Haki za Binadamu na Nadharia ya Hak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu na Nadharia ya Haki katika Uislamu

Question

 Je, ipo Nadharia ya Kiislamu maalumu katika haki, inajengwa juu yake Nadharia ya Haki za Binadamu katika mawazo ya (Fikri ya) Kiislamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
4- Hakika Uislamu una Nadharia maalumu katika haki, unatokana na mtazamo wake wa kiujumla kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwanadamu, ulimwengu, na uhusiano baina ya mamabo hayo yote pamoja. Kwa hiyo, Haki za Binadamu hazikuwa isipokuwa ni katika mfululizo, na sehemu kutokana na mzunguko na mtazamo wa pekee au unaopunguza, nao unakaraha na chuki zaidi kuelekea mawazo wa Kiislamu, na mtazamo wa ujumla na wa undani ni kitu kinachopendeza zaidi kwake.
5- Ikiwa haki za Binadamu ni sehemu ya Nadharia ya Haki katika Uislamu, basi tunapaswa kusimama hata lau kwa ujumla katika Nadharia ya kweli katika Uislamu.
6- Na kwa ujumla kwamba haki ziko aina nne:
A- Haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake.
B- Haki ya kila mja kwa nafsi yake
C- Haki ya baadhi ya waja kwa wengineo
D- Haki ya wanyama juu ya waja (wanadamu).
7- Haki hizo zinagawika katika Faradhi ya Lazima (faradhi iliyofaradhishwa kwa kila mwanadamu), na Faradhi ya kutosheleza, (Faradhi ambayo ikitendwa na baadhi ya watu huondoka kwa watu wengine), na Sunna ya Lazima na Sunna ya kutosheleza, na miongoni mwa haki ni zile halisi za kiakhera: kama vile ufahamisho na Imani. Na miongoni mwake haki halisi za kidunia kama vile utashi wa vyakula, vinywaji, mavazi na ndoa. Na miongoni mwake ni haki za kiakhera kwa anaejitolea ya kidunia kwa wanaokubalikia, kama vile ihsani kwa kulipa halali au kuiwezeshea,
8- Na Nadharia ya Haki katika Uislamu huungana kitimamu na nadharia ya masilahi na maovu, basi kuleta masilahi na kutoa mbali kwa maovu –kwa upande wa kutaalakia kwake (kuhusiana kwake) haki- ni aina mbli;
Aina ya kwanza: ni yanayohusiana na haki ya Mwumbaji (Mkawini) kama vile Utii na Imani, na kuacha ukafiri na wasi.
Na aina ya pili: ni mambo yanayotaalakia (yanayohusiana) na haki za viumbe kutoka kuleta masilahi na kutoa mbali maovu.
9- Ama haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni sehemu tatu:
Ya Kwanza: Mambo yanayohusiana na Mwenyezi Mungu pekee; kama vile, maarifa, hali zinazojengewa juu yake na kuaminia kwa mambo yanalazimishwa kuyaaminia.
Ya Pili: mambo yanayoundana na haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waja wake kama vile; Zaka na Sadaka …, basi hayo ni kusogezea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa upande mmoja, na manufaa kwa waja wake kwa upande mwengine, na lengo dhairi zaidi ni manufaa ya waja wake, na kuwaongoza kwa mambo yaliyowajibika miongoni mwa hayo.
Ya Tatu: ni mambo yanayoundana na haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu na Haki za Mtume wake S.A.W. na haki za mtu mzima (mkalifiwa) na waja au yanayokusanya haki hizo tatu; kama vile Adhana ina haki tatu; ama haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kauli ya Allahu Akbar mara tatu, na kushahidia kwa Umoja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee, ama Haki ya Mtume S.A.W. ni kushahidia kwa Mtume S.A.W. kwa Ujumbe, na ama haki ya waja ni kuongoza kwa kuingia wakati wa Swala …
10- Ama Aina ya Pili: Mambo yanayohusiana na haki za viumbe, ya kuleta masilahi na kutoa mabali maovu, basi haki hizo ni sehemu tatu pia;
Sehemu ya Kwanza: Haki za mkalifiwa juu ya nafsi yake, kama vile kujipatia mavazi, makazi, matumizi na kadhalika haki zake katika kulala usingizi, na chakula cha Asubuhi na kuacha kwa kutisha.
Sehemu ta Pili: Haki za baadhi ya wakalifiwa juu ya wengine, na Udhibiti wake ni kuiletea kila masilahi wajibu au halali, na kutoa mbali kila ovu haramu, au lenye karaha. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka}. [AN NAHL 90], Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema pia: {Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!} [AZ ZALZALAH 8] Na hayo ni kuaripia (kukemea) kutoka kwa maovu yote, ya chache yake na ya mengi yake, kwani sababu zake ni miongoni mwa jumala ya mashari, na Qur'ani na Sunna zinakusanya mambo ya masilahi yote ndogo zake na kubwa zake, na kukana kutoka kwa maovu yote; madogo yake na makubwa yake.
11- Na haki za baadhi ya wakalifiwa juu ya wengine, ni maudhui ya Tangazo la Haki za Biadamu, basi haki za ujumla ambazo zilitaja chini ya sehemu hiyo, wakati wa Haki za Binadamu katika Uislamu haziambatani tu sehemu hiyo pekee.
12- Na haki za baadhi ya wakalifiwa juu ya wengine yana mifano mingi: miongoni mwake; Hukumu ya watawala, maimau na maliwali kwa insafu ya wadhalimiwa kutoka wadhalimu, na kupatikana haki kwa wenye haki walio vilema. Na miongoni mwake yaliyo ni wajibu juu ya mwanadamu toka haki za matendeano, na miongoni mwake kuamirisha kwa mema na kukataza uovu (munkari), na miongoni mwa mifano ya haki za baadhi ya wakalifiwa juu ya wengine ni mtajiri husamehe mdeni, na miongoni mwake kusalimia alipofika, kumzuru wagonjwa, na kusaidia katika ubora na ujamungu, na kusaidia katika kila jambo halali.
13- Haki za waja juu ya waja wengine ni aina mbili: Ya Kwanza; haki wakati wa maisha yao na Ya Pili; haki baada ya kifo chao. Na tunatanguliza mifano ya haki za waja katika maisha, ama mifano ya haki zao baada ya kifo. basi miongoni mwake ni: kuwakarimishia, kuwasambizia, kuwachukua, kuwakafinia, kuwazikia, na kuwaelekea Kibla, kusalia juu yao, na kuwaombea rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuwazuru na kuwaombea maghifera ….
Ya Tatu: Haki za wanyama juu ya mwanadamu; Mwanadamu analazimishwa kuwaharijia matumizi hata lau wanyama walikuwa wanyonge sana au wakiuma, na walikuwa hana manufaa, na hawahamilishii mizigo mkubwa zaidi ya uwezo wake, na hawakusanyii baina yake na wanyama wengine wanaowaudhia kwa kuvunja, au kuguta, au kujeruhia. Na walipowachinjia lazima achinjie vizuri, na hawapasuki ngozi yake, na hawavunji mifupa yake.
14- Na kwa upande mwengine; basi haki zote ni aina mbili: Ya Kwanza: Makusudio. Na Ya Pili: Njia, na kitendea cha njia, na haki hizo zote zimegawikia kwa zilizokuwa na sababu, na zisizokuwa na sababu, na mazungumzo katika tafiti za haki ni marefu mno, katika kugawika kwake kwa haki tofauti na haki sawa na zenye hitilafu, na katika kuzitanguliza baadhi ya haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na katika uwezo wa kuzitanguliza baadhi ya haki za wanadamu na nyinginezo.
15- Na inafuatana na kugawika haki kwa haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki ya mtu mmoja mmoja; utaofautisho baina yake katika athari, tunazikusanyia katika yafuatayo : Basi haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu hazijuzu kuzidondolewa ama haki za mtu mmoja mmoja basi mkalifiwa anaweza kuzidondosha kwani yeye ni mwenye haki ndani yake . Lakini ziko haki ziliwekwa kwa ajili ya masilahi hasa, na sababu ya hayo kwamba yawe haki kwa mtu mmoja mmoja, na ingawa ya hayo hazijuzu kuzidondosha, na hayo ni kama vile, uharamisho wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa riba na wizi ili kuhifadhi mali ya mwanadamu, na kuharamisha zinaa ili kuhifadhi nasaba yake, na kuaramishia kuwasingizia wanawake ili kuhifadhi uheshimu wake, na kuharamisha uaji na kujeruhi ili kuhifadhi nafsi yake na viungo vyake.
Na mja akiridhia kuifutia haki yake katika mambo hayo, basi ridhaa yake haizingatiwi na hazitekelezwi, kwa hiyo, haki hizo zitazingatiwa kutoka haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ama haki za kushirikia, basi haki ambazo mara nyingi hupindukia haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hazijuzu kuzidondoshea kama mfano haki ya kusingizia, na haki zinazohusiana na mwanadamu basi makalifiwa anaweza kuzifutia kama mfano haki ya kupiga kisasi.
16- Na katika upande wa urithi; basi haki ambazo zinahusiana na Mwenyezi Mungu Mtukufu au zile ambazo mara nyingi hupindukia haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hazirithishwi. Ama haki zinazohusiana na mwanadamu, baadhi yake zinarithiwa na baadhi yake hazirithiwi, na Imamu Al Qarafiy amewaka udhibiti kwa haki zinazorithiwa na haki zisizorithiwa miongoni mwa haki za wanadamu, basi alizingatia haki zinazorithiwa miongoni mwa haki ni ambazo zinahusiana na mali ambayo alirithia, au iliyomlindia madhara kwa kusahilishia (kuhafifisha) maumivu yake.
Ama haki ambazo zilikuwa zikihusiana na nafsi ya mrithishi, akili yake, matakwa yake, utashi wake basi mrithishwa harithi kitu cho chote.
17- Na kwa upande wa Kuzuia: Hakika Haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu au zile ambazo mara nyingi hupindukia haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Miliki ya Jamii zile zinazokuwa ndani yake zina mlango wa Kuamrisha Mema, Waziri Mhusika anatakiwa apambane nazo yeye mwenyewe, na Jamii inawajibika kwa mambo hayo kama anavyolazimika kila mtu, kama vile kuacha Kuswali Sala ya Ijumaa. Na zinazokuwa ndani yake katika mlango wa kukatazana maovu (mabaya), na zinazohusika na Ibada mbalimbali basi Waziri Muhusika, yeye binafsi anapaswa kuzikana na kumuadabisha mkaidi katika hizo kama hajasema alichokikosea Imamu anayefuatwa, na hivyo ni kama vile kukiuka kwa maumbo ya Ibada, ama zile zinazokuwa miongoni mwa Makatazo basi waziri mhusika lazima awazuiwe watu kwa ajili ya kuondosha hali za kutia shaka, na mambo ya kudhaniwa ambayo ni tuhuma, na kwa hivyo kwanza panatangulizwa kukana na wala hakuharakishwi kuadabisha kabla ya kukana. Ama kwa upande wa Miamala (matendeano) inayochukiza kama vile mauzo yaliyoharibika na pia riba, basi kila kilichoafikiwa kikatazwe na kuzuiwa basi Waziri Mhusika atalazimika kukikemea na kuzuia kisifanyike na kukanya pia.
18- Ama kwa upande wa Haki za mtu mmoja mmoja, na kinachohusika na Kuamrisha mema, basi kinachokuwa cha wote kama vile, nchi iwapo mfumo wake wa maji utaharibika au uzio wake ulibomolewa basi Waziri Mhusika ana jukumu la kurekebisha kilichoharibika kwa gharama zinazobebwa na Hazina ya Mali ya Umma, na kama hakufanya hivyo basi jukumu la kufanya hivyo litakuwa juu ya wote wenye uwezo katika watu na halazimiki kufanya hivyo mtu mmoja miongoni mwao, na iwapo wakiamua kutekeleza kazi yao na wakaenda kuifanya kazi hiyo basi jukumu la Waziri Mhusika litadondoka na wala hawatakuwa na ulazima wa kumwomba idhini ya kurekebisha huko. Na ikiwa kinachokusudiwa kitakuwa ni maalumu kama vile Haki ikiwa zitacheleweshwa basi Waziri Mhusika atalazimika kutoa amri ya kutoka katika hali hiyo pamoja na na kuwa na uwezo ikiwa wenye haki watamwomba awasaidie. Na ama kwa upande wa Kukata maovu, Waziri Muhusika hawezi kupinga kama hajaombwa na Mwenye haki msaada wa kumsaidia kwani hiyo ni haki inayomuhusu yeye inajuzu kwake kuisamehe na inajuzu kuidai.
19- Ama haki zinazoshirikia; basi kuhusu kuamirishia mema miongoni mwake ambayo apambane nazo yeye mwenyewe bila ya kuomba toka mwenye haki, na miongoni mwake haki ambazo hazipambani isipokuwa kwa kuomba toka mwenye haki. Na kuhusu maovu basi ana jukumu kumzuilia ambaye aliwataradhia waislamu kwa kuwatusia, udhia, na anaweza kumtia adabu (kumwadibishia) mtu mhalifu.
20- Na kwa upande wa daawa ya Hesba, basi kuhusu haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu inajuzu kwa kila mwaislamu mwenye adili, (anajiepuka madhambi makubwa, na hutekelzea mafaradhi, na kazi zake bora ni zaidi kuliko kazi zake mbaya). Kufanya daawa (ya Hesba) ili kuhifadhia Haki halisi za Mwenyezi Mungu Mtukufu au zile ambazo mara nyingi hupindukia haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hayo toka mlango wa kufuta maovu, na kutekeleza kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na uwe kutokana na nyinyi umma unaolingania kheri na unaoamrisha mema na unakataza maovu. Na haondio waliofanikiwa} [AAL IMRAAN 104] Na kauli ya Mtume S.A.W. "Mtu yeyote miongoni mwenu huona mauvo basi ayageuzie kwa mkono wake, na asipoweza basi kwa ulimi wake, na asipoweza basi kwa moyo wake na hilo ni Imani dhaifu zaidi kuliko Imani zote".
21- Ama Haki za mtu mmoja mmoja basi haijuzu isipokuwa kwa mwenye masilahi mwenyewe kufanya daawa kuhusu masilahi hiyo, na miongoni mwa haki za mtu mmoja mmoja zinazothibitishwa ni kukana kwa Mtume S.A.W. kutazamia nyufa za milango ili kuthibitisha kwa uharamisho wa maskani, kualika kwake kwa kujifunza ili kuthibitisha kwa haki ya elimu, kutendea kwake kwa ushauri wa Al Habab Bin Al Mundher ili kukaza kwa uhuru wa rai,
Na Qur'ani Tukufu huunga baina ya haki na masilahi ya ujumla, basi Qur'ani huthibitisha kwamba katika kudondoa kwa haki ni kupuuza kwa masilahi ya ujumla, na kukanushia heri. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Ama kina A'di walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Nani aliye kuwa na nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!} [FUSILAT 15] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema pia: {Bali lawama ipo kwa wale wanao wadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu} [AS SHURA 42] Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu alijaalia kujivuna katika ardhi (nchi) na kuwadhulumia watu, na kufanya jeuri na kuwataadia ni kudondoa haki inaelekea kupuuza masilahi ya ujumla, kwa hiyo, ilikuwa adhabu ya watu wanaojivuna miongoni mwa kaumu (wafuasi wa) ya Aad, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku za ukorofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera inahizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa} [FUSILAT 16].
22- Kutokana na hayo, hakika kwamba haki katika Fiqhi ya Kiislamu yenye maana ya ujumla, ndani yake yamo maana ya uhuru, basi huria za kijumla ni aina miongoni mwa haki. Basi ikitaja katika sheria ya Kiislamu au katika Fiqhi ya Kiislamu neno la haki, basi haki hiyo maana yake ni haki ya kimali, au haki kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au haki ya kibinafsi, au uhuru miongoni mwa huria kutokana na kuziashiria maana yake.
23- Haki na Wajibu na Adili: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ametumia wajumbe, na akateremsha vitabu vyake, ili watu wafanye kwa uadilifu, na huo ni adili ambayo ilifanyiwa kwa ardhi na mabingu, basi ishara za adili zikidhahiri na uso wake uling'aa kwa njia yoyote, basi ipo sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na dini yake. Na sheria ya Kiislamu; mwundo wake na msingi wake umejengwa kwa Hekima, na masilahi ya waja katika maisha yao na miaadi yao, na sheria hiyo yote ni adili, na yote ni rehema, basi kila suala limetokea adili kwa jeuri, na kutoka rehema kwa dhidi yake, na kutoka masilahi kwa ufisadi, na kutoka hekima kwa upuuza basi zote siyo kutoka kwa sheria. Kwani sheria na adili baina ya waja wake, na rehema yake baina ya viumbe wake.
24- Na adili katika Uislamu ni maana kamili umekusanya yote, na pana hakibanii kitu cho chote, na hakitokewi nayo kitu cho chote, basi wakati mtawala anaamirishwa kwa adili katika hukumu yake, mwanadamu pia anaamirishwa kwa adili baina ya miguu yake, basi haijuzu kuvaa kiati kimoja katika mguu mmoja bila ya mguu mwengine, bali huvaa viatu katika miguu yake miwili au anaihifadhia yote, ili ahakikishe adili baina ya miguu yake yote miwili. Na Uislamu huamirishia mwanadamu asiketi kwa baadhi ya mwili wake katika Jua na baadhi nyingine katika kivuli, bali ama anaweka mwili wake wote Juani au kivulini, na hiyo ni adili baina ya mwili wake wote.
25- Katika kivuli cha adili hiyo, usawa pekee baina ya haki na wajibu huyakinia, kwa hiyo, wakati wa falsafa nyingine zimeelekea kupigana kwa matabaka, au kudondoa kwa ajili ya mtabaka maalum. Na wakati mizunguko ya jamii inapigana bila ya usawa mzuri baina ya haki tufauti za mtu mmoja mmoja, Uislamu unakuja kuhakikishia upatanisho na wasiliano, bali na rithimu (uwiano) baina ya mtu mmoja mmoja, na kwa ajili ya kuhakikisha utu kwa mwanadamu. Basi hukumu za sheria ya Kiislamu –Kama anavyosema As Sahtwibiy - Hazihalalishia ispokuwa kwa masilahi za watu, na endapo masiliahi yalipatikana basi hupatikana sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Rejeo: Sehemu ya Tafiti katika Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri.

 

 

Share this:

Related Fatwas