Haki za Binadamu katika Mtazamo wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu katika Mtazamo wa Kiislamu.

Question

Je, ni ipi hadhi ya Haki za Binadamu katika Mtazamo wa Kiislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizo huo:
Haki za Binadamu ni miongoni mwa maudhui zinazojulikana katika ndimi za watu na zimekuwa maudhui ya mazungumzo yao, na watu wengi miongoni mwao wanaulizia msimamo wa Uislamu wa Haki hizo. Na Uislamu unauangalia Ulimwengu kwa kuzingatia kama kiumbe cha Muumba aliye Mtukufu kwa sifa zake aliyetukuka katika dhati yake, na kwamba Ulimwengu huo ni vyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwamba Ulimwengu wa vitu, Mimea, Wanyama, Mwanadamu, vyote hivyo vimeumbwa kwa kuwa kwake sehemu ya Ulimwengu, kisha ataona sura iliyo wazi na iliyoainishwa ya jinsi ya Mwanadamu anavyouchukulia huu Ulimwengu, na haki za Ulimwengu huo juu yake, na Wajibu wake wa jinsi ya kuutendea Ulimwengu huo.
Kwa hiyo Haki za Binadamu ni sehemu ya mpangilio wa haki za Ulimwengu huo, na kwa mtazamo huu, na utangulizi huu unaangazia Suala la Haki za Binadamu katika Uislamu kupitia Haki za Ulimwengu mpaka iwe wazi kwetu nafasi ya hizo Haki za Binadamu kwa mpangilio huu na kiwango cha kina chake na kuingia kwake katika mfumo wa mtazamo wa Mwislamu kiujumla, na Akida yake Samehevu ambayo daima huhangaika kuufikia Ukweli na Haki na kiasi cha umfungamano wa Haki na Ukweli katika mtazamo huo wa kiujumla wa Hukumu za Kisheria, na kwa kumpa jukumu la hukumu Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetukuka.
- Maana ya Haki za Binadamu katika Lugha na Istilahi:
Kirai cha kiunganishi hatuwezi kuijua maana yake isipokuwa kwa kujua maana ya sehemu zake zote. Basi neno la (Huquq) katika kiarabu ni wingi wa (haqi) haki, nalo linamaanisha katika maana yake ya kisarufi, na maana ya kikamusi ni jambo thabiti, na neno la (Insaan) Binadamu; kutokana na kidahizo cha (Nun, Siin, Yaa), na katika kauli ya mshairi:
Binadamu hakuitwa (Insaan) isipokuwa kwa kusahau kwake, na mtu wa kwanza aliyesahau ni mtu wa kwanza katika wanadamu.
Mshairi anaashiria hapa kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; {Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukuona kwake azma kubwa} [TWAHA 115].
Na Uunganishaji unakuja katika Kiarabu kwa maana ya herufi ya (Laam), na herufi hiyo inakuja kwa kumiliki na kuhusika; maana ya hayo kwamba kirai cha kiunganishi hicho kinamaanisha mambo thabiti ambayo yanahusika mwanadamu basi hayabadiliki, na ubadliko unatokea kwa kawaida katika upande mmoja miongoni mwa pande nne: wakati, mahali, watu na hali. Basi kuna mila na mapokeo yanayobadilika kutokana na mabadiliko ya zama, na kupitia zama na dahari. Na yako mambo ya vyakula, vinywaji, madhehebu na fikira ambavyo vyote hivyo vinabadilika kutoka mahali hadi mahali pengine kutokana na tabia na matokeo yake. Na yako mambo mengine yanayoungana na binadamu, yanabadilika kutokana na mabadiliko ya watu, na yanayowamalizia wengine wao kama vile rangi, jinsi, sifa za kimwili, kutoka unguvu, unyonge, urefu, ufupi, ume, uke. Na labda sifa zimebadilika; na pia mambo yanayohusiana na mwanadamu, yanaungana na hali zake kama vile; afya, ugonjwa, kuendelea, kuchelewa, kukufuru, na kuamini, lakini yako mambo thabiti hayabadiliki na hayageuki, mambo hayo ni ya kweli yanayomuunda mwanadamu na hayo ni mambo thabiti ambayo yanamhusu mwanadamu, mambo hayo ni Haki za Binadamu.
Dhana hiyo ni dhana ambayo inaungana na akili ya mwarabu alipokishikilia kishazi hicho. Je, ni nini maana yake ya kiistilahi?
Katika mada ya hamsini na tano (55) aya (G) kutoka katika Katiba ya Umaoja wa Mataifa iko ibara ambayo imetaja kuwa:
Paenee Ulimwenguni jinsi ya kuziheshimu Haki za Binadamu na kila aina ya uhuru wa msingi wa Kisiasa bila ya ubaguzi wowote wa kijinsia, kilugha, au Kidini, wala kuwatofautisha wanaume na wanawake, na kuziangalia haki hizo kwa yakini, na Tamko hilo ambacho ni (Haki za Binadamu na kila aina za Uhuru wake wa kimsingi) kiwe ni anwani ya juhudi zake zinazotokana na Maazimio na nyaraka mbalimbali za Umoja wa Mataifa na mikataba yake mbalimbali.
Na mnamo tarehe mosi ya mwezi wa Desemba mwaka wa elfu moja mia tisa, arobaini na nane (1/12/1948) lilitolewa Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo liliambatana na orodha ya haki mbali mbali za kisiasa, kiraia na kijamii kwa binadamu.
Na Baraza Kuu la Umoja ya Mataifa limekuwa likilikariri Azimio hilo isipokuwa nchi nne ambazo ni: Urusi, Yugoslafia na Afrika Kusini, Na Sudia Arabia imekataa mada zinazopingana na sheria ya Kiislamu. Azimio hilo limejumuisha mada thelathini zilizokusanya nyanja za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na utamaduni.
Na katika tarehe ya kumi na sita mwezi wa Desemba, mwaka wa elfu moja mia tisa, sitini na sita (16/12/1966), Jumia Kuu ya Umoja wa Mataifa iliafikiana na nyaraka tatu za kimataifa:.
Ya kwanza: Mkataba wa Haki za Kiuchumu, Haki za Kijamii na Haki za Kiutamaduni. Ya Pili: Mkataba wa Haki za Kiraia na Haki za Kisiasa. Ya Tatu: Mpango wa kihiari umeambatana na Mkataba wa pili umezihusikia madawa (mashitaki) ya watu dhidi ya kuziangamiza Haki za Binadamu. Na nyaraka hizo zinaitwa kwa kuongezea Tangazo la Kimataifa kwa Haki za Binadamu istiliahi ya: "Waraka ya Kimataifa kwa Haki za Binadamu". [Rejea: Kitabu cha: Kanuni (Sheria) ya Kimataifa kwa Haki za Kibinadamu kwa Dkt. Jaafar Abusalaamu Uk. 40].
Na kutoka upande mwengine, kwamba ulimwengu wa kimagharibi unajishughulikia tango kipindi kisicho kifupi, kwa suala la Haki za Binadamu, na tango ya Tangazo la Kimataifa la Haki za Binadamu linalotolewa kutoka Umoja wa Mataifa katika mwaka wa elfu moja mia tisa, arobaini na nane (1948) na mpaka leo, na upo ushughulikio wa kimataifa kwa suala hilo, na mikataba na nyaraka nyingi zimetolewa kwa suala hilo, licha ya makumi ya maelfu ya masomo na tafiti kwa lugha tofauti nyingi za kimataifa, na mashirika mengi na jumia nyingi zisizo za kisirikali na kisirikali zimeanzishwa kwa ulenzi wa Haki za Binadamu na kuuhifadhia ukarama wa mwanadamu.
Na haki hizo hazitokii mambo yafuatayo:
Haki ya Kujiamua, haki ya kazi na kuchuma riziki ya maisha, haki kuunda vyama, haki ya kudhani ya kijamii, haki ya ulenzi wa familia, haki ya afya ya kimwili nay a kiakili, haki ya kitaaluma, kiutamduni na ulenzi, haki ya kuboresha kiwango cha maisha, haki ya uhuru ya kiujumla; (Uhuru wa kuondoka, wa kazi, wa fikiri, wa rai, wa itikadi, wa ushirikiano wa kisiasa, wa ndoa na uhuru wa usawa).
Na kwa hiyo, mambo yameendelea katika Hahi za Binadamu, na uhuru wake wa kiujumla, yanafupishwa katika kwamba yapo mafungu makuu mawili ya haki hizo uhuru; nayo ni ya kimaisha na ya kisiasa.
Sehemu ya Kwanza: Haki zinzoambatana na Maisha:
Inaonekana na kuyahifadhia maisha yenyewe halafu juu ya maisha mazuri ambayo yanadhamini vyakula, nguo, madawa, utaaluma na ndoa na nyinginezo. Na kwamba mwanadamu awe mwenye uhuru kuondoka kwake, kazi yake, itikadi yake, maoni yake, mawazo wake na nyinginezo, haki zake za kisiasa zinaambatana na kutenda kipindi chake kwa uongozi maisha na kuyaedeshea.
Na unaweza ukaiona sehemu ya kwanza ambayo tunaweza tukaiita ya Kimaisha ni upande wa kiuchumi na kijamii na kitamaduni na kidini na ambao tunapangiwa na Malengo Makuu matano ambayo yalijaaliwa na Wanachuoni wa Usuli; tango Al Ghazaliy katika kitabu cha: [Al Mustswfa], kisha As Shatwibiy katika kitabu cha: [Al Mwafaqaat] kama makusudi ya wenye jukumu na hayo ni: Kuhifadhi kwa Nafsi, Akili, Dini, Ukarama ya mwanadamu na Mali (Miliki na zilizoandaa kwa kumiliki). Na waislamu walizijaalia katika viwango vitatu: Yenye dharua, Yenye haja na ya kukamilishia, na wanazigawa hukumu za Kisheria juu yake kwa viwango viwili katika kila sehemu; ni ya kiasili na ya kitawi.
Na hapa inafaa tuangalie ya kwamba Suala hili lina umuhimu mkubwa sana nalo ni kuwa Haki za Binadamu katika Sheria ya Kiislamu zimegeuka na kuwa katika mambo ya wajibu ambayo lazima yapatikane na kama hayajapatikana basi huwa dhambi kwa mwenye kupuuzia. Mwanadamu haitaji tena kuomba haki zake na kusubiri wengine wamuamulie bali asili ya kuumbwa kwake na kupewa majukumu kunafanyika kwa kuzipata haki zake na ni wajibu Wake.
Na kuanzia hapo Watu wengi wamechanganya mpangilio wa Ustaarabu wa Waislamu kwamba ni Ustaarabu wa mambo ya wajibu yaliyopelekea udikteta na mabavu na kwamba Ustaarabu wa Magharibi ni wa Haki za Binadamu, na jambo hili sio hivyo bali ustaarabu wa kiislamu – ambao uliifanya Dini kuwa ndio msingi wake na mwanzo wake – ndio Ustaarabu wa haki za Binadamu zilizofikiwa Kiwanga cha kuwa miongoni mwa mambo ya Wajibu.
Sehemu ya Pili: Haki za Kisiasa:
Kwani zipo kama sehemu ya mpangilio wa Jamii, na njia za upangiliaji huo na marejeo yake katika Uislamu ni katika Fiqhi – kwa maana ya kanuni inayoyaendesha Maisha ya Binadamu – na ndani yake kuna ufafanuzi zaidi wa kile kinachoifanya picha yake iwe Kamili na yenye kupangika na isiyo na mgongano ndani yake au ukinzani. Na kuanzia hapo, hakika haki za kisiasa na aina mbalimbali za uhuru wa kimsingi unaoambatana nazo hauna aina yoyote ya ugomvi juu yake ambapo Mfumo Mkuu wa kuheshimu haki za Binadamu unapatikana kupitia Historia kwa wenye Hekima.
Haki za Binadamu katika Uislamu:
Waislamu wameshughulikia haki hizo, na miongoni mwa yaliyoyasemea na yaliyoyatekelezea katika ustaarabu wao (mwanadamu kabla ya kujenga) na (ulezi wa mwenye kusujudu kabla ya kujenga kwa misikiti), kwa hiyo wameshughulikia kwamba ulenzi unaelekea mwanadamu na kwamba kuremba majengo yatakuwa katika cheo cha pili baada ya kutosha kwa mwnadamu na kutenda kwa mambo wake yote, na kama alivyosema Mtume S.A.W.: "Nimejaaliwa ardhi yote kuwa ni Msikiti na Tahiri". [Hadithi hiyo wanavyuoni wanaiafikiana nayo; na imetolewa na Al Bukhariy katika kitabu cha Taiamum, katika mlango wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na msipate maji, basiukusudieni mchanga safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu} AN NISAA 43, hadithi ya mia tatu na thelathini ya tano (335), na katika kitabu cha Sala, mlango wa kauli ya Mtume S.A.W. "Nimejaaliwa ardhi yote kuwa ni Msikiti na Tahiri", hadithi ya 438. Na Muslim katika kitabu cha Misikiti na mahali pa Sala, hadithi za (521, na 523) kutoka hadithi ya Jader Bin Abdullahi R.A. wote wawili].
Inawezekana kabisa kwa Mwislamu na amekalifishwa kusali swala tano kwa siku nzima aswali pale swala inapomkutia katika sehemu yoyote iwayo duniani, bali hakika mawasiliano ya Binadamu na ardhi hii anayoitumia kumsujudia Mwenyezi Mungu Mtukufu haikuishia katika hilo tu bali imeenda mpaka katika kuutumia mchanga wake katika kutayamamu ambako njia mbadala ya maji pale Mtu anapotakiwa, kwani Maji hutumika kwa kuogea na kutawadhia na tunapoyakosa tunatumia Ardhi badala yake, kama vile kunaashiria Mwanzo na Mwisho.
Ama kwa upande wa chanzo ni kauli ya Mwanezi Mungu Mtukufu: {Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu naardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?} [AL ANBIYAA 30], na ya mwisho katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; {Kutokana nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo tunakurudisheni, na kutoka humo tutakutoeni mara nyengine} [TWAHA 55].
Na waislamu wamekuwa wakimjali mwanadamu na wakayafanya Makusudio Makuu ya Sheria ambayo yanamsemesha yeye na yeye na yanawasemesha Watu wote na yanakwea Muda na Zama katika hali zote ni matano: Kuilinda nafsi mpaka iweze kusimama ikiwa hai inayoweza kuambiwa, Kuilinda Akili na kutoishambulia kwa kuidhibiti au kuitenza nguvu bali kuna kuilinda katiba Msingi wake na Kuilinda katika mfumo wake wa kufikiri na kuilinda katika Uhuru na Ubunifu wake.
Hata katika masuala ya Imaani Mwenyezi Mungu Mtukufu aksema: {Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongo fuumekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua} [AL BAQARAH 256]. {Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu} [AL KAFERUUN 6]. {Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi.Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama hema. Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka.Yatayo wababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno!} [AL KAHF 29].
Kwa kuongezea kumhifadhia mwanadamu kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpatekufikiri} [AL BAQARAH 219].
Na kutoka kwa Umu Salamah R.A. Mtume wa Mwenyezi Mungu amekemea na kukataza kila Kilevi na Chenyekuudhoofisha mwili Mtume S.A.W. akasema: "Ni marufuku kwa taifa langu kila Kilevi na Chenyekuudhoofisha mwili". [Hadithi hii imetolewa na Ahmad katika kitabu cha: Musnad Ahmad 309/6, Hadithi Namba (26676), na Abu Dawud katika kitabu cha: (vinywaji), "Mlango wa kuzuia kilevi" hadithi ya (3686), na Atwbaraniy katika kitabu cha: (Al Kabiir 337/23), na Al Baihaqiy katika kitabu cha: Asunan Al Kubra 296/8, kutoka katika hadithi ya Umu Salamah R.A.]
Na Kuilinda Dini kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda Wachamungu, Wavumilivu, Wenye kumtegemea yeye, na Watendao Mema, na wala hawapendi Waharibifu wala wenyekujikweza na Wahaini na anapenda Katiba ya Kistaarabu ya Kibinadamu. Na Kulinda Utukufu wa Binadamu ambao unaitwa katika Urithi wetu wa Uislamu kama ni Heshima. Na hakika Heshima ya Mtu imezungukwa na Uzio mkubwa wenye kila aina ya hakikisho linalozuia kuwekwa kizuizini kwa nguvu na kukamatwa hovyo hovyo na kumuadhibu mtuhumiwa. Na ni Haramu Kutukana na kumsingizia mtu jambo lolote na Tuhuma zisizokuwa na dalili inayokubalika. Na Ubaguzi umeharamishwa katika kila umbo wake, na nyinginezo nyingi ili kuhifadhia Haki za Binadamu katika ukarama wake.
Na waislamu wameshughlikia kuhifadhi mali miliki ya mwanadamu, na kuharamishia kuzishambulia na kuziangamizia haki zake na inajaalia mambo hayo ni miongoni mwa madhambi makubwa ambayo yanaharibikia ukusanyiko wa kibinadamu. Na kutoka hayo yote Ustaarabu wa Kiislamu umejengwa kutegemea halmashauri wa makadhi.
1- Na Haki za Binadamu zilizojadiliwa katika Umoja wa Mataifa ni – ambazo tunatumaini kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu zisiwe zimejadiliwa kwa Uzito kisha wakazizuia kwa Watu – Waislamu wa zama hizi walizikubali na wakakubali pia kila aina ya wito wa kufanya mazuri na juu ya kila Makubaliano yaliyofanyika kwa Upevu, na walikubali pia kuufuta utumwa na wakaona kwamba ndani yake kuna hali ya kuafikiana ambayo Watu wote wanaweza kukubaliana na kuishi kwa Amani.
Lakini bila ya Uasisi wa kinadharia au Kifalsafa na bila ya mfumo ulio na maumbile ya wazi tumewaona wanaodai kufufua Haki za Binadamu ambazo Watu hawajaafikiana baina yao, na Haki zinazozingatiwa za kulazimisha ni Haki zinazoafikiana na watu. Ama katika yale ambayo Watu hawajaafikiana hayawezi kuwa na zingatio lolote ndani yake, na hii bado inaonekana kuwakilisha Utamaduni unaotawala kwa wale waliogundua au kuafikiana nao. Na hoja hii lazima iwepo katika wakati huu ambao kuna Sauti nyingi zinazopazwa na makelele yanayopigwa ambavyo hivi sasa vimekuwa ndio alama ya wengi katika Watu baada ya kuchelewa kwa Kufikiria Uchangamfu, kama anavyosema mwenye fikiri na mwanafalsafa wa Kifaransa (Reneh Juno), anapofikiri katika kuchelewa kwa hali ya kifikiri kwa ulemwengu kwa ujumla, wapi (Mwanisiko. Luuk, Spinser, Volteer, Jan Jack Ruso na Huyuom), basi walikuwa wakizungumzia jambo linawezekana kulitafitia na kujadiliana, na wanaonyesha mawazo wao kwa njia wazi, pamoja ukatao wetu kwa mambo mengi waliyatungulizia, lakini inaonekana kwamba adui mwenye akili ni bora zaidi mara elfu kuliko rafiki mjinga (jahili).
2-Limetokea wapi Suala chafu la mapenzi ya jinsia moja na hata likawa katika Haki za Binadamu? Ni nani aliyelifanya Jambo hili chafu lenye kuchukiza linaloenda kinyume na Dini zote zilizopo Duniani alizowahi kuzijua mwanadamu, tabia chafu ambayo inamsababishia Mwanadamu kuingiza katika Maisha yake Moto wa Jahannamu usiokwepeka, ambao hakuna anayeweza kutoka ndani yake, na Watu wakakumbwa na msongo wa mawazo na maradhi mbalimbali? Ni nani aliyeliingiza kinyemela jambo hili katika Haki za Binadamu? Kwa nadharia au falsafa ipi? Hakika hizi ni kelele tu na Sauti zisizo na maana yoyote zinazosema eti: "Mwacheni Mtu na maisha yake ambayo yeye ana uhuru wake wa kufanya atakavyo! Je? Mtu yuko huru kujiua? Na je, mtu yuko huru kuufanya uhaini mkubwa dhidi ya nchi yake? Au dhidi ya Jamii yake? Na je, mtu yuko huru kutumia madawa ya kulevya atakavyo na kufanya umalaya atakavyo? Na kuua kwa kuchoshwa tu na Mtu? Au kuua kwa sababu ya ugonjwa? Au kwa makubaliano? Mpaka mwisho wa orodha hii ndefu mno iliyohalalishwa na baadhi ya watu katika Jamii zao. Na je, uhalalishaji wa baadhi ya Watu kwa mambo haya kunayafanya yawe sehemu ya haki za binadamu ambazo Watu wote wanalazimika kuzifuata? Hakika sharti la kwanza kabisa la Haki za Binadamu ni kukubaliana Watu wote juu yake.
3-Na msiba mwingine mkubwa ni Suala la adhabu ya kifo ambayo inakusudiwa kuzuiwa na kufutwa, nayo inahitaji sisi tuiangalie kwa undani, na adhabu hii inakuja kwa kuwepo kila aina ya hakikisho na hali yake ni haki miongoni mwa Haki za Binadamu, ambapo falsafa yake imejengwa kwa lengo la kumkemea na kumzuia Mhalifu na kutokomeza Uhalifu wa Mauaji. Dhamana pamoja na Masharti yaliyowekwa yanatosha kulifikia lengo hilo Na nadharia ya kulipiza Kisasa katika Sheria ya Kiislamu ambayo inawezesha kutolewa msamaha na Watu wa aliyeuawa, na hapo ndipo kisasi kilipoanzishwa kwa lengo la kutuliza machungu na kuwasuluhisha Watu, imeboreka zaidi kwa upande wa Binadamu kuliko adhabu ya kifo inayofanywa hii leo. Kwa hiyo fursa ya msamaha wa familia ya marehemu na fursa ya kulipa fidia ya Mali ijulikanayo kama Diya, inauonesha Ubinadamu wa juu zaidi kuliko Msamaha mtupu usio na chochote. Ama kuhusu kufuta adhabu ya kifo kwa mhalifu kwa jumla kama walivyosema wenye sauti ya juu, isiyotegemea mtazamo sahihi, na wala falsafa wazi basi hiyo ni ujambazi (taadi) katika mwisho wake juu ya Haki za Binadamu.
4- Mwislamu anauangalia ulimwengu kama ni kiumbe cha Muumba aliye Mtukufu na kwamba Ulimwengu huu unaosabihia kwa ajili ya Muumba wake, na kwamba unahusiana na Matukio, na ukanyenyekea unyenyekevu ule ule wa viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu Mtukufu yeye pekee, na kwamba unapita katika Mwelekeo wa unaomsaidia Mwanadamu anayepitia mwelekeo huo huo, na unatofautiana na Mwanadamu anayeenda kinyume nao na hii ni moja kati ya Alama nyingi ambazo hazihitaji maelezo ya kufafanua jambo hili lionekane kwa uwazi zaidi. Mwenyzi Mungu Mtukufu amesema:
1. {AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; naYeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ninani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. NaYeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha}. [AL MULK 1,2]
2- {Huu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Basi nionyesheni wameumba nini hao wasio kuwa Yeye! Lakini madhaalimu wamo katika upotovu uliyo dhaahiri}. [LUQMAAN 11]
3- {Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama.Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji} [AL MUUMINUN 14]
4-{Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyoteviliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwasifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira}. [AL ISRAA 44]
5- {Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhivinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenyenguvu, Mwenye hikima.} [AJ JUM'AH 1]
6- {Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduniMola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe.} [AL HAJJ 77]
7- {Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwanguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iif}. [FUSWALAT 11]
8- {Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu naardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua navikaogopa. Lakini mwanaadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhaalimu mjinga.} [AL AHZAAB 72]
{La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, walahawakupewa muhula}. [AD DOKHAAN 29]
Ulimwengu unamsabihi na kumsujudia Mwenyezi Mungu Mtukufu, unalia na unakuja na unatii, na uko chini ya nguvu za Mwenyezi Mungu Mtukufu – vyote vimekuwa katika nafasi moja – na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtofautisha Mwanadamu kwa kumpa akili na akamdhalilishia Ulimwengu huu ambao aliuonea huruma ya kuubeba Ujumbe wake wa Amana nzito.
Mungu Mtukufu akasema: {Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni navilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.} [AJ JASIYAH 13]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi,na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayoakatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amriyake, na akaifanya mito ikutumikieni. Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daimadawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu. [IBRAHIMU 32, 33]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa, mwenye kuzikufuru neema}. [IBRAHIIM 34]
Na kuanzia hapo, inaonekana wazi kwamba Ulimwengu huo una haki vikiwemo vitu mbalimbali kama mawe na mimea na wanyama. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametubainishia kwamba sisi tunashirikiana navyo na kwamba sisi sio sehemu ya vitu hivyo bali sisi tumefadhilishwa juu ya viumbe vingi alivyoviumba, na tukadhalilishiwa mbingu na ardhi vyote kwa pamoja – ametukuka Mwenyezi Mungu Mtukufu – na kwamba sisi tumepewa Utukufu wa kuibeba Amana nzito ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni wajibu wetu kuitunza uzuri wa kuitunzana kwa ajili hiyo, tukapewa majukumu ya kutekeleza Amri zake Mwenyezi Mungu Mtukufu na Makatazo yake ambayo kwayo tunaulinda Ulimwengu huu Wote na tunautendea kama kiumbe cha Mwenyezi Mungu Muumba Wetu
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vyakupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vituvizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba}. [AL ISRAA 70]
Na kutumia kitendo ni kwa ajili ya kutilia mkazo, na hiyo katika mahali hapa inakanusha maana iliyoazimwa na inauthibitisha ukweli, na maana inakuwa kwamba kuwafadhilisha huko ni kweli, na siyo maana ya kuazimwa.
Kwa hiyo, Ulemwengu una haki, na mwanadamu ni bwana wake, ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu alimdhalilishia yeye.
Na tutaje kwa hayo baadhi ya Hadithi za Mtume S.A.W. zinazobainisha mtazamo wa kiimani wa Haki za Viumbi, Mimea na Wanyama, hata kama tukifikia kilele cha mambo na kilele chake (Binadamu) tutakuwa tumejua alikuwa wapi katika kundi hilo na mpango huo, na vipi haki zake zitakuwa kwake kama mwislamu.
1- Kutoka kwa Abu Kaab R.A. alisema: Mtume S.A.W. anasema: "Msiutusi upepo, na mtakapokiona mnachokichukia basi ni bora mkasema: Ewe Mola Wetu Mlezi hakika sisi tunakuomba heri ya upepo huu na heri ya kilichomo ndani yake na heri ya ulichokiamrisha na tunakuomba utukinge na Shari ya upepo huu na Shari ya yaliyomo ndani yake na shari ya uliyoyaamrisha" [Imetolewa na At Tirmidhi katika kitabu cha: Fitina, mlango wa: "Yaliyotaja katika kukania kutusi pepo" Hadithi ya 2252, na akasema: Ni Hadithi Sahihi na Nzuri"].
2- Kutoka kwa Abu Hurairah R.A. alisema: Nimemsikia Mtume S.A.W. anasema: "Upepo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu: na Nguvu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu huwa inakuja na rehema au adhabu, na pindi mtakapouona basi msiutukane, na Mwombeni Mwenyezi Mungu Mtukufu heri ya upepo huo na mjikinge kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Shari ya Upepo huo" [Imetolewa na Abu Dawud katika kitabu cha Adabu, mlango wa "Yaliyotaja zikivuma pepo, hadithi Na. ya 5097].
3- Kutoka kwa Twalha Bin Ubaid Allah R.A. alisema: Kwamba Mtume S.A.W alikuwa pindi anapouona mwezi husema: " Ewe Mola Wetu Mlezi tunakuomba tuandamishie kwa heri, Imani, Usalama na Uislamu, Mola Wangu Mlezi na Mola Wangu mlezi Mola wako" [Imetolewa na At Termidhi katika kitabu cha: Ad Da'wat, mlango wa: "Aliyoyasema mtu akimwaona Mwezi", hadithi Na. ya 3481].
4- Kutoka kwa Abu Saidi Al Khodriy amesema kuwa Mtume S.A.W. alipokuwa akila au akinywa husema: "Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetulisha na kutunywesha na akatujaalia sisi tukawa Waislamu" Imetolewa na Abu Dawud katika kitabu cha Vyakula mlango wa: "Anayoyasema Mtu anapokula au kunywa ", Hadithi ya 3850. Na At Termidhiy katika kitabu cha: Ad Da'wat, mlango wa: "Anayoyasema mtu akimaliza kula chakula chake", hadithi Na. 3457. Na Ibn Majah katika kitabu cha: Vyakula mlango wa: "Anayoyasema mtu anapomaliza kula chakula chake", Hadithi Na. 3283]
5- Mtume S.A.W. anasema: "kiheshimuni Chakula" [Imetolewa na Al Baihaqiy katika kitabu cha: As Shua'ab 84/5, Hadithi ya 5869. Na Al Haakem katika ktiabu cha: Al Mutadrak 136/4, Hadithi ya 7145 na akaisahihisha kwa Hadithi ya Aisha R.A.]
6- Mtume S.A.W, anasema: "Uhudi ni Mlima unaotupenda na tunaoupenda" [Imetolewa na Al Bukhariy katika kitabu cha: Al Maghaziy, mlango wa: "Kutelemka kwa Mtume S.A.W. kwa Al Hijr, Hadithi ya 4422, kutoka katika Hadithi kya Abi Hemed R.A.]
7- Hadithi ya Mche mdogo.
8- Hadithi ya Kuukata Mti wenye kivuli na Mtende.
9- Hadithi kutorejesha uvumba.
10- Kutoka kwa Abdullahi Bin Omar R.A, kwamba Mtume S.A.W. anasema: "Hakuna Mtu yoyote aliyemuua ndege mdogo au mkubwa bila ya haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamuuliza kuhusu ndege huyo" ilisemwa: nini haki yake Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Basi akasema: "Akamchinja na akamla na wala hakikati kichwa chake na kukitupa" [Imetolewa na An Nasa'iy katika kitabu cha: Kukwinda na Michinjio, mlango wa "Kuhalaisha kwa kula ndege mdogo" hadithi Na. ya 4349.
11- Kutoka kwa Shadad Bin Aus R.A. anasema: mambo mawili nimeyahifadhi kutoka kwa Mtume S.A.W. anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameandika Wema katika kila kitu na pindi mnapoua ueni vizuri na mnapochinja basi chinjeni vizuri na kila mmoja wenu anoe vyema kisu chake ili aweze kumstarehesha mnyama wake" [Imetolewa na Muslim katika kitabu cha: Kuwinda na Vichinjo na wanyama wanaoliwa; mlango wa: "Amri ya Uzuri wa Kuchinja, kuua na kunoa makali ya kisu, Hadithi ya 1955.
12- Kutoka kwa Abdullahi Bin Omar R.A, alisema: Mtume S.A.W. anasema: "Mwanamke mmoja aliingia motoni kwa sababu ya paka aliyemfunga bila ya kumlisha chakula au kumwacha huru ajitafutie mwenyewe chakula ardhini" Ina Hukumu ya Makubaliano juu yake, imetolewa na Al Bukhari katika kitabu cha: Chanzo cha Viumbi, katika mlango wa: "Wanyama watano walio nje ya hukumu ya kuwaua watauliwa ndani ya Eneo Tukufu la Makka", Haditi ya 3318. Na katika pahali pengine, Muslim katika kitabu cha Al Kusuf, mlango wa yaliyooneshwa kwa Mtume S.A.W, Hadithi ya 904 na katika pahali pengine]
13- Kutoka kwa Abu Hurairah R.A. kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Wakati Mtu mmoja alipokuwa akitembea njiani alipatwa na kiu kikali akaona Kisima akateremka kisimani na akanywa maji kisha akatoka na kumkuta mbwa akihema na kulamba mchanga kwa kiu silichokuwa nacho akasema yule mtu: mbwa huyu hakika amefikia Kiwanga cha kiu kama kile kile kilichonifikia Mimi, akateremka kisimani yule mtu na kuchota maji kwa kuyajaza kwenye kiriba chake cha ngozi kisha akamshika yule mbwa mdomo wake na kumnywesha maji, yule mtu akamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akamsamehe yule mja wake" Wakasema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, tuna thawabu kutoka wanyama? Basi akasema: Ndiyo, "Ndio, katika kila mnyama mwenye uhai kuna malipo" [Ina Hukumu ya Kuafikiana juu yake, imetolewa na Bukhari katika kitabu cha: Adabu, Mlango wa (Huruma ya watu kwa wanyama), Hadithi ya 6009. Na Muslim katika kitabu cha: As Salaam, malngo wa (Kuwanywesha maji wanyama wema na kuwalisha), Hadithi ya 2244, kutoka katika Hadithi ya Abu Hurairah R.A. na kwa tamko la Bukhariy].
14- Kutoka kwa Abdullahi Bin Mas'uud R.A. alisema: Mtume S.A.W. alimwona mtu akikichukua kifaranga kutoka kwa mama yake, na akasema: "Ni nani aliyemuhuzunisha huyu mama kwa kumuondolea Mtoto wake? Mrejesheeni Mtoto wake kwake", na Mtume S.A.W. alikiona kijiji cha, kimechomwa moto, basi akasema: "Hakika mambo yalivyo ni kwamba haadhibu kwa moto isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeumiliki moto". [Imetolewa na Abdu Dawud katika kitabu cha: Jihadi, mlango wa (katika Kuchukukiza kwa kuwachoma maadui moto), Hadithi ya 2675].
Huo ni mkusanyiko wa Hadithi za Mtangamanona na Kuishi pamoja na vitu vigumu, wanyama na mimea, zikiwa ni miongoni mwa mamia kama bali maelfu ya Hadithi zinazohusiana na maana hii inayobainisha uhusiano wa kina baina ya Muumini na vinavyomzunguka, kama vilimwengu na zinabainisha pia haki za vilimwengu juu ya mwanadamu katika hukumu mbalimbali za kufafanua zinazomwamrisha atende na kumzuia asitende maovu yanayosababisha madhambi, na yote hayo yako katika mzunguko wa rehma na urafiki.
- Hayo yanachukuliwa kutoka:
1- Wapole wote Mwenyezi Mungu Mtukufu anawahurumia, kwa hiyo wahurumieni walio ardhini mtahurumiwa na walio mbinguni. [Imetolewa na Abu Dawud katika kitabu cha: Adabu, mlango wa (katika huruma), Hadithi ya 4941. Na Tirmidhiy na tamko lake, katika kitabu cha Ubora na Uhusiano, mlango wa (yaliyotajwa katika huruma ya watu), Hadithi ya 1924. Na Hakem katika kitabu cha: Al Mustadrak 175/4, Hadithi ya 7274, na akaisahihisha kutoka katika Hadithi ya Abdellahi Bin Amru R.A, na Tirmidhiy amesema: Hadithi hii ina hukumu ya Hassan na Sahihi].
2- Ewe Aisha! Hakika urafiki hauwi katika kitu isipokuwa hukipendezesha, na hauondoshwi katika kitu isipokuwa hukifanya kiwe kibaya [Imetolewa na Muslim katika kitabu cha: Ubora, Uhusiano na Adabu, mlango wa (Ufadhili wa Huruma), hadithi Na. ya 2594].
Na kwa ujumla wake, pamepangika hukumu za Fiqhi na Maadili ya Kisheria yaliyoenea na kuongoza na kujengea Ustaarabu wa Kiislamu, kutoka hayo:
1- Kwamba kumwadhibu mnyama ni Haramu.
2- Kwamba kukata mmea bila ya dharura ni Haramu.
3- Kwamba miongoni mwa maadili ni mwislamu kutoupigiza mlango anapoingia na anapotoka kwa sababu mlango unamsabihi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
4- Hakika wao waliweka manywesheo ya mbwa waliopotea katika barabara za miji ya Kiislamu, na wakawa wanayasafisha kwa ajili ya wanyama hawa wanyonge,
5- Hakika wao walianzisha maeneo ya kuwatibu Wanyama kwa kutambua kwamba ni kwaili ya kuwapunguzia maumivu ya wanyama, na jambo hili linaenda zaidi na kupanuka mpaka likawa linafaa kufanyiwa Utafiti wa kitaalamu ulio mpana na unaojitegemea.
Ama Haki za Binadamu katika Uislamu ni kumlindia aina zote za uhuru wake wa kimsingi kwani haki hizo zinaambatana na Makusudio matano, na tuna mtazamo maalumu katika makusudio hayo, tunataka tuuoneshe, labda uwe na faida akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu (Inshaa Allah) ni:
Utangulizi wa Mpangilio wa Kanuni Kuu Tano:
Hakika sisi katika kuushughulikia Urithi wetu (mapokeo) hatusimami katika Masuala ya Waliotutangulia katika wakati ambao tunachukua ndani yake mifumo yao, mifumo ambayo inamaanisha utekelezaji wa Wahyi juu ya Maisha au Kuuachia kwa Kiwango katika mazingira yake ya kihistoria, basi tuitumie mifumo yao kwa ajili ya mwingiliano uliopo wa Mipangilio na Vifaa ambavyo tunawe kupitia vyombo hivyo, kufanya uzalishaji wa mifumo hiyo ili iendane na hali ya Maisha yetu ya Kisasa, yakiwamo mapya yanayotengenezwa katika Uhalisia wetu pamoja na wengine kutushambulia.
Na kuanzia hapo: Mpangilio wa Kanuni Kuu Tano za uratibu na mpangilio maalumu wa Wema waliotangulia, umetoa mchango wake katika zama zake, na uliyashughulikia Masuala yote yaliyokuwapo au yaliyotazamiwa kutokea katika zama zao isipokuwa katika zama zetu hizi – pamoja na kuwepo kwa kasi kubwa ya maendeleo ya Kimaisha na mwanzo mkubwa sana wa mapinduzi ya maelezo na kiteknolojia, iImekuwa lazima kuyatumia Makusudio haya Makuu matano, lakini kwa njia ambayo ni ya kiutendaji zaidi inayoendana na mazingira pamoja na matakwa ya zama hizi, na kwa ajili hiyo Sisi hatukuenda kinyume mfumo wa waliotutangulia katika mpangilio wa Makusudio haya, bali tumeyapangilia kwa Kiwango kinachoruhusu kuyatumia zaidi pamoja na matunda ya Ustaarabu wa kibinadamu uliofungamana tangu mwanzo wa karne hii mpaka sasa na hayajawahi kutoka katika Suala la lililoafikiwa na wote.
Mpangalio ambao tunauona unaafikiana na mahitaji hayo:
Kuilinda nafsi kisha akili kisha Dini kisha Ukoo kisha Mali. Kwa wakati ambapo Waliotutangulia walipanga utaratibu tofauti na huu kwa kuzingatia kwamba Maana yetu ya Dini hapa ni Ibada mbalimbali ambazo zinahitaji Nia au kuabudu kama kulivyo au Ibada yenyewe kama ilivyo hata kama ni katika miamala au ni utambuzi, na wala sio kusudio letu la Dini hapa kwa maana ya Uislamu, bali ni Uislamu ule wa marekebisho Jumla zaidi kuliko Dini kwa mweleweko huu, na kwa hivyo inakusanya Makusudio haya Makuu matano, na hivyo kutatua matatizo mengi.
Uislamu ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Watu wake na maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Watu wake –kama ilivyojulikana– ni hali ya kiungu ielekeayo kwa wenye akili iliyosalimika katika yale yaliyo na manufaa kwa Dini yao na Dunia yao; kwa hiyo Sisi tuko katika nafasi ya kuweka maneno kwa kutumia Istilahi mbalimbali mpaka tuelewe na tunapoyaweka maneno kwa ajili ya kuleta maana basi hapana budi ipingane na hali nyingine, wameiweka Wanachuoni waliotutangulia, na kuanzia wakati huo, hapatakuwa na hitilafu yoyote kimaana, bali huwa kinyume na hali yake.
Na utaratibu huu ingawa ni mpya isipokuwa kwa hakika hautokani na maneno ya Waliotangulia au kupingana nao na kwa hivyo haitokani pia na dalili ya kishairi na ikawa uzushi kwa mfano, bali hakika mambo yalivyo, hilo ni lango Miongoni mwa milango ambayo kwayo hali ya Umma husimama kidete katika zama hizi.
Utangulizi huu maana yake ni kwamba Uislamu ambao ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa watu, umeamrisha amri na amekanusha ukanusho, amri na kanusho hizo zinzkusudia kwamba wakihifadhia nafsi zao na wanahifadhia akili zao katika nafsi hizo, na kadhalika wanahifadhia uhusiano wao pamoja na Mola wao, ili kuhakikisha kusudi la kwanza kwa ukwepo wa wanadamu likiambatana na nafsi na akili na hilo ni (Ibada). Kisha Uislamu ukawaamuru baada ya hayo kwa kuhifadhia vizazi wao na haki zao na uimarishaji ardhi na hayo ambayo yanahkikisha Uimarishaji na Ibada, na uimarishaji kwenye Ibada, huo ambao dunia inautendea, na huo pia akhera inautendea.
Na mpangilio wa Misingi Mikuu mitano ni kwa utaratibu uliopitishwa na Wanachuoni ambao ni kama ifuatavyo: Nafsi, Akili, Dini, Ukoo, na Mali. Huu ni utaratibu wa kiakili wenye zingatio ambao ni wajibu kuulinda, Kwanza ni juu ya Nafsi ambayo kwayo vitendo vinafanyika, kisha akili ambayo ndio njia ya kubebeshewa majukumu. halafu tunaihifadhia Dini ambayo ina ibada ya kuimarisha ulemwengu. Halafu tunayahifadhia mambo yanayotokana na kuhifadhi akili, nafsi na Dini. Na hayo ni kuhifadhia vizazi vya mwanadamu. Na yanayofungamana au kuwa chini ya anuani hii Jumuishi ni katika kulinda Heshima, Haki za Binadamu na Utukufu wake kisha baada ya hayo ni kulinda Suala la Umiliki wa Mali ambao ndani yake kuna Ujenzi wa Dunia kwa mzunguko wa Mali, Mali ambayo inapozungushwa huwa ni uwakilishi wa mambo ya msingi kimaisha.
Mifano ya Matunda ya Utaratibu wa Mpangilio huu:
Miongoni mwa diapaji hiyo, na kwa kujua uhusiano uliopo baina ya Uislamu na makusudio matano hayo na ambayo Dini miongoni mwake, mambo kadhaa yanajengwa kwetu:
Uhusiano Wetu na Wengine nje na ndani ya nchi na ambao kwa ndani umejengeka juu ya ulezi wa Mambo ya Umma wote na nje umejengeka juu ya Ulinganiaji, na kwa hivyo Uhubiri Wetu kwa Walimwengu unakuwa na hekima, kwani katika uhusiano wetu na mwingine, sisi tunawabainishia ya kwamba Uislamu huu ni zaidi ya kuwa ibada tu, ambapo ni uhubiri wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa watu, na uhubiri wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa watu unakusanya mambo yanamwezeshea mwanadamu kuunda ustaarabu, na juu ya mambo yanamwezeshea kuimarishia ardhi, na kadhalika juu ya mambo yanayomwezeshea kuibada Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutii amri zake kwa utengeneshaji na siyo kwa jumla.
Na kwa ajili hiyo, hapana budi kwa yule aliye ndani ya nchi awe sehemu ya huo Uislamu na Ustaarabu wake hata kama hatakuwa mfuasi wa Dini yetu au Akida yetu na hapo ndipo inapotubainikia sisi kwamba Uislamu huu unakusanya Dini inayomuhusu aliyesilimu na akamwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, lakini pia na Nchi inayowalinda Watu wote na kuwalindia Malengo Makuu matano ambayo miongoni mwake ni: Dini, Mwenyezi Mungu Mtukufu amehalalisha kumkubali mwingine ndani ya wigo wake au chini ya kivuli chake.
Na akawahalishia Watu wa Kitabu wakae na Sisi na wawe wananchi na tule, tunywe na tuoane nao, ingawa Dini yetu Sisi inazuia wao kuwaoa wanawake Wetu na ingawa pia Dini yetu inatuzuia tusile baadhi ya vyakula vyao, isipokuwa katika kiwango cha Kiislamu wao wanaishi na Sisi na Lugha yetu ni moja na Ustaarabu Wetu ni mmoja, na matumaini na machungu yetu ni mamoja… na kuendelea, na haya ni kwa upande wa Mwingine ambaye yuko ndani ya nchi pamoja na Sisi.
Ama kwa mwingine aliye nje, uhusiano uliopo baina yetu na wao kimsingi unajengwa kwa Ulinganiaji na wala hatuna sisi na wao uhusiano wa amani au vita bali amani au vita huja kutokana na Suala la Ulinganiaji, kwani sisi tunapozuiwa au tukalazimishwa mazingira ya uwepo wa vita, na tiba ya mwisho ni kupiga chuku. Na kama hayawi kadhalika; {Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemeeMwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua} [AL ANFAAL 61]
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anayekutoleeni salamu: Wewe si Muumini; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii, hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu zipo ngawira nyingi. Hivyo ndivyo mlivyo kuwa nyinyi zamani, na Mwenyezi Mungu akakuneemesheni. Basi chunguzeni sawa sawa. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda} [An Nisaa 94]. {Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri} [AL Baqarah 191]. {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walio ongoka} [An Nahl 125].
Na kadhalika Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua} [AL Baqarah 256].
Na wala haituelekezi katika Nafasi hii Kauli ya kuifuta aya ya Upanga kwa aya nyingine, kwani wao hawajakubaliana hivyo, ukiongezea na kwamba kila aya moja wapo wamekubaliana ya kwamba inafuta, bali wakahitilafiana pia ndani yake, ukiongezea na utata huo mkubwa ambao unagubika Asili ya Kauli ya kufuta.
Na kwa kumalizia, tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ajaalie Haki za binadamu zisiwe egemeo la kila Mtu la kutundikia utamaduni na matamanio yake na mambo yake mengine binafsi, kwani haki za binadamu ni jambo muhimu sana na ni la hatari mno na hapana budi tuliepushe na ugumu na kuliweke kwa kila binadamu, na tuyahangaikie yale tuliyokubaliana badala ya maneno matupu ambayo akili wala moyo haviyakubali.
Rejeo: Kitabu cha: [Semaatu Al Aswar, kwa Mheshimiwa Mufti wa Misri Dkt. Ali Juma].
 

Share this:

Related Fatwas