Mfumo Ulioonyooka wa Kufikiri kwa ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mfumo Ulioonyooka wa Kufikiri kwa Mtazamo wa Kiislamu.

Question

 Ni zipi Sifa Maalumu za Mfumo wa Kufikiri Kiislamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kufikiri ni neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake aliyowapa. Na katika kushukuru Neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuzizungumzia. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie.
(¹) Na anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, S.A.W: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kuona Athari ya Neema zake kwa Mja wake( ). Na amesema Kuhusu kupunguza Swala – kisha Kauli yake ikawa ni Msingi endelevu: [ Sadaka aliyoitoa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Waja basi ipokeeni Sadaka yake.] ( )
Na Dalili ya kwamba kufikiri ni Neema na sisi tumeamrishwa kwayo katika Maisha yetu yote na ni ndani ya Qur`ani Tukufu, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.( )
Kwa hivyo, mfungamano uliopo kati ya kufuata Maamrisho na kuacha Makazo katika Akida, Sheria na Maadili, na kati ya Kufikiri ambako ni Msingi wa Kufahamu .
1 – Na Kufikiri: ni kupangilia maelezo anayoyatumia Mtu kukifikia kisichojulikana. Na mambo yanayojulikana yanakuwa katika sura ya Jumla inayoeleweka, fikra inakusanya jumla na jumla nyingine na kuzifungamanisha baina yake pamoja na kutoka na matokeo ya jumla hizo, na kila Jumla yenye maana inaweza ikawa inaelezea uhalisia na inaweza ikawa inaelezea ombi. Na Kufikiri kulikonyooka, huanzia katika kutafiti jumla inayoulezea uhalisia na inachukua katika kuthibitisha usahihi wake, na kama sio hivyo basi fikra itaelekea kuwa ngano na haitanyooka. Na kila jumla yenye maana ina nyanja zake, na kila nyanja zina njia zake za kuzithibitisha, na dalili inayotilia mkazo usahihi wake, na vigezo vya kukubalika au kutokubalika kwake.
2 - Na kuna mambo hurejea katika hisia na majaribio, kama vile jumla ya : Moto unaunguza, jua limechomoza. Na Dalili ya mambo haya huwa kwa kudiriki kihisia, au kwa maelezo yenye mlolongo wa mapokezi yake na kuaminika kwake, na kuna mambo mengine hurejea katika akili kama vile ukweli wa mahesabu, na kuna mambo yanayorejea katika Kunukulu kama vile sheria za lugha, hukumu za Sheria ya Kiislamu, na vyote hivyo vinahitaji Mfumo au njia ya kujaribu na kufuatilia matokeo yake na matokeo
3 – Na miongoni mwa sura za kwenda mrama na Fikra iliyonyooka ni sisi kutafuta dalili katika suala la kiakili katika Nukulu, au suala la hisia katika akili, au suala la kunukulu katika hisia, na kinachoyadhibiti yote hayo ni Elimu, na Elimu katika lugha ya Kiarabu haiishii tu katika maana iliyotafsiriwa kutokana na neno sayansi ambalo linamaanisha elimu ya kujaribu kwa vitendo tu, bali lina maana ya kiasi ainishi cha maarifa; na kwa hivyo inatofautishwa baina ya Elimu yenye Uhakika na Elimu yenye Dhana na mipaka ya kila moja kati ya aina hizi mbili za elimu inajulikana. Na kwa hivyo, kuchanganya baina ya aina mbili za elimu ni katika mionekano ya fikra iliyopinda, na kuchanganya baina ya Nyanja za Hisia, Akili na Kunukulu na kutopambanua baina yake ni katika mionekano ya fikra zilizopinda vile vile, na kupita katika njia yenye mabonde bila ya kuweka wazi namna ya kunufaika na kila nyanja; kwani hiyo inawakilisha uhalisia Maisha miongoni mwa Mionekano ya huo mfumo wa fikra iliyopinda, na kuchukia Nyanja kwa ajili ya Nyanja nyingine za mionekano ya fikra iliyopinda vile vile.
4 - Fikra iliyopinda hutupeleka katika hasara na akili iliyokengeuka, na hutupeleka katika mfumo wa uongo ambao unamaanisha kwenda kinyume na uhalisia au kwenda kinyume na uhalisia pamoja na Itikadi; na kwa ajili hiyo Uongo katika Lugha ya Kikureshi, umepewa maana ya kosa, kama alivyosema Mtume S.A.W, katika siku ya Ufunguzi wa Makka: "Saad alisema Uongo" aliposema Saad bin Ibaadah: Leo ni siku ya Mapambano ya Kivita. Mtume S.A.W, akasema: "bali leo ni siku ya Huruma" na amedanganya hapa maana yake amekosea kwa alichokisema, na Mtume S.A.W, akamvua cheo cha uongozi, na kumteua nafasi yake Mwanae Kais.
Hakika fikra iliyopinda humfanya mtu aishi katika mambo ya kufikirika, na inapoenea na kusambaa fikra hii basi mambo huenda kombo, na hiki huwa kizuizi kikubwa sana cha maendeleo ya binadamu na Ubunifu wa kibinadamu pia, na kusonga mbele na kuongoza, lakini pia kwa Elimu na jinsi ya kujipatia Nguvu, na ikiwa hivyo basi kila jaribio la marekebisho litakwama na kitakachoenea ni mambo ya hovyo na uholela.
5. Na ikiwa tutalinganisha hali yetu na mawazo yaliyonyooka na fikira potofu na hali ya mababu zetu; Ambapo Ustaarabu ulijengwa na kumnufaisha mwanadamu kila mahali – tungegundua kwamba wao walikuwa wanatumia Fikra iliyonyooka na wakapambana na Fikra potofu kwa nguvu zote. Na ikiwa tutailinganisha hali yetu katika hayo na hali ya Ustaarabu wa Magharibi, tunaona pia kwamba na wao walipambana na fikira potovu na kuikataa, na moja ya dhihirisho la kukataliwa kwake ni suala la Ubobezi na Kuwa na Marejeo. Na hakika wao waliuamini Ubobezi na Kuwa na Marejeo, na hivi sasa ule Ubobezi wa mtu kujua kila kitu na ambao ulienea katika Utamaduni wa Kienyeji, haupendwi tena au hata njia yake pia haipendwi, bali mtu wa aina hiyo anazingatiwa kuwa amepindukia katika ushamba na kuporomoka kimaadili. Na uwongo kwa watu hawa – iwe kwa mababu zao au kwa Magharibi – unawakilisha thamani hasi ambayo wale wanaoifanya watawajibika katika ngazi zote, na kusema uwongo ni kosa la jinai anapofanya hivyo afisa au mtu mwenye jukumu la kuwahudumia watu.
6 - Chini ya wazo la kuheshimu Marejeo, pametofautishwa kati ya Ukweli na Maoni. Hakuna maoni juu ya mambo ambayo yanahitaji uzoefu na hisia. Maoni yanatumika katika kuyashughulikia maswala ya Umma, na inakuwa katika nyanja zinazotegemea maoni, iwe kutoka kwa Wabobezi au kutoka kwa wengine kwa ujumla wenye kuyaangalia kwa kina pamoja na waandishi.
Na maoni – ili yaheshimiwe – lazima yaasisiwe kwa msingi wa fikra ilioyonyooka, na lazima pia yawe na maslahi na faida kwa umma. Na iwapo maoni hayo yatatoka katika fikra nyoofu au yakawa yanabeba Shari na Uharibifu basi hayakubaliki na yatarejeshwa kwa muhusika, yatatengwa na lazima kujiepusha nayo. Inaonekana kwamba mambo haya ya kweli na mepesi, ambayo watu wote wanakubaliana juu yake, ni vigumu mno kwa watu wengi kuyafuata, na hawawezi Isipokuwa tu kuelekea katika ukorofi wao wa kifikra na kujikweza kwao kikazi kwa sura mbaya sana ambayo inakosa uaminifu wa Neno na mtindo wa mazungumzo unaporomoka pamoja nayo.
7 – Hakika ung’ang’anizi wa kufuata Fikra zilizopinda na kuziingilia bobezi mbalimbali kwa sura inayokusanya baina ya ujinga na kiburi – lazima kupigwe vita kimfumo, kuanzia Mitaala ya Elimu mpaka kwa Wataalamu; mpaka turejee katika matumaini ya kuleta mabadiliko ya hali zetu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
( )Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake. Sisi tunapaswa kutambua kwamba Fiqhi ya Kiislamu ni Elimu miongoni mwa Elimu mbalimbali, ambayo Wanachuoni wameieleza kuwa: Ni Elimu ya kujua Hukumu za Kisheria za Kiutendaji zinazopatikana kutokana na Dalili zake Fafanuzi. Nayo ni Elimu yenye masuala yake na Mfumo wake na pia ina vifaa vyake na vyanzo vyake vya kuchotea yanayodurusiwa, lakini pia ina vitengo vyake vya Kifikra na Elimu zake zinazoisaidia, na ina faida zake na matokeo yake, na kwamba Elimu hii sio njia ya anayoipitia kila mwenye kutaka, au akafikiria bila ya kutegemea Elimu hii. Hii ni Elimu ambayo haiutambui ubaguzi na haiutaki; na kwa hivyo, kila mwanaume au Mwanamke, mweusi au mweupe anaweza kufuata njia ya Elimu hii, lakini haijuzu kwake kwa namna yoyote iwayo, kuchupa mipaka yake na aseme asiyotakiwa kuyasema, sio katika Uhuru kuipinga Elimu ya Sayansi ya Kemia kwa mafanikio yake makubwa yaliyofikiwa na Wataalamu wake katika Mifumo yake na Vyombo vyake, na si katika Uhuru kuingilia mambo ya tiba na kuzipinga rai za watu ndani ya Elimu hii, bali hili ni zao la Akili ya Kingano ngano inayoikokota Elimu na kuipeleka katika Mionekano ya awali, Utashi, Matamanio na Mitazamo.
Na Fiqhi ni moja kati ya Elimu nyingi nyingine; na Mtu yoyote atakayeitumia kwa njia hii, atakayeujua ukweli, atajikuta katika hali ya kicheko kilichochanganyika na kilio, basi hakika Shari ya msiba mkubwa ni kile kinachochekesha. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
( ) Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya wazi na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua.
Na onyo lake Mwenyezi Mungu Mtukufu likawa kali zaidi Kwetu kutokana na Njia hii iangamizayo, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
( ) Basi ni nani aliye dhaalimu zaidi kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu na akazikanusha Ishara zake? Hakika hawafanikiwi wakosefu.
Chanzo: Kitabu cha Simaatul Aswri, cha Samaahat Mufti wa zamani wa Misri, Dkt Ali Juma.

Share this:

Related Fatwas