Haki za Binadamu na Tatizo la Dhami...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu na Tatizo la Dhamira ya Kimagharibi

Question

 Je, inaweza kusemwa kwenye matatizo ya kimataifa ambayo Ubinadamu Uliyapitia katika miongo kadhaa iliyopita, kwamba lipo tatizo fulani katika dhamira ya kimagharibi.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Inaonekana kwamba dhamira ya Ulimwengu wa kimagharibi ni dhamira isiyonyoofu, na lazima ivuke katika mgogoro mkubwa ili irejee katia unyoofu wake, na kwa haraka athari ya tatizo hilo ikaondoka. Na dhamira hiyo inarejea katika hali iliyoumbiwa.
2- Tumejua kutokana na yaliyotanguliza kwenye kuongelea historia ya Azimio la Haki za Bindamu kwamba lilikuwa baada ya tatizo la vita vya pili vya Dunia. Na kwa hakika kama sio yale mamilioni ya watu wahanga wa vita hivyo vichafu dhamira ya Ulimwengu wa Kimagharibi isingelihisi kuwa hilo ni tatizo la kibinadamu, na mwanadamu ameangizwa chini ya mabavu ya utamaduni wa kimagharibi. Na utamaduni wa kimagharibi haukutosheka na damu ya wahanga wake wa Mataifa iliyoyatawala mpaka kumwaga damu ya wananchi wa Mataifa hayo, na ubinadamu umeipa kipaumbele thamani ya Azimio hilo ili kuuridhisha utamaduni huo unaotawaliwa, mpaka unalitangaza, na hadi unamkiri mwanadamu kwa utu wake, hata lau kidhahiri kwa tangazo haikuwa na hadhi ya undani (uhakika), na kwa uhakika wa mambo.
3- Matukio hayo ni mengi – na yanaumiza mno pia – matukio hayo ambayo yanatuzungumzia tatizo la dhamira ya wazungu, na kama lilivyo Azimio la Haki za Binadamu la Kimataifa – katika uhalisia wake – ni kama vile Azimio maalumu la Haki za Binadamu mweupe tu, na lazima watu wengine wazilinde Haki za Binadamu huyu mweupe, bila ya wao kuwa na haki zinazolindwa, na hii ni aina nyingine ya kutawaliwa.
4- Na wakati wa kwamba uhuru wa kisiasa ni mmoja miongoni mwa haki thabiti kwa mwanadamu mweupe, lakini aliubagua kutoka mwanadamu wa kiislamu katika nchi ya Aljeria, alipomchagulia aliyewakilisha katika uchaguzi wa mijini uliojulikana katika Aljeria, ambao serikali za kimagharibi –hasa Ufaransa ambao ulijifanya kulinda haki za binadmu kwa ujumla- zilifanya juhudi kuu ili kuzuia waliochaguliwa na watu wao kutenda majukumu yao, na uingizaji wa watu wa magharibi ulielekea vita vya watu vinavyofanywa leo katika nchi hiyo ya Kiislamu.
5- Na wakati wananchi wa Afghanistan na wananchi wote wa Iraq; wazee, watoto na wanyonge wake, wanaadhibiwa kwa sababu ya kwamba hawakutekeleza Maazimio ya Umoja wa Mataifa, Israel inaachwa ikiwa huru na haikulazimika kutekeleza azimio lolote lile miongoni mwa maazimio ya umoja wa Mataifa.
6- Na tatizo la majaribio ya nuklia ya Kihindi na Kipakistan ambalo yanaendelea muda ndefu, linadhahirisha kwa undani kwa tatizo la dhamiri ya kimagharibi na yanafedheheka uwili wa vigezo.
7- Masilahi ya kiuchumi ya mwananchi wa kimagharibi yanasababisha kusahaulika kwa Haki za Binadamu wengine, na wakati ambao makundi ya kutetea haki za wanyama katika nchi za Magharibi yanafanya maandamano ili kulinda wanyama wa majaribio ya kimaabara kutokana na hatari wanazozipata katika maabara mbalimbali za mashirika ya madawa. Na mashirika hayo yenyewe yanalazimika kufanya majaribio yake kwa wanadamu katika Nchi za Ulimwengu wa tatu, na makundi hayo hayo ya kulinda haki za wanyama, hayaangalii kamwe wala kuzijali haki za mwanadamu wa Ulimwengu huo wa tatu, kwani mwanadamu na wanyama wa Ulimwengu wa kwanza hawana tatizo.
8- Na wakati zikifanyika kampeni pana Nchini Marekani dhidi ya uvutaji wa sigara, jambo ambalo linayasababishia hasara kubwa mashirika yanayotengeneza sigara, na kwa ajili ya kutosimamisha kilimo cha tumbaku -na hilo ni miongoni mwa Mazao makuu ya kibiashara Nchini Marekani – misafara hiyo haiangalii masharti ya viwango vya (asilimia) vya Nikotini na kemikali katika tumbaku inayosafirishwa kuzielekea nchi zisizo za Magharibi.
9- Na pamoja na hayo, Marekani inatumia Haki za Binadamu kama silaha ya kuzibana nchi ambazo haziungi mkono Marekani. Na kama tulivyotaja katika maudhui iliyotangulia, kwamba Haki za Binadamu ni zana moja miongoni mwa zana mbalimbali za kivita baina ya Mataifa na siyo kwa ajili ya wahanga wa kweli. Na katika ziara ya Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton Nchini Uchina mwisho wa mwezi wa Juni mwaka wa elfu moja mia tisa, tisini na nane, waraka wa Haki za Binadamu ulikuwa mmoja miongoni mwa nyaraka muhimu ambazo Clinton alitumia kwa ajili ya mashinikizo mbalimbali juu ya serikali ya Uchina, na lengo lililotangazwa katika ziara hiyo ni kujadiliana kuhusu Haki za Binadamu, na kuanzisha ushirikiano wa kimkakati baina ya nchi zote mbili. Na Rais wa Marekani alitangaza kwamba majadiliano yake na Uchina na siyo Kushinikiza, ndio njia pekee itakayoleta athari juu ya suala la Haki za Binadamu.
10- Na jambo lichekeshalo kwamba serikali ya Uchina iliwakamata wachina kadhaa miongoni mwa waliopingana na serekali hiyo kabla ya ziara ya Rais wa Marekani, jambo ambalo lilisababisha maandamano rasmi ya Kimarekani yenye lahaja kali, na pamoja na hayo; Raisi wa Marekani alisema: "Hakika kukamatwa kwa Wachina watatu miongoni mwa wapinzani wakubwa wa kisiasa wanaotaka kujitenga, kulimsumbua sana yeye, … kisha akasema: hakika suala la Haki za Binadamu Nchini Uchina na kuwakamatwa wapinzani hakutageuza msimamo wa Sera za Washington". Na Rais wa Marekani akatangaza kwamba atamwomba Mwenzake wa Uchina atoe uhuru zaidi wa kujieleza Nchini mwake, na pia Rais wa Marekani alitoa wito wa Uhuru zaidi wa Kidini Nchini Uchina. Na pamoja na maneno ya kujipamba na kusifu, maraisi wawili wa Marekani na wa Uchina, waligongana katika mkutano wa wazi na waandishi wa habari kuhusu suala la Haki za Binadamu, mkutano huo ulitazamwa na mamilioni ya watu wa Uchina na sehemu nyingine Ulimwenguni.
11- Na kundi la Wapigania Haki za Binadamu katika Jimbo la Hong Kong la Uchina lilimwalika Rais wa Marekani kuzuru kambi za kazi za Kichina, ili kuiangalia rekodi mbaya ya Haki za Binadamu Nchini Uchina, kama lilivyosema kundi hilo. Na Bill Clinton alikabiliana na shutuma kali mno kuhusu kuzilinda kwake Haki za Binadamu Nchini Uchina, ambapo wasomi wa Uchina waliokutana naye walimkosoa vikali wakisema: "Hakika haiwezekani kuilazimisha Uchina, dhana ya kimagharibi ya Haki za Binadamu". Na Rais wa Marekani akautetea msimamo wake akisema: "Hakika vyovyote ziwavyo tofauti kuhusu dhana ya Haki za Binadamu, kuongeza zaidi uhuru wa kujieleza na Uhuru wa Dini kinaifanya Nchi iwe na nguvu zaidi kwa muda mrefu" .
12- Na kwa upande mwingine, Marekani ilitangaza mwishoni mwa mwezi wa Juni, mwaka wa elfu moja mia tisa, tisini na tisa, kumteua afisa anayehusika na Uhuru wa Kidini Ulimwenguni, cheo ambacho hakijawahi kusikika hapo kabla katika zama zozote. Afisa huyo ana jukumu la kufuatilia Unyanyasaji wa Kidini Ulimwenguni. Na kwa hakika suala hili halikuwa isipokuwa ni moja ya mlolongo wa matukio yaliyoanzishwa na Marekani kwa jina la Uhuru wa Kidini Ulimwenguni, ambao unazingatiwa ni sehemu ya Haki za Binadamu zilizoanzishwa na Marekani katika zama zilizopita.
13- Pengine Marekani ilianza kuchora picha mpya ya uhusiano wake pamoja na Mataifa mbalimbali kwa kuanza na silaha mpya inayompa umaarufu katika uso wa wasioitumia au wasioiunga mkono, silaha hiyo ni Haki za Binadamu na Uhuru wa Kidini (uhuru wa wakristo Ulimwenguni na uhuru wa Kuhubiri). Kwa hiyo, Marekani inazitumia Haki za Binadamu kama silaha ya kupitisha maamuzi ya kisiasa katika Tawala za Nchi mbalimbali Duniani na kuingilia chaguzi zake za Kisiasa, na inajipa ruhusa ya kuangalia hayo na kupingana nayo na kujiingiza kwa hoja ya kulinda Haki za Binadamu. Na pia Marekani sasa inatoa silaha mpya nayo ni kulinda Uhuru wa Kidini ili kujiwezesha kwa silaha hiyo kuingia katika maisha ya Kijamii ya Mataifa hayo.
14- Na hatukuusikia upinzani wowote wa Marekani dhidi ya mateso makali yanayowaumiza vibaya Waislamu wachache katika nchi mbalimbali Ulimwenguni. Bali mtu yeyote anayefuatilia matukio atagundua mchango mbaya wa majeshi ya Kimataifa katika kuwaandaa Waseribia kufanya mashambulizi makali zaidi dhidi ya Waislamu wakati wa matukio ya Bosnia. Na lilipoisha tatizo la Bosnia, Waserbia walielekea mkoa wa Waislamu wa Kusovo, ili kukirejea tena kisa cha matukio hayo. Jambo ambalo linadhihirisha wazi tatizo la Dhamira ya Kimagharibi, na kukumbwa kwake na maradhi ya kudhulumu, na Undumilakuwili.
15- Na matukio ya hivi karibuni katika sehemu mbalimbali Duniani yanashuhudia tatizo la Dhamira ya Kimagharibi, na kwenye shambulio kali la Kiyahudi dhidi ya Ghaza, meli ya kijeshi ya nchi za kimagharibi huangalia pwani ya Ghaza, siyo kwa ajili ya kumzuia mshambuliaji na kuwalinda wanyonge, bali kwa ajili ya kuzuia majaribio yoyote ya kuwasaidia wanyonge katika Ghaza, na kuzuia kupitishwa misaada yoyote ya kibinadamu au ya kijeshi kuwasaidia katika kukabiliana na mashambulizi, wakati ambapo hawakuzuia misaada yoyote ya kijeshi kwa lengo la kuimarisha Uyahudi. Mambo hayo yote yanadhihirisha wazi tatizo la Dhamira ya Kimgharibi, jinsi inavyoshughulikia Haki za Biadamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Marejeo: Kituo cha Tafiti za Kisheria katika Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas