Kutoa Hongo kwa Ajili ya Mateka na Kufanya Mazungumzo na Wahalifu.
Question
Baadhi ya makundi ya wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa, na huenda yakawa makundi ya wahalifu ambao huitwa “Maharamia” hufanya kazi ya kuteka watu kwa lengo la kulipwa hongo, nini hukumu ya kufanya nao mazungumzo watekaji hawa na kulipa hongo ya kuwakomboa waliotekwa?
Answer
Shukrani zote za Mwenyezi Mungu peke yake, sala na salamu ziwe kwa yule ambaye hakuna utume tena baada yake naye ni Mtume wetu Muhammad pamoja na watu wake na Masahaba wake na wale wote wanaomfuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Watu hawa wanaotekwa nyara wanakuwa katika hukumu ya mateka, kwa sababu mara nyingi watekaji nyara huwa wanazitishia nchi na familia za mateka kuwauwa ikiwa hawatatekeleza matakwa yao, na hayo yametokea mara nyingi sana.
Hivyo nchi kisheria inatakiwa kuwakomboa mateka hawa kwa njia yoyote ile iliyo nyepesi, inaweza kuwa kwa njia ya mazungumzo, kubadilishana mateka, kurahisisha njia ya kutoroka au kwa kushambuliana. Vilevile inafaa kuwakomboa kwa kulipa fedha. Amesema Omar Ibn Al-Khatwab R.A: Kumkomboa Muislamu kutoka mikononi mwa makafiri ni jambo lenye kupendaza zaidi kwangu kuliko eneo zima la rasi ya Kiarabu [Angalia: Kitabu cha Ibn Abi Shaiba, 12/418, Ch. ya India].
Mtume S.A.W. ametoa amri ya kuwakomboa mateka, asili ya amri yake ni jambo la lazima kufanya hivyo, katika Hadithi inayopatikana katika kitabu cha sahihi Al-Bukhari kutoka kwa Abi Musa R.A. amesema: Amesema Mtume S.A.W: “Wakomboeni mateka, mlisheni mwenye njaa, mtembeleeni mgonjwa”.
Ibn Batwal amesema: “Kuwakomboa mateka ni jambo la faradhi ya kutoshelezana, kwa kauli yake Mtume S.A.W. “Wakomboeni m. Amri hii ni kwa wanachuoni wote, imepokelewa kutoka kwa Omar Ibn Al-Khatwab amesema: “Utekelezaji wa kukomboa mateka Waislamu ni jukumu la kitengo cha hazina ya nchi”.
Pia amesema Is-Haq: imepokelewa na Ibn Zubeir kuwa alimwuliza Hassan Ibn Ally kuhusu mateka gani anayekombolewa akasema: “Aliyetekwa kwenye ardhi ya mapigano”, imepokelewa na Ash-habu na Ibn Nafii kutoka kwa Malik kuwa aliuliza: “Hivi ni lazima kwa Waislamu kuwatolea fidia Waislamu wenzao waliotekwa? Akasema: Ndiyo, kwani haikuwa lazima kwa Waislamu kupigana mpaka wawakomboe!! basi ni vipi wasiwatolee fidia kwa mali zao?”
Na amesema Ahmad: “Watawalipia fidia kwa kuwaacha huru mateka wa maadui, ama fidia ya mali wala sifahamu” na kauli ya Mtume S.A.W. pale aliposema: “Wakomboeni mateka” ni jumla ya kila kinachotolewa kwenye fidia, hivyo haina maana kauli ya Ahmad, na amesema Omar Ibn Abdulaziz: “Ikiwa Waislamu watamkomboa mateka ambaye ni Dhimmiy, basi si halali kwa Waislamu kumrejesha kwenye ukafiri, warejeshewe fidia yao kwa kile watakachoweza kulipa”. Amesema Mwenyezi Mungu: {Na wakikujieni mateka mnawakomboa} [AL BAQARAH, 85]. [Sharhe ya Sahihi Al-Bukhari cha Ibn Batwal, 5/210, Ch. ya Maktabat ibn Rushd]
Hivyo tunasema: Ikiwa mali ya kumkomboa mateka ni mali haramu kupewa kafiri isipokuwa katika hali hii itakuwa ni halali kwa Muislamu kuitoa, hali hii inaondolewa kwenye kanuni inayosema: Kilichokuwa haramu kuchukuliwa na mchukuaji, basi ni haramu pia kwa mtoaji kukitoa, kama inavyozungumzwa katika vitabu vya kanuni, amesema Al-Zarkashy: “Kilichokuwa haramu kuchukua mchukuaji ni haramu kwa mtoaji kukitoa: Kama vile kufanya malipo ya nai zumari na rushwa kwa kiongozi ikiwa atatumia ili kuhukumu kinyume na haki, au kumkomboa mateka na kutoa kitu kwa kuhofia udanganyifu: {Na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji}[AL-BAQARAH, 220]. Kitabu cha: [Al-Manthur cha Zarkashiy, 3/140, Ch. ya Baraza la mambo ya Waislamu Kuweit].
Imepokelewa katika sira ya Mtume S.A.W. matendo yake tofauti ya kuwakomboa mateka Waislamu, miongoni mwa matendo hayo:
Ibn Hisham amesema: “Ameniambia mtu ninayemwamini kuwa Mtume S.A.W. amesema alipokuwa Madina: “Ni nani anaweza kuniletea Iyaash Ibn Abiy Rabiiah na Hishaam Ibn al-Aaswy? Waleed Ibn Waleed Ibn al-Mugheerah akasema: Ni mimi naweza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, akatoka kwenda Makkah akafika akiwa mwenye kujificha, akamuona mwanamke amebeba chakula akamuuliza: Unataka nini ewe mja wa Mwenyezi Mungu? Yule mwanamke akajibu: Ninawataka hawa mahabusu wawili – mateka wawili – akamfuata mpaka akafahamu walipo, walikuwa wamefungwa kwenye nyumba haina dali, ilipofika jioni aliruka ukuta na kuingia ndani kisha akachukuwa jiwe na kuwawekea chini ya vile walivyofungiwa navyo, akapiga kwa panga lake na kuvikata, kwa sababu hii panga lake lilikuwa linaitwa “panga la jiwe” kisha akawachukuwa na kuwapakia kwenye ngamia wake na kuondoka nao.... kisha akawafikisha kwa Mtume S.A.W huko Madinah” Sira ya Mtume kitabu cha: [Ibn Hisham, 1/476, Ch. ya Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiya].
Is-haq amesema: “Pindi ilipoteremka Qur`ani na amri hii, na faraja ya Mwenyezi Mungu kwa Waislamu ambapo hawakuwa na huruma Mtume alikamata mateka wawili wakati ambapo makuraishi walituma ujumbe kuleta fidia ili wakambolewe Othman na Hakam Ibn Kaisani, ndipo Mtume S.A.W. akasema hatutochukua fidia kwa ajili yao mpaka mtupatie watu wetu - kwa maana ya Saad Ibn Abi Wiqas na Otba Ibn Ghazawan - kwani sisi tunakuogopeni juu ya hawa ikiwa mtawaua, basi na sisi tutaua watu wenu, ndipo wakatolewa Saad na Otba na Mtume akawaachia huru mateka wao”. Kitabu cha: [Al-Bidaya wa Al-Nihaya cha Ibn Kathiir, 3/250, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Kwa mujibu wa tuliyoyasema mitazamo ya wanachuoni ni kama ifuatavyo:
Ibn Qudama amesema: Ni lazima kuwakomboa mateka Waislamu pindi linapowezekana hilo, katika hili amesema Omar Ibn Abdilaziz, Malik na Is-haq, na imepokelewa na Ibn Zubeir kuwa alimwuliza Hassan Ibn Ally kuhusu ni mateka gani anakombolewa? Akasema: Aliyetekwa kwenye ardhi ya mapigano, imethibiti kuwa Mtume S.A.W amesema: “Mlisheni mwenye njaa, tembeleeni mgonjwa, komboeni mateka”. Na imepokelewa na Said kwa upokezi wake kutoka kwa Hibban Ibn Abi Jabalah, kuwa Mtume S.A.W amesema: “Ni jukumu la Waislamu katika fidia zao kuwakomboa mateka wao, na kuwapa fidia mahasimu wao”.
Imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kuwa aliandika makubaliano kati ya wahamiaji wa mji wa Madinah na wenyeji kulinda maeneo yao na kuwakomboa mateka wao kwa njia nzuri, na Mtume aliwakomboa Waislamu wawili kwa mtu mmoja ambaye alimteka kutoka katika kabila la Aqil, na alimkomboa mwanamke mmoja na kumkabidhi kwa Salama Ibn Al-Ak-waa kwa fidia ya watu wawili. Kitabu cha: [Al-Mughniy, 9/284, Ch. ya Maktabat Al-Kahira].
Shiraziy amesema: “Inafaa kukubaliana utulivu kwa mali inayochukuliwa kwao kwa sababu katika hilo kuna masilahi kwa Waislamu, wala haifai mali kupelekwa kwa makafiri pasipokuwa na dharura, kwa sababu katika hilo kunaleta madhara kwa Uislamu hivyo haifai pasi na kuwepo kwa dharura, ikiwa kutakuwa na dharura ya hilo kama makafiri kuwazingira Waislamu na wakahofia mgongano au kutekwa Mwislamu na kupata matesa basi katika hali inafaa kutumika mali ili kuwaokoa.
Kwa mapokezi ya Abi Huraira R.A. kuwa “Haarith Ibn Omar Al-Ghatafany kiongozi wa Ghatafany alisema kumwambia Mtume S.A.W.: Ikiwa utanipa sehemu Madina kinyume na hivyo nitakujazia humo farasi na wapiganaji, Mtume S.A.W. akasema mpaka niwashauri wakina Saad – kwa maana ya Saad Ibn Muadh na Saad Ibn Ibada pamoja na As-ad Ibn Zurarah – wakasema: Ikiwa amri hii kutoka mbinguni basi watapewa kwa amri ya Mwenyezi Mungu, ikiwa ni rai yako basi rai yetu inafuata rai yako, lakini kama si amri kutoka mbinguni na wala si rai yako basi tunaapa kwa Mwenyezi Mungu katika zama za ujinga hatukuwa tukiwapa hata kokwa ya tende isipokuwa kwa kununua, ni vipi hali ya kuwa Mwenyezi Mungu ametupa nguvu kupitia kwako hawatopewa chochote” kama isingekuwa katika hali ya dharura isingefaa kurudi kwa wanyeji “Ansar” ili walipie ikiwa wataona hivyo, kwa vile hofu ni kutokea mgongano na mateso kwa mateka ni katika dharura kubwa sana ya kutumika mali, inafaa kuondoa madhara makubwa zaidi kwa kuacha madhara madogo. Je inafaa kutumia mali?
Kuna mitazamo miwili, kutokana na mitazamo hiyo miwili kuna ulazima wa mtu kujilipia mwenyewe na tumeshaeleza, ikiwa si kwa sababu hiyo ikatolewa mali na kupewa makafiri basi hawana haki ya kuimiliki kwa sababu ni mali iliyochukuliwa kinyume na haki ni sawa na mali iliyochukuliwa kwa nguvu”. Kitabu cha: [Al-Muadhab cha Shiraziy 2/260, Ch. ya Isa Al-Halabiy].
Sheikh Zakariya Al-Answariy amesema katika sharhe ya Al-Minhaj: “Ikiwa wamemteka Muislamu hata kama hawakuingia kweye nchi ya Kiislamu kwa kuwa kwao karibu na sisi kama tunavyolazimika wakiwa wameingia kwenye nchi yetu kuwalipa kwa sababu heshima ya Muislamu ni kubwa kuliko heshima ya nchi, ikiwa wataingia katika nchi yao na wala haikuwezekana kuwawahi kwa haraka tutawaacha huko kwa dharura”. Kitabu cha: [Fat-h Al-Wahab kwa sherhe ya Minhaj, 2/209, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Sheikh Saleh Ibn Abdilsameei Al-Aabiy Al-Azhariy Amesema: “Inafaa kwa kiongozi au makamu wake tu kusimamia makubaliano ya utulivu kwa maana ya suluhu ya kivita kwa kuacha mapigano kwa muda, ikiwa kuna masilahi katika hilo yataainishwa na kama hakuna, basi hatua hiyo itazuiliwa, akataja kwa mujibu wa anuwani ya suluhu au makubaliano ya sharti baya kama vile sharti la kubakia mateka Muislamu mikononi mwao au kutolewa hukumu kati ya Mwislamu na kafiri kwa hukumu zao basi hukumu hiyo hafai, hii ikiwa tofauti na mali bali ikiwa kwa mali makafiri ndio wataitoa kumpa kiongozi kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Basi musiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda} [MUHAMAD, 35].
Al-Mazry: Kiongozi wa kivita hatatafuta utulivu kwa kutoa mali kwa sababu hilo ni kinyume na maslahi halali ya kutoa malipo kwao isipokuwa kwa hali ya dharura ili kumalizana nao kwa kuhofia kuwateka Waislamu, Mtume S.A.W. alishauri pindi makabila yalipowazingira Saad Ibn Muadh na Saad Ibn Ibada washirikina wapewe theluthi ya matunda kwa sababu ya kuogopa wenyeji “Answar” wakazidiwa na vita na wakasema hao wawili: Ikiwa amri hii imetoka kwa Mwenyezi Mungu, basi tumesikia na tunaitekeleza, ikiwa ni rai tu basi katika zama za ujinga hawakuwahi kula hata tende moja isipokuwa kwa kununua, ni vipi leo hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Ametupa nguvu kwa Uislamu, basi Mtume S.A.W. alipoona dhamira yao ni kupigana akaacha, lau kama isingekuwa inafaa kutoa wakati wa dharura basi Mtume asingeshauri hivi, isipokuwa alishauri hivyo kwa kuhofia madhara zaidi kuliko sharti hovu kama vile wangeweza kuwateka Waislamu”. Kitabu cha: [Jawahir Al-Ikliil sherhe fupi 2/269 Ch. ya Al-Maktaba Al-Thaqafiya – Beirut].
Amesema As-Sarkhasiy: “Ikiwa washirikina wameingia kwenye nchi ya Kiislamu wakachukua mali vizazi na wanawake, kisha wakafahamika na kundi la Waislamu na wakawa ni wenye nguvu kwa Waislamu, basi ni lazima kwa Waislamu kuwafuata madamu wamo ndani ya nchi ya Kiislamu, kwa sababu Waislamu wanaweza kuishi kwenye nchi ya Kiislamu kwa kusaidiana kupata ushindi, katika hali ya kuacha kusaidiana ni kutoa nafasi ya kujitokeza adui ambapo si halali hilo kwao, watu wa vita kufanya hivi ni jambo la kupingwa na ovu, na kukemea ovu ni jambo la lazima kwa Waislamu, wale ambao wenye kufanyiwa hivyo ni wenye kudhulumiwa na anatakiwa Muislamu kuondoa dhuluma kwa mwenye kudhulumiwa na kumwondoa dhalimu kama alivyosema Mtume S.A.W.:
Ikiwa waliopo mikononi mwa makafiri ni kizazi cha Waislamu, basi ni lazima kwa Waislamu kuwafuatilia ikiwa wengi wao wanaona wana nguvu ya kuokoa kizazi kilichokuwa mikononi mwa makafiri ikiwa watawawahi kabla ya kuingia kwenye ngome zao, kwa sababu hawakuwapata kizazi cha Waislamu ndani ya nchi ya kivita, ili kuwa kwao mikononi mwao ndani ya nchi ya vita kuwe ni sawa sawa na nchi ya Kiislamu, kinachozingatiwa ni uwezekano wa Waislamu kufanyiwa uadilifu na wao,na hilo linazingatiwa kwa vile bado hawajaingia kwenye ngome zao, ama ikiwa wataingia kwenye ngome yao basi ikiwa Waislamu watakuja na kuweza kupigana nao ili kuokoa kizazi cha Kiislamu kilichotekwa hilo ni bora kufanywa, ikiwa watawaacha kwa kusubiria kuwa na nafasi lililowazi ni kuwa baada ya kufika kwenye maeneo yao na kuingia kwenye ngome yao Waislamu watashindwa kuwaokoa mikononi mwa makafiri, isipokuwa kwa kutumia juhudi kubwa zaidi na kujitoa sana kwa nafsi na mali katika hilo, ikiwa watafanya hivyo basi hiyo ndiyo dhamira.
Na ikiwa wataacha ili kukinga nafsi zao na taabu pamoja na matatizo hilo kwao linakuwa ni ruhusa, hivi hatuoni kuwa sisi tunafahamu mikononi mwa makafiri wa Roma na India kuna baadhi ya mateka Waislamu, na wala si lazima kwa yeyote miongoni mwetu kutoka ili kupigana nao kwa lengo la kuwaokoa mateka Waislamu waliopo mikononi mwao”. Kitabu cha: [Sharhe As-Sair Al-Kabiir, 1/207, Ch. ya Shirika la Mashariki la Matangazo].
Kutokana na maelezo yaliyotangulia ni lazima kuwakomboa mateka kadiri inavyowezekana kwa njia yeyote halali inayowezekana, hata kama italazimisha kuwatolea mali, ama wakiwa ni watu wa amani kama vile kutekwa mabalozi na wanadiplomasia wasiokuwa Waislamu vilevile inapaswa kulipiwa na kukombolewa, na tumezungumza usalama wao kwenye Fatwa iliyopita kwa anuwani: (Viza ya kuingia).
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.