Umma wa Kiislamu – Miongoni mwa Sif...

Egypt's Dar Al-Ifta

Umma wa Kiislamu – Miongoni mwa Sifa zake ni: Hisia za Umoja wa Kijamii

Question

Je, ni lipi kusudio la Hisia za Umoja wa Kijamii kama ni sifa miongoni mwa sifa za Umma wa Kiislamu?  

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hisia za Umoja wa Kijamii ni upande katika pande za kuvutia za falsafa ya Mtazamo wa Kiislamu wenye kulenga Ujenzi wa Ustaarabu wa Binadamu kupitia Binadamu yeye Mwenyewe, na wala sio kupitia kupora na kung’oa mizizi yake, kwa hiyo maneno yanayohusiana na Ustaarabu wa Kiislamu hayajengwi na silika ya kujipendelea ya mtu mmoja inayoyafikia maeneo ya Dhati kwa ukuzaji usio Wafaa wengine, lakini pia haujengwi na silika ya utenzaji nguvu wa hali ya juu unayoyabadilisha maneno ya Uwepo wa Mwanadamu na kuwa tu mapitio yenye sifa ya kujiendesha kama bubu.
Hakika falsafa ya Mtazamo wa Kiislamu inaegemea zaidi kwa kuegemea kwake elementi za Ujenzi wa Kistaarabu wa Hisia za Kijamii zinazoipa nafsi nafasi ya kuitumia haki yake ya kimaumbile katika tatuzi mbalimbali ardhini na katika Historia, na Jamii inapaswa kuitumia haki yake ya kimaumbile katika kujiundia sifa za Umma wake.
Na Hisia za Pamoja hazimaanishi mtu kuchupa mipaka na kuelekea katika Mkusanyiko, kwani mtu mmoja ni sehemu ya mjengeko wa awali unaounda mweleweko wa Jamii ya Kibinadamu, vilevile hisia za kijamii hazitokani na mtu mmoja ambaye yupo tu, ni watu wangapi wanaoishi duniani wakiwa watupu kikamilifu bila ya kuwa na hisia za kuwasiliana kiroho na Jamii yao ya Kibinadamu. Hakika mambo yalivyo, ni kwamba Hisia za Umoja wa Kijamii hutokana na nafsi ya mtu kutokana na yanayoivuta nafsi hiyo miongoni mwa Maadili mema maalumu, Maadili yasiyo na umimi ndani yake, au kwa utenzwaji nguvu, bali maadili yenye kuungana na uhalisia wa yaliyomo Ulimwenguni bila ya mgongano nayo, Maadili yanayoamini ya kwamba mwanadamu hayuko peke yake katika Ardhi hii. maadili haya hayajengeki isipokuwa kwa maadili ya kudumu ya Uislamu.
Hisia hizo za Umoja wa Kijamii ambazo zinazingatiwa kuwa ni sifa miongoni mwa sifa za Umma wa Kiislamu zinatokana na uwepo wa aina mbalimbali uliopo katika Kiislamu:
Uwepo wa Kwanza: Hakika Qur'ani Tukufu imekuwa ikipupia juu ya kuotesha na kujenga hisia za upendo na kuwapendelea wengine ndani ya Waislamu kupitia Aya na Sura zake, mpaka kufikia katika kuiunda Jamii ya Qur'ani Tukufu katika mchanganyiko mmoja, hakika Qur'ani Tukufu inatuwekea mbele yetu katika upande huu, sura iliyo hai ya Hisia za Ujamii. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma}. [AT TAWBAH 128] Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Huenda ukaiangamiza nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya!} [AL KAHF 6]
Kwa hivyo, licha ya kuwa Aya Tukufu zinazoelezea uelezo huo wa kuvutia kwa mateso ya Mtume S.A.W. kwa ajili ya watu wote, ambao ni Mkusanyiko wa Kiislamu, jambo ambalo linaakisi hisia hizo za Umoja wa Kijamii kama uwepo miongoni mwa aina mbalimbali za uwepo wa falsafa ya mtazamo wa Kiislamu katika ujenzi wa Ustaarabu wa mwanadamu.
Uwepo wa Pili: Hakika Hisia za Umoja wa Kijjami kwa Umma wa Kiislamu zinarejea kwenye falsafa ya umoja wa Uislamu, kuanzia Umoja wa Mola Muumba (Mwenyezi Mungu Mtukufu), na kufikia umoja wa viumbe, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile}. [AZ ZUMAR 6] Na kupitia umoja katika nyanja zote kutoka katika umoja wa Qur'ani Tukufu na umoja wa Mtume S.A.W., umoja wa Kibla, umoja wa sheria na kadhalika.
Uwepo ya Tatu: Uhusiano wenye nguvu baina ya Uongozi na Ngome, basi kuna hisia za pamoja zinazomwunganisha kiongozi na anaowaongoza, na baina ya wanaoongozwa na Kiongozi wao, hakika Mtume S.A.W alipigana vita akiwa pamoja na Maswahaba wake, na alichimba mahandaki akiwa nao, na aliwatembelea wagonjwa wao, na aliwaliwaza waliokuwa na huzuni miongoni mwao, na alifurahia watu wayatamani mazuri ya wengine waliofanikiwa, ama kwa upande wa Waislamu hakika mambo yalivyo wao walimpa kiapo cha Utiifu kwamba wangemlinda kwa namna wanavyowalinda wake na watoto wao, na kujitoa kwa roho zao, mali zao na watoto wao ili wamkomboe.
Basi masafa (umbali) baina ya Mtume S.A.W. na wafuasi wake Waislamu yalikuwa finyu zaidi, na masafa hayo pamoja na ufinyu wake yalikuwa na ung'avu na siyo yenye giza, na hayo ni lazima yawepo siku zote baina ya Umma na viongozi wake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Rejea: Kitabu cha [Katika mtazamo wa Kiislamu katika Upande wa Fasihi, cha Dkt. Mohammad Ahmed Al Azab. Baraza Kuu la Utamaduni, Cairo 1983, Uk. 91-102]
 

Share this:

Related Fatwas