Maana ya Kuagiza na Kukataza katika...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya Kuagiza na Kukataza katika Masuala ya Adabu.

Question

Tulipitia masomo yetu ya vyanzo vya fiqhi katika ngazi ya Chuo Kikuu kwamba maana ya kutoa amri ni kulazimisha, na kwamba maana ya Katazo ni kuharamisha, lakini je, kutoa amri kwa jambo maalumu au kulikataza kwa kuzingatia ukweli kwamba jambo hilo lililoamuriwa au lililokatazwa ni miongoni mwa maadili au desturi, je hali hii hulazimishwa sana au hukatazwa kabisa, au hiyo ni sababu ya kuligeuza jambo hilo kutoka katika kulazimisha na kukataza? 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na sala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, Jamaa zake na Maswahaba wake, na wataowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo.
Miongoni mwa mihimili ya taaluma ya Vyanzo vya Fiqhi ni Agizo na Katazo, kwa hivyo wanavyuoni wa taaluma hii wanataja hivyo katika mada ya maneno. Kama uwekezaji wa hukumu kutokana na dalili inayotegemea maana yake, na umuhimu wa mada hizi mbili na zinazohusiana nazo ni kwamba zinanufaika nazo katika kutoa hukumu za kisheria ambazo ni matunda na lengo linalohitajika katika vyanzo vya Fiqhi; Kwa hivyo, Al-Sarkhasi anasema katika utangulizi wa kitabu chake cha Vyanzo vya Fiqhi: “Kwa hivyo kile kilichoanzishwa katika taarifa ya jambo ni kutoa amri na Katazo, kwa sababu shida nyingi ziko pamoja nazo, na kwa ufahamu wao hukumu zinajulikana, na inawezekana kutofautishwa kati ya jambo ambalo ni halali na jambo ambalo ni haramu.” [Usuul Al-Sarkhasiy 11/11, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, Toleo la Kwanza, 1414 AH]. Hukumu za Sheria mara nyingi huzunguka kwa kutoa amri na Katazo. Hukumu za kukalifisha zimeoneshwa kwa njia ya kutoa amri na Katazo, lakini kutoa amri ni mzunguko zaidi kuliko katazo, na kwa sababu hiyo wanavyuoni wamelitangulia jambo hili, na wakapitisha baadhi ya masuala kutokana na Katazo kwa masuala ya kutoa amri. Al-Zarkashiy anasema katika kitabu cha: [Al-Bahr Al-Muhiit 3/257, Ch. ya Dar Al-Kutub, toleo la kwanza, Mwaka wa 1414 AH]: “Suala la kutoa amri lilitanguliwa na katazo, kwa sababu ya kutanguliwa kwa hali ya kuthibitisha na kukanusha, au kwa sababu paliulizwa kwa ajili ya kupata jambo, na Katazo ni ulizo la kuendelea kwa ukosefu wake. Kwa hivyo basi hali ya kutoa amri ilitanguliwa kama lilivyotanguliwa jambo lililopo na jambo lisilokuwepo, na kwa kuzingatia utaratibu wa nyakati, basi hali ya kukataza inatanguliwa na hali ya kutoa amri kama lilivyotanguliwa jambo lisilokuwepo na jambo lililopo. Kwa sababu jambo lisilokuwepo ni la zamani zaidi kuliko jambo lililopo. Ibn Qudamah alisema baada ya kutaja sura ya kutoa amri: “Jua kwamba yale tuliyoyataja miongoni mwa maagizo yanaonesha makatazo, kwa sababu kila suala la maagizo lina mfano wake katika makatazo, na kinyume chake, kwa hivyo, hakuna haja ya kurudia ispokuwa katika masuala machache tu.” [Rawdat Al-Nadhir, uk. 226, Ch. ya Chuo Kikuu cha Imam, Toleo la Pili, Mwaka 1399 AH]
Wanavyuoni wametofautiana katika maana ya kauli ya kutoa amri na kauli ya kukataza, kati ya wale ambao wamesema kwamba inaashiria kulazimisha na kuharamisha, kama ilivyo katika madhehebu ya wa wanavyuoni, na Al-Raziy alinukuu rai hiyo katika kitabu chake [“Al-Mahswul] kutoka kwa wengi wa wanavyuoni wa fiqhi, na akasema: “Ni kweli.” [Al-Mahswul 44/2, Ch. ya Muasastu Ar-Resalah]. Na wengine waliosema inaashiria kukokoteza na kuchukiza, wengine walikataa kusema maoni yao, na wengine waliosema kuhusu kushirikiana, lakini mabishano yanawekwa ikiwa kuna kauli ambayo ni tupu na hakuna dalili yoyote inayogeuza jambo kwa moja ya maana zake zinazowezekana. Ibn As-Samani anasema katika kitabu chake cha [Al-Qawati 1/92, Ch. ya Maktabat At-Tawbah, Toleo la kwanza, mwaka wa 1419 AH]: “Suala: Jambo la lazima ni la lazima kwetu, na hii ni kwa mujibu wa maoni ya wanavyuoni wengi. Hii ni kwa kauli ambayo ni tupu isiyo na dalili yoyote...”. Kuainisha dalili hizi, kufahamu maana zake na athari zake ni muhimu katika kuvuta hukumu na kuelekeza dalili, na tunaona kwamba tofauti ya hukumu inaweza kusababishwa na kupuuza uwepo wa dalili hizo.
Ikiwa ukweli wa jambo ni kulazimisha na kukataza ni kuharimisha, basi ikiwa itatumiwa kwa njia nyingine basi hayo ni matumizi yasiyo ya kweli ambayo lazima pawepo na dalili ya kuzuia kutoka kwa uwezo wa maana ya kweli, na dalili kama inavyoelezwa na Al-Jurjani ni: “Jambo ambalo linaashiria kile kinachotakiwa.” [At-Taarifaat, uk. 223, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Arabiy, Toleo la Kwanza, Mwaka 1405 AH]. Lakini walitofautiana katika aina ya dalili hii, Adhahiriyah waliiainisha matini na makubaliano [Al-Ihkam 3/259, Ch. ya Dar Al-Hadith - Kairo, Toleo la Pili, Mwaka 1413 AH]. Kinyume na umma, ambapo wao walisema: dalili yoyote kali ambayo inageuza jambo kutoka katika uwajibu na kuwa hali nyingine, ikiwa ni Matini, au Makubaliano, au Kipimo, au Dhana, au Muktadha wa maneno, au dalili yoyote nyingine inayogeuza jambo hilo kutoka katika kuwajibisha na kuwa hali nyingine isipokuwa kukiwa na dalili nyingine yenye nguvu zaidi. Katika kitabu cha: [Al-Burhan” kwa Al-Juwiyni 1/260, Ch. ya Dar Al-Answar, Kairo]: “Kauli ambayo ni tupu haiwi ila katika hali ambazo zinaonesha kuwa hali yake hii siyo ya hovyo, kwa hivyo haizingatiwi kauli kwa kutokuwa kwake na dalili ... Ikiwa kauli hii imekusudiwa kwa ukweli kabisa, basi tunabahatisha dalili nyingine zaidi juu ya yale tuliyoyataja katika sehemu ya kizuizi, na imegawanywa katika dalili za kauli na dalili za hali. Al-Zarkashiy anasema katika kitabu cha: [Al-Bahr Al-Muhiit 2/364), baada ya kutaja maana ambazo zina kauli ya kutoa amri: “Ikiwa unajua hivyo, basi hakuna ubishi kwamba sio kweli kwa maana hizi zote, kwa sababu maana nyingi hazikueleweka kutokana na kauli ya "fanya" “amri” lakini kupitia dalili.” Anasema pia: “Alqaffal alisema: Sehemu za amri ni nyingi ambazo hazina mpangilio, na zote zinajulikana kupitia maana ya maneno, muktadha wake na dalili zinazozitegemea.”
Miongoni mwa dalili hizo zinazoadhimisha amri na katazo, kwa sababu zimo katika sehemu ya adabu au mila, ni dalili inayogeuza amri kutoka katika kuwajibisha na kuwa kukokoteza, na inageuza Katazo kutoka katika kuharamisha na kuwa kuchukiza. Wanavyuoni wengi wamesema hivyo. Imam Shafiy alisema katika kitabu chake [Al-Um 7/305, Ch. ya Dar Al-Fikr, Mwaka 1410 AH}: “Asili ya makatazo kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., kwamba kila kitu ambacho kimekatazwa ni marufuku mpaka ije dalili inayoonesha kwamba Mtume alikikataza kwa maana nyingine isipokuwa kuharamisha, au alikusudia kukataza baadhi ya vitu pasipo na vingine, au alikusudia kukataza kwa kujitakasa, na hatutofautishi kati ya marufuku ya Mtume, S.A.W., isipokuwa kwa dalili kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu au kitu ambacho Waislamu hawakutofautiana nacho.” Imamu Shafi'i alisema katika kitabu chake cha: [Ar-Risalah 2/352, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Amri yake kuhusu kula kutoka mbele upande wa sahani yake au kula kutoka kati kati ya chakula kama iliruhusiwa kwake kula kutoka mbele yake na kula chakula chote basi amri yake haikuwa isipokuwa kwa ajili ya kuhifadhi adabu ya kula kutoka mbele ya upande wa sahani yake; Kwa sababu hali hii ni nzuri zaidi na itakuwa mbali naye kutokana na ubaya wa ulafi katika kula, na amri yake Mtume alipoitoa kwa yule Swahaba kwamba asile kutoka katikati ya chakula ni kwa sababu baraka huteremka kutoka upande wake ili Mwenyezi Mungu Mtukufu ambariki baraka ya kudumu, na anamruhusu kula kile kilicho karibu na katikati ya chakula kwa kuwa anaruhusiwa kula kilicho katikati yake.
Na katika kitabu cha: [At-Tamhiid kwa Ibn Abd Al-Barr 3/215, Ch. ya Wizara ya Waqfu ya Moroko, Mnamo Mwaka wa 1387 AH] wakati akielezea Hadithi hiyo: “Nilikukatazeni kula nyama za vichinjwa baada ya siku tatu, basi kuleni, toeni sadaka na wekeni akiba, na nilikukatazeni kuweka zabibu au tende katika maji kisha mnayanywa, basi inaruhusiwa kufanya hivyo...” Akasema: “Na katika Hadithi hii kwamba hukumu ya marufuku ni kuliacha jambo lilalokatazwa na kutolifanya, na kwamba Katazo hilo maana yake ni kuharamisha jambo hadi inapoambatana nalo dalili inayoligeuza jambo hilo kutoka sehemu hii hadi mlango wa kuelekeza na kukokoteza. Pia anasema (1/140, 141): “Kuhusu yaliyotajwa juu ya Zuio au Katazo kwa ajili ya adabu na kutendeana vizuri na kumwongoza mtu, ni kama Katazo la Mtume S.A.W., kwa mtu mmoja kutembea kwa kiatu kimoja tu, na kula tende mbili kwa pamoja, na kula kuanzia katikati ya chombo. Na kunywa kwa mdomo wa chupa moja kwa moja, na mambo mengi kama hayo, yalifahamika makusudio yake... Mtume amekataza kula kuanzia katikati ya chombo, kwa sababu baraka huanzia mwanzo wa upande kwake, na amekataza kula tende mbili kwa pamoja, kwa sababu hii ni tabia mbaya mtu anapokula pamoja na mwenzake akala tende mbili kwa pamoja, na mwenzake akala tende moja tu, kwa hivyo anayefanya hivyo hana aibu. Vile vile Katazo lake kwa mtu anayekunywa kwa mdomo wa chupa moja kwa moja kwa kuogopa viumbi lenye madhara, kwa sababu midomo ya chupa za maji imeelekewa na viumbi hilo ambalo lina madhara, na huwenda katika mdomo wa chupa kuna aina yoyote ya madhara.
Al-Hafiz anasema katika kitabu cha [Al-Fath 9/523, Ch. ya Dar Al-Maarifa – Beirut] wakati alipoeleza Hadithi ya Mtume S.A.W., alipomwaamuru Amr ibn Salamah kula kwa mkono wake wa kulia: “Al-Qurtubiy alisema: amri Hii ni kwa ajili ya kupendeza tu, kwa sababu ni suala la kuuheshimu mkono wa kulia zaidi kuliko mkono wa kushoto; kwa sababu una nguvu zaidi, na unafanya kazi haraka zaidi, na Mwenyezi Mungu amewapa heshima watu wa Peponi kwani walitambulishwa kwa kuwa watu wa upande wa kulia, na kinyume chao ni watu wa upande wa kushoto. Alisema: kwa ujumla, kwa hivyo basi upande wa kulia na kinachohusika nao na kile kinachotokana nao kinasifiwa kwa lugha na Sheria na Dini, na upande wa kushoto ni kinyume na hayo. Kama ikiamuliwa hivyo, ni kutokana na adabu inayofaa kwa maadili na tabia nzuri wa wema kuainisha mkono wa kulia kwa ajili ya vitendo vya heshima na hali safi. Alisema pia: Amri hizi zote ni kwa ajili ya tabia nzuri na maadili mema, na asili yake ni kwa ajili ya mambo ya kupendeza.”
Alisema pia (1/253): "(Kauli yake: Sura kuhusu Katazo la kustanji kwa mkono wa kulia) na anaelezea makatazo mengine huku akiashiria kwamba haikuonekana kwake ikiwa makatazo hayo ni kwa ajili ya marufuku au ni kwa ajili ya kutakasa, au kwamba ni ishara inayogeuza hali ya kukataza kwa kuharamisha haikuonekana kwake, yaani, kwamba hali hii ni adabu miongoni mwa maadili na kwani ni kwa ajili ya kutakasa.
Inadhihirisha kuwa kugeuza ishara hiyo kwa amri na katazo kutoka katika hali inayowajibisha inatokana na kauli ya wanavyuoni wengi kwamba amri hii inaleta uwajibu na katazo linaleta Uharamishaji, na kwa maneno ya wale wanaosema kwa pamoja, kukokotezwa au kuchukiza kunathibitishwa kwa masuala ya adabu na mila kwa anayesema kwamba mfumo wa amri ambao hauna ishara yoyote una maana ya kukokoteza na mfumo wa kukataza una maana ya kuchukiza.
“Mila” maana yake ni hali ambayo watu wameiendeleza na kuirudia rudia”. [Mujaam maqayiis Al-Lugha 4/181, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Kuhusu maana ya “Mila” katika istilahi, kuna tofauti kati ya wanavyuoni, na tofauti hii inatokana na kuzingatia uhusiano kati ya mila na desturi, kwa hivyo aliyeona kwamba maneno haya mawili ni visawe, alifafanua kama: “Ni ile hali ambayo watu wameiendeleza kwa mujibu wa akili, na wamekuwa wakiikariri,” ambapo huu ni ufafanuzi wa Jerjani, na maana ile ile iliyosemwa na Al-Hamawi katika kitabu cha: [Shari Al-Ashbah. At-Tarifaat, uk. 188, Ghamz Uyuun Al-Basaair 1/295, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, Toleo la Kwanza, Mmwaka wa 1405 AH]. Al-Hamwi alisema, akinukuu kutoka kwa kitabu cha: [Al-Siraj Al-Hindi]: “Mila ni kile kinachokaa katika nafsi, nacho ni mojawapo ya masuala yanayokaririwa na mtu mwenye tabia inayokubalika. Hiyo ndio maana iliyosemwa na Ibn Abdin: “Mila ni kile kinachokaririwa, kwa sababu kinarudiwa rudiwa mara nyingi na kinajulikana katika nafsi na akili zinazopokelewa kwa kukubalika bila uhusiano au ishara hadi kikawa uhalisia wa kimila, na kwa hivyo basi mila na desturi ina maana moja, ingawa zinatofautiana katika suala la dhana.” [Nashr Al-Urf, miongoni mwa jumbe zake 2/114].
Na miongoni mwa wanavyuoni ambao walikusanya kati ya mila na kigezo (kinachokubaliwa na watu) ujumla na umaalumu kabisa, lakini walitofautiana katika tabia ya maoni mawili: La kwanza: kukifanya kigezo kuwa ni cha jumla zaidi, na mila ni sehemu ya kigezo hicho, na kwa hivyo basi, mila inahusishwa na kitendo zaidi. Ibn Al-Hamam anasema: “Mila: ni jambo linalorudiwa, hata bila uhusiano wa kiakili, na kinachomaanishwa hapa ni kigezo cha vitendo." [Taysiir Al-Tahriir 1/386, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Tofauti hii kati ya mila na kigezo ni moja ya maana inayoeleweka kutokana na maneno ya Al-Fakhr Al-Bazdawi, ambapo alipotofautisha kati ya dhana ya mila na dhana ya matumizi, alisema: “Nazo ni aina tano ambazo zinaweza kubaki na dhana ya mila na matumizi.” [Usuul Al-Bazdawi Bihamish Sharhu Kashf Al-Asrar 2/95, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy]. Kinachokusudiwa kwa matumizi ni mambo ambayo yanasemwa kwa kukaririwa mara kwa mara, ambayo ni kila neno lililogeuzwa kutoka katika maana yake ya kweli kwenda katika maana isiyo ya kweli katika Sheria au kigezo hadi ikawa ukweli ndani yake, na maana ya asili ikaachwa au kama ilivyoachwa, na hiyo ndiyo kama ilivyo katika maana ya sala na wanyama. Kuhusu mila, ni jambo linalohusishwa na kitenzo zaidi, ambalo ni kila neno lililogeuzwa kutoka katika maana yake halisi na kuwa na maana yake isiyo halisi, lakini halikuachana na maana yake halisi, na hiyo ni kama kuapa kutokula kichwa, kwa hivyo Abu Hanifa alieleza maana hii kwamba kinachokusudiwa ni kichwa cha ng'ombe na kondoo siyo kichwa cha ngamia kwa ajili ya kupendelea.
La pili: Aliendelea kusema kuwa mila hiyo ni ya jumla zaidi kuliko kigezo, ili kutofautisha kati ya mila inayotokana na mtu mmoja na ile inayotokana na kundi la watu. Na miongoni mwa waliosema maoni hayo ni Sheikh Abu Sinnah katika kitabu chake cha: [Al-Urfu wal Ada, uk. 13, Ch. ya Matbatul Azhar, 1947], Al-Zarqa katika kitabu cha [Al-Madkhal 1/874, aya 485, Ch. ya Dar Al-Qalam, Toleo la Kwanza, 1418 AH].
Kuhusu “Adabu”, maana yake katika lugha ni dua, na “Adabu” imeitwa hivyo; Kwa sababu inakusanya watu kwa ajili ya kutekeleza maadili. [Lisan Al-Arab 1/206, Kidahizo cha Adab)].
Na maana ya Adabu kawaida istilahi siyo mbali na maana yake ya kilugha, kwa hivyo inaitwa sifa nzuri ambazo mtu anapaswa kuwa nazo, na kutoka kwake imesemwa: Adabu za kutia udhu, Adabu za Mufti na kadhalika, ambayo ni mambo yanayopaswa kufanyika. Pia adabu inaitwa kuweka vitu katika mahala pake, na wanavyuoni wa Fiqhi wanatumia neno hilo kwa kukusudia jambo linalokokotezwa, na wanaelezea maana hii kwa maneno kadhaa, pamoja na: Sunnah, mustahab, na jambo ambalo kulifanywa kwake ni bora kuliko kuliachwa, na kadhalika. [Al-Mawsuah Al-Fiqhiyah 2/346, Istilahi ya: Adabu].
Miongoni mwa adabu ambazo zimetajwa katika matini za kisheria zinazohusiana na uagizaji au ukatazaji, ni kuamurisha kula na kunywa kwa mkono wa kulia, na kutostanji kwa mkono ule ule wa kulia, na kuamurisha kula kuanzia upande ulio mbele ya mtu moja kwa moja, na kumkataza kula kuanzia katikati ya sahani, na kukataza kushikilia Uume wake wakati wa kukojoa, na kutembea akiwa amevaa kiatu kimoja, vile vile kukataza kupumulia ndani ya chupa, na kula tende mbili kwa wakati pamoja, na kadhalika kutoka kwa adabu. Kati ya mila ambazo zimetajwa katika matini za kisheria ni kukataza kubadilisha rangi ya nywele za kijivu, na kuamurisha kuziachia ndevu na kutozinyoa.
Kuhusu kula kwa mkono wa kulia, kwa mfano, imepokelewa kutoka kwa Amru Ibn Salama Hadithi inayoamurisha hivyo akisema: “Nilikuwa kijana mdogo chini ya ulezi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., na mkono wangu ulikuwa ukizungukazunguka kwenye bakuli, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., akaniambia: “Ewe kijana: taja jina la Mwenyezi Mungu, na kula kwa mkono wako wa kulia, na ule kilicho mbele yako. ”(Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari na Muslim).
Vile vile imepokelewa kukataza kula kwa mkono wa kushoto katika Hadithi ya Ibn Omar kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., amesema: “Hairuhusiwi kwa yeyote kati yenu kula au kunywa kwa mkono wake wa kushoto.” (Imepokelewa kutoka kwa Muslim).
Wanavyuoni wengi wanaamini kwamba kula kwa mkono wa kulia ni jambo ambalo linalopendeza, na kula kwa mkono wa kushoto ni jambo ambalo linachukiza; Kwa sababu hili ni suala la adabu, na wakati wa kuwa kwake ni adabu, ikawa hukumu yake inakokotezwa, kulingana na Ibn Abd Al-Barr katika kitabu cha: [Al-Istidhkaar 5/288, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, Toleo la Kwanza, Mwaka 1421 AH] alisema: “Asili ya kukataza ni kwamba uangalie jambo linalokatazwa kama unalimiliki au hulimiliki, kama utakuwa unalimiliki, basi ni miongoni mwa adabu na kuna uwezekano wa kuchagua kulifanya au kutolifanya, na lile ambalo hulimiliki basi litakuwa limeharimishwa. Je! Hauoni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alikataza kunywa na kustanji kwa mkono wa kulia bali kwa iwe kwa mkono wa kushoto tu na alikataza kula kwa mkono wa kushoto bali kwa kuwe kwa mkono wa kulia tu. Mambo hayo yote ni miongoni mwa adabu, kwa sababu yanamilikiwa na mwanadamu, na atakayefanya lolote kati ya hayo sio marufuku kulifanya, na lolote linalohusiana na chakula chake au mavazi yake.
Kuhusu Hadithi inayohusiana na anayekula kwa mkono wake wa kushoto ni shetani, Hadithi hii haimaanishi kuharamisha, na kuna Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume S.A.W., anasema: “Pindi atakapokula mmoja wenu ale kwa mkono wake wa kulia, na akinywa anywe kwa mkono wake wa kulia, akichukua achukue kwa mkono wake wa kulia, akitoa basi na atoe kwa mkono wake wa kulia, hakika shaitwani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto, na anatoa kwa mkono wake wa kushoto, na anachukua kwa mkono wake wa kushoto.”' Lakini, hakuna mtu yeyote aliyesema kuwa ni wajibu kufanya mambo hayo kwa mkono wa kulia, lakini wameafikiana Wanachuoni kuwa hayo yote yanakokotezwa tu.
Na dua ya Mtume, S.A.W., kwa yule aliyekula kwa mkono wake wa kushoto haimaanishi uharimishaji pia, na wanavyuoni wa fiqhi wamejitahidi kuifafanua hali hiyo, Al-Qadhi Ayad alisema kwamba mtu yule alikuwa mnafiki, kama inavyothibitishwa kupitia kukataa kwake amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kiburi na majivuno. Al-Manawi anasema katika kitabu cha: [Fayd al-Qadeer]: “Na dua yake Mtume S.A.W., dhidi ya mtu yule ni kwa sababu ya kiburi chake ambacho kilimpelekea kuachana na utii, kama inavyoonekana.” Na inaruhusiwa kuomba dua dhidi ya yeyote ambaye hali yake inafanana na hali ya mtu yule, wakati ambapo Al-Nawawiy anaona kuwa kuomba dua dhidi ya mtu yule ilikuwa kwa ajili ya kuikiuka hukumu ya Kiislamu kwa ujumla, na dua sio lazima iwe kwa ajili ya kuachwa wajibu au kufanya vitendo vilivyokatazwa.
Kuhusu kuacha nywele za ndevu, ilitajwa katika Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa kundi la masahaba, na pia ilithibitishwa na Sunnah ya Mtume, S.A.W. ya kivitendo: miongoni mwa Hadithi za Mtume kuhusu jambo hilo ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Jabir ibn Samra katika Sahih ambayo ilisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alikuwa na mvi katika sehemu ya mbele ya kichwa chake na ndevu, akiweka mafuta nywele hizi zinaficha, na kama nywele zake zikitawanyika basi mvi zake hazifichi, na alikuwa na ndevu nyingi... (Imepokelewa kutoka kwa Muslim).
Pamoja na Hadithi hizi kuna Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ali bin Abi Talib aliposema: “Mtume S.A.W., alikuwa na kichwa kikubwa, Rangi ya ngozi yake ilikuwa ile nyeupe-nyekundu, mikono yake na miguu yake mikubwa, na alikuwa na ndevu nyingi.” (Imepokelewa kutoka kwa Ahmad).
Vile vile kuna Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Bara ibn Azib, ambaye alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alikuwa na mabega mapana na ndevu zake zilikuwa nyingi.” (Imepokelewa kutoka kwa Al-Nasai).
Lakini, Hadithi hizi hazisimami peke yake kama dalili ya kuwa ndevu lazima ziachwe na kwamba ni marufuku kuzinyoa. Kwa sababu kuacha kwa Mtume S.A.W. ndevu zake ilikuwa kufuatana na kawaida ya Waarabu na desturi yao kwa hilo, bila kuhusishwa na dini, makafiri wa Kikoreshi na miongoni mwao Abu Jahl walikuwa na ndevu pia, na kisa cha Omar kinachojulikana kabla ya kusilimu na kuwa mwislamu wakati alipomwua binti yake na kwamba binti yake alikuwa akisafisha ndevu zake kwa kuondosha udongo wakati alipokuwa akichimba shimo la kumfukia binti huyo. Waarabu walikuwa walikuwa hawanyoi ndevu zao, na mpaka walifikia hatua ya kumlaumu mtu anayefanya hivyo, na walikuwa wanazingatia kwamba kung'oa ndevu au sehemu ya ndevu hizo ni tusi kubwa kwa mwenye ndevu kujidhumulumu, lakini badala yake walikuwa wakiapa kwa ndevu hizi, na kiapo hicho kilikuwa kinazingstiwa kuwa ni kikubwa mno.
Kuhusu mambo yote yanayofanana na mambo hayo miongoni mwa vitendo vyake Mtume, S.A.W., na yalikuwa yanaambatana na Sheria yanapokuwa ya Kuagiza au Kukataza basi hukumu yake siyo wajibu au lazima, na yakiwa hayaambatani na Sheria, basi hukumu yake ni kwamba yanapendeza kuyafanya kwake, Al-Ghazaliy katika kitabu cha: [Al-Mustaswfa 2/214] anasema wakati alipozungumzia maana ya vitendo vya Mtume S.A.W.: “Kuna taarifa ya wajibu, kama vile kauli yake Mtume, S.A.W.: “Salini kama mlivyoniona mimi nikisali” na “Chukueni kutoka kwangu ibada zenu.”
Kwa sababu hii, Sheikh Mahmoud Shaltout, Mwenyezi Mungu amrehemu, anasema katika “Fatwa zake” [uk. 229, Ch. ya Dar Al-Shorouk): “Ukweli ni kwamba suala la mavazi na sura za mtu binafsi, pamoja na kunyoa ndevu, ni moja ya mila ambazo mtu anapaswa kuzingatia yanayokubalika katika Jamii yake. Na asiyeifuata Jamii yake, basi anakuwa ameukiuka mfumo wa maisha yao”
Kuhusu suala hilo, lilikuja katika Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa masahaba kadhaa, pamoja na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Omar, kutoka kwa Mtume, S.A.W., aliposema: “Jitofautisheni na washirikina, kithirisheni kuacha ndevu, na punguzeni masharubu”.
Na amri iliyotajwa katika Hadithi hii ilitajwa kwa sababu ya kutofautiana na washirikina, na ina maana kwamba hukumu iliyomo ndani yake ni hukumu ya busara ambayo haiwezi kukubaliwa kabisa wala huzingatiwa bila sababu hiyo, na agizo la kujitofautisha hapa halifikii ngazi ya uwajibu, kwa sababu kama ingekuwa hivyo, basi uwajibu huu ungekuwa lazima uthibitishwe na kila aina ya ukiukwaji huu, na haikuthibitishwa hivyo, kwa sababu agizo lilikuja pamoja na mambo ambayo yameelezwa na kupingana kwa washirikina, na wengine walikubali kwamba baadhi yake sio ya lazima, pamoja na Hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Abu Hurairah, ambaye alisema: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., alisema: “Hakika Mayahudi na Manasara hawatii rangi mvi zao basi nendeni kinyume nao” , lakini, imeripotiwa kuwa baadhi ya masahaba wa Mtume S.A.W., walikuwa wakijiepusha na kutia rangi, na kama kufanya hivyo ingelikuwa ni lazima, basi haingeruhusiwa kuepukana na lazima hiyo.
Sheikh Abdul Aziz Al-Ghammariy amesema: “Wanavyuoni wengi walikubaliana kwamba kutia rangi hiyo ni Sunnah tu, ingawa kuepukana nayo ni kujifananisha na Mayahudi na Manasara.” [Ifadat Dhawi Al-Afhaam bian Halq Allihyah Makruh walisa Haraam, uk. 54, Ch. ya Dar Al-Athar Al-Islamiyah]
Pia miongoni mwa mambo hayo ni kusali hali ya kuvaa viatu. Katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Shaddad Ibn Aws kutoka kwa baba yake, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., amesema: “Nendeni kinyume na Mayahudi, kwa sababu wao hawasali na viatu wala hufu zao.” Pamoja na hayo, wanavyuoni wa Fiqhi wanakubaliana kuwa mambo hayo sio wajibu, hata kama wakitofautiana kwenye Usunnah wake.
Licha ya hayo, Hadithi ya sifa kumi ni dalili kwamba ndevu ni moja ya Sunnah, na sio moja ya mambo ambayo ni Wajibu.
Dalili ya kwamba agizo au katazo vinahusiana na adabu, nazo ni miongoni mwa mambo mazuri yanayokokotezwa. Ibn Rushd anasema katika kitabu cha: [Bidayatul Mujtahid 1/65, Ch. ya Dar Al-Fikr]: “Nyingi miongoni mwa hukumu zinazokubaliwa kiakili katika Sheria ni miongoni mwa adabu, au kutoka katika sehemu inayohusiana na masilahi, na hizi ndizo zinazokokotezwa.
Kuhusu suala la agizo au katazo vinahusiana na mila, Al-Zarkashi alitaja kutoka kwa Al-Qaffal katika kitabu cha: [Al-Bahr Al-Muhiit 2/364]: "Chochote kinachoweza kuwa dalili juu ya kuainisha jambo la ujumla kinaweza kuwa dalili pia juu ya kwamba agizo sio kwa uwajibu.”
Kuhusiana na ujumla na mila sio kawaida, lakini badala yake ni pamoja na maelezo. Mila hiyo inaweza kuwa ya kimaneno au ya kivitendo. Na jambo ambalo ni muhimu zaidi ni kuhusisha ujumla bila ubishani. (Rejea: Nihatul Suul 2/469). La pili ikiwa ni ya dharura kwa ujumla, basi kujua kulitokeaq katika zama ya Mtume, S.A.W., pamoja na kutolizuia, basi unahusishwa ujumla huo - na unaohusishwa ni kukiri kwake Mtume S.A.W., hata ikifahamika kutotokea kwake basi haihusishwi. Imetajwa katika kitabu cha: [Sharh Al-Mahali ala Jamu Al-Jawamii 2/34]: "(Na) ni sahihi zaidi (kwamba mila ya kuacha baadhi ya maagizo) au kufanya baadhi ya mambo yaliyokatazwa kwa utaratibu wa ujumla (inahusishwa) ujumla, yaani inaainishwa kwa yoyote isipokuwa yaliyoachwa au yaliyofanyiwa kazi (yaliyopitishwa na Mtume S.A.W.) kwamba mambo hayo yalikuwa katika zama zake na aliyajua na hakuyakataza (au kukubaliana nayo) kwamba watu waliyafanya bila ya wao kuyakana, na yaliyohusishwa kwa ukweli ni yale yaliyopitishwa au yaliyokubaliwa na Wanavyuoni wengi. Al-Attar anasema: “Kinachokusudiwa ni mila inayofuata baada ya kutajwa kwa ujumla.”
Ikiwa mila itautangulia ujumla, basi kuna kutokukubaliana kati ya Wanavyuoni, baadhi yao wanaona kutenganisha, na wengine wanasema kwa ujumla. Assafi Al-Hindi anasema katika kitabu cha: [Ghatul Wsuul 5/1759, Ch. ya Al-Maktaba At-Tujariyah - Makkah Al-Mukarramah]: “Ya pili ni kwamba mila hiyo inaendelea na tendo fulani, kama vile kula chakula fulani, kwa mfano. Halafu Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., akawakataza kwa kuwaambia: Niliwakatazeni kula chakula hicho, je, Katazo hilo linahusisha kula chakula hicho tu, au linafanyika kwa ujumla wake na hauathiri mila yao katika hilo.
Sahihi zaidi - kama ilivyoainishwa na Ibn Al-Subki - kwamba mila kama hiyo haiainishi ujumla, na Ibn Al-Hajeb alisema: “Ni kweli.” [Sharhul Adhud 3/85, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]. Lakini, Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa wanakubali kwamba mila kama hiyo imeainisha kwa ujumla, na katika rai hiyo baadhi ya Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Maliki walisema hivyo, Al-Baji anasema katika kitabu cha [Ihkaam Al-Fusuul]: “Inaruhusiwa kuainisha ujumla wa mila, na hivyo ndivyo alivyosema Ibn Khuwayz Mendad, kwa sababu neno linapotajwa, linachukuliwa kulingana na kigezo cha watu wanaolitamka. Na Al-Qadhi Abu Muhammad alisema: Ikiwa kigezo kinatokana na upande wa kitendo, basi kigezo hicho hakikuainisha, na ikiwa kigezo kinatokana na upande wa kusemwa, kinaainisha. [uk.275. Dar Al-Gharb Al-Islami].
Na imetajwa katika maelezo ya Sheikh Jait juu ya [Sharhu At-Tanqiih” na Al-Qarafi 2/53, Ch. ya Matbat Al-Nahdha - Tunis, 1926 BK]: “Katika maswala ya Kitabu cha Wakalat kutoka Msimbo na vitabu vingine vya madhehebu, zinayoonesha dalili kuainisha kwa vitendo, hata ikiwa ni pekee.”
Ikumbukwe kwamba mwenendo wa Wananvyuoni wa Fiqhi katika masuala haya, unaonesha kuwa hawazingatii tofauti kati ya mila ya kusema na ya kutekeleza, na kwamba ujumla unaainishwa kwa moja kati yao, na kuhusu hali hii Sheikh Jait [2/54]) anasema: “Dhahiri ya masuala ya Wanavyuoni wa Fiqhi ni kwamba hakuna tofauti kati ya kuwa kigezo cha kusema au cha kivitendo.” Al-Dusouqiy alisema katika Hashiya yake, akimpinga mwandishi wa kitabu cha Mukhtasar Khalil, ambaye alichukulia kuwa kigezo cha kusema kinaweza kuainishwa tofauti na kigezo cha kivitendo: “Kile kilichotajwa na mkusanyaji hapa na kwa ufafanuzi ni kwamba kigezo cha kivitendo hakikuzingatiwa, na mwelekeo huu umefuatwa na Al-Qurafiy. Ibn Abd Assalam alitaja kwamba masuala ya Wanavyuoni wa Fiqhi yanadhihirisha kuzingatiwa kwa kigezo hata kikiwa cha kivitendo. Al-Wanughi alitaja kutoka kwa Al-Baji, kwamba alisema kuwa kigezo kinachukuliwa kuwa maalum na kinazuiliwa, na akasema: Inajibiwa hivyo kwa yale aliyoyadai Al-Qarafiy, na Al-Lakhmiy alisema kuwa kinazingatiwa pia, na katika Al-Qalishani: Hakuna tofauti kati ya kigezi cha kusema na kigezo cha kivitendo katika uwazi wa maswala ya Wanavyuoni wa Fiqhi. [Hashiyat Al-Dusouqi 2/140, Ch. ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah] Lakini Al-Sibki anasema kwamba mila ya kivitendo ikitajwa mara nyingi inaainisha ujumla wa makubaliano ya Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Shafiy. [Takmilat Al-Majmuu 11/124, Ch. ya Maktabat Al-Irshaad]
Na ikiwa imeamuliwa kuwa mila ya kusema inaainisha ujumla, na vile vile ya kivitendo, basi inaruhusiwa kuonesha kwamba hali hii ni miongoni mwa dalili zinazogeuza wajibu kuwa agizo, kama ilivyoainishwa kwa maneno ya Al-Qaffal.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas