Urithi wa Kiislamu na Miundo ya Kil...

Egypt's Dar Al-Ifta

Urithi wa Kiislamu na Miundo ya Kilugha na Kimantiki Kama Chombo cha Kuifahamu Lugha.

Question

Ni ipi nafasi ya miundo ya kilugha na kimantiki katika kufahamu urithi wa Kiislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Miundo ya kilugha na kimantiki ni vipengele muhimu ambavyo vimeandikiwa urithi, na ambavyo sisi tunahitaji kuvifahamu ili tuweza kuwa na ufahamu wa kina kwa yale tuliyonayo ikiwa ni pamoja na maandiko ya urithi.
Kuna uelewa maalumu na mtazamo maalumu wenye kuingiliana na miundo ya kilugha na kimantiki, na kutengeneza sura jumla ya muundo wa fikra kwa watu waliotangulia, na huu umaalumu wa kwanza wa miundo hii ni Jumla kamilifu. Kumekuwa na tofauti ya maana ya jumla kamilifu – maana iliyowazi na muhimu – kati ya elimu za balagha mantiki na zinginezo, na kama ilivyotangulia na kuwekwa wazi – katika somo la kwanza – jumla kamili inagawanyika sehemu mbili zilizowazi na sehemu ya tatu haipo wazi, kumekuwa na tofauti ya kuitwa kila sehemu katika sehemu hizi kwa tofauti ya elimu ambayo unayoitumia, watu wa mantiki wanazungumza walivyoitwa kwa jina la “Maudhui” na “Ukamilisho” watu wa balagha wanasema “Chanzo” na “Kinachoegemezewa” watu wa kanuni za lugha wanaita “Mwanzo” na “Habari” au “Kitenzi” na “Mtendaji” na kama hivyo, hivyo jumla kamilifu yenyewe inaitwa kwa majina tofauti, mfano: Kadhia, masuala, na maneno yote hayo yaliyotangulia yanakubaliana katika maana.
Kila elimu miongoni mwa elimu ambayo imezaliwa na wana urithi ndani yake kuna jumla kamilifu ambayo imesha ashiriwa, katika elimu ya Fiqih au Sharia ya Kiislamu inaitwa, Maudhui – au sehemu ya kwanza ya jumla – nayo ni “Kitenzi kilichopewa jukumu” na ukamilisho – au sehemu ya pili ya jumla – ni hukumu katika hukumu za Mwenyezi Mungu Mtukufu, swala kuuza na kununua vyote hivi ni vitendo vinafanywa na mwanadamu, ima vitakuwa halali, lazima, vinachukiza ambapo kila hukumu katika hakumu hizi za kisharia zinaelezea kitendo cha mwanadamu, pindi tunapokusanya kati ya kitendo na hukumu yake huwa tunatengeneza jumla timilifu au masuala au kadhia ya kifiqih.
Katika elimu ya msingi, tunakuta kuwa maudhui – au sehemu ya kwanza ya jumla – ni “Dalili ya kisharia” na “Kuithibitisha kwake kwenye hukumu” ndio kamilisho. Kitabu sio kwa upande wa kuwa kwake kipo katika sura ya msahafu au kwa upande wa namna ya kuandikwa wala sio kwa upande wa kuhifadhiwa kwake, lakini ni kwa upande wa namna gani ya kufahamika kwa hukumu za kisharia, vilevile Sunna, Ijmai (Makubaliano ya wanachuoni) kipimo cha hukumu….nk, dalili hizi hutengeneza jumla au kadhia kwenye elimu ya misingi ya sharia.
Hivyo basi kadhia ya jumla kamili ni kadhia muhimu sana, tunaangalia ndani yake kile kinachoitwa “Chanzo” au “Nasaba” au “Kipengele cha tatu kilicho jificha, ambacho ndio uhusiano kati ya vipengele viwili, cha kwanza: Ni mwanzo na habari. Hivyo Nasaba ni kuthibitisha jambo au kulikanusha.
Ili nimfikishie ninayemzungumzisha kile ninachotaka kumwambia na kuwa ni chenye kufahamika ni lazima kuhakikisha utimilifu wa uhabari, ikiwa utasema: Mti mrefu wa kijani ambao upo nje, yote haya ni mambo au sifa za kuainisha maudhui ni lazima tuelezee kwa uwazi maudhui hii, kinyume na hivyo basi hali ya jumla kutoeleweka itatokea kwa mwenye kuzungumzishwa ambapo kwenye akili yake kutaibuka maswali mengi kuhusu maneno yako: Upo wapi mnasaba kwenye maelezo hayo? Na kwa hali hiyo ikiwa utasema “Mti” na ukanyamaza utakuwa umezungumza neno lisilofidisha maana, ikiwa utasema baada yake “…….wenye matunda” sentensi au jumla inakuwa ni imekamilika na kuleta faida au kunufaisha.
Na hali hiyo, pindi tunaposoma urithi ni lazima tutafute mnasaba kamili, kwa maana kwenye sentensi yenye kufidisha, kinyume na hivyo ikiwa hatuwezi kuwa na chanzo cha sentensi kwenye habari, wala kitendo na mtendaji basi inakuwa haiwezekani kutengeneza ufahamu kamili na sahihi wa matini ya urithi huu.
Ndani ya baadhi ya vitabu vya urithi tunakuta miundo ya sentensi ni yenye mianya mirefu kati ya chanzo cha sentensi na habari yake, au mtu anaweza kusoma matini kwa usomaji wenye makosa na kuamini kuwa kuna mwanzo wa sentensi ameuelezea wakati ambapo mwandishi anakuwa hajaelezea, kwa mfano mtu anasema “Mti wa kijani upo nje….. wenye matunda”, msomaji atafahamu kuwa habari hapa ni hili neno nje au kijani, na hili ni kosa, kwa sababu sifa hizo – kwa ukweli – zipo kwa kuainisha maudhui tu lakini ni lazima kuwepo na habari inayoelezewa, hivyo ni juu yetu kuyafahamu maswala haya na kutafuta sentensi yenye kufidisha.
Mtazamo wetu kuwa muundo wa kilugha wote unajengeka juu ya “Sentensi au jumla yenye kufidisha” inatusaidia kufahamu mambo mengi ya urithi.
Sentensi yenye kufidisha madai kadhia na masuala, ni mambo yanatuhitaji dalili. “Swala ni lazima” ni jumla iliyokamilika, lakini ni nani aliyesema kuwa Swala ni lazima? Ni ipi dalili ya hilo? Hapa tunaangalia maana za jumla mbalimbali: Kuna jumla njia ya kuthibitisha mnasaba (Kwa maana ya uhusiano kati ya habari na mwanzo) ni kwa hisia, kwa maana ya ufahamu wa kihisia, pia kuna baadhi ya jumla njia ya kuthibitisha mnasaba inakuwa ni kwa akili, na kuna jumla zinathibitishwa mnasaba kwa kunukuu ni sawa sawa kunukuu kwa watu wenye weledi maalumu au kwa njia ya Sharia Takatifu. Hivyo basi kuna dalili ambazo zinakuwa ni dalili za hisia, na zingine zinakuwa ni dalili za kiakili, na zingine zinakuwa ni dalili za kisharia, na zingine zinakuwa ni dalili za kutungwa, kwa maana ya zimewekwa na kikundi maalumu, na tumelitolea hilo mifano kwa ufupi huko nyuma.
Hivyo masuala na kadhia huwa na tofauti, hutofautiana dalili zinazothibitisha hayo, kwa maana ya kuthibitisha minasaba hiyo, lakini nini maana ya uthibiti? Baada ya kukutwa kuwa lugha inatengenezwa na jumla au sentensi yenye faida kwa maana ya kufidisha, na hii jumla yenye faida inatengenezwa na sehemu mbili kati yake kuna uhusiano, na kuna dalili zinazothbitisha uhusiano huo, kisha baada ya hapo kumekuwa na aina mbalimbali za dalili na kuwa kuna dalili ya kisharia na nyingine ya kunukuu na nyingine ya kihisia ili kuthibitisha uhusiano, wamekuta kuwa mambo ya dalili yanaibua aina ya maswali yenye faida: Je ni lazima kuwepo dalili kwenye kila sentensi au jumla mpaka anayeambiwa aamini ninachosema? Pindi anaposema mzungumzaji: “Mti wenye matunda” basi kuna kuwa na uwezekano wa aina mbili kwa anayeambiwa: Ima aamini au asiamini. Ikiwa hatoamini basi jumla hiyo inahitaji dalili ambapo dalili yenyewe hapa ni mzungumzaji kumchukua huyu anayeambiwa na kumuonesha huo mti, ama ikiwa atasema: Swala ni lazima, na akasema mwenye kuambiwa: Ipi dalili ya hilo? Basi mzungumzaji anapaswa hapa kungalia dalili ya kimaandiko, na atasema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: “Simamisha Swala” na hii ni amri, na kila amri ina uwajibu, hivyo Swala ni lazima, na kuwa kila amri inawajibu inarejea kwenye kusoma na kufuatilia, tunakwenda kwenye Sunna na makubaliano ya wanachuoni ili kuthibitisha kuwa kila amri ni wajibu au ina maana ya lazima.
Hakika hali hii – kwa maana ya kusimamisha dalili kwenye jumla au madai – inakwenda kwenye hatua mbili ambazo: Mtu kufahamu nayo ni hatua ya kufikiria, kisha kufahamu mnasaba pamoja na kukubali hiyo ni hatua ya kusadikisha, hivyo tunakuwa na sehemu mbili kufahamu – kwa maana ya kupata picha ya kitu kwenye akili – sehemu ya kwanza inaitwa Taswira, nayo ni mtu kufahamu, sehemu ya pili inaitwa kukubali nayo ni kufahamu mnasaba kiakili, pindi uliposema: “Mti” nimefahamu picha fulani inayojengeka akilini, na pindi uliposema “Wenye matunda” akili inajengeka picha tunda na matunda kama vile akilini kuna kuwa na uhusiano kati ya hayo mawili, kufahamu mti na kufahamu matunda na tunda na kufahamu kunasibishwa matunda na mti kunakuwa ni katika upande wa taswira kwa sababu kufahamu vitu pasi ya kuvikubali kuwa hivyo ni vitu sahihi na jumla hii au sentensi hii imefahamika na kukubalika.
Watu wote – kwa mfano – wanajua maana ya “Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu”, “Muhammad” S.A.W wanafahamu kuwa ni mtu ambaye alizaliwa katika mji wa Makkah na alifariki ndani ya mji wa Madinah, kaburi lake linatembelewa mpaka leo hii, amekuja na Dini inayoitwa Uislamu…..na kama hivyo. “Mtume wa Mwenyezi Mungu” pia maana yake inafahamika kuwa ni kiumbe na amefunguliwa ufunuo toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu….mpaka mwisho wake. Vilevile inafahamika mnasaba huo, lakini haina maana “Kufahamu kwao” yote hayo ni kuwa wanayaamini, kukipatikana kuamini kwenye akili hapo wanakuwa wameamini, ikiwa hakuna imani hiyo akilini hawatakuwa waumini, hivyo kuna tofauti kati ya kufahamu na kuamini.
Kuleta taswira ni hatu ya kufahamu ama kuamini ni hatua nyingine, ikiwa kwa mfano nina picha ndani ya akili yangu ninataka kuihamisha na kuileta kwenye akili yako ili unifahamu basi ni namna gani nitaiwasilisha kwako?
Hapa wamesema wanachuoni: Kufikisha kile kilichokuwa akilini kwa msikilizaji kupitia maneno yanakuwa kupitia “msamiati” unaoitwa kwa jina la uelewa au mpaka. Kwa mfano mtu anapomwambia mwenzake: “Al-Hintwah ni nyingi” neno hintwah huwenda likawa si neno maarufu na kufahamika na mwingine, hivyo anasimama bila ya kufahamu na kulazimika huyu mtu wa kwanza kuliweka wazi zaidi kwa tamko lingine, kuwa hiyo Hintwah ni ngano. Hapa ambacho kimetokea ni kule mzungumzaji kufahamisha neno kwa uelewa wa kitamko, kwa maana amekuja na neno kisawe na lile lisilofahamika, amekuja na tamko lenye kufahamika kwa msikilizaji ili kumfahamisha neno hilo kwa neno lingine ambalo hakulifahamu.
Na huenda kusudio la uelewa ni kufahamu kitu, kwa maana ni nini hiko kitu, hapa tunakimbilia kwenye taswira jumla ambayo imeelezewa kwenye vitu vilivyomo ambavyo vinagawanyika kati ya vile visivyo na upande wowote na vile vilivyo na upande fulani, kuwa upande fulani ni maudhui, na kutokuwa upande wowote ni lengo, ama maudhui pindi inapokuwa ni moja huwa tunaiita sehemu ambayo isiyogawika, ama ikiwa ni nyingi huwa tunaita mwili, huu mwili kuna aina nyingi, miongoni mwake ni pamoja na ule unaokuwa na usiokuwa, kwa mfano ubao wa kuandikia ukiuacha siku moja na kuendelea hauzidi lakini unabakia kama ulivyo, ama mmea ukiwa utauacha siku moja na kuendelea utaukuta unaongezeka kidogo kidogo, vilevile mtoto anakuwa na tunda linawiva, na katika aina hii ya tunda tunakuta linagawanyika sehemu mbili: Sehemu ya kwanza inafanya kazi kwa utashi na sehemu nyingine si kwa utashi, kwa mfano mmea ukiwa utauacha sehemu fulani basi hata kama utakuwa wewe hautakugundua mabadiliko yeyote sehemu yake baada ya siku mbili za kuuacha, ama sehemu ambayo inafanya kazi kwa utashi ni mfano wa ng’ombe ambaye anakwenda huku na huku ikiwa utamwacha peke yake akitafuta chakula chake na kinywaji chake, kwani mnyama ni mwenye kufanya harakati kwa utashi wake, ama mmea hapana, huwa anataharaki kwa upepo au unataharaki kwa mwanga au unataharaki kwa majibu ya kitendo cha kinyume kama vile mimea ya porini haina harakati kwa utashi kwa kukosa huo utashi.

 

Hapa inawezekana kuchora ramani ya vitu kama ifuatavyo:
UWEPO
Kufungamana Kutofungamana

Maudhui Mwili
Chenye kukuwa Kisichokuwa

Chenye haraka Kisicho na haraka
Chenye kufikiri Kisichofikiri
Mti huu unatengenezeka kwa ngazi mbalimbali, tunakuta kila kitu kina tawi na kina asili, kila kitu kilichopo chini yake kina sehemu ya juu yake, na kuna kitu hakina kitu chini yake na chingine hakina kitu juu yake, aina zote hizi watu wa mantiki wameanza kuziita kwa jina maalumu, wakasema kwa kitu kilichokuwa chini yake kuna aina kuwa ni “Jinsi” na katika tawi lake “Aina” kuwepo ni jinsi katika jinsi, mwenye kuzungumza (Mwenye kufikiri) ni aina yeyote ile ambayo haina kitu chini yake, na tunakuta kuwa kila kimoja baada ya hapo ni jinsi kwa kilichokuwa chini yake na ni aina ya kilichokuwa juu yake…. Na kama hivyo tumekuwa na misamiati ya aina mbili.
Kama tunavyoona jinsi na aina ni kitu kimoja isipokuwa jinsi chini yake kuna vitu mbalimbali vilivyotimiliza vyenyewe kwa vyenyewe, kwa mfano mnyama ni jinsi lakini chini yake kuna wanyama, na chini yake wanyama kuna mwanadamu mwenye kufikiri na kutamka, na mwanadamu anatofautiana kwa tofauti ya wazi kabisa na mnyama, isipokuwa wote hao wanashirikiana kwenye harakati na kuwa na utashi, ama aina chini yake kuna vitu vinashikana, mwanadamu ni aina watu wake hawatofautiani ya kuwa kwake mwanadamu.
Lakini ni kitu gani kinatengenisha aina moja na nyingine katika jinsi? Mwanadamu ni mnyama na mnyama bado ni mnyama, ni kitu gani kinatenganisha kati yao? Wakasema: Ambacho kinatenganisha kati yao ni kule kutamka, mwanadamu anatamka kwa maana ya kuwa ni mwenye kufikiri na kupangilia mambo yanayofahamika na kufikia kwenye kitu kisichofahamika, ama mnyama hapana, tofauti ipo kwenye kufikiri, ama mpangilio wa mambo na kuzalisha fikra vyote hivi ni taratibu ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amempa mwanadamu ili apate kuijenga na kuiendeleza hii dunia ambavyo hivyo havipo kwa mnyama, hivyo wameita tofauti hii kwa jina la “Kipambanuzi” kisha tumekuwa na vitu vitatu ndani ya ramani iliyopita: Jinsi Aina na Kipambanuzi. Lakini tumeona sifa zinazohusisha aina, na tumeona sifa zinazoshirikiana kati ya aina na aina zingine chini ya jinsi moja, pamoja na kutotofautiana. Mfano kama kucheka kwa mwanadamu, mwanadamu anacheka kwa sababu amefahamu kitu tofauti kati ya vitu viwili, na kwa hali hii anafanya mzaha na utani, hali hii haipo kwa mnyama kwa maana hawezi kucheka, sifa hii ni maalumu kwa mwanadamu.
Lakini mwanadamu anatembea na simba pia anatembea, sifa ya kutembea ni ya jumla inashirikisha ndani yake vilivyo kwenye jinsi moja pamoja na tofauti na aina.
Kwa kuzingatia na kuweka akilini wamesema: Vitu hivi vitano ndio ambavyo mwanadamu ameweza kuvichunga na kuviita ni mambo jumla matano, nayo ni Jinsi, Aina, Kipambanuzi, Maalumu na Sifa shirikishi.
Jinsi wanaielezea kuwa ni dhati jumla inayotumika na kuitiwa wengi ndani yake waliotofautiana kwa ukweli katika jibu la swali la nani huyo, ndani yake kukiwa kuna “Mnyama” pia.
Aina: Ni vitu jumla vinavyoitiwa vitu vingi kwa ukweli vinakubaliana katika jibu la swali la nani huyo, kukiwa kuna “Mwanadamu” ndani yake.
Kipambanuzi: Ni dhati jumla inayotumika kuitia vitu vingi vinavyokubaliana katika jibu la swali la ni kitu gani hicho?
Maalumu: Ni hali jumla inayotumika kwa wengi wenye kukubaliana katika swala la ni kitu gani hicho maalumu?
Sifa shirikishi: NI hali jumla inayoitwa kwa wengi waliotofautiana katika swali la ni kitu gani hicho cha sifa shirikishi?
Wamesema: Pindi tunapotaka kufahamisha kitu na kuhamisha taswira hii ambayo ipo akilini mwetu na kwenda kwa wasikilizaji wetu, tunapaswa ufahamishaji huu kuwa ni jinsi na katika kipambanuzi, inawezekana kuwa katika jinsi na katika umaalumu, vilevile inawezekana kuwa katika jinsi tu au katika kipambanuzi tu au katika umaalumu,
Ikiwa ni katika jinsi na kipambanuzi basi wameita “Kiwango kamili”, ama ikiwa katika kipambanuzi tu au jinsi ya mbali na kipambanuzi cha mbali wameita “Kiwango pungufu”, ama ikiwa ni katika jinsi na umaalumu basi wameita “Mchoro kamili” ikiwa katika jinsi ya mbali na umaalumu au kwenye umaalumu tu basi wao wameita “Mchoro pungufu”….Nk.
Ikiwa tutaongeza kwenye uelewa wa matamshi kila kigawanyo na uelewa kwa mifano, basi aina za uelewa kwa watu wa mantiki zitatimia.
Lakini watu wa taaluma zingine – wasiokuwa watu wa mantiki – wanaita vyote hivyo ni “Uelewa” wanasema – katika maelezo yao – na “Wanafahamisha kwa maana hii….” Na huenda hilo likawa kwa mchoro au kwa mpaka kiwango fulani, ni jambo pana lakini katika kila uelewa ni lazima kutafiti kuhusu aina ambayo ina ainisha jinsi, na kipambanuzi kuainisha kati ya aina mbalimbali.
Imeenea hivyo kwenye matamshi ya kisharia, misamiati kama kuuza kumiliki au swala… wakati wa kuelezea kwake tunakuja na neno linalofanana na jinsi, na baadaye tunaleta vigezo ikiwa ni kipambanuzi au vipambanuzi vinavyo ainisha kusudio, imekuwa falsafa ya uelewa wa kitu ni jambo lililoenea na muhimu ili mwanadamu afahamu anachokusudia mwenzake, na ili ajengee maneno baada ya hapo yaliyo ainishwa au kuletewa uelewa wake mwanzoni mwa maelezo, kwa sababu kama hatutafanya hivyo huenda kutakuwa na tofauti ya wazi pamoja na ukweli tunakubaliana, na kugongana sisi kwa sisi na kuanzisha madhehebu katika tafiti, kwa sababu hiyo masuala ya kuleta uelewa au ufahamu wa kitu umekuwa ni jambo thabiti ndani ya vitabu vingi vya urithi, nayo vile vile katika utaratibu wa utafiti wa masomo ya kisasa, na kwa sababu hiyo kupangilia masuala haya wamezungumzia kwenye mambo matano jumla, na vile vile kwenye aina za uelewa.
Ikiwa tunaleta ufahamu au uelewa basi tunaweza kufikia kwenye taswira ya namna gani tutafika kwenye kuamini? Kitenda kazi hiki kinawezekana kupitia chenyewe kufikia kwenye kuamini na kutofautiana jina lake – kwa nafasi yake – kati ya wanachuoni wa elimu zingine tofauti, watu wa mantiki wameita kipimo, na katika sharia wameita dalili, na inaashiriwa kipimo ni upangiliaji wa mambo yanayofahamika ili kufikia jambo jipya lisilofahamika, kama tulivyotaja tunasema: “Swala lazima” inakuja dalili kwa kusema: Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: “Simamisha Swala” ni muundo wa amri, na amri ni jambo la lazima, hivyo Swala ni lazima, mfululizo uliopita wa jumla au sentensi ambazo kupitia zenyewe tumefikia kauli ya “Swala Lazima” ndio ambayo imeletewa ufumbuzi na mantiki katika kadhia za “Tangulizi”. Kwa sababu hiyo imepaswa kwetu kujifunza mantiki, na sehemu hii ya kipimo cha kimantiki ambacho kina aina maalumu mpaka kufahamu maneo ya kiurithi wamefanyia kazi vitendea kazi vyote hivi kwa wepesi pasi ya uzito kwa sababu kwao vimekuwa ni vyenye kukubalika.
Kuna mkusanyiko wa miundo ya kilugha na kimantiki inapaswa kufahamika na kueleweka kabla ya kuingi kwenye kitabu chochote katika vitabu vya urithi, wakati wa kufanyia mazoezi hayo mtu au msomaji anatengeneza umiliki kupitia umiliki huo anaoweza kufafanua maelezo na kuyafahamu kwa ufahamu wa kiwango cha juu zaidi ya ufahamu uliopo kwake katika kusoma kwake mara ya kwanza ya matini ya kiurithi.
Tukirejea kwenye matini yetu ambayo tunaichambua ili kuona umuhimu wa tuliyoyataja. “Kitabu cha mambo ya kuuza, imecheleweshwa na mlango wa Ibada kwa sababu ni katika matendo yaliyobora kabisa, na kwa sababu ya kulazimika nayo ni zaidi na kwa uchache wa watu wanaofanya mambo hayo”. Hapa tunaona aina ya muundo unaopaswa kuangaliwa katika vitabu vyao, ambapo inatajwa jumla kisha baada ya hapo inaishia na dalili zake, na huenda ikatajwa baada ya dalili “Sababu”, kwa maana ni kwa nini hii imekuwa ni dalili ya hilo.
Siku zote urithi katika akili yake ni kadhia kwa maana ya “Jumla fidishi” anasema: Amechelewesha mauzo na Ibada. Ni jumla inayoelezea kitu, nacho ni kuwa kuuza kumecheleweshwa na Ibada ndani ya vitabu vya wanachuoni, lakini dalili ipo wapi? Dalili – hapa – ni hisia, mana yake kana kwamba anasema: Angalieni vitabu vya Fiqih na kitabu hiki, lakini – pia – ipo wapi sababu? Inatajwa kwenye jumla mpya ambayo “Kwa sababu ni katika matendo bora” kisha ikaja sababu nyingine: “Kwa sababu kulazima katika hilo ni zaidi” na sababu ya tatu: “Na kwa uchache wa watendaji wake” sababu hizi tatu zimekusanya na kuwa sababu katika mpangilio wa wagawaji kuchelewesha somo la miamala (la kwaza lake uuzaji) na somo la Ibada, na inafahamika kuwa pindi alipotaka kutaja sababu amekuja na neno “kwa sababu” nayo neno hilo linazingatiwa kwenye lugha ya Kiarabu ni herufi ya upambanuzi wa sababu.
Anakamilisha: “tamko lake kwa asili ni chanzo kwa sababu hiyo ni imekuwa umoja” amefanya mtunzi kwa neno la umoja sababu ya kutaja mwandishi wa kwanza “kitabu cha uuzaji” na wala sio “kitabu cha mauzo” ambapo neno “uuzaji” – asili – ni chanzo, na chanzo hakiwi wingi isipokuwa pale kunapokuwa na tofauti na aina.
Anakamilisha: “Ikiwa chini yake kuna aina” maana yake hata ikiwa chini yake kuna aina, na hapa mtunzi anatueleza uelewa wake kuwa baadhi ya watunzi wa vitabu wanaleta uwingi wa “uuzaji” kwa kuwa kwao wanaona kuwa kila aina ya uuzaji umekuwa ni uuzaji wenyewe.
Kisha anakamilisha: “kisha imekuwa kwa kila chenye mabadilishano kama itakavyoelezwa, kisha ikatakiwa moja ya makubaliano mabaya ambayo huitwa yule mwenye kuleta muuzaji….” Madamu amekuja na neno lenye kueleweshwa hapa basi inakuwa ameingiza kwenye kadhia ya jinsi na kipambanuzi, na akataka kuhamishia kwenye akili uelewa maalumu kuhusu uuzaji” na kufahamisha kuwa “Ni umiliki kwa mbadalishano kwa njia maalumu” umiliki – hapa – ni jinsi, kana kwambo mmoja wao amemuuliza mtunzi: Ni aina gani katika aina za umiliki? Ambapo sababu za umiliki ni nyingi, mfano: Utoaji wa zawadi mirathi umiliki halali mfano wa uvuaji samaki, anasema mtunzi: “Kwa mabadilishano kwa sura maalumu” ikawa hiki alichokitaja ni “Kipambanuzi” kwa maana ya neno “Umilikishwaji” au “Umiliki” ni jinsi, na neno “Kwa mabadilishano kwa sura maalumu” ni kipambanuzi.
Na kukubaliana na kununua ambako ni sehemu nyingine na ambayo inaitwa kwa mwenye kuja mnunuzi, na kuelezewa kuwa ni kumilikishwa kwa mabadilishano pia, inafaa kuita jina la muuzaji mnunuzi na kinyume chake, na kielezo cha kwa kumiliki au kumilikishwa kwa kuangalia maana ya kisharia kama itakavyokuja, ikiwa itakusudiwa maneno yenye pande mbili kwa maana sababu iliyopo kwa pande mbili ambazo zina uhalali na kuharibika, husemwa – kilugha – mkabala wa kitu kwa kitu kwa njia ya kuuziana, inaingia ndani yake kisichofaa kukimiliki kama vile kitu binafsi, na kisichokuwa na muundo kama vile kitu cha kupewa, na kutolewa kwenye mabadilishano mfano amani. Na hufahamika – kisharia – kuwa ni makubaliano.
Hapa limekuwa neno “makubaliano” ni jinsi, kwani makubaliano ni ya aina nyingi kiwemo makubaliano ya biashara ya Salam, makubaliano ya ndoa uwakala, aina ipi hapo ni katika aina za makubaliano? Anasema mtunzi “makubaliano ya kubadilishana mali” kauli yake “mabadilishano ya kimali” ni kigezo katika vigezo. Na anakamilisha: “inaleta maana ya umiliki wa kitu au manufaa” na hiki ni kigezo cha pili, anakamilisha, “sio kwa sura ya ukaribu” na kuendelea kila kigezo katika vigezo hivi kimetolewa kitu sehemu ya uelewa wake.
Nguzo zake ni tatu,” mwenye kuingia mkataba chenye kuingiwa mkataba na sura ya mkataba” na “nguzo zake ni tatu” zenyewe kwa ukweli ni sita, na makubaliano au mkataba – katika uelewa wake – jinsi, kwa maana ulivyo ni kuingiza kwenye akili ya mwanadamu ukweli wa jinsi maalumu, nayo ni makubaliano. Anakamilisha: Lakini ikiwa kati yake na kipambanuzi chake kuna ujumla na kutolewa kila kimoja kilichoingizwa kwenye jumla nyingine” kwa mfano neno “mnyama” ni jumla wa wanyama linakusanya ndani yake mwanadamu na simba lenyewe ni jinsi na kazi yake ni kuwa neno jumla, ama lau litaletwa neno “mwenye kutamka” hilo – kama linavyoonekana na baadhi – linakusanya mwanadamu na malalika, malaika ni wenye kusifika ndani ya Qur`ani kuwa ni wanazungumza na Mwenyezi Mungu na kupewa kazi ya kupeleka wahyi au ufunuo, ikiwa hatuwezi kuthibitisha kwao akili isipokuwa kinachoweza kusema ni kuwa wao wanaakili kwa hali zote, huenda ikiwa si kwa kuwa na ubongo lakini wanaakili na kufahamu na wala hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa yale aliyowaamrisha. Zote hizo ni sifa zinazosisitiza kuwa hawa ni viumbe vyenye kutamka waliopewa amri, hivyo “mwenye kutamka” huenda akawa ni mwanadamu au si mwanadamu, lakini pindi tunapoweka duara mbili zilizo sawa: Unyama upande mmoja na utamkaji upande mwingine basi huenda itatokea kwetu eneo la wazi la pamoja kati ya maduara mawili, eneo hili la wazi ni “Mwanadamu”, bali haliwakilishi isipokuwa ni “Mwanadamu”.
Hivi ndivyo walivyosema wanachuoni wa mantiki: Pindi jinsi inapokuwa kwa ujumla na kipambanuzi pia kwa sura jumla, pindi tunapoiweka jinsi pamoja na kipambanuzi basi ujumla wa kila upande una vigezo kwa upande mwengine. Unyama unafidisha kuwa ni wenye kutamka, na utamkaji unafidisha kuwa unyama, kadhia ni ngumu mno kwa wana mantiki, wameifahamu baada ya mijadala migumu nayo ni kadhia inayozalishwa na akili ya Kiislamu.
Anasema: “Kwa sababu hiyo imetolewa kwenye makubaliano upewaji, kwenye mabadilishano imetolewa zawadi, kwenye mali ndoa, na kunufaika na umiliki wa kitu ukodishaji, kinyume na sura ya kujenga ukaribu mkopo, na kusudio la manufaa ya kuuza ni mafano wa haki ya kupita, na kukitoa kitu kimoja kwa vigezo viwili si jambo la aibu.
Uelewa huu ni katika uelewa bora kwa sababu ni mabadilishano ya mali kwa mali kwa sura maalumu isiyojificha….kisha uuzaji umekusanywa kwenye pande tano: “Upande wa kwanza ni katika kufaa kwake na kutofaa kwake, upande wa pili ni kufaa kwake na ulazima wake, upande wa tatu ni katika hukumu yake ya kabla ya kukabidhi na baada, upande wa nne ni katika matamshi, upande wa tatu ni katika muungano na mashirikiano……”.
Hapa ndio mwisho wa jumla fidishi katika matini na kuanza kwa jumla mpya sehemu nyingine kwa jumla fidishi nyingine. Amesema: “Mapato yaliyobora zaidi ni uzalishaji wa kiwanda kisha kilimo kisha biashara kwa kauli yenye nguvu”.
Angalia muundo wa kilugha, kifafanuzi “Kauli yenye nguvu” inakuwa wazi kwa kauli hiyo kuwa kwenye kadhia kuna kitu kinapewa nafasi kubwa, kwa maana kuna kauli zaidi ya moja, na kuna tofauti kati ya hizo katika masuala, hivyo amesema: “Kauli yenye nguvu”. Baadhi yao wameipa nafasi zaidi biashara mapato bora zaidi na kuizingatia ndio yenye mapato bora, na baadhi ya wengine wameipa nafasi uzalishaji wa kiwanda na kutoa dalili kuwa Mtume S.A.W alishika upanga na akasema: “Mimi nimependa sisi kutengeneza huu” na mfano wa hivyo kumekuwa na tofauti na kauli, lakini kauli yenye uzito mkubwa – kwenye kundi hili la wanachuoni ambao mtunzi analifuata – ni uzalishaji wa kiwandani kisha kilimo kisha biashara, na kauli yeyote ile hakuna kinachotupa faida hapa kuwa kielezi “Yenye nguvu” hapa maana ina maanisha kuwa kuna tofauti kati ya wanachuoni.
Na kauli yake: “Uuzaji ni makubaliano ya kubadilishana mali yanayopelekea umiliki wa kitu wa muda mrefu sio kwa njia ya ukaribu” inakuwaje ikiwa tutasema ni makubaliano ya kifedha yanayopelekea umiliki wa kitu maalumu, bila ya kutaja neno mabadilishano? Hii inakubalika pia kwenye kujitolea zawadi na zawadi huwa hairudishwi, hivyo basi haiwezekani kuingia kwenye maana ya “Uuzaji” na ni lazima kuleta uelewa huu kwa kuweka kigezo cha “Mabadilishano”.
Lau tutasema kuwa ni makubaliano ya mbadala yanayopelekea umiliki wa kitu, hapo tunakuwa hatuwezi kuliingiza kwenye makubaliano ya ndoa, kwani mume hammiliki mke wake kwa makubaliano ya ndoa, mahari hupewa mwanamke ikiwa ni kumkirimu, na kwa hili ni lazima tutofautishe kati ya ndoa na uuzaji kwa neno “Kifedha” na neno “Miliki”. Pindi anaposema: Makubaliano ya badala kwa kigezo cha “Umiliki wa kitu” inatolewa hapo ukodishaji, kwa sababu kwenye kukodi ni kumiliki manufaa lakini si kumiliki kitu chenyewe au sehemu yenyewe.
Miongoni mwa kauli hapa ni kuwa Fiqih ya Kiislamu inatenganisha kati ya kitu cha kukodiwa na manufaa. Miliki kamili maana yake ni kumiliki kitu na manufaa, miliki pungufu ni kumiliki kimoja kati ya viwili hivyo, kumiliki kitu hutolewa kwenye makubaliano kukodi, “Bila ya sura ya kuleta ukaribu” hutolewa mkopo kwenye makubaliano haya, kwani mkopo ni makubaliano ambapo upande mmoja hutoa kiwango cha mali na kumpa upande mwingine mkabala na kurudisha kiwango kama hicho cha mali.
“kusudio la manufaa ya uuzaji mfano wa haki ya kupita”, kama vile kuwepo sehemu ya ardhi iliyogawanywa sehemu mbili: Sehemu imeungana barabarani au kwenye mtaa mkuu na sehemu nyingine ipo kwa ndani haina sehemu ya kupitia kuja mtaa mkuu, mwenye eneo la ndani anataka kuingia eneo lake kutokea barabarani, hapa anapaswa kumuomba mwenye eneo la mbele au barabarani kumuachia sehemu au uchochoro wa kupita na kuingia kwenye miliki yake kupitia njia hiyo au uchochoro huo, na hapa ni katika haki ya mwenye eneo la kwanza kutaka kwa huyu anayetaka sehemu ya kupitia thamani ya sehemu hiyo, hapa mnunuzi atakuwa na haki ya kudumu ya kupita kwenye eneo hili kwa thamani aliyoilipia, lakini hamiliki sehemu yenyewe ya kupita, hivyo haki ya kinjia cha kupita huuzwa na kununuliwa, nayo ni kuuza na wala sio kukodisha na pia ni kwa muda mrefu, na hupewa haki huyu mwenye haki na aliye nyuma yake ni sawa sawa huyu aliye nyuma yake ni mrithi au mnunuzi wa sehemu ya ndani, masuala hapa si ukodishaji au kusamehe lakini maswala ni kuuza na kununua.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Chanzo Kitabu: Njia ya kufahamu urithi, cha Fadhilatuh Mufti wa Misri.
Dr. Ally Jumaa.

 

Share this:

Related Fatwas