Kuondoa Makaburi Yaliyopo Ndani ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuondoa Makaburi Yaliyopo Ndani ya Jiji la Kairo.

Question

 Ni ipi hukumu ya kuondoa makaburi yaliyopo ndani ya Jiji la Cairo na kuyapeleka nje ya Jiji? Ambapo huhamishwa kwa madai kuna masilahi zaidi ya kufanya hivyo, kwa sababu eneo hilo ni pana na linaweza kugeuzwa na kuwa eneo la kijani, pamoja na kuwepo katika hilo usafishaji wa maeneo haya kutokana na wahalifu na waporaji humo miongoni mwa watu wanaotishia usalama wa watu wa amani na kueneza vitendo vya kihalifu, na wanatoa sababu pia ya kwamba baadhi ya Wanachuoni wamepitisha suala la kuhamisha mwili wa maiti, na miongoni mwao pia wapo waliopitisha matumizi ya ardhi ya makaburi pindi miili ikishatoweka kabisa, na kuwa maamuzi ya kuhamisha makaburi yakitolewa na kiongozi mkuu wa nchi, basi ni lazima kutekelezwa, kwa sababu mkuu wa nchi ana mamlaka ya kupangilia ruhusa. Tunaomba ufafanuzi wenu na Mwenyezi Mungu akunufaisheni.

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, Sala na salamu zimwendee Mtume wa mwisho ambaye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na Jamaa zake Masahaba zake na wale waliomfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Mwenyezi Mungu Amemkirimu mwanadamu kwa aina mbalimbali za ukarimu, Akamfanya awe na cheo kama alivyosema Mola: {Na hakika Tumewatukuza wanadamu, na Tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na Tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na Tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa Tuliowaumba} [AL ISRAA; 70].
Ikawa miongoni mwa ukarimu wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake pia katika hali ya kuwa kwao wamefariki kwa kutoa miongozo ya kuwazika, kama alivyotuhadithia Mwenyezi Mungu kisa cha watoto wa Adamu kinasema: {Hapo Mwenyezi Mungu Akamleta kunguru anayefukua katika ardhi ili amuoneshe ni vipi atamsitiri ndugu yake} [AL MAIDAH; 31].
Hiyo ikawa ni katika jumla ya neema za Mwenyezi Mungu kwa watoto wa Adamu. Mwenyezi Mungu anasema: {Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya * Walio hai na maiti?} [AL MURSALAAT, 25: 26], kwa maana: tumekuneemesheni kwa kuidhalilisha ardhi kwa ajili ya masilahi yenu, na Tukaifanya yenye kuwakusanya nyinyi nyote, kwa maana: Kukusanya miili yenu kuwa juu ya mgongo wake katika hali ya uhai wenu na kuwakusanya ndani ya tumbo lake katika hali ya kufa kwenu, kama vile miongoni mwa neema zitokazo kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake walio hai ni pamoja na kuwaweka sehemu za juu na majumba ya kifahari, miongoni mwa neema zake kwa watu waliofariki ni kuwaweka ndani ya makaburi, ikiwa ni haki yao ya kuhurumiwa, na kusitiri miili yao isiliwe na wanyama wakali na wengineo, na kuzuia kero kwa watu walio hai kutokana na harufu mbaya.
Kuzika katika Sharia takatifu kunazingatiwa ni jambo la lazima la kutoshelezeana, kwa maana wakitekeleza baadhi ya watu katika jamii, basi hawana dhambi wale wengine waliobakia, na ikiwa wataacha kutekeleza hao wengine, basi watu wote wa eneo hilo watapata dhambi ya kutomzika ndugu yao Amesema Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha Al-Majimuu 5/112 chapa ya Al-Minbariya: “Kuosha maiti na kumkafini pamoja na kumsalia na kumzika ni faradhi ya kutoshelezeana bila ya tofauti yoyote ile ya Wanachuoni ”.
Mwislamu anapozikwa kwenye sehemu miongoni mwa sehemu ambazo zinafaa kuzikwa, basi eneo hili linakuwa ni kinga kwake maadamu mabaki ya mwili wake bado yapo na hayajaoza wala mifupa yake bado haijageuka na kuwa udongo isipokuwa panapokuwa na hali ya dharura, wala sehemu hii haichukui mwili wa mtu mwingine mpaka mwili wa maiti ya kwanza uwe umeshamalizika pamoja na mifupa yake ambapo mwishowe inakuwa udongo.
Amesema Mwanachuoni Al-Kharashy mtoto wa Imamu Malik katika sherehe yake ya Mukhtasar Khalil 1/225 chapa ya Dar Al-Fikr: “Kaburi ni kifungo hauondoshwi mwili wala kuchimbwa juu yake”.
Hivyo zoezi la kuhamisha makaburi lina sura mbili:
Sura ya Kwanza: Ndani yake kaburi linakuwa bado halijaozesha mabaki ya mwili wa marehemu na kubadilika mifupa yake na kuwa udongo, katika hali hiyo asili yake kisheria ni haramu kulihamisha, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ukiukaji wa utukufu na utu wa mwanadamu, na Sharia Takatifu imesema juu ya kumtukuza maiti, kwani imepokelewa na Abu Dawud na Ibn Maja na wengine kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Kuvunja mfupa wa maiti ni kama vile kumvunja akiwa hai”, maana yake: ni dhambi. Amesema Mwanachuoni At-Tiibiy katika sherehe ya kitabu cha Mishkat Al-Masabiih 4/1412 chapa ya Maktabatil Bar: “Ndani yake kuna dalili kuwa kutukuzwa kwa maiti kunahitajika katika hali zote kama ilivyokuwa wakati wa uhai wake, na kumdharau pamoja na kumpuuza ni jambo linalokatazwa kama ilivyokatazwa wakati wa uhai wake”.
Amesema Mwanachuoni Ibn Al-Haj akielezea Hadithi hii katika kitabu chake cha Al-Madkhal 3/242 chapa ya Dar At-Turath: “Hilo ni kwa ujumla wake kwenye mifupa na isiyokuwa mifupa iwe kwa uchache au kwa wingi, kila kisichokubalika katika hali ya uhai wake, basi hapaswi kufanyiwa baada ya kufa kwake, isipokuwa ikiwa Sharia imeruhusu, na kisichoruhusiwa na Sharia, basi huzuiwa katika hali zote”.
Akasema pia kwenye kitabu hicho hich 2/18, 19: “Huruma ya Mwenyezi Mungu iwe kwa Wanachuoni, wamekubaliana kuwa sehemu aliyozikwa Mwislamu ni wakfu kwake maadamu ndani yake kunaendelea kuwepo kitu katika sehemu ya mwili wake, mpaka pale anapooza kabisa, ikiwa ataoza, basi hapo anaweza kuzikwa mtu mwengine, ikiwa kitabakia kitu chochote kiwe ni sehemu ya mifupa yake, basi uharamu utaendelea kuwepo kama vile mwili wake wote bado upo, wala haifai kuchimbwa juu yake wala kuzikwa pamoja naye mtu mwingine, wala hafukuliwi kwa makubaliano ya Wanachuoni isipokuwa kama eneo la kaburi lake ni la kuporwa”.
Amesema Sheikh Al-Islam Zakaria Al-Ansariy Al-Shafiy katika kitabu cha Asnaal-Matalib 1/331 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy: “Haramu kuchimbua kaburi kabla mwili haujaoza na kumalizika kabisa kwa mujibu wa mtazamo wa watu wenye uzoefu na maeneo hayo ya ardhi ili kuchunga heshima ya maiti”.
Wanachuoni hawajapitisha suala la kuhamisha makaburi isipokuwa katika hali maalumu na kwa masharti maalumu na maelezo yake yatakuja.
Sura ya Pili: Kaburi ambalo mwili wake umeshavurugika na mifupa kulainika na kuwa udongo, hapo inafaa kuhamisha kaburi, kwa maana ya kuzikwa katika eneo lengine na kusitishwa kuzika eneo la kwanza, hapa pia inawezekana kunufaika kwa sura za kunufaika kunakofaa, na hili linafanyika kwa sharti la kuwa mwenye kuhamisha awe na haki ya kuitumia hiyo ardhi.
Amesema Imamu Zailiii katika kitabu cha: [Tabyeen al-Haqaiq 1/246 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: “Ikiwa mwili wa maiti umeshamalizika na kuwa udongo, basi inafaa kuzikwa mtu mwingine kwenye kaburi lake na kulima eneo hilo na hata kujenga juu yake”.
Amesema Imamu An-Nawawy katika kitabu cha: [Sharh Al-Muhadhab 5/273 chapa ya Al-Mimbariya]: “Inafaa kuchimbua kaburi ikiwa mwili wa maiti umeshakwisha na kuwa udongo, hapo inafaa kuzika mtu mwingine, na inafaa kulima kwenye kipande hicho cha ardhi na kujenga juu yake na kufanya mambo mengine yenye manufaa na kukitumia kipande hicho kwa makubaliano ya wenye ardhi, ikiwa eneo hilo la kuazimwa, basi aliyeazima atalirudisha kwa mwenye eneo, haya yote ikiwa hakuna kilichobakia kwenye mwili wa maiti athari ya mifupa au viungo vingine vya mwili, wamesema watu wetu Mwenyezi Mungu Awarehemu: Linatofautiana hilo kutokana na tofauti ya nchi na nchi ardhi kwa ardhi nyingine, lakini inapitishwa kauli ya watu wenye uzoefu na eneo hilo”.
Amesema Imamu Ibn Qudama Al-Maqdisiy mtu wa Imamu Hanbaliy katika kitabu cha [Al-Mughniy 2/194 chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby]: “Ikiwa atakuwa na uhakika kuwa maiti tayari imeshavurugika na kuwa udongo, basi inafaa kuchimbuliwa kaburi na kuzikwa mtu mwengine, ikiwa ana shaka katika hilo, basi atarudi kwa watu wenye uzoefu”.
Na kwa maelezo hayo: Hali inayohusiana na hili zipo mbili:
Hali ya Kwanza: Kusimamisha kuzika kwenye makaburi haya yanayotakiwa kuhamishwa, na kuanzisha maeneo mengine mapya yaliyoandaliwa kwa lengo la kuzika, na kupita muda wa kusajili miili ya zamani kuwa imeshakuwa udongo, kisha husajiliwa makaburi haya katika lengo ambalo limetakiwa na nchi.
Hali ya Pili: Kukamilika matumizi ya makaburi na kubadilishwa kabla ya kupita huu muda.
Katika hali ya Kwanza: Huwa makaburi haya miongoni mwake ni yenye kumilikiwa na watu au taasisi, na mengine yapo kama wakfu, basi yale yanayomilikiwa na watu au taasisi haiwezekani kuhamishwa isipokuwa kwa kuuzwa na wamiliki wake na kuuziwa serikali kwa ridhaa zao, au serikali ichukue umiliki kwa yule asiyeridhia kuuza makaburi yake, na hukumu ya kufaa kuchukua umiliki kupitia mkuu wa nchi limeachwa tu kwa utashi wake, bali kuna masharti katika jumla ya masharti:
Sharti la Kwanza: Ni kuwa msukumo wa kuchukua umiliki ni kwa sababu ya masilahi ya Umma.
Sharti la Pili: Ni kuwa masilahi ya Umma yamekuwa ya dharura kwa Umma au mahitaji ya Umma huteremshwa kwenye nafasi ya dharura.
Sharti la Tatu: Uchukuaji huo uwe kwa lengo la kufikia masilahi hayo.
Sharti la Nne: Kulipwa fidia mmiliki fidia ya haraka na adilifu.
Sharti la Tano: Kutoharakisha uhamishaji wa umiliki kabla ya kufika muda wake.
Ikiwa litakosekana sharti moja au baadhi ya masharti, basi haifai kuhamisha umiliki wa eneo la kaburi, kwa mujibu wa asili ya Kisharia katika wajibu wa kuchunga umiliki wa mtu na kulinda kutokana na uadui wowote ule, hivyo watu waliomilikishwa maeneo yao haitakiwi kwa yeyote kulichukua au kufanya kitu chochote pasi na ridhaa ya wamiliki, na wana haki ya kuyatumia na kunufaika nayo namna watakavyo katika wigo wa Sharia.
Imepokelewa na Darkatwniy kutoka kwa Habban Ibn Abi Jibillah kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Kila mmoja ana haki kwenye mali yake kwa wazazi wake watoto wake na watu wote”, Hadithi hii inazungumzia asili ya uhalali wa mtu kutumia mali zake.
Ama kuhusu makaburi kuwa wakfu au kuandaliwa kwa mazishi, haifai kuvuka makusudio hayo, ambapo hakuna dharura au udhuru wa Kisharia, na makaburi yanayopatikana eneo la juu la Mukattam ni katika makaburi yanayokusudiwa kubadilishwa na kuhamishwa, sehemu hii ni ngome ya Misri ambayo imeelezewa na watu wa mila kuwa ni sehemu ya wakfu yenye kinga, na miongoni mwa waliosema hayo ni Imamu Al-Khatwab katika kitabu cha [Mawahib Al-Jalil 2/243 chapaya Dar Al-Fikr], na Sayyid Ahmad Al-Dardir katika [Sharhu Al Kabeer 1/425 na kitabu cha Dusuqiy chapa ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiya], na Mwanachuoni An-Nifrawy katika kitabu cha [Al-Fawakih Ad-Duwany 1/291 chapa ya Dar Al-Fikr, na Sheikh Hassan Al-Adawy katika kitabu chake cha Sherehe ya Risalah 1/422 chapa ya Dar Al-Fikr, na Imamu Ad-Damiry katika kitabu cha Nihayatul Muhtaj cha Mwanachuoni Ar-Ramaly 3/34 chapa ya Dar Al-Fikr, na Imamu Al-Khatiib Ash-Sharibiny katika kitabu cha Mughniy Al-Muhtaj 2/55 chapa ya Dar Al-Kutubil Elmiyah, na Mwanachuoni Sulaiman Al-Jamal katika kitabu chake cha Sherehe Al-Minhaj 2/207 chapa ya Dar Al-Fikr, na Mwanachuoni Al-Bujairamy katika kitabu chake cha Sherehe ya Minhaj 1/ 496 chapa ya Dar Al-Fikr Al-Arabiy] na wengine.
Wamesema kuwa eneo hilo ni wakfu tokea zama Amiri wa Waumini Umar Ibn Al-Khattab R.A. kwa ajili ya Waislamu, amepokea Ibn Abdulhakam Al-Qurashiy kwa upokezi wake ndani ya kitabu chake cha Futuh Masri wa Akhbaraha kurasa ya 108 chapa ya Maktabat Madbouly kuwa Muqawqis kiongozi wa Misri alimwambia Amr Ibn Al-Aas R.A. kuwa anauza maeneo ya makaburi ya Mukattam kwa thamani ya Dinar elfu Sabini, ndipo Amr aliposhangaa hilo na akasema: Katika hilo mwandikie Kiongozi Mkuu wa Waumini, ndipo akamwandikia Umar Ibn Al-Khatwab R.A. na kumwambia: Uliza je sijakupa maeneo niliyokupa kuwa hayalimwi wala hapatolewi maji wala hakuna kunufaika nayo kwa chochote? Akauliza na akasema: “Hakika tunakuta kwenye vitabu kuwa kuna mche wa Peponi” akamwandikia hivyo Umar, na Umar akamwandikia: “Sisi hatufahamu uwepo wa mche wa Peponi isipokuwa kwa Waumini, na mzike hapo Mwislamu atakayefariki wala hatuuzi chochote” ikwa mtu wa kwanza kuzikwa hapo ni mtu mmoja anaitwa Aamir, na ikasemwa alikuwa ni Amarat.
Katika mapokezi mengine ni kuwa Muqauqis alisema kumwambia Umar: Sisi tunakuta kwenye kitabu chetu: Kuwa kati ya milima hii ambayo mmeteremka kunaota mti wa Peponi”, basi akaandika kumwambia Umar na akasema: “Ni kweli, basi fanya eneo hilo ni sehemu ya makaburi ya Waislamu”.
Amesema Mwanachuoni Taqiy Ad-Din Al-Maqreziy katika kitabu chake cha: [Al-Mawaidh wal Iitibaar bidhikr Al-Khutatu Wal-Aathar 1/124]: “Amesema Asad Ibn Musa: Nililiona jeneza nikiwa na Musa Ibn Lahiiaa tukawa tumekaa pembezoni mwake akainua kichwa chake na kuangalia kwenye milima - kwa maana ya milima ya Mukattam na akasema: Hakika Issa Ibn Maryam A.S. amepita kwa miguu kwenye milima hii, akiwa amevaa nguo ya sufi na amefunga mkanda katikati yake pembezoni mwake akiwepo Mama yake, akageukia kwenye milima ile na akasema: “Ewe Mama yangu haya ni makaburi ya Umma wa Muhammad S.A.W.”.
Imeelezwa kuwa Mkuu wa Mkoa alikwenda kwa Sheikh Al-Islam na Mufti wa zamani wa Misri Mwanachuoni Muhakiki Sheikh An-Nawawy - Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe kwake -- alishika nafasi hiyo ya Mufti mwaka 1313H. baada ya miezi michache ndani ya mwaka huo huo alichukua nafasi ya kuwa Sheikh Mkuu wa Al-Azhar, nilimwuliza nini kinachothibitisha Kisharia kuwa ardhi ya Ngome ya Misri ikiwa pamoja na Ngome ya Al-Mujawirina zimewekwa wakfu kwa ajili ya kuzikia? Akajibu kwa kwa Fatwa iliyopitishwa kuhusu jambo hili ya mwezi 8 Mfungo Kumi 1313H. Fatwa ikaja kama ifuatavyo:
“Tamko la Wanachuoni kuwa ngome ya Misri ni waqfu, na kuwa haifai kunufaika na mambo mengine zaidi ya kuzikia ... wakasema kuwa eneo hilo la Mukattam ni waqfu kutoka kwa Umar kwa ajili ya kuzikia Waislamu, na ngome hiyo Amiri wa Waumini Umar Ibn Al-Khatwab R.A. aliifanya kwa ajili ya kuwa sehemu ya kuzikia Waislamu, na hali imeendelea kuwa hivyo, na wakasema pia kuwa inafaa Kiongozi kutoa waqfu sehemu ya ardhi ya hazina ya taifa kwa ajili ya Umma wa Waislamu, kama alivyotoa waqfu Omar R.A. eneo la Sawad huko nchini Iraq, na wamesema kuwa eneo la chini ya milima ya Mukattam iliyowekwa waqfu na Mfalme Al-Muqawqis ambapo limekuwa ni eneo la jeshi lenye kufahamika hivi sasa kwa jina la - Basatin - na kuitwa Al-Yahmuum - nao ni mlima mwekundu unaozunguka eneo la Jiji la Kairo kwa upande wake wa Kaskazini Mashariki inayopatikana eneo la Mashariki mwa Abbasia - imefahamika kuwa ardhi ya ngome ya Misri ambayo ndani yake kuna eneo la ngome la Al-Mujaawiriina limetolewa waqfu kwa ajili ya kuzikia Waislamu kutoka kwa Sahaba Umar Ibn Khattab R.A. kuanzia wakati huo mpaka hivi sasa, pia wamesema kufanyia kazi hoja kama hiyo ni kama kufanyia kazi sharti la waqfu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi”.
Pia Mufti wa zamani wa Misri Mwanachuoni Sheikh Abdulrahman Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe kwake: “Alichukua nafasi ya Mufti mwaka 1339 H. sawa na mwaka 1921 na aliendelea na nafasi hiyo kiasi cha miaka saba, aliulizwa kuhusu eneo hilo la milima ya Mukattam kama eneo la ngome ndogo na ngome ya Imamu Shafiy Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe kwake, pia ngome ya mapito ya Nasru ambapo limewekwa waqfu ili kuzikia maiti za Waislamu, je ikiwa mtu atapa kibali cha kujenga kaburi katika eneo la wazi inaweza kugeuka kutoka kuwa waqfu na kuwa miliki ya mtu kwa sababu ya kuwa na hiki kibali?
Akajibu siku ya mwezi 23 Mfungo Mosi 1342H. sawa na tarehe 27 May 1924 kwa Fatwa aliyosema:
“Wamesema Wanachuoni kuwa ardhi ya ngome ambayo inapatikana eneo la milima ya Makattam Misri limewekwa waqfu na Amiri wa Waumini Umar Ibn Al-Khatwab R.A. ili liwe eneo hilo ni sehemu ya kuzikia maiti za Waislamu, na likatumika kwa kazi hizo tokea zama zake mpaka hivi sasa, na kwa vile limekuwa ni eneo la waqfu hivyo halifai kumilikiwa wala kumilikisha mtu, kutokana na maelezo hayo halizingatiwi ni miliki ya mwenye kibali cha kuruhusiwa kujenga”.
Ama katika hali ya pili - nayo ni kuhamisha kabla ya kupita muda kuandikishwa miili na kuwa udongo - zinakuja sababu za kuzuia zilizotajwa katika hali ya kwanza kwa ufafanuzi uliotajwa, pamoja na maelezo yaliyotangulia ya asili ya uharamu wa kuchimbua kaburi la maiti Mwislamu na kukiuka heshima yake, na uvunjaji wa heshima hii unakuwa mkubwa zaidi ikiwa ufukuaji huo ni wa kaburi la wengi.
Na huongezwa katika haya yote pia hali mbili: Hali ya kwanza na ya Pili: Ni ile iliyopitishwa na Wanachuoni ikiwa ni pamoja na uharamu wa kufukua kaburi la waliomo wana uharamu zaidi hata baada kuoza, kama vile kaburi la Sahaba, Wanachuoni, Mawalii na waja wema, katika hili ni kuinua nafasi yao na kutukuza nafasi zao pamoja na kuhuhisha utajo wao na kuwatembelea pamoja na kutafuta baraka zao.
Amesema Sheikh Muwaffiq Ad-Din Hamza Ibn Yusuf Al-Hamawy katika kitabu chake cha: [Sharhu ya Mushkilat Al-Wasiite 2/390] maelezo ya pembeni ya kitabu cha [Wasiit cha Imamu Ghazaliy chapa ya Dar As-Salaam], kwenye kauli ya Imamu Abi Haamid Al-Ghazaliy: “Si halali kufukuwa kaburi isipokuwa baada ya kuvurugika viungo vya maiti kwa sababu ya kuchukua muda mrefu”:
“Amefanya Sheikh kusagika viungo vya mwili kwa kupita muda mrefu ni sababu tosha ya moja kwa moja ya kufukua kaburi na si kinyume na hivyo, bali ikiwa aliyezikwa ni Sahaba au mtu aliyekuwa na umaarufu wakati wa utawala wake basi haifai kulifukuwa kaburi lake hata kama viungo vyake vitakuwa vimeshasagika”.
Amesema Sheikh Al-Islam Zakaria Al-Ansaariy katika kitabu cha [Asnaa Al-Matalib 1/321 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamy]: “Ni haramu kufukua kaburi kabla ya mwili wa marehemu kuoza kwa mtazamo wa watu wenye uzoefu na eneo hilo, ili kuepuka kukiuka utukufu wa maiti, ikiwa mwili utakuwa umeshaoza, kwa kusagika mwili wake mifupa yake na kuwa udongo, basi inafaa kufukua kaburi lake na kuzikwa mtu mwengine sehemu hiyo ... baadhi ya wengine wakavua ikiwa aliyezikwa hapo ni Sahaba au kiongozi maarufu basi haikufukuliwa kaburi hata kama mwili utakuwa umeshaoza, akasema Az-Zarkashy: Naye ni Hassan na kuunga mkono yaliyotolewa wasia kuwa: Unafaa wasia wa kuyajengea makaburi ya Manabii na waja wema, kutokana na kuhuhisha ziara na kutafuta baraka”.
Amesema Mwanachuoni Al-Khatwib Ash-Sherbiniy katika kitabu cha: [Mughniy Al-Muhtaj 2/60 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Amesema Al-Muwaffiq Hamza Al-Mahmoudy katika kitabu cha [Mushakkal Al-Wasiit]: Ikiwa aliyezikwa ni Sahaba au kiongozi maarufu haifai kufukua kaburi lake hata kama mwili wake utakuwa umeshasawajika na udongo. Amesema Ibn Shubhat: Akiunga mkono yaliyosemwa na Masheikh wawili - kwa maana ya Maimamu wawili ambaye ni Imamu Raafii na Imamu An-Nawawiy - katika wasia: Kuwa unafaa wasia wa kuyajenga makaburi ya Manabii na waja wema, kwa sababu ya watu kutembelea na kutafuta baraka, kadhia yake ya kufaa kujenga makaburi ya waja wema pamoja na kusisitiza hapa ni kuwa pindi mwili utakapokuwa umeshasawijika haifa kujengea kaburi lake na kuweka sawa udongo wake kama makaburi mengine.
Ameelezea pia Sheikh wa madhehebu ya Imamu Shafiy: Mwanachuoni Shihab Ad-Din Ibn Hajar Al-Haitimy katika kitabu cha [Tuhfatul-Muhtaj 3/206 chapa ya Dar Ihyaa Turath Al-Arabiy], na Mwanachuoni Shams Ad-Din Ar-Ramly katika kitabu cha [Nihaayat Al-Muhtaj 3/41 chapa ya Dar Al-Fikr].
Kuyalinda makaburi ya Wanachuoni mawalii na waja wema kuyachunga na kuyahuhisha kwa kutembelea makaburi hayo ni mambo yanayofanywa na Waislamu wa hapo zamani na hata wa sasa, ambapo yamebakia kuwa ni maeneo yenye kufahamika kwa watu Mashariki na Magharibi, ikiwa Waislamu wameendelea kuyalinda makaburi ya Mafarao na athari zao pamoja na kuwa si Waislamu hawakuyagusa wala kuyaondoa, basi kuyahifadhi makaburi ya wakubwa wa Umma ni bora zaidi, na haya makaburi yanayokusudiwa kuhamishwa yaliyofurika kwa uwingi wa makaburi yakiwemo ya Wanachuoni waja wema na Mawalii bali ndani yake pia kuna makaburi ya Masahaba Watukufu R.A. nchini Misri mamia ya Masahaba, anasema Mwanachuoni Ibn Zuulaaq katika kitabu chake cha [Fadhail Misr ukurasa wa 27, 28 chapa ya shirika la umma la vitabu la Misri]: “Nchini Misri waliingia Masahaba wa Mtume S.A.W. kiasi cha elfu moja, miongoni mwao ni Masahaba walioshiriki vita vya Badr, tofauti na wale waliokuwa kwenye kambi ya Amr Ibn Al-Aas, wote hawa walimwahi Mtume S.A.W. miongoni mwao wamo waliopokea Hadithi kutoka kwa Mtume S.A.W. na wengine wamo waliomwona Mtume S.A.W. na wengine walimwahi Mtume lakini hawakumwona, na kulikuwa na askri wengi kiasi cha elfu kumi na mbili wakati wa kuifungua Misri, na wamekufa nchini Misri miongoni mwa Masahaba maarufu wa Mtume S.A.W. ukiacha wale ambao hawakufahamika, miongoni mwa hao waliofarikia Misri ni: Amr Ibn Aas, Uqba Ibn Aamir, Abu Basra Al-Khaffariy, Kharijah Ibn Hudhafa, Qais Ibn Abi Al-Aas, Abdillah Ibn Al-Haarith Ibn Juzu”. Na imepokelewa Hadithi na Tirmidhy kutoka kwa Abdillah Ibn Barida kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Sahaba wangu yeyote akifariki kwenye eneo lolote isipokuwa atafufuliwa akiwa kiongozi na nuru kwao Siku ya Kiyama”.
Miongoni mwa waliozikwa katika ngome ya Misri katika watu wa nyumbani kwa Mtume S.A.W. ni pamoja na Hassan Al-Anwar Ibn Zaid Al-Ablaj Ibn Al-Hassan Ibn Ally, na ndugu yake Yahya aliyeitwa kwa jina la Al-Anwaar, na Muhammad Al-Anwar Ibn Zaid Al-Asaghir ndugu wa Bi. Nafisah na ndugu wawili Al-Hassan na Al-Muhassan watoto wa kassim Ibn Jafar As-Swadiq, na Yahya Ibn Kassim At-Twayyib Ibn Muhammad Al-Maamun Ibn Jafar As-Swadiq mwenye umarufu kwa jina la Yahya As-Shabih na ameitwa kwa jina hilo ni kutokana na kufanana kwake na babu yake ambaye ni Mtume S.A.W. na dada yake Bi. Fatma Al-Ainaa, na ameitwa kwa jina hilo kutokana na uzuri wa macho yake na kufanana kwake na Bi. Fatma Zaharaa, na Fatma Binti Hussein Ibn Ally na dada yake Bi. Sakina, na Bi. Amina Binti Musa Al-Kadhim Ibn Jafar As-Sadiq, na Bi. Ruqiyah Binti Ally Ridha, na Bi. Fatma Binti Muhammad Ibn Al-Hassan, na Bi. Kulthum Binti Kassim At-Tayyib Ibn Muhammad Ibn Jafar As-Swadiq.
Na katika watu wa Sufi na wa zuhdi kwa maana ya wenye kuipa nyongo dunia pamoja na waja wema ni pamoja na: Abu Ally Rudbary na Dhunnuun Al-Masry na mke wake Maimuna Al-Abidah, na Bi. Aikah Al-Adawiyah mke wa Muhammad Ibn Abi Bakr, na Hamdunah Al-Aabidah, na Abul-Hassan Diinuuriy, na Abu Kassim As-Samit, pamoja na Sheikh Abu Bakr Al-Ansary Al-Qurtwubiy Az-Zahid, na Sheikh Ibrahim Ar-Ruqy na Ibn Tabataba, na Imamu Ibn Aby Hamza, pamoja na Sheikh Yusuf Al-Ajamy naye ndiye aliyehuhisha tarika ya Imamu Juneid nchini Misri, na Abu Suud Ibn Aby Al-Ashair, na Sheikh Wajih Din Al-Aidarus Al-Hadharamiy, na kundi la Wanachuoni na Masheikh wa tarika ya Nakshabandia kama vile Sheikh Al-Murabbiy Ahmad Muhammad Musa, na Sheikh Abdulaziz Al-Sharif pamoja na Sheikh Ahmad Hamadah, na Sheikh Muhammad Al-Amir, na kundi lingine la Wanachuoni viongozi wa tarika ya Shadhiliya kama vile Sheikh Shafiy Ad-Din Abi Mawahib Ash-Shadhily, na kundi la viongozi tarika ya Al-Khulutiya kama vile Sheikh Mustafa Al-Bakry na Sheikh Al-Hifny pamoja na Sheikh Al-Haddad.
Miongoni mwa wasomaji: Ni Imamu Warsh Al-Masriy mpokezi wa kisomo cha Imamu Nafii, na Imamu Ismail Ibn Rashid Al-Haddad ambaye ni Sheikh wa wasomi wa Qu`rani katika zama zake, na Walii wa Mwenyezi Mungu Imamu Shatiby mwenye kasida ya Shatibiya katika visomo, na Taqiy Ad-Adin Ibn Al-Swanii Al-Misry, na Sheikh wa wasomaji wa Qur`ani nchini Misri ndani ya wakati wake ambaye ni Sheikh Mutawalli.
Miongoni mwa Wanachuoni wa Salaf: Ni Maimamu: Muhammad Ibn Al-Hanafiya, Muhammad Ibn Siriin na Wakiii Ibn Al-Jarraah.
Miongoni mwa watu wa madhehebu ya Abu Hanifa ni pamoja na: Kadhy Bakkary Ibn Qutaibah, Imamu Abu Jafari At-Twahawiy, na Mwanachuoni Ibn Nujaim mwenye Bahar Ar-Raq, na Mwanachuoni Fakhr Ad-Din Zailaii mshereheshaji wa kitabu cha Kanzu, Mwanachuoni At-Twahtawy mwenye Hashiyat Ally ni sherehe ya kitabu cha Tanwiir Al-Absar.
Katika wafuasi wa Imamu Malik ni pamoja na: Abdulrahman Ibn Kassim, Ashhab Ibn Abdulaziz, Asabagh Ibn Al-Farh, Abdillah Ibn Wahab mwanafunzi wa Imamu Malik, na Kadhy Abdulwahaab, Imamu Shihab Ad-Din Al-Qurafiy, Khatwib At-Telmesaaniy mshereheshaji wa kitabu cha [Ash-Shafaa], Imamu Ash-Shaawiy, Sheikh Ally Saidy Al-Adawy na Mwanachuoni An-Nafrawiy.
Kwa wafuasi wa Imamu Shaafiy ni: Imamu Al-Murabiy, Abu Yaakuub Al-Buutwiy, Younus Ibn Abdul Aalaa As-Swadafiy ni mwanafunzi wa Imamu Shafiy, na Ibn Haddad, Abu Is-haq Al-Maruziy mwanafunzi wa Ibn Suraij, na Kadhy Mujally mwenye kitabu cha Ad-Dhukhair, Sheikh Abu Abbas Al-Irby mwanafunzi wa Ilkiya Al-Harraasiy, na Sultani wa Wanachuoni Al-Izz Ibn Abdulsalaam, pamoja na Imamu Al-Haafidh Ibn Dakiik Eid, pia Sheikh Ibn Razin Al-Aamiry, Imamu Badr Ad-Din Az-Zarkashy, Imamu Badr Ad-Din Jamaah, Haafidh Ibn Sayyid An-Naas, Imamu Shams Ad-Din Al-Asafahaniy mshereheshaji wa kitabu cha Al-Mahsuul.
Kwa watu wa Imamu Hanbal ni: Tegemezi la Misri ndani ya wakati wake ambaye ni Sheikh Abu Hassan Al-Khalaii, na Hafidh Abdulghany Al-Maqdisy, na katika Masheikh wa mwisho wa dhehebu la Imamu Hanbaly na Muasisi wa madhehebu yao: Mwanachuoni Mansour Ibn Younus Al-Bahuty.
Katika wazungumzaji ni: Yahya Ibn Bukair mpokezi wa kitabu cha Al-Muutwa kutoka kwa Imamu Malik, na Abdullah Ibn Luhaia, Hafidh Abu Hassan Al-Huufy, Al-Haafidh Ibn Hajar Al-Asqalaany mshereheshaji wa kitabu cha sahih Bukhari, na Haafidh Al-Mundhiry, na Imamu Sharaf Ad-Din Ad-Demyatwiy, pamoja na Hafidh Jalal Ad-Din As-Suyutiy.
Katika watu wasarufi na wanalugha: Abul-Hassan Ibn Babshadh mwana sarufi, na Kadhi Al-Fadhil Abu Muhammad Al-Bayaany.
Katika watu wa historia: Imamu Al-Hafidh Omar Ibn Dahiyah Al-Kalabiy, na Hassan Ibn Zuulaq mwanahistoria maarufu.
Katika Wanachuoni wa Al-Azhar na Masheikh wake ni pamoja na: Sheikh Ahmad Ad-Damhuriy, Sheikh Hassan Al-Ataar, Sheikh Muhammad Al-Amiir Al-Malikiy, Sheikh Ibrahim Al-Baijuuiry, Sheikh Shams Ad-Din Al-Ambabiy, Sheikh Ahmad Ibn Arafa Ad-Dusuuqiy, Sheikh Muhammad Abulfadhl Al-Jiizawiy, Sheikh Salim Al-Bashariy, Sheikh Muhammad Mustafa Al-Maraghiy, Sheikh Muhammad Al-Ahmadiy Ad-Dhawahiriy, Sheikh Mustafa Abdulrazik, Sheikh Muhammad As-Samaalutwiy, Sheikh Ally Al-Bablawiy, Sheikh Muhammad Abdul pamoja na wanafunzi wake Sheikh Muhammad Rashid Ridhaa, Sheikh Mahmoud Abu Dakikah, Omar Makram kiongozi maarufu wa kitaifa.
Ambao hatujawataja ni wengi zaidi ya tuliowataja, hawa mbali na wale waliozikwa kwenye ngome ya Misri na makaburi yao yakajengewa Misikiti kama vile Bi. Aisha Binti Jafar As-Swadiq, na Bi. Nafisa Binti Hassan Al-Anwar Ibn Zaidi Al-Ablaj Ibn Hassan As-Sabt, Imamu Allaith Ibn Saad, Imamu Shafiy, Sheikh Al-Islaam Zakaria Al-Answariy, na Kamal Ibn Al-Himam, Al-Aarif Ibn Ataallah Askandariy, Umar Ibn Al-Faridh, Abu Suud Al-Jaarihy, Sheikh Shahiin Al-Khalwaty, Sheikh Kareem Deen Al-Khalwatiy wakubwa wa tarika ya Al-Wafaiyah, Sheikh Abdillah As-Sarqawy Sheikh wa Al-Azhar, Sheikh Mahmoud Abi Al-Yaan na kiongozi wake Sheikh Ibrahim Al-Khalil Ibn Ally, na mtoto wa kiongozi wake Sheikh Muhammad Zakiy Ad-Din Ibrahim na wengine wengi - Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe kwao wote.
Hivyo kuhamisha makaburi yao ni ukiukaji dhidi ya hawa watukufu na ni kufanya uadui juu yao.
Wamesema Wanachuoni kuwa sababu ya kuitwa Kairo ni yenye kulindwa: Ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameilinda na kuihifadhi kutokana na waliozikwa kwenye ardhi yake ikiwa ni pamoja na watu wa nyumbani kwa Mtume S.A.W. na waja wema wenye kufahamika na idadi kubwa ya Mawalii, zimekuja Hadithi na athari kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Anawalinda waja na nchi kwa baraka za waja wema wakiwa hai au wakiwa wamefariki.
Imetokana na Ibn Jarir na Ibn Adiy kutoka kwa Ibn Umar R.A. amesema: Amesema Mtume S.A.W: “Hakika Mwenyezi Mungu hulinda balaa kwa Mwislamu mwema mmoja zaidi ya watu wake mia moja na pamoja na majirani zake”. Kisha Ibn Umar R.A akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watu basi dunia ingeliharibika} [AL BAQARAH; 251].
Imetokana na Hafithi Ibn Asakir katika kitabu cha [Tabyiin kadhbu Al-Muftary kutoka kwa Abi Said Al-Khudriy] R.A. amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Hakika Mwenyezi Mungu humlinda Muumini na watoto wake na vizazi vyao, na humlinda Muumini pamoja na majirani zake”.
Imepokelewa pia katika kitabu hicho cha Tabiin kutoka kwa Anas Ibn Malik R.A amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Hakika Mwenyezi Mungu humlinda mja mwema na watu wake na watoto wake na wanaomzunguka”.
Imetokana na Ibn Hajar na Abu Sheikh katika kitabu cha Tabaqat Al-Muhaddithiin na Ibn Mardawiih kutoka kwa Jabir R.A. amesema: Amesema Mtume S.A.W.: “Hakika Mwenyezi Mungu Anafanya wema kutokana na wema wa mtu mmoja Mwislamu kwa watoto wake na watoto wa watoto wake pamoja na watu wanaomzunguka wataendelea kuwa katika hifadhi ya Mwenyezi Mungu maadamu yupo nao”.
Na imepokelewa na Ibn Aby Hatim kutoka kwa Ibn Abbas R.A. ikiegemezwa kwake kauli yake.
Na imetokana na Ibn Al-Mubarak katika kitabu cha mambo ya Zuhdi na Abdulrazik na Ibn Aby Shaibah katika kitabu cha Al-Musannif na Ibn Al-Jaad katika Musnad na Al-Hamidy katika Musnad pamoja na Al-Balaadhury katika kitabu cha Ansaab Al-Ashraf, na Abu Naeem katika Haliyatul-Auliyaau na Ibn Asaakir katika Tabiin Kadhbu Al-Muftary kutoka kwa Muhammad Ibn Al-Munkir R.A kauli yake.
Na tamko la Al-Hamidy: “Hakika Mwenyezi Mungu huwalinda kwa ulinzi wa mtu mmoja mwema watoto wake na watoto wa watoto wake na wanaomzunguka wakiendelea kuwa katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na sitara yake”.
Tamko la Abi Naeem: “Wanaendelea kuwa katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu kipindi chote anachokuwa pamoja nao”.
Ama kulima kwa lengo la kutaka kubadilisha eneo hili na kuwa la kijani si katika jambo muhimu sana na wala si katika jambo lenye kuhitajika sana na kufikia kiwango cha kuwa ni dharura kufanyika, kwa sababu linalokuwa katika nafasi ya udharura: Ni sehemu inayofungamana na kulinda moja ya makusudio matano ya Sharia, ambayo ni: Kuinda Dini, nafsi, akili, heshima na mali, ambapo ikiwa halijafanyika, basi litapotea moja ya makusudio haya au kuharibika.
Ama uwepo wa haja: Ni kinachokosekana kwa upande wa upanuzi na kuondoa kero inayopelekea mara nyingi kuleta tatizo kwa waliopo kwa kupitwa na mahitaji, ikiwa halitaangaliwa basi hupelekea tatizo kwa mwenye jukumu.
Kugeuza eneo la makaburi na kuwa la kijani hakuendani na amri ya kulinda moja ya Makusudio matano ya Sharia kwa kukosekana moja ya makusudio ikiwa halijafanyika hilo, vilevile haliendani kuachwa kwake kupatikana matatizo kwa watu, ikiwa tutachukulia kuwa ni katika jambo la dharura au lenye kuhitajika sana basi si kuainisha, kwa sababu inawezekana kupanda miti eneo lengine lisilokuwa hili ambapo lengo litafikiwa, bali inawezekana kupanda miti eneo hili na kuendelea kubakia makaburi pasi ya kuhitajika kuondolewa, hata eneo la wazi lenyewe linawezekana kupanda miti, na inakuwa katika hili ni kupunguza adhabu na rehma kwa maiti Waislamu, kwani imepokelewa na Masheikh wawili Bukhar na Muslim kutoka kwa Ibn Abbas R.A. amesema: “Siku moja Mtume S.A.W. alipita kwenye eneo lenye makaburi mawili na akasema: Hakika maiti hawa wanaadhibiwa na wanaadhibiwa si kwa kufanya kosa kubwa, kwani mmoja wao alikuwa hajistiri wakati wa haja ndogo, na mwengine alikuwa msengenyaji, kisha akachukua tawi bichi la mti wa mtende na kulichana sehemu mbili kisha akapandikiza kila moja kwenye kaburi. Masahaba wakauliza ni kwanini Mtume S.A.W. umefanya hivi? Mtume S.A.W. akasema: Huenda wakapunguziwa adhabu kabla hayajakauka”. Na Buraida Al-Aslamiy R.A aliusia kwenye kaburi lake yawekwe matawi mawili mabichi ya mtende.
Amesema Al-Hafidh Ibn Hajar Al-Asqalaniy katika kitabu cha: [Fat-h Al-Baariy 1/320 chapa ya Dar Al-Maarifa]: “Imesemwa kuwa: Maana ya hilo ni kuwa matawi hayo ya mtende humtakasa Mwenyezi Mungu kipindi chote bado hayajakauka, hivyo hupatikana punguzo la adhabu kwa baraka ya utakasaji huo, na kwa maana hiyo ndiyo huwekwa kila kilichokibichi katika miti na isiyokuwa miti”.
Amesema Imamu Ibn Hajar Al-Haitimiy katika kitabu cha: [Tuhfat Al-Muhtaaj 3/197 chapa ya Dar Ihayaa Turath Al-Arabiy]: “Ni Sunna kuweka au kupandikiza tawi bichi kwenye kaburi ... kwa sababu hupelekea kupunguziwa adhabu maiti kwa baraka za tasbihi au utakaso unaofanywa na tawi bichi, kwani ni katika tasbihi kamilifu zaidi za vitu vikavu, na pima hilo na ile iliyozoeleka upandikizaji wa miti ya raihan yenye harufu nzuri na mfano wake”.
Amesema Mwanachuoni Ibn Muflih Al-Hanbaliy katika kitabu cha: [Al-Furuu 2/306 chapa ya Aalam Al-Kutub]: “Ni Sunna kinachopunguza adhabu - kwa maana ya: Maiti - ikiwa atapata kero kwa uovu basi atanufaika na kheri, na wakasema pia wengine. Uwazi wake: Ni kuweka angalau tawi bichi kwenye kaburi, kutokana na Hadithi, na Buraida aliacha wasia - kama ilivyotajwa na Imamu Bukhari - maana yake: Ni kupanda kitu chengine”.
Ama eneo kuwa lina wahalifu wengi na kupiga kambi hapo na kama tutawaacha basi tunasema: Hakika kudhibiti uhalifu na kutokomeza wahalifu hakuna shaka kwenye umuhimu wake, bali na wajibu wake, lakini kuondoa makaburi sio njia itakayosaidia kufikia hilo, kwa sababu linaweza kufikiwa na serikali kwa njia nyengine, kama vile kuzuia ukazi kwenye makaburi, au kuweka utaratibu ambapo hautaruhusu isipokuwa kupanda miti tu kwa mfano, na wala sio kuondoa eneo kikamilifu kuwa ndio ufumbuzi bora zaidi wa kuthibiti uhalifu na kuwabana wahalifu, kinyume na hivyo basi kila eneo likizidi viwango cha uhalifu - ikiwa tutaacha - basi yawezekana kukatakiwa kuondoa makaburi, wakati ambapo uthibiti wa viwango unakuwa ni kwa kutekeleza sheria kuadhibu wahalifu na kufanya kazi ya kuwarekebisha na mfano wa hayo.
Ama madai kuwa baadhi ya Wanachuoni wamepitisha kuhamisha maiti, hilo si kwa sura ya moja kwa moja, kwani katika Wanachuoni waliopitisha kuhamisha maiti baada ya kuzikwa wamepitisha kwa masharti, ikiwa masharti hayatakamilika basi amri ya kuzuia inabaki pale pale, yakuzingatiwa kwenye matamshi yao tunakuta kuwa wao wote wameanza na asili ya kuzuia kuhamisha maiti, na kitendo cha kufaa kuhamisha kwa upande wao ni jambo la kuzuka tu halizingatiwi isipokuwa ni katika hali ya dharura, kisha wamezingatia dharura katika wigo mwembamba sana, kama vile Wanachuoni wa Imamu Abu Hanifa na Imamu Shafiy, na kwa wigo mwembamba zaidi kama vile Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Malik na Imamu Hanbal, vile vile inazingatiwa katika maelezo yao yote kuwa inafungamana na kuhamisha mwili wa mtu mmoja na wala si miili ya wengi ambapo itakuwa ni wigo mwembamba zaidi bila shaka yoyote.
Amesema Imamu Al-Haswkafy katika kitabu cha: [Al-Durru Al-Mukhtaar] miongoni mwa vitabu vya Masheikh wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa [ 2/237, 238 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] - na Hashiyat Ibn Aabideen: “Wala hatolewi humo - kwa maana: Maiti -baada ya kufukiwa na udongo isipokuwa kwa haki ya kibinadamu kama vile kuwa ardhi aliyozikiwa imeporwa au imepatikana kwa kuomba, hupewa hiyari mmiliki wake kati ya kutoa mwili wa marehemu na kuwekewa sawa ardhi yake”.
Amesema katika kitabu cha [Al-Minhaaj] na kushereheshwa na Mwanachuoni wa vitabu vya Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Shafiy 1/412 chapa ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiya: “Kumfukua - kwa maana ya maiti - baada ya kufukiwa kwake ili kuhamishwa ni haramu isipokuwa kwa dharura, kama vile awe amezikwa bila kuoshwa, na kuoshwa ni katika mambo ya lazima, basi itapaswa kufukuliwa ili aweze kutimiziwa wajibu wa kuoshwa ikiwa mwili bado hauja haribika, amesema kwenye sherehe ya Al-Muhadhib: Na kumsalia, amesema: Ikiwa ameshabadilika na ikahofiwa kuharibika kwake basi haifai kufukuliwa, kwa kuwepo ndani yake ukiukaji wa heshima yake, au sehemu ya ardhi au nguo kwa maana ya sanda ni vya wizi au uporaji, ni lazima kufukuliwa hata kama mwili utakuwa umeshaharibika, ili ipate kurudishwa haki kwa mwenyewe ikiwa hatoridhia kubakia kwa marehemu”.
Amesema Ahmad Ad-Dardiir katika kitabu cha: [Sharh Al-Kabir Alaa Mukhtasar A-Khalil ni katika vitabu vya Masheikh wa madhehebu ya Imamu Malik 1/421 – pamoja na Hashiyat Al-Dusuqy - chapa ya Dar Al-Fikr]: “Inafaa kuhamisha maiti kabla ya kuzikwa vilevile baada ya kuzikwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine kwa sharti la kutoharibika wakati wa kumhamisha kwake na kutokiuka utukufu wake, na jambo hilo liwe ni kwa masilahi, kama vile kuhofia hapo alipozikwa kaburi lake lisije kufukuliwa na maji ya fukwe ya bahari, au kwa matumaini ya baraka ya eneo analohamishiwa, au ili azikwe karibu na ndugu zake, au kwa sababu ya ukaribu wa kutembelea ndugu zake”.
Amesema Mwanachuoni Al-Dusuqiy katika Kitabu chake akielezea: “Ikiwa litakiukwa sharti katika masharti haya matatu basi kuhamisha mwili wa marehebu litakuwa ni jambo haramu”.
Amesema pia 1/428 kwenye kauli ya Khalil: Kaburi ni kizuio: Kwa maana: Cha kuzikia, ikiwa mwili utaondolewa humo au ukaoza halitumiki zaidi ya kuzikia”.
Imekuja katika kitabu cha: [Sharhu ya Minhaj Al-Iraadat katika vitabu vya madhehebu ya Imamu Hanbal 1/378, 379 chapa ya Aalam Al-Kutub]: “Wala si halali kufukuwa kaburi la Mwislamu pamoja na kubakia mwili wake isipokuwa kwa hali ya dharura, kama vile kuzikwa kwenye eneo la miliki ya mtu mwengine pasi na ruhusa yake, au kuzikwa na sanda ya wizi hapo litafukuliwa na kuchukuliwa vilivyo baki ili kurudishwa kwa mwenyewe, ikiwa kutakuwa na ugumu basi atalipishwa katika mali yake aliyoacha, na kama si kwa sababu hizo basi halifukuliwi ili kuepuka kuvunja utu wake pamoja na uwepo wa uwezekano wa kuondoa madhara pasi na kufukua ... inafaa kufukua maiti kwa malengo sahihi kama vile kukafiniwa vizuri ... inafaa kufukuliwa ili kuhamishiwa eneo lengine zuri na lililo jirani”.
Ama kutumia makaburi yaliyopitwa na muda mrefu si lenye kuendana na hali ya muhusika wake, kwa sababu makaburi ya Kairo yanayokusudiwa kuhamishwa si yaliyopitwa na muda mrefu kwa inavyokusudiwa, kwa sababu kusudio la kupita muda mrefu ni kitu kukanyagwa sana na kufutika athari yake, lakini yenyewe hayapo hivyo.
Ama madai kuwa maamuzi ya kuhamisha ikiwa yatatoka kwa mkuu wa nchi inakuwa ni lazima kutekelezwa, kwa sababu mkuu wa nchi ana mamlaka ya kuipangilia ruhusa.
Jibu:
Ni kuwa hili si halali, na kiongozi kuwabebesha watu kitendo cha haramu au chenye kuchukiza si katika upande huo.
Amesema Imamu Al-Suyuty katika kitabu cha [Al-Ashbah Wan-Nadhair ukurasa wa 121 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Kanuni ya tano: Kiongozi mkuu anaweza kuwa na maamuzi aliyopewa kwa raia kwenye mambo yenye masilahi, kanuni hii ameielezea Imamu Shafiy, na akasema: Nafasi ya Kiongozi kwa raia ni kama nafasi ya mlezi na msimamizi wa mayatima ... miongoni mwa maelezo hayo: Ni pamoja na aliyoyasema Al-Maaruudy kuwa haifai kwa yeyote katika wazimamizi wa mambo ya watu kumtanguliza Imamu kwenye sala mtu fasiki - hata kama Swala yetu itafaa kuswali nyuma yake - kwa sababu kitendo hicho kinazingatiwa kinachukiza, na msimamizi wa mambo ya watu ni mwenye kuamrishwa kuchunga masilahi, wala hakuna masilahi kuwabebesha watu kitendo chenye kuchukiza”.
Tunasema kuwa: Haya makaburi ni sehemu ya utambulisho wa Umma na nguzo ya historia yao, sehemu kubwa ya historia inazingatiwa ni moja ya alama za historia ya Kairo ya utawala wa Fatimiya, Mamluki na Uthman, jambo linalofanya kuwa ni urithi wa sanaa ya ujenzi ya kihistoria ni lazima ihifadhiwe, na kufanywa kuwepo kwake kunafungamana na makubaliano pamoja na mikataba ya kimataifa inayoelezea kuzuia kubomoa athari kama hizi, kwani nchi nyingi duniani zenye sifa ya maendeleo na kupiga hatua kubwa za mambo ya ustaarabu kunapatikana makaburi yao kati kati ya Miji yao au pembezoni mwake bila ya aibu yoyote bali yenyewe ni maeneo ya kutembelea na ni katika alama za uzuri ndani ya hizi nchi, hivyo makaburi ya watukufu yanapatikana sehemu nzuri katika eneo la Montmartre ambalo ni moja ya maeneo yanayopatikana kati kati ya Mji mkuu wa Ufaransa Paris, nalo ni eneo la utalii maarufu huko, ambapo linapokea idadi kubwa wabobezi wa fasihi na sanaa, vilevile makaburi Highgate, Brompton na Kensal huko London, vile vile huko Washington Mji Mkuu wa Marekani ambapo kunapatikana makaburi Congress ya kihistoria, na makaburi ya Glenwood, makaburi ya Oak hill ambayo yanapatikana katika eneo la Georgetown ambalo ni katika maeneo mazuri sana ya Mji wa Mkuu wa Marekani, katika Mji wa Roma pia kuna mkusanyiko wa makaburi ya kihistoria, makaburi ya Watawa Capuchin Crypt, ambapo panazingatiwa ni sehemu ya mvuto wa utalii.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: Sisi tunaona kuwa kuhamisha makaburi ndani ya Mji wa Kairo na kuyapeleka maeneo ya pembezoni mwake au nje kabisa ya Kairo ikiwa zoezi hilo litafanyika kabla ya muda ambao unafahamika na watu wenye uzoefu kuwa kwa muda huo haiwezekani mwili wa maiti uwe umeshabadilika na kuwa udongo basi inakuwa haramu kuhamisha, ikiwa baada ya muda huo: Basi ikiwa ni eneo lenye kumilikiwa na mtu mwingine - awe mtu binafsi au taasisi - basi limewekwa sharti la ridhaa yake kuuza au kubadilisha kinyume na ridhaa yake pia ni haramu, wala haifai kwa serikali kuwalazimisha kuuza au kuyaacha pasi na ridhaa yao, huondolewa makaburi ya Wanachuoni Mawalii na Waja wema kwani haifai kabisa kuchimbua makaburi yao kwa lengo la kuhamisha hata kama tutachukulia wamiliki wa sasa wa haya makaburi wameridhia kuchukua fidia serikalini. Na yale yaliyowekwa wakfu kama vile makaburi ya Mukattam haifai kutumika zaidi ya kazi za kuzikia, kisha kitendo cha kupendezesha maeneo haya na kupanda miti pamoja na kuyafanya ya kijani ni jambo zuri na linahimizwa, vilevile kuyasafisha kutokana na wahalifu ni jambo la lazima, na inawezekana kufanyika yote haya pamoja na kulinda sura ya Makaburi hayo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
17/08/2010

 

 

Share this:

Related Fatwas