Haki za Binadamu Ufupisho wa Kihis...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu Ufupisho wa Kihistoria Kimagharibi na Kisheria

Question

 Je! inawezekana kuelezea ufipisho wa kihistoria kimagharibi na kisheria utakao tuweka wazi juu ya maendeleo ya fikra ya binadamu kuhusu mtazamo wa haki za binadamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hilo linawezekana kupitia nukta zifuatazo:
Nukta ya Kwanza: Haki za binadamu katika jamii za mwanzo. Nukta ya Pili: Ufupisho wa historia ya Kimagharibi. Nukta ya Tatu: Makubaliano ya haki ya Kimagharibi. Nukta ya Nne: Matangazo ya haki za Kimataifa. Nukta ya Tano: Nafasi ya sheria kwenye mikataba ya haki.
Nukta ya Kwanza: Haki za binadamu ndani ya Jamii za mwanzo( ):
1- Tafiti za kijamii ambazo zimejikita zaidi kwenye jamii hizo zimeonesha kuwa binadamu amekuwa na nafasi kwa sehemu kubwa katika haki hizo ambazo zimekuwa kawaida katika zama za sasa kuitwa kwa jina la “Haki za Binadamu” na huenda hatuongezi maneno pindi tukisema: Hakika binadamu amestarehe katika wakati huu wa kwanza wa maisha yake wakati ambao ameishi kwa sehemu kubwa ya maisha yake duniani akiwa na haki zake kama binadamu zaidi ya wakati mwingine uliofuata.
2- Katika jamii za mwanzo desturi kwa mtu ilisimamia maisha yake na usalama wa haiba yake, na kufikwa na adhabu kwa yule mwenye kuzifanyia uadui haki hizi, jamii ya mwanzo wala haikuwa ikifahamu tabia hizo ovu ambazo zilijitokeza katika hatua ya pili ya historia ya binadamu hatua ambayo ilikuwa ni ya kuwindwa binadamu, na kutolewa kafara kwa makuhani wa wanadamu, pamoja na kula nyama za binadamu.
3- Kama vile utafiti umeonesha kuwa haki ya uhuru na usawa zilikuwa zinafanya kazi ndani ya jamii hizo, hapakuwa na utumwa watu wote walikuwa ni huru wapo sawa kwa kiwango ambacho hakuna kwenye jamii za sasa, usawa katika jamii za mwanzo haukuwa wenye kusimamiwa na sheria bali ni sehemu ya maisha, hakuna tofauti, tajiri na masikini, kiongozi na anayeongozwa bali wote walikuwa na duru katika jamii kwa usawa, na hata wale ambao walikuwa na sifa ya kuwa na akili, uzoefu na usimamizi sifa hizi hazikuwa sababu ya kusamehewa kutekeleza wajibu wao wala kuwapa sifa ya kipekee.
4- Hatushangai kwenye utafiti wa jamii za mwanzo kuwepo usawa kati ya jinsia mbili kwa sura ambayo lazima ifanyiwe husda na jamii zetu za sasa, na wanakaribia watafiti wa jamii hizo kukubaliana juu ya kiwango cha usawa kati ya jinsia mbili ndani ya jamii za mwanzo haujafikiwa baada ya hapo na hatua yoyote ile ya historia ya binadamu.
5- Kama vile kuna ushahidi mwingi kuwa ndoa katika jamii za mwanzo zilikuwa zina usawa kati ya mume na mke, ambapo ugawaji wa haki na wajibu ulikuwa kwa sehemu kubwa ni kwa kiwango sawa kati yao, ama kwa upande wa haki za watoto katika jamii za mwanzo watoto walikuwa wanapata umuhimu maalumu na malezi maalumu ambapo ushahidi wote unakubaliana kiwango ailichokuwa anakipata mtoto cha ushirikiano laini na kupewa umuhimu mkubwa.
6- Pamoja na kuwa maisha ya mwanzo: Lakini haki ya kulinda uzalishaji wa kifasihi na kielimu ambao umekuwa ni fahari kwenye jamii za kisasa zilikuwepo katika jamii za mwanzo, kwa mfano unachofahamu jamii hii katika maisha ya mwanzo ya kitamaduni, ikiwa ni pamoja na mashairi nyimbo na mfano wake miongoni mwa harakati za kitamaduni zinazoendana na binadamu tokea zama za mwanzo kabisa.
7- Tofauti na yanayofikiriwa na wengi kwani jamii ya mwanzo haikuwa ikiishi maisha ya kukata tamaa na uovu bali walikuwa wakiishi maisha yenye furaha wakiwa na ukamilifu wa mambo muhimu ya maisha pasi ya tabu, kulikuwa na mifuko ya hifadhi za kijamii kwa mwenye kushindwa mgonjwa na mtu mzima, mpaka mmoja wa wanachuoni wa mambo ya wanadamu aliwahi kuita: Jamii yenye asili ya ustawi.
8- Ama mambo ambayo anapazia sauti binadamu wa zama za sasa: Ni haki ya kisiasa: Hatuachi kuelezea kuwa hakuwa na nafasi kwa mkandamizaji au muovu katika jamii za mwanzo, kwani jamii nyingi za mwanzo hazikuwa na rais kwa maana ya kina zaidi, na hata jamii ambayo ilikuwa na rais lakini mamlaka yake yalikuwa ni dhaifu sana, na cheo chake hakikuwa cha kurithiwa, kama vile alikuwa hachaguliwi kwa njia ya umbile bali alikuwa anapatikana kwa njia ya kimaudhui zaidi, na kwa uchaguzi wa pamoja na wa ndani zaidi kwa yule mwenye sifa zinazokubaliana kuwa rais, wanasema baadhi ya watafiti wa jamii hizo: “Jamii ndogo za mwanzo siku zote zilikuwa ni jamii za kidemokrasia, ni mara chache sana kuonekana uongozi kandamizi kati ya watu wa jamii za mwanzo”.
9- Ama kuhusu haki za binadamu kutokuwa na vitendo vya mateso: Ni wazi kuwa masuala ya mateso na adhabu hayakuwa na nafasi kwenye jamii hizo, kama vile watu wake walikuwa ni wenye kupenda utulivu na kuishi kwa amani tofauti na fikra zilizoenezwa, kisha kukaenea hali ya kuheshimiana kati ya watu jambo ambalo lilipunguza nafasi ya mizozo, na mahakama ilisimamia haki na uadilifu mpaka mwenye haki aliweza kupata haki yake, pamoja na kutokuwepo mahakama kwa maana ya kina zaidi, isipokuwa kulikuwa na njia nyingi ambazo zilikuwa zikifuatwa kwenye jamii za mwanzo ili kuwezesha watu wenye haki.
10- Mwisho kabisa haki za binadamu zinakuja katika amani ambayo ilikuwa ni moja ya haki iliyothibiti katika jamii za mwanzo: Pamoja na fikra iliyotangulizwa kuwa jamii hizo zilikuwa zenye chuki na kiu ya damu siku zote vita vilikuwa vikiendelea kati yao: Lakini maelezo halisi mengi kutoka kwenye jamii hizo yanathibitisha kuwa fikra hii iliyotangulizwa haikuwa mbali sana na ukweli( ).
11- Katika kipindi kijacho cha binadamu: Ni kipinidi cha jamii ya kikabila zikionekana kwa mara kwanza baadhi ya mila mbaya na ovu: Ambapo haki ya binadamu ya uhai ikivunjwa katika hali nyingi sana kama vile kula nyama ya binadamu na kumtoa binadamu kafara kwa makuhani .. lakini la kuzingatiwa katika jamii za kikabila kwa upande wa haki ya uhuru ni kuwa pamoja na kuwepo vyanzo vingi vya utumwa lakini kwa hali yoyote ile haiwezekani mtu mmoja wa kabila kuwa mtumwa, wakati ambapo tunakuta tukio hili ndani ya jamii za mijini ambapo inawezekana mmoja wa mwananchi akapoteza uhuru wake kwa masilahi ya mwananchi mwengine, kama ilivyo hali ya utumwa kwa mdaiwa aliyeshindwa kulipa deni lake, na hali ya wizi ambapo huadhibiwa ndani ya jamii za Kiyahudi zamani kwa kufanywa mtumwa.
12- Pamoja na kuwepo matukio ya utumwa kwenye jamii za kikabila lakini ni lazima usawa utikisike kwa mtu wa kisheria ambaye walikuwa nayo watu wote kwenye jamii za watu wa mwanzo, na jamii za kikabila zinachukuwa mwelekeo wa kuelekea katika kukosekana usawa kati ya watu huru, na ubaguzi wa dhidi ya wanawake, kama ilivyokuwa kuwepo kwa baadhi ya masharti kwenye haki ya kuoa, na kwenye usawa kati ya wana ndoa wawili, isipokuwa haki za mtoto ndani ya jamii za kikabila ziliendelea kuwa kama zilivyo kwenye jamii za watu wa mwanzo, ambapo mtoto kwenye jamii nyingi za kikabila anapata ushirikiano mzuri na usimamizi mzuri, isipokuwa tunakuta tukio la ubaguzi kati ya mwanaume na mwanamke, kama vile tunakuta tukio la kuzikwa watoto wa kike wakiwa hai ndani ya baadhi ya makabila.
13- Ama kuhusu haki ya kushiriki kwenye maisha ya kitamaduni ndani ya jamii za kikabila yenyewe inasimamiwa na watu wote wa kabila, kama vile jamii ya kikabila inatambua wale wenye kuzalisha uzalishaji wa kiakili kwenye haki za kifasihi na mali hasa kwa uzalishaji wao.
14- Kwa upande wa haki za kisiasa kwenye jamii za kikabila, katika makabila hayo ambayo yasiyokuwa na Rais au kiongozi mkuu tunakuta kuwa watu wamekuwa na uhuru kwa kiwango kikubwa sana, ama jamii zile ambazo kuna rasi: Kumekuwa na tofauti kubwa katika njia ya kumteua Rais huyo, na katika kikomo cha mamlaka yake pia kinatofautiana na – Uhalisia wa hali – ya haki za kisiasa kwa watu wengine.
15- Kwa upande wa haki za kutoadhibiwa ndani ya jamii za kikabila, haki hiyo pamoja na kuwa inasimamiwa kwa sehemu kubwa ndani ya kabila lenyewe, lakini imekuwa ikivunjwa kwa kiwango hicho hicho sawa na makabila yenye uadui. Haki ya kimahakama pia ni yenye kusimamiwa kwenye jamii hizi za kikabila kwa njia ya mfumo wa hukumu na mfano wake. Kama vile jamii ya kikabila inasimamia haki ya makazi, kama vile upo mfumo wa ujirani na kumlinda mpangaji.
16- Ama haki ya binadamu katika amani kumeshuhudiwa kushuka sana ndani ya jamii za kikabila zaidi kuliko kwenye jamii za watu wa mwanzo, ambapo jamii za kikabila zilifahamu vita vya mfumo( ).
Nukta ya Pili: Ufupisho wa kihistoria na Kimagharibi:
17- Haki za binadamu katika ustaarabu wa Kimagharibi zina historia ndefu, na yenye machungu katika baadhi ya kurasa zake, ni lazima sisi kama Waislamu wa zama za leo kuifahamu historia hiyo na kufahamu hasa nini kilitokea, lakini pia tufahamu kuwa nchi za Magharibi bado zimechelewa katika masuala ya maadili na mtazamo wa kibinadamu, na Uislamu bado umeendelea kupiga hatua kubwa kuliko watu wa Magharibi kwenye viwango vya mitazamo na maadilli, lakini kwa masikitiko makubwa sisi hatufanyii kazi kwa kiwango kinachopaswa kufanyiwa kazi.
18- Pindi tunapoangalia kuhusu haki za binadamu katika Uislamu, na kuathiri kwake kwenye ustaarabu wa kisasa wa Kimagharibi, zinatuwezesha kupendezesha historia ya haki za binadamu kwa nchi za Magharibi katika maeneo yafuatayo:
19- Kilichothibiti kihistoria ni kuwa Wafaransa walikuwa ni watu wa kwanza kuita jina hili kwenye mikataba ya haki, na wakaita sifa za haki katika tangazo lao ambalo lilitolewa mwaka 1789, kwa kuzingatia kuwa haki hizo hazihusu binadamu bila ya mwingine bali zenyewe zinafungamana moja kwa moja na binadamu kwa kumzingatia ni binadamu vyovyote atakavyokuwa, hivyo basi hawakuzielekeza kwa Wafaransa kama walivyofanya Waingereza na wananchi wa Marekani katika matangazo yao( ).
20- Lakini miongoni pia mwa yaliyothibiti kihistoria ni kuwa maudhui ya fikra, na msingi wake kifalsafa ulizaliwa huko Athena kupitia kwa wanafalsafa wa sheria za asili walikuwa ni watu wa shule ya Wasophists( ). Tofauti ni kuwa fikra imeendelea kuwa ni fikra ya kifalsafa isiyotekelezeka kivitendo katika nchi za tawala za kiraia za Kigiriki, au tawala za Kiroma, ni fikra ambayo ilikuwa bado haijatambua binadamu katika ustaarabu wa Kimagharibi kuwa ana haki yoyote, kabla ya kuanzishwa kwa dola ya sasa.
21- Ukristo ulijaribu mwanzoni mwa kuanza kwake kuthibitisha kuwa binadamu anathamani yake kama binadamu na kusisitiza juu ya haki yake iliyopewa uzito kwa sehemu ya kwanza nayo ni uhuru wa kuamini, na ilikuwa ni hatua kubwa ya kuelekea kutambua kuwa binadamu ana haki zake za mwanzo isipokuwa wasimamizi wa mambo ya Dini ya Kikristo walirudi nyuma kwenye hatua hiyo ndani ya karne ya kumi na nne pindi kuliposhika kasi kurudi nyuma kwao, na kutambulika na mtawala wa Constantine kuwa ni Dini rasmi ya utawala wa Kiroma, na kuzingatia ndio imani pekee inayoruhusiwa ndani ya utawala( ).
22- Kisha fikra ya “Haki za Binadamu” Barani Ulaya ikapotea baada ya hapo katokana na kiza cha karne ya kati isipokuwa kutokana na ukwapuaji wa machungu mfano wa zama kubwa nchini Uingereza ambayo ilitokea mwaka 1215, na kupelekea kikomo cha mamlaka ya Mfalme, Viongozi na Watu wa dini kwa masilahi ya wananchi.
23- Ikiwa huu ndio mwelekeo wa fikra kwa nchi za Magharibi wenyewe kwa upande wa nchi za Mashariki pamoja na kuanza kwa Uislamu mwanzoni mwa karne ya saba ilionekana orodha ya kwanza ya kweli na yenye kushirikiana ya haki za binadamu katika historia ya fikra ya binadamu, na dola ya kwanza ya Kiislamu ndiyo ilikuwa dola ya kwanza duniani kutekeleza kwa dhamira kubwa haki zote hizo.
24- Na kwa kuingia karne ya kumi na saba ndipo walipoanza kuonekana wanafikra wa Kimagharibi ambao wanajiita kwa jina la “Watu binafsi” au wanafalsafa wa madhehebu binafsi kama vile mfano wa: John Locke 1632 – 1704. Jean-Jacques Rousseau 1712 – 1778. Adam Smith 1723 – 1790. Jan Baptist Say 1826 – 1896. Mitazamo yao ni kuwa lengo kubwa la sheria ni “Kulinda haki ya binadamu na uhuru wake”( ). Hawa walianzisha falsafa zao kwa msingi wa nadharia ya haki na uhuru asili ambao umekuwa ni zao la fikra za shule ya sheria za asilia.
Nukta ya Tatu: Mikataba ya haki ya Kimagharibi:
25- Kuna mikataba mingi ya Kimagharibi ya haki miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na mikataba ya Uingereza, Marekani na Ufaransa.
26- Ama Mkataba wa haki wa Uingereza: Ulipelekea kuzaliwa mapinduzi ya mwaka 1668 nchini Uingereza kung’oka kwa bunge la Mfalme James II, na kuitwa William Orange kuchukuwa Ufalme, siku ya tarehe 13 February mwaka 1688 alitoa “Waraka wa Haki” ili kuwa ndio msingi wa utawala na sharti kuu, katika waraka huo ulikuwa unaungana na ulinzi wa masilahi ya kiuchumi kwa tabaka la kati, na kwa mujibu wa waraka huo Mfalme aliachia mamlaka zake nyingi na kuzikabidhi kwenye bunge, tabaka la kati lilishikilia Ubepari bungeni jambo lililopelekea mabadiliko makubwa katika mfumo wa uwakilishi wa kibunge, na kukaribia mfumo wa kuwapigia kura wawakilishi hao( ), na vyovyote itakavyo kuwa kwenye waraka huo na tuhuma za baadhi kuwa haukuwa waraka wa kidemokrasia( ) lakini kitendo tu cha Mfalme kuachia baadhi ya mamlaka yake na kuyakabidhi kwenye bunge hayo ni mafanikio makubwa ya demokrasia, kwa sababu maamuzi hayo yamehamisha utawala kutoka kwa mtu “Mfalme” na kwenda kwa “Wengi” kwa maana ya bunge, na walikuwa kwa kiwango kikubwa wanawakilisha bungeni ni wananchi na kila yanapoongezeka mamlaka yao inakuwa ni kwa masilahi ya wananchi.
27- Pamoja na kutokuwepo waraka au mkataba wa haki nchini Uingereza ulioandikwa sawa na mkataba wa Marekani au Ufaransa, au katiba kuu iliyoandikwa lakini hata hivyo kuheshimu uhuru ni jambo lenye kuendelea wakati huo huo ni uteteza wa haki za msingi, kwani kulinda uhuru wa jadi nchini Uingereza ni mfano uliobora zaidi wa nguvu ya jadi na roho ya ushindi ya wananchi, haki za mtu nchini Uingereza ni zenye kulindwa na kuangaliwa kwa nguvu ya utekelezaji wa kanuni za sheria.
28- Pamoja na kuwa kisiasa kwa Uingereza lakini nukta dhaifu ambayo imeharibu haki za msingi kwao ni kuwa nchi hiyo ilidumu kwenye haki za Mwingereza, hakuna haki za binadamu, wakazuia wakazi wa makoloni yao mpaka hapo baadaye sana( ). Hii inatukumbusha demokrasia ya Athena ambayo ilikuwa inajihusisha kwa wananchi huru pasi na watumwa, kwa maana wageni kwa ujumla wanaotoka mataifa mengine.
29- Kwa upande wa Mkataba wa haki wa Marekani: Unazingatiwa ni mapinduzi ya Kimarekani ikiwa ni haki ya kwanza kurasimishwa kwa sura ya wazi ndani ya zama za sasa ni haki za binadamu, na kuunganishwa na mkataba wa tangazo la uhuru wa muungano wa majimbo ya Jamhuri ya watu wa Marekeni baada ya mapinduzi yao ya kuishinda Uingereza mnamo tarehe 04/07/1776 ushindi ambao ulitanguliwa na tangazo la Umoja na katiba ya mwaka 1777, na kupitishwa mwaka 1781. Na yaliyokuja kwenye katiba: “Sisi tunaendelea kama msingi wa wazi kuamini yafuatayo: Watu wote wapo sawa na wote wana haki kama walivyopewa na Muumba ni haki ambazo hazifai kuachwa, miongoni mwa haki hizo ni haki ya uhai uhuru na juhudi za kutafuta furaha”( ).
30- Haki za binadamu nchini Marekani zinazingatiwa ni zenye kupangiliwa zaidi kuliko mfumo wowote ule mwingine wa kidemokrasia, na zinaonekana ni zenye usalama zaidi katika nyenzo zake, katika kuzilinda kwake haki za binadamu na uhuru ni vyenye kuandikwa ndani ya katiba ya Kifederali, na katika katiba za Marekani, ndani ya katiba hizi zinahamasisha mazingira ya “Sheria Kuu” nayo imelindwa si kufanyiwa uadui na mamlaka ya utekelezaji tu bali imelindwa kutokana na uadui pia wa mamlaka ya kutunga sheria, kumekuwa na mahakama huru ambazo hufanya kazi za kuhakikisha katiba inafanya kazi( ).
31- Lakini mipaka na vigezo kwenye haki hizi vimekuwa wazi hata kwenye nchi kama Marekeni chini ya mminyo matatizo na mikakati ambayo hufanywa na harakati za makundi ya sasa na mminyo wa kijamii usio kuwa wa kisheria( ).
32- Ama Mikataba ya haki nchini Ufaransa: Wanachuoni wengi wa masuala ya sheria kinyume na wengine wamekuwa wakipongeza na kutukuza hizi haki, kwa kuwa “Zina maanisha ni falsafa ya kidemokrasia ya Kimagharibi kuhusu uhuru….”( ), pamoja na kuwa kuna mikataba mingine ya zamani ya haki ya Uingereza na Marekani ilikuwa na ubora mkubwa katika kuunga mkono haki binafsi na uhuru wake, mapinduzi ya Ufaransa yalitoa kipaombele na umuhimu mkubwa kwenye haki za binadamu tokea mwanzo kabisa mpaka likatolewa tangazo la haki la tarehe 26 August 1789, katiba haikugawanywa baada ya kukusanywa na kutengenezwa isipokuwa siku ya tarehe 14 September 1791 kwa maana baada ya miaka miwili tokea kutolewa tangazo la haki( ).
33- Katika tangazo hili kwenye kifungu chake kwanza kilieleza “Watu wanazaliwa wakiwa huru na wapo sawa mbele ya sheria”, ama kifungu chake pili kinaelezea kuwa “Lengo la kila kundi la kisiasa ni kulinda haki asili za binadamu, na zilizothibiti. Na haki hizi ni: Haki ya Uhuru. Umiliki. Usalama na Kupambana dhidi ya vitendo vya matumizi ya nguvu”. Miongoni mwa yanayoonesha uzito na umuhimu uliotolea na Wafaransa kwenye haki hizo ni kukaribia wawekaji wa katiba ya Nablion kusajili kwenye sheria hii yale yaliyopitishwa na mapinduzi ya Kifaransa katika “Tangazo la Haki” ikiwa ni uwepo wa sheria asili na iliyothabiti haibadiliki, kwa hili ulikuja muswada wa kwanza wa sheria hizo lakini walikomea kufuta tamko hili silo kwa kuzingatia kuwa si sahihi bali kwa kuzingatia sehemu ya kufuata madhehebu ya kifalsafa yasiyoendana na asili ya tamko la kisheria( ).
34- Katiba zilizofuata nchini Ufaransa bado zilitoa umuhimu mkubwa kwenye haki za binadamu ikiwa ni pamoja na katiba ya mwaka 1946 na katika ya mwisho ya mwaka 1958, katika utangulizi wa katiba hii iliyotolewa tarehe 04/10/1958 unasema: “Wananchi wa Ufaransa wanatangaza wazi kushikamana kwao na haki za binadamu, misingi ya utawala wa kiraia, kama ilivyokuja kwenye tangazo la haki la mwaka 1789”( ). Kinyume na Waingereza: Tunakuta kuwa Wafaransa tokea zama za mapinduzi makubwa walipaza sauti zao kwenye “Haki za Binadamu”, na wala sio haki za Wafaransa, Wafaransa waliendesha vita vitakatifu kuhusu haki na uhuru baadhi ya vita hivyo vilikuwa ndio chanzo cha mabadili na maendeleo ya nchi za demokrasia huru( ).
Nukta ya Nne: Tangazo la haki la Kimataifa:
35- Baada ya dunia kuingia kwenye vita vikuu viwili vya dunia ndani ya muda wa chini ya nusu karne ulimwengu ulipaswa kufanya hima kubwa ya kutafuta njia zitakazosimamia kutorudia tena mfano wa hayo ili kulinda ujinsia wa kibinadamu na haki zake kisheria.
36- Wakakutana watu wa mataifa yote ili kuanzisha Jumuiya ya Umoja wa Mataifa ambayo tamko la dibaji yake lilianza: “Sisi ni wananchi wa Umoja wa Mataifa tumekubali wenyewe kuokoa vizazi vijavyo kutokana na cheche za moto wa vita ambavyo ndani ya kizazi kimoja kwa binadamu vimeleta huzuni mara mbili isiyoweza kuelezeka. Na kusisitiza tena uzalendo wetu kwenye haki za msingi za binadamu, na kuheshima mtu na uwezo wake, na walichonacho wanaume na wanawake, mataifa makubwa na madogo miongoni mwa haki sawa”.
37- Kisha mkataba unasimamia baadhi ya vipengele maalumu kwenye haki hizi miongoni mwake: “Kifungu cha kwanza sehemu ya tatu: Miongoni mwa makusudio ya Umoja wa Mataifa ni kufikia ushirikiano wa Kimataifa ili kutatua masula ya kiuchumi, na kuimarisha kuheshimu haki za binadamu na msingi wa uhuru kwa watu wote, pamoja na kuuhamasisha, pasi ya kubagua kwa sabubu za kijinsia au lugha au dini, hakuna kutofautisha kati ya wanaume na wanawake”.
38- Kifungu cha 13 sehemu ya (1) b kinasema: “Tunaanzisha kwenye Jumuiya Kuu tafiti na kufikia maadhimio kwa lengo la kusaidia kufikia haki za binadamu na msingi wa uhuru kwa watu wote, bila ya ubaguzi kati yao kwa sababu za kijinsia ... ”.
39- Kifungu cha 55 c kinasema: “Utashi wa kuandaa masharti ya utulivu na ustawi ni muhimu ili kujenga mahusiano salama yenye upendo, mahusiano yanasimama kwenye msingi wa kuheshimiana, ambao unapelekea kwa wananchi kuwa na haki sawa, na kuwafanya na maamuzi ya mustakabali wao, Umoja wa Mataifa utafanya kazi ya kusimamia kuheshimu haki za binadamu duniani kote, pamoja na misingi ya uhuru kwa wote pasi ya ubaguzi wowote kwa sababu za kijinsia na mivutano kwenye haki hizo na uhuru huo”.
40- Pia vifungu vya 76, 68,62,56 vimekusanya ishara za haki za binadamu, liliundwa baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa “Tume ya haki za binadamu” kwa lengo la kuandaa muswada wa waraka wa Kimataifa wa tangazo la haki za binadamu, misingi ya uhuru wake, namna ya utekelezaji wake, zipi njia za utekelezaji wake na hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya ukiukaji wa haki hizi, tume iliendelea na kazi zake kiasi cha miaka miwili huko Lake Sex na Jeneva, kisha ikawasilisha muswada wa kwanza maalumu wa waraka wa tangazo la haki na uhuru na kupitishwa na Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa.
41- Miongoni mwake ni pamoja na maamuzi nambari (217) ya kwenye kikao cha kawaida cha tatu kilichofanyika Paris siku ya tarehe 10 December 1948, tangazo la Kimataifa lilikusanya haki za binadamu kwenye vifungu thelathini vyote vinazungumzia kuhusu haki za binadamu kwa sura zake zote, na mada yake ya kwanza inaelezea kuwa: “Kuzaliwa watu wote wakiwa huru wenye usawa katika heshima na haki wamepewa akili na dhamira, ni juu yao kushirikiana wao kwa wao kwa roho na undugu….”.
42- Yalitolewa makubaliano mengi ya Kimataifa kuhusu haki za binadamu kama vile makubaliano ya Kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa yaliyotolea kwa maamuzi ya Umoja wa Mataifa nambari (2000) katika kikao chake cha kawaida cha (21) cha tarehe 16 December 1966, na makubaliano mengine ya tarehe hizo hizo na duru kuhusu haki za kiuchumi kijamii na kitamaduni.
43- Kuna makubaliano mengine mengi, hatuwezi kuelezea yote, na maudhui zake ni: Kupambana na ubaguzi wa rangi, kuzuia mauaji ya kimbari ya jinsi ya wanadamu, kuzuia utumwa, uhuru wa vyama vya wafanya kazi, haki ya kuamua mustakabali, kulinda wahanga wa vita, familia, usawa katika mishahara, kuzuia dharau…..n.k.( ).
44- Jambo tunalolipa umuhimu kwenye tangazo hili la Kimataifa la haki za binadamu ni kuwa limekusanya haki zote za binadamu, limezungumzia juu ya kulinda haki zake kisiasa, kiraia, kijamii, kitamaduni na kiuchumi nazo ni haki mpya hazikuingizwa kwenye matangazo yaliyopita ya haki, ni tangazo lenye sifa ya pekee nzuri kwa maana ya kulazimisha nchi kufikiwa haki hizi kwa watu, mfano vifungu vya 22 mpaka 28( ).
Nukta ya Tano: Nafasi ya kisheria kwenye Mikataba ya haki:
45- Ikiwa hakuna tofauti kuhusu ya katiba kuwa ndio chanzo cha kwanza cha sheria ndani ya nchi mbali mbali, lakini tofauti inaibuka katika sheria na kanuni kuhusu nafasi na thamani ya makubaliano ya haki ambazo zinatengenezwa na kujitegemea nje na katiba, vilevile tangulizi za katiba hizi ambazo zinakusudiwa na watunga sheria – mara nyingi – mjumuiko wa misingi yenye kufuata imani za nchi na madhehebu yake kwenye pande mbalimbali za maisha, na kumekuwa na rai pamoja na mitazamo mingi katika hilo( ):
46- Rai ya Kwanza: Yenyewe ina nafasi kubwa kuliko nafasi ya matamko yenyewe ya kikatiba, ikiegemezewa kuwa yenyewe inaelezea utashi wa Mataifa, na kukusanya misingi huru ya kikatiba katika dhamira ya kibinadamu ambayo inalazimisha kuheshimiwa na kufanyiwa kazi hata kama hakuna tamko lake katika matangazo au utangulizi wa katiba, kuongezea na ugumu wa katiba yenyewe, yenyewe inaelezea misingi ambayo imejengewa matamko ya katiba, hivyo wafuasi wa rai hii huita “Katiba ya Katiba zote”. Kwa sababu hiyo yenyewe ni inawajibisha kwa mamlaka husika inayosimamia katiba, na zaidi ni serikali kuu ambayo imetajwa na katiba.
47- Rai ya Pili: Inatoa nafasi sawa na matamko ya katiba kwa kuwa inatokana na pande yenye mamlaka ya kutengeneza katiba, na pande zengine ni zenye kufasiri misingi ya katiba.
48- Rai ya Tatu: Inatoa nafasi inayolingana na sheria za kawaida, yenyewe haipandi kufikia nafasi ya matamko ya kikatiba kwa sababu wawekaji wake lau wangetaka hivyo wangeleta ugumu wa katiba, na kutokana na hilo bunge linaruhusiwa kufanya marekebisho kwa mujibu wa masilahi ya Umma kinyume na idara husika.
49- Rai ya Nne: Inapinga nafasi zote za kisheria kwa sababu haipelekei kuanzisha vituo vya kisheria vilivyo wazi visivyojumuisha isipokuwa ni misingi ya kifalsafa na kisiasa wala havielezei isipokuwa ni matumaini na misingi yenye nafasi ya kifasihi pasi na wajibu wa kisheria.
50- Rai ya Tano: Nayo ni baraza la nchi la Ufaransa ambalo halizuii kuongeza sifa ya kisheria, lakini halipo wazi katika kuainisha nafasi yake kati ya matamko hayo, lenyewe limezingatia kama ni kanuni za kidesturi, vilevile misingi ya kisheria, na mwisho baraza limezingatia kuwa ni matamko ya kisheria yanayolazimisha, nayo katika hali zote ni yenye kuelekea upande wa kiidara tu, ambapo mahakama ya Kifaransa mpaka hivi sasa hachukui sheria kwa usimamizi wa kikatiba hivyo upande wa idara ni wenye kulazimika nazo pasi ya mtunzi sheria.
51- Rai ya Sita: Nayo ni rai ya kati na kati inatenganisha kati ya miundo ya misingi hii katika umbo la kanuni za kisheria zilizowazi ili kuanzisha vituo maalumu vya sheria, hii inayapa nguvu matamko ya katiba kulazimisha. Ama misingi ambayo inaishia kwenye maelekezo makuu malengo na sheria kuu yenyewe inaepukana na kila nafasi ya kisheria hata kama itabakia nafasi ya kifasihi.
52- Rai ya Saba: Inatenganisha kati ya aina mbili za kanuni, yenyewe inatengenisha kwenye matamko ya matangazo kati ya yanayotengeneza misingi ya kisheria kwa maana sahihi na mwanzilishi wa vituo vya wazi vya sheria, na hii inatoa nguvu sheria kulazimisha, ama yanayoelezea malengo matumaini na misingi ya kifalsafa hayana isipokuwa thamani ya kisiasa na nguvu ulazima wa kifasihi, nayo inatoa nguvu kwenye misingi ya mwanzo inayolazimisha kisheria kwa kiwango cha juu kuliko matamko ya katiba, na kulazimisha mamlaka za Kitaasisi bali hata mamlaka za kikatiba, kwa sababu kama ilivyoelezewa na watu wa rai hii inajumuisha misingi mikuu huru katika dhamira ya kibinadamu( ).
53- Rai ya Nane: Ni kuwa matangazo haya ni maelekezo kwa mamlaka zinazopaswa kulazimika nayo tofauti ya ulazima huu kisiasa na wala hauna nafasi kisheria( ).
54- Baadhi ya watafiti wanaona kuwa rai hizi zimechanganya kati ya mambo mawili: Jambo la Kwanza: Zimechanganya kati ya mikataba ya haki na tangulizi za katiba na kuyaweka kwenye safu moja, wamejaribu kuyapa thamani na nafasi moja na kanuni moja, pamoja na kuwa kila moja inasifa tofauti na nyingine, na ina asili tofauti na asili nyingine. Jambo la Pili: Kumekuwa na tofauti ndani ya makubaliano ya haki na tangulizi za katiba kati ya matamko ambayo yanajumuisha misingi ya kisheria iliyowazi, na kuyapa nguvu za lazima za kisheria kwa katiba ya aina yoyote ile, au sheria ya kawaida na kuendelea, ama sheria na misingi ya kifalsafa ambayo inapatikana kwenye matamko haipo wazi katika mikataba na tangulizi imekosa nafasi zote za kisheria ukiacha kile kilichoelezewa ulazima wa kifalsafa. Kilichowazi ni kuwa hii inazingatiwa ni kuchanganya kati ya kadhia ya nafasi ya isheria kwa matamko yaliyokuja kwenye mikataba yote ya haki na tangulizi za katiba, na kadhia ya tafasiri ya matamko haya, je yenyewe yapo wazi au kuna hali ya kutofahamika? Yana ainisha wajibu wa kisheria au hapana?
55- Na kuna rai inayosema inapaswa kuanza kuweka mbali mikataba ya haki na katiba na tujaribu kuhukumu kwa kila moja kwa hukumu huru na hukumu zengine kwenye wigo wa asili ya kila mkataba na hali za wawekaji wake, kwani tangulizi za katiba na dibaji zake huwekwa na mwekaji wa katiba, na kuunda waraka mmoja na kufupisha watunga sheria, imani, falsafa na sheria za nchi na kuanzisha matamshi mengine ya kikatiba ynayotokana na muongozo wa sheria, hatufikirii kuwepo tofauti kati ya matamshi ya katiba na tangulizi zake, kisha hakuna sababu ya kutenganisha yeyote kati ya hizo na nyengine na kuipa nafasi sheria, kinyume na hivyo inazingatiwa ni uholela katika kanuni zisizo na sababu za msingi, hivyo basi maandiko ya katiba na utangulizi wake yanabeba nafasi ya maandiko ya kikatiba, na kuwa na ulazima, utangulizi unakutana katika kanuni za mikataba ya haki inayoungana na katiba kwenye mkataba mmoja.
56- Ama mikataba ya haki inayojitenga na katiba yenyewe ni mikataba inayotolewa na mamlaka za kikatiba, nayo mara nyingi inabeba asili ya fikra za kifalsafa, na nafasi kubwa wanayotaka wawekaji wake jamii yote kufuata muongozo wake kwa sababu wao kwa uhalisia hawakutegemea isipokuwa misingi ya jamii inayoongoza ndani ya kipindi hicho na kutokana na matarajio yake ya kishera ili kufika kwenye viwango vya maendeleo na ustawi, mikataba hii pamoja na kutokuwepo misingi maalum iliyo wazi yenye kufaa kulazimisha kisheria, yenyewe kihistoria na kifikra - kama ilivyotangulia ubainifu wake - haikuwa isipokuwa ni uhalali wa misingi yake na kufuatilia hatua zake, hivyo mikataba hii inazidi kuwa na nafasi yake kisheria nafasi ya maandiko au matamko ya kikatiba na pia hulazimisha mamlaka zote ndani ya nchi na hilo kwa maandiko yake maalumu au yasiyokuwa maalumu, kwa sababu kutenganisha ndani ya mkataba mmoja kati ya tamko moja na lengine ni kuleta kasoro kwenye misingi ya sheria ambazo hazitoi hukumu mbili tofauti kwenye maudhui mmoja, kwa hali hiyo inawezekana kwetu kushinda matamko yaliyowazi na yasiyowazi, hakuna haja kwetu ya kufahamu ni yepi maandiko ambayo yana misingi maalum ya kisheria na mengine ambayo yana misingi mikuu, kwa sababu maandiko hayo ni yenye nafasi kisheria na wajibu, na inaweazekana kuweka kanuni kwenye mahakama kuu za kikatiba ndani ya nchi ili kufahamu je moja ya mamlaka imekwenda kinyume kwa kuanzia na mamlaka ya kikatiba mpaka mamlaka ya chini ya kuandika mikataba na kukosekana kwanda kinyume( ).
57- Maelezo yaliyotangulia yanazingatiwa ni maandalizi muhimu yaliyo lazima ili kutoa mtazamo mpana unaotuwezesha kupitia mtazamo huo kufahamu nafasi ya kweli ya mtazamo wa haki za binadamu katika Uislamu, na kwa kiwango gani hutofautiana mtazamo wake kiustaarabu kiutu na Kisharia.
Na Mwenyzi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Chanzo: Kitengo cha tafiti za Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.

 

 

Share this:

Related Fatwas