Kutumia Sifa ya Shahidi.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumia Sifa ya Shahidi.

Question

Ni kwa nini kila anayekufa katika matukio fulani huitwa “shahidi” hali ya kuwa marehemu hakupambana na adui wala hajafa kwa ajili ya kulinda heshima yake, nafsi yake au hata mali zake? Ni ipi hukumu ya Kisharia kwa yule aliyekwenda kwenye maandamano au kushiriki kwenye mgomo na kutokea matukio yaliyopelekea kifo chake? Je, mtu huyu atakuwa Shahidi au ni mtu tu aliyeuwawa na atafufuliwa kwa mujibu wa na nia yake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Asili ya neno Shahidi, ni sifa ya kila aliyeuwawa katika kupigania njia ya Mwenyezi Mungu, kisha likatumika kwa upana zaidi na kikatumika kwa kila aliyeitwa na Sharia Takatifu kuwa yeye ni Shahidi hata kama hakuwa kwenye mapigano.
Kumekuwa na dalili nyingi zinazoelezea ubora wa mtu shahidi na mashahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa dalili hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali wao wako hai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi} [AAL IMRAAN, 169]. Imepokelewa na Imamu Muslim kutoka kwa Masrouq amesema: Tulimuuliza Abdillah Ibn Masoud R.A. kuhusu Aya hii, akasema: Ama sisi tuliuliza hilo kwa maana tulimuuliza Mtume S.A.W. na akasema: "Roho zao zipo kama mfano wa ndege wa kijani mwenye taa na kutundikwa kwenye arshi, zikiwa zinaelea peponi kama zitakavyo, kisha zinaenda kwenye hiyo taa na kuangaliwa na Mola wao kisha anaziambia: Je mnapenda chochote? Zitasema: ni kitu gani tunapenda hali ya kuwa sisi tunaelea peponi kama tutakavyo, kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ataendelea kuziuliza hivyo mara tatu, pindi roho zitakapoona kuwa hazitoachwa kuulizwa ndipo zitasema: Ewe Mola, tunataka roho zetu zirudi kwenye miili yetu ili tupigane kupigania njia yako kwa mara nyingine, pindi atakapoona kuwa hazina mahitaji ataziacha".
Kwa hakika shahidi ameitwa shahidi kwa sababu Mwenyezi Mungu na Mtume wake S.A.W. wameshuhudia kwake kuwa ni mtu wa Peponi, au kwa sababu Malaika wanamshuhudia na kumbashiria neema, kwa maana hizi mbili anakuwa shahidi kwa maana ya kushuhudiwa kwake, tena inasemekana: Kwa sababu roho yake itashuhudia Peponi kabla ya roho za watu wengine, na kwa maana hii basi anakuwa ni shahidi kwa maana ya mwenye kushuhudia, na pamesemwa tofauti na hivyo [Angalia: Kitabu Taj Al-Arus, 8/253, 254, Ch. Dar Al-Hidaya, na Hashiat Al-Baijuriy, 1/254 Ch. Al-Halabiy].
Na shahidi ni aina tatu:
Aina ya Kwanza: Shahidi wa dunia na Akhera: Naye ni yule aliyeuwawa na adui, katika kutangaza na kuinua neno la Mwenyezi Mungu.
Aina ya Pili: Ni shahidi wa dunia tu: Naye ni kama aliyepigana na kuuawa na adui kwa sababu ya mahitaji ya kidunia, kama vile kujionesha au kupata ngawira.
Aina ya Tatu: Ni shahidi wa Akhera tu, naye anatofautiana na shahidi wa kwanza pamoja na shahidi wa pili kwa kuwa anaoshwa na kusaliwa tofauti na mashahidi wawili wa kwanza, na malipo yake ni kwa Mwenyezi Mungu, na vigawanyo vya aina hii ni vingi na vimetajwa katika Hadithi nyingi za Mtume miongoni mwazo ni pamoja na Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari na Muslim kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mashahidi ni watano: Aliyefariki kwa ugonjwa wa tauni ni shahidi, mwenye kufa kwa maradhi ya tumbo ni shahidi, mwenye kufariki kwa kuzama majini ni shahidi, mwenye kufariki kwa kubomokewa na ukuta au nyumba ni shahidi na shahidi aliyefariki katika njia ya Mwenyezi Mungu”.
Na Hadithi iliyopokelewa na Abu Dawud na wenzake kutoka kwa Jabir Ibn Atiik R.A. amesema Mtume S.A.W. amesema: “Kifo cha Ushahidi kina aina saba ukiondoa kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu: Mwenye kufariki kwa ugonjwa wa tauni ni shahidi, aliyekufa kwa ajali ya kuzama majini ni shahidi, na aliyefariki kwa sababu ya maradhi ya kuharibika kwa mapafu ni shahidi, aliyefariki kwa kuzama majini ni shahidi, aliyefariki kwa kuungua moto ni shahidi, na aliyefariki kwa kuangukiwa na nyumba au ukuta ni shahidi na mwanamke aliyefariki akiwa na mtoto tumboni ni shahidi”.
Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Abi Huraira amesema: Kuna mtu mmoja alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi unaonaje akija mtu anataka kuchukua mali zangu? Akasema “Usimpe mali zako” akasema: Unaonaje ikiwa atanishambulia? Mtume akasema: “Pambana naye” akasema: Unaonaje ikiwa ataniua? Mtume akasema: “Basi wewe unakufa shahidi” akasema: Unaonaje ikiwa nitamuua? Mtume akasema: “Yeye ni mtu wa motoni”.
Imamu Jalal Ad-Din As-Suyutiy ameelezea ndani ya kitabu chake alichokiita: “Milango ya furaha katika sababu za ushahidi” na ameelezea Abdillah Ibn Saddik Al-Ghumariy katika kitabu chake alichokiita “Ubora wa shahada na aina za mashahidi”.
Hukumu ya ushahidi unafungamana na kila aina katika aina zilizotajwa, ama kuhusisha ushahidi maalumu kwa yule anayeaminika kuwa ni mmoja wapo, basi hili ni katika lisilowezekana kufahamika kwa kawaida, kwa sababu ushahidi ni ahadi, na kutekeleza ahadi maalumu kunakuja kwa kufikiwa masharti, basi huyu aliyeainishwa jambo lake lipo kwa Mwenyezi Mungu, na kinachowezekana kusemwa katika hali fulani ya kuhesabiwa ni shahidi wala hatumtakasi kwa Mwenyezi Mungu mtu yeyote.
Imepokelewa na Imamu Bukhari katika kitabu chake kutoka kwa Abi Huraira R.A. amesema kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mwenyezi Mungu Anamjua mwenye kupigana Jihadi katika njia yake”.
Kutoka kwa Sahl Ibn Saad Al-Saidy R.A. amesema kuwa, Hakika ya Mtume S.A.W. alikutana na washirikina na kupigana nao, pindi Mtume alipoelekea kwa askari wake na washirikina wakaelekea kwa askari wao, na katika Masahaba wa Mtume kulikuwa na mtu huwa aachi jambo lolote isipokuwa hulifuatilia na kulishambulia kwa upanga wake, pakasemwa: leo hakuna aliyetugawa kama alivyowagawa fulani, Mtume S.A.W. akasema: “Ama huyo ni mtu wa motoni” mtu mmoja akasema mimi nimfahamu, akaambiwa: toka naye kila anaposimama simama naye na akitembea haraka tembea naye, akasema yule mtu akajeruhiwa kwa majeraha makubwa na kuharakisha mauti, panga lake likiwa chini ardhini na makali ya panga akayaweka kwenye kifua chake kisha akajiua mwenyewe, ndipo yule mtu akatoka kwenda kwa Mtume S.A.W. na akasema ninashuhudia kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume akauliza “Na vipi kuhusu yule mtu” akajibu kuwa yule mtu uliyemtaja hapo mwanzo ni katika watu wa motoni watu wakashangazwa na hilo, akasema yule mtu mimi nilikuwa naye kisha yule mtu alijeruhiwa majeraha makubwa na kufariki kwa kujiua mwenyewe, Mtume S.A.W. akasema baada ya maelezo hayo: “Hakika mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa peponi kama vile inavyoonekana kwa watu, hali ya kuwa yeye ni mtu wa motoni, na kuna mtu anaweza kufanya matendo ya watu wa motoni namna yanavyoonekana kwa watu, hali ya kuwa yeye ni mtu wa Peponi”.
Imamu Bukhari amezigawa Hadithi hizi mbili na akasema: “Mlango hausemi: fulani ni shahidi”. Amesema Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Fat-h Al-Bari, 6/90 Ch. Dar Al-Maarifa]: “kwa maana ya maelezo ya moja kwa moja isipokuwa ikiwa kwa njia ya Wahai”.
Imepokelewa na An-Nisaaiy na Ahmad na wengine kutoka kwa Omar Ibn Al-Khatwab R.A. kuwa amesema: Watu wengine husema kwa yule aliyeuwawa kwenye mapigano yenu au akafa, basi fulani ameuwawa shahidi au amekufa shahidi, huenda ikawa ni kushindwa kwa mnyama wake au kuondoka taratibu kwa mnyama wake au ni mambo ya biashara basi wala msisema hivyo lakini semeni kama alivyosema Mtume S.A.W.: “Atakaeuawa au akafariki katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi huyo ni mtu wa Peponi”.
Imepokelewa na Abu Naim katika kitabu cha: [Al-Hiliya, 8/251 Ch. As-Saada] kutoka kwa Abi Dharr R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Ni nani mnamdhania ni shahidi kati yenu? Wakasema: Ni yule aliyeshambuliwa kwa silaha. Mtume akasema: “Ni wangapi wameshambuliwa na silaha na wamekufa hali ya kuwa si mashahidi wala vifo vizuri, na wangapi waliokufa wakiwa vitandani mwao hali ya kuwa wakizingatiwa kwamba wao ni mashahidi Mwenyezi Mungu?”
Lakini kuzuiwa huku kunachukuliwa moja kwa moja ushahidi una sura maalumu kama tulivyoelezea, na dalili ya hilo ni kuwa shahidi ni kwa yule aliyeuwawa kwa kupigania neno la Mwenyezi Mungu liwe juu basi huyu ndiye aliye kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kuthibiti kuwa yupo kwenye njia ya Mwenyezi Mungu basi huyo hupewa hukumu ya ushahidi.
Ama kuitwa kwake shahidi kwa njia ya kuitwa au kuzingatiwa mbele ya Mwenyezi Mungu bila ya dalili ya moja kwa moja, basi hakuna ubaya kwenye hilo kama inavyosemwa: Marehemu fulani na inakusudiwa ni kuombewa dua ya huruma; kama kwamba anasema: Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu fulani, ni utaratibu huu unaofahamika katika lugha ya Kiarabu kama ni mfumo wa habari ambao hukusudiwa uanzishaji kitu na mfano wake ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani}[AAL IMRAAN, 97]. Kwa maana mpeni amani, wala asikutwe na hali ya mauaji au dhuluma na visivyokuwa hivyo.
Na inaonesha kufaa kwa kutumika maana hii: ni Hadithi iliyopokelewa na Muslim kutoka kwa Omar Ibn Al-Khatwab R.A. kuwa amesema: Siku ya Khaibar alikutana na kundi kubwa na Masahaba wa Mtume S.A.W. wakasema: fulani shahidi fulani shahidi ndipo Mtume S.A.W. akasema: “Hapana hakika yangu nimemuona akiwa motoni”, kisha Mtume akaendelea kusema: “Ewe Ibn Al-Khatwab nenda na uwaambie watu kuwa hakuna atakayeingia Peponi isipokuwa Waumini”. Anasema nikatoka na kuwaambia watu kuwa hakuna atakayeingia Peponi isipokuwa Waumini.
Katika Hadithi hii ni dalili kuwa Masahaba walitumia neno shahidi kwa kuwaita watu na Mtume hakuwapinga mpaka pale alipofikiwa na Wahai kuwa mmoja wao si shahidi, pindi Masahaba walipokuwa hawawezi kufahamu moja kwa moja mwisho wa mtu basi kauli yao ilikuwa inachukuliwa kama vile tulivyoeleza au kuwa ni shahidi kwa maana ya sura ya wazi inayoonekana.
Vile vile yale yaliyopitishwa na vitabu vya Fiqhi miongoni mwa hukumu za shahidi kwa Muislamu ambaye amekufa vitani dhidi ya maadui wa Dini ikiwa ni pamoja na kuacha kumuosha na kutomsalia huchukuliwa kwa sura ya nje inayoonekana lakini jambo la maiti baada ya hapo linaachwa kwa Mwenyezi Mungu na matendo huchukuliwa kwa mujibu wa nia.
Anasema Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Al-Fat-h, 6/90]: “Wameifanyia kazi watu waliotangulia juu ya kuitwa waliofariki kwenye vita vya Dadr na Uhud na visivyokuwa vita hivyo kuwa ni mashahidi, na kusudio la hukumu hiyo limejengewa juu ya dhana.
Imekuwa ni kawaida kwa Maimamu kuwa wameita wasifu huu kwa makundi, amesema Al-Hafidh Adh-Dhahabiy katika tafsiri ya Imamu Abi Hanifa kwenye kitabu cha: [Siar Al-Aalam An-Nublaa, 7/403, Ch. Taasisi ya Risala]: “Wamekufa mashahidi”.
Na pia katika tafsiri ya Abi Naim Ibn Dakeen, 10/151: “Abuu Naiim alikufa Shahidi kwa sababu alipigwa kisu shingoni”.
Amesema Imamu Ibn Jawziy katika tafsiri ya Abi Mahasin Ar-Ruyaniy katika kitabu chake: [Al-Muntadhim, 17/113, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] “Amekufa shahidi kwa kuuawa kwa njia ya dhuluma siku ya Aashuraa”.
Na katika kitabu cha: [Miraat Al-Jinan cha mwanachuoni Al-Yafii, 3/261, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] katika tafsiri ya Wazir Ibn Habir amesema: “Amekufa shahidi mwenye kufa kwa sumu”.
Amesema Al-Hafidh Ibn Hajar katika tafsiri ya Ahmad Ibn Abdillah Al-Mazy katika kitabu Inbaa Al-Ghamr, 1/242, Ch. Baraza kuu la Kiislamu: “Alidondoka kutoka kwenye paa la nyumba na akafa Shahidi.
Amesema Al-Hafidh As-Seyutiy katika tafsiri Ash-Shams Al-Asfahaniy kwenye kitabu cha: [Min Husn Al-Muhadhara, 1/545, Ch. Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah]: “Amekufa shahidi kwa sababu ya ugonjwa wa tauni”. Na kuna maelezo mengine mengi zaidi ya haya yaliyotolewa.
Kwa maana hiyo sifa ya shahidi kwa Muislamu aliyekufia vitani dhidi ya maadui, au aliyekufa kwa sababu miongoni mwa sababu ambazo Sharia inamzingatia yule atakaekufa kwa sababu hizo kwamba ni shahidi, basi hakuna ubaya wowote kwa Kuwa Msemaji hakusudii kuikata shauri kwa ushahidi wake bali anakusudia kwa kuitumia kwake wazi iwe tegemeo au iwe Dua.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: mwenye kutoka kwa ajili ya maandamano kisha yakatokea matukio yaliyopelekea kifo chake, hali yake pia kama tulivyoeleza, hivyo inafaa kuzingatiwa shahidi ikiwa hakuwa mwenye kufanya uadui na ikawa sababu ya kifo chake ni sababu za maasi kama vile kwenda kinyume na sharia au kanuni, au akiwa ametoka kwa ajili ya kulingania fitina au kufanya matendo ya kuuchochea moto wa fitina, au kufanya uadui dhidi ya roho za watu na mali za umma au za watu binafsi na mfano wa hayo, basi mwenye kuwa katika hayo huyo si shahidi, wala haifai kwa mtu huyo kupewa sifa hii Tukufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas