Urithi wa Kislamu – Kupitia Vyombo ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Urithi wa Kislamu – Kupitia Vyombo Vilivyoelezea – Mitazamo Yetu kwa Ulimwengu.

Question

Ni upi mtazamo wa wanachuoni Waislamu kwa ulimwengu wa nje? Je mtazamo huu umeathiri urithi wa Ulimwengu wa Kiislamu? Na je ni lazima kwetu kufahamu mtazamo huu ili utusaidie kufahamu yaliyo bora zaidi kwenye urithi wetu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ili nielezee vipengele vya mtazamo wa urithi wa ulimwengu, uwepo, mwanadamu na maisha, nahitaji kufunga safari ya kuangalia mitazamo ya akili ya kiurithi: Mtazamo wa Al-Mauridy, Al-Juweiny, Al-Ghazaly, An-Nawawy, Ibn Taimiyah, Ibn Hajar, As-Suyuutwy na wengineo, hawa ndio ambao wameishi ndani ya zama za urithi na ndio ambao wameshikilia – na ni lazima – vifaa vya uelewa wa Qur`ani na Sunna, vilevile wameshikilia mtazamo maalumu wa Ulimwengu wa nje.
Tunafupisha mtazamo wa mzalishaji wa urithi wa Ulimwengu wa nje katika vipengele maalumu, na hilo bila ya kuangalia vyanzo vyake kwa sababu vyanzo vyake ni vyenye mpangilio mgumu: Baadhi yake ni Itikadi ya Kiimani na baadhi vinatokana na mazingatio na kina cha kufikiri kuhusu Ulimwengu vitu na vilivyo nyuma ya Ulimwengu au kutokana na ufupisho wa falsafa ya zamani au mchanganyiko wa staarabu zingine zilizoingiliana na ustaarabu wa Waislamu kama vile ustaarabu wa Kihindi Kichina Kifarao Kifoiniki Kiashuri na Kibabeli….mwisho ustaarabu wa Kigiriki kwa aina zake zote bila ya kuangalia tu Shule ya Aristotle yenye umaarufu mkubwa – ambapo ilikuwa ni mkusanyiko wa fikra nyingi ambazo zilipokelewa kutoka kwa akina Pythagoras Sophocles Socrates Plato na wengine.
Na mpangilio huu wa vyanzo sio kusudio muhimu bali nimeutaja ili kuweka wazi kuwa kuna vyanzo vyingine tofauti na chanzo cha Aristotle ambaye aliandaa baadhi na kuwa ndio kila kitu au ndio chanzo pekee, hali haipo hivyo kwani Waislamu walishirikiana na mantiki hii ya Aristotle na kuifanyia marekebisho kwa kuondoa na kuongeza pamoja na vyanzo vyingine.
Ni vigumu sana – hata kwa watu wa urithi – kubainisha – hasa – kuwa vipengele hivi vya mtazamo wa Ulimwengu vimeja kutoka wapi, kwa sababu huenda vikaja kutoka moja ya vyanzo hivi au kwa kufanya kazi pamoja kati yao….nina amini kuwa kulitafiti hilo sio jambo muhimu sana kwenye maudhui hii ambapo kimsingi tunajikita zaidi kuangalia mtazamo wenyewe na wala sio vyanzo vyake.
Vyovyote itakavyo kuwa turudi kujiuliza: Ulikuwa vipi mtazamo huu wa Urithi?
Mtazamo huu ndio ambao umesaidia Elimu ya Maneno, na ufupi wake ni kuwa mtazamo huu ulikuwa unaangalia huu uwepo ima ni wenye kufungamana na sehemu au si wenye kufungamana na sehemu: Kufungamana hapa kwa upande wa – lugha – ni kuwa, ima kuwa ni wenye kuelekea upande mmoja bila ya kuelekea upande mwingine, au ima ni kila chenye kikomo na mipaka au kufanya kazi upande mmoja, na kufungamana – katika mtazamo huu – ima mfungamano mwepesi na unaitwa “Kiini” au mfungamano wenye mpandano unaitwa “Mwili”.
Mwili – kwa mfano – ni kama mwili wa kiumbe hai wenye mpangalio wa seli mbalimbali, wakati ambapo kinachochukuwa nafasi ya Kiini ni seli tu. Hivyo seli ni yenye hali ndogo sana ya kufungamana na sehemu na walikuwa wanaiita “Seli pekee” kwa sababu si yenye kukubali kugawanyika, hata kama inagawanyika kisayansi….hii imeelezewa na mitazamo mingi ya Elimu ya Kimaumbile au Elimu ya Fizikia katika masuala ya kugawanyika kwa seli.
Taswira hii ya Kiini au Seli – ikiwa itawezekana kuwa ipo kwenye vyanzo tofauti katika vyanzo vilivyotajwa - isipokuwa yenye msingi imechukuliwa kutokana na Akida au Imani ya Kiislamu ambayo inatambua kuwa Mwenyezi Mungu Pekee hakuna kitu chochote kabla yake na wala baada yake, wala hakuna chochote cha kufanana na Yeye katika uwepo, bali kila kitu kimeumbwa na Yeye, Yeye Mtakasifu Ndiye Muumbaji na kila kitu kilichopo katika Ulimwengu huu kitakwisha, kwani hakuna kitu kisichokuwa na mwisho katika vile vilivyopo ulimwenguni….na viumbe vyote duniani vyenye kuhisika ni vyenye fungamana kati ya mwanzo na mwisho.
Kisha kisichofungamana katika vilivyopo huitwa “Chenye kuzuka”: Nacho ni kitu kipo kupitia kingine hakiwezi kusimama chenyewe bila ya kuwepo kingine, mfano wa sifa na hali mbalimbali: “Kama vile umasikini na utajiri, afya na maradhi, furaha na huzuni, nguvu utambuzi rangi urefu….nk, sifa zote hizi zinazingatiwa ni za kuzuka zisizojitegemea peke yake bali zinahitaji mahali pa ufumbuzi, ni lazima tufahamu uwepo wa masikini na tajiri mtu mzima na mgonjwa mwenye furaha na mwenye huzuni mwenye nguzu…..nk.
Mwenyezi Mungu Mtukufu sio hivyo na zaidi ya hivyo…..kisha Yeye Mola Mtukufu si mwenye kufungamana na sehemu si mwenye mwili wala seli wala si mwenye kuzuka! Wanaelimu ya maneno wamesema kuwa umuhimu wa kumtoa Mwenyezi Mungu kwenye maudhui hii na kigawanyo hiki ili hata ikisemwa kuwa “Si mwenye kufungamana na chochote” basi kutofungamana kwake Mola Mtukufu kunatofautiana na kutofungamana kwa mwingine!
Hivyo wameona kuwa vyenye kufahamika ni Vitatu:
- Mola Mtukufu kwa Sifa zake Kamilifu, Nzuri na Tukufu.
- Mfalme, nao unafahamika kwa hisia kwa kuwepo alama za vitu watu na matukio….inaniwezesha kuona kwa kutumia darubini au kwa hisia tu.
- Ufalme, nao ni uwepo usioonekana kwenye hisia za ndani au hisia za wazi, kama vile Malaika Jini roho…..nk, lakini siku moja tunaweza kuvigundua au kuvifikia.
Kila siku tunapogundua kitu basi hiko kitu kinatoka kwenye ulimwengu wa ufalme na kuingia kwenye ulimwengu wa mfalme ambapo tunaona vikiwa vinazidi katika historia ya mwanadamu, kama vile kugundua kwetu nishati ya umeme, mawimbi, chombo cha kuchukulia picha ambacho kimetokana na ufanisi wa kemia kutoka katika ulimwengu wa ufalme na kwenda kwenye ulimwengu wa (Seli mpaka hivi sasa bado ipo kwenye ulimwengu wa ufalme, hata baadhi ya shule bado zinapinga uwepo wake kutokana na mambo ya kifalsafa na fikra maalumu za kifizikia).
Mambo yote haya yameathiri akili ya Muislamu bila hata kusema Aristotle chochote ndani ya hayo lakini yamekuja kwa kufuata na kufuatilia Imani iliyotulia.
Wametegemea fikra hii ya “Seli Pekee” kwa lengo la kuthibitisha kiakili na kihesabu uwepo wa Mungu na kukanusha uwepo wa mfano, na kupelekea kupinga “Mtiririko usio na mwisho” kihesabu, jambo linalothibitisha kauli kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwenye kwisha, kama ilivyopelekea kupinga masuala ya “Mzunguko” ambayo yanamaanisha kuwa vitu vinahusiana katika kupatikana, hiki kimezaa kile na kile kimezaa hiki, na kupelekea mzunguko unaofanana na kisa cha yai na kuku kama kilivyoashiriwa hapo nyuma, Waislamu wamekataa hilo kwa msingi kuwa ni lazima kuwepo chanzo au mwanzo, kwao kuumba kwa Mwenyezi Mungu ni moja ya sababu mbili iliyoizaa sababu nyingine.
Hii katika kufungamana na sehemu, ama vya kuzuka amezungumza Aristotle kuwa kuna aina tisa, isipokuwa Waislamu wao wameona kuwa uchambuzi unaofikia aina hizi tisa ni aina mbili tu zinafungamana na sifa saba au zaidi, wametengeneza mgawanyo wa Aristotle wa watoto na wanafunzi katika sura fupi na nyepesi na wakasema:
Zaidi mrefu wa bluu mtoto wa Mfalme - nyumbani kwake jana alikuwa amekaa.
Mkononi ana fimbo ameinyanyua na kuipinda – haya ni masuala kumi yaliyotengenezwa.
Zaidi: NI mtu, naye ni seli au mwili mwenye kufungamana na sehemu, naye akiwa kwenye seli na si mwili, ambapo sifa hapa ni tisa nazo ni:
Mrefu: urefu, nayo ni sifa inayoungana kama vile idadi ya mita….na isiyoungana kama vile idadi ya punje za ngano.
Bluu: Namna, kama vile rangi afya utambuzi…..na mengineyo.
Mtoto: Nasaba, anayonasibishwa kwa Mfalme.
Mfalme: Nyumbani kwake: Sehemu.
Jana: Muda.
Mwenye kuegemea: Hali, kama vile amerukuu amesujudu.
Mkononi kwake: Umiliki, mfano “Ninayo” na “Yangu”.
Kunyanyua: Ni kitenzi.
Kupinda: Athari ya kitenzi.
Haya ndio aliyoyasema Aristotle, tofauti na kuwa Waislamu wamesema kuwa hivi vyote inawezekana kuita “Unasibishaji”, na unasibishaji huu hauhusishi vitu tisa tu huenda ikawa ni zaidi ya tisa kwa uwingi sana, jambo ambalo linatubainikia kushirikiana kwao na maarifa ya wengine na wala sio ufuasi au uelewa wa upofu.
Ikiwa tutaweza kuainisha aina hizi kumi (Zenye kufungamana na kuzuka kwa sifa zake tisa) basi tutaweza kuainisha uhalisia na hali kwa uainishaji kamili unao karibia kuwa kama picha ya fotoghrafi.
Waislamu wameelezea sana katika kuleta sifa matukio halisi na kuyakusanya, ni jukumu la msingi ambalo linamshuhurisha mtafiti katika sayansi ya sasa ya jamii ya watu kwa kiwango kikubwa.
Maelezo haya namna ya kufahamu urithi wa Kiislamu wa uwepo na athari zake katika kufahamu sehemu ya uhalisia, yanatusukuma kuangalia tena urithi huu, kwani maelezo yake katika masuala ya mtazamo jumla – kwa ibara zake fupi – inaelewesha kuwa mitazamo mingi ya karne ya ishirini na gunduzi zake tayari ilishaelezewa na Waislamu, lakini kwa matamshi mengine yanayoelezeka kwa lugha yao ambayo tunafanya jitihada ya kuifahamu lugha yao na kuwa nayo karibu.
Kwa mfano, ni kwanini mwanga unazingatiwa ni kitu chenye kasi zaidi katika mwendo wake? Jibu la mitazamo ya kisasa – kama vile nadhari ya mwanga wa kamera“ – inazungumzia kuwa mwanga hautembei kwenye mistari iliyonyooka bali unatembea kwenye mawimbi na katika vipande, na hii inamaanisha kuwa huu mwanga unaisha kisha unakuja mwingine kwa muda mfupi sana unakadiriwa chini ya sekunde moja, nadharia hii ni sawa na nadharia ya urithi wa Kiislamu lakini kwa matamshi tofauti: Kuwa kila cha kuzuka – ikiwa pamoja na mwanga – si chenye kuthibiti, kinaisha na kurudi tena katika hali inayokaribia ulazima wa hivyo.
Vilevile Waislamu wamefikia vyanzo vyote vilivyopita ambavyo tumevielezea, na kwa mujibu wa Imani ya Kiislamu ambayo inasema: {Kila siku Yeye anakuwa na jambo} Ar-Rahman: 29, na kuifikia nadharia muhimu inayoitwa “Nadharia ya Kuumba na kuendeleza”.
Hivyo kuna hali ya kuumba {Je! Hakumbuki mwanadamu ya kwamba tulimuumba kabla na hali hakuwa chochote?} Mariyamu: 67.
Na kuna hali ya kuendeleza, na mwendelezo huu ni {Kuwa! Nalo huwa} [AL BAQARAH: 117], wenye kuendelea usiokatika….lau Mwenyezi Mungu Mtukufu atakatisha mwendelezo huu basi atakufa aliyekatiwa, hiyo haina maana atakufa kwani kifo ni kiumbe kingine {Ambaye Ameumba kifo} Al-Mulku: 02, isipokuwa atamalizika kwa maana ya kutokuwepo kabisa…..Mwenyezi Mungu Mtukufu bado ni Muumbaji, na kukatisha mwendelezo – Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mfano bora – ni kama kutaka mawimbi ya umeme kwenye taa sura hujificha na mwanga hukatika.
Mwendelezaji ndiye ambaye analinda uumbaji na kuupa uhai, naye ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika na yeyote, kutokana na hili wamefahamu maana ya maneno (Hakuna hila wala nguvu isipokuwa ni kwa Mwenyezi Mungu) kwa maana kukatika kila uwezo au hila au nguvu isipokuwa ni kwa msaada wa Mweneyzi Mungu na kuendeleza kwake, na wakafahamu maombi ya Mtume (S.A.W): “Usinibebeshe kwenye nafsi yangu hata kidogo”( )
Kwa sababu lau atanibebesha kwenye nafsi yangu basi huenda nitakwisha na kumalizika, hivyo hakuna hila kwa upande wangu wala nguvu ya kujiweka mwenyewe au kujibakisha isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Aliyejuu na Mkubwa….anapofikia mwenye Imani kwenye hili anakuwa amefika kwenye viwango vya kutegemea na kusimamiwa na kumuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa moyo wote fikra na umuhimu katika ibada na maisha, hivyo mimi natokana na Yeye na mwenye kuelekea kwake, na katika hilo pia tunafahamu maneno ya Mtume: “Nakuitikia Wewe, na kheiri zote zipo mikononi mwako, shari sio ya kwako, mimi ni wako na kwako ndio marejeo yangu” ( ).
hii ilikuwa ndio imani iliyoenea mpaka ndani ya karne ya kumi na tisa, lakini kimsingi ilikuwa kwa wengi, leo hii umma umeingia kwenye ujinga na kubadilika na kuwa umma usio na elimu usiojua dini yake wala Qur`ani yake tokea baada ya karne ya nne Hijiria sawa na karne ya kumi ambapo imeisha zama za uzalishaji elimu na kuanza zama za utasa wa kielimu, kwa mfano Imamu Fakhr Ar-Raazy anafanya sherehe kubwa na kuonesha dalili elfu moja za uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakati ambapo maelezo ya mmoja wa aliyeshindwa katika hilo: Je alikuwa na shaka elfu moja katika uwepo wa Mungu Mtukufu? Haya ndio tunayokusudia utasa wa elimu.
Kwa upande mwingine, ni lazima ifahamike kuwa misingi ya kujenga ustaarabu ni kitu kimoja na yanayosimamisha staarabu miongoni mwa falsafa na mitazamo ya kiakili na kimawazo ni kitu kingine, lakini kumekuwa na mchanganyiko mkubwa kati ya falsafa inayojenga ustaarabu na uhalisia au ukweli unaoendana na falsafa, jambo ambalo linazalisha na kuibua mijadala mingi, kwani maendeleo ya ustaarabu yana kanuni zake na sifa ya pekee ya ustaarabu zina misingi yake.
Waislamu walitangulia wakiwa wanajibu maswali haya makubwa kama vile maswali ya jumla ya mwanzo, vilevile Magharibi imepiga hatua ya maendeleo bila ya kujibu maswali hayo, kadhia hii hata ikiwa inaathiri katika kujenga ustaarabu isipokuwa tu kazi za ujenzi wa ustaarabu zina njia nyingine. Mtazamo jumla maalumu kwangu unaniambia, muabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha mimi ninaujenga ustaarabu wangu wote juu ya: Ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambao huo ni ustaarabu wa kuabudu, na juu ya kujenga ulimwengu: {Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo} [HUUD: 61].
Kisha ikiwa kazi ya ujenzi itapingana na utendaji na kukawa na uharibifu basi mtazamo unanizuia mimi kusonga mbele kwenye njia hii na kunilazimisha kutafuta njia nyingine…..siwezi kutengeneza ndege yenye sauti inayo haribu tabaka la orzoni na kuangalia uharibifu kabla ya kuangalia manufaa.
Hii haina maana kuwa mwingine amepiga hatua na kujenga ustaarabu wake kwa sababu hivyo alivyo…msingi ni kufanya juhudi kwa nguvu kubwa na kushikamana. Na Magharibi ya sasa imefanya juhudi na kujenga dunia kwa falsafa na uelewa pamoja na teknolojia na utawala wa uelewa wa “soko” na mengineyo, na wamemaliza kwa kujenga ustaarabu huu kwa hali iliyonayo na kujenga ustaarabu wao kwa nguvu kubwa: Kufanya kazi kwa umahiri, kufanya kazi vizuri wakiwa timu na roho ya pamoja, kuwa na malengo maalumu, kwa njia sahihi…..nk. Huko Magharibi waliunganisha uhalisia wao na falsafa zao hata kama falsafa hizo zilikuwa ni ukafiri na upingaji Mungu, na kwa kushirikiana ndipo ulipokuja mwendelezo.
Sauti ya ustaarabu wa Kiislamu umeshuka na kupoteza cheche zake kwa kukosekana roho ya kweli katika ujenzi wa ustaarabu baada ya kuwa ustaarabu wao ulikuwa umeenea sana hapo mwanzoni kama tunavyoona hapo kwa kujisomea urithi wao, ambapo walifikia kiwango cha zaidi cha upendo hofu na uelewa katika kufungamana kwao na Mola wao pamoja na Dini yao, na wakiwa na lengo la kina juhudi na umakini katika kujenga dunia yao kwenye msingi huo, na ustaarabu wa Kiislamu ulisita pale ulipokosekana mshikamano: Mshikamano kati ya Imani na maadili, kati ya mtazamo na mfumo uliopo: Uwe wa kisiasa kijamii au kiuchumi, hakika misingi ya ustaarabu wa Kiislamu ulirudi nyuma baada ya miaka elfu moja ambayo Waislamu ndani ya kipindi hicho walikuwa wanazalisha ustaarabu na elimu mbalimbali, hati za Misahafu zikashindwa na kushuka utaalamu kugawanyika programu ya kila siku kwa Muislamu sio kwa sababu falsafa na mitazamo yenye kujenga vilikuwa na kasoro au kuwa kinyume na harakati za maendeleo bali ni Waislamu kwenda kinyume na mwenendo wa maendeleo ya ustaarabu.
Kwa upande wa kubakia, kumekuwa na staarabu zilizoanza na kuwa tasa kwa sababu zilitanguliza ujenzi kabla ya binadamu, ama ustaarabu wa Uislamu ulibakia kwa muda mrefu – pamoja na kurudi nyuma – kwa sababu ulitanguliza ubinadamu kabla ya ujenzi na hili halina uhusiano na maendeleo.
Lakini ni kwa nini akili hii ya kiurithi ilipotea? Tatizo ni nini ambalo lililopelekea kwenye mgawanyiko na mpasuko kati ya maandiko na ukweli halisi? Tatizo ni kuwa mwanadamu ni mwenye kumiliki mfumo wa kimaarifa na kimarejeo bado anakutana na matatizo halisi na mizizi yake pamoja na yaliyokuwa nyuma yake…yametokea haya nchini Misri tokea zama za Muhammad Ally na mradi wake pindi alipotenganisha kati ya aina mbili za elimu: Elimu ya kiraia na elimu ya kidini…na tokea alipoitwa mwanachuoni wa elimu ya Kisharia: Hakika wewe ni mtu wa dini na wala sio mtu wa dunia hivyo unatakiwa kuwa mbali na vitu kama hivi ambavyo vinafanyika katika uhalisia…leo anaambiwa: Ni kwa nini haufanyi jitihada katika kuleta hukumu ya Kiislamu na ufumbuzi wa Kiislamu wa matatizo haya….na yanatoka wapi matatizo haya? Na kwa mfano huu hufanywa pamoja na uhalisia kwa msomi wa sayansi ya kijamii ya kisasa pindi anapotakiwa kuwa na mitazamo ya Kiislamu hali ya kuwa yupo mbali kikamilifu na elimu ya kitu chochote katika Uislamu.
Hayo yakapelekea kukosekana na kupotea Sharia ya Kiislamu na baada ya hapo kudhoofika Imani na Akida katika umma.
Kwa mfano pindi alipokuja Khedewy Ismail – nchini Misri – akifanya harakati na juhudi za kujenga msingi wa kuikomboa dola ya Othman ambayo ilikuwa inaangaliwa kama dola ya utawala wa Kiislamu….pindi alipoona inalingania kwenye utekelezaji wa Sharia kwa mfumo ambao ulionekana katika “Eneo la hukumu za kiuadilifu” pamoja na juhudi zake za kutenganisha alimwita “Majdy Saleh Basha” na kufanya kazi ya kuandika Sharia ya Kiislamu isipokuwa hakuifanyia kazi mpaka ilipochapishwa tafsiri yake kwa sababu iliendelea kufungiwa kwenye makabati…na kuendelea mashambulizi katika uandishi na uwekaji Sharia mpaka akatuhukumu kwa kanuni si za kwetu na wala sisi si sehemu yeyote katika hukumu hizo.
Iliendelea hivyo mpaka alipokuja Dr. Sanahury na kuweka kanuni za kiraia, na Ahmad Basha Amin akaweka kanuni za kijinai – na hilo likiwa ni chimbuko la jumla za kanuni au sheria za dunia, Sanahury aliposherehesha kanuni za kiraia – kwenye juzuu kumi na mbili – ikaja sherehe yake ya kanuni mbalimbali: Kibelgiji Kifaransa….na katika Sharia ya Kiislamu pia, na hivi sasa sisi ni wenye kuhukumiwa nazo, baadhi yake zimetokana na Msingi Mkuu wa uadilifu ambao kila kiongozi anautumia kwa ajili ya kutolea maamuzi…. haikubakia katika Sharia isipokuwa kanuni zilizofahamika Sharia za ndoa na baadhi ya nadhari za makubaliano au mikataba…..nk. Hali hii tunajaribu kuifahamu hivi sasa kupitia kuelezea kanuni mpya za taasisi ya kidini kabla ya kuweka kwake.
Hivyo kuna mtengano kati ya Akida na Sharia kwa upande mmoja na kati ya mfumo wa maisha yetu yalivyo kivitendo, hali hii haiwezekani kusimama katika hali yake ya ustaarabu au maadili….angalia ni kwa nini watu wanategemea kuvunja sheria za barabarani bila ya kuona aibu, bali mbaya zaidi wahusika wa kufuatilia uvunjifu huu ndani ya nafsi zao hawana msukumo wa kuwakamata wakiukaji au kuwaadhibu, ama lau atafahamu kuwa sheria hizo zinatokana na Imani yake na yeye ni mwenye kuhukumiwa na Sharia anayoiamini basi hakuna shaka kuwa atasimama kuifanyia kazi ikiwa katika mlango wa Ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu wote….hakika haya ni yenye kuibua mishangao yetu kwa watu wa Magharibi na tumetangulia kuelezea huko nyuma: Mshikamano.
Chanzo: Kitabu cha Njia ya Kuufahamu Urithi, cha Mufti wa Misri. Dr. Ally Jumaa.

 

Share this:

Related Fatwas