Zama za Sasa na Sifa Zake kwa Mtaza...

Egypt's Dar Al-Ifta

Zama za Sasa na Sifa Zake kwa Mtazamo wa Kiislamu

Question

Ni zipi sifa za zama za sasa ambazo tunaishi? Na ni vipi tunazifanyia kazi kutokana na mtazamo wa fikra ya Kiislamu? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Sifa hizo tunazikusanya kwa ujumla wake kama ifuatavyo:-
1- Uraia: Nao ni matokeo ya ulinganiaji wa usawa kisha kuwa sawa katika kila kitu, usawa hata kama utakuwa ni asili yenye kuzingatiwa na kuwa sawa hata kama itakuwa ni mwenendo katika maeneo mengi isipokuwa uwingi wa ulinganio huu ni kuipa zama sifa hasi nayo ni kuondoka kwa umakini ambao ulikuwa ndio kichwa kwenye mwili, kufikiri na kuangalia kwa lengo la kuja na jambo linalokubaliana na kule kufikiri, na kufanya kazi sawa na kiwango cha elimu, sifa hii inakusanya uzuri wa kuondoa matabaka, nayo inakubaliana na tamko la Mtume S.A.W.: “Nyinyi nyote mnatokana na Adam na Adam anatokana na udongo” ( ). Ambapo inaelezea usawa pamoja na kulingania unyenyekevu, tofauti ni kuwa sifa hii inakusanya pia ubaya nao ni kuondoka kwa umakini hivyo Mola wetu ametuamrisha kutowapa ufunuo katika kila jambo ambapo Mola Mtukufu Amesema: {Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui} ( ).
2- Kwa sababu hiyo zama zimeitwa – kama ilivyoelezewa na Abdulwaahid Yahya mwanafalsafa Muislamu – kuwa ni zama za harakati zimetangulia fikra, na ilikuwa katika mfumo wa Kiislamu moyo unakuwa juu ya akili na akili ipo juu ya viungo hivyo ikawa maarufu hivi sasa kuwa viungo vinatangulia akili, ikiwa kuna matumizi ya akili yanatangulia moyo na kutoka kwenye muktadha wake.
3- Zama hizi zimekuwa na sifa za hisia za uwastani, na kuwa haki inaweza kuwa na pande nyingi, lakini Waislamu wanaona kuwa haki haiwezi kuwa na pande nyingi bali haki ni moja na uwastani huu umeathiri katika fasihi sanaa siasa jamii pamoja na harakati zingine za maisha, na kuamini moja kwa moja kulikuwa ni asili za zama zilizopita maeneo yote ya dunia mpaka ikaitwa zama za Imani kwa maana ya Faith Age.
Masuala yalianza kwa “Hegel” ambapo alijaribu kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo ambayo kwa msingi yanatokana na akili ya mwanadamu pindi anapoachana na ufunuo au kuupinga ufunuo, na kufikia yale aliyoyasema “Hegel” kwenye hisia hii ya uwastani au asilimia ambayo inasimamia matendo na tabia, ufupi wa falsafa ya “Hegel” ni kuwa: Mwenyezi Mungu yupo, ulimwengu upo, usasa ambao unaolinganiwa ikiwa na maana ya kuupa umuhimu huu ulimwengu, hivyo basi kuna fikra iliyotolewa inayopelekea kinyume, na kufanya rai yetu kuwa ni moja nayo ni kumfanya Mwenyezi Mungu ndio mfumbuzi katika ulimwengu huu, na kuwa ulimwengu ni Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni ulimwengu, na hii ina maanisha kuwa watu wa mtazamo wa nadharia ya vitu vinavyoonekana wapo sawa kwa sababu wao hawaoni isipokuwa ulimwengu, kisha wakaja watu wa nadharia za Marks wakachukuwa fikra inayotokana na falsafa hii na kuiteremsha kwenye nadharia ya uchumi na nchi.
Nietzsche (1900) amezingatia kuwa maneno ya Hegel ni mazuri, lakini alitaka kueleza zaidi ya maelezo ya Hegel ambapo alisema: Hakika Mwenyezi Mungu ni tofauti na ulimwengu, na Waumini wanaamini kuwa Mola ni Mola na mja ni mja, na kuna tofauti kati ya kiumbe na Muumba, na hii ndio imani ya watu wa dini zote kwani waanaamini kuwa Mwenyezi Mungu kitu na ulimwengu ni kitu kingine, kama alivyosema Mola Mtukufu ndani ya Qur`ani Tukufu: {Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika wanyama dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona} ( ).
Kisha akasema Nietzsche: Hakika Mwenyezi Mungu hayuko huko – kwa maana sio nje ya ulimwengu - na kuzingatia kuwa Mungu anayemzungumzia Hegel ameshakufa kwa sababu hayupo, Hegel akakubali kutokuwepo Mwenyezi Mungu nje ya ulimwengu, kisha akasema: Hivyo atakuwa hayupo, lengo la hayo ni kuwa ufunuo pia sio kweli ikiwa mwenye ufunuo amekufa, hivyo ufunuo pamoja na jumbe mbalimbali vimekuwa ni maelezo makubwa ya kale, na inakuwa hakuna chochote isipokuwa ni ulimwengu, na hii inaashiria jambo la ajabu sana ambalo linaipa sifa ya pekee akili au kile kinachoitwa sifa za akili.
Walikuwa wanataka kujitenga kikamilifu na Kanisa la Kikristo, na Kanisa – lilipinga elimu nyingi kama ilivyotajwa katika msimamo wa Papa kwa hotuba iliyoitwa “Basant” ikiwa ni katika kupambana na kujitenga na huu usasa kwa kutumia nguvu, Hegel alijaribu kuunganisha kati ya watu wa kisasa na watu wa Imani lakini Nietzsche alisema: Hakuna kitu cha kweli isipokuwa ni huu ulimwengu, wala hakuna Mungu sasa hivi.
Lakini madhehebu haya yanatufanya tujiulize: Ikiwa Mwenyezi Mungu hayupo basi ni namna gani tunahukumu vitu? Ni vipi tunafahamu kuwa ukweli uzuri kheri ni vitu vyenye sifa nzuri? Na vipi tunafahamu kuwa shari uongo dhuluma ni vitu vyenye sifa mbaya?
Watu wa fikra ya kutokuwepo Mungu wanalingania katika uwastani moja kwa moja, wanasema: Hakuna cha kusifiwa vizuri moja kwa moja wala kusifiwa sifa mbaya moja kwa moja lakini vitu hivi huwa vinasifiwa kwa uzuri kwa yule anayeona ni kizuri na kibaya kwa yule anayeona ni kibaya.
Hapa linazuka swali lingine nalo: Ni vipi tunauona ulimwengu? Mtazamo wao unatakiwa kuwa na jibu kuwa ni kama vile unavyoona, ikiwa mtazamo wako unaona ulimwengu ni wenye kuleta huzuni basi utakuwa mwenye huzuni kwa upande wako, na ikiwa kwa mwenzako anauona ni wenye kuleta furaha basi atakuwa ni mwenye furaha kwa upande wake, jambo linalotufanya tunachukuwa mfano wa kauli ya Mola wetu Mtukufu: {Je! Umemuona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hivi Hamkumbuki}( ).
Mwenyezi Mungu ameondoa katika imani yake na fikra zake na akaweka badala yake matamanio, na kwa sura hii anapoteza mdau kwenye maneno yake na kupotea kikamilifu faida ya maneno, kisha baada ya hapo kunazaliwa mpasuko na kuzaliwa dini za fujo.
Tulikuwa tunaenda kwa Sheikh au kwa Mtawa na kutaka miongozo yao katika yale yaliyotokea ili kupata usahihi kutokana na makosa, hivi sasa tunakwenda kwa nani ili kufahamu haki na batili? Wakasema: Hivi sasa unachukuwa haki yako kwa nguvu, ikiwa ni mwenye nguvu basi wewe upo kwenye sawa kwa sababu hakuna kipimo cha moja kwa moja cha haki na batili, vipimo vyote ni vya wastani kile unachoona wewe ni haki kwa masilahi yako binafsi mimi naona ni batili, na wala hakuna kinachonilazimisha mimi kukiamini wala kukulazimisha wewe kuamini kile ninacho amini mimi isipokuwa ni kutumia nguvu ndio ambayo inayopelekea kwenye hali halisi ya haki na batili.
Hivyo hali halisi ndio kipimo na hali hiyo hutengenezwa na mwenye nguvu zaidi, je hii inamaanisha kuwa uhusiano kati ya mwanamme na mwanamke utakuwa katika mwenendo huu? Kwa maana mwanamme atalazimisha hali halisi na kuwa hiyo ndio sahihi kwa sababu tu yeye ni mwenye nguvu kimwili? Tatizo linakuja ikiwa mwanamke ni mwenye nguvu zaidi ya mwanamme basi ni nani ataainisha usahihi na kuleta hali halisi? Katika miaka ya sitini tulimkuta mwanamke anaingia kwenye mieleka na kucheza michezo ya kutumia nguvu zaidi.
Haya ndiyo aliyoyataka Nietzsche na alimalizika Nietzsche mwaka 1900 na kutuachia kile kinachoweza kukiita “Uwastani wa kila kitu” ambao umekuwa ni sifa katika sifa za zama za leo, na kuenea nadharia hiyo kati ya makundi ya wanafikra wa Ulaya na kukinai nayo, lakini ilikuwa imezungukwa na hali nyingi za wasi wasi ikiwa ni pamoja na wasiwasi wa kupotea kwa jamii ya wanadamu, ambapo watu watafanyiana uadui na uovu wao kwa wao, hakutokuwepo na mtangenezaji sharia kwa kuzuia hali hii ya fujo.
Wakasema: Ni lazima fikra ya wastani wa kila kitu kuifanya ni yenye kukubali kutekelezeka na kuifanyia kazi katika maisha ya watu, tunaweza kumaliza fujo hii kwa kuweka kipimo kinachokubalika na watu katika kufanya kitendo au kuacha, na kufikia mwisho kuwa kipimo hiki ni yale “Maslahi” ambayo huitwa “Diplomasia ya kimanufaa” yamesemwa haya na “John Dewey” pamoja na “James Cohen” ambao wanazingatiwa ni makuhani wakubwa wa mfumo wa “Secularism” Usekula, ambapo wameleta vipimo vipya vya kusimamia uwastani wa kila kitu, na kufanya mafanikio ndio thamani inayotangulizwa kuliko thamani zote kwa kuzingatia ndio inayofikia masilahi, na ikawa miongoni mwa sifa za zama za leo ni “Mafanikio”.
4- Mafanikio ndio yamekuwa kipimo, wakati ambapo maadili mema na wajibu vimekuwa ni vipimo vya tathmini, na Mwenyezi Mungu akakemea watu wanaofanya mafanikio ndio kigezo na kipimo cha ubora wa hali zao hali ya kuwa wapo kwenye shirki na maasi. Mola Mtukufu Amesema: {Je! Munajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi * Na munajenga majengo ya fakhari kana kwamba mtaishi milele! * Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari} ( ).
5- Kipimo hiki kipya kikazaa ushindani usio na heshima kati ya watoto katika hatua za kwanza za shule, na kusahaulika ushindani wenye heshima ambao Mwenyezi Mungu ameusemea: {Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindane wenye kushindana} ( ).
Na Mtume S.A.W anahimiza kwa kusema: “Lau watu wangefahamu yaliyomo kwenye safu ya kwanza basi ingekuwa ni watu kupiga kura” ( ).
Kwa sababu hiyo inawapelekea kutomzuia muovu wa maadili ambaye fedheha zake zinaweza enea kwenye ndimi za watawala wa nafasi za juu ndani ya nchi mpaka iwezekane kuongoza nchi ikiwa tu atafikia maslahi ya nchi, kwa kuboresha hali za kiuchumi na hali za kisiasa, ama mambo haya wanasema kuwa ni mambo binafsi, hutofautiana katika ufahamu wetu na kadhia ya “Kuamrisha mema na kukataza maovu” na nasaha katika Dini zinasimama kwa mwanadamu kumkataza ndugu yake mwanadamu pindi anapomuona akiwa kwenye makosa au akiwa kwenye hatari, na kumpa nasaha kwa kumwambia kuwa: Hili halipaswi.
Huenda akauliza mwenye kuuliza: Hivyo ni kwanini wana muhukumu mfano wa rais mwenye fedheha? Jibu ni kuwa wanahukumu kwa kumzingatia ni mwenye kwenda kinyume na sheria ambayo imewekwa kwa msingi wa kiwastani wa kila kitu na maslahi, na wala sio kwa kumzingatia anakwenda kinyume na maadili mema desturi na dini, kwa hili sheria inazingatia ndio kipimo cha hukumu wale wenye kwenda kinyume, nayo ndio imezaa kile kinachoitwa kipimo cha sheria.
6- Kipimo cha Sheria: Ni sifa nyingine katika sifa za zama za leo, na sifa hiyo inajibu maswali mengi ambayo: Ni nani anayeweka sheria? Jibu: Ni bunge au baraza la wazee, na wakina nani hao wajumbe wake? Jibu: Kwa – sifa hii – ni wale wanaochaguliwa na watu kwa uhuru kamili kwa msingi wa uwastani wa kila kitu na maslahi, na kwa hali hii tunakuwa tumefika kwenye “Demokrasia” na kwa msingi huu bunge au baraza la wananchi linapitisha maamuzi na kutengeneza sheria kwa kuchunga masilahi, nayo ni kufikia manufaa maalumu hata kama yatakuwa si katika haki yake la msingi ni baraza linaweza kufikia masilahi hayo kwa sababu lina nguvu zaidi.
7- Kabla ya kuelezea kwa wingi wa sifa hizo acha tuzungumzie kuhusu maana ya sifa zilizokwisha tajwa hapo nyuma nazo ni: (Uraia – uwastani – masilahi – mafanikio – kipimo cha sharia) sifa hizi za kinadharia hazikuwa zenye kuwezekana kutekelezwa kwenye uhalisia kwa mara moja, kwa sababu muelekeo huu ulikuwa utapambana na kupingwa vikali na watu, ni sahihi kuwa sifa huanza kwa mtazamo na kwa fikra ya kifalsafa, kisha hubadilika baada ya hapo na kuwa mwelekeo na uhalisia wenye kuonekana, kwa mfano Waprostant wa zamani walikuwa wanafahamu maadili mema na ubaguzi wa kidini, tulikuwa tunaona kuwa mtalii wa kike wa Kimarekani katika miaka ya 1960 ndio bora zaidi katika maadili ya kustiri mwili wake na kufuata dini yake.
Baada ya mwaka huo wa 1960 kulianza kujitokeza jambo jipya katika sura iliyoitwa “The Beatles” nayo ni aina ya muziki, na hii ni pamoja na kundi la watu kwenda kinyume na desturi, katika muziki baada ya kuwa ni muziki wenye ladha nao ni muziki wa “Beethoven” Ambao pindi unaposikia msikilizaji anataja sura za kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa kuuelezea kutokana na sauti inayotokana na nguvu ya maji yanayokimbia na sauti ya upepo, hubadili muziki wa “The Beatles” ambao kwa lugha ya Kiingereza una maana ya fujo na makelele.
Baada ya watu kuwa wanapenda muziki wa zamani ambao unachanganyika na nafsi, hawa watu walielekea kuwa muziki ni ukombozi wa vikwazo na kukomboa mfumo, wakatuambia: Acheni mwenye kutaka kufanya atakalo ndani ya wakati autakao, mwacheni aoneshe uwezo wake, aelezee kilichomo ndani mwake hata kama atakuwa nje ya mfumo na desturi pasina kujua na bila ya kitu chochote, kisha akafanya harakati na kuwa harakati hiyo ni miongoni mwa sifa za zama za sasa, jambo ambalo linapelekea kupinga kunakosa sababu, kwa mfano desturi za chakula ambazo zimewekwa na mfalme na kuziita kwa jina la misingi ya adabu za kifalme za chakula, uma kushikwa mkono wa kushoto, kisu mkono wa kulia, kijiko kuwekwa mezani, na Muislamu anapotaka kula kwa mkono wake wa kulia basi atakuwa amekwenda kinyume na mfumo huu na mara moja anakuwa mshamba, anapotaka kula wali lazima ale kwa kutumia uma, kwa sababu hana ruhusa kutumia kijiko isipokuwa kwa kunywewa, ikiwa ikitokea mtu kwenda kinyume mbele ya mfalme basi ukiukaji huu unapaswa kumfanya mfalme akasirike pale pale mezani, hivyo ni lazima kwa wote kujifunza kanuni za adabu za chakula za mfalme wa Uingereza, kinyume na hivyo atajikuta amejiweka kwenye matatizo.
Kisha yakabadilika yote hayo, na kukawa na zama za Hamburger, nayo ni zama yenye alama ya kuachana na mfumo wa zamani wa kula chakula, anashika sandwich yote kwa mikono yake yote na anakunywa kwenye chupa ya coca cola kisha anafuta kwa mkono wake kwenye nguo zake pasina kuheshimu desturi na mfumo wa zamani.
8- Mifano miwili niliyoitaja ya kutoka nje ya mfumo ni upande katika pande za ujuzi na upande katika pande za jamii, ama katika masula ya adabu kikaanzishwa kitu kinachoitwa “Instraction” ikiwa na maana ya mpasuko, nayo ni adabu isiyofahamika inayokuja na vitu visivyokuwa na uhusiano wa vyenyewe kwa vyenyewe ni kama vile kusema: Chukulia kuwa sisi tupo katika eneo la golf, kisha anasema: Huko kuna mtu anatoa muhadhara kwa wakina mama, kisha anasema: Hivyo basi samaki ni aina katika aina ya viumbe hai, pindi unaposema: Mimi sifahamu unayoyaongea, anakujibu: Wewe si mtu mwelevu, hali hii imeendelea kuwepo kwenye vyuo vyetu vikuu kwa muda mrefu, mpaka akaja Dr. Abdulaziz Hamudah Mkuu wa Kitengo Cha Masomo ya Lugha ya Kiingereza na Fasihi zake Chuo Kikuu Cha Kairo, akatunga kitabu chake cha kwanza kisha akatunga kitabu cha pili na kufundisha hali hii kisha kubainisha kuwa hali hii imefikia katika hatua ya mgongano wa kiakili, pamoja na weledi wake katika masomo ya fasihi ya Kiingereza – alilazimika kufundisha hali hii kwa muda wa miaka mine na hakukuta wengi wanauelewa, akachapa vitabu vyote viwili katika mfululizo wa maktaba ya Kimataifa ya maarifa ambayo inachapa vitabu vyake huko nchini Kuweit.
Tatizo ni baada ya muda wa sasa ni hatua isiyo na mwisho ambapo inazingatiwa hatua hii yenyewe ni maendeleo imezuka kutokana na maendeleo yenyewe ya sasa, na wamezingatia kuwa maendeleo ya kwanza yaliwezesha kujivua na mfumo wa dini, na wao wanalenga kujivua na asili na misingi iliyobakia katika maisha ya watu kwa madai kuwa inakwamisha gunduzi uhuru na fikra, wakati wa hatua hiyo ilipanuka kwa kufuta na kuondoa Fasihi za zamani na ujuzi wa zamani, vile vile hatua hiyo ikaondoa uelewa wa familia ya zamani na kuwa yote hayo hayana thamani baada ya kuondoa dini katika maisha ya watu.
Kwa vitendo likaasisiwa kanisa ili kueneza ndoa za jinsia moja na kuwepo uelewa mpya wa familia, huenda baba na mama wote wakawa ni wanaume au wanawake, wala hakuna kinachotupasa kuwa kwenye umbo la familia ya zamani.
Na kwa utaratibu huu mpya unakosekana uwezo wa pamoja kati ya watu wote na kuenea mauaji na matumizi ya nguvu, kwa kukosekana kanuni ya kujadiliana na kufahamiana hasa walitaka pia kubadilisha lugha, na wakasema: Lugha ambayo inazingatiwa mke wa mtu ni mwanamke tubadilishe na kufanya mke wa mtu ni mwanaume, na uke kuwa ni uume na uume ni uke, na kubadilisha uelewa wa (Dini – utamaduni – familia – lugha – nchi) kugeuza wizani wote, na hali hii tunatoka nje ya misingi na vipimo ambayo ilikuwa inawezekana kuwa ni marejeo, na kujitokeza sifa ya kutoka nje ya mfumo na kanuni zinazofahamika.
Hivyo basi kuwa nje ya misingi na desturi ni sifa katika sifa za zama za sasa, na sifa hii huzaa jamii isiyo na uwezo wa kufahamiana na watu wengine, na anakuwa kila mmoja miongoni mwetu na lugha isiyofahamika isipokuwa na mzungumzaji tu, na ulimwengu unakuwa na lugha zaidi ya milioni sita, ima utuuwe sisi kwa sisi au tuachane nao kwa sababu ya kutokuwepo kiunganishi kati yetu.
Muelekeo baada ya usasa ni juhudi za kuondoa ujinsia, na wanamfanya mwanadamu ndiye ambaye anaainisha ujinsi wake na wala sio Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuumba katika umbile la mwanaume basi yeye anataka kuwa mwanamke na kubadilika kuwa mwanamke ndani ya mwili wa mwanaume au kinyume ikiwa anataka kuwa mwanaume na Mwenyezi Mungu amemuumba kuwa mwanamke basi wala hakubaliani na hali hii na kuibadilisha kuwa mwanaume ndani ya mwili wa mwanamke, na kwa hali hii hatua baada ya usasa hukiuka misingi yote ambayo hufahamika na wanadamu, na kuonekana ukiukaji kama sifa mpya miongoni mwa sifa za zama za sasa.
9- Ukiukaji umekuwa ni katika sifa za zama za sasa, tayari umeshafanyika ukiukaji wa hatua ya familia (Family) na kwenda hatua ya (Couple) kwa maana ya uwili, ama familia (Family) ina maanisha ni mume mwanaume na mke mwanamke, na wameifanya familia ya kijadi ni moja ya aina ya (Couple) uwili, kwa sababu couple ina maanisha uwili, ima mwanaume na mwanamke au mwanaume na mwanaume au mwanamke na mwanamke, hivyo msamiati mpya umekuwa ni mpana zaidi na kuwa na aina tatu za uwili, wakiwa wanafanya juhudi ya kuwa aina tatu zenye kukubalika ndani ya jamii pasina kupingwa, ikiwa tutazungumza ni kwa nini familia haiwi ni mwanaume na mwanamke tu, basi wanatujibu na wanasema: Sisi tumeshavuka hatua hiyo.
Na kuondoa tatizo la kukamilisha uwili huo mpya basi kumekuwa na ujenzi wa watoto kutokana na wanandoa wawili wote wanaume au wanandoa wawili wote wanawake na kuwepo hali ya biashara ya mifuko ya uzazi, na kuwepo benki ya shahawa za wanaume, na hivi sasa wanafikiria upandikizaji wa mfuko wa uzazi kwa mwanaume.
Sisi pindi tunapo shughulikia kadhia hizi kama wanachuoni basi ni lazima kufahamu asili ya maudhui, wala haipaswi kwetu kuangalia masuala ya biashara za mifuko ya uzazi – kwa mfano – kuwa haina uhusiano na hayo yote, nalo ni jambo linalozaa kauli ya uboreshaji, na uwastani, na ukiukaji huu tunauona katika silabasi za masomo, na katika juhudi za kuboresha mitazamo, na katika mahitaji ya viwango vya kielimu pamoja na utungaji vitabu na usomeshaji, na katika staili nayo ni muundo mwingine na aina za mavasi mapambo fani za ujenzi shule za wanamashairi na Fasihi pamoja na mielekeo ya kiufundi, wakati upande wa pili tulikuwa na tunalinda urithi na elimu na kufanya juhudi za kufahamu ukweli na ukamilifu wake, chombo cha habari cha Kimarekani kimekuwa kikionesha filamu zake na programu zake za kihabari kwa ajili ya kuhudumia maana hizo, watazamaji wa filamu wanafikia maana hizo au zaidi au kufikia maana zote jumla.
Inapaswa kusisitiza juu ya umuhimu wa Muislamu kufahamu kuwa uwastani wa kila kitu ni upotoshaji na kitu batili, na ukweli ni ule anaoamini Muslamu na kufahamu kuwa ulimwengu huu umeumbwa na Muumba, na Mwenyezi Mungu huamrisha matendo mema kwa ajili ya kuijenga nafsi na ulimwengu, na mwanadamu ni mwenye kuhesabiwa kwa kutowajibika na amri hizi, haya ndiyo tunataka kuyasisitiza katika kupambana na maana hizo mpya ambazo zimekuwa sifa za zama tunazoishi.
10- Katika sifa za zama hizi: Ni mchanganyiko wa maendeleo, na kuwa hakuna misingi thabiti kwetu, na mwanadamu mwenyewe ni sehemu ya maendeleo haya, na yeye akiwa amekuja kutoka hali ya upweke basi huenda hapo baadaye atafika kwenye kitu kingine, kichwa chake kikubwa na mwili wake ni mdogo, au ataundika na maumbile ya mwanadamu pamoja maumbile ya robot, na anaweza kuyahukumu mauti na kutengeneza serikali ya dunia itakayo shikilia ulimwengu ambao unapaswa kugawanywa kwenye nchi 400 badala ya nchi 196 zilizopo hivi sasa, na inawezekana kufuta na kuondoa asasi mfano wa shule hospitali na maofisi ya serikali kwa njia ya mapinduzi ya mawasiliano usafiri na teknolojia ya kisasa, na anaweza pia kwa njia ya kijenitiki kushikilia ulimwengu wa nje.
Pamoja na maendeleo haya ambayo uwazi wake ni nguvu, tunaona hofu ndani ya nafsi zinazotokana na fasihi zinazoonekana kupitia riwaza za sinema kutokana na ubaya ambao haiwezekani kuuvunja kwa nguvu, au bacteria wasiokubali matibabu au vita vya angani kwa ajili ya ardhi, au kuwabadilisha watu kuwa mabwana na watumwa au na mengine mengi yasiyokuwa hayo, lakini katika fikra zote hizo fikra ya kuondoa kifo hii itashindikana, kisha itafuata katika kushindwa fikra ya kuondoa misingi thabiti mitano.
11- Wanachuoni wengi wa kimagharibi leo hii wanaamini ukweli kuwa kifo kinapaswa kutokuwa hali ya mwisho, au kwa maana nyingine watu hawapaswi kuwa madhaifu au wagonjwa, inapaswa kuanzia hivi sasa kufahamika – kwa mujibu wa kuamini kwao – kufanya kazi kusimamisha utu uzima au uzee, bali zaidi ya hapo ni kuakisi kazi za uzee mwanadamu kuwa mwenye nguvu siku zote.
Pamoja na kushindwa kwao lakini matukio na vitendo vya matumizi ya nguvu havitajificha watu watakuwa wanakumbana na mauaji kila wakati kutoka kwa watu waovu miongoni mwao, lakini pamoja na kusalimu amri kwao bado wanaamini kuwa kifo cha uzeeni au kifo kuwa ndio mwisho wa maisha kitakuwa ni kitu kilichopita na kumbukumbu yenye kiza ya masiku ya mwanzo.
Huenda dalili ya kina ya imani yao hiyo pamoja na maelezo yaliyotolewa na (William R. Clark) mtaalamu wa maradhi ya kinga za mwili ni Mmarekani katika maelezo yake juu ya uhusiano wa kifo na uhai alisema kuwa: “Kifo hakiingiliani sana na maana ya uhai” kwa maana uhai unaweza kuendelea pasina kulazimika mwisho wake uwe ni kifo, na maana ya kifo siku zote imekuwa ni mwisho wa waliotangulia, na hii haimaanishi kwa umuhimu kuwa wanaofuata siku zote watakufa.
Wakati hivi sasa unaelekea kwenye maslahi ya uhai, maendeleo haya ya leo ya kibailojia na kitabibu ambayo yanategemewa kufikiwa ndani ya miaka ishirini ijayo kile kitakacho ruhusu kwa mwanadamu kuishi baada ya miaka mia kwa muda mrefu zaidi, jambo ambalo litampa nafasi mwanadamu kunufaika zaidi na zaidi na maendeleo ya kitiba na kibailojia na kuishi zaidi na zaidi.
Hivi leo wanachuoni wengi wanaamini kuwa kuishi milele ni kitu kinachowezekana kwao, kwani utafiti wa kisayansi umefungua njia ya mwanadamu kuishi milele, miongoni mwa watu wa mwanzo kupita njia hiyo – katika miaka ya sabini – ni msomi na mtaalamu wa mambo ya biolojia Mmarekani (Leonard Heflick) ambaye amegundua kuwa kwenye aina nyingi za seli za mwanadamu kwa asili yake kuna idadi zaidi ambayo inawezekana kugawanyika au kuwa nyingi zaidi, baadhi ya aina za seli ni mfano wa zile ambazo huzalisha chembechembe za damu nyekundu na nyeupe zinawezekana kugawanyika mara kadhaa, na baadhi ya nyingine mfano wa seli nyingi haziongezeki kabisa, hii imepelekea kufahamu kila kinachoitwa kiwango cha Heflick, kwa mfano, ikiwa kiwango cha Heflick ni seli 50, seli zitagawanyika mara 50 kisha unakuwa mtu mzima, kisha hali ya kukonda kisha unakufa, pindi zinapokufa idadi kubwa ya seli zetu basi na sisi tunakufa, na kupelekea katika hilo kufikiwa ukweli muhimu sana, ambao ikiwa hazitokuwa baadhi ya seli basi kuna seli zitakuwa ni za kudumu, nayo ni maelezo yaliyopitishwa na Heflick katika tafiti zake ambapo alifikia yafuatayo:
12- Bakteria: Hawafi ikiwa tutaondoa uwezekano wa kuwauwa kwa makusudi kwa njaa au kwa miyale ya jua au kwa upungufu wa maji au kumlazimisha kiumbe mwingine ili kuwaua, hilo lina maana kuwa seli za bakteria hazikui au hazi zeeki, zenyewe zinaendelea kugawanyika siku zote mpaka zitagongana na sababu yeyote ile iliyopita kuelezewa au zisigongane.
13- Seli za Saratani: Nazo pia ni za kudumu, zenyewe zinaendelea kwenye kugawanyika na kugawanyika kusiko na mwisho, isipokuwa ikiwa watakufa kwa miyonzi ya jua au kitu kingine au kufa kwa muwezeshaji.
14- Seli za Hela: Neno hii limechukuliwa kutokana na ugonjwa wa (Hinrepta Lux) mwaka 1951, bado zimeendelea kugawanyika mpaka hivi sasa kama ilivyokuwa ikifanya kwa zaidi ya miaka hamsini.
15- Seli (Germline) za mwanadamu: Ni seli ambazo zinatengeneza mayai, na seli za manii pia hazionekani kwa maana ya Heflick, kwa kuangazia maelezo yaliyopita kuna swali muhimu nalo: Ni kwa nini baadhi ya seli zinaweza kuendelea kugawanyika na kuwa nyingi wakati zingine zinazunguka na zinakufa baada ya kufikia idadi maalumu za kugawanyika? Swali hili linajibiwa na Dr. Michael Fossel ( ) katika kitabu chake maarufu “Kuzuia uzee wa mwanadamu” kilichapishwa na maktaba ya William Morrow Marekani mwaka 1996.
Dr. Fossel alitangaza kupitia kitabu hiko maarufu katika moja ya vituo vya vyuo vya taifa vya masomo ya afya mnamo tarehe 16/04/1996 na kutoa muhadhara chini ya ulezi na usimamizi wa Chuo cha Shamsuni ( ), alisomea kwenya taasisi hiyo masomo ya maradhi ya (vifo vya haraka au uzee wa mapema Progeria), na akathibitisha kwa dalili huru za maradhi haya pamoja na ukweli uliotangulia kuwa seli za saratani na seli za vijududu hazizeeki, na uzee ni mfumo uliopangiliwa, na wenyewe ni kazi ya kubadilika kwa gen na wala sio kazi ya kula na kuharibu.
Ndani ya kitabu hiko ameonesha tafiti muhimu kuhusu (Telomere) ambayo inasifa ya kuandaa uzee, utafiti huu haukuwa kitu chochote kuliko (D.N.A) mwishoni mwa kila Chromosome hupoteza sehemu ya urefu wake pamoja na kila mgawanyiko wa seli, Fossel alifananisha mfano wa kichwa cha nyuzi za viatu, upoteza ncha kidogo kidogo kutokana na urefu wake, mwisho nyuzi za viatu zinakuwa ni zenye kushindwa kufanya kazi yake na kuonekana kiatu, kwa mfano pindi inapokuwa (Telomere) katika seli fupi sana basi seli huonekana na husimama kugawanyika.
Hii ni tafsiri mpya na mtazamo thabiti wa seli za mwanadamu huweka wazi kwa nini hatuzipi nafasi zaidi ya maisha ya muda mfupi, na kuweka wazi pia kwa nini kuna kuwa na vizuizi kwenye mwenendo wa joto ambalo anakuwa nalo mwanadamu na ambalo hupelekea kwa nafasi yake kukwamisha kazi za damu nyeupe kisha kusimamisha kugawanyika kwa seli, wakati ambapo inawezekana kupelekea kurefusha umri, na kuweka wazi kwetu pia kwa nini (Progeria) haiwezekani kuishi maisha mafupi, bali huzaliwa pamoja na (Telomere) fupi, ni lazima pia kwenye maswali yetu kuuliza ni kwa nini tunabakia nyakati zingine kuwa wadogo wenye nguvu wenye afya kisha tunakuwa kama mwamba ndani ya wakati fulani.
Majibu ya maswali haya yote ni kwenye Chromosome ambapo kunapatikana kwa ukaribu kile kinachoitwa geni za mpangilio, na utendaji wa geni hizo kazi zake zinategemea urefu wa (Telomere), wakati inapoishia Telomere kwenye kiwango maalumu geni hizi sehemu kubwa huwa ni zenye kushindwa kutekeleza kazi zake, huu ni ukweli wa kisayansi haukuwa na athari kwa wasomi katika seli za saratani na seli za bakteria, kwa hali hiyo hizo seli wakati wote hujitengeneza kwa wingi na hugawanyika pasina kusimama.
Kwa kutafuta sababu ya kweli nyuma ya hali hizo inakutwa kuwa seli hizi huzaa kitu kinachoitwa (Telomorase) ambacho hutengeneza (Telomere) kwa mara nyingine, ili kuchukua nafasi ya hizo zilizokosekana pamoja na vigawanyo vyote, kwa maana ya ndani zaidi ni kuwa haizalishi (Telomere) kwa kuanza lakini huzuia kupotea Telomere zilizopo.
Fikra ambayo inaelezwa na kitabu inajengeka kwenye ukweli huo muhimu wa kisayansi, nao ni je inawezekana kufikia umilele ikiwa itawezekana kutanguliza hizi (Telomerase) kwenye seli asili au kuzihimiza kuzalisha kwake?
Kwa mujibu wa mtazamo wa Dr. Fossel kupitia tafiti zake na watu wengine, alitangaza katika kitabu chake imani yake kuwa kipindi cha miaka 10 mpaka 20 elimu ya mwanadamu itakuwa ni yenye uwezo wa kuzuia mchakato wa utu uzima au uzee wa mwanadamu, badala ya kuwa uwastani wa umri wa mwanadamu miaka 120, itakuwa inawezekana kuishi miaka mia mbili kisha miaka elfu moja na mia mbili kisha miaka elfu mbili.
Akabashiria Dr.Fossel katika kitabu chake watu wengi chini ya miaka arobaini kuwa huenda itakuwa mategemeo haya mazuri yanawezekana hivi karibuni tu, kwa sababu baada ya miaka hiyo arobaini mwili wa mwanadamu utakuwa umepata kero na adha ambapo hautakuwa wenye kuwezekana kurefuka zaidi.
Kitabu chake kimeelezea mjadala juu ya kadhia za kijamii na kimaadili ambazo zitapelekea uwezekano wa kuzuia na kuchelewa mchakato wa uzee wa mwanadamu, na kuzingatia kuwa mjadala huo kutoka kwa baadhi ya wasomi na watafiti isipokuwa hiyo ni mwanzo wa kwenda sehemu ngumu zaidi, kama vile alijadili vikwazo vya urefukaji huo unaotegemea umri wa mwanadamu, na kuuliza ni nani atakayesimamia mikakati ya elimu na taratibu za mivutano kwenye ngazi ya kibiashara.
Lakini kwa mujibu wa kauli yake Dr.Fossel kuwa kwa bahati mbaya hatuwezi kufikia umilele kwa mfano wa wepesi huu kwa sababu nyingi miongoni mwa sababu hizo:-
Kwanza: Baadhi ya aina za seli kwa msingi hazigawanyiki: Kama vile mapigo ya moyo au seli za ubongo – kwa mfano – na hii ina maanisha kuwa zipo nje ya mzunguko wa kazi hii ambayo huandaa uzee wa seli kwa maana haitonufaika na (Telomerase) na huenda seli hizo zikazeeka.
Pili: Seli nyingi za saratani hupunguza kuwa ni za kuishi milele na hufa kwa wepesi kwa sababu zinapoteza uwezo wa kuzalisha (Telomerase) kwa sababu moja au nyingine.
Tatu: Kuongezeka mwili wa mwanadamu kwa (Telomerase) kwa njia kuu katika sura ya vidonge au sindano yawezekana kutengeneza hatari ambapo huenda ikahifadhi seli zenye kukimbia kugawanyika kwa sura isiyo maalumu hali ambayo inaonya kuzaliwa kwa saratani.
Dr. Fossel ana mategemeo huenda siku moja itakuwa kwa wasomi kuwa na uwezo wa kuwezesha seli asili kuendelea katika kuzalisha Telomerase wakati huo huo kuzuia kuzalisha kwake seli zenye kukimbia isipokuwa anaona katika kitabu chake kuwa hali hivi sasa inatufanya kupendelea tafiti ambazo huzuia seli kuzalisha Telomerase ambapo huenda hazitaongeza uhai wa moja kwa moja kwa sehemu kubwa, kwani bado kumekuwa na hali nyingi ambazo humaliza uhai mfano: Virusi bakteria majeraha sumu makosa ya geni na zinginezo.
Tumerefusha kwenye sifa ya maendeleo na kuingia kwenye mazungumzo yanayohusu kumalizana na umauti kama moja ya tukio la sifa hiyo, na kuna sifa zingine nyingi za zama hizi za maendeleo miongoni mwa sifa hizo ni: Uhuru, usawa, utandawazi, muungano wa mwanadamu, uwazi, usiri, matirio, taasisi, fujo, kugundulika kwa siri, kulingania kwenye nafsi yenye kuimarisha ubaya, kuharibu muungano na kutofautiana hali za vita na mfumo wa soko.
Chanzo: Kitabu cha sifa za zama za leo cha Fadhilatuh Mufti wa Misri.
Dr. Ally Juma.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas