Hijabu ya Mke Ambaye ni Katika Watu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hijabu ya Mke Ambaye ni Katika Watu wa Kitabu.

Question

Je! Mume muislamu anapaswa kumuamuru mkewe ambaye ni miongoni mwa watu wa kitabu kuvaa hijabu? 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na swala na salaam ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya aali zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo
Suala hili katika asili yake hutegemea suala linalojulikana, ambalo ni: "Kumkalifisha mtu ambaye sio Muislamu atekeleze Matawi ya kifiqhi", na suala hili lina madhehebu matatu kufuatana na rai inayojulikana, na Al-Isnawi alilifupisha katika kitabu chake cha: [Al-Tamhiid Uk. 126, Ch. ya Muasastu Al-Risala] kwa kusema: “Je, Makafiri wanakalifishwa kutekeleza matawi ya Sharia? Kuna madhahebu katika suala hili; iliyo sahihi zaidi ni ndiyo. Al-Isnawiy alisema katika kitabu chake cha: [Al-Burhaan]: hiyo ni dhahiri ya madhehebu ya Imam Al-Shafiy. Kwa hivyo, anakalifishwa kwa kufanya jambo la wajibu na kuacha jambo la haramu, na kuamini mambo yaliyopendekezwa, yanayochukiza, na yanayoruhusiwa. Madhehebu ya pili: hapana, na rai hii ilichaguliwa na Abu Ishaq Al-Isfaraiiniy, na madhehebu ya tatu ni: kwamba watu wa kitabu wanakalifishwa kwa marufuku tu, siyo maagizo.
Lakini, wanavyuoni wengi wa Fiqhi kwenye vitabu vya Matawi hawakuelezea kuwa watu hawa wasio waislamu wanatakiwa kufanya vitendo hivi vya ibada, na Imam Al-Nawawi aliondoa dhahiri ya upinzani huu katika vitabu vya Misingi na matawi miongoni mwake ni kitabu cha: [Al-Majmuu'] kwa kusema kuwa [3/5, Ch. ya Al-Muniriyah]:
“Kuhusu makafiri, wenzetu walikubaliana katika vitabu vya matawi kwambasi wajibu kuswali, wala kutoa zaka, wala kufunga, wala kuhiji na matawi mengine ya Uislamu. Kuhusu vitabu vya Msingi, wanavyuoni wao walisema:
Mtu wa kitabu anaelekezwa katika kutekeleza Matawi, kama anavyoelekezwa katika asili ya imani, na ikasemwa: Hashughulikiwi kwa matawi, na ilisemwa: hushughulikiwa kwa yaliyokatazwa, kama vile kuharamisha uzinzi, wizi, mvinyo, riba, na mengineyo, pasipo na mambo yanayowajibika kama Swala. Mtazamo ulio sahihi ni wa kwanza, usiopinga mitazamo yao katika matawi; kwani iliyokusudiwa hapa siyo kama iliyokusudiwa pale, katika vitabu vya matawi ya kifiqhi: hawatakiwi mambo yanayowajibika duniani pamoja na ukafiri wao.
Lakini kama mmoja wao akiingia Uislamu hatakiwi kufanya mambo yaliyopita, na hawakutaja adhabu ya Akhera kwake. Makusudi yao katika vitabu vya misingi ya kifiqhi kwamba: wanaadhibiwa kwa mambo hayo katika Akhera, licha ya adhabu ya ukafiri, wanaadhibiwa kwa hivi vyote pamoja na adhabu ya ukafiri pia, si kwa ukafiri peke yake, wanavyuoni hawakutaja hukumu ya mambo yanayowajibika duniani, walitaja katika vitabu vya misingi ya kifiqhi hukumu ya kipande kimoja, na katika vitabu vya matawi walitaja hukumu ya kipande kingine, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi”.
Labda sababu ya uhaba wa kunukuu katika tawi hili ni tabia ya adabu kwa ujumla kwa kuzingatia Sharia Tukufu, pamoja na kuanzishwa kwa mfumo wa hesabu, na kuenea kwa maadili ya hali ya juu. Jambo dhahiri ni kwamba hijabu ya mwanamke hiyo iliongezeka siku baada ya siku, kama ilivyopokelewa katika kitabu cha: [Sahih Al-Bukhari, Na. 318] kutoka kwa Hafsah bint Sirin ambaye alisema:
Tulikuwa tukiwazuia wajakazi wetu wasitoke siku ya Eid, basi mwanamke alifika kasri ya Bani Khalaf nikamjia, akasema kwamba mume wa dada yake amepigana vita pamoja na Mtume S.A.W. vita kumi na mbili, dada yake alikuwa pamoja naye katika vita sita. Akasema: Tulikuwa tunahudumia wagonjwa na kuwatibu waliojeruhiwa, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu ana aibu akiwa hana mavazi ya kutokea ili kushuhudia Swala ya Eid. Alisema: “Rafiki yake amvishe mavazi yake, washuhudie mema na kuomba dua ya waumini.” Kwa athari hii, tunaona kwamba ilitokea katika enzi ya Tabiina, kuzuia wajakazi kutoka kwa ajili ya Swala ya Eid hizo mbili, hata ingawa hali hii ilikuwa kinyume na hali iliyokuwa katika enzi ya kwanza.
Lakini, imepokewa kwa Said bin Abi Said alimwambia kaka yake, Hassan Al-Basri: Hakika wanawake wa Waajemi hufunua vifua vyao na vichwa vyao! Alisema: Yaepushe macho yako na wao [Al-Bukhariy (5/2299)], na hii ni dalili ya kwamba hali hii ilikuwepo katika enzi ya Maulamaa waliotangulia bila ya kukanusha.
Lakini neno "Wanawake wa Waajemi" halimaanishi wanawake wa Kitabu, au wanawake wamajusi na wanawake wa kitabu kwa pamoja. Badala yake, inawezekana kuwa wanaokusudiwa ni wanawake wamajusi tu sio wanawake wa Kitabu, hata ikiwa neno hilo lina maana ya ujumla, lakini hakuna matini maalumu zinazomaanisha kuwa miongoni mwao hao waliokuwa wake wa Waislamu, lakini kwa hali yoyote maana ya sentensi hii inawezekana ni kwa wote. Ikiwa hatuwezi kutoa dalili kwamba inaruhusiwa kwa mume kumwacha mke wake ambaye ni wa Kitabu bila hijabu kufuatana na uwezekano wa hapo awali, lakini tunaweza kusema kuwa inaruhusiwa kumwacha kwa mwenye madaraka naye, na kuhumu ya mume hupimwa kwake katika usimamizi na uangalizi katika hali zote hizi mbili.
Licha ya hivyo, Muislamu anaruhusiwa kumwoa mjakazi - kulingana na masharti ya kisharia yaliyotajwa katika sura yake - na inajulikana kuwa uchi wa mjakazi ni tofauti na uchi wa mwanamke huru, kwa hivyo hii ilionesha kuwa amri ya hijabu inapaswa kutilewa kulingana na hali ya mke, na sio kulingana na hali ya mume.
Wanavyuoni wengi wamesema kwamba mume haamzuii mkewe kutokana na kile alichopewa katika dini yake, isipokuwa kwamba kitu hicho kinachoruhusiwa katika dini yake kinamzuia mume kumaliza haki ya starehe, ambayo ni haki yake kwa mujibu wa mkataba ambao mahari ililipwa kwa ajili ya kupata haki ya starehe, lakini mume humzuia kwa yale yaliyokatazwa katika dini yake, kama vile kumzuia mkewe myahudi kula nguruwe sio mkewe mkristo.
Al-Dusuqiy alisema katika maelezo yake ya ziada katika kitabu chake cha: [Ash-Sharhul Kabiir 2/268, Ch. ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah]: “Hali hii iliichukia Malik katika nchi ya Uislamu, kwa sababu mkewe hunywa mvinyo na kula nguruwe na humlisha mtoto wake pia, na mume anamkubali na kulala naye, na haruhusiwi kwake kumzuia hivyo hata akiudhiwa kwa harufu yake wala haruhusiwi kwake kumzuia kwenda kanisani.
An-Nafrawiy alisema katika kitabu chake cha: [Fawakih Ad-Dwani 2/19, Ch. ya Dar Al-Fikr] kuwa: “Inachukizwa katika nchi za Waislamu kumwoa mwanamke wa Kitabu, kwa sababu mume haruhusiwi kumzuia kula nyama ya nguruwe, kunywa mvinyo, au kwenda kanisani."
Al-Bahwatiy alisema katika kitabu chake cha: [Kashaf Al-Qinaa 2/190, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] kuwa: “(anazuiliwa), maana: mume ana haki ya kumkataza mkewe (wa Kitabu kwenda kanisani), kwa hivyo yeye hatoki isipokuwa kwa idhini ya mumewe. (Na) ana haki ya kumzuia (kula chakula haramu), (na kunywa mvinyo) kwani ni haramu kwake, na hazuii jambo lingine; kwani yeye anaamini kuwa inaruhusiwa katika dini yake, ((na mume ana haki ya kumlazimisha asafishe midomo yake na uchafu mwingine kama ilivyowasilishwa hapo awali); Kwa sababu hali hii huzuia kumbusu, (na hairuhusiwi kwa mwanamke wa Kitabu kufanya tendo la ndoa wakati wa kufunga kwake) (wala hairuhusiwi kuharibu Swala yake) kwa kujamiiana au kwa vinginevyo, kwa sababu anamdhuru, (na) wala hairuhusiwi (kuharibu ibada yake, na hairuhusiwi kumnunulia) – yaani kwa mke wa Kitabu - mkanda wa kiuno (Wala hairuhusiwi) kununua (kwa mjakazi wa kitabu mkanda wa kiuno kwa sababu ni msaada kwao kuonesha hisia zao, (badala yake, yeye mwenyewe aende na kujinunulia mkanda wa kiuno)”.
Kwa maana hii hufahamika maneno ya wale wanavyuoni walioruhusu kumkataza mwanamke wa Kitabu. Al-Khatib Al-Sherbiniy alisema katika kitabu chake cha: [Al-Mughni Al-Muhtaaj 4/313, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Islami]: (Mwanamke wa kitabu aliyeolewa hali yake ni kama mwanamke Muislamu katika matumizi, mgawanyo, na talaka) na venginevyo kwa ushiriki wake katika ndoa ... (na analazimishwa) mke anayekataa akiwa Muislamu au wa kitabu, na vile vile mjakazi (kuoga kutokana na hedhi na baada ya kujifungua) yaani, mwenye mke ana haki ya kumlazimisha afanye hivyo... (vile vile kuoga janaba), maana, mwanamke wa kitabu analazimishwa kukoga kutokana na janaaba (na) analazimishwa (kuacha kula) nyama (ya nguruwe) na mengineyo, hali ambayo hufanya starehe hiyo huondolewa kwake, pia analazimishwa kuondoa uchafu. Mtazamo wa pili: hakuna kulazimishwa; Kwa sababu hali ile haizuii starehe, na suala la kutokubaliana kuhusu kumlazimisha mwanamke wa Kitabu kuzuia kula nyama ya nguruwe akiwa anafikiria ni halali kama mkristo, akiwa anaamini kwamba ni haramu kama myahudi anazuiliwa jambo hilo kutoka kwake (na) mwanamke wa kitabu (na mwanawake muislamu pia wanalazimishwa kuosha kile kiungo kilicho najisi katika mwili wake) ili aweze kufurahia kama alivyobainisha Ar-Rifa'I, na kama alivyobainisha Al-Mawardi kwa sababu ya ugumu ambao husababisha uchafu, na tatizo lake ni kwamba hairuhusiwi kufurahia kiungo kilicho najisi.
Al-Mawardiy alisema: mume ana haki ya kumzuia mkewe kuvaa mavazi yaliyo najisi kabisa, na katika kitabu cha: [Ar-Rawdha] imetajwa kuwa inaruhusiwa kwake kumzuia mkewe kuvaa ngozi ya mnyama aliyekufa kabla ya kuitengeneza kwake, na kuvaa kitu ambacho kina harufu mbaya, na pia ana haki ya kumlazimisha ajisafishe uchi wake, kukata kucha, kuaondoa nywele za kwapani na uchafu ukizidi ndani yake, na hata kama haujazidi, na pia ana haki ya kumzuia kula kile kilichoathiriwa na harufu yake, kama vitunguumaji na vitunguusaumu, na kula kile kinachoweza kusababisha ugonjwa, na ana haki ya kumzuia mke wa Kitabu kunywa kile kilicho mvinyo, na pia kutokana na vinginevyo na kuuza na makanisa kama ambavyo anaweza kumzuia mke Muislamu kunywa mvinyo ikiwa anafikiria inaruhusiwa kwa kiasi kisichosababisha ulevi, na pia kutokana na vinginevyo, na anaruhusiwa kumzuia kwenda misikiti na kuswali Swala ya jamaa, na hali ya Bwana inafanana na hali ile ya mume kama ilivyoelezwa, na hana haki ya kumlazimisha mjakazi wake ambaye ni mmajusi au mpagani kuingia Uislamu; Kwa sababu utumwa ulimnufaisha kupata amani kutokana na kuuawa .
Baadhi ya Maulamaa waliotangulia – kama Sufian Al-Thawriy - wamesema kwamba hairuhusiwi kuangalia nyuchi za wanawake wa Kitabu, kwa kuogopa kwamba jambo hilo linaweza kusababisha kufanya makosa yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu, sio kwa sababu wanao utakatifu wa kujitosheleza wao wenyewe ambao unakataza kujiangalia kama walivyo, na akatoa dalili kutoka kauli yake Mwenyezi Mungu: “Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana ili wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.” [AL HAZAAB: 59]. Hiyo ni, ikiwa watafanya hivyo, watajua kuwa ni wanawake huru na sio wajakazi wala malaya. [Rejea: Tafsir Ibn Kathir: 6/425, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Ufupisho: Mume ana haki ya kumwamuru mke wake ambaye ni katika watu wa Kitabu (wakristo na wayahudi) kuvaa hijabu, ikiwa hajamwamuru au amemwamuru, akakataa hana dhambi, kwa sababu yeye hakukalifishwa kwa ajili ya Matawi ya Fiqhi, au kwamba kinachokusudiwa kumkalifisha kwa ajili ya Matawi ya Fiqhi ni kuhesabiwa Akhera.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas