Hukumu ya Kuchukua Kodi katika Biashara Zilizoharamishwa
Question
Ni ipi hukumu ya kuzitoza kodi biashara zilizoharamishwa kama vile pombe na mfano wake, na kunufaika na kodi hizo katika Matumizi ya Nchi?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, na rehma na amani ziwe juu ya Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na Maswahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu;
Kodi: ni kiasi maalumu cha fedha kinachotozwa na serikali katika katika mali za wananchi bila ya kupewa mkabala wa manufaa maalumu. Kodi hutozwa kwa vinavyomilikiwa, kazi, na pato, kwa kupewa huduma na majukumu yanayotekelezwa na serikali kwa ajili ya watu wote. Na kodi inatofautiana kwa kutofautiana sheria na mazingira mbali mbali.
Kodi – kama wasemavyo watu wa uchumi - : Ni tozo la fedha la lazima linalotozwa na serikali kwa mujibu wa uwezo wa anaetozwa; na ni mchango wa wenye mali katika mzigo wa taifa wa matumizi, bila kujali Manufaa Maalumu ya umma yanayorejea kwa mtoaji, na kutokana na pato la kodi, serikali hunufaika kwa kukidhi matumizi ya umma, na kuyafikia malengo yake, yawe ya kisiasa, kifedha au kiuchumi. (Tazama katika: Kitabu cha Uchumi wa Kiislamu cha Dkt Muhammad Abdul Muniim Jamal, 2/673. Ch. Dar Al kitaab Al Masriy bilqaahirah, pamoja na Darul kitaabil Libnaaniy Bibairuut.)
Na inajuzu kwa Kiongozi kuamua kutoza kodi kiadilifu katika makadirio yake na uwezekano wake kwa wenye kuweza, ili kukidhi hitajio la matumizi ya umma na mahitaji ya lazima ya serikali, na inaeleweka ya kwamba Bajeti za serikali za Kiislamu kwa sasa hazijengeki kwa Zaka peke yake, bali kuna vyanzo mbali mbali ikiwemo kodi na ushuru wa aina mbali mbali na nyinginezo. Na kuna kinachoitwa Bajeti Kuu za Mataifa, nazo ni Mapato ya umma na matumizi yake. Matumizi ya umma yanapokuwa makubwa kuliko mapato yake basi hutokea nakisi ya Bajeti ya nchi. Na hulazimika kuziba pengo hilo kwa njia mbadala, ikiwemo kuweka kodi, isipokuwa ni lazima pachungwe katika uwekaji wa kodi hizo kutoongeza mzigo mzito kwa wenye kipato cha chini na kuwaongezea umasikini wao, na kodi zikusanywe kutoka katika mali ya matabaka ya wale ambao hawashindwi kuilipa kama vile tabaka la wawekezaji na wafanyabiashara ambao wanalazimika kutekeleza wajibu wao kwa taifa.
Kisheria imepitishwa ya kwamba mali ya mwislamu ina haki ukiachana na ile ya kutoa zaka; na hayo yamesemwa na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake:
Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa anashika Swala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapoahidi, na wanaovumilia katika shida na madhara na wakati wa vita; hao ndio waliosadikisha, na hao ndio wajilindao. [AL BAQARAH: 177]
Na upande wa dalili katika Aya hii – kama asemavyo Imamu Fakhru Raaziy katika Tafsiri yake ya [Mafaatiihul Ghaib, 5/216, Ch. Dar Ihyaai At Turath Al-Arabiy – Beirut]: Kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameambatanisha Utoaji wa Zaka katika kauli yake {na akawa anashika Swala na anatoa Zaka} na katika Kutoa Sadaka katika kauli yake: {na anawapa mali kwa kupenda kwake…}, na kinachounganishwa na kinachounga vinaweza kutofautiana, na kwa hivyo maana isiyokuwa na Zaka ikaothibitika katika aya, kisha haiepuki kuwa ima katika mambo ya kujitolea au katika mambo ya wajibu, na inawezekana ikawa ni katika mambo ya kujitolea. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {hao ndio waliosadikisha na hao ndio wajilindao}. Kwa hivyo uchamungu umesimamia juu ya hivyo, na kama ingelikuwa ni Sunna basi Uchamungu usingesimamia juu yake, na kwa hivyo ikathibiti ya kwamba Utoaji huu kama utakuwa sio wa Zaka utakuwa ni katika Mambo ya Wajibu. (Mwisho)
Naye Imamu Qurtubiy amesema katika Tafsiri yake ya [Aljaamiu li-Ahkaamil Qur'ani, 2/242, Ch. Dar Al-Kutub Al-Maswriyah- Al Qaahirah] Utajo wa Zaka na Swala katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {akawa anashika Swala na anatoa Zaka} kuna dalili ndani yake ya kwamba kinachokusudiwa kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na akatoa Mali kwa kupenda kwake} sio Zaka iliyofaradhishwa; kwani hiyo itakuwa ni kukariri, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mjuzi zaidi… kisha akasema: Wanachuoni wamekubaliana ya kwamba panapowashukia Waislamu hitajio baada ya kutoa Zaka basi ni wajibu kutumia fedha kwa ajili ya hitajio hilo. Amesema Malik Mola amehemu: Watu wanalazimika kuwakomboa mateka wao hata kama kufanya hivyo kutawagharimu Mali zao. Na huu ni mtazamo wa Wote pia.
Na Misingi Mikuu ya Fiqhi Inayotumika inaunga mkono mtazamo huu na kuupa nguvu. Na katika yanayohusiana na jambo hili: ni kama ilivyokuja katika kitabu cha [Al-ashbaahu Wa-nadhwaair cha Ibnu Najiimu, wa Madhehebu ya Hanafi, ukurasa wa 74 na 75, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah – Beirut: Madhara ya mtu mmoja yanavumiliwa kwa ajili ya kuondosha Madhara ya wengi, na kwamba Madhara makubwa huondoshwa kwa Madhara madogo. (Mwisho)
Na hii haieleweki kuwa ni uhalalishaji wa Kodi tu, bali hupelekea kuhalalika na kutozwa, kwa ajili ya kuyafikia masilahi ya Umma na nchi, na ni kwa lengo la kuzuia ufisadi na madhara pamoja na hatari zinazotokana na kutowekwa kodi. Kundi la wanazuoni wa Fiqhi ya Madhehebu yanayofuatwa, limezipitisha kodi lakini hazikuzipa jina hili. Tunakuta kwamba baadhi ya wafuasi wa Madhehebu ya Hanafi wanaziita kodi kwa jina la tozo kwa maana ya zile zitozwazo na Kiongozi wa nchi kwa njia ya haki au ya makosa. Na zifuatayo ni baadhi ya kauli zao: Imekuja katika Hashiya bin Abidiin [Radul-Muhtaar, 4/282] katika ufafanuzi wa maana ya kodi zilizokusudiwa hapo, na kwamba miongoni mwake ni: Ni kile kinachotozwa kwa ajili ya ujira wa Mlinzi, au kwa ajili ya kusafisha au kuzibua Mto unaotumiwa na watu wote, na mali inayowekwa kwa ajili kuandaa Jeshi la nchi, na kuwakomboa Mateka kama Hazina haitakuwa na fedha za kutosha kwa majukumu hayo, na aina nyingine nyingi ambazo hutozwa kwa ajili ya haki ya Umma. Kwa hivyo Ulezi kwayo unajuzu kwa makubaliano ya Wanachuoni; kwani kufanya hivyo ni wajibu kwa kila muislamu mwenye uwezo kukubali kwa kumtii Kiongozi wa nchi kwa yale yenye masilahi kwa Waislamu, na akawa hakuibebesha Hazina jukumu hilo au aliipa jukumu Hazina lakini ikawa haina fedha zozote. Na iwapo itakusudiwa kutolewa kodi hiyo kinyume na haki kama tozo mbali mbali zitolewazo na watu katika zama zetu hizi katika nchi ya Fursi kwa Fundi cherehani, Mpakarangi na wengine kwa ajili ya Sultani, na hutolewa kila siku au kwa mwezi, hii ni dhuluma.
Na imenukuliwa pia kutoka kwa Jaafaril Baaji, anasema: kinachotozwa na Sultani kwa wananchi kwa ajili ya masilahi yao kinakuwa deni la kulipwa kwa lazima na ni haki ya nchi, kama vile tozo za ushuru. Na wanasema Mashekhe zetu: na kila kinachotozwa na Imamu juu yao kwa ajili ya masilahi yao jibu lake ni liko hivyo, hata ujira wa walinzi wa barabara, walinzi wa usalama, kwa maana: kwa kila kinachohitaji matumizi ya fedha kwa ajili ya kuhifadhi barabara, usalama na ulinzi wake, na kuweka vituo, na kuweka milango ya njia kuu, na hili linajulikana na wala halitambulishwi kwa ajili ya kuchelea fitna. Kisha akasema: na kwa ajili hii kinachochukuliwa katika mali ya umma kwa ajili ya kukarabati chochote katika maslahi ya umma ni deni na ni lazima kilipwe na haijuzu kabisa kukataa kukilipa na wala sio dhuluma. Lakini jawabu hili linajulikana kwa kufanyiwa kwake kazi na kuuzuia ulimi wa Kiongozi wa nchi na nafasi aliyonayo, sio kwa lengo la kutaka kutangaza; mpaka wasije watu wakathubutu kutoa zaidi ya wanavyostahiki kutoa. (Mwisho) [Haashiyatu Ibni AAbidiin, 2/57].
Na amesema Imamu Abu Haamid Ghazal, miongoni mwa wanachuoni wa Madhehebu ya Shafiy, katika kitabu cha [Almustaswfaa, ukurasa wa 177, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah] Mikono inapokuwa mitupu haina pesa, na mali ya masilahi ya umma ikawa haitoshi kwa matumizi ya jeshi, na kama wanajeshi watajiengua na kuanza kufanya kazi zingine za kujitafutia ziriki basi pangechelewa kuingia kwa makafiri katika nchi ya Kiislamu, au pangehofiwa kutokea kwa fitna kwa wale wenyekufanya ufisadi ndani ya nchi ya kiislamu, na kwa hivyo inajuzu kwa Kiongozi wa nchi kuwatoza matajiri kiasi cha kodi inayotosha kumhudumia mwanajeshi.
Na Sheikh Taqiyu Diin bin Taimiya amezungumzia katika [Majmuuil Fataawa, 30/337, na yaliyo baada ya kurasa hizo, Ch. Majmaul Maliki Fahdi litwabaatil Mushafi Shariif Bi Suudia] baadhi ya kinachochukuliwa na Kiongozi wa nchi kwa namna inayomaanisha kukiri kwake jambo hilo kwa kulizingatia ni katika jihadi ya Mali iliyo wajibu kwa matajiri, na akaiita tozo ya Sultani, kwa maana ya: tozo za kifedha anazoziweka kiongozi kwa wananchi wake au sehemu ya wananchi hao. Na katika [Almuhallaa libni Hazmi Dhwaahiriy, 4/281, Ch. Dar Al Fikr Bairut]: Na ni faradhi kwa Matajiri miongoni mwa wananchi wa kila nchi kufanya hivyo kwa Mafukara wao, na Kiongozi wa nchi atawalazimisha wafanye hivyo kama Zaka hazitoshi kwa Mafukara hao. (Mwisho)
Na kwa maelezo yaliyotangulia inabainika wazi uhalali wa Kiongozi wa serikali kuwatoza watu kodi kwa ajili ya kutumia kinachopatikana katika Masilahi ya Umma. Ama kwa upande wa kuchukua kodi za vilivyoharamishwa kama vile pombe na mfano wake, inajuzu pia kwa maelezo yafuatayo:
Kwanza: Kuna tofauti baina ya thamani ya kilicho haramu na Kodi inayotozwa juu ya kitu hicho; Thamani ya Pombe kwa mfano ni mali ambayo inatolewa kama malipo ya kununulia bidhaa hii iliyoharamishwa, na Pombe ni Haramu kwa Makubaliano ya Waislamu wote, na thamani yake katika nchi ya Kiislamu ni Haramu kwa makubaliano ya waislamu wote pia, na kwa hivyo haijuzu kuinunua au kuiuza na kuchukua thamani yake baina ya Waislamu.
Na hii ni kinyume na Kodi mbali mbali. Na tayari tumekwishaainisha, nayo hapa ni kiwango maalumu cha pato kinachokatwa kutokana na biashara hizo na Bidhaa za Haramu na wala sio thamani yake; na kwa hiyo hakuna uhusiano wowote wa kuwa bidhaa hii ni halali au haramu, na wakati huo kodi haiwi juu ya pombe au mfano wake katika vilivyoharamishwa, kama thamani ya chochote katika hivyo, na kwa ajili hiyo sio Haramu kuichukua kodi yake na kunufaika nayo.
Pili: Ni kwamba Jambo hili lina mfanowe katika Fiqhi ambao hupimwa kwa mfano huo, nao ni Kodi ya Kichwa; Kodi hii ya Kichwa imewekwa kwa wasiokuwa Waislamu na katika Mali zao juu ya thamani za Pombe na faida za Riba, na pamoja na hayo hakuna yoyote katika makhalifa au Viongozi aliekataa Mali hizo na kuziingiza katika Hazina ya Mali za Waislamu pamoja na kunufaika nazo.
Na kauli ya kwamba hii ni kwa wasiokuwa Waislamu tu, na kwamba kwa Waislamu haifai, jibu lake ni kwamba: Hakika inajuzu kuchukua kodi kutoka kwa Waislamu kwa mfano huo pia; na hiyo ni kwa kuwa kutochukua kodi kutoka kwa watu hao katika biashara hizo za Haramu ni kama katika biashara zingine za halali, inakuwa ni sawa na kuwapa msukumo wa kuendelea kuzifanya, na kwa hivyo wanakuwa wanakusanya baina ya Biashara katika vilivyoharamishwa na baina ya kustarehe na Mapato kwa ukamilifu, na hii inaweza kupelekea kukua kwa biashara zao. Ama kwa upande wa kuchukua kodi kutoka kwao juu ya biashara zao, kuna kuwabana ikiwa kuna uhalisia huo haiwezekani kamwe kuuondosha kwa mara moja.
Na hili lina upande mwingine katika kauli za Wanachuoni na Wanachuoni wa Fiqhi; baadhi yao wanaona ya kwamba atakayetekeleza malipo kwa ajili ya kilichoharamishwa kutoka kwa mtu anaekimiliki na kwa ridhaa yake mwenyewe kisha akatubu basi hawajibiki kurejesha kilicholipwa kwa mtu huyo mpaka asije akawa anamsaidia mwenzake katika maasi kwa ajili ya kujipatia anachokilenga na kurejea kwa mali yake kwake.
Na katika walioashiria jambo hili ni Imamu Ibin Qayim katika kitabu cha: [Zadul Maadi Fii Hudaa Khairil Ibaad, Juzuu ya 5/690-691, Ch. Muasasatul Risaalah]; ambapo alisema akiwa anazungumzia kuhusu kipato cha mzinifu anapokipokea, kisha ikathibitika hivyo, je analazimika kukirejesha alichokipokea, kwa wenyewe? Au kinakuwa kizuri kwake kukitumia, au akitoe sadaka? Ni kama ifuatavyo: "Hili linajengeka katika Msingi mkubwa kati ya misingi ya Uislamu, nao ni kwamba mwenye kupokea kisichokuwa chake atakuwa amekipokea kisheria, kisha akataka kuachana nacho, kikiwa hicho kilichopokelewa kimechukuliwa bila ya ridhaa ya mwenyekukitoa, na kikawa hakijatimiza masharti ya malipo, basi atakirejesha kwa mwenyewe. Na ikishindikana kukirejesha kwa mwenyewe basi atalipia deni analolijua la huyo mwenyewe, na ikishindikana hivyo, basi atakirejesha kwa warithi wake, na ikiwa itashindikana basi atakitoa sadaka, na iwapo atachagua mwenye haki kujipatia thawabu siku ya Kiama basi atazipata. Na iwapo atakataa isipokuwa atakapoyachukua mema ya mwenye kukipokea atakuwa ametekeleza malipo kwa mali yake, na thawabu za Sadaka zitakuwa kwa aliyekitoa sadaka. Vile vile imethibitika kutoka kwa Maswahaba wa Mtume S.A.W, R.A, kwamba: ikiwa kilichopokewa ni kwa ridhaa ya mtoaji na amelipia kilicho haramishwa, kama vile aliyelipia pombe au nguruwe au juu ya uzinifu au uchafu wowote, hapo haiwajibiki kurejesha malipo yake kwa mtoaji kwa sababu yeye amekitoa alichokitoa kwa ridhaa yake mwenyewe, na ametekeleza malipo ya kilichoharamishwa, na kwa hivyo haijuzu akusanye baina ya malipo mbadala na aliyelipiwa, kwani kufanya hivyo ni kumsaidia katika makosa na uadui, na kuwarahisishia wafanya maasi dhidi yake.
Na ni kipi akitakacho mzinifu na mtendaji wa kitendo hicho ikiwa atajua kuwa atalifikia lengo lake na atarejesha mali yake, na hili ni katika yanayolindwa na Sheria kufanyika kwake. Na wala haifai kutia neno juu yake. Na hii inakusanya baina ya Dhulma na Uzinzi na Uvunjaji wa ahadi. Na kwa hivyo, mtu yoyote atakayekichukia kitu kinachochukiza anapaswa kutekeleza malipo yake mbadala kutoka kwa mziniwa kisha akirejeshe tena kwa nguvu alichokitoa, na ubaya wa kitendo hicho umetulizana katika maumbile ya wote wenye akili, haiwezekani.
Na sisi tunawasisitizia wenye majukumu na wenye kuyasimamia masilahi ya nchi na wananchi, wachukue hatua za kihalisia kwa ajili ya kuzuia uzaji wa bidhaa au huduma zilizoharamishwa na kuzifyeka zisiwepo katika nchi za kiislamu, na au kuruhusu waislamu kwa vyovyote vile kuzifanya kazi hizo za haramu, ili mambo yatulizane na uzito uondoke.
Kisha hakika yake kwa kuhama mali hii kutoka katika dhima ya mtu anayefanya biashara ya vitu vilivyoharamishwa na kuelekea katika hazina ya nchi, basi mali hiyo huwa safi na inajuzu kujinufaisha kwa mali hiyo katika masilahi ya Umma, na baadhi ya Wanachuoni wa Fiqhi wametaja ya kwamba Uharamu hauvuki dhima mbili, na kwa hivyo kwa kuhama mali kutoka katika dhima ya muhusika na kuelekea katika hazina ya serikali, itakuwa halali na itajuzu kujinufaisha nayo.
Katika Hashiyatul Alaama bin Aabidiin, wa Madhehebu ya Hanafi, [Radul Muhtaar alaa Durril Mukhtaar, 2/292. Darul Fikri]: na katika Hashiyatul Hamawiy an Dhakhiirah: Mwanachuoni wa Fiqhi Abu Jafar aliulizwa kuhusu mtu aliyechuma mali yake kwa njia ya Matarishi wa Masultani, na akakusanya mali kwa kutoza fidia za Haramu na kwa njia nyingine, je ni halali kwa mtu anayejua hivyo kula chakula chake? Akasema: Kwa upande wangu inapendeza zaidi asile chakula cha mtu huyo, na kuna hukumu ya kutosha kuwa anaweza kukila kama chakula hicho hakikuwa katika mikono ya mlishaji aliepora au kula rushwa. Kwa maana chakula hicho sicho kilichochukuliwa kwa nguvu au kwa rushwa; kwani yeye hakukimiliki kwa hiyo uharamu ni ule ule na hauwi halali kwake au kwa mtu mwingine.
Na imetajwa hapa katika kitabu cha Bazaaziyah kwamba mtu ambaye sio halali kwake kuchukua sadaka, basi ni bora kwake asichukue zawadi kwa Sultani, kisha akasema: na alikuwa Mtaalamu Khawaarizmi hali chakula chao na anachukua zawadi zao, akaambiwa kuhusu jambo hilo akasema: kutoa chakula ni halali, na Uhalali unakuwepo kwa umiliki wa halali kwa hivyo inakuwa ni mwenye kula chakula cha dhalimu, na uhalali ni kumiliki na kwa hivyo mwenye kumiliki anafanya atakavyo katika anachokimiliki. Mimi nikasema: huwenda pamejengewa hoja kwa kauli ya kwamba Haramu haivuki na kuelekea katika dhima ya watu wawili kwa wakati mmoja. Mpaka mwisho. Na ilitajwa katika kitabu cha Bazaaziyah hapa kuhusu asiyehalali kukichukuwa kitu….
Anasema Mwanazuoni Muflih wa Madhehebu ya Hambal katika Kitabu cha: [Al Furuugh, 4/390. Ch. Muasasatul-Risaalah]: Na Kundi la wapokezi limepokea Hadithi ya Thauriy kutoka kwa Salama bin Kuhail, kutoka kwa Dharu bin Abdillahi, kutoka kwa Ibnu Masud – R.A – kwamba Mtu mmoja alimuuliza akasema: Mimi nina jirani yangu anaekula riba na huwa anaendelea kunialika chakula, akasema: Wewe kwako ni halali na madhambi ya riba ni yake mwenyewe. Na kuna kundi la watu pia wamepokea Hadithi kutoka kwa Muamar kutoka kwa Abu Ishaaq kutoka kwa Zubeir bin Khariit kutoka kwa Salmaan R.A, amesema: Unapokuwa na rafiki mfanyakazi akakualika chakula basi mkubalie, kwani hakika chakula chake kwako ni halali na madhambi ya riba ni yake. Na Alhasan aliulizwa kuhusu chakula cha wafanyakazi wa benki akasema: Hakika Mwenyezi Mungu amekuelezeni kuhusu Mayahudi na Manaswara kwamba wao wanakula riba na mmehalalishiwa chakula chao. Na anasema mmoja wao kumwambia Ibrahim Nakhiiyu: …kwetu sisi anachuma kutokana na dhuluma na ananialika mimi na wala simkubalii mwaliko wake, akasema Ibrahim: Shetani ana lengo katika jambo hili ili atie uadui baina yenu.
Na kwa maelezo yaliyotangulia, jibu la swali lililoulizwa linajulikana wazi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.