Utekelezaji wa Kanuni ya Kiapo kwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Utekelezaji wa Kanuni ya Kiapo kwa Mwenye Kukataa katika Mashtaka.

Question

Je! katika Mashtaka - kwa mfano, ya wizi – hutekelezwa kanuni ya kiapo kwa mwenye kukataa? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni zake Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Inajulikana katika sehemu ya mahakama kwamba kuna Ushahidi wa mwenye madai, na kwamba kiapo ni kwa mwenye kukataa, na sheria hii ni ya jumla na ina mambo ya pekee. Je, hali ya kudai mtu kuwa ni “mwizi”, kanuni hii inatumika katika kama hali hii?
Kanuni hii asili yake ni Hadithi Tukufu ya Mtume S.A.W., iliyopokelewa kutoka kwa Al Baihaqiy na wengine kwa mapokezi hayo, na baadhi ya mapokezi haya katika Sahihi mbili, na mapokezi ya Imamu Muslim ni yafuatayo: "Ikiwa watu watapewa madai yao, watu watadai damu ya wanaume na pesa zao, lakini ushahidi unatakiwa kwa mwenye kudai".
Jambo lilikuwa hivyo kwa sababu mwenye kudai anadai jambo lililofichwa, anahitaji lidhihirike, na ushahidi una nguvu ya kudhihirisha; kwani ushahidi ni maneno ya wasio maadui, nao ni mashahidi. Ushahidi unafanywa kuwa hoja kwa mwenye kudai.
Kiapo kilichotajwa na mshitakiwa, ingawa kilithibitishwa kwa kutajwa jina la Mwenyezi Mungu, lakini ni maneno ya adui, na hakitumiwi kiapo hicho kama hoja ya haki hiyo, lakini kinatumika kama hoja ya mshtakiwa, kwa sababu anashikilia dhahiri na asili, ambayo ni kutokuwa na kosa na kwa hivyo, anahitaji kuendelea na hukumu ya dhahiri. Na kiapo, ingawa ni maneno, huwa kinatosha kwa Al-Istiswahab (yaani kukamatana na hali ya mwanzo); na kwa hivyo, kufanya ushahidi kuwa ni hoja ya mwenye kudai na kiapo ni hoja ya mshtakiwa, kuweka kitu mahala pake, hali hiyo ni upeo wa hali ya juu wa hekima.
Al-Khatwib As-Sherbiniy alisema: Maana yake ni kwamba upande wa mwenye kudai ni dhaifu kwa sababu ya kudai kwake kinyume na asili kwa hivyo alitakiwa kutoa hoja ya nguvu, na upande wa mshtakiwa ni nguvu kwa hivyo inatosha kutoa hoja dhaifu, lakini Ushahidi ulikuwa wa nguvu na kiapo ni dhaifu kwa sababu mwenye kiapo anatuhumiwa kwa uongo katika kiapo chake; kwani anajiepusha na adhabu kwa kiapo hicho kinyume na shahidi”. [Mughni Al-Muhtaaj 6/399, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Badr Ed-Diin Al-Ainiy alisema: “Imesemekana kwamba: Hekima ni katika hali ya kufanya ushahidi kwa mwenye kudai kwa sababu upande wake ni dhaifu, kwani anasema kinyume na hali iliyo dhahiri anajitia nguvu kwa ushahidi, na upande wa mshtakiwa ni nguvu, kwa sababu asili ni kutokuwa na hatia, kwa hivyo inatosha kula kiapo kwani kiapo ndicho ni hoja dhaifu. [Umdet Al-Qarii' Sharhu Sahihi Al-Bukhariy 13/248, Ch. Dar At-Turath Al-Arabiy].
Ibn Rajab Al-Hanbaliy alisema: “Wanavyuoni miongoni mwa wenzetu walitofautiana na wanavyuoni wa madhehebu ya Shafi katika tafsiri ya mwenye kudai na mshtakiwa. Baadhi yao walisema kwamba: Mwenye kudai ni anayeomba jambo lililofichwa kinyume na asili au dhahiri, na mshtakiwa ni kinyume naye” [Jamii' Al-Ulum wal Hikam uk. 230, Ch. Muasastur Resalah].
Kuhusu hukumu ya suala la kumtuhumu mwingine, kuwa msingi uliotajwa hapo juu unatekelezwa kwa ujumla wake. Lakini, ikumbukwe kwamba mfano uliotajwa na aliyehojiwa katika swali lake – nao ni wizi - kwa kweli umegawanywa katika sehemu mbili: sehemu inayohusu haki ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni adhabu ya wizi, na sehemu inayohusu watu, nayo ni kurudisha pesa zao zilizoibiwa. Kuhusu haki ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni adhabu, haihitaji kiapo, lakini haki ya watu kiapo hutumika, basi anayemtuhumu mwingine kwa kuiba pesa, anatakiwa kutoa ushahidi, na kama hakuuleta ushahidi, mshtakiwa anaweza kula kiapo, kama atakula kiapo, basi atakuwa ametekeleza wajibu wake na lazima aachwe huru, lakini kama akikataa kula kiapo lazima arudishe pesa, lakini haadhibiwi, kwa sababu kiapo kilikuwa kwa ajili ya haki ya watu na siyo kwa ajili ya adhabu.
Dalili ya kwamba adhabu ni mbali na suala la kula kiapo ni kwamba kuachana na kula kiapo kwa kweli ikiwa tukichukulia kuwa ni kukiri, basi ni uthibitisho wa tuhuma lakini una shaka, na adhabu inaondolewa kwa mashaka, kana kwamba akikiri juu ya nafsi yake mwenyewe kwa adhabu kisha akarudi kabla ya kurudi kutoka kwake na hakuadhibiwa, hali ya kuacha kula kiapo pamoja na kutokiri hali hii ni bora zaidi, kwa sababu sheria huita kwa kujificha mwanadamu mwenyewe, na hali ya kula kiapo ni kinyume na hilo.
Wanavyuoni walisema kama tulivyosema, lakini kwa maelezo zaidi:
Al-Sarkhasi alisema: “Hakuna kiapo katika adhabu, kwani haizingatiwi hali ya kukataa kula kiapo, na hali ya kukataa kula kiapo ni sawa sawa na kukiri, na hairuhusiwi kuizingatiwa hali hiyo.” [Al-Mabsout 16/117, Ch. Dar Al-Maarifah].
Ibn Abd Al-Barr alisema: “Hairuhusiwi kula kiapo katika adhabu yoyote isipokuwa katika Al-Qassamah na kiapo cha liaan.” (Al-Kafiy fi Fiqhi Ahalu Lmadinah 2/923, Ch. Maktabtur Riyadh Al-Hadithah].
Al-Mawardiy alisema: “Kuhusu ushahidi maalum ni shahidi na wanawake wawili, na shahidi na kiapo; kwani ni ushahidi unaolazimisha pesa wala haulazimishi adhabu, lakini katika wizi unalazimisha pesa na adhabu pia.” [Al-Hawiy Al-Kabiir 13/336, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Ibn Qudaamah alisema: "Haki ya Mwenyezi Mungu ni aina mbili, moja yao ni adhabu, ambayo hakutumiwi kula kiapo. Hatujui kwamba wanavyuoni wametofautiana katika suala hilo; kwa sababu kama kukiri, kisha akarudi anakubaliwa na kuachwa huru pasipo na kula kiapo, kwa hivyo ni bora zaidi kutoombwa kula kiapo pamoja na kutokiri, kwa sababu inapendekezwa kumsitiri mtu yule, na kumwashiria kwa mwenye kukiri kuacha hali hi ya kukiri, na mashahidi pia waache kutoa ushahidi na kumsitri kwa mujibu wa Hadithi ambayo Mtume wakati alipomwambia Hazzal katika Hadithi ya Maaiz: "Ewe Hazzal, Kama ukimsitiri kwa nguo zako, ilikuwa ni vizuri kwako". Basi hakuna kiapo katika hali hiyo kabisa. Aina ya pili: Ni haki za kifedha, Kama kudai kwamba mwenye pesa huyo analazimishwa kutoa Zaka, na kwamba mwaka umemalizika na ana pesa zilizostahiki Zaka. Imam Ahmad alisema: kauli ni kauli ya mwenye pesa pasipo na kula kiapo, wala watu wanaombwa kula kiapo kwa ajili ya pesa zao za Sadaka.
Imam As-Shafiy, Abu Yusuf na Muhammad walisema: anaombwa kula kiapo kwani ni madai yanayosikika, nayo yanafanana na haki za binadamu, na kwetu, ni haki ya Mwenyezi Mungu, kama adhabu sawa sawa, na kwani jambo hili ni ibada, basi haiombwi kula kiapo kama swala, na kama akidaiwa kuwa ana kafara ya kiapo au nadhri au sadaka au kitu kingine, inazingatiwa kauli yake tu pasipo kiapo, hauzingatiwi uhasama huu wala katika adhabu kwa Mwenyezi Mungu, kwani hakuna haki kwa mwenye kudai katika hali hiyo, wala hakuna utawala juu yake, basi uhasama huu hauzingatiwi kabisa”. [Al-Mughni 10 / 213- 214, Ch. Maktabat Al-Qahirah]
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu: Ni wazi kwamba kanuni ya “Kiapo kwa mwenye kukataa” inatekelezwa katika madai ya mashtaka - kama vile wizi -, katika adhabu ya haki za watu, lakini kwa upande wa adhabu zinazokadiriwa na Mwenyezi Mungu (ambazo ni huduud) kanuni hiyo haitekelezwi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas