Kuchelewesha kwa Mmoja wa Warithi k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuchelewesha kwa Mmoja wa Warithi katika kugawa Mirathi

Question

Ni ipi hukumu ya Kisheria katika kuchelewesha na kuvuta muda kunakosababishwa na baadhi ya warithi katika kuwawezesha waliobakia kupata mafungu yao ya mirathi katika hali ambayo ucheleweshaji huo utakuwa kwa ajili ya masilahi ya anayevuta muda bila ya ridhaa ya warithi wengine? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wanachuoni wamekubaliana ujumla ya kwamba Mali baada ya mtu kufariki, umiliki wake unahamia kwa warithi wake; kwani umiliki huo huwa unakatika kwa mmliki kwa kufa kwake. Basi katika Hadithi ya Anas kuwa Mtume S.A.W. amesema: "Vitu vitatu humfuata maiti baada ya kufa kwake na viwili hurejea naye hubakia na kimoja tu: Hufuatwa na watu wake, mali yake na matendo yake. Mali yake hurejea pamoja na watu wake na hubakia na matendo yake tu". [Bukhari na Muslim]
Na Urithi baada ya kufa mwenye kurithiwa, ni haki ya warithi wote kama ijulikanayo – wake kwa waume, wadogo kwa wakubwa. Kila mrithi anastahiki kurithi fungu lake maalumu la mali iliyoachwa na mrithiwa baada ya kutoa matumizi ya maandalizi ya maiti na mazishi yake, na kulipa madeni yake yote, na kutekeleza Wasia wake na kulipa kafara zake pamoja na Nadhiri alizoziweka, na mfano wa hayo.
Na haijuzu kwa yeyote katika warithi kuwanyima wengine mafungu yao yaliyokadiriwa kisheria, vilevile haijuzu kumpendelea mmoja wao kufanya atakavyo katika Mali ya urithi kinyume na warithi wengine au bila ya idhini yao na hasa wakiwa ni watu wazima waliobaleghe au kwa idhini ya Kadhi au Muusiwa wao wa kisheria kama haiwatakuwa hivyo. Basi kuzuia au kuchelewesha mgao wa mirathi bila ya udhuru wowote wa Kisheria – kama vile kufanya kazi ya maandalizi au kulipa madeni na haki zingine – au idhini, ni Haramu Kisheria. Na hayo kwa sababu zifuatazo:
Ya Kwanza: Mtume S.A.W. amesema; "Mtu yeyote atakaezuia mirathi iliyofaradhishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ataizuia mirathi yake ya Pepo". [Imepokelewa na Al Baihaqiy katika kitabu cha: As Sho'ab, Na Saiyed Bin Manswor katika Sunna zake, Na imepokelewa na Al Ajluniy katika kitabu cha Kashf Al Khafa kwa neno: "Mtu yeyote atakaemzuia mrithi kurithi Mali yake, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamharamishia Pepo". Halafu akasema: "An Najm akasema: sikujua Hadithi hiyo kwa lafudhi hiyo"; lakini kwenye Ibn Majah kutoka kwa Anas: "Mtu yeyote atakaezuia mirathi ya mwenye mirathi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ataizuia mirathi yake ya Pepo". 310/2, Ch. ya Maktabat Al Qudsiy]
Na Hadithi hiyo ni maandiko ya kwamba kumzuia yeyote katika warithi kurithi ni haramu; Kwani onyo kali juu ya kitu ni dalili ya uharamu wake, na Zuio lililopo katika Hadithi ni la jumla na ndani yake kunaingia kuzuia Urithi kwa hali zote, au kuchelewesha wakati wake wa kutolewa bila ya udhuru wowote au idhini.
Ya Pili: Hakika kuzuia na kuchelewesha bila ya udhuru wowote wa kisheria au idhini ya kukiuka haki za watu na, kuvunja haki yake, na kufanya hivyo ni katika dhuluma, na dhuluma ni katika madhambi makubwa yaliyoahidiwa adhabu kali. Basi katika sahihi kutoka kwa Jabir kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Iogopeni dhuluma. Kwani hakika dhuluma ni katika kiza cha Siku ya Kiama." [Imepokelewa na Muslim]. Na Mtume S.A.W. amesema: "Hakika Mwenyezi anampa muda dhalimu mpaka atakapomchukia atakuwa hawezi tena kukwepa". [Bukhari na Muslim]
Na Mtume S.A.W. amesema: "Mtu yeyote atakaye kuwa na chochote alichomdhulumu nduguye basi na aachanane nacho kwani hakika mambo yalivyo hana chochote Siku ya Kiama kama dinari au dirhamu kabla ya kunyang’anywa na kupewa nduguye katika mema yake, na kama hatakuwa na mema basi maovu ya nduguye yatachukuliwa na atatupiwa yeye". [Imepokelewa na Al Bukhariy]
Na Mtume S.A.W. akasema: "Mtu yeyote atakaye dhulumu kipande kidogo cha ardhi basi atazungukwa na ardhi saba" [Bukhari na Muslim]. Na Mtume S.A.W. amesema: "Haki zitapelekwa kwa wenyewe mpaka patakapolipizwa kisasa cha kondoo asiye na mapembe kwa kondoo mwenye mapembe aliyempiga pembe mwenzake". [Imepokelewa na Muslim]
Vilevile zuio hilo au ucheleweshaji huo ndani yake kuna kula mali ya watu kwa dhuluma. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.} [AN NISAA 29].
Na Mtume S.A.W. amesema: " Hakika mwenye kufilisika katika umma Wangu atakuja Siku ya Kiama na Swala zake, na Saumu zake na Zaka zake, na atakuja akiwa amemtusi huyu amemtuhumu yule na amekula mali ya huyu na amemuua yule na amempiga huyu, na huyu atapewa mema yake na huyu mema yake, na ikiwa mema yake yatamalizika kabla ya kumaliza deni alilonalo, basi madhambi yao yatachukuliwa na atatupiwa yeye kisha atatupiwa Motoni". [Imepokelewa na Muslim]
Ya Tatu: Kauli ya Mtume S.A.W.: "Kila mmoja ana haki ya Mali yake kutoka kwa baba yake au mama yake na watu wote" [Imepokelewa na Al Baihaqiy na Ad Darqitwniy]. Na Hadithi hiyo ni Msingi wa kwamba Mwanadamu ana haki ya kufanya atakavyo katika Mali yake. Vilevile Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kubainisha mafungu ya warithi katika Suratul Nisaa, ameanza kwa lamu ya kumiliki. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi fungu lenu ni robo ya walicho acha}, na akasema: {Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha}, na akasema: {Basi sehemu yao ni thumni ya mlicho kiacha}, na akasema: {Basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi}, na akasema: {Basi watapata thuluthi mbili za alicho kiacha maiti}, na kasema:{Basi fungu lake ni nusu}.
Jambo linalothibitisha kwamba kila mrithi ni mmiliki wa fungu lake katika Mali iliyoachwa hawezi kushirikiana na yeyote na haki ya kutumia atakavyo bila ya kumshirikisha yeyote, na asili yake ni kwamba haijuzu kwa yeyote kuitumia haki au miliki ya mtu mwingine isipokuwa kwa idhini yake ya kisheria au kwa idhini ya mmiliki wa mali hiyo, na kuzuia fungu la mrithi yeyote au kuchelewesha mgao wake bila ya idhini ya warithi wengine, basi kufanya hivyo ni kutoa maamuzi katika mali ya mwingine bila ya idhini na hairuhusiwi kufanya hivyo.
Ya Nne: Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu}, [AALI IMRAAN 133].
At Twaher Bin Ashuur amesema katika Tafsiri yake: "Na uharakishaji wa makadirio yote kinatokana na mfungamano wake na sababu za kusamehewa na kuingia Peponi, na kufungamanisha kwake na msamaha na Pepo ni mfungamano wa vitu na utashi wa hali zake panapotokea ukosefu wa faida kufungamanisha na dhati yake", [Kitabu cha: At Tahrer Wat Tanweer 89/4, Ch. ya Ad Dar At Tunisiyah].
Katika Aya kuna Amri ya kuharakia sababu za kusamehewa na kuingia Peponi, na katika sababu kuu za kuingia peponi na kupata radhi za Mwenyezi Mungu ni kuzitekeleza haki bila kikomo, ziwe haki hizo ni za Mwenyezi Mungu, za watu au za mtu binafsi.
Katika Utekelezaji wa Haki za watu, unaingia pia utekelezaji wa Walii au mbeba jukumu la Mali iliyoachwa na marehemu, haki ya warithi waliobakia na kuharakisha katika jambo hili, na kutoila mali hiyo au kuichelewesha wakati wake wa kutolewa bila ya udhuru wa kisheria au idhini.
Na Kutokana na maelezo yaliyotajwa: kuzuia au kuchelewesha mmoja wa warithi, au kucheleweshwa warithi waliobakia kutokana na mafungu yao bila ya udhuru wowote au idhini ya warithi ni haramu kisheria, na muhusika wake anakuwa amefanya dhambi kubwa na amekula mali ya watu kwa dhuluma na analazimika kufanya toba na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale aliyoyafanya pamoja na kuirejesha kwa wenyewe Mali aliyoichukua kwa kuwapa warithi mgao wao na kutowawekea kizuizi chochote baina yao na kile wanachokimiliki kama mirathi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Ofisi ya Kutoa Fatwa

 

Share this:

Related Fatwas