Haki za Binadamu na Utendaji wake Kazi katika Ustaarabu wa Kimagharibi
Question
Ni zipi pande za Kimagharibi katika maudhui ya haki za binadamu, na mvutano wa madhehebu ya kifikra ya Kimagharibi pamoja na uhusiano wake na utawala wa nchi na mvutano wa Kimataifa?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Inawezekana kuzungumzia haya kupitia vipengele vifuatavyo:
Kipengele cha kwanza: Mvutano wa madhehebu na haki za binadamu.
Kipengele cha pili: Uongozi wa nchi na haki za binadamu.
Kipengele cha tatu: Mvutano wa Kimataifa na haki za binadamu.
******
Kipengele cha Kwanza: Mvutano wa madhehebu na haki za binadamu.
1- Makubaliano ya haki katika hatua hii yalipatwa na ukosoaji mkubwa wa watu wanaohusika na masuala ya haki kuwa yanatumika vibaya katika upeo wake na uchache wa umuhimu wake katika mahitaji ya makundi mbalimbali, katika ubaya wake ni kuwa haki hizi zinasisitiza ukombozi wa vitu vingi katika msisitizo wake wa kutoa uhuru, tuhuma hizi za mwisho zinaakisi hisia kuwa uhuru wa kuongea na kuulinda ya ukamataji wa kiholela ni majonzi kwa watu walionyimwa fursa ya kupata maisha yao na kujiendeleza kwenye mifumo ya maisha hayo( ).
2- Kwa vile haki za binadamu kwa sura yake ya Kimagharibi ni kiini cha madhehebu binafsi ambapo baadhi huzingatia kuwa Azimio la Haki za Binadamu la mwaka 1789 “Ndani ya mapinduzi ya Ufaransa” lilikuwa mazingatio kamili ya madhehebu binafsi( ). Madhehebu haya chini ya mminyo wa mivutano ya ujamaa, matatizo ya kiuchumi, uovu wa ukiritimba, na mafanikio ya mapinduzi ya Kirusi mwishoni mwa mwaka 1917, yalipelekea baadhi kulingania kuwa wajibu wa nchi ni pamoja na kuwaandalia watu njia za kutekeleza hizo haki, na hilo ni kwa kuanzisha na kupangilia maeneo ya Umma yatakayosimamia ufikiwaji wa lengo hili, bali watu kuwa na haki ya kuitaka serikali ifanye hivyo, kwa maana ya wajibu wa nchi kuboreka baada ya kuwa kuzorota.
3- Hapa inatuwezesha kuelezea yaliyomo kwenye makubaliano hayo kuwa ni haki kwa maana sahihi, na wala siyo ibara ya ruhusa tu isiyompa mtu haki isipokuwa ni kwa kufanya kazi, au kumzuia kufanya kitu na nchi wala haipaswi isipokuwa ni kutomkwamisha mtu kutekeleza hizo haki. Mwelekeo huu ulionekana kwa sura ya wazi kwenye katiba za nchi za Ulaya ndani ya kipindi ambacho vita ya kwanza ya dunia ilifikia mwisho wake “Katiba ya Kidemokrasia ya Weimar ya mwaka 1919 nchini Ujerumani, na Katiba ya Jamhuri ya Uhispania ya mwaka 1931”.
4- Vilevile imeonekana ndani ya katiba nyingi za Ulaya ambazo zilitengenezwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia kama utangulizi wa katiba ya mwaka 1946 nchini Ufaransa. Vilevile tunakuta andiko kwenye haki hizo ndani ya katiba ya Jamhuri ya India( ).
Tunakuta zuio hilo ambalo tumelielezea katika kauli za baadhi kuwa Azimio la Haki za Binadamu halikuwa isipokuwa ni kielelezo cha jamii, au tabaka la wanafikra ndani ya jamii kwa lugha ya jamii nzima kuhusu sura ambayo inayofikiriwa na jamii kwa masilahi ya pamoja, au ya jamii au ya Umma, na wala matangazo haya hayakuwa kwa mtazamo wa katiba ili kuwa na thamani, kwa sababu ya kubadilika upande wa fikra ya jamii kuhusu mafanikio ya pamoja( ).
Katika Nchi za Magharibi, Haki za binadamu hubadilika kwa kubadilika fikra ya jamii, na siku zote haki hizi huwa zinafikiwa na mabadiliko kwa kubadilika hali ya kisiasa kama ilivyotokea kushindwa kufanya kazi haki za binadamu huko Magharibi hasa nchini Marekani mwishoni mwa matukio maarufu ya mwezi wa September, lakini haki za binadamu haziko hivyo katika Uislamu, ambapo haki hizo sio zawadi kutoka kwenye mfumo wa kisiasa au Taasisi ya Kimataifa au kamati ya kisheria, bali zenyewe zimethibiti na ni za kudumu kwa kudumu Sharia ya Kiislamu.
Je! haki na uhuru wa zamani vimepoteza thamani yake?
5- Pamoja na mabadiliko yaliyotokea kwenye orodha ya haki na uhuru wa mwanadamu kama tulivyoonesha, haki na uhuru wa mtu bado vimeendelea kuilinda thamani yake na kila mtu kupata matumaini wanapofanya jaribio la maisha katika wigo wa utawala wa pamoja, kukosekana kwa uhuru kunatufanya tuyakadirie yale tunayoyachukua kwenye kadhia ya Mwislamu kwa kuwa yapo kwenye umiliki wetu. Maisha katika hali ya vurugu za makundi mbalimbali huwa yanafundisha upya watu umuhimu wa msingi wa uhuru wa mtu, hasa hasa msingi wa uhuru wa mtu uliowekwa kwa maana ile ya kwanza nayo ni ukombozi wa kukamatwa kamatwa kiholela.
6- Miongoni mwa mambo yenye kuonesha kuwa katiba imeondoa orodha nyingi ambazo zilipangiliwa na katiba ya Weimar ya Kijerumani mwaka 1919 ikiwa ni pamoja na haki za kiuchumi na kijamii, wakati ambapo imeonesha tena maelezo ya haki za asili( ). Tofauti ni kuwa yametokea mabadiliko mapya katika masuala ya uhuru wa zamani katika jamii za sasa, mfano wa haki ya Watu ya kupinga kuwa wahanga wa kampeni na matangazo, na uhuru wa kusafiri ulimwengu mzima, siyo ndani ya mipaka ya nchi tu, vilevile mtu kulinda uchavuzi wa mazingira, pia kelele za hovyo, haya yanatukumbusha tatizo lililoibuka kati ya Marekani kwa upande mmoja na Uingereza pamoja na Ufaransa kwa upande mwingine, ambapo mamlaka za ndani za Jiji la Washington zilizuia ndege kubwa za Concord kutua kwenye uwanja wa ndani wa Jiji ambazo Uingereza na Ufaransa zilishirikiana kuzitengeneza. Lengo la Marekani lilikuwa ni kulinda wananchi kutokana na uwingi wa kelele zinazotokana na ndege hizo, kuzuia huko kulikaribia kutishia kuibuka matatizo makubwa kati ya pande hizo.
7- Maana ya hayo ni kuwa maeneo muhimu ya haki za msingi bado ni maeneo ya sheria za zamani zinazofahamika kwenye maeneo ya haki, kutokana na sheria hizi imethibiti mipaka muhimu ya uhuru, na zaidi ya hivyo kumekuwa na daraja kati ya madhehebu huru “Liberally” na Demokrasia, kwa sababu Demokrasia sahihi kwa maana ya hukumu na utawala wa raia inakuwa ni pigo pindi unapokosekana usimamizi wa baadhi ya haki za kiraia na kisiasa, kama vile haki ya kupiga kura, kuzungumza, kukusanyika, vyombo vya habari, kutokamatwa watu kiholela ... n.k. ( ).
8- Vyovyote itakavyo semwa kwenye umuhumu wa haki za kijadi za binadamu zenyewe zipo chini ya mminyo wa harakati za kimakundi, na mminyo wa msimamo wa Kimataifa umeanza kubana kwa kiasi kikubwa zaidi ya hapo mwanzo, maazimio ya haki yamepanuliwa na kuwa kwenye muundo unaokubalika kati ya upingaji wa “Haki za Binadamu” na ulinzi jumla wa utetezi wa mifumo.
9- Juhudi hizi zimeonesha wazi kuwa fikra ya kikatiba ya sasa imeliathiri jaribio chungu ambalo Demokrasia imepitia kati ya Vita viwili Vikuu vya Dunia, vilevile maazimio haya yamepanua kipimo kinachozuia haki za binadamu ikiwa utekelezaji wake unatishia kupindua mfumo wenyewe ambao unazilinda hizo haki( ). Kwa hali hiyo, Demokrasia ya leo haijitoshelezi katika kukemea na kuadhibu vitendo vinavyoonekana sio vya kisheria ambavyo vinahusika na kushambulia mifumo ya nchi, bali yenyewe huadhibu mfungamano wa mitazamo ambayo inaona kuwa yenyewe inapingana na mfumo wa kijamii na kisiasa, kama vile vitendo vya fujo na ujamaa kwa hoja kuwa mpango wake wa kisiasa si halali, kwa sababu hiyo, ni lazima kuvisimamisha katika maeneo yake ya kinadharia( ).
10- Tunakuta kuwa pamoja na dhamana rasmi zilizopo kwenye haki nchini Marekani kwa baadhi ya watu, na wengine kuwekwa jela kwa hoja iliyosemwa kuwa wao wanatetea misingi, na wala sio kwa sababu ya vitendo maalumu walivyovifanya, hakuna shaka kuwa kulinda haki za watu katika wigo wa mminyo kama huu hakuhitaji udhibiti binafsi wa serikali mbali mbali, na kwa mujibu wa muamko wa siku zote wa wananchi( ).
Kipengele cha Pili: Uongozi wa nchi na haki za binadamu.
11- Asili yake ni kuwa kila nchi ni yenye mamlaka huru ya kuteua falsafa ya kijamii na kisiasa ambayo itatathmini mifumo ya utawala. Na yenyewe ina haki ya kufanya marekebisho ya falsafa hii na mifumo hiyo wakati wowote itakapotaka maadamu tu inaheshimu wajibu wa Kimataifa, kwa maana kila nchi ina mamlaka kamili ndani ya mipaka yake. Ukweli huu ni wa mwanzo usio kuwa na shaka yoyote katika ulimwengu wetu wa leo, kwa sura kwamba jamii ya Kimataifa kwa muda mrefu haikuwa mbali na haikuwa ikifanya hivyo.
12- Miongoni mwa malengo muhimu ya Muungano kati ya Australia Belarusia na Urusi katika theluthi ya kwanza ya karne ya kumi na tisa yalikuwa ni kuingilia kati masuala ya nchi zingine za Ulaya kwa lengo la kukandamiza mapinduzi, na kulinda mfumo wa Kifalme, nao ni mfumo unaoongoza ndani ya wakati huo, uingiliaji huu ulipata maamuzi ya wazi katika mkutano ambao ulifanyika kwenye Mji wa Turbo mwezi Novemba mwaka 1820, mkutano ambao yalifikiwa maamuzi ya wazi ya kutumia Muungano ili kupambana na mapinduzi sehemu zote, tamko lake lilikuwa: “Hakika nchi ambazo serikali zake zitabadilika kutokana na mapinduzi basi hizo zitaondoshwa kwenye jamii ya Ulaya, na kubakia hivyo hivyo mpaka zilete dhamana za kurudisha mfumo wake, ikiwa mabadiliko haya yataleta hatari inayotishia amani ya Mataifa mengine basi nchi zitachukuwa na kutumia njia zote salama na za kutumia nguvu ikiwa hali italazimu kufanya hivyo ili kurejesha usalama sehemu yake, na Mataifa yaliyopasuka kuyarejesha kwenye undugu”.
13- Uingereza ilipinga maamuzi haya kwa sababu yanapingana na uhuru wa Mataifa, na kugusa uhuru wa kila nchi wa mambo yake ya ndani isipokuwa hata hivyo ulikuwa ni upingaji usio na matokeo yoyote( ). Bali baadhi ya Waandishi walikosa uhuru wa moja kwa moja ulioachwa kwa kila nchi kuteua mfumo wake wa kikatiba na kuunda serikali yake, ambapo uhuru huo ungepelekea serikali kandamizi kusimama dhidi ya wananchi wake. Mwalimu Sambaliy Muitaly, alisema kwamba kila nchi iachwe huru katika mambo ya kikatiba, na kutambua kila serikali vyovyote itakavyoundwa na kwa misingi yake yoyote ile maadamu tu itatekeleza wajibu wake wa Kimataifa. Msingi huu wakati mwingine unaweza kufikia Kiwango cha uhalifu dhidi ya binadamu( ).
14- Ni wazi kuwa hivi sasa mtazamo wa Umma wa Kimataifa hauridhishwi na kuundwa dola isiyotegemea kuungwa mkono na wananchi, au msingi wake ni nguvu tofauti na nchi zisizofanya hivyo kwa kufanya kitendo chochote kizuri kinachoelezea kutoridhika kwao, na zinaishia kutoitambua nchi yenye kufanya hivyo, nacho sio kitendo kizuri chenye matokeo yoyote kwa upande wa kifasihi na kimaana( ). Ndani ya nusu ya kwanza ya karne hii Jamii ya Kimataifa imekutana na vita viwili vya kuangamiza vilivyouzindua ulimwengu kupitia athari zake kuwa ni lazima kwa uchache pawepo kauli moja ya Jamii ya Kimataifa, lakini kwa kuwa na misingi thabiti yenye nguvu, ndipo yalipofikiwa Makubaliano ya Francisco mwaka 1945, ambayo yalipelekea kuzaliwa kwa Shirikisho la Mataifa.
15- Makubaliano ya Kimataifa yalitoa kipaumbele maalumu kwa haki za binadamu mpaka tume ya utafiti wa haki za binadamu ikaanzisha katika kikao chake cha kawaida cha mwaka wa 1946, na kudhaminiwa na waraka wa Makubaliano ya Kimataifa, na ndipo lilipotolewa Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu mwaka wa 1948. Tofauti ni kuwa kanuni za Azimio hili hazikupata sifa ya uwajibibishaji ambapo mpaka hivi sasa hazijawa msingi wa Sheria za Kimataifa, Azimio hili halijaacha kuwa ni wasia uliotolewa na Kamati Kuu ya Umoja wa Mataifa ukiyataka Mataifa wanachama kufuata kanuni ambazo zimekusanywa kwenye Azimio hilo. Na Azimio kwa sifa hii ni waraka hatari wenye nafasi yake kisiasa isiyowezekana kupingwa, lakini kanuni zake haziwajibishi isipokuwa ni baada ya kufikiwa makubaliano kati ya Mataifa na kuyapitisha makubaliano hayo, kwa hatua hiyo kanuni hizo zitakuwa na nguvu za msingi wa kikanuni ambazo zitafaa kutumika dhidi ya nchi pale itakapoenda kinyume( ).
16- Jambo la kutajwa ni kuwa wakati wa mjadala wa Kamati Kuu wa Azimio la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, kulitokea makundi mawili, ambapo kundi moja lililoongozwa na mjumbe wa Ufaransa lilisema kuwa kanuni za ruhusa zina thamani halisi na ya kweli, kwa sababu zinazingatiwa ni tafasiri ya kanuni za waraka wa Makubaliano ya Umoja wa Mataifa, nazo zinaweka masharti kwa nchi katika wigo wa sheria za ndani ambazo zinatolewa, kama vile alivyosema mjumbe wa Chile kuwa kwenda kinyume na ruhusa hii kunazingatiwa katika kiuhalisia kwamba ni kwenda kinyume na waraka wa Umoja wa Mataifa.
17- Na kundi la pili likasema kuwa ruhusa iliyopo inazingatiwa kwamba ni kwenda kinyume na msingi wa utawala huru wa nchi, na ni ukiukaji wa kanuni zilizopo kwenye waraka wa kipengele cha pili katika sehemu yake ya saba ambayo inaelezea sifa za Umoja wa Mataifa kwenye masuala ambayo yanaingia katika ujenzi wa mamlaka za ndani kwa kila nchi.
18- Kundi hili liliongozwa na mjumbe wa Umoja wa Soviet “Urusi ya sasa” na mjumbe wa nchi za Muungano za Mashariki. Tunafupisha kauli za wajumbe hawa kuwa ruhusa haijataja haki za msingi za nchi, nazo ni haki zinazotokana na haki ya utawala, na haki ya utawala si katika haki za pembeni bali ni sharti la kimaudhui miongoni mwa masharti ya ushirikiano wa Kimataifa.
19- Nchi hizi za mwisho kuzitaja, Umoja wa Kisovieti na nchi zingine za Kijamaa zilijizuia kuvipigia kura vipengele vya Azimio, pamoja na kwamba baadaye zilikuja kukubali makubaliano mawili maalumu ya haki za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kijamii, ambapo mwana ujamaa wa Mashariki aliutafsiri wito wa haki za binadamu, ambao nao ni wito wa Kimagharibi kwa hatua ya kwanza, uliosimama kwenye falsafa ya Kiliberali kuwa ni jaribio la kupiga vita mifumo yake na kudondosha jengo lake kwa sura isiyokuwa ya moja kwa moja.
20- Nchi za Ulaya zikaongeza sifa ya kisheria kwenye kanuni za Haki za Binadamu kwa kukutana nchi kumi na tano kati ya nchi wanachama wa Baraza la Ulaya tarehe 5 Novemba mwaka 1950, na kuunda rasimu ya makubaliano ya Ulaya ya kutetea haki za binadamu na misingi ya uhuru, na ikafuatiwa na uanzishwaji wa Mahakama ya Ulaya ya haki za binadamu, na kuzifanya kanuni zake ziwe na sifa ya ulazima wa kutekelezwa na pande zote za makubaliano( ).
21- Ikiwa haki za binadamu na uhuru wake zimekuja kutoka kwenye wigo wa utawala wa ndani kwa upande wa nchi za Ulaya, pande za makubaliano zilizoashiriwa, kazi ilifanyika kwenye Matawi ya Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia haki hizo na uhuru ni masuala yanayotoka kwenye wigo maalumu wa ndani ya nchi, na yana muundo wa Kimataifa unaoingia kwenye umaalumu wa Umoja wa Mataifa, masuala yanayofungamana na kuheshimu haki hizi yalijadiliwa, na kukataliwa kwa nguvu zote ambazo ziliibuka katika suala la kutohusishwa Umoja wa Mataifa kuutafiti msingi wa kufungamana kwake na mamlaka za ndani za kila nchi.
22- Miongoni mwa matatizo muhimu ni pamoja na “Mashirikiano na wananchi wa umoja wa Afrika ya Kusini wenye asili ya India, ambapo suala hilo lilifikishwa kuanzia tarehe 22 June 1946, na kuheshimu haki za binadamu kwa nchi za Bulgharia, Hangari na Romania ambapo zilifikishwa kuanzia mwezi March 1946 ... n.k.”( ). Na vyovyote itakavyokuwa sisi tunaamini kuwa nchi ambazo zilikubali makubaliano ya Umoja wa Mataifa zinapaswa kuheshimu Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu, na kulazimika kulitekeleza hata kama hazijalipigia kura, na hilo ni kuwa waraka wake unajengeka kwa matamko yanayoonesha ulazima kwa upande wa hizo haki na uhuru na hasa kwenye kipengele cha “55, 56” cha waraka( ). Na nchi za mwanzo ni zile ambazo ziliukubali waraka huo na kulikubali pia Tangazo la Kimataifa( ).
Kipengele cha Tatu: Mvutano wa Kimataifa na Haki za Binadamu.
23- Pamoja na kwamba Shirikisho la Umoja wa Mataifa limenga maudhui za haki za binadamu na uhuru wake katika mambo maalumu ya ndani ya nchi, na muundo wake wa Kimataifa pamoja na jaribio la kuutetea, haki za binadamu zinavunjwa, bali zinaporwa kwa nguvu kwenye nchi nyingi duniani, kama si nchi zote, pamoja na kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa, hata kama kutakuwa na tofauti ya ukiukaji na kiwango chake, ikiwa tutaacha yale yaliyokuwa yakitokea katika zile nchi zilizokuwa zinaitwa nchi za ujamaa ambazo zilikuwa haziangalii haki za binadamu, shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Binadamu ambalo makao yake makuu yalikuwa mji mkuu wa Uingereza, liliashiria katika ripoti zake kuwa nchi nyingi zisizo za ujamaa eneo la Marekani ya Kusini Asia na Afrika zimekuwa zikiendesha vitendo vya unyanyasaji wa kisiasa, na kuwaadhibu wapinzani. Shirika hilo linakadiria kuwa kuna zaidi ya wafungwa elfu thelathini wa kisiasa ndani ya nchi za Chile, Argentina, Brazili na Urugwai. Ripoti hiyo imesisitiza kuwa nchi zenye ukiukaji mbaya zaidi wa haki za binadamu ni Chile.
24- Ripoti hiyo ikathibitisha kuwa nchi ya Umoja wa Kisovieti zinavunja na kukiuka haki za binadamu kwa njia ya ukandamizaji wa rai za upinzani, wakati ambapo Marekani inavunja haki hizi kwa njia ya siasa za ubaguzi dhidi ya Wamerikani weusi na Wahindi wekundu( ). Jambo la ajabu ni kuwa baadhi ya nchi ambazo zilikuwa zina hamasa kubwa wakati wa kujadili Azimio la Kimataifa la haki mwaka 1948 kwenye Kamati Kuu ya Umoja wa Mataifa, na kusema kuwa kwenda kinyume na Azimio hilo ni kukiuka Makubaliano ya Kimataifa, ni nchi ya Chile kwa kauli ya aliyekuwa mjumbe wa nchi hiyo, ndani ya mwaka huo huo, ambapo mjumbe huyo wa Chile alilifikisha tatizo la nchi ya Umoja wa Jamhuri ya Kikomonisti ya Sovieti kwenye Jumuiya Kuu ili kujadiliwa, nchi hii ndio iliyotuhumiwa na Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu, mwaka 1977 kuwa ni nchi yenye Kiwango cha juu zaidi cha vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu( ).
MAKUBALIANO YA HELSINKI YA MWAKA 1975:
25- Kuelekea kwenye hali hii yenye kuzorotesha haki za binadamu na ukiukaji wa wazi wa uhuru wa binadamu, nchi 35 zilikutana huko Helsinki mwezi wa Agosti 1975, nazo ni nchi zote za Ulaya za Kijamaa na za Kibepari na zile zisizofungamana na upande wowote, pamoja na Marekani na Canada( ) ambapo Suala la haki za binadamu lilikuwa na mambo matatu, ambayo Nchi hizo zilikubaliana kushirikiana zenyewe kwa zenyewe kwa wananchi wao na kuziheshimu, na kusimamiwa na “Maelezo ya Halsinki”, pembezoni mwa suala la usalama wa Ulaya na ushirikiano wa kiuchumi.
26- Haki za binadamu kwa maana ya kwanza ni uhuru wa mwananchi kuishi sehemu yoyote ndani ya nchi yake, na uhuru wa kusafari nje ya nchi yake, uhuru wa kujua, uhuru wa mtu kufikiri na kuhama kati ya nchi za Ulaya bila kujali mfumo wake wa kijamii. Kipengele cha haki za binadamu kiliendelea kuwa katika wino kwenye karatasi mpaka mwaka 1977 ambapo Rais wa Marekani Jimmy Carter alipolifanya suala la haki za binadamu kama jukumu lake la kwanza, na kipengele kikuu katika mpango wa siasa zake za nje, aliweza kuchukua hatua za utekelezaji kama Rais wa nchi kubwa yenye nguvu zaidi duniani, pia alitumia uwezo wa nchi yake katika kuliunga mkono suala hilo, na kulipa nguvu ngazi ya Ulimwengu, vilevile kusitisha misaada ya nje kwa nchi ambazo hazichungi haki za binadamu kama vile Argentina Uruguwai na Selvado, na kutopeleka silaha kwa baadhi ya nchi zingine kama vile Ethiopia.
27- Suala la haki za binadamu lilionekana kama suala nyeti Kimataifa, na hasa kati ya Nchi ya Umoja wa Soviet ambayo ilipata kukosolewa sana na Rais Carter, na hii ni kutokana na uovu mkubwa waliokuwa wanaufanya kwa mwananchi wa Kisoviet pamoja na kuzikiuka haki na uhuru wao, mpaka Suala hili likatishia pande mbalimbali za Kimataifa zilizopo kati ya Mashariki na Magharibi, na ikawa ni sababu iliyokaribia kupelekea kushindwa kwa mkutano wa maandalizi ambao ulifanyika huko Belgrade tarehe 15/06/1977, maandalizi ya mkutano wa pili wa nchi za Helsinki yaliendelea kwa muda wa wiki nane, ambao uliamuliwa kufanyika ndani ya tarehe 4 Oktoba, kwenye mkutano huo kulijadiliwa suala la haki za binadamu kati ya Marais wa nchi, baada ya suala hili kudhitiwa katika mkutano huo wa maandalizi ili kuepuka mpasuko kutokea kati ya nchi hizo ambazo zilipiga hatua kubwa katika mambo ya mashirikiano ya kijeshi na kiuchumi.
28- Mkutano ulifanyika ndani ya wakati wake, na kipengele cha haki za binadamu kiliibua hisia za kipaumbele cha kwanza wakati wa mjadala ambao uliendelea ndani ya mkutano huo, pamoja na kuchukuliwa tahadhari ya hali ya juu na nchi wakati wa mjadala wa jambo hilo kwa lengo la kuepuka kuibuka mgongano kati ya nchi za Magharibi, ambazo wakati huo zikiongozwa na Marekani na nchi za Kijamaa wakati huo zikiongozwa na Urusi jambo ambalo lingepelekea kufeli kwa mkutano huo. Katika maazimio ya mwisho ya mkutano huo, ni pamoja na kujiepusha na ishara yoyote ya suala ya binadamu kwa sababu za kutokubaliana kwenye mkutano huo, ndani ya mwezi Septemba katika mkutano wa maandalizi ya mkutano mkuu wa Madridi utakaofanyika tarehe 11 Novemba 1980, walikubaliana ndani ya kipindi hiki vifanyike vikao viwili kwa ngazi ya wataalamu, kikao cha kwanza: kijadili utatuzi wa matatizo ya Kimataifa kwa njia za amani huko Mentro nchini Uswisi siku ya tarehe 31 October 1978, na mkutano wa pili utafanyika Malta ili kujadili maudhui ya mazungumzo ya Ulaya na nchi za bahari nyeupe( ).
Sababu za kukiukwa kwa haki za binadamu:
29- Huenda sababu kuu ya Umoja wa Matiafa kutoheshimu haki za binadamu ni nchi kutokubaliana kubainisha na kuainisha ni nini haki za binadamu! Hata nchi ambazo zimekubaliana maana ya karibu ya haki za binadamu tunakuta kwamba bado zinatafautiana katika njia ya kuzishughulikia haki hizo zinazosababisha mzozo mkubwa. Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anarahisisha na kufupisha jambo hili kama alivyoonekana kwenye hotuba yake ambayo aliitoa wakati wa ziara yake ya nchi za Marekani ya Kusini kuwa yeye hapendi kumkasirisha mtu yeyote, pia hapendi kuingilia masuala ya ndani ya nchi yoyote ile, na hapendi kurudisha vita baridi kwa mara nyingine tena, lakini anaamini kuwa kila mwanadamu ulimwenguni kote anapenda kuelezea mtazamo wake kwa uhuru bila ya kuteswa na yeyote( ).
30- Ama Brezhnev Rais wa zamani wa Umoja wa Soviet, na Katibu wa kwanza wa chama cha Ujamaa cha Kisoviet walionesha mtazamo wao katika kampeni ya Marekani ya kuheshimu haki za binadamu na kujikita kwenye nchi za Kijamaa, katika hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa Umoja wa Vyama vya Wafanya kazi wa Kisoviet alisema kuwa: Serikali ya Rais Jimmy Carter inaingilia masuala ya ndani ya Umoja wa Soviet kupitia kampeni hizo, na kuwa haiwezekani kukuza mahusiano asili kati ya Moscow na Washington ikiwa Marekani itaendelea kuwaunga mkono wale wanaojitoa kwenye utawala wa Kisoviet, pamoja na wapinzani ndani ya nchi zingine za Kijamaa.
31- Rais Brezhnev aliwaashiria hawa wanaojitoa kwenye utawala wa Kisovieti na akasema: “Jamii ya Kisovieti inawapinga kwa sababu wanafanya juhudi na harakati za kudhoofisha jamii yetu ya kijamaa, na wanatafuta kuungwa mkono na nguvu za kikoloni, na kwa sababu hiyo, wananchi wa Kisovieti wanatoa wito kushirikiana na hawa wanaotaka kujitenga na utawala wa Kisovieti sawa na kushirikiana na mkoloni pamoja na wasaidizi wake kwa vile wanajitolea kufanya uhalifu dhidi ya wananchi” ( ).
32- Ikiwa nchi za kibepari za Magharibi zinamuunga mkono Rais wa Marekani Carter katika mkakati wake wa kutaka haki za binadamu ziheshimiwe isipokuwa zenyewe zilitofautiana katika njia ya kushughulikia haki hizo, kwa mfano Rais wa zamani wa Ufaransa Giscard d'Estaing alitangaza kupitia runinga ya taifa kuwa Ufaransa inaunga mkono uhuru wa haki za binadamu kama msingi, na vilevile inajitenga na uingiliaji kati wa masuala ya ndani ya nchi zingine kama msingi, pia Chancellor wa zamani wa Ujerumani ya Magharibi Helmut Schmidt alijiunga na msimamo huo, ambaye alipendelea zaidi diplomasia yenye utulivu kwa Rais wa Ufaransa, wala hakuwa na hofu wala wasiwasi kwenye njia anayotumia Rais wa Marekani katika kuiendea kadhia hii, na athari zake katika peo za Kimataifa ambazo wakati huo zilikuwa hazizidi na umri wa miaka miwili, lakini kwa upande mwingine Rais wa Italia wa wakati huo Andreotti naye aliungana na Rais Carter wa Marekani, vile vile Callahan Waziri Mkuu wa Uingireza wa wakati huo.
33- Serikali zilielezea pamoja na marais wa nchi za Magharibi ambao walikuja baada ya hapo na mpaka hivi sasa tukiwa ndani ya muongo wa kwanza wa karne ya ishirini na moja tunakuta kuwa waraka wa haki za binadamu kwa ufahamu wake na uelewa wake wa Kimagharibi hauna uwiano kisha utekelezaji wake ni mbaya zaidi kwa kutumia ukandamizaji wa kisiasa mifumo isiyokubaliana na Magharibi, pamoja na kuwa Marekani yenyewe inazingatiwa mvunjaji mkubwa wa haki hizi za binadamu, ambapo haki za binadamu zimekuwa zikuhusishwa na “Haki za binadamu wa Kimagharibi” tu, na kwa mtazamo wenye ubaguzi mkubwa zaidi, na mtazamo huo wa kibaguzi ulirudisha nyuma harakati za kimaendeleo kwa sababu ya ubaguzi wa Magharibi.
34- Tatizo hivi sasa linakaribia kujenga swali la zamani lifuatalo: Je haki za binadamu na uhuru wake ni masuala ya Kimataifa au ni uingiliaji wa wigo wa mamlaka za ndani ya kila nchi? Ikiwa Umoja wa Mataifa umejibu mfano wa swali kama hili tokea hapo zamani, na kuzingatia haki hizo na uhuru huo hata kabla ya kutokea kwa tangazo la Kimataifa la haki za binadamu mwaka 1948 kuwa mambo haya yapo nje ya maeneo ya mamlaka za nchi, mjumbe wa Marekani wa wakati huo ndugu Andruyoung alisema: Ni muhimu Marekani kusaidia wahanga wa ukiukaji wa haki za binadamu, kama vile ilivyokuwa ikisaidi wahanga wa matetemeko ya ardhi, hata kama hilo litapelekea kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi zingine mbali mbali…”.
35- Akaongeza kusema: “Pamoja na Marekani kujenga haki za binadamu kwa uwazi, hakutokuwa na changamoto kwa mamlaka za nchi ikiwa tutafanya mambo mazuri nyuma ya mipaka yake”( ). Lakini kuna maswali mengine lazima yajitokeze baada ya jibu la swali la kwanza, nalo ni je nyuma ya kampeni hii kubwa ndiyo kusudio? Kampeni ambayo hatuna shaka na umuhimu wake ni sawa sawa kwa muda mfupi au mrefu, na ilianza kwa vitendo kwenye nchi za ujamaa ambazo zilisaini mkataba wa Helsinki, na kuwataka wananchi wao kutekeleza vipengele vya makubaliano hayo, hasa kipengele cha uhuru wa kusafiri, pia makubaliano yeliyo hamasisha upinzani ndani ya nchi hizi, tunarudia tena kwenye swali ambalo: Je kusudio la kweli ni kulinda haki za binadamu au mchezo wa kuleta mvutano kati ya Mataifa…?
36- Sisi tunaamini kuwa kampeni inatafuta mambo mawili kwa pamoja, pamoja na mchezo wa mvutano ndio asili, na kulinda haki za binadamu ni tawi, au kwa maana nyingine mvutano ndio maudhui kuu, ama kutetea haki za binadamu ni ukinaishi, linabakia swali lingine je kwanza tumekubaliana juu ya uelewa ulioainishwa kwenye haki za binadamu? Na kwa muundo mmoja wa haki hizi?
37- Kinachoaminika ni kuwa sisi bado hatujafika, na wala hatutafika kwa kipindi kifupi kijacho, kwa sababu sisi bado hatujakubaliana juu ya maana moja ya “Uhuru” unaoelezewa kati ya wanafalsafa wa madhehebu ndani ya zama hizi, katika mambo yenye kuibua hisia ya kweli ni kuwa sisi tunamkuta yule mwenye kubeba bendera ya kulinda haki za binadamu leo hii ndiyo wale ambao wamerithi ustaarabu wa wana mapinduzi wa Mji wa Athena, nao ndio watu wa shule ya Sophists ambao walikuwa ndio watu wa kwanza kulingania haki asilia za binadamu, dhidi ya mfumo wa utawala wa kiimla, ambao ulikuwa ndio unaotawala huko Athena.
38- Tunakuta nchi za madhehebu binafsi zinaendesha kampeni hizi hii leo dhidi ya utawala mwingine wa kiimla katika Jamhuri ya Urusi ya Kisoviet kwa tofauti moja tu nayo ni tofauti ya miaka elfu mbili na mia tano, na historia siku zote ni yenye kujirudia( ).
39- Jambo la kutajwa ni kuwa makubaliano ya haki ambayo yalitolewa na Uingereza Marekani pamoja na Ufaransa kwa mfululizo kwa ukweli na kiuhalisia yanazingatiwa ni makubaliano ya kwanza kuruhusiwa rasmi kwa upande wa nchi fikra mbili ya haki asilia na haki ya makubaliano, yalianza hayo kwa uwazi kwenye makubaliano mawili ya Marekani na Ufaransa, ambayo makubaliano hayo ni zao asili la fikra hizi mbili.
40- Ikiwa fikra hizi mbili zimezungumziwa kwenye vitabu vya wanafalsafa na wanafikra, na wakakutana kwenye kuzielekea fikra hizo na ukaidi na mateso, kuruhusu fikra hizi kunazingatiwa ni ushindi sio kwa jitihada za hawa wanafikra, lakini ni kwa ajili ya jitihada za wananchi dhidi ya mamlaka, na kuzuia kupitwa na haki zao pamoja na uhuru wao.
41- Hakuna ubishi wala mjadala kuwa kujikita kwa makubaliano haya na hasa makubaliano ya Marekani na Ufaransa kama tulivyotaja kwenye haki ya uhai uhuru usawa kupambana na mateso holela…n.k. na kuyazingatia ni haki kwa kila binadamu isiyoweza kuachwa, kwa maana kuwa haiwezekani kwa mamlaka yoyote ile ni sawa sawa mamlaka inayoongozwa na Rais au inaoyoongozwa na Khalifa kuzuia haki hizi, au kuzichukuwa toka kwa mwenyewe, uzingatiaji huu ulikuwa unapelekea – ili haki hizi zisiwe ni ibara tu ya ulazima wa kinadharia – kutengenezwa katiba za nchi hizi ikiwa na vipengele vinavyoonesha uwepo wa haki hizi, na kutoa usimamizi na njia za kulinda hizi haki.
42- Ikawa katika njia hizi muhimu ni haki za wananchi katika kuisimamia serikali na kuiuliza kwa njia halali na zilizopangiliwa, pale kila serikali inapokiuka haki hizi au kwenda kinyume na vipengele vya katiba, au kuharibu haki za watu au kukwamisha uhuru wao, haikuchukuwa muda mrefu likatolewa Azimio la Kimataifa la Haki za binadamu mwaka 1948 ambalo lilipelekea haki hizi za binadamu kuwa ni haki zenye muundo wa Kimataifa, na wala sio muundo wa ndani kwa maana ya kupewa umuhimu na uzito na Jamii nzima ya Kimataifa.
43- Tumeelezea utendaji kazi wa haki za binadamu katika ustaarabu wa Kimagharibi, na kuibua mvutano unaozunguka kati ya makundi ya Imani na Madhehebu mbalimbali kwenye Suala hili, na matokeo yake vyovyote yatakavyokuwa ya mvutano huu lakini haki za binadamu ni za msingi. Miongoni mwa haki hizo ni pamoja na haki ya uhuru wa kujielezea, kukosoa, kusimamia serikali, kupambana na vitendo vya mateso holela, dhuluma, n.k. Haki zote hizi katika mtazamo wetu zimekuwa ni haki thabiti na kuambatana na binadamu kwa kumzingatia yeye kama ni binadamu, bila ya kuangalia mazingatio ya kijinsia, rangi au imani ya kisiasa ambayo inafuatwa na nchi ambayo huyo binadamu anaishi. Vilevile haki hizi zimekuwa ni haki za Kimataifa zinatokana – sawa na mwelekeo mkubwa wa sasa – na wigo wa utawala wa ndani ya nchi( ).
Chanzo: Kitengo cha Utafiti wa Kisharia ofisi ya Mufti wa Misri.