Alama za Manunuzi kwa Njia ya (Cred...

Egypt's Dar Al-Ifta

Alama za Manunuzi kwa Njia ya (Credit Card).

Question

Baadhi ya maduka makubwa humpa mnunuzi wa bidhaa zake kwa njia ya kadi ya manunuzi (Credit Card) Alama za manunuzi ya bidhaa hizo kwa mujibu wa uchache au uwingi wake, na mwenye Alama (alama) hizi huwa anaweza kuzinunulia bidhaa kwa wakati wake baadaye, na kwa hivyo kuna baadhi ya maswali, na miongoni mwa maswali hayo ni:
1-Je, inajuzu kuzinunua bidhaa kwa Alama zinazopatikana kutoka katika maduka hayo?
2-Je, inajuzu kuziuza Alama hizi kwa mtu mwingine?
3-Mtu yeyote mwenye salio akinunua kwa mtu mwingine bidhaa kutoka katika maduka haya na kuzilipa pesa, na wakati huo huo mnunuzi wa kwanza mwenye salio kwenye kadi ya manunuzi (credit card) akapata Alama za salio kutokana na uuzaji huo, je, jambo hili ni kama mkopo wa faida, na anayekopa haruhusiwi kuuchukua?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Njia za matangazo ya biashara ni nyingi na lengo lake ni kuwavutia wanunuzi katika maduka ya wenye matangazo hayo, na miongoni mwa njia hizi, baadhi ya maduka humpa mnunuzi baadhi ya motisha, kama: Kumpa mnunuzi baadhi ya Alama zinazomnufaisha baada ya kukusanya idadi maalumu ya alama hizo ambazo anaweza kunufaika nazo kwa kuzinunulia bidhaa zingine katika duka hilo hilo, na wakati huo huo mnunuzi mwenye Alama hizi anaweza kuziuza Alama zake kwa mtu mwingine.
Na katika hali nyingine baadhi ya wenye Alama hizi huwa wanataka kuongeza Alama zao za salio ili kuzinunulia bidhaa zingine wasizozihitaji wao wenyewe, kwa salio lao, na baadaye kumtamafuta mtu mwingine anaezihitaji bidhaa hizo na kumuuzia kwa fedha taslim. Na huwa kama vile anamkopesha thamani ya bidhaa kwanza na akanufaika na alama zake kutokana na mkopo huo.
Na mwuzaji anapompa mnunuzi Alama za salio wakati wa kununua bidhaa kutoka kwake ni kama zawadi yenye masharti iliyozungumzwa na wanachuoni wa Fiqhi katika mlango wa Zawadi. Ama uuzaji wa Alama hizo baadaye huingia katika mlango wa kuuza. Kama inavyodhihirika na ilivyo wazi, na sehemu yake ni katika mlango wa Kuuziana. Ama mnunuzi kukopa mkopo wakati wa kununua, na akurejesha mkopo huo kwa faida – nayo ni alama za salio – kwa faida ya mkopeshaji, wanazuoni wanalitaja jambo hili kuwa ni katika mlango wa kukopa.
Na hukumu ya kisharia katika suala la kwanza ambalo ni kununua bidhaa kwa sababu ya kupewa Alama za salio kutoka kwa mchuuzi kwenda kwa mnunuzi ni jambo linalojuzu, na ni sawa na zawadi inayoshurutishwa.
Na dalili ya kuswihi kwake ni Hadithi iliyopokelewa na Imamu Tirmidhi kutoka kwa Amru bin Auf Al-Muzani kwamba: Mtume S.A.W., anasema: "Waisilamu wanafuata MAsharti yao waliowekeana, isipokuwa sharti lililoharamisha Halali au lililohalalisha Haramu". Imamu Tirmidhi amesema: "Hadithi hii ni Hasan na ni Sahihi".
Na dalili ni kwamba Sharia imejuzisha masharti yasiyokiuka Sharia hiyo, na hasa kwa kuwa zawadi ni katika mlango wa mambo ya misaada, na inajulikana kuwa makubaliano ya kujitolea yana usamehevu ndani yake tofauti na yale ya kulipana.
Na kwa mfano wa tuliyokwishayasema, kuna Jamhuri ya Wanachuoni inaoufuata mwelekeo huo. Anasema Karafiy: Ibnu Yunus amesema: unaonaje kama mtu atakuomba umpe Dinari, na kisha ukakubali kwa kusema: Ndio. Kisha ikakudhihirikia, Malik anasema: wewe hulazimiki kutoa. Na lau ingelikuwa kuachana kwa wanaodaiana kwa kupeana ahadi na kuwekeana mashahidi, basi ingekulazimu wewe kwa kubatilisha kwako deni kwa kuchelewa. Anasema Sahnuun: kinachowajibika kwa kuhesabika ni kwa kuweka masharti kama vile unaposema: Ivunje nyumba yako na mimi nitakukopesha; au toka na uende Hijja, au: nunua bidhaa fulani, au muoe mwanamke na mimi nitakukopesha; kwani wewe umemuingiza katika ahadi yako kwenye jambo hilo. Ama ikiwa ni kiaga tu kama kilivyo basi hakiwi wajibu kukitekeleza bali kukitekeleza ni katika maadili mazuri. Anasema Asbaghu: iwapo atakwambia mtu: ninataka kuoa kwa hiyo nikopeshe, na wewe ukamkubalia kwa kuitikia ndio, basi maamuzi yanakuangukia, ni sawa sawa mtu huyo alioa au la. Na vile vile mtu akikwambia: niazime mnyama wako mpaka sehemu Fulani, kwa sababu ya hitajio alilolisema, au: nikopeshe kiasi kadhaa ili ninunulie bidhaa Fulani, na wewe ukasema: Sawa. Hivyo ndivyo alivyotoa hukumu Umar bin Abdul Aziiz. [Al-Zakherah kwa Al-Qorafy 6/297, cha, Dar Al-Gharb Al-Islamy].
Anasema Mardaawiy: Kauli yake "Haijuzu kuambatanisha zawadi na sharti) huu ni mwelekeo, na ndio unaofuatwa na wafuasi wetu isipokuwa yule tuliomtenga, na wengi wao wameafikiana na mtazamo huu, na Harethiyu ametaja kuwa inajuzu kuambatanisha zawadi na Sharti. Nilisema: na Sheikh Taqiyu Diin, Mola amrehemu, aliichagua rai hii, na aliitaja kutoka kwake katika kitabu cha Al-Faeq". [Al-Insaf 7/133, Ch. Dar Al-Turath Al-Araby]
Ibn Al-Qayyim anasema: Ni ipi dalili ya uharamu wa kuambatanisha zawadi na sharti? Na ilisihi kwa Mtume S.A.W kwamba yeye aliambatanisha zawadi na Sharti, kwa Hadithi ya Jaabir aliposema: Kama mali ya kutoka Bahraini ingeletwa ningekupa kiasi hiki, na kiasi hiki, na kiasi hi. Utoaji wa aina tatu. Na alikuja kulifanikisha jambo hili, Rafiki yake Kipenzi R.A, pale mali ya kutoka Bahraini ilipoletwa baada ya Mtume S.A.W., kuiaga dunia. Na ikiwa itasemwa: hiyo ilikuwa ni Ahadi ya Mtume sio sharti, sisi tunasema: Na zawadi inayoambatanishwa na sharti ni ahadi. Na hivyo ndivyo alivyofanya Mtume S.A.W., alipomtumia zawadi ya Miski mfalme Najashi, akamwambia Ummu Salama: Hakika mimi nimemzawadia Mfalme Najashi Vazi na chupa za Miski. Na mimi simuoni Najashi isipokuwa ameshaiaga dunia, na mimi sioni zawadi yangu isipokuwa ni yenye kunirejea mwenyewe, na ikiwa itarejeshwa basi ni yako. Na imetajwa hii Hadithi. Imepokelewa na Ahmad. Kilicho sahihi ni kuambatanisha zawadi na Sharti, kwa kufuata Hadithi hizi mbili za Mtume S.A.W. [Ighathatu Al-Lahfan Min Masayed Al-Shaytan 2/16, Ch. Maktabatu Al-Maaref-Al-Reyadh].
Na hakuna ubaya wowote wa kuziuza alama hizi, na dalili ya jambo hili: ni kwamba alama hizi zina thamani ya halali kisheria, na kwa hivyo zinaingia katika ujumla wa kujuzu kwake mtu kuuza anachokimili. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amehalalisha kuuza} [AL BAQARAH: 275]. Na jambo kama hili halihitaji maneno mengi ya kuliweka wazi.
Ama kuzipatia Alama hizi baada ya kumkopesha mnunuzi kunajuzu na hakuna chochote ndani yake. Na dalili yake: Jambo la haramu katika mkopo ni nyongeza inayoshurutishwa; kwani nyongeza hiyo ni riba. Ama kulipa deni la mkopo kwa kuongeza kitu ambacho hakikushurutishwa hakuna ubaya wowote. Na jambo hili limepokewa katika Hadithi kutokana na kitendo cha Mtume S.A.W., kutoka kwa Abu Huraira R.A., anasema: Mtu mmoja alikuwa anamdai Mtume S.A.W., ngamia wa mwaka mmoja, akaja mtu huyo kumdai Mtume amlipe, akasema: Nilipe na Mwenyezi Mungu atakulipa, Mtume S.A.W., akasema: Hakika Mbora wenu ni Mzuri wenu katika kulipa deni lake. Hadithi hii ni Mutafaqu alaihi.
Al-Imam Al-Nawawy anasema: "Katika Hadithi hizi kuna kujuzu makabidhiano ya wanyama, na hukumu yake ni hukumu ya mkopo, na ndani yake ni kwamba inapendeza kwa mwenye deni la mkopo na mengineyo arejeshe kilicho bora zaidi kuliko kile alichokichukua, na hii ni katika Sunna na Maadili mema, na wala hakuna kutaka masilahi katika mkopo kwani kufanya hivyo kumekatazwa; na kwamba kilichokatazwa ni yale makubaliano ya mkopo yenye sharti ndani yake , na madhehebu yetu ni kwamba inapendeza kuongeza katika malipo ya deni alilokuwa nalo mkopaji, na inajuzu kwa mkopeshaji kuchukua nyongeza iwe katika sifa ya kinachorejeshwa au idadi, kwa mfano kama alimkopesha kumi naye akamrejeshea kumi na moja. Na Madhehebu ya Imamu Malik ni kwamba nyongeza katika idadi inakatazwa, na hoja yao ni kwamba imo ndani ya ujumla wa kauli ya Mtume S.A.W., aliposema: Mbora wenu ni Mzuri wenu katika kulipa deni lake". [Maelezo ya Al-Nawawy katika Swahihu Muslim 11/37]
Na Ibn Qudamah amesema: "Na iwapo atalipa kilicho bora zaidi katika kiwango au sifa bila ya sharti lolote kuwekwa, basi inajuzu kufanya hivyo; kwa mujibu wa Hadithi ya Abu Raafiu. Na kama akiandikiwa kumkopea mtu mwingine, au akilipia ndani ya nchi nyingine, au akampa zawadi baada ya kulilipa deni lake, basi hakuna ubaya wowote katika hilo. Na Ibn Abu Musa anasema: Akizidishia mara moja basi haitajuzu kwake kuchukua nyongeza au ziada mara ya pili, kwa kauli moja. Na wala haichukizi kukopa mkopo kwa wema, kutokana na uzuri wa kulipa. Na Kadhi ametaja upande mmoja wa kuchukiza kwake; kwa kuwa mtu ana tama ya kulipwa zaidi ya deni lake. Na hukumu ya kwanza inasihi kwa sababu Mtume S.A.W., alikuwa akijulikana kwa ubora wa kulipa madeni yake, na mkopo wake haukuwahi kuwa Unachukiza, kwani Mbora wa watu ni yule Mzuri wao katika kulipa Madeni yake. Na katika kuchukiza mkopo wake kuna ufinyu wa kuwatendea wema watu, na wenye kujulikana kwa maadili na mienendo mizuri. [Al-Kafy katika Feqh Al-Imam Ahmad 2/72, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Al-Khateb Al-Sharbini amesema: "(Na Haujuzu) mkopo katika pesa taslimu na nyinginezo (kwa sharti) la kurejesha kilicho sahihi na kamili ya kile kilichovunjika, au krejesha nyongeza au kurejesha kilicho kizima au bora zaidi ya kile kilicho chini kwa ubora au kilichoharibika, na kwa njia hii mkataba wa mkopo wa kitu kilicho kizima unaharibika kwa kauli ya Hadithi: Kila mkopo unaovutia manufaa basi huo ni ni mkopo wa Riba, na hiyo Hadithi hata ikiwa Dhaifu, Imamu Baihaqiyu amepokea Maana yake kutoka kwa Maswahaba wengi, na maana iliyomo ndani yake ni kwamba lengo la mkataba wa mkopo ni kufariji mkopaji, na iwapo atajishurutishia yeye mwenyewe kiukweli, basi atakuwa ametoka katika lengo lake na atakuwa amezuia kusihi kwa mkataba huko wa mkopo. Na kama atarejesha alichokikopa kikiwa na nyongeza ya kiasi chake au sifa zake bila ya sharti lolote basi ni bora, na inapendeza zaidi kufanya hivyo kutokana na Hadithi iliyotangulia: Hakika Mbora wenu ni Mbora wenu katika kulipa deni lake, na mkopeshaji halazimishwi kuchukua kilichoongezwa au kuchukua zawadi iliyotolewa na mkopaji bila sharti lolote. Anasema Maarudiy: Na kujiepusha na hilo ni bora zaidi kabla ya kurejesha mbadala wa kilichoazimwa. Na ama kuhusu Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhariy na wengine, kuhusu yanayoonesha uharamu, baadhi yake sharti lililo ndani yake ni muda, na baadhi yake ni kuzingatiwa hivyo kwa kushurutisha zawadi katika makubaliano ya mkopo, na katika kuchukiza ukopeshaji kwa yule aliyezoea kurejesha nyongeza kuna mitazamo miwili: na ullio bora kati ya hiyo miwili ni kuchukiza kwake. [Mughniy Al-Muhtaji, Sharhu ya Minhaju Al-Twaalebiin 2/119, Ch. Dar Al-Fikr]
Al-Kassaey anasema: "Na mtu anayerejea tena katika mkopo uleule, basi pasiwepo ndani yake manufaa yoyote, ikiwa ndani yake kuna manufaa yoyote basi haijuzu, kwa mfano anapomkopesha kiasi cha dirhamu za chakula, kwa sharti amrejeshee zikiwa sawa sawa, au alimkopesha na akamwekea sharti ndani yake kuna manufaa; na ni kwamba nyongeza iliyowekewa sharti inafanana na riba; kwani hiyo ni nyongeza isiyokuwa na mkabala wa malipo, na kujiepusha na uhalisia wa riba na mazingira yanayofanana na riba ni wajibu, na hii ikiwa nyongeza imeshurutishwa ktika mkopo, ama nyongeza ikiwa haijashurutishwa kwenye mkopo lakini mkopaji akamlipa kilicho kizuri zaidi ya hivyo viwili, basi hapana ubaya wowote; kwani riba ni jina la nyongeza iliyoshurutishwa katika makubaliano ya mkopo, na hapo haijapatikana, bali huu ni mlango wa ubora wa kulipa, na kwamba hili ni jambo lililosuniwa. Anasema Mtume S.A.W.: Mbora wa watu ni mbora wao katika kulipa deni. Na alisema Mtume S.A.W.: Wakati wa ulipaji wa deni kwa kutumia mizani: Pima na uzidishe kiasi kipimo". [Badaea Al-Sanaea katika utaratibu wa sheria 7\395, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kama ambavyo inafaa pia kusemwa: Hakika mambo yalivyo, Manufaa hapa ni kinyume cha upande wa kuazimwa na bila ya ushurutishaji juu yake, basi inajuzu kama vile udalali.
Na ufupisho wa yote ni kwamba: Hakika kila kilichopatikana katika maswali haya kinajuzu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas