Kumwondoa Mporaji
Question
Nini hukumu ya Sheria katika hali ya afisa wa polisi kulinda kituo cha polisi wakati wa kuvamiwa na yule anayekusudia kumwua afisa wa polisi, watu, kutorosha mahabusu, kuiba silaha za moto kituoni, kuchoma moto nyaraka, mafaili na madaftari?
Na ipi hukumu ya Kisheria kwa yule aliyejeruhiwa au kuuwawa na washambuliaji wa kituo kwa kupigwa risasi ya moto kwa kutumia silaha ya hapo kituoni au silaha binafsi ya wavamizi?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Masuala haya huitwa kwenye vitabu vya Fiqhi “Kumwondoa mporaji mtenza nguvu kwa silaha”.
Mporaji katika lugha: Ni yule ambaye humshinda mwenzake kwa kumtenza nguvu. [Kitabu cha Mukhtar As-Sahah].
Na maana ya Kisheria haipo mbali sana na ile maana ya kilugha, mwanachuoni Shams Ad-din Ar-Ramly amesema katika kitabu cha: [Nihayat Al-Muhtaj 8/23, Ch. ya Dar Al-Fikr]: Mporaji ni yule mwenye kumtenza nguvu mwenzake kwa kutumia silaha.
Asili katika Sheria ya kumwondoa mporaji ni kumwondoa kwa kutumia kilicho chepesi kadiri itakavyowezekana, ikiwa itawezekana kumwondoa kwa maneno laini - kama vile kumpa mawaidha - au kutumia maneno makali - kama kutishia - au kutaka msaada kwa watu - basi itakuwa haramu kumpiga, ikiwezekana kumwondoa kwa kumpiga kwa mkono ni haramu kumchapa. mijeledi, au ikiwezekana kumwondoa kwa mjeredi, basi haifai kutumia fimbo, ikiwa itawezekana kumwondoa kwa kutumia mabomu ya machozi, basi haifa kutumia risasi za plastiki, ikiwa itawezekana kumwondoa kwa risasi za plastiki haifai kutumia risasi za moto, ikiwa itawezekana kumwondoa kwa kumjeruhi mguuni, basi haifai kumpiga sehemu inatakayopelekea kifo au kumpiga usoni kwake, na mfano wa hayo, kwa sababu kumwondoa huko hakufai isipokuwa katika hali ya dharura, na wala hakuna dharura nzito panapokuwepo uwezekano wa kufikia makusudio kwa njia nyepesi, kwa sababu kanuni inasema chenye kuhalalishwa kwa dharura hukadiriwa kwa kiwango chake. [Kitabu cha: Al-Manthur cha Zarkashiy, 2/321, Ch. ya Wizara ya Waqfu nchini Kuweit]
Kwa maelezo hayo ikiwa atajikinga na shari ya huyu mporaji wa kutumia silaha kwa kitu chingine kama vile kumtupia kwenye maji au shimoni au kwenye moto au kumvunja mguu wake au kukawa kati yao uzio wa ukuta au visivyokuwa hivyo, basi hapaswi kumpiga, ikiwa atampiga pigo likamwumiza hapo atakuwa amejitosheleza na shari yake, kwa sababu kinachozidia zaidi ya kile cha kumwondoa hakihitajiki na wala hapaswi kukifanya.
Cha kuzingatiwa katika kumwondoa huko ni kuwa na uhakika kwa huyu atakayeporwa kuwa huyo mtu anataka kweli kumpora, haitoshi kwa kudhania au kwa kumletea shaka, hivyo haifai kuepuka utaratibu uliotajwa, au kubadilisha na kutumia nguvu kubwa zaidi hali ya kuwa kuna uwezekano wa kutumia nguvu nyepesi.
Dalili ya hayo ni kauli ya Mola: {Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni} [AL BAQARAH, 194]. Sura ya dalili ipo wazi ikiwa ni uhalali wa kujibu uadui kwa mwenye kufanya uadui, na kwa Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mtetee ndugu yako akiwa ni mwenye kudhulumu au kudhulumiwa, Masahaba wakauliza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu huyu tunamtetea kwa sababu ni mwenye kudhulumiwa ni vipi tunamtetea mwenye kudhulumu? Akasema: unamshika mkono” sura ya dalili ni kuwa: Huyu mporaji wa kutenza nguvu kwa kutumia silaha ni mwenye kudhulumu, hivyo huzuiwa kufanya vitendo vya dhuluma, kwa sababu katika hilo ni kumsaidia kama ilivyokuja kwenye Hadithi iliyotajwa, ikiwa kumwondoa huko kutafaa kwa mtu mwengine, basi kwa mtu mwenyewe ni bora zaidi, vilevile Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim na Imamu Bukhari kutoka kwa Ibn Umar R.A. hakika Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kuuwawa kwa ajili ya mali yake anakufa shahidi” na imepokelewa na Abu Dawud kutoka kwa Saad Ibn Zaid R.A. hakika ya Mtume S.A.W amesema: “Mwenye kuuwawa kwa ajili ya damu yake anakufa shahidi, na mwenye kuuwawa kwa ajili ya mali yake anakufa shahidi, mwenye kuuwawa kwa ajili ya familia yake anakufa shahidi” dalili ni kuwa: Pindi alipomjaalia akifa anakufa shahidi imeonesha kuwa anaweza kujitetea na kuuwawa, kama vile mwenye kuuliwa na watu wa vita amekuwa shahidi pia aliweza kujitetea na hata kuuwawa.
Kwa sura tuliyotaja kumekuwa na kauli za madhehebu ya watu wa elimu: Imamu Zailii amesema katika watu wa Hanafi katika kitabu cha: [Al-Haqaiq ambacho ni sherehe ya Kanz Adaqaiq”, 6/111, Ch. ya Al-Amiriya]: “Mwenye kuvamiwa na mtu mwingine wakati wa usiku na akaiba akamfuatilia na mwishowe akamwua, basi hana kosa lolote” kwa dalili ya kauli ya Mtume S.A.W.: “Kuuwawa kwa ajili ya kumiliki” maana yake: Kwa ajili ya kuwa mmiliki, ikiwa atafahamu kuwa ikiwa atapiga kelele atapata mali pamoja na hivyo akamwuwa anapaswa kufanyiwa kisasi, kwa sababu amemwuwa kinyume na haki, naye anakuwa sehemu ya mwenye kuporwa ikiwa mporaji atauwawa, ambapo anapaswa kufanyiwa kisasi, kwa sababu alikuwa na uwezo wa kumwondoa kwa kutaka msaada kwa Waislamu na kwenye mahakama, wala haitadondoka damu yake tofauti na mwizi ambaye haondolewi kwa kupiga kelele”.
Amesema mwanachuoni Al-Kharshy mtu wa Malik katika sharhe yake ya kitabu cha: [Mukhtasar Khalil, 8/112, Ch. ya Dar Al-Fikr]: “Mporaji wa kutumia silaha ni sawa sawa ametumwa au hajatumwa ikiwa atapora nafsi au mali, basi ni halali kumwondoa katika hilo baada ya kuonywa ikiwa anafahamu, kwa kumwambia, ninakuonya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mara tatu, ikiwa si mwenye kuelewa kama vile mnyama, basi anaondolewa pasi na kuonywa, na anaondolewa kwa jambo jepesi zaidi, ikiwa itapelekea kuuwawa, basi atauwawa, na hukubalika kauli yake kwa kiapo ikiwa hapakuwepo watu wakati wa tukio, jambo la wazi ni kuwa kuonya ni jambo linalopendekezwa, kama ilivyokuja kwenye kitabu cha [Munashadat Al-Maharib]”.
Imekuja katika kitabu cha: [Al-Minhaj” na sharhe yake ya [Mughniy Al-Muhtaj cha Sheikh Al-Khatib Al-Sharbiny miongoni mwa watu wa Shafiy, 5/530, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Na huondolewa mporaji wa kutumia silaha kwa njia chepesi zaidi ikiwa itawezekana, la kuzingatiwa ni dhana sahihi ikiwa itawezekana kumwondoa kwa maneno au kutaka msaada kwa watu, basi inakuwa haifai kumpiga, kwa maana kumwondoa kwa kumpiga au ikawezekana kumwondoa kwa kumpiga kwa mkono, basi haifai kumwondoa kwa kumchapa mijeledi, au kiwezekana kumwondoa kwa mijeledi hivyo haifai kumwondoa kwa kumchapa na fimbo, au ikiwezekana kumwondoa kwa kumkata kiungo cha mwili wake inakuwa haifai kumwua, kwa sababu hilo limepitishwa katika hali ya dharura, na wala hakuna dharura kwa jambo zito zaidi ikiwa uwezekano wa kufikiwa makusudio upo kwa njia nyepesi, ikiwa shari yake itaondolewa - kama vile kusukumiwa kwenye maji au kwenye moto au kuvunjwa mguu wake au kukawa na uzio wa ukuta kati yao au handaki - basi asimpige, kama ilivyoelezewa kwenye kitabu cha: [Ar-Rawdha], na faida ya utaratibu uliotajwa ni kuwa wakati wowote mtu anapokwenda kinyume na kubadilisha kufanya kubwa zaidi hali ya kuwa uwezekano wa kujitosheleza na kilicho chepesi zaidi, basi aliyetendewa anakuwa na utetezi.
Imamu Ibn Qudama amesema katika watu wa Imamu Hanbaliy kwenye kitabu cha: [Al-Kafiy”, 4/112 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Na huondolewa mporaji kwa njia nyepesi zaidi itakayowezena kutumika, ikiwa itawezekana kumwondoa kwa mkono, basi haifai kumpiga kwa fimbo, ikiwa ataondolewa kwa fimbo, basi haifai kumpiga kwa chuma, ikiwa itawezekana kumwondoa kwa kumkata kiungu cha mwili, basi haifai kumwua, ikiwa haiwezekani kumwondoa isipokuwa kwa kumwua, basi atamwua pasina kutetewa huyu mporaji kwa sababu ameuwawa kwa haki, ikiwa mwondoaji mporaji ataua, basi mporaji anakufa shahidi, na anapata utetezi kwa mujibu wa Hadithi, kwa sababu amemwua hali ya kuwa ni mwenye kudhulumiwa, hivyo imefanana na ikiwa atamwua tofauti na kumwondoa kwenye uporaji, ikiwa itawezekana kumwondoa pasi na kumkata kitu chochote, basi kumkata kiungo anatetewa, ikiwa itawezekana kumwondoa kwa kumkata kiungo lakini akamwua au kukata zaidi ya kinachoweza kumwondoa pia mporaji anapata utetezi, kwa sababu amefanyiwa uhalifu kinyume na haki, na mtendaji anakuwa ni mhalifu, na anazuiliwa kufanya huo uhalifu, kilichohalalishwa kile kinachoweza kuondoa shari zake, kinyume na hivyo anabakia kuwa ni mwenye kuzuiliwa, ikiwa atampiga na kumjeruhi, basi haifai kupigwa sehemu nyengine kwa sababu imetosha kuondoa kero yake na ndio jambo linalokusudiwa, ikiwa atamkata mkono wake akampiga kisha akamkata mguu wake, basi mguu wake utatetewa kwa sababu ameukata kinyume na haki, pasi na kutetewa mkono, kwa sababu umekatwa kwa njia ya haki, ikiwa atakufa mmoja wao hakuna kisasi cha nafsi kwa sababu ni katika halali na haramu, na itatetewa nusu ya malipo yake ya dia”.
Hakuna shaka kuwa mwenye kuvamia kituo cha polisi akiwa ni mwenye kukusudia kufanya vitendo vya uhalifu ambavyo vimetajwa kwenye swali ikiwa ni pamoja na kukusudia kuua maafisa polisi, watu, kutorosha mahabusu, kuiba silaha za moto, kuchoma moto nyaraka zote, mafaili na madaftari yaliyopo kituoni, basi huyo ni mhalifu mwenye kukiuka na kupata dhambi na anahukumiwa Kisheria ni mporaji wa kutumia nguvu ya silaha, na kutakiwa polisi waliopo kituoni kupambana na hawa wahalifu na kuwatisha kwa hatua zinazotakiwa katika kumuondoa mporaji wa kutumia silaha, ama mwenye kujeruhiwa miongoni mwa askari polisi au akauawa kwa silaha ya wahalifu, basi askari huyo hazingatiwi hata mara moja kuwa ni mwovu bali ni mwenye kutekeleza wajibu wa kazi unaotakiwa Kisheria na kisheria, ama ikiwa ni kujeruhiwa kupitia silaha za wenzake kwa njia ya makosa, basi hana dhambi kwa mwenye kukosea, lakini kiwango cha utetezi kinatofautiana kwa tofauti ya jeraha na sehemu yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi