Maulidi ya Mtume S.A.W. na Vipindi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maulidi ya Mtume S.A.W. na Vipindi vya Dhikri na Matumizi ya Neno la Bwana kwa Mawalii

Question

Baadhi ya wahutubu wa Swala za Ijumaa katika nchi zetu wanadai kuwa:
1- Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume si jambo la Kisharia.
2- Ketembea kwa kutumia vipando kupeperusha bendera na kupiga dufu kwa ajili ya maulidi si jambo la Kisharia.
3- Kufanya maadhimishao ya mazazi ya Mtume usiku si jambo la Kisharia.
4- Kununua vitu vitamu na kuvitoa sadaka kwa sababu ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume si jambo la Kisharia.
5- Kusimama katika vipindi vya Dhikri na kuyumbayumba si jambo la Kisharia.
6- Kutumia neno: “Bwana” kwa mawalii si jambo la Kisharia.
Ni ipi hukumu ya hayo?
 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume S.A.W. kunazingatiwa ni katika matendo yaliyo bora zaidi na ni katika mambo makubwa ya kumuweka mtu karibu, kwa sababu maadhimisho ni kielelezo cha furaha na upendo kwa Mtume S.A.W. ambapo upendo huo ni asili katika asili za Imani, imepitishwa kutoka kwake Mtume S.A.W. amesema: “Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka niwe ni mwenye kupendwa zaidi kwake kuliko anavyowapenda wazazi wake, watoto wake na watu wote”. imepokelewa na Imamu Bukhari.
Kuadhimisha kuzaliwa kwake Mtume S.A.W. ni katika upande wa kumuadhimisha, na kumwadhimisha Mtume S.A.W. ni jambo ambalo uhalali wake umepitishwa moja kwa moja, kwani Yeye Mtume ni neema kubwa kwa ulimwengu, na kushukuru neema ni jambo linalohitajika na ni zuri kwani mtendaji wake halaumiwi bali hushukuriwa.
Kwani Mtume S.A.W. ametuwekea mfumo yeye mwenyewe jinsi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuzaliwa kwake Mtume S.A.W., na ni sahihi kwamba Mtume S.A.W. alikuwa anafunga siku ya jumatatu na alikuwa anasema: “Hiyo ndio siku niliyozaliwa” imepokelewa na Imamu Muslim katika Hadithi ya Abi Qatadah R.A. nayo ni shukrani yake Mtume S.A.W. kwa neema ya Mwenyezi Mungu kwake na kwa Umma wake, ni bora kwa Umma kumuiga Mtume S.A.W. katika kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila aina za shukurani kwa kupewa kwao Mtume huyu na kuteuliwa kwake Mtume S.A.W.
Kusudio la maadhimisho ya Kisharia ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume ni kukusanyika watu kwenye kumtaja, na kuimba katika kumsifu yeye S.A.W., kulisha chakula watu kama sadaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kutangaza upendo kwa bwana wa viumbe ambaye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., kutangaza furaha kwa siku aliyokuja Mtume S.A.W. kwenye dunia yetu.
Kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake katika tuliyoyasema miongoni mwa yaliyofanywa na waja wetu wema waliotangulia tokea karne ya nne na tano, na kutaja juu ya uhalali wake si Imamu mmoja miongoni mwa Wanachuoni mbalimbali walioandika au katika kusifu kwenye vitabu vyao, miongoni mwao ni: Abu Shaamah Al-Maqdasiy Sheikh wa Imamu An-Nawawiy, na Ibn Al-Haaj katika kitabu chake cha: [Al-Madkhal] “Utangulizi”, na Hafidh Ibn Hajar mshereheshaji wa kitabu cha Imamu Bukhari, na Al-Jalaal As-Suyutiy katika kitabu cha: [Risaalatul Mustaqilah alichokiita Hasanul Maqsad fi Amalil Maulidi]: “Makusudio mema katika mambo ya maulidi”.
Imenukuliwa na mja mwema katika kitabu chake cha: [Sira ya Mtume Subulul Hudaa warrashaad fii Siirati Khairil Ibaad] “Njia ya uongofu katika mwenendo wa mbora wa waja” baadhi ya maneno ya waja wema kuwa: Siku moja alimuona Mtume S.A.W. usingizini, akamfikishia malalamiko kuwa baadhi ya watu wanasema ni uzushi kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mtakatifu. Mtume S.A.W. akasema: “Mwenye kutufurahia tunamfurahia” kuona ndotoni pamoja na kuwa haithibitishi hukumu ya Kisharia isipokuwa huchukuliwa kama ushahidi katika yale yanayokubaliana na asili ya Sharia Takatifu.
Yale yaliyozoeleka kwa watu ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vitu vitamu na kutoa kama zawadi katika maadhimisho ya kumbukumbu za mazazi ya Mtume S.A.W. yenyewe ni mambo yanayofaa, hakuna dalili zilizokuja kuzuia maadhimisho haya au kuhalalika kwake wakati mmoja pasina wakati mwingine, hasa ikiwa kutajumuisha katika hilo makusudio mema kama vile kuingiza furaha kwa watu wa familia na kuunganisha undugu wakati huo linakuwa ni jambo lenye kupendeza na kutakiwa na kuna thawabu Kisharia, kauli ya uharamu au kuzuiliwa ni aina ya maelezo yasiyokubalika.
Ama yanayofanyika baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na vitendo vya kupanda vipando na kuwatembeza waadhimishaji wa mazazi ya Mtume wakiwa wamebeba bendera zilizonakishiwa baadhi ya alama za kidini, wakiimba kwenye misafara hiyo nyimbo za sifa mbalimbali za Mtume S.A.W. jambo hilo halina ubaya wowote pindipo tu limeepukana na na yanayopingana na Sharia kama vile mchanganyiko usiokubalika au kukwamisha masilahi ya umma na mfano wa hayo.
Ikiwa upigaji wa dufu katika mambo ya ndoa ni jambo lililopitishwa na Sharia ikiwa ni katika kuonesha hali ya kufurahia ndoa, na katika hilo kuna Hadithi inayotokana na Tirmidhiy: “Tangazeni ndoa hizi, na zifanyieni misikitini na pigeni na dufu” matumizi ya dufu ili kuonesha furaha ya kuzaliwa kwa mbora wa viumbe basi ni bora zaidi, na kufaa kwa hayo yote kwa sharti la kuchunga adabu zinazotakiwa Kisharia katika tukio kama hili.
Ama kuhusu kusimama katika vipindi vya dhikri na kuyumbayumba katika kusifu kwake, tunasema: Hakika Mwenyezi Mungu Amewataka Waislamu kuleta utajo moja kwa moja na Akasema: {Enyi mlio amini! Mtajeni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumtaja} [AL AHZAAB: 41], Akasema tena Akiwa Anawasifu waja wake Waumini: {Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala} Aal-Imraan: 191, na kutoka kwa Abi Musa Al-Ash’ary R.A. anasema Mtume S.A.W. amesema: “Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake ni mfano wa mtu hai na maiti” imepokelewa na Imamu Bukhari. Na imepokelewa na Imamu Tirmidhiy na Ibn Majah Hadithi inayotokana na Abdillah Ibn Masuud R.A. amesema kuwa kuna mtu mmoja alimwambia Mtume S.A.W.: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika Sharia za Kiislamu zimekuwa nyingi kwangu basi nifahamishe kitu cha kushikamana nacho, akasema: “Ulimi wako usiache kuwa laini kumtaja Mwenyezi Mungu”, kuhimiza juu ya dhikri kumekuja moja kwa moja kwenye Sharia Takatifu, hivyo asili ni kuwa dhikri haufungamanishwi kwa hali moja pasina hali nyingine au kufungamanishwa na wakati pasina wakati mwingine.
Kwa vile Sharia haijakataza kusimama wakati wa dhikri, hilo limekuwa kwa asili ni halali, pindipo tu mwenye kufanya dhikri amewajibika na hali ya utulivu wakati wa dhikri, wala hakuja na jambo linalopingana na adabu zinazohitajika mbele ya Mwenyezi Mungu wakati wa dhikri, na anatakiwa mwenye kudai uwepo wa zuio au uharamu kuleta dalili ya madai yake ambayo yanapingana na asili.
Na inasisitizwa kufaa ikiwa harakati za mfanyaji dhikri zimefanyika katika hali ya kutojijua kama vile kuzidiwa kwenye dhikri kwa hali ya upendo zaidi na kufanya kitendo pasina kukusudia kama alivyosema mshairi:
Hakika yangu napata utukufu kwa mtikisiko wa utajo wako - kama anavyoamka ndege aliyeloweshwa na umande.
Imepokelewa na Haafidh Abu Naiim kutoka kwa Imamu Ally R.A. amesema katika wasifu wa Sahaba: “Pindi anapotajwa Mwenyezi Mungu, basi yumbeni kama unavyoyumba mti wakati wa upepo na kutangatanga macho yoa kabla ya nguo zao” hii ni athari ya wazi kuwa Masahaba walikuwa wakiyumbayumba sana katika dhikri.
Amesema Mwanachuoni Ibn Kamal Basha ni miongoni mwa Wanachuoni wa Imamu Abu Hanifah pindi alipokuwa akitoa Fatwa kwenye masuala haya:
Hakuna ubaya wowote unapofanukiwa kujikurubisha (kwa Mwenyezi Mungu)
Wala sio vibaya kuyumbayumba unapokuwa na nia njema
Ufupisho ni kuwa, kwa vile kumekuwa na udhibiti wa adabu kwenye utajo pasina ukiukaji wa matamshi ya utajo kwa hali inayo haribu maana yake basi hakuna maana ya kuzuia.
Ama kuhusu kutumika bwana kwa viumbe, ikiwa bwana anayekusudiwa ni Mtume S.A.W. basi jambo hilo ni halali na linatakiwa kwa kauli za Wanachuoni wote Wakiislamu, kwani mwenyewe Mtume amelitaja hilo kwake na akasema: “Mimi ni bwana kwa watoto wa Adam” katika upokezi mwingine “Mimi ni bwana kwa watu wote” imepitishwa na Wanachuoni wa Hadithi, na Mwenyezi Mungu Ametuamrisha kumuheshimu na kumtukuza Akasema: {Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumheshimu, na mumtakase asubuhi najioni} [AL FAT'H: 09], katika kumuheshimu ni pamoja na kumfanya bwana, kama alivyosema Qatadah “Kumuheshimu” ni kumfanya bwana.
Ama kuitwa mtu bwana asiyekuwa Mtume S.A.W. nalo pia ni jambo halali kwa andiko la Qur`ani na Sunna pamoja na matendo ya Umma waliotangulia na waliopo pasina kupingwa.
Amesema Mola kuhusu Nabii Yahya A.S.: {Alipokuwa kasimama chumbani akiswali, Malaika akamwita: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, atayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mtawa na Nabii kwa watu wema} [AAL IMRAAN: 39]. Amesema Imamu Qurtubiy: “Ndani yake kuna dalili kufaa mwanadamu kuitwa Bwana kama vile inafaa kumuita kipenzi au mtukufu”.
Ama kwa upande wa Sunna ni kauli ya Mtume S.A.W. kuhusu Hassan na Hussein A.S.: “Hassan na Hussein ni mabwana wa vijana peponi” imepokelewa na Tirmidhiy na Haakim na kuisahihisha.
Na kauli yake Mtume S.A.W. iliyopokelewa na Imamu Bukhari kuhusu Hassan Ibn Ally A.S.: “Hakika mtoto wangu huyu ni Bwana”.
Na kauli yake S.A.W. kuhusu Saad Ibn Muadh R.A. – akiwaambia Masahaba watukufu – “Msimamieni bwana wenu” imepokelewa na Imamu Bukhari.
Ama kitendo cha Umma: Miongoni mwake ni kauli ya Umar R.A. kuhusu Abubakar na Bilal R.A.: “Abubakar ni bwana wetu na amemkomboa bwana wetu” imepokelewa na Imamu Bukhari.
Nukuu za mfano wa hili ni nyingi, imesikika kwa Masahaba pasina kupingwa, hilo likawa ni sehemu ya kukubalika kwa wote, na walionyamazia miongoni mwao juu ya uhalali wake, ni hoja pia kama inavyosemwa kwenye kanuni.
Kwa maelezo hayo, kutumika neno bwana kwa watu wa nyumbani kwa Mtume na kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu ni jambo la Kisharia, bali ni lenye kutakiwa Kisharia, kutokana na kuwemo ndani yake adabu njema kwao na heshima pamoja na utukuzo, na Mtume S.A.W. anasema: “Si katika sisi asiyemuheshimu mkubwa wetu na kumuhurumia mdogo wetu na kufahamu haki za wasomi wetu” imepokelewa na Ahmad pamoja na Hakim na kusahihishwa na Ibadatu Ibn Saamit R.A.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Katibu wa Fatwa 2007/04/12

 

Share this:

Related Fatwas