Kushikamana na Mavazi ya Mtume na K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kushikamana na Mavazi ya Mtume na Kukiuka Uvaaji wa Nguo za Watu wa Nchi.

Question

Tunawaona baadhi ya walioshikamana na dini wanasema: Sisi tunalazimika kuvaa mavazi yaliyopokelewa kuwa Mtume S.A.W, alikuwa akiyavaa, na kuwa hii ni Sunna, na asiyefanya hivyo atakuwa amepinga Sunna. Je, maneno kama haya ni sahihi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba zake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mavazi ni: nguo inayousitiri mwili na kuepusha joto na baridi. Na kutumia mavazi kuna hukumu tano: Faradhi ni: Ni mavazi yanayoisitiri tupu na kuepusha joto na baridi, na Mwenyezi Mungu amesema: {Enyi wanaadamu! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila Sala}. [AL AARAF: 31], yaani mavazi yanayositiri tupu zenu wakati wa Swala; linalotakiwa na linalopedeza ni: Mavazi yanayoleta asili ya mapambo na kudhihirisha neema, na Mwenyezi Mungu amesema: {Na neema ya Mola wako isimulie}. [AD DHUHAA: 11]; Makuruhu ni: Mavazi yanayopelekea dhana ya kiburi na kujiona; Haramu ni: Mavazi kwa kusudio la kiburi na kujiona.
Na asili ya hukumu ya mavazi ni halali, kwa kutojali mada ya kutengenezwa mavazi, isipokuwa kuwepo dalili inayosababisha uharamu, kama vile kuvaa hariri kwa wanaume.
Sunna katika istilahi ya wanazuoni wa Misingi ya Fiqhi ni asili miongoni mwa asili za hukumu ya kisheria, na dalili miongoni mwa dalili zake, ambayo ngazi yake ni ya pili baada ya Qur`ani Tukufu; na wanazuoni waliifafanua kuwa: “Ni ile iliyotoka kwa Mtume S.A.W., isipokuwa Qur`ani, na ikiwa ni kauli inaitwa ni Hadithi, au kitendo au kukiri”. [Sharh At-Talwiih Ala At-Tawdhiih: 2/3, Ch. ya Maktabat Subeih]
Na kwa wanazuoni wa Fiqhi Sunna ni: ile Inayolingana na wajibu, mubaha (halali) na mengineyo, na kwa maoni yao Sunna ni hukumu iliyochukuliwa katika dalili, nayo ni kuitekeleza kuna thawabu, na kuiacha hakuna adhabu, yaani Sunna ni kisawe cha kinachotakiwa, kinachopendeza, kujitolea, utiifu, ibada ziada, wema, kinachohimizwa, na fadhila.
Na kwa wanazuoni wa Hadithi Sunna ni: ile iliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., ikiwa ni kauli, tendo, kukiri, au sifa ya kiumbo au ya kimaadili, na ikiwa hii ilikuwa kabla ya Utume au baada yake.
Tunaangalia kuwa wanazuoni wa Hadithi walirefusha dhana ya Sunna; kwa sababu wao hawaiainishii iwe aina ya kuleta hukumu ya kisheria tu, lakini makusudio yao ni kubainisha kuwa Mtume S.A.W, ni mwongozi wetu, na Mwenyezi Mungu alituambia kuwa yeye ni kigezo chetu na mfano wetu, kwa hiyo walinukulu kila linaloambatana na yeye la sira na tabia, sifa na habari, na ikiwa hilo lilinathibitisha hukumu ya kisheria au la, na hii ni kinyume ya wenye misingi ya Fiqhi, ambapo wanatafuta Sunna ambayo ndani yake kuna dalili ya hukumu ya kisheria. [Hashiyat Sheikh Bakhiit Al-Mutii’iy Ala Nihayat As-Suul: 3/5, Ch. ya A’alam Al-Kutub, na It-haaf Dhawiy Al-Basair na Dkt. Abdul Kariim An-Namlah: 3/14, Ch. ya Dar Al-A’asimah].
Kwa mujibu wa hayo, haifai kuweka muradi wa wenye Hadithi- kuhusu maana ya Sunna inayoambatana na kumwelezea Mtume S.A.W, sura yake na mavazi yake- mahali pa maana ya Sunna kwa istilahi ya wenye Fiqhi kutokana na inavyopendeza na inavyotakiwa iwe; kwa sababu huu ni mchanganyo wa wazi.
Mavazi ya mwanamume na mwanamke ni miongoni mwa mambo ya mazoeo yanayoambatana na desturi ya kila taifa na jamaa, zamani yake na mahali pake, na kwa kuangalia faida na madhara kutokana na matumizi yake, na siyo ya mambo ya ibada yanayomlazimu mwenye mavazi apate aina au mavazi maalumu, na asili ya hayo ni mubaha, lakini mavazi yakilingana na uharamu kisheria kwa mfano akivaa aina ya mavazi kwa ajili ya kiburi au kujioa, au mwanamke anavaa mavazi yanayodhihirisha tupu yake, au anavaa mavazi yanayolingana na mavazi ya makafiri, basi hayo yote hayajuzu kisheria, siyo kwa sababu ya mavazi yenyewe, lakini kwa ajili ya makatazo yanayoambatana nayo, na huenda hayo ni haramu au makuruhi kutokana na mazingatio ya makatazo hayo.
Imamu Bukhari amepokea Hadithi Mua’allaq kuwa Mtume S.A.W, alisema: “Kuleni, kunyweni, vaeni, na toeni sadaka, bila ya ubadhirifu wala kujiona”, na Ibn Abbas alisema: kula unavyotaka, vaa na kunywa unavyotaka, lakini yaepuke mambo mawili, nayo ni ubadhirifu na kujiona. [Sahih Al-Bukhariy, Kitaab Al-Libaas]. Na hii huonesha kuwa katazo linahusu tendo la ubadhirifu na lililokusudiwa kujiona, na kama mambo hayo mawili yakiepushwa basi hakuna matata.
Na haikutajwa matini katika Sharia Tukufu ambayo yanaainisha aina ya mavazi wala sura yake; kwa sababu Uislamu unatunga kanuni zinazofaa kwa kila zamani na mahali, na ilivyokubaliwa na watu kuhusu sura ya mavazi, upendo wa mapambo, na kutengeneza mavazi, hayo yote ni mambo ya kisheria katika Uislamu, na Vitabu vya Sunna vimenukulu kuwa Mtume alikuwa akivaa mavazi myembamba na mapana sawasawa, na mfano wa hayo Masahaba na Matabii’in. [Fat-h Al-Bariy na Ibn Hajar: 10/268, Ch. ya Dar Al-Ma’arifah], na hakupokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, na mmoja kati ya Masahaba wake, na Matabii’in sifa au sura maalumu kuhusu mavazi, wakiwa wanaume au wanawake.
Na Sharia sharifu imeacha kubainisha sura ya mavazi na njia ya kuyazunguka mwili na maelezo yake, kwa kuzingatia kuwa hayo ni mamabo ya dunia, ambayo yanajulikana yawe dharura, majaribio, na mazoeo, lakini amekataza kuvaliwa mavazi ya kujiona akisema: “Aliyevaa mavazi ya kujiona, Mwenyezi Mungu, siku ya Kiyama, atamvalisha mavazi mfano wake, kisha yatawashwa moto”. [Sunan Abu Dawud: 4029].
Na Imamu Ahmad aliona mtu akivaa juba yenye mistari myeupe na myeusi, akamwambia: Yaache haya, na vaa mavazi ya watu wa mji wako, na akasema: Siyo haramu, na ungelikuwa Makkah au Madinah, basi nisingelikulaumu. [Ghdhaa Al-Albaab: 2/163, Ch. ya Muassasat Qurtubah]
Na Ibn Abi Shaiba katika Muswanaf yake, kutoka kwa Abbaad Ibn Al-A’awaam, kutoka kwa Al-Huswain, akisema: “Zabiid Al-Yamiy alikuwa akivaa mavazi ya zamani, akasema: nilimsikia ibrahim akimlaumu, akasema: watu walikuwa wakiyavaa mfano wake, akasema: ndiyo, lakini waliokuwa wakiyavaa walikwenda, na kama mtu akiyavaa siku hizi basi watu watamfedhehesha na kumuashiria kwa vidole”. [Muswanaf Ibn Abi Shaiba: 5/205, Ch. ya Maktabat Ar-Rushd]

Na Ibn Hajar alisema: “Kuangalia mavazi ya wakati ni miongoni mwa uungwana, isipokuwa yale mavazi yenyekusababisha dhambi, na kupinga ada ya mavazi ni aina ya kujiona”. [Fat-h Al-Bariy: 10/306].
Kwa hiyo, haifai kwa muislamu kupingana na watu wa zama zake kuhusu mavazi na mila na desturi zao ambazo ni nzuri, kwa sababu hali hii hupelekea kujiona mpweke.
Imamu Ibn Taimiyah alisema: “Ada ya Muislamu kuhusu mavazi kuwa: Anavaa na kula alivyopewa na Mwenyezi Mungu kwa chakula na mavazi ya mji wake, na hayo yanahitilafiana kutokana na miji”. [Majmuu Al-Fatawa: 22/311, Ch. ya Majmaa Al-Malik Fahd Li Tibaa’at Al-Mus-haf Ash-Shariif]
Kwa mujibu wa maelezo hayo yaliyotangulia tunasema: Njia ya kuvaa mavazi yaliyojulikana wakati wa Mtume S,A.W., ambayo Mtume S,A.W., alikuwa akiyavaa, muislamu halazimiki kuifuata; kwa sababu ni mambo ya mila na desturi nzuri, ambazo zinaambatana na makubaliano ya kila taifa au jamaa, pamoja na kuzingatia zama na mahali pake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas