Kutumia Silaha za Maangamizi Dhidi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumia Silaha za Maangamizi Dhidi ya Nchi Zisizo za Kiislamu

Question

Katika zama za hivi karibuni kumeanza kuonekana baadhi ya maandishi kutoka kwa baadhi ya makundi ambayo yanadai kwa watu wao kuwa inafaa kwao kutumia silaha za maangamizi dhidi ya nchi zisizo za Kiislamu wakidai kauli yao hii inakubaliana na sharia, wakileta baadhi ya maandiko ya kifiqhi kama dalili ya masuala yaliyotajwa. Je, maneno haya ni kweli yanakubaliana na sharia? 

Answer

Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu peke yake, sala na salamu ziende kwa Nabii wa mwisho naye ni Mtume wetu Muhammad pamoja na watu wake maswahaba zake na wale wanaomfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Silaha za maangamizi huitwa jina hili katika misamiati ya kijeshi, na kusudio lake ni aina ya silaha ambazo si za kawaida zenye kuharibu kwa nguvu kubwa sana, zinapotumika husababisha maangamizi makubwa katika eneo zima lililohusishwa, ni sawa sawa huangamiza viumbe hai wakiwemo wanadamu, wanyama, mazingira na kila kitu kinachoyazunguka mazingira hayo.
Silaha hizi zinagawanyika sehemu tatu: Silaha za atomiki, kama vile kombora la nyuklia Haidrojeni na kombora la naitrojini. Kombora la aina hii husambaza miyale yenye kuangamiza viumbe katika maeneo husika, na husababisha uchafuzi kamili wa mazingira unaodumu kwa muda mrefu na baadhi yake huangamiza wanadamu tu pasi na maeneo.
Silaha za kemikali, kama vile gesi za kivita zenye matumizi mengi pamoja na mada za kulipuka, zinakuwa na athari yenye madhara makubwa – wakati mwengine hupelekea kifo – kwa kiumbe chochote kile kilicho hai, kama ambavyo huaribu mazao na mimea, na mara nyingi maada hizi za kemikali zinakuwa na sumu katika hali ya gesi au mmimikiniko wenye kufoka haraka na mara chache sana kuwa kitu kigumu.
Silaha za kibailojia, hukusudiwa virusi ambavyo hutumiwa kueneza maradhi sugu hatari kwa upande wa adui, na kuleta hasara kwa upande wa wanyama au hata mimea.
Dola za Kiislamu kutumia silaha kama hizi kwa njia ya kutishia maadui ni jambo linalohitajika kisharia, na dalili ya hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu}[AL ANFAAL, 60], amesema mwanachuoni Al-Aaluusy katika tafsiri yake: [Maana yake ni kutumia kila chenye kuwapa nguvu kwenye vita 10/24, Ch. ya Dar Ihyaai At-Turaath Al- Araby]. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameamrisha katika Aya iliyotajwa kuwatisha maadui mpaka wasije kufanya uadui kwa Waislamu, kutishia kama ilivyo ni msingi wa kisharia huonekana kwenye wigo wa adhabu pamoja na kuadhirishwa, lakini pia ni msingi wa kisiasa wenye kuzingatiwa unategemewa na nchi katika siasa zake za kujilinda kama ilivyo katika elimu ya mkakati wa kijeshi, kutumia silaha hizi ni katika ukamilifu wa hayo mahitaji, na ukamilishaji wenye kuhitajika unahitajika, hivyo kuruhusu kitu katika ukamilifu ndio kusudio, wala hakuna cha kuficha katika hilo ikiwemo uwepo wa faida za kuleta uwiano wa kimkakati na kijeshi kati ya Mataifa, ambapo hilo hutengeneza muhimili wa kujilinda dhidi ya nchi ambayo huenda ikataka kuishambulia nchi ya Kiislamu, ambapo mwishowe huepusha ulazima wa kuingia katika vita ambapo kiasili sio kusudio.
Hii ni kwa upande wa silaha hizi na kuzitumia kama njia ya kutishia maadui, tofauti kati ya kutumia kama silaha za kutishia na kati ya kutangulia kuanza kuzitumia kama silaha za maangamizi, na sura inayolazimisha kuanza kuzitumia, sura hii imejengeka na baadhi ya jitihada za watu au mtazamo ambao unawahusu baadhi ya makundi, matumizi haya kisharia hayafai, na kauli ya kusema yanafaa na kunasibishwa na sharia pamoja na wanachuoni wake ni uongo na uzushi dhidi ya sharia na Dini, na dalili ya hili ni mambo yafuatayo:-
Jambo la Kwanza: Ni kuwa asili katika vita ni kutokuwa vita isipokuwa chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa Waislamu, jambo hilo lipo kwa msingi wa jitihada zake, kwa upande wa wananchi ni kuitikia amri yake jitihada zake, na lililowakilishwa kwake si jengine isipokuwa ni ule uelewa wake na usimamizi wake wa mambo ya wazi na yale yaliyojificha na kufahamu kwake mwelekeo wa matendo na matokeo yake pamoja na masilahi ya wananchi wake, kwa sababu hili tangazo la vita kuingia mikataba ya nchi au dola limewekwa kwake kwa cheo chake hicho, naye kwa nafasi yake hawezi toa maamuzi kwa utashi tu wa nafsi yake isipokuwa ni baada ya kurejea kwa watu husika wa maeneo yote yenye uhusiano na maamuzi yake, wakiwemo wazoefu wataalamu watu wa usalama washauri wa mambo ya siasa ambao mwisho wanazingatiwa ni washiriki katika kutoa maamuzi ambayo haiwezekani kwa kiongozi mkuu kuamua peke yake pasi na kupata ushauri wao.
Uamuzi wa mtu mmoja au kikundi ndani ya jamii ya Waislamu wa kutumia silaha kama hizi si kwenda kinyume na kiongozi tu bali ni kuukiuka uma kwa ujumla wake, ambapo hawa wanajipa wao wenyewe haki ya kuchukuwa maamuzi yanayofungamana na mustakabali wa uma wote pasi na kurudi kwa viongozi wa nchi wala wataalamu wa nchi kwenye mambo yanayo hatarisha nchi na wananchi wake.
Amesema mwanachuoni Al-Bahuty katika kitabu cha: [Sharhu ya kitabu cha Muntaha Al-Iraadat]: “NI haramu kuingia kwenye vita pasi na amri ya kiongozi mkuu, kwa sababu amri ya vita inarudi kwake kwa kuelewa kwake uwingi wa maadui uchache na vitimbi vyao isipokuwa ikiwa maadui wamestukiza na wakaogopa madhara yao na kero basi inafaa kuwapiga vita pasi na amri ya kiongozi mkuu kwa kuchunga masilahi” 1/636 chapa ya Aalam Al-kutub.
Jambo la Pili: Kutokana na kuwepo hali ya ukiukwaji wa makubaliano na mikataba ya kimataifa ambayo iliridhiwa na nchi za Kiislalmu na kujiunga pamoja na kukubali kwa hiyari yao ikiwa ni kwenda sawa na jamii ya kimataifa ili kufikia usalama na amani vya kimataifa kwa kadri ya kuwajibika kwa nchi zilizotia saini. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi} [AL MAIDAH, 01]. Na ahadi hutumika kwa kila wajibu uliopo kati ya pande mbili katika utekelezaji wa mambo fulani, amesema Sheikhul-Islaam At-Tuunisy mwanachuoni Ibn Aashur akiwa anaelezea Aya hii katika tafsiri yake, anasema: “Uelewa wa ahadi au makubaliano ni uelewa jumla unaojumuisha makubaliano ya Waislamu na Mola wao, nayo ni kufuata sharia zake...mfano wa makubaliano ya Mtume S.A.W, na Waumini kuwa hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu kwa kitu chochote wala hawataua wala kuzini...yanajumuisha makubaliano waliyoyafanya Waislamu na washirikina.... yakiwemo pia makubaliano ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe”. Kitabu cha: [At-Tahrir Wa Tanweer 6/74 Ch. ya Dar Tuunisiya].
Amepokea Imamu Tirmidhiy kutoka kwa Amr Ibn Auf Al-Muzny R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Waislamu wanafuata masharti waliyowekeana isipokuwa masharti yoyote yanayoharamisha halali na kuhalalisha haramu”, amesema Imamu Al-Hisas: “Ni jumla ya utekelezaji wa yote ambayo mwanadamu amekubaliana nayo pindipo tu hakuna dalili ya kuwa makubaliano maalumu”. Kitabu cha: [Ahkaam Al-Quran 2/418 Ch. ya Dar Al-Fikr].
Amepokea Imamu Bukhariy kutoka kwa Ally R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Ahadi ya Waislamu ni moja hutekelezwa na wachache wao, Mwislamu yeyote mwenye kuvunja ahadi laana ya Mwenyezi Mungu Malaika na watu wote ipo juu yake, na Mwenyezi Mungu hapokei chochote katika matendo yake”, basi inakuwaje kwetu kuvunja ahadi ya kiongozi mkuu!
Amepokea Imamu Bukhari katika kitabu chake kutoka kwa Abdillah Ibn amru R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mambo manne mtu anapokuwa nayo basi anakuwa ni mnafiki moja kwa moja, na mwenye kuwa na sehemu ya mambo hayo basi anakuwa na sehemu ya unafiki mpaka pale atakapoacha. Pindi anapo aminiwa anapoteza imani, anapo zungumza huongopa, anapo ahidi hatekelezi ahadi na pindi anapogombania kitu hufanya uovu”
Amepokea Al-Baihaqiy kutoka kwa Amr Ibn Al-Hamaq Al-Khazai kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Ikiwa mtu amejiaminisha mwenyewe kwa mtu kisha akamuua basi mimi nipo mbali na muuaji hata kama aliyeuliwa ni kafiri”.
Kutokana na hayo pande zote zinazohusika na makubaliano pamoja na mikataba ya kimataifa zipo katika hali ya amani na zinapaswa kuacha mapigano kwa mujibu wa makubaliano yao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye mwenye kusikia mwenye kujua} [AL ANFAAL, 61].
Jambo la Tatu: Yanayojumuishwa kwenye matumizi ya silaha hizi ni pamoja na mauaji. Imepokelewa na Abu Dawud na Hakim kutoka kwa Abu Huraira R.A, kuwa Mtume S.A.W, amesema: “Muumini hawezi kuua, imani huzui kuua”.
Pindi Khabib Al-Answar R.A. alipotekwa na washirikina na Khabib katika vita vya badri alikuwa amemuua Al-Harith Ibn Amir, siku moja Khabib alimchukuwa bint wa Al-Harith pindi alipokuja mama yake akamkuta binti yake amekaa na Khabib alichanganyikiwa kisha Khabib akamuuliza: “Vipi unaogopa kuwa nitamuua? Siwezi kufanya kitu kama hicho. Akasema binti wa Harithi: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu sijapata kumuona mateka mwema kama Khabib”, huyu Khabib Mwislamu akiwa mateka mikononi mwa maadui wake wakiwa wanapanga kumuua na akiwa karibu na umauti, pamoja na hayo pindi ulipowadia wakati wa majonzi kwa kuuliwa mtoto wao wanasamehe, kwa sababu maadili ya Mwislamu huwa hayana udanganyifu.
Jambo la Nne: Matumizi ya silaha hizi husababisha mauaji kwa wanawake na watoto. Imepokelewa Hadithi na Bukhari pamoja na Muslim kutoka kwa Abdillah Ibn Omar kuwa, mwanamke mmoja alikutwa ameuawa kwenye moja ya vita vya Mtume S.A.W, Mtume akakasirishwa na mauaji hayo ya huyo mwanawake na watoto. Katika mapokezi mengine: Mtume S.A.W, alikataza kuua wanawake na watoto wadogo. Amesema Imamu An-Nawawi: “Wamekubaliana wanachuoni wote kuifanyia kazi Hadithi hii, na uharamu wa kuua wanawake na watoto wadogo ikiwa hawajashiriki kwenye mapigano. Na ikiwa watashiriki, jopo la wanachuoni wamekubaliana kuwa watauliwa”. Kitabu cha [Sharhu Muslim 12/48 Ch. ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Jambo la Tano: Miongoni mwa madhara yanayosababishwa na silaha hizi angamizi ni mauaji ya Watu wakiwemo Waislamu waliomo ndani ya nchi husika wakiwa ni miongoni mwa wakazi wake wa asili au miongoni mwa wale waliohamia. Sharia takatifu imetukuza damu ya Mwislamu na kutishia vikali ikiwa itamwagwa au kuguswa pasi na haki, pale Aliposema Mola Mtukufu: {Na mwenye kumuua Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa} [AN NISAA, 93]. Na Akasema tena: {Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israil ya kwamba aliye muua mtu bila ya yeye kuua, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote} [AL MAIDAH, 32].
Hadithi iliyopokelewa na An-Nisaa'iy kutoka kwa Abdillah Ibn Amru R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Kuondoka kwa dunia ni kitu jepesi zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko kuua Mwislamu”. pia Ibn Maja na Umar R.A, amepokea Hadithi na amesema: Nimemuona Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akiwa anazunguka Kaaba na anasema: “Uzuri wako ulioje na harufu yako, ukubwa wako ulioje na utukufu wako, naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo mikononi mwake, utukufu wa Muumini ni katika utukufu mkubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko wewe, mali yake na damu yake, na tunatakiwa kumdhania mazuri”. Uhalifu wa kumuua Mwislamu kwa makusudi na kwa uadui ni uhalifu mkubwa kabisa, na hakuna uhalifu mwingine ulio mkubwa baada ya kukufuru kuliko uhalifu huo. Katika kukubalika kwa toba ya muuaji kuna tofauti kwa Masahaba na waliokuja baada yao.
Jambo la Sita: Kuna Matatizo yatakayojitokeza kwenye matumizi ya silaha hizi kwa Waislamu wote bali kwa ulimwengu kwa ujumla, kwa sababu nchi yenye kushambuliwa inaweza kurejesha mashambulizi hayo kwa kiwango sawa na walivyofanyiwa au zaidi ya walivyofanyiwa, na isitoshe, athari za maangamizi zinazotokana na baadhi ya silaha zinaweza kuvuka kutoka sehemu iliyoathirika na kuhamia sehemu nyingine kwa njia ya hewa, kwenda hata nchi zengine jirani zisizohusika. Uharibifu unaosababishwa na silaha hizi unaoweza kutokea papohapo na hata hapo baadaye ni mkubwa zaidi kuliko masilahi yake, na katika kanuni kuu za kisheria kuna ulazima wa kuepusha uharibifu na kutangulizwa masilahi ya Watu.
Jambo la Saba: Madhara yanayotokana na matumizi ya silaha angamizi ni pamoja na uharibifu wa mali za Watu binafsi na mali za umma, na uharibifu wa mali ni kuzipoteza ambao sharia imeuharamisha, na uharamu unaongezeka zaidi ikiwa mali hizo zilizoharibiwa si zenye kumilikiwa na muharibifu bali ni miliki ya mtu mwengine, kutokana na uharamishaji wa sharia imekataza kwa upande mmoja na haki za waja kwa upande mwengine.
Jambao la Nane: Kutumia silaha hizi katika baadhi ya sura zake zinalazimisha mtumiaji kuingia ndani ya nchi anayoikusudia, na hilo ni baada ya kukamilisha hatua rasmi zinazohitajika kuingia nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na nchi kukubali kuingia mtu huyo kwa sharti la kukubaliwa kuingia kutofanya uharibifu ndani ya nchi hiyo iliyompokea, na hili hata kama halijatamkwa wazi lakini linafahamika, na wanachuoni wa fiqhi wameutaja mfano wa hili. Amesema Imamu Al-Khiraqiy katika ufupisho wake: “Mwenye kuingia kwa amani kwenye nchi ya adui, hapaswi kuharibu mali zao”. Amesema Ibn Qudama akiwa mwenye kusherehesha ibara yake: “Ama kuwafanyia hiyana ni haramu, kwa sababu wao wamempa amani kwa sharti la kutowafanyia hiyana hata kama hilo litakuwa halijatajwa kwa tamko la wazi kwani ni lenye kufahamika, kwa sababu hiyo yeyote mwenye kutujia kwa amani basi hiyana yetu inakuwa ni kuvunja ahadi kwake, ikiwa litathibiti hili si halali kwake kufanyiwa hiyana kwa sababu hiyana ni uovu na katika Dini yetu uovu haufai” kitabu cha: [Al-Mughny 9/237 Ch. ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Ama maandiko ya kisharia na kifiqhi ambayo yamefanywa kuwa ndio tegemeo la kutangaza fikra hii yenye dhambi ni matamko yaliyovuliwa muundo wake na kuwa tofauti na sura yake, ambapo ndani yake kuna kuzipoteza tofauti zenye kuzingatiwa kati ya nyakati tofauti, kama vile tofauti kati ya wakati wa vita na wakati wa amani, kwani wakati wa vita una hukumu zake maalumu zenye kutafautiana na wakati wa amani ambapo huzuiwa umwagaji damu uharibifu wa mali pamoja na kuharibu heshima, tofauti hii ni yenye kuleta athari isiyoendana na matumizi ya silaha hizi kwa kile kilichoelezwa katika vitabu vya fiqhi ikiwa ni pamoja na kufaa kumshambulia adui na kufaa kutumia ngao na zenginezo ni katika masuala yaliyopokelewa kwenye fiqhi ya Kiislamu, kulinganisha silaha hizo na silaha za mangamizi ni kosa moja kwa moja, ikiwa masuala haya yaliyo nukululiwa ni masuala sahihi na yametoka sehemu yake iliyokusudiwa na wanasharia na hukumu zake ambazo zimepakuliwa, lakini ni kosa kabisa kuhamisha hukumu hii sahihi kutoka sehemu yake na eneo lake na kwenda sehemu iliyotofauti kwa sura yake na hukumu.
Kama vile haifai kulinganisha matumizi ya silaha hizi katika kushambulia adui na kumuua, ambapo inafahamika kuwa kuna tofauti kati ya hukumu ya kumuondoa adui na hukumu ya jihadi, miongoni mwa tofauti hizo ni kuwa: Adui kwa hatua ya kwanza huondolewa kwa njia iliyonyepesi zaidi, ikiwa ataondolewa kwa maneno basi inakuwa ni haramu kumuondoa kwa kumpiga, ikiwa itawezekana kumuondoa kwa mkono basi haifai kumshambulia kwa upanga na mfano wa hivyo, ambapo haikubaliani na matumizi ya silaha za maangamizi kwa sura iliyotajwa.
Dalili inayochukuliwa katika hili ni Hadithi nyingi zilizopokelewa na ambazo zinaonesha kuwa inafaa kutumia dhidi ya washirikina silaha kama vile urushaji mawe kwa kutumia manati au kuchoma moto, ama kipimo cha kutumia silaha za maangamizi kwa sura hii kwa kweli ni Kipimo batili, kwa kuwepo tofauti ya wazi na kubwa mno kati ya silaha hizo za aina mbili, na Hadithi hizi zimepokelewa zikielezea wakati wa vita, na kuna tofauti kati ya hukumu za wakati wa vita na wakati mwengine, kama vile kuna tofauti kubwa kwa upande wa athari kati ya silaha za kurusha mawe kwa kutumia manate na kati ya kutumia silaha za maangamizi, kwa sababu matumizi ya silaha za manate athari yake ni ndogo sana ukilinganisha athari za matumizi ya silaha za maangamizi zilizotajwa, kama vile uhalisia uliokuja katika Sunna ya Mtume S.A.W. unafundisha kuwa kukamilika kwake kuna kuwa chini ya amri ya kiongozi mkuu, ambapo ni tofauti ya wazi kati yake na kutoka amri nje ya kiongozi mkuu, na kupewa watu wa upande mmoja au kikundi haki ya kutangaza vita wao wenyewe tu ni kwenda kinyume na uma pamoja na viongozi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni jihadi. Vilevile Hadithi hizi usahihi wake ni katika uhalisia wa matukio na wala sio ujumla wake, na kwa sababu hii jopo la wanachuoni limekubaliana kuwa asili ni kutofaa uharibifu na uchomaji moto, kwa kutegemea maandiko ya Kitabu ambayo yanasifa ya ujumla.
Tunaona kuwa usahihi wa matumizi ya aina za silaha za maangamizi ambazo husababisha maangamizi kwa wote, ikiwa ni kufuata katazo la maandiko la uchomaji moto baada ya kuamrishwa kwanza na Mtume S.A.W, kisha akalikataza hilo kabla ya hata kufanyika, pamoja na kuwa ilikuwa wakati wa vita na akasema katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari kutoka kwa Abi Huraira R.A. kuwa: “Hakika moto hautumiki kwa adhabu isipokuwa na Mwenyezi Mungu”. Mtume S.A.W. amekataza kumchoma moto mtu kama adhabu. Inafahamika kuwa silaha za maangamizi husababisha moto mkubwa, na kilicho sahihi ni kuzuiliwa kwa Silaha hizo kutumika hata wakati wa vita kwa katazo la kuwaadhibu Watu kwa kuwachoma moto.
Ama kukutanisha masuala haya na masuala ya kumshambulia adui ni aina ya makosa, kwa sababu kufaa kulikopitishwa na wanachuoni katika masuala ya kushambulia adui kuna masharti yake. Na miongoni mwa masharti hayo: Ni kuwa wakati wa vita, na adui anayekusudiwa kushambuliwa awe ni adui anayeruhusiwa kumuua, tofauti na yule mwenye makubaliano kati yetu na yeye ya kuishi kwa amani, huyu haifai kumshambulia kwa kuwepo makubaliano kati yetu na yeye ya utulivu au majukumu au makubaliano na mikataba ya kimataifa, ambapo kila upande una jukumu la usalama kwa pande zengine, usalama wa nafsi, mali na heshima. Ikiwa hawa haifai kuwashambulia na mfano wa hao basi matumizi ya silaha hizi za maangamizi dhidi yao kuwa kwake haramu ni bora zaidi kuliko kuzitumia dhidi yao, ama masuala ya kujikinga kwa kufanya ngao na mfano wake ni kuwa haifai isipokuwa wakati wa vita kwa sharti na sura maalumu iliyoelezewa na wanasharia kwa kina zaidi. Rejea: Kitabu cha: [Al-Bahr Ar-Raaiq 5/80, kitabu cha Ibn Abideen 3/223, kitabu: Raudhat at-Twaalibeen 10/239, kitabu: Mughniy Al-Mihtaj 4/223, kitabu: Al-Mughniy cha Ibn Qudama 8/449, 10/386].
Kutokana na maelezo yaliyotangulia, tunasema kuwa wito huu ni katika miito batili, kutumia wito huu na kuueneza ni katika uhalifu mkubwa na uharibifu katika ardhi ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu Amekataza na kumuahidi mtendaji wake adhabu kali. Anasema Mola Mtukufu: {Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawataacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu} [AL-AHZAAB, 60]. Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini} [AL AARAF, 85]. Na anasema: {Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu? * Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao} [Muhammad, 22: 23].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Dkt. Ally Juma. Mufti wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.

 

Share this:

Related Fatwas