Kipindi Kifupi.
Question
Imepokelewa Hadithi Takatifu kuwa mtoto pindi anapomkuta baba yake yuko utumwani kisha akamnunua na kumwacha huru, na kuanzia hapo anakuwa amemlipa. Vipi tunakubali kati ya Hadithi hii na ya maelezo yaliyopitishwa na Wanachuoni kuwa mwanadamu haifai kumiliki asili au tawi lake? Mpaka iwezekane yeye kumwacha huru: Lazima kwanza aingie kwenye miliki yake?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Yaliyopitishwa kwenye Sharia ni kuwa binadamu hamiliki asili yake wala tawi lake, ama asili yake ni kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaoneahuruma} [AL ISRAA: 24.] Wala haiwezekani kuinamisha bawa la huruma pamoja na hali ya utumwa. Ama tawi lake, ni kauli ya Mola: {Wala hahitajii Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema kuwa na mwana * Hakuna yeyote aliomo mbinguni na ardhini isipokuwa atafika kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema akiwa ni mtumwa wake} [MARYAMU: 92, 93.] Na Akasema Mwenyezi Mungu: {Na wanasema: Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, anamwana!} [AL ANBIYAA': 26], nayo ni dalili juu ya kukanusha kukutana baina ya utoto na utumwa.
Ama Hadithi iliyoashiriwa kwenye swali, ni Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslimu katika Kitabu chake kutoka kwa Abu Huraira R.A. amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Mtoto hawezi kumlipa mzazi wake, isipokuwa anapomkuta anamilikiwa kisha akamnunua na kumwacha huru”.
Amesema Mwanachuoni Al-Khatwib As-Sharbiniy katika kitabu cha: [Mughniy Al-Muhtaj 6/458 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: Kwa maana: Kumnunua ni kumkomboa, kwa sababu mtoto si hana haki ya kuanzisha haki”.
Na amesema Mwanachuoni Abu Saadat Ibn Al-Atheer Al-JazrIy katika Kitabu cha: [Jaamiul Usuul 1- 400 chapa ya Maktabat Helwaany na Maktabat Dar Al-Bayaan] – kauli yake “Atamwacha huru” sio maana yake: Kuanza kuachwa huru baada ya kumilikiwa, kwa sababu kauli za Wanachuoni zimekubaliana kuwa baba ana mkomboa mtoto wake ikiwa ana mmiliki hivi sasa, lakini maana yake ni kuwa: Ikiwa atamnunua na kuwa kwenye miliki yake basi ataachwa huru, kwani kumnunua ndiyo sababu ya kumkomboa, limeongezwa kuachwa huru kwenye makubaliano ya kumnunua, lakini hili limekuwa ni malipo kwake, kwa sababu kumkomboa ni bora zaidi na ni katika yanayoneemesha mtu kwa mtu, pale anapokuwa amemmalizia hali ya utumwa, na kumuondoshea mapungufu ambayo alikuwa nayo, pamoja na kumkamilishia hukumu za uhuru katika matendo yake yote”.
Hadithi hii imekuja hasa kwa mzazi, lakini kuna Hadithi nyingine pana zaidi ya hiyo, nayo imepokelewa na wapokezi wanne, kutoka kwa Samra Ibn Jandab R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kummiliki mwenye undugu ulioharamishwa, basi huyo yupo huru”.
Na katika mapokezi ya An-Nisaa katika kitabu cha: [Al-Kubraa] kutoka kwa Omar R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kummiliki mwenye undugu naye wa karibu, huachwa huru”.
Amesema Mwanachuoni Al-Manawaa katika kitabu cha: [At-Taiseer Sherehe ya Kitabu cha Al-Jaamii As-Swagheer -2/445 chapa ya maktabat Imamu Shafiy huko Riyadh]: “Mwenye kummiliki mwenye undugu wa karibu” kwa maana: Asiyekuwa halali yake kumuoa kutokana na undugu huo “Basi huyo yupo huru” kwa maana: Anamwacha huru kwa kuingia kwake tu kwenye miliki yake, na kwa ujumla wake, hukumu hii imechukuliwa na Wafuasi wa Imamu Abu Hanifah, na amesema Imamu Shafi: “Hakombolewi isipokuwa mzazi kwa mtoto”.
Amesema Ibn Al-Atheer katika Kitabu cha: [Jaamii Al-Usuul 8/74] “Mwenye kummiliki mwenye undugu wa karibu”, na hasa walio maswala ya mirathi huitwa ndugu wa karibu kwa upande wa wanawake, na aliye haramu kuoana naye kwa undugu: Ni yule asiye halali kumwoa, kama vile mama binti na dada, hao ndio waliotajwa sana na Wanachuoni miongoni mwa Masahaba na waliofuata baada ya Masahaba, pia wameelezewa na Imamu Abu Hanifah na wafuasi wake, na Ahmad kuwa: Mwenye kummiliki mwenye undugu naye basi huachwa huru, awe ni mwanaume au mwanamke, na ameelezea hayo Imamu Shafi kuwa huachwa huru watoto baba na mama, wala hawaachwi huru ndugu, wala yeyote katika watu wengine wa karibu, na ameelezea Imamu Malik kuwa huachwa huru mtoto, mzazi na ndugu, na wala haachwi huru asio kuwa katika hao”.
Na mwenye ufahamu wa masuala haya kumejengeka kwa kile kinachoitwa na Wanafiqhi kwa jina la “Kipindi kifupi” nacho ni kipindi cha kuzingatiwa muda wake chini ya muda unaowezekana kukamilika makusudio, pindi Hadithi ya kwanza ilipokuwa inaonesha juu ya kuwa mzazi hukombolewa kwa kule kununuliwa tu, kwa sababu haifai kwa mtoto kummiliki baba yake, kumekuwa na tatizo: Ni kuwa kuthibiti kuacha huru mtoto ni kuthibiti kwa umiliki, ikiwa ni lazima kukadiriwa kuwa baba ameingia kwenye miliki ya mtoto wake ndani ya wakati mfupi sana, unaosamehewa kwa dharura, kisha huachwa huru kwa mamlaka ya Sharia.
Amesema Imamu As-Sarkhasiy katika kitabu cha: [Al-Mabsuut 7/69 chapa ya Dar Al-Maarifa], baada ya kutaja Hadithi: “Katika hili kuna dalili kuwa mwenye kummiliki ndugu wa karibu, basi Ndugu huyo huachwa huru, kwa sababu kauli yake: “Basi huyu yupo huru” ni malipo ya kauli yake: “Mwenye kummiliki” pamoja na uwepo wa undugu wa karibu, basi hupatikana uhuru wa mwenye kumilikiwa pasina mmiliki. Na katika baadhi ya mapokezi amesema: “Huachwa huru,” kuna dalili kuwa sababu ya kuacha huru mmiliki ni pamoja na kuwepo undugu wa karibu, hivyo mfano wa hili katika Tamko la Sharia kwa maana ya kubainisha sababu, kama alivyosema: “Mwenye kubadili dini yake basi na auawe” na akasema Mola: {Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu na afunge} [AL-BAQARAH: 185, na katika hili wamesema Wanachuoni wengi: Pindi Mtu anapommiliki baba au mama yake au mtoto wake basi huachwa huru…. Na kusudio lake Mtume S.A.W. katika kauli yake: “Basi humwacha huru” ni kule kumnunua tu, na wala sio kwa sababu nyengine, kama inavyosemwa: Amemlisha na kumshibisha, akamnywesha na akashiba, akamchapa na kupata maumivu. Kwa hakika tumethibitisha kwake umiliki tokea mwanzo, kwa sababu kukamilika kwa utumwa hakufikiwi isipokuwa kwa mambo hayo, ikiwa hajammiliki hawezi kumwacha huru”
Maeneo haya na mengine pamoja na kutoelezewa na Wanachuoni masuala ya kipindi kifupi, isipokuwa wao wameelezea katika matawi mengine tofauti. Miongoni mwa matawi hayo: Ni pamoja na aliyoyasema Imamu Alaadeen Al-Kasaaniy katika kitabu cha: [Badaai As-Swanaai 4/146 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Wala haufai wasia wa mwenye kuandikiwa uhuru katika mali yake, hata akiwa ameacha usia huo, ikiwa hajaacha basi hakuna shaka ndani yake, kwa sababu amefariki akiwa mtumwa hivyo haufai wasia wake. Ama ikiwa ameacha utekelezaji kwa mtu fulani ikiwa tutahukumu kuachwa kwake huru kwa hakika tumehukumu kabla ya kufariki bila pingamizi, na kwa saa ya muda mfupi usiowezekana kutamka wasia”.
Na miongoni mwake: Ni pamoja na yaliyosemwa na Wanachuoni Az-Zailaiy katika kitabu cha: [Tabyeen Al-Haqaaiq 2/206 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamy]: “Ikiwa atamwambia mwanamke: Wewe ni mwenye kuachwa ikiwa sikuachi, au ikiwa sijakuacha, au pindi nisipokuacha: haachwi mpaka afe mmoja wao kabla ya kumwacha… kisha ikiwa atakufa mume talaka inakuwa kabla ya kufa, ili kufikiwa kushindwa kwake kutoa talaka, basi mwanamke atarithi, hata kama itakuwa talaka tatu pindi akiwa ameshaingiliwa, na kufanya kifo chake mwanamke ni kama kifo kwa mwanamume, katika hali chache: Haitoki talaka kwa kifo cha mwanamke….na kauli sahihi ni kauli ya kwanza”.
Amesema Sheikh Shalabiy katika kitabu chake: Kauli yake “Kauli sahihi ni ya kwanza” ni kwa sababu ya kukaribia kufikwa na kifo na kubakia uhai wake usiotosha kuzungumza talaka, na hilo ni makadirio ya muda unaofaa kutokea mtundikaji wa talaka, ikapatikana sharti na sehemu bado imebaki basi inatoka. Na mtundikaji talaka ni kama mtumaji kihukumu kwani hakuna uhakika, wala hakuwekwi sharti linalowekwa katika uhakika wa utumaji, kwa hali hii anatokea mtundikaji talaka, ikiwa haikadiriwi kwa mtumaji katika saa hizi chache, basi hakuna mirathi kwa mume kwa sababu imebainika kabla ya kifo, wala hakukubakia kati yao wawili maisha ya ndoa wakati wa kifo”.
Katika masuala haya mawili kumekuwa na sababu ya kutokuwepo wasia katika hali ya kwanza: Kwa kukosekana kuwepo muda ambao unaweza kutokea wasia kabla ya kifo, katika kauli ya pili: Kwa kuwepo muda ambao unatosha kutokea talaka, nao ni muda mdogo unaokadiriwa, vilevile katika masuala ya sehemu ya sali, kwa vile suala la kuacha huru ni sehemu ya mmiliki, imekuwa ni lazima kuwepo mmiliki ni jambo la dharura, kukadiriwa muda mfupi na kutokea ndani ya muda huo umiliki kisha mmiliki akaacha huru, kwa hakika hapa imezingatiwa, kwa sababu unapatikana muda unaokadiriwa uwezekano wa kutokea yote hayo ndani ya huo muda.
Masuala ya muda mfupi ni moja ya masuala ambayo inawezekana kutafutwa chini ya anuwani: “Muda na athari zake kwa mwenye kutundika hukumu ya Kisharia”, wanachuoni wa Sharia na mambo ya asili wameelezea kwa kutafuta athari za muda katika asili na tawi katika milango tofauti na matawi mengi, miongoni mwake: Maelezo yao juu ya wajibu mpana na wajibu finyu, na maelezo yao juu ya mgongano mkuu na ule maalumu, je huchukuliwa ule maalumu moja kwa mjoa ni iwe amefahamu kuchelewa kwake dhidi ya ule mkuu au kutangulia, au hakufahamu chochote katika hivyo viwili? Au lazima kufikiwa kutangulia kwa mtazamo mkuu. Vile vile katika maelezo yao juu ya hukumu ya kuchelewesha maelezo kuepukana na wakati wa haja na kuyapelekea kwenye wakati unaohitajika, na katika rai ya Wanachuoni kupunguza Alasiri, na kubadilisha Fatwa kwa mabadiliko ya upande wa muda, na mengine miongoni mwa masuala ya asili. Ama masuala ya matawi, inakuwa ni vigumu kuyakusanya yote, ni kama vile maelezo yao juu ya usafishaji usiowezekana, na kinachobadilika kwa kukaa muda mrefu, na hukumu za msafiri, kufunga, kutimiza mwaka mali ya zaka, na muda wa mwisho wa mimba na mengineyo.
Haya ni katika yanayofungamana na muda kwa ujumla. Ama yanayofungamana na muda mfupi kwa sifa maalum miongoni ni:
Yaliyonukuliwa na Burhandeen Ibn Mazah Al-Bukhariy miongoni mwa wanafiqhi wa Abu Hanifah katika kitabu chake cha: [Al-Muheetwu Al-Burhany”, 4/166 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya] kuhusu kitabu cha [Ziyaadat cha Imamu Muhammad Ibn Hassan] kuwa lau kutakuwa kuna mtumwa aliyeandikiwa, ana mtoto huru aliyemzaa na mwanamke huru, kisha akafa huyu mtumwa na wala hakuacha mtoto zaidi ya mtoto huyu, na ikawa ameusia kwa mtu huru, basi usia unafanya kazi ya uandishi wa mwenye kuandika mali zake, ikiwa ameacha kitu atavihukumu kwa kitu, na ikiwa hajaacha kitu huuzwa nyumba yake na vilivyomo, kwa sababu wasia unasimama nafasi ya muandikiwa na amekuwa mwandikiwa katika hali ya uhai wake anatakiwa kumlipa mwandishi kitu au nyumba, vile vile inakuwa kwa mwenye kuchukua nafasi yake, ikiwa atalipwa muandishi, basi mwenye kuandikiwa anakuwa huru wakati wa mwisho wa sehemu ya uhai wake na kilichobakia miongoni mwa mali za mwandikiwa zinakuwa ni urithi wa mtoto wake.
Amesema Sheikh Ibn Majah: “Imeelezewa na Sheikh Al-Imamu Al-Jaleel Abibakr Muhammad Ibn Al-Fadhli Al-Bukhariy R.A. alikuwa anasema kuwa uhuru unathibiti sehemu ya mwisho katika sehemu za maisha yake katika muda mfupi wa maisha yeke”.
Vile vile: aliyoyasema mwanachuoni Ibn Najiim katika kitabu cha: [Al-Bahrurraaq 3/292 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy] “Lau atasema: Ikiwa nitamuoa Zainabu kwa muda mfupi kabla ya kumwoa Amarah - ina maana: wote wawili wameachwa, kisha akamuoa Zainabu peke yake, basi haachwi, kwa sababu neno (muda mfupi kabla) ni ibara ya saa chache, inakubaliana na aliyosema Aqeebah, na hilo halifahamiki isipokuwa kwa kumuoa Umarah, kama akisema: “Wewe nitakuacha muda mfupi kabla ya kuingia usiku” anakuwa hajaachika isipokuwa litakapozama jua, ikiwa atasema: “Kabla ya usiku” ataachika hivi sasa, ikiwa atamuoa Umara baada ya hapo: Atakuwa ameachika Zainab na wala sio Umara, ikiwa muda utakuwa mrefu kati ya wawili inakuwa hajaachika mmoja wao”.
Vilevile: Yaliyosemwa na Wanachuoni wa Imamu Shafiy - nao ni Wanachuoni wengi waliotumia neno muda mfupi - katika mlango wa mambo ya usafi, kwenye kadhia ya utaratibu wa viungo vya kuoshwa ikiwa hatokaa ndani ya maji kwa muda unaoruhusu kufanyika utaratibu.
Amesema Sheikh Al-Islam Zakaria Al-Answaariy katika kitabu cha: [Asnaal-Matalib 1-34 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy] “Ikiwa ataoga mwenye uchafu kwa nia ya kuondoa uchafu au mfano wake, hata ikiwa kwa makusudi au kwa nia ya kuondoa janaba au mfano wake au kuzamia kwa nia iliyotajwa, ikiwa mwenye kuanza kwa chini yake (inamtosha) na kutawadha, hatakama hatokaa katika kuzamia muda unaowezekana kufuata mpangilio, kwa sababu kuoga kunakotosha kwa osho kubwa, basi dogo ni bora zaidi, na kwa kukadiria utaratibu katika wakati mfupi, kinyume na Rafii katika kauli yake: “Kwa hakika inamtosheleza ikiwa atakaa muda”.
Vilevile: Yaliyotajwa kuwa mwenye kukojoa inapendaza kwake kusubiri kiasi cha saa moja baada ya kumaliza kwake kukidhi haja yake, ili aweze kupata kujitenga na mkojo, amesema Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Sharh Al-Muhadhab 2/90, chapa ya Dar Al-Fikr]: “Wamesema watu: Inapendeza kusubiri saa, wana maanisha: Muda mfupi”.
Vilevile yaliyosemwa kuwa mwenye kuwahi kusimama Arafa kwa muda mfupi tu kati ya wakati wa kuzama kwa jua siku ya Arafa na kuchomoza kwa Al-fajiri ya pili ya siku ya kuchinja, basi huyo anazingatiwa ni katika watu waliosimama: Ni sahihi kusimama kwake na kwa kisimamo hiko atakuwa ameipata Ibada ya Hija. [Angalia kitabu cha Al-Majmuu, 8/102].
Amesema An-Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Majmuu, 8/203]: “Amesema Imamu Shafi na watu wake: Cha kuzingatiwa ni kuhudhuria sehemu ya eneo la Arafa, walau kwa muda mfupi sana kwa sharti kuwa kwake ni mtu wa Ibada”.
Hapa muda mfupi ni: Anayoyapata ndani ya muda huo ni machache zaidi ya yanayoaminika kwa jina la kusimama.
Na vilevile: Kuvua kwao masuala ya uuzaji kamili kutoka kwenye hiyari katika kuuza:
Amesema Imamu Shihaabdiin katika kitabu chake cha: [Asnaa Al-Matalib 2/46] “Inapaswa kuvuliwa uuzaji kamili katika kauli yake: (Mwache huru mtumwa wako kwa ajili yangu kwa thamani fulani) inakuwa ni lazima kukadiria kuingia kwake katika umiliki wa mnunuzi kabla ya kuachwa kwake huru, na hilo ndani ya muda mdogo usioweza kuletewa makadirio mengine, hiyari ndani ya huo muda haiwezekani”.
Miongoni mwa hayo: Yaliyokuja katika kitabu cha Mwanachuoni Sheikh Abdulhameed As-Sharwaniy kwenye kitabu cha: [Tuhfatul-Muhtaj cha Ibn Hajar, 4/335 chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Ikiwa atasema: Ikiwa nitakuuza, basi wewe upo huru, kisha akamuuza, ni sahihi na atamwacha huru haraka, sababu anakadiriwa kuingia katika miliki ya mnunuzi ndani ya muda mfupi, sawa na ilivyoelezewa na mfafanuzi katika uuzaji kamili”.
Pia: Waliyoyasema katika maswala ya uuzaji wa kitu cha kukodiwa.
Imekuja kwenye kitabu cha: Al-Minhaj na Sherehe yake [Tuhfatul Muhtaj cha Ibn hajar Al-Haitamy, 6/199]: “Inafaa kuuza kitu cha kukodi wakati wa kukodishwa ambapo hakuna kizuizi kama vile kuuza kitu kilichoporwa na mporaji, lakini haifai kuuza mnunuzi kabla ya kukabidhiwa na muuzaji, hii ni kutokana na udhaifu wa umiliki wake, wala hakuvunjwi kukodi kwa kauli sahihi, kwa sababu kina manufaa, na kumiliki mtumwa hakupingani… Hata kama kilichouzwa kitarudishwa kwa kasoro: kamilisha kwa muda uliobaki, au kuvunja makubaliano ya kukodi kwa kasoro au kuharibika kwa kitu: rudisha malipo kwa muda ulio baki, “Ikiwa atakiuza kwa mtu mwengine” na imekadiriwa kwa muda: Inafaa kwa kauli ya wazi, hata kama si ruhusa ya mkodishaji, na mkono wa mkodishaji hauzingatiwi kizuizi kwa sababu ya uaminifu, na kisha mnunuzi hazuiliwi kukipokea ndani ya muda mfupi ili kiingie kwenye miliki yake, kisha kinarudi kwa mkodishaji, na husamehewa kiwango hiki kidogo kwa dharura”.
Pia: Masuala ya kumtaka mwengine kuacha huru:
Ametaja Imamu Al-Haramain katika kitabu cha: [Nihaayat Al-Matwalab 14/538, chapa ya Dar Al-Minhaj] masuala: Ikiwa mtu atasema kumwambia mmiliki wa mtumwa “Mwache huru mtumwa wako kwa ajili yangu nitakulipa elfu moja” kisha akamwachia, basi atatakiwa kumwacha huru, na anakuwa kwa aliyemhitaji, na anastahiki mwenye kuacha huru kulipwa badala.
Kisha Imamu Al-Haramain akatengeneza sura hii na kuhamisha muundo wake katika sura ya kuhamisha umiliki na wakati wake, kwa sababu katika umuhimu wa kumtumia mtumwa kwa muhitaji ni kuhamishia umiliki kwake, ambapo ni katika yasiyowezekana kufungamana kuacha huru kwa muachaji kwenye miliki yake kisha ikawa na mtu mwengine.
Amesema Imamu Al-Haramain, ]14/538, sura ya tatizo]: Ni kuwa ikiwa tutasema: Umiliki unahama kabla ya kutamka kuacha huru, hilo linakuwa ni kutanguliza hukumu ambayo inayolazimisha tamko juu ya tamko, na hili haliwezekani. Ikiwa tutahamisha umiliki baada ya kuacha huru, maneno yanakuwa ni yenye mgongano, ikiwa tutaweza kuamisha umiliki pamoja na kuacha huru, inakuwa ni kukusanya pamoja kati ya vinyume viwili”.
Kisha akataja Imamu Al-Haramain, [14/539] kuwa kichwa na njia ya watu wa Imamu shafii wa Iraq Sheikh Aba Hamid Al-Isfuraabiniy ameleta ufumbuzi kwenye tatizo hili kwa kusema: “Pindi akimaliza neno la kuacha huru, baada ya muda mfupi akataka umiliki hutekelezwa kuacha huru kunakotona na tamko, na hilo ni katika nyakati mbili hazifahamiki kwa hisia kuzitengenisha”.
Na njia hii ya Sheikh Abi Hamid ni yenye pande tano katika masuala yaliyotajwa na Imamu katika kitabu cha: [Nihaya 14/538, 539] na sura hii ndiyo ambayo ameisahihisha Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Ar-Rawdha 8/295 chapa ya Al-Maktab Al-Islamiy] na kupitishwa na watu wa Shafiy, amesema Sheikh Al-Islam Zakaria Al-Answariy katika kitabu cha: [Asnaal – Matwaalib 3/366]: “Mtumwa aliyeachwa huru kwa mwenye kumhitaji, basi anaingia kwenye miliki yake, ambapo hakuna kuacha huru pasi na kumiliki, kisha kuacha huru kunafungamana na kumiliki na kuwa inaungana nayo na hilo ni katika wakati mfupi, kwa sababu kuacha huru kumetokea kwa mtu mwingine, inatakiwa kutangulia umiliki, ikiwa atakuta kutafungamana na kumwacha huru”.
Akasema pia katika kitabu cha: [Sherehe ya Bahjat Al-Wardiya, 5/308 chapa ya Al-Maimaniyah]: Kuacha huru katika: Mwache huru mtumwa wako kwangu hufungamana na umiliki kwa muda mfupi, ambapo kwa kuacha miliki maana yake: Muhitaji anammiliki mtumwa kwa kuachwa kwake huru, ni ngumu kukadiria kutoa miliki yake kwa kukamilika tamko la kuacha huru, kutokana na kuwa ndani yake kuwepo yanayolazimisha kuyatolea tamko, wala haiwezekani kutanguliza kuacha huru kwa kubakia umiliki kwake wala kufikiwa vyote viwili kwa pamoja kwa kupingana kwake, na wala hakuna isipokuwa atachelewa kuacha huru kwa kile anachomili”.
Pia: Aliyoyataja An-Nawawiy katika kitabu cha: [Ar-Rawdha 12/65] miongoni mwa ufafanuzi unaodai hakuna ulazima wa kuthibiti umiliki kwake, lakini unadhihirika, hivyo kulazimika kuwa mmiliki aliyepita unaendelea umiliki wake, lakini bila kushartisha kupita muda mrefu, inatosha kupitishwa na mashahidi kwa muda mfupi.
Hapa muda mfupi: Ni chini ya muda unaozingatiwa mmiliki yupo huru.
Ikiwa ni pamoja na maswala: Ikiwa binadamu atataka kutoa sadaka manufaa anayomiliki na kufanya imani hiyo inakamilika baada ya kufa kwake, ambapo hunufaika na manufaa hayo wakati wa uhai wake, njia ya hilo: Ni kusimamisha hayo manufaa katika uhai wake, na inashurutishwa kutoa kilichosimamishwa kinaendana na kifo, na amenukuu Imamu Zarkashy kufaa kwake kutoka kwa kadhi Al-Hussein miongoni mwa watu wa shafii, kama alivyotaja Mwanachuoni Al-Khatwib katika kitabu cha: [Alknaai” 3/252 chapa ya Dar Al-Fikr], na matumizi haya yamekuwa yenye kusuasua kati ya kuendana na wakfu na kuendana na wasia, ambapo kuna hali ya kufanana kati ya wakfu na wasia, na waliopitisha kuwa kwake wakfu kunakuja kutokana na muda mfupi kabla ya kutekeleza makusudio ya mmiliki, na kuingia makubaliano ya wakfu wakati wa uhai wake, na muda huu mfupiunaofananishwa hakuingii matumizi hayo katika mlango wa wasia ambao unanasibishwa kikamilifu na yale ya baada ya kufa.
Pia: Ikiwa mtu amenunua kitu na akadai mwenye kudai na akakichukua kwa hoja, basi inathibiti kwake kukirejesha kwa muuzaji, kwani ufafanuzi haulazimishi umiliki bali hudhihirisha kitu, ni lazima kuwa mmiliki wa kwanza kuwa nacho, na kukadiriwa kwake muda mfupi, angalia kitabu cha: [Al-Bahrul-Muheet cha Imamu Az-Zamarkashiy chapa ya Dar Al-Kutub, Kairo 8/25].
Amesema Sheikh Al-Islaam Zakaria Al-Answariy katika kitabu [Asnaa Al-Matwalib 4/412]: “Ushahidi wa mdai huonesha umiliki wake ni lazima ukweli wake kutolewa hata kwa muda mdogo”.
Ufupisho wa yote: Masuala yaliyokuja kwenye swali yamekuwa na Hadithi nyingi, moja wapo ni Hadithi iliyopo kwenye sahihi ya Muslim na vitabu vingine vya Sunna. Wanachuoni wamechukulia kwa ujumla, pamoja na kutofautiana katika ufafanuzi wake, baadhi ya Wanachuoni wameleta ufumbuzi na kufahamu uwazi wa tamko la hizi Hadithi kwa kile kilichoelezewa “Muda mfupi” na wakati mwiengine wanaelezea “Saa chache” au “Muda mfupi” nao ni: Muda unaokadiriwa hupanuka kwa kufikiwa kusudio, wameutumia Wanachuoni wengi katika kuondoa matatizo ya kielimu na kutatua migongano ya Kisharia katika masuala mengi na matawi mbalimbali yaliyopelekea kuondoa kanuni kuu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Ofisi ya Kutoa Fatwa.