Ndoa ya Mwanamke Aliyejitolea

Egypt's Dar Al-Ifta

Ndoa ya Mwanamke Aliyejitolea

Question

Hivi karibuni kupitia baadhi ya vituo vya runinga kuna mtu amejitokeza na kutangaza kile kinachoitwa “Ndoa ya Mwanamke aliyejitolea” na anasema: Ndoa hii inakamilika ikiwa mwanamke atasema kumwambia mwanamume: “Nimejimilikisha kwako mimi mwenyewe”, kisha mwanamume akamjibu: “Na mimi nimekubali, na nitakuandikia uhuru kwa kusoma Surat Al-Ikhlas kwa - mfano - itakuwa ni thamani ya uhuru wako”. Kisha akasema huyu mtu: Hakika mwanamke kwa maneno haya anakuwa ni mtumwa kwa huyu mwanamume, hivyo anaweza kuishi naye maisha ya ndoa, na kuwa na uwezo mwanamke wa kuimaliza ndoa hii au utumwa huu kwa kusoma Surat Al-Ikhlas kwa nia ya kutengana, basi atakuwa huru kwa mara nyingine,
Huyu mtu anajaribu kuyaunga mkono maneno yake kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana}[AN-NISAA, 03].
Pamoja na kauli ya Mola Mtukufu: {Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara}[An-Nisaa, 25].
Na kuwa Mtume S.A.W. alijiwa na mwanamke mmoja na kujitoa yeye mwenyewe mwanamke kutaka kuolewa na Mtume - na wala hakusema nimejioza kwako mimi mwenyewe - basi baadhi ya Masahaba walitaka kumwoa, akamwambia: “Nimekumilikisha kutokana na Qur`ani uliyonayo” anasema: Hakika hii ni dalili ya uhalali wa kuoa mwanamke aliyejitoa kama zawadi yeye mwenyewe kwa mwanamume, na anasema: Hakika makubaliano ya kimataifa ya kuondoa utumwa hayazingatiwi ni jambo la lazima kutekelezwa na Waislamu katika kuharamisha kilichohalalishwa na Mwenyezi Mungu, na anasema pia: Hakika hizi ni jitihada zake ambazo haipaswi kwa yeyote kuzizuia, hivyo tunatarajia uwazi na ukweli wa madai haya kwa upande wa kisharia.
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Sheria ya Kiislamu imekuja duniani hali ya kuwa mifumo ya utumwa ilikuwapo na inafanya kazi katika maeneo mbalimbali ya dunia, ambapo inawezekana kwa mwanadamu kumtumia mwanadamu mwenzake, akamnunua au kumuuza, kumrithi au kurithiwa naye.
Utumwa ulikuwa na vyanzo mbalimbali, miongoni mwa vyanzo hivyo ni:
Ufakiri: Ikiwa mwanadamu ni masikini, basi ana uwezo wa kuiuza nafsi yake ili kujikimu, au kumuuza mmoja wa watoto wake ili kupunguza matatizo ya familia na kupata thamani ya kumuuza kwake.
Deni: Ikiwa mwenye kudaiwa alishindwa kulipa deni, basi mwenye kudai alikuwa ana haki ya kumfanya mdeni wake kuwa mtumwa ikiwa ni katika kulipa deni lake.
Adhabu ya Uhalifu: Baadhi ya sheria za zamani makosa ya jinai hukumu yake ilikuwa kwa mkosefu mwenyewe kufanywa mtumwa kwa yule mwenye haki.
Utekaji: Kulikuwa na wahalifu barani na baharini wakiwafanyia chuki wenzao pamoja na kuwateka miongoni mwao wale wanaowaweza miongoni mwa watu dhaifu.
Vita: Ilikuwa mwenye kutekwa mateka wakati wa vita inawezekana kufanywa mtumwa badala ya kuuliwa.
Uislamu ukafunga vyanzo vyote vya utumwa tulivyovitaja isipokuwa chanzo kimoja, nacho ni chanzo cha utumwa wa mateka wa vita pindi zikikamilika sharti mbili: Ukafiri na Vita - kwa maelezo ya kina yanayopatikana kupitia vitabu vya Fiqhi - na hii ni aina katika aina za kulinda umwagaji damu hata kama mateka mwenyewe ni kafiri, kwa sababu kukosekana hali hii hakutokuwa utumwa na uhuru bali ni utumwa na kifo.
Pamoja na kuwa hali iliyotajwa si utumwa wa moja kwa moja, isipokuwa ni moja ya hiyari aliyonayo kiongozi wa nchi, na hilo ni kwa mujibu ya masilahi atakayoyaona, hiyari ya kwanza ni: Kuua au kutoa msamaha na kuwaacha huru bila ya gharama au malipo yoyote, hiyari ya pili: Kuwalipisha fidia ya mali au kuwabadilisha na mateka Waislamu, na hiyari ya tatu: Kumfanya mtumwa kama ilivyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi mnapowakuta waliokufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu angeliwashinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwakatika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao} [MUHAMMAD, 4]
Vile vile utumwa unathibiti pindi unapohama umiliki wa mtumwa kutoka kwa anayemmiliki kwa njia sahihi na kuhamia kwa mwingine kwa njia ya kuhamisha umiliki halali, kama vile kumuuza au kumtoa zawadi au kumtoa kwa njia ya wasia, vile vile pindi mtumwa wa kike anapojifungua mtoto na asiyekuwa bwana wake, basi mtoto aliyezaliwa anamfuata mama yake katika utumwa ni sawa sawa baba yake akiwa ni mtu huru au mtumwa pia.
Qur`ani Tukufu wakati mwingine inaelezea watumwa kwa maana ya miliki ya mkono wa kiume, amesema Imamu Al-Qurtwubiy katika tafsiri yake [5-20, chapa ya Dar Al-Kutub Al]-Misriya: “Mola Mtukufu Ameegemeza neno Miliki ya mkono wa kiume ikiwa yenyewe ni sifa, na mkono wa kiume imehusishwa kwa uwezekano wa kufanyiwa mazuri”.
Kwani Dini imeamrisha kufanyiwa wema watumwa, imepokelewa na Imamu Muslim toka kwa Abi Dhar Al-Ghafariy R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Wao ni ndugu zetu, Mwenyezi Mungu Amewafanya kuwa chini ya usimamizi wenu, basi walisheni kile mnachokula, wavesheni vile mnavyovaa, msiwafanyishe kazi zinazowashinda, ikiwa mtawafanyisha kazi basi wasaidieni”.
Uislamu umefungua mlango wa kuwakomboa watumwa, mpaka jambo hilo likawa ni katika jumla ya ibada ambayo mtu humfanya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, na kuwa sababu ya kufutiwa dhambi, kwani ni mojawapo ya aina nane zinazopaswa kupewa mali ya zaka ambazo zimetajwa kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibuulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima} [AT TAWBAH, 60].
Amesema Al-Baidhawiy katika tafsiri yake [1/121, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Na katika utumwa: Ufupisho wake ni kumsaidia mtumwa aliyeandikiwa kupata uhuru, au kumwachia huru mateka, au kumuuza mtumwa kwa lengo la kuachwa huru”. Imepokelewa na Imamu Muslim katika kitabu chake kutoka kwa Abi Huraira R.A. Hakika Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kumwacha huru mtumwa, basi Mwenyezi Mungu Ataviacha huru viungo vyake na adhabu ya Moto sawa na kila kiungo cha mtumwa”. Uislamu ukafanya kitendo cha kumwacha huru mtumwa ni kafara ya kumpiga mtumwa , imepokelewa na Ahmad kutoka kwa Ibn Omar R.A. hakika ya Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kumpiga mtoto, basi kafara yake ni kumwacha huru mtumwa” wakati mwingine kumwacha huru mtumwa ni jambo la lazima kwa haki ya mwenye kuweza katika kafara ya kuua kwa njia ya makosa na mwenye kufanya dhihar (Mwanamume kumwambia mkewe ni sawa na mgongo wa mama yake) pia kuharibu ibada ya Funga ya Ramadhani kwa kauli ya wanachuoni, na inapatikana hali ya kuacha huru mtumwa ikiwa mtumwa ataandikiwa na bwana wake kuachwa huru ikiwa atajilipia kiwango cha fedha walichokubaliana kati yao, ambapo bwana wake atamruhusu kufanya kazi ili kutafuta fedha za kujikomboa, na makubaliano waliyoandikiana yanakuwa ni makubaliano ya lazima ambapo bwana wa mtumwa hana uwezo wa kuvunja makubaliano hayo pasi na ridhaa ya aliyeandikiwa.
Pia unapatikana uhuru kwenye utumwa ikiwa bwana atazaa na mtumwa wake wa kike, basi anakuwa huru kwa kufariki kwake tu, ni kama kwamba Uislamu kwa haya umefungua mlango mmoja wa utumwa lakini ukaweka milango mingi ya kuacha huru kwa upande mwingine, ambapo tunaweza kusema kuwa ni kupunguza vyanzo vya utumwa.
Katika hukumu zinazofungamana na utumwa ni kuwa: Bwana huanzisha kati yake na watumwa wake uhusiano halali inakuwa ni halali kwake kwa mujibu wa uhusiano huo kushirikiana naye kwa ushirika wa ndoa, Mwenyezi Mungu Amesema: {Na ambao wanazilinda tupu zao * Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa} [AL MU'MINUUN, 5: 6].
Imamu Shafi R.A. alisema ndani ya kitabu cha: [Al-Umm, 5/47 Ch. Dar Al-Maarifah]: “Kitabu cha Mwenyezi Mungu kimeonesha kuwa kilichohalalishwa katika tupu, basi kimehalalishwa kwa moja ya sura mbili: ndoa, au mwanamke kujitoa mwenyewe”.
At-Twabariy alisema katika tafsiri yake [23/276 Ch. Hajar]: Maana yake ni: Kukubali kwao, wakiwa wenye kulinda kila Alichoharamisha Mwenyezi Mungu kwao, isipokuwa wao hawana lawama kuacha kulinda kwa wake zao au wale wanao wamiliki miongoni mwa wajakazi wao”.
Wakati huo mtumwa wa kike huitwa “Suriya” lakini hali hiyo ina masharti nayo ni: Kuwa mtumwa wa kike ni mwenye kumilikiwa na bwana wake kwa njia yoyote katika njia za umiliki halali, na umiliki huo uwe wake peke yake pasi na kuwa na ushirika, na wala asiwe mtumwa wa nusu kwa nusu kwa maana ya nusu mtumwa nusu yupo huru kwa kutotimia umiliki, na awe ni Muislamu au mtu wa Kitabu, kwani si halali kwa wasiokuwa hao wawili, kama vile mtu wa kuabudia masanamu, na wala asiwe miongoni mwa wanaozuiliwa muda wote au kwa muda fulani, asiwe mke wa mtu mwingine, na mwenye ujauzito haingiliwi mpaka ajifungue na mwenye kufikia umri ni mpaka pale anapopata hedhi.
Ikiwa masharti haya yatakamilika basi, mjakazi anakuwa ni halali kwa bwana wake akihusishwa na yeye tu na wala si halali kwa mwingine, na katika sharia hii kuna hekima nyingi, miongoni mwa hekima hizo: Ni kufungua mlango katika milango ya kumkomboa mtumwa, kwa sababu mtumwa mwanamke pindi anapojifungua kwa kuzalishwa na bwana wake anakuwa ni mama watoto huwa huru baada ya kufa kwa bwana wake, na mtoto aliyezaliwa naye anakuwa huru. hekima nyingine: Ni kukidhi mahitaji asili ya mwanamke kimwili ambayo ikiwa kama hatokidhi, basi ataingia kwenye ufisadi na uharibifu, na kumwezesha kuanzisha familia mpya baada ya kuwa wengi wao wamepoteza familia zao kwa sababu ya vita.
Basi suala la kumchukua mwanamke mtumwa “Suriya” ni halali iliyothibiti, uhalali wake haukuwa pekee kwenye Uislamu tu, bali hata katika sheria za Mitume waliopita. Imenukuliwa kutoka kwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Suleiman A.S. kuwa alifanya hilo, naye Nabii Ibrahim A.S. akafanya hilo hilo na Bi. Hajar na kuzaliwa Nabii Ismail A.S. vile vile Mtume wa Mungu S.A.W. akafanya hilo hilo na Bi. Maria R.A. Mama wa mwanawe Ibrahim ambaye alitolewa zawadi kwake Mtume na Al-Muqawqis mtawala wa Misri wakati huo.
Imamu Ibn Qudama Al-Maqdasiy alisema katika kitabu cha: [Al-Mughniy” 10/411 Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Hakuna tofauti katika uhalali wa “Suriya” na kumwingilia mwanamke mjakazi, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na ambao wanazilinda tupu zao} (5) {Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa }(6) na alikuwa Bi. Maria Al-Qibtwiya Mama wa mtoto wa Mtume S.A.W. ambaye ni Ibrahim. Mtume alisema: “Ameachwa huru na mtoto wake” na alikuwa Bi. Hajara Mama wa Mtume Ismaili A.S. ni mwanamke aliyepewa Nabii Ibrahim kipenzi cha Mwenyezi Mungu, na ilikuwa kwa Omar Ibn Khatwab R.A. Mama wa watoto wake, pia ilikuwa kwa Ali R.A. Mama wa watoto wake, pamoja na Masahaba wengine wengi”.
Ama hivi sasa makubaliano ya kimataifa yamefuata hukumu ya utumwa na biashara ya utumwa kuwa ni kosa la jinai, idadi ya makubaliano ya kimataifa ambayo yalipitishwa tokea mwaka 1832 mpaka hivi sasa ni kiasi cha makubaliano mia tatu. “Angalia: kitabu cha Dkt. Abdulsalam At-Tarmaniy cha utumwa wakati uliopita na hivi sasa, ni chapa ya Kuwait, mfululizo wa chapa za ulimwengu wa maarifa nambari 23”.
Mnamo mwezi August mwaka 1877 katika zama za utawala wa Khedewiy Ismaili serikali ya Misri ilisaini makubaliano huko Alexandria yanayopelekea uharamu wa biashara ya utumwa, na kuwekwa adhabu kali katika hilo.
Kukosekana kwa sababu ya utumwa kumeondoa utumwa duniani, na watu wote wamekuwa kwenye uhuru asili; Imamu Ibn Qudama Al-Maqdsiy alisema katika kitabu cha: [Al-Mughniy, 6/35]: “Asili ya wanadamu ni uhuru; kwani Mwenyezi Mungu Amemwumba Adamu na kizazi chake wakiwa huru, lakini utumwa ni wenye kuibuka, ikiwa hakufahamiki kuzuka huko, basi hukumu ni asili”.
Kabla ya kuzungumzia hukumu inayoitwa kuoa mwanamke wa miliki ya kulia kwa maana ya mwanamke aliyejitoa mwenyewe ni lazima kusisitiza juu ya maana mbili:
Maana ya Kwanza: Hakika ya kuoa ni jambo la wazi ni tofauti na umiliki wa mkono wa kulia, kwani kuoa ni makubaliano yenye maana ya uhalali wa kustarehe mwanamume kwa mwanamke ambaye haijazuiliwa kumwoa kwa kizuizi cha sheria [Kitabu Ad-Dur Al- Mukhtar cha Al-Haskafiy] - na kitabu cha [Ibn Abideen – 3/3, 4 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya]”.
Ama miliki ya mkono wa kulia, huitwa na kukusudiwa umiliki huo huo ambao anakuwa mwenye kumilikiwa ni mwanadamu, au hukusudiwa yanayofungamana na umiliki, nao ni utumwa wa kumilikiwa ni sawa sawa wakiwa wanaume au wanawake. Na katika hilo kuoa na umiliki wa mkono wa kulia vina pande mbili zinazo halalisha kuingilia, kila upande ni sehemu isiyo ingiliana na pande nyingine.
Na tofauti hii inafahamika kwa uwazi kutokana na dalili ya kisharia, kama vile kauli ya Mola katika kuelezea waja wake Waumini: {Na ambao wanazilinda tupu zao * Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa} [AL MU'MINUUN, 5, 6], na kutenganisha kati ya wake na wamilikiwa wa mkono wa kulia kwa kile kinachoonesha kuwa hao ni aina mbili tofauti, kwani umeunganishwa umiliki wa mkono wa kulia kwa wake, na asili ya kuunganisha kati ya kiunganisha na kiunganishwa, kwa sababu kitu hakijiunganishi chenyewe.
Na kama kauli yake Mola - akimwambia Mtume wake S.A.W. haramu kwake kuoa wanawake wengine wasiokuwa wake zake, na kuhalalisha kwa Mutume wanawake wengine wakiwa ni katika miliki ya mkono wa kulia: {Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine, wala kuwabadilisha kwa wake wengine ingawa uzuri wao ukikupendeza; isipokuwa yule uliyemmiliki kwa mkono wako wa kulia. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu} [AL AHZAAB, 52].
Amepokea Abu Dawud na Tirmidhiy kutoka kwa Muawiya Ibn Haida R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Hifadhi tupu yako isipokuwa kwa mkeo au mjakazi”.
Maana ya Pili: Sifa ya mke na sifa ya miliki ya mkono wa kulia ni sifa mbili tofauti hazikutani katika maudhui moja kwa upande wa mtu mmoja - nayo ni mmiliki au mume, kwani ikiwa mtu ameoa mjakazi wa mwingine kisha akamnunua basi katika hali hii ndoa huvunjika na kuwa ni miliki yake ya mkono wa kulia, kwani miliki ya kulia ina nguvu zaidi ya miliki ya ndoa, kwa sababu anamiliki mtu na manufaa yake, ama miliki ya ndoa.
Haimiliki isipokuwa upande wa manufaa, Ibn Qudama alisema katika kitabu cha: [Al-Mughniy, 7/113, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Haiwi kwa bwana kumwoa mjakazi wake, kwa sababu kummiliki mtu kunapelekea kumiliki na manufaa na uhalali wa kumwingilia, hivyo haiwezi kukutana kwake makubaliano yaliyo dhaifu zaidi, ikiwa amemwoa mke wake hali ya kuwa ni mjakazi, basi ndoa huvunjika, vilevile ikiwa mjakazi ana mume wake ndoa huvunjika, wala hatufahamu tofauti katika hili, wala haifai kumuoa mjakazi akiwa yeye ana umiliki kwake, wala kumwoa mjakazi aliyemwandikia kwa sababu bado ni mmilikiwa wake”.
Vile vile umiliki wa mkono wa kulia unathibiti kwa mtumwa mwanamume, ikiwa huyu mtumwa wa kiume mmiliki wake ni mwanamke, basi si halali huyu mwanamke kuolewa naye, Ibn Mundhir alisema: “Wanachuoni wamekubaliana kuwa ndoa ya mwanamke na mtumwa wake wa kiume ni batili” kitabu cha: [Al-Mughniy cha Ibn Qudama, 7/113 Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Ibn Al-Qayyim alisema katika kitabu cha: [I’lam Al-Muwaqqiin, 2/66 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya]. “Bwana ni mwenye nguvu kwa mmiliki wake, mwenye kumsimamia, mwenye kummiliki, na mume ni mwenye nguvu kwa mke wake, mwenye kumsimamia, na yeye mke huwa chini ya mamlaka ya mume wake na hukumu yake inafanana na hukumu ya mateka, na kwa sababu hii mtumwa mwanamume amezuiliwa kumuoa bwana wake wa kike, ili kuepuesha kuwa kwake mwenye kumilikiwa na huyu mwanamke na kuwa kwake huyu mwanamke bwana wa mtumwa wa kiume na muingiliwa wake”.
Ikiwa yatabainika haya, basi neno (Ndoa ya miliki ya mkono wa kulia) kwa upande wa haki ya mwanamume haifasiriki isipokuwa ni kwa moja ya sura mbili:
Sura ya Kwanza: Bwana kuwa na mjakazi miliki yake ya mkono wa kulia anamwacha huru na anamwoa, imepokelewa kutoka kwa Abdillah Ibn Qais R.A. kuwa hakika ya Mtume S.A.W. amezungumzia kuhusu mtu atakayepata malipo mara mbili: “Ni pamoja na mtu alikuwa na mjakazi akamlisha vizuri, kisha akamfunza maadili na kuwa na maadili mema, kisha akamwacha huru na kumuoa, basi ana malipo ya aina mbili”. Na kuita jina la ndoa ya miliki ya mkono wa kulia ni uitaji wa fumbo mazingatio ni kile kilichokuwa - kwa maana: Mtu kuoa yule aliyekuwa ni miliki ya mkono wake wa kulia.
Sura ya Pili: Kuolewa mjakazi - ambaye ndiye miliki ya mkono wa kulia - na mtu mwingine kwa ndoa iliyokamilika nguzo masharti na yaliyo wajibu hili halifai, isipokuwa ikiwa atahofia kuingia kwenye uzinifu pamoja na mambo yaliyo haramu, na akawa hawezi kuoa wanawake huru. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara. Na wanapoolewa kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyo wekewa waungwana} [AN NISAA, 25].
Al-Hafidh Ibn Kathiir alisema katika tafsiri yake [2/260, Ch. Dar Tiba]: “Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini”, kwa maana: “Waoeni wajakazi waumini ambao wanamilikiwa na waumini…. Na kauli yake: “Hayo ni kwa yule miongoni mwenu anayeogopa kuingia katika zina” kwa maana: Ni halali kuoa mjakazi kwa sharti zilizotangulia kwa yule mwenye kuhofia nafsi yake kuingia kwenye uzinzi, na akapata tabu kuvumilia kwa kutoingilia, na kufanya uzinifu kwa sababu ya yote hayo, basi kwa hali hiyo ataoa mjakazi, na ikiwa ataacha kuoa mjakazi na kupambana na nafsi yake katika kujizuia na uzinifu, basi hilo ni bora kwake, kwa sababu ikiwa atamuoa mjakazi na akapata naye watoto watakuwa ni watumwa kwa bwana na kwa sababu ya hii akasema: “Bwana halazimiki kumuoa kijakazi wake”.
Ama yaliyotajwa kwenye swali kuwa mwanamke anasema kumwambia mwanamume: “Nimejimilikisha kwako mimi mwenyewe” mwanamume akajibu: “Na mimi nimekubali, na nimekuandikia kwa mfano Surat Al-Ikhalas kuwa ndiyo thamani ya uhuru wake”, kwa maelezo haya basi anakuwa ni mtumwa kwake, anaweza kuishi naye wakati huo maisha ya ndoa, na kuwa na uwezo wa kuumaliza uhusiano huu kwa kusoma Surat Al-Ikhlas kwa nia ya kuachana na ujakazi, basi hapo anakuwa ni huru kwa mara nyingine, basi huo ni mchezo usiofungamana na chochote katika yaliyotajwa, kwa sababu mwanamke huyu ni huru, na uhuru ni haki ya mtu isiyokubali kutumiwa vibaya kwa njia ya fidia au kuuachia, haifai kwa mtu aliye huru kujiuza yeye mwenyewe au kumilikiwa na mtu mwingine ni sawa sawa kwa kulipia thamani au pasi na malipo, alisema Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Majmuo', 9/242, Ch. Al-Munira]: “Kumuuza mtu huru ni batili kwa makubaliano ya wanachuoni wote”, na alisema Ibn Qudama Al-Hanbaliy katika kitabu cha: [Al-Mughniy, 4/174, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Wala haifai kumuuza mtu huru, wala kuuza usichokimiliki, kama vilivyo halali kabla ya kuwa nacho mkononi na kuvimiliki, wala hakuna tofauti tunayoijua katika hilo, kwani Mtume S.A.W. amesema: “Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu aina tatu mimi ni wagomvi wangu Siku ya Kiyama: Mtu amenipa mimi kisha akaondoka. Mtu amemuuza mtu huru kisha akala thamani yake. Na mtu amempa mtu kazi akaitekeleza lakini yeye asimpe malipo yake” imepokelewa na Imamu Bukhariy.
Kama vile uhuru unafungamana na haki ya Mwenyezi Mungu; katika wajibu wa ibada ya Zaka, Swala ya Ijumaa, ibada ya Hija na utekelezaji wa adhabu ya jinai, hivyo basi haifai utumwa kwa mtu huru kwa ridhaa yake, ni kutokana na kuwepo ubatilifu wa haki ya Mwenyezi Mungu. [Angalia: Kitabu cha Ghamz Uyun Al-Basair, 2/288 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Ibn Najiim alisema katika kitabu cha: [Al-Bahr Ar-Raiq, 4/293 Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: “Katika uhuru kuna haki ya Mwenyezi Mungu, haiwezi kuondoka kwa kufutika utumwa”.
Wanachuoni wametaja kanuni ya kifiqih na wakasema: “Mtu huru hawezi kuingia kwenye utumwa”. [Angalia kitabu: Al-Ashbah wa An-Nadhahir cha Imamu As-Suyutiy, uk. 124, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya], na kitabu cha: [Al-Ashbah wa An-Nadhair cha Ibn Najeem, uk. 111, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya], amesema Shihab Ad-deen Al-Hamawiy katika kitabu cha: [Ghamz Uyun Al-Basair katika sharh Al-Al-Ashbah wa An-Nadhair 1/390]: “Jambo la haraka la mtu kuwa huru hawezi ingia kwenye kutawaliwa na kumilikiwa”.
Vile vile kanuni ya kisharia inasema kuwa: “Asili katika tupu ni haramu” neno tupu ni fumbo la kusudio la wanawake na ndoa, na uharamu huu ni jambo la wazi, wakati ambapo kinyume na hivyo ni jitihada yenye misingi ya dhana na dhana haipingi ukweli, hivyo basi jitihada kwenye jambo kama hili inakuwa si yenye kuzingatiwa kisharia, ikiwa kutaongezwa kwenye msingi huu, msingi mwingine wa tamko la wazi la sharia na kanuni zake pamoja na makusudio yake na kauli za Waislamu, ni wazi ubatilifu wa madai ya jitihada, amesema mwanachuoni Az-Zarkashy katika kitabu cha: [Kanuni za kifiqih 1/177 Ch. Wizara ya Waqfu ya Kuwait]: “Asili katika tupu ni haramu”.
Ama dalili iliyotajwa ya madai yao ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne. Na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana} [AN NISAA, 3], ni dalili batili na uzushi kwenye maana ya Qur`ani Tukufu kwa sababu maana ya Aya Tukufu: Ni kuwa halali kwa mwanamume kuoa kutokana na kile anachokipenda kwa mwanamke na kuwa chini yake wanawake wanne kwa kiwango cha juu, na uhalali huu unafungamana na sharti la uadilifu kati ya wake hao wanne, kinyume na hivyo mwenye kuhofia nafsi yake kutofanya uadilifu, basi abaki na mke mmoja au miliki ya mkono wake wa kulia miongoni mwa wajakazi, hii ndio maana ya wazi ya Aya Tukufu na wala hakuna kinachowezekana kuegemeshewa katika kauli ya uhalali wa mwanamke huru kujitoa mwenyewe zawadi kwa mwanamume na kuwa mtumwa kwake na kuitwa hiyo kuwa ni ndoa.
Sheikh Twahir Ibn Ashur alisema katika tafsiri yake ndani ya kitabu cha: [At-Tahrir wa At-tanwir, 4/224: 227, Ch. Dar Tunisia ya uchapaishaji na usambazaji] kauli yake: “Na mkuogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu,..” kwa maana: Ni mwanamke mmoja tu kwa kila mwenye kuhofia kutoweza kufanya uadilifu… Na kuhofia kutoweza kufanya uadilifu maana yake: Ni kutofanya uadilifu kati ya wake, kwa maana: Kutoweza fanya usawa, na hilo ni katika upande wa chakula mavazi furaha kuingilia kuacha kudhuru katika kila kinachoingia chini ya uwezo wake, kutoelemea moyo wake upande mmoja… na kauli yake: “au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki” ni kiunganishi cha kauli yake: “basi mmoja tu, ..” amepewa hiyari kati ya mke mmoja kwa kuzingatia ni wake wengi, kwa maana: Mke mmoja au wajakazi wengi, na hilo ni kuwa wanawake wamilikiwa hawana sharti la kuwa na uadilifu kama sharti lilivyo kwa wanaume, lakini ni sharti kwao hao wanawake kuonesha ushirikiano mzuri na kutofanya mambo yenye madhara, na kiunganishi cha kauli yake: “ basi oeni mnao wapenda…” ilikuwa ni hiyari kati ya ndoa na ujakazi kwa mujibu wa hali za watu, na uadilifu kwa mjakazi una sharti sawa na wake wa ndoa.
Ama kauli Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara} [AN NISAA, 25], inafungamana na ndoa ya wajakazi ikiwa wanamilikiwa na mtu mwingine, na inaonesha kuwa Aya inazungumzia ndoa ya mjakazi anayemilikiwa na mtu mwingine: Yaliyokuja kutimiza Aya Tukufu ni miongoni mwa amri ya kutaka ruhusa kwa wasimamizi wa mjakazi, wasimamizi wa mjakazi wanaokusudiwa: Ni wale wanaowamiliki, vilevile amri ya kuwatolea mahari kama ilivyoamrishwa kwenye ndoa za wanawake huru, na hilo ni kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara.} amesema Imamu An-Nasfiy katika tafasiri yake [1/349 Dar Al-kalim At-Twayyib]: “Basi waoeni kwa idhini ya watu wao” ni wale mabwana zao, nayo ni hoja kwetu… kuwa haiwi kwa mtumwa au mjakazi kuolewa isipokuwa kwa ruhusa ya msimamizi, “na wapeni mahari yao kama ada,”: na wapeni mahari yao pasi ya usumbufu wala madhara, na wamiliki ni wasimamizi wao, kwani utekelezaji wao kwao ni utekelezaji wa usimamizi, kwa sababu hao wajakazi na wanavyomiliki ni mali za mabwana zao”.
Ibn Ashuur alisema katika tafsiri yake [5/15]: “Wasimamizi wa wajakazi hapa: Ina maana ya mabwana wanaowamiliki, ambapo kwa matumizi mapana ni bwana wa mtumwa katika maneno ya Uislamu, ni misamiati ya Qur`ani, ikiwa ni ishara ya kufanya upole kwa mtumwa, kama vile katazo la mtumwa kumwita msimamizi wake: Bwana wangu, isipokuwa anatakiwa kumwita, kiongozi wangu, kama ilivyokuja kwenye maelezo ya Barira kuwa watu wake wa karibu ni baba isipokuwa ikiwa usimamizi wao upo mikononi mwa mabwana zao”.
Na wala hakuna kwenye Aya Tukufu ishara yeyote ya uhalali kwa mwanamke kuachia uhuru wake na kujimilikisha kwa mwanamume haiwezekani kufanya hivyo, na hili huitwa “Ndoa ya mkono wa kiume” au kwa jina lingine.
Hakuna kwenye Aya Tukufu ishara yoyote ya uhalali wa mwanamke kuushusha uhuru wake na kuimilikisha nafsi yake kwa mwanamume ni jambo lisilowezekana kuwa hivyo, na hili huitwa “Ndoa ya miliki ya mkono wa kulia” au kwa msemo mwingine.
Ama Hadithi Tukufu ambayo inadhaniwa inaelezea kuwa mwanamke alijitoa mwenyewe kwa Mtume S.A.W. kisha akamilikiwa na Sahaba mmoja masikini baada ya kutakiwa huyu mwanamke kuolewa ikiwa Mtume S.A.W. hana haja naye, Hadithi hii kuifanya ndio dalili ya kufaa mwanamke huru kuacha uhuru wake kwa ajili ya mwanamume wa kigeni na kuwa ni mmilikiwa wake wa mkono wa kiume - ni ufahamu potofu na kuzama zaidi kwenye dhana potofu, kwani tamko: “Nimejitoa mwenyewe kwako” lililopo kwenye Hadithi, halina maana ya mwanamke kuingia kwenye kumilikiwa na Mtume S.A.W. bali lina maana ya uhalali wa kuolewa na Mtume S.A.W. huyu mwanamke kwa ibara yeyote ile bila ya mahari, na hili linazingatiwa ni jambo maalumu kwake Mtume tu, kama Alivyosema Mola Mtukufu: {Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako ulio wapa mahari yao, na ulio wamiliki kwa mkono wako wa kulia katika alio kupa Mwenyezi Mungu, na mabinti ami zako,na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako walio hama pamoja nawe; na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwaNabii, kama mwenyewe Nabii akitaka kumwoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Sisi tunajua tuliyo wafaridhia wao katika wake zao na wanawake iliowamiliki mikono yao ya kulia. Ili isiwe dhiki kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [AL AHZAAB, 50].
Amesema mwanachuoni Abu Suud katika tafsiri yake [7/109, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwa Nabii” Kwa maana: Amemmilikisha tupu yake kwa ibara yoyote itakayoonesha bila ya utoaji mahari ikiwa mwanamume atakubali hilo, kama inavyoelezea Hadithi kukataa kwake Mtume, lakini sio ukataaji wa moja kwa moja, bali kama angetaka Mtume S.A.W. basi angemuoa, kama ilivyotamka kauli ya Mola Mtukufu: {kama mwenyewe Nabii akitaka kumwoa} kwa maana ya: Kumiliki na tupu yake pia, maana yake ni: Pasi ya mahari, hilo linafaa kwa Mtume S.A.W. ikiwa atakubali”.
Na amesema Al-Hafidh As-Suyutwiy katika kitabu cha: [Al-Khasais Al-Kubra” 2/429, 430, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Na katika mambo yanayomuhusu Mtume S.A.W. ni pamoja na kuweza kuoa kwa tamko tu la mwanamke kujitoa mwenyewe pasi na kutaka mahari, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwaNabii, kama mwenyewe Nabii akitaka kumwoa. Ni halali kwako wewe tu,} na Hadithi iliyopokelewa na Said Ibn Mansour na Al-Baihaqiy katika kitabu chake kutoka kwa Ibn Al-Musayyib amesema: “Si halali kwa mwanamke kujitoa zawadi kwa mwanamme yeyote baada ya Mtume S.A.W.”. Je inatosha neno kujitoa zawadi kwa upande wa mwanamme kama inavyotosha kwa mwanamke au lazima kuwe na sharti ya neno ndoa? Kuna mitazamo miwili, wa kwanza ni sahihi hali zote mbili: na mtazamo wa pili, ni kutokana na uwazi wa kauli yake: “akitaka kumwoa” amezingatia kwa upande wake kuwani ndoa”.
Na kauli yake Mola Mtukufu kwenye Aya: {kama mwenyewe Nabii akitaka kumwoa} ni dalili kuwa neno kujitoa zawadi halina maana ya umiliki wa mkono wa kulia, kwa sababu hakusema: “anammiliki” bali amesema “anamuoa” kwa maana: Anataka kumuoa, kuna tafauti kati ya matamshi mawili.
Na Hadithi iliyochukuliwa kuwa dalili imekuwa na matamshi mengi kwenye mapokezi yake na kuwa na tofauti nyingi zinazoonesha kuwa imepitishwa katika kunukuu matamshi yake juu ya mapokezi ya kimaana, Imamu Bukhari yeye peke yake amepokea kwenye kitabu chake karibu njia kumi kati yake kuna tofauti nyingi za matamshi, miongoni mwa matamshi ambayo yamekuwa na tofauti kwenye kauli ya Mtume S.A.W. kwenye Hadithi hii ni: “Nimekumilikisha kutokana na Qur`ani uliyonayo”, pia ikapokelewa kwa tamshi: “Nimekuozesha” pia kwa tamshi: “Nimemilikishwa” na tamshi: “Nimekumilikisha” pia tamshi: “Tumekuoza” pia tamshi: “Tumekuwezesha” na imepokelewa kwa tamko: “Nenda kwa hakika nimekuoza”, na kusudio la matamshi haya ni “kuoza” au “kuoa” au “kumiliki” au “kuwezesha” lakini pia imepokelewa pasi na tamshi: “Kuoza” au “kumiliki” au “kuoa” kama ilivyokuja kwenye mapokezi ya An-Nisaiy katika kitabu cha: [Al-Kubra na Kitabu cha Al-Muntaqiy cha Ibn Al-Jarudiy], ndani yake, amesema Mtume S.A.W: “Je unafahamu sehemu ya sura yeyote ya Qur`ani?” akasema: Ndio. Akasema - kwa maana ya Sahal Ibn Saad R.A.mpokezi wa Hadithi: “Basi akamuoza kwa sehemu aliyonayo ya sura ya Qur`ani”.
Pamoja na tofauti ya matamshi haya baadhi ya wazungumzaji wamefuata njia inayopewa nguvu zaidi, na wengine wakafuata njia ya wengi, wengi katika wahifadhi wa Hadithi wakapitisha mapokezi ya kuoa, miongoni mwao ni Imamu Al-Baihaqiy na Dar Al-Qatwuniy pamoja na Ibn Al-Juziy. Anasema Al-Baihaqiy katika kitabu cha: [Sunan As-Saghir 3/32 chapa ya Chuo Kikuu cha Kiislamu nchini Pakistan], baada ya kuthibiti tamshi la kuoa: Vile vile mapokezi ya watu wa Abi Hazim, kutoka kwa Sahal Ibn Saad, miongoni mwao pia Imamu Malik Ibn Anas, na wakasema baadhi yao: “Nenda kwa hakika nimekumilikisha”, na wahifadhi wengi ni bora kuliko muhifadhi mmoja”.
Na akasema pia katika kitabu cha: [Maarifat As-Sunan wa Al-Athar” 10/74, Ch. Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Pakistan]: Imepokelewa ndani yake: “Nimemilikishwa” ikapokelewa “Nimemmiliki” pia ikapokelewa: “Nimekumilikisha kutokana na sehemu ulinayo ya Qur`ani, na nimekuoza”.
Na akasema Ibn Al-Juziy katika kitabu cha: [At-Tahqiq fi Masail Al-Khilaf” 2/271, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Hadithi hii imepokelewa na Malik na Al-Thauriy pamoja na Ibn Ayina na Hamad Ibn Zaidi na Zaidat na Wahiib pamoja na Darawardiy pia Fadhil Ibn Sulaiman, wote wamesema: “Nimekuozesha” na imepokelewa na Ghassan amesema: “Tumekuoza” na limepokelewa neno: “Nimekumilikisha” kwa watu watatu: Mughammar, alikuwa ni mwingi wa makosa, na Abdulaziz Ibn Aby Hazim na Yakoub Al-Iskandarany, hawa wawili si wahifadhi wa Hadithi, wamechukuwa kwa mapokezi ya wanachuoni wahifadhi.
Na anasema Ibn Mulqin Shafi katika kitabu “Kufahamu faida za muhimili wa hukumu” 8/289, chapa ya Dar Al-Aswima: “Kumekuwa na tofauti ya mapokezi katika tamko: “Nimekuozesha” neno lililopokelewa na wengi miongoni mwa hao ni Imamu Bukhariy na Muslim: “Nimekuozesha” amesema Kadhi Ayyadh: Amesema Dar Al-Qatwniy: Nayo ni kauli sahihi na ndio iliyopokelewa kwa wingi na kuhifadhiwa, imepokelewa na mpokeaji: “Nimemilikishwa” ni mapokezi yasiyo na nguvu.
Na mtazamo wa kundi lengine la wahifadhi wa Hadithi ni kuwa matamshi haya yaliyopita yanawezekana kukusanywa, anasema Al-Baghwiy katika kitabu cha: [Sharh As-Sunna, 9/122, Ch. Al-Maktab Al-Islamiy]: “Wanapinga wale waliopitisha kufungika ndoa kwa tamshi la umiliki kwa mapokezi ya aliyepokea: “Hakika nimekumilikisha” nayo ni kauli ya watu wenye rai hiyo, lakini haijapitishwa na kundi la wanachuoni pasi na tamko la: “Kuoza au kuoa” nayo ni kauli ya Imamu Shafi, hakuna hoja ndani yake kwa mwenye kupitisha tamko la umiliki, kwa sababu kifungo cha ndoa ni kimoja, haiwi isipokuwa ni tamshi moja, kumekuwa na tofauti ya mapokezi, yaliyo wazi ni kwa tamshi la kuoa kwa kukubaliana na kauli ya muoaji, “Niozeshe” ambapo mara nyingi ni katika makubaliano pamoja na kutofautiana tamshi la wafunga ndoa, na aliyenukuu tofauti na tamshi la kuoa haikuwa kusudio lake kuchunga tamshi la kufunga ndoa, lakini kusudio lake ni kuweka wazi kuwa kufunga ndoa kunaendana na mafundisho ya Qur`ani, kwa dalili baadhi yao wamepokea kwa tamshi la “Kuwezekana” na wakakubaliana kuwa kufunga ndoa kwa tamshi hili haikubaliki”.
Amesema mwanachuoni Al-Khatweeb Al-Sherbiny katika kitabu cha: [Al-Mughniy 4/229, 230 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Wala haifai” kufunga ndoa “Isipokuwa kwa tamshi” linalotokana na tamshi la “Kukuozesha au kukuoza” pasi na kutumika tamshi la kujitoa mwenyewe, kumiliki, na yanayofanana na hayo, lakini kama neno kuhalalisha, na uhalali, kwa Hadithi ya Imamu Muslim: “Muogopeni Mwenyezi Mungu katika wanawake kwa sababu mumewachukuwa kwa uaminifu wa Mwenyezi Mungu na kuhalalishiwa tupu zao kwa tamko la Mwenyezi Mungu”. Wakasema: Tamko la Mwenyezi Mungu ni kukuozesha au kukuoza, haijatajwa ndani ya Qur`ani isipokuwa ni maneno hayo mawili, ni lazima kuyatumia maneno hayo kama ibada kwa sababu ndoa ni katika ibada kwa kupokelewa kwake kuwa ni Sunna muhimu, na utajo wa kwenye ibada unakuja kutokana na sharia, na sharia huwa inapokelewa kwa tamko: Kukuozesha au kukuoza, na yaliyo kwenye Hadithi iliyopokelewa na Bukhariy kuwa Mtume S.A.W. alimuozesha mwanamke mmoja na akasema: “Nimekumilikisha kutoka na Qur`ani uliyonayo” Imesemwa na wapokezi kuwa, mpokeaji amepokea kwa upande wa maana, akidhania kuwa ni visawe, na kwa kuangalia usahihi wake unapingana na mapokezi ya wanachuoni: “Nimekuozesha” amesema Al-Bayhaqiy: Wanachuoni wanaona ni bora kutumia neno moja, na inachukuliwa kuwa Mtume S.A.W. alitumia matamshi mawili, ni katika maelezo yaliyopingwa na watu wanao ona kauli ya Mwenyezi Mungu: {Ni halali kwako wewe tu,} ndoa imefanywa kwa tamshi la kujitoa zawadi ni katika mambo binafsi kwa Mtume tu S.A.W.”.
Ama madai ya muulizaji kuwa makubalino ya kimataifa ya kuondoa utumwa hayazingatiwi ni jambo la lazima kwa Waislamu bali ni katika kuharamisha kile Alichokihalalisha Mwenyezi Mungu. Basi jibu lake ni kuwa: Makubaliano haya hayaharamishi yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa yanaweka vigezo, kwani kunatofauti kati ya kuharamisha halali na kuweka vigezo vya halali ambavyo vinakwenda sawa na masilahi, bali vinakwenda sawa na makusudio ya sharia na malengo yake katika kufikia uhuru wa mwanadamu, kwa sababu lau vigezo hivyo vingesimamisha utumwa uliokuwepo wakati wa kuanzishwa kwa sheria hizo basi vingejumuisha na uhuru wake, lau vigezo hivi vingesimamisha utumwa ungeweza kutokea hapo baadaye kwa njia ya vita au zenginezo, katika haki za vita kiongozi Mwislamu kwa mujibu wa makubaliano haya atachagua moja ya hiyari zilizowekwa na sharia dhidi ya haki ya mateka wa vita, wakiwa hawa mateka ni wanaume basi kuna hiyari nne kama ilivyoelezwa kwa urefu hapo nyuma, wakiwa mateka ni wanawake - si wapiganaji - basi kiongozi anahiyarishwa kati ya kuwafanya watumwa au kudai fidia - kama ilivyoelezewa na baadhi ya wasomi - hakuna mtumwa wala utumwa tofauti na sababu za kivita.
Kiongozi kwenye makubaliano haya ya kimataifa atatekeleza kutokana na masilahi, hakuna shaka kuwa ulazima wa makubaliano haya ni katika masilahi ya Waislamu, kwa sababu kutowajibika nayo kunapelekea adhabu ya kimataifa yenye madhara kwa Waislamu.
Kwa vile makubaliano haya ni mikataba iliyosainiwa hivyo ni lazima kutekelezwa yale yaliyokubalika, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi mlioamini! Timizeni ahadi. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo, ila wale mnaotajiwa. Lakini msihalalishe kuwinda nanyi mmo katika Hija. Hakika Mwenyezi Mungu anahukumu Apendavyo} [AL MAIDAH, 1].
Amesema Al-Aluosiy katika kitabu cha: “Rouh Al-Maaniy” 6/48, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Utekelezaji: Ni kuhifadhi yale yanayopelekea makubaliano na kusimama kwa mujibu wake”. Imepokelewa na Tirmidhiy kutoka kwa Amru Ibn Auf Al-Mazniy R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Waislamu wana sharti zao, isipokuwa sharti la kuharamisha halali, au kuhalalisha haramu”.
Kama vile kushirikiana Waislamu na watu wa mataifa mengine katika kuchunga masilahi ya watu wote, hasa masilahi ambayo yanasimamia malengo ya maadili mema, na misingi ya utu na ubinadamu, ni katika mambo ya sharia ya Kiislamu na wala sio sheria za kigeni, na yote yaliyo kwenye sura kama hiyo ni katika mlango wa mashirikiano, na kutekeleza mashirikiano ni katika mambo mema kisharia, imepokelewa na Baihaqiy katika kitabu cha: [As-Sunan Al-Kubra] kutoka kwa Talhat Ibn Abdillah Ibn Auf R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Nimeona kwenye nyumba ya Abdillah Ibn Jadaan makubaliano niliyoyapenda, na lau ningetakiwa makubaliano hayo yawe ndani ya Uislamu basi ningetekeleza”. Kisha akasema Baihaqiy baada ya maelezo hayo [6/596 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya: Amesema Al-Qateebiy katika yale yaliyonifikia kutoka kwake kuwa: “Sababu ya makubaliano hayo ilikuwa ni Makuraishi walikuwa wanadhulumiwa katika eneo la Msikiti wa Makka, akasimama Abdillah Ibn Jadaan na Zubeir Ibn Abdilmuttalib kuwaita Makuraishi kwenye makubaliano ya utetezi, ili mwenye kudhulumiwa apate haki yake toka kwa mwenye kudhulumu, wakaitikia watu wa Bany Hashim na baadhi ya makabila ya Kikuraishi… wakakubaliana ndani ya nyumba ya Abdillah Ibn Jadaan, na kuitwa makubaliano hayo ni makubaliano ya Fudhuul, yakifananishwa na makubaliano yaliyofanyika Makka ndani ya zama za Jurhum, mtu dhaifu kupata haki yake kwa mtu mwenye nguvu, mgeni kupata haki yake kwa mwenyeji, walisimama watu wa Jurhum wanaitwa: Fadhlu Ibn Al-Haarith, pia Fadhlu Ibn Wadaa na Fadhlu Ibn Fadhaala, na kuitwa makubaliano ya Al-Fudhuul kutokana na majina ya hawa watu”.
Ama madai ya kauli ya uhalali wa kile kinachoitwa “Ndoa ya kujitoa zawadi” ni jitihada yenye kukubalika hata kama haijazungumziwa na wanachuoni wowote wa Kiislamu kabla ya hapo, lakini jibu ni kuwa: Jitihada ni yenye kukubalika pindi ikiwa ni kwa watu wahusika, kinyume na watu hao jitihada inakuwa haifai, wala sio kila mwenye kukisoma kitabu kimoja au viwili anafaa kuwa mufti kwa watu na kutoa Fatwa za hukumu mbalimbali za sharia kisha akaitwa ni mtu mwenye sifa ya kufanya jitihada na kuwa na mtazamo, kupata nafasi hii ya juu ina lazimisha mtu awe na jumla ya zana na vitendea kazi, ikiwa mtu atafanya kazi za kufutu masuala ya kisharia na kuzungumzia maneno ya Mwenyezi Mungu kinyume na kuwa na sifa ya kazi hiyo basi anakuwa ni mwenye kuzungumza ya Mwenyezi Mungu pasi ya elimu nayo, ni mwenye kumsemea uongo Mola Mtukufu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanaomzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa} [AN NAHL, 116].
Amesema Imamu Shafiy R.A.: “Si halali kwa yoyote kufutu katika Dini ya Mwenyezi Mungu isipokuwa ni kwa mtu mwenye kufahamu kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa Aya zake zilizofutwa na zile zilizofuta, hukumu zake na yanayofanana na hukumu, ufafanuzi wake na kuteremshwa kwake, kufahamu Aya za Makka na Madina, na kile kilichokusudiwa kwenye Aya hizo, na anatakiwa baada ya hapo kuwa ni mtu mwenye uelewa na ufahamu wa hadithi za Mtume S.A.W. na zile hadithi zilizofutwa na zenye kufuta, na afahamu Hadithi kama vile anavyofahamu Qur`ani, na awe ni mwenye uelewa wa lugha ya Kiarabu, mwenye uelewa mashairi ya Kiarabu, na yale yanayohitajika kwenye Sunna na Qur`ani, na atumie haya yote kwa uadilifu, baada ya haya yote atakuwa ni mwenye uwezo wa kusimamia miji mbalimbali, na anaweza kuzungumza na kutoa Fatwa katika halali na haramu, na kama hana sifa hizi basi hapaswi kutoa Fatwa ya masuala ya kisharia”. Kitabu cha “Al-Faqih wa Al-Mutafaqih cha Khatib Al-Baghdad 2/331, 332, chapa ya Dar Ibn Al-Juziy”.
Na uhakika wa mtu kuwa na vitendea kazi hivi hauwi isipokuwa ni kwa ushuhuda wa wanachuoni wanaomtambua yeye, na wala siyo kwa dhana tu ya mtu mwenyewe ya ukamilifu na kuwa muhusika, amesema Imamu Ibn Arafa Al-Maliky: “Ama sharti la kutoa Fatwa: Ni haipaswi kwa mwanafunzi kutoa Fatwa mpaka watu wamuone ni mwenye sifa ya kutoa Fatwa”, na akasema Sahnun: “Watu hapa wanaokusudiwa ni wanachuoni” na akasimulia Imamu Malik kauli ya Hurmuz: “Ni katika haki kwa mtu kuto toa Fatwa mpaka ajione yeye mwenyewe kuwa ni mwenye sifa ya hilo, na watu wakamuona ana sifa”. Kitabu cha: [Mawaahibu Al-Jaleel cha Hattab 6/96, chapa ya Dar al-Fikri].
Amesema Imam Malik yeye mwenyewe: Sijafutu masuala ya kisharia mpaka nimethibitishwa na watu sabini kuwa mimi ninafaa” Kitabu cha: [Hilyat Al-Auliyaa cha Al-Aswfahaniy, 6/316, chapa ya Dar Al-Fikr].
Pia akasema: “Sijajibu fatwa mpaka nimemuuliza mwenye kufahamu zaidi kuliko mimi: je unaonaje fatwa yangu? Nimemuuliza Rabia, na nikamuuliza Yahya Ibn Said, wakanijibu, akaulizwa: Ewe Abdillah, kama utazuiwa kutoa Fatwa? Akasema: Ningeacha, kwani haifai kwa mtu kujiona yeye mwenyewe kuwa anafaa mpaka aonekane na yule mwenye elimu zaidi yake” kitabu cha Al-Faqih wa Al-Mufaqih, 2/326.
Ama kauli iliyosema: Hiyo ni rai yake haipaswi kuzuiliwa, huo ni mtazamo batili zaidi ya batili, na uzushi zaidi ya uzushi, bali ni lazima kwa kiongozi wa Waislamu kumzuia katika yale ya uzushi juu ya sharia Takatifu, na kumchukua kwa mkono wake mpaka aweze kuwaidhika, na awe ni mazingatio kwa watu wa mfano wake waharibifu wenye kufanya uadui dhidi ya Dini ya Mwenyezi Mungu, waharibifu wa maadili ya Dini yao.
Amesema Al-Khatweeb Al-Bughdadiy katika kitabu cha: [Al-Faqih wa Al-Mufaqih” 2/324, 425]: “Anapaswa Imamu au kiongozi wa Waislamu kupembua hali za watoa Fatwa, yule atakayemuona anafaa kutoa fatwa, basi atampitisha kwa kazi hiyo, na atakayemuona kuwa hana sifa basi atamzuia na kazi hiyo, na kuambiwa kutoifanya kazi hiyo pamoja na kumuahidi adhabu kali ikiwa hatoacha… Na kwenda mbali zaidi kufahamu hali za mwenye kutaka kuiba kazi za utoaji Fatwa: Kuwauliza wasomi na wale watu maarufu katika wanachuoni wa zama zake, na kuyajengea maelezo yale wanayomwambia”.
Wamezungumza wanachuoni kile kinachoitwa kwa jina la “Mufti Mjinga” na wakataja kuwa inapaswa kiongozi wa Waislamu kwa mkono wake kumzuia, kwani Mufti Mjinga: Ni yule anayefahamu hila batili, au mjinga ambaye anafutu masuala kwa ujinga. Angalia kitabu cha: [Durar Al-Hukam cha Ali Haidar, 2/674, Ch. Dar Al-Jil].
Amesema mwanachuoni Al-Kasaniy katika kitabu cha: [Badaii As-Sanaai” 7/170, Ch. Dar Al-Kutub El-Elmiyah]: “Imepokelewa toka kwa Abi Hanifa R.A. kwamba alikuwa hata kawaida ya kuzuia jambo isipokkuwa kwa watu wa aina tatu: Mufti Mjinga, daktari mjinga, na mkodishaji wanyama aliyefilisika….kwa hakika amekusudia uzuiaji wa kihisia, kwa maana: anawazuia na kazi zao watu hawa wa aina tatu uzuiaji wa kihisia, kwa sababu kuzuia kwa hilo ni katika kazi za kuamrisha mema na kukataza maovu, kwa sababu Mufti mjinga anaharibu Dini ya Waislamu, na daktari mjinga pia anaharibu Dini ya Waislamu, na mkodishaji wanyama aliyefilisika muharibifu wa mali za watu, na kuwa kuwazuia kwao katika hilo ni kwa upande wa kuamrisha mema na kukataza maovu”.
Dini yetu imetuhabarisha kuhusu Mamufti hawa wafitinifu wanaoiba maneno katika hukumu za sharia na Dini pasi ya uelewa na kuwa watu wenye sifa, na imetutahadharisha nao pamoja na uzushi wao, imepokelewa na Bukhari kutoka kwa Abdillah Ibn Amr R.A. hakika ya Mtume S.A.W. amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu hachukui elimu kwa mkupuo moja toka kwa waja, lakini huchukua elimu kwa kuwachukua wanachuoni, mpaka anakosekana mwanachuoni na watu wakawachukuwa watu wajinga kuwafanya viongozi, wakaulizwa na kutoa Fatwa pasi ya elimu, wakapotea na kupoteza watu”.
Imepokelewa na Ibn Maja kutoka kwa Abi Huraira R.A. hakika ya Mtume S.A.W. amesema: “Itakuja kwa watu miaka ya udanganyifu, mtu muongo anaaminika, na mkweli anapingwa, msaliti anaaminika, na muaminifu haaminiki, na anazungumza mtu Ruwaidha”, akaulizwa ni nani huyu Ruwaidha? Akasema: “Ni mtu mjinga anayezungumza mambo ya umma”.
Akasema mwanachuoni As-Sindy katika kitabu chake cha: [As-Sunan, 2/494, chapa ya Dar Al-Jil]: “Na kauli yake: katika mambo ya umma, inafungamana na yale anayoyazungumza, mtu Tafih… maana yake ni mtu mjinga”.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: kila kinachoitwa “Ndoa ya kujitoa zawadi” kwa muundo wa swali lilivyokuja ni ndoa batili kwa sura yake na madhumuni yake, na kauli ya uhalali wake haitegemei msingi wowote wa sharia ya Kiislamu, na kunasibishwa na sharia takatifu ni uzushi na upotevu pamoja na upotoshaji lakini pia ni uharifu kwenye heshima za watu kwa huo ujinga, ni uadui wa wazi katika Dini na ubinadamu, kilicho wajibu kwa kila Mwislamu kabla ya kufanya jambo kupembua kwanza hukumu za kisharia kwa kutafuta Fatwa kutoka kwa wanachuoni wenye weledi wanaokubalika, na kiongozi anapaswa kuzuia illi kuepusha kuenea uchafu huo na uharibifu na kuwachukulia hatua wale wenye kudai hayo kwa uharifu wanaoufanya.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas