Kuchukua Hatua Wakati wa Uhai.
Question
Nina kaka mmoja na dada wanne, na baba yetu aliwaandikia watoto wawili wa kiume nusu ya mali zake alipokuwa hai, na akaacha nusu ya utajiri wake kwa watoto wake wawili wa kiume na wote wa kike, na nimemsikia Mufti –Mwenyezi Mungu Amuhifadhi– akitoa Fatwa kwamba kila mtu yuko huru kwa mali yake anayoimiliki, ana haki ya kumpa na kumuandikia yoyote amtakae awe wa karibu au wa mbali. Je? Alichokifanya baba yangu ni sahihi kisheria au sio sahihi? Je hakuna dhuluma hapo kwa watoto wa kike? Je hatua hii haipandikizi chuki na bughudha baina yao? Na wanarithishana uovu huu kizazi hadi kingine kama tunavyoshuhudia katika uhalisia wa maisha yetu tukaja kukuta machungu na majanga na huzuni baina ya watoto na wajukuu? Na je vipi kuhusu zawadi ya Nuumani R.A kwa mmoja wa watoto wake alipomzawadia bustani ambapo alitaka mke wake waandike mkataba akamtaka amfanye Mtume S.A.W, kuwa shahidi Mtume S.A.W, akamuuliza: Je umewapa watoto wengine waliobaki mfano wa hicho ulichompa huyo mtoto? Akasema: Hapana, akasema Mtume S.A.W, Mimi siwezi kuwa shahidi wa jambo lililokiukwa, mcheni Mwenyezi Mungu na mfanye uadilifu baina ya watoto wenu. Na je vipi kuhusu kauli ya Mtume S.A.W: Ukiwaacha warithi wako wakiwa wamejitosheleza ni bora kwako kuliko kuwaacha wakiwa mafukara wanawaomba omba watu? Na kauli ya Mtume S.A.W: Hakuna wasi wasi wowote kwa mrithi? Na hakika mimi nilikuwa ninadhani kuwa mtoto ambaye ni halali kumpendelea kuliko ndugu zake ni mtoto mlemavu, na mtoto aliyemsaidia baba yake katika kuuongeza utajiri wake, na yule ambaye hana uwezo wa kielimu kwa mfano akawa mtoto huyo ni mkulima, na kwamba kufanya hivyo ni kufuata Madhehebu ya Imamu Ahmad bin Hanbal tu kinyume na Wenye kujitahidi wengine katika wanachuoni. Je Ni ipi rai yenu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na watakaowafuata. Na baada ya utangulizo huo:
Kuwapa watoto zawadi zinazolingana ni katika mambo yanayotakiwa kisheria ambapo sheria ya Uislamu imeyasisitizia na kuamrisha yafanyiwe kazi, lakini katika hali ya Sunna na kupendeza sio kwa njia ya lazima na uwajibu. Mzazi anapowapa watoto wake zawadi yoyote, kisha akambagua mmoja wao kwa ziada ya zawadi hiyo zaidi ya wengine au akampa nafasi ya kuanza kwa kitu kinyume na wengine waliobakia katika ndugu zake, mzazi huyu anakuwa ni mwenye kuacha Sunna inayopendeza na hazingatiwi kama ameacha wajibu ambao mtu huandikiwa madhambi kwa kuuacha kwake. Na hivi ndivyo ionavyo Jamhuri ya Wanachuoni wa Madhehebu ya Hanafia, Maliki na Shafiy.
Imekuja katika kitabu cha: [Al Bahru Raaiq], miongoni mwa vitabu vya Wanachuoni wa Madhehebu ya Kihanafiy: inachukiza kuwapendelea baadhi ya watoto juu ya watoto wengine katika zawadi wanapokuwa wote na afya njema isipokuwa kwa kuongezeka fadhila za Dini.
Anasema Mwanachuoni Mkubwa Al Kharshiy katika kitabu cha: [Sharhu Mukhtaswar Khaliil Fiqhil Maalikiyah]: Ama zawadi ya Mzazi kwa baadhi ya watoto wake kwa kutoa chote alichonacho au sehemu kubwa ya kitu hicho ni jambo linalochukiza.
Ama kwa upande wa Wafuasi wa Madhehebu ya Kishafiy, Sheikh Zakariyal Answaariy, Sheikh wa Uislamu, anasema katika kitabu cha Asnaal Matwaalib: Inachukiza kwa mzazi na kwenda juu kiukoo (babu na baba yake na babu) kumpa yoyote kati ya watoto wake wawili zaidi ya mwingine hata kama ni mtoto wa kiume.
Haya yote ni maandiko yao yanayomaanisha ya kuwa usawa baina ya Mitume wote katika kutoa kwao ni katika mambo yanayopendeza na wala sio jumla ya mambo ya wajibu, na kwamba atakayempendelea yoyote kati ya watoto wake katika anavyowapa atakuwa amefanya jambo linalochukiza na wala hajafanya jambo lililoharamishwa..
Na jamhuri ya wanachuoni imetoa dalili juu ya waliowaunga mkono kwa dalili. Na miongoni mwazo ni: Hadithi iliyopokelewa na Bukharin na Muslim katika Vitabu vyao viwili vya Swahiihaini – na Tamko ni la Muslim – kutoka katika Hadithi ya Nuuman bin Bashiir – R.A: Baba yangu aliondoka na mimi akiwa amenibeba na kuelekea kwa Mtume S.A.W, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ninashuhudia kuwa mimi nimempa Nuumani katika mali yangu hii na ile. Akasema Mtume S.A.W: je umewagawia watoto wako wote kama ulivyomgawiya huyu Nuuman? Akasema: Hapana. Mtume S.A.W akasema: Basi mshuhudishe haya mtu mwingine. Kisha akasema: Je? Inakufurahisha wao wanapolingana katika kukufanyia wewe wema? Akasema: ndio. Akasema Mtume S.A.W: basi kwa hiyo hivyo sivyo. Kama alichokifanya Bashiiru kingelikuwa haramu basi Mtume S.A.W, asingemuamrisha amshuhudishe mtu mwingine; kwani Mtume S.A.W. haamrishi kufanya kilicho haramishwa.
Na wametoa dalili pia kwa maelezo yaliyokuja katika baadhi ya Mapokezi ya Hadithi ya Nuumani bin Bashiir kwa Muslim katika kitabu chake cha Swahiihu, na ndani yake kuna kauli ya Mtume S.A.W, akimwambia Bashiir: Je Inakufurahisha wewe watoto wako wote walingane katika kukutendea wema? Akasema Bashiir: Ndio. Na Mtume S.A.W, akasema: kama ni hivyo basi hapana.
Na katika Hadithi nyingine: Je umempa hivyo hivyo kila mtoto wako? Akasema: Hapana. Akasema: Je wewe hupendi wema wao kwako mfano wa utakavyo kwa huyo? Akasema: ndio. Mtume S.A.W. akasema: Hakika mimi siwi shahidi.
Kwa hivyo Mapokezi haya mawili ya Hadithi yanaonesha dalili ya kwamba amri ya kuwapa watoto zawadi zinazolingana ni amri ya jambo linalopendeza na wala sio Amri ya wajibu; kwa kufungamanisha hilo na kupatikana kwa wema kutoka kwa watoto kwenda kwa mzazi wao kwa usawa, na kulingana katika wema wakati sio wajibu kwa watoto bali ni Sunna kwao, ni kwa kuwa usawazishaji huu katika kutoa ni wajibu kwa wazazi bali ni Sunna' hii inamaanisha kuwa Mtume S.A.W, hakika mambo yalivyo, alikuwa anamzindua swahaba wake kuhusu jambo hili kwa kuchunga kilicho bora zaidi.
Na vile vile imepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahaba R.A, kwamba wao waliwapendelea baadhi ya watoto wao kinyume na wenngine; Abu Bakar alimpendelea zaidi Bi Aisha, na Omar alimpendelea zaidi mwanae Aaswim kwa baadhi ya vitu alivyompa, na Abdul Rahman bin Auf alimpendelea zaidi mtoto wa Ummu kulthuum, na inasemekana: alimpendelea zaidi binti yake kuliko Ummu kulthum kwa kumpa Dirham elfu nne na Ibn Omar alitoa vichwa vitatu au vine (vya mifugo) kwa mtoto wake kinyume na wengine.
Na ama yale yaliyokuja katika baadhi ya mapokezi ya Hadithi ya Nuumani bin Bashiir yaliyotajwa na Muulizaji ya kwamba Mtume S.A.W, alikataa kuwa shahidi wa zawadi ya Bashiir kwa mwanae na akamwambia: Mimi siwezi kuwa shahidi wa ukiukwaji huu. Hakuna dalili yoyote ya uwajibu wa kuwalinganisha watoto wote katika kuwapa zawadi; kwani uovu ni kumili katika kusudio. Na Usawa na Uadilifu, nayo kwa zingatio hili kunamaanisha kuchukiza kama ambavyo kunamaanisha kilichoharamishwa. Kwa hiyo kinachochukiza kinaepukana na Sunna za Kuwa sawa, na kinatoka katika Usawa, na kila kinachotoka katika Usawa basi kinakuwa kiovu, ni sawa sawa kiwe kitu hicho Haramu au kinachochukiza. Na kukusanya baina ya Dalili kunaainisha maana ya kuchukiza.
Ama kauli ya kwamba alichokifanya Baba katika uhalisia wake uliotajwa katika swali kwa kuwapendelea baadhi ya watoto wake wa kiume kwa zawadi, kunapelekea kupandikiza chuki na kero pamoja na bughudha baina ya watoto na kuuvunja undugu baina yao, na ni haramu pia, na hili limejengeka katika kauli ya kuzuia mianya, na jawabu lake ni: kuzuia zingatio la kuziba mianya, kama ilivyo katika Madhehebu ya Imamu Shafiy na wengine miongoni mwa Wanachuoni.
Vile vile haifai kuweka sababu; kwani kunatofautiana katika hali na sura nyingi; kuna uwezekano ikamtokea mtu na isimtokee mwingine, au hakitokei kitu kimsingi katika hali ambayo hakuna mtu yoyote asiye na kipaji aliyeiangalia, na hivyo ikawa mwenye kuharamishiwa sio aliyekusudiwa.
Na sahihi ni kuiita maana hii hekima na wala sio sababu, na Hukumu zinafungamana na sababu zake na wala hazifungamani na hekima zake.
Ama kuhusu kilichotajwa na Muulizaji kuhusu kauli ya Mtume S.A.W, kwa Saad bin Abuu waqaas R.A: Hakika yako wewe ikiwa utawaacha warithi wako wakiwa wanajitosheleza ni bora kwako kuliko kuwaacha wakiwa masikini wanawaomba omba watu kwa mikono yao. Na kauli yake: Hakuna wasia kwa mrithi; hakuna uhusiano wowote na mwenye jukumu; kwani Hadithi mbili ni za Wasia, na Picha ya Mwenyekuulizwa hapo ni ile inayohusiana na Zawadi wakati wa uhai wa mtu, na wakatengana, na wala hakuna yoyote anayejua nani atamrithi nani; na ni mara chache kijana akiwa katika ujana wake, akafa kabla ya mzazi wake aliyezeeka.
Na kilichotajwa na Muulizaji ya kwamba Mtoto ambaye inaruhusiwa kumtenganisha na ndugu zake (kwa kumpa zaidi) ni yule Mlemavu, na yule aliyemsaidia zaidi baba yake katika kukuza utajiri wake, na mtoto ambaye hakuwa na bahati katika masomo na anafanya kazi ya ukulima na kwamba yule aliyeruhusu kufanya hivyo ni Imamu Ahmad Bin Hanbal tu kinyume na Wanachuoni wengine waliobakia, hayo sio sahihi, bali hoja inayotegemewa katika Madhehebu ya Imamu Ahmad ni kwamba inazuiliwa kutenganisha watoto kiupendeleo kwa njia yoyote iwayo. Amesema Al Bahuutiy: na huo ndio uwazi wa Maneno ya Wenzake. Na akatoa Andiko katika Mapokezi ya Yusufu bin Musa yanayomuhusu Mtu mwenye Mtoto Mwema kwa wazazi wake na mwingine aliye kinyume na hivyo; hakuna kumpendelea zaidi mwema kinyume na mwingine asiye mwema. Mwisho.
Jamhuri ya Wanachuoni wa Fiqhi inaona kuwa hakuna ubaya wowote wa kumpendelea mtoto kati ya watoto wengine wa mtu, ikiwa ni kwa maana inayozingatiwa kwa mujibu wa umaalumu; kwa mnfano kama vile kumtenganisha mmoja wao kwa haja maalumu au kwa maradhi au kwa wingi wa watoto, au kwa kujishughulisha na elimu na mfano wa hayo. Na vile vile ikiwa mtoto ananyimwa kile kinachotolewa na mzazi kwa wenzake wengine, kutokana na kuwatendea vibaya wazazi wake au kutokana na uovu wake, basi hiyo haichukizi kumnyima huko.
Inasemwa katika kitabu cha: [Majmaul Anhaar] miongoni mwa vitabu vya Madhehebu ya Hanafi: Na ikiwa baadhi ya watoto wake watakuwa wanajishughulisha na masomo na sio kufanya kazi basi hapana ubaya wowote kuwapendelea kinyume cha wengine. Na kwa jibu la waliokuja baadae, ni kwamba hakuna ubaya wowote wa kumpa mtoto katika watoto wake mtu, aliye na elimu na mwenye adabu, na wala hampi miongoni mwao aliye mwovu na mchafu wa matendo. Mwisho. Na Abul Waliidl Baaji amenukulu kutoka kwa Utaibah kwamba Maliki aliulizwa kuhusu Mtu mwenye mtoto anayemtendea wema na akataka kumpa sehemu ya mali yake kinyume na wengine, akajibiwa: hakuna ubaya wowote kufanya hivyo.
Na hivi ndivyo walivyoamua Wanachuoni wa Fiqhi wa Madhehebu ya Shafi; amesema Mwanachuoni Mjuzi Alkhatwiibu katika Sharhul Minhaaj: Angalizo: Sehemu ya Chukizo la kusawazisha katika haja au kutokuwapo kwa haja, na kama sio hivyo basi hakuna chukizo lolote… na anatengwa Mlemavu na Mwovu ikiwa itajulikana kuwa mtoto huyo mwovu anazitumia fedha alizopewa katika maasi, basi haichukizi kumnyima fedha mtoto huyo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.