Hati ya Uaminifu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hati ya Uaminifu

Question

Je, Sheria inalazimisha kuandika Deni katika Waraka wa Uaminifu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwa jinsi ilivyoamuliwa kisheria ni kuwa kila kinachomshughulisha mtu katika mali na akawa anatakiwa kukitekeleza kinazingatiwa kuwa ni Deni.
Aubaidu Allah Bin Masoud alisema katika kile kinachojulikana kama (Wito wa Sheria) kitabu cha: [At Tawdhieh Fii Sharhi Ghawamedh At Tanqeeh 132-133/2, Ch. ya Maktabat Swubaih]: "Deni: ni kuwajibika kwa haki iliyo katika dhimma ya mtu". (Mwisho)
Na Kuandika ni katika njia za kuhifadhi kumbukumbu za Deni kisheria. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni}. [AL BAQARAH 282]
Na Wanachuoni wemekubaliana wote juu ya kutakiwa Uthibitisho katika waraka kisha wakatofautiana baada ya hapo katika kiwango kinachotakiwa, wapo miongoni mwa Wema waliotangulia, waliosema; ni Wajibu kuwa na uthibitisho kwa Maandishi, na Jamhuri ya Wanachuoni wa Fiqhi, wa Madhehebu ya Imamu Maliki, Shafiy, Hanafi na wa Hanbali, wanaona ya kwamba inapendeza kufanya hivyo, na dalili waliyoitoa ni kwamba amri iliyopo kwenye Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {basi andikeni} ina maana ya Sunna na kuongoza; kwani Mwenye kudai ana haki ya kudai au kusamehe kwa makubaliano ya Wanachuoni wote, kwani Sunna ya kuelekea katika Uandishi wa Deni hakika mambo yalivyo ni kwa ajili ya kumbukumbu kwa watu; kwa kuchelea kugoma mwishoni, na kuepusha mzozo na ugomvi. [Tazama Tafsiri ya Al Qortwubiy 383/3, Ch. ya Dar Ihiyaa At Turaath Al Arabiy]
Na Kadhalika basi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu baada ya hayo: {Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake}. [AL BAQARAH 283], Inaonekana kuwa Uandishi hauhitajiki kama uaminifu utakuwepo baina ya wenye kukopeshana, na kwa hivyo Amri ya Kuandika iliyomo ndani ya Qur'ani inakuwa ni Sunna na Mwongozo, na wala sio wajibu wa kutekelezwa kwake.
Ibn Al Arabiy Al Malikiy amesema katika kitabu cha: [Ahkaam Al Qur'aan 328/1, Ch. ya Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ;{Basi andikeni}; Anataka iwe Hati ya kumbukumbu ili ajikumbushie kwayo muda wake wa malipo; kutokana na kutegemewa kujisahau katika muda ambao ni wa baina ya muamala na utatuzi wa kipindi cha kulipa kilichowekwa, na kusahau kunabebwa na Mtu, na Shetani huwenda akasababisha mtu kulikana deni, na yanayoweza kujitokeza kama Kifo na mengine na kwa ajili hiyo pakawekwa utaratibu wa kuandika na kuweka ushahidi".
Na Imamu As Sarkhasiy alitaja katika kitabu cha: [Al Mabsuotw 168/30, Ch. ya Dar Al Maarifah] Faida za kuandika kwa ajili ya kuzihifadhi haki, na akasema:
"Moja ya faida hizo ni: Kuzilinda Mali na tumeamrishwa kuzilinda Mali na tukakatazwa kuzipoteza".
Na faida ya Pili: "Kumaliza ugomvi, kwani Kuandika kunakuwa mwamuzi mzuri baina ya wawili wanaoamiliana na wanarejea katika maandishi pale mzozo unapojitokeza, na inakuwa ni sababu ya kutuliza fitna, na hakuna yoyote kati yao anaeizuia haki ya mwingine; kwa kuchelea asije Mwandishi akatoka na Mashahidi wakashuhudia jambo hilo, na akaumbuka kwa ubaya mbele ya watu".
Na faida ya Tatu: "Kujikinga na mikataba mibovu; kwani Wawili wenyekuamiliana huwenda wasijielekeze kwenye mikataba mibovu kwa ajili ya kuifunga na ili wajiepushe nayo. Na kwa hivyo Mwandishi akawaelekeza katika hilo ikiwa watarejea kwake kwa ajili ya kuandika".
Na faida ya Nne: "Kuondosha shaka shaka; huwenda Watu Wawili wanaoamiliana wakashukiwa - kama muda utakuwa mrefu sana - Kiwango cha mbadala na Kiwango cha Muda, na wanaporejea kwa Mwandishi basi hakuna Shaka yoyote kati yao inayoweza kubakia. Na kadhalika baada ya mauti yao, shakashaka inatokea kwa mrithi, kila mmoja miongoni mwao kutokana na yaliyodhahiri katika kawaida ya wengi wa watu katika kutotendea amana kama inavyotakiwa, na wanaporejea kwenye Hati ya Uaminifu, hakuna shakashaka yoyote baina yao inayoweza kujitokeza".
Na hati ya Uaminifu ya amana inatuzunguka kwa watu hivi sasa haiwi isipokuwa waraka ulioandikwa ndani yake deni; na iwe ni kwa kuandikwa jina la mdai na jina la mdaiwa pamoja na saini yake au muhuri wake maalumu, na vilevile Kiwango cha Deni hilo. Na labda huwenda pakatajwa ndani yake muda wa kulilipa deni hilo, na kwa hivyo kilichoandikwa ndani ya waraka huo kinakuwa sawa na kukiri kwa mdaiwa haki iliyoandikwa ndani yake juu ya mdaiwa na analazimika kulipa na kuhukumiwa kwa mujibu wa waraka huo pindi itakapobidi.
Na hati ya amana hata kama tamko lake la asili halikuwa la wazi kwa maana ya kidini basi hakika desturi iliyozoeleka katika matumizi yake kama vile waraka wa deni, itarekebishwa matumizi yake ndani yake, na maneno ya kila Mtu huchukuliwa kwa mujibu wa lugha na desturi yake hata kama yataenda kinyume na sheria na desturi zake.
Na mbeba jukumu anapaswa kupanga mambo yanayohusu namna ya hati ya amana baina ya watu na adhabu ya kutolipa fedha ambazo zimo kwenye deni hilo kwa mujibu wa aonavyo inaendana na masilahi ya umma; na yeye ana jukumu la kupangilia adhabu anayoiona inafaa kwa mwenye kukataa kulipa fedha za watu; ambapo hakika mambo yalivyo haikupokelewa adhabu yoyote iliyopangwa kisheria kuhusu kosa hilo, na kwa hivyo ikawa adhabu yake ni katika mlango wa kuadabishwa na kuonywa (Taaziri); Nazo ni adhabu zinazohusu Kutenda maasi ambayo hayana adhabu maalumu iliyoainishwa kisheria. Na uamuzi wa kiwango cha adhabu hizi kwa kiasi chake na jinsi zilivyo, kunamuhusisha zaidi Kiongozi mwenye kubeba jukumu hilo na kukadiria Kiwango hicho, kwa lengo la kumkanya mtendaji wa kosa husika kwa upande mmoja, na kumfunza adabu kwa upande mwingine.
Al Mawardiy amesema katika kitabu cha: [Al Ahkaam As Sultwaniayah Uk. 293, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: Kukanya ni kuadhibu kwa makosa ambayo hayajawekewa na Sheria kiwango cha adhabu, na hukumu yake hutofautiana kwa kutofautiana hali ya kosa na hali ya mkosaji, na huafikiana na adhabu maalumu kwa upande mmoja, kwa kuwa huko ni kuadabisha kwa ajili ya kurekebisha na kukemea na kinatofautiana kwa kutofautiana kosa.
Na kutokana na hayo yaliyotangulia, hakuna kizuizi chochote cha kisheria kinachofanya hati ya amana iwe ni njia ya kuyalinda madeni na kuyalipa, na upangaji wa kiwango cha adhabu ya mdaiwa ambaye inathibitika kuwa anachelewesha kulipa Deni lake, ambapo inakusanya pia hati ya amana aliyobebeshwa kwa adhabu zilizopangwa kisharia.
Ama madai ya kutokuwa na usheria wa hati hiyo ya amana kama kiambata ambacho ni waraka wa kisheria unaozingatiwa au kutokuwapo msingi wa kisheria wa adhabu inayotokana na kutolipa, basi hakika jambo hili ni katika mambo ambayo wahusika hurejewa, na Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misri sio upande bobezi wa kuyaingilia masuala ya aina hii.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Ofisi ya Kutoa Fatwa

 

Share this:

Related Fatwas