kwa hiyo ni haramu kwa sababu nyingine na siyo sababu yake yenyewe.
Kwa hiyo wanazuoni waliangalia jambo hili inavyokusudiwa na Sharia na kuihimiza kama kujisitiri na kukataza tangulizi za kupelekea haramu, kama vile mtazamo na upweke, n.k., na jambo hili lina mifano mingi.
Baadhi ya wanazuoni walieleza kukataza mwanamke kudhihirisha urembo wake kwa wengine, isipokuwa mume wake, hata akiwa miongoni mwa jamaa zake. Katika kitabu cha [Sharh Matn Al-Iqnaa’, na Al-Bahuutiy mfuasi wa madhehebu ya Hanbal; Kashful Qinaa’: 5/15, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]: “(Inaharamishwa kujipamba) mwanamke isipokuwa kwa Mume wake na Bwana wake; (akiwa ni mtumwa) kwa sababu ni dhana ya fitina”. [Mwisho].
Kama walivyoeleza baadhi yao pia kuwa uharamu wa kutazama uso na vitanga vya mwanamke, japo kuwa vimesalimika na fitina; katika kitabu cha [Sharh Al-Minhaaj, na Al-Mahalliy, miongoni mwa vitabu vya Fiqhi ya madhehebu ya Shafiy: 3/209, Bi-Hashiyatay Qalyubiy wa A’amira, Ch. ya Dar Al-Fikr]: “(Inaharamishwa kabisa kwa mtu baleghe kuitazama tupu ya mwanamke huru, mkubwa, aliye halali kumuoa , hata kidogo; na muradi wake kwa kusema: (mkubwa) yaani asiye mdogo, ambaye hana matamanio, (na uso wake na kitanga chake) yaani kitanga kimoja katin ya vitanga viwili, (kwenye kuogopa fitina) yaani kila sababu kama kuwa pweke (na aliye halali kumuoa), kwa sababu kutazama ni dhana ya fitina, na kuchochea matamanio, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Waambie Waislamu wanaume wainamishe macho yao (wasitazame yaliyokatazwa)}. [AN NUUR 30], na kauli yake Mwenyezi Mungu: {wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika}. [AN NUUR: 31], na hii imetafsiriwa kuwa ni uso na vitanga. [Mwisho}.
Kwa mujibu wa maelezo hayo yaliyotangulia: inajuzu kisheria kuvaa vazi pana la suruali kwa mwamanake ambalo linayafikia masharti ya mavazi, na hakuna kosa juu yake. Na hii ni kinyume na suruali nyepesi na ya kubana ambayo inaainisha kiwango cha utupu, na hii haijuzu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas