Uangazaji kwa Mtazamo wa Fikra ya K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uangazaji kwa Mtazamo wa Fikra ya Kiislamu

Question

 Kuna mazungumzo mengi juu ya Uangazaji katika Jamii ya Wanachuoni wa Kiislamu. Je, hii inamaanisha nini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1. Neno hili liliibuka kuanzia katika mawazo ya Magharibi, na lina dhana maalumu ndani yake ambayo inaelezea enzi maalumu ya kukua kwa fikra ya Kimagharibi, na wakati watu wa Magharibi wanapotaja fikra ya Uangazaji, hakika wao wanamaanisha wazo maalumu lililooneshwa na wanafalsafa maalumu wakati wa hatua maalumu ya kukua kwa fikra ya Kimagharibi katika karne ya kumi na nane BC, na kwa sababu hii, Uangazaji ni neno lenye asili ya Magharibi, kimaoni na yaliyomo ndani yake, na kwa sababu hii, Kamusi ya Falsafa iliyotolewa na Taasisi ya Lugha ya Kiarabu, iliielezea kama: Neno hili ni "Maudhui ya kimuundo ya kiakili ambayo inawakilisha vuguvugu la kifalsafa katika karne ya kumi na nane ambayo inaheshimu Akili na Uhuru wa maoni, na inaamini athari za maadili mema, na inategemea mawazo ya Maendeleo na kuwa huru mbali na mamlaka pamoja na mila na desturi", na yanaposemwa maneno haya katika jamii ambayo mamlaka ndani yake yalikuwa ya Kikanisa na Kikuhani, Kidini, Kitheolojia, na mila na desturi ndani yake, zilikuwa za Kikanisa, kwa hivyo maana hasa ya maneno haya ni kwamba Uangazaji wa Kimagharibi ulimaanisha kujikomboa na kuwa mbali na Dini ya Kikristo kwa wakati huo wa Historia, na kwamba ilikuwa vuguvugu la kiakili la kukomboa Serikali na Maoni viwe mbali na Dini, Kanisa na Theolojia. Kwa hiyo Uangazaji huko Ulaya ulikusudiwa kufichua giza ambalo Zama za Kati za Ulaya zenye Giza tetere, zilikuwa zikiishi ndani yake, wakati ambapo Sisi tulikuwa katika utukufu zaidi wa zama zetu, na ndio sababu inaweza kuonekana kuwa watetezi wa Uelimishaji kwetu sisi kwa maana ya Kimagharibi sio Waelimishaji, lakini ukweli ni kwamba wao ni Watia giza.
2. Baadhi ya watetezi wa Uangazaji kwa maana ya Kimagharibi walisema kwamba "Uangazaji” unamaanisha kuwa hakuna mamlaka juu ya Akili isipokuwa Akili," na kwamba "ni kutoka katika Ngano za kale na kuelekea katika Akili," kwa jinsi ilivyo katika dhana hii ni kwamba hakuna Siri, hakuna Ufunuo, hakuna Sheria, na hakuna Dini. Na kinachomaanishwa kwa neno Ngano za Kale ni Dini. Haimaanishwa hapa Dini ya Uislamu peke yake, bali Uangazaji wa Kimagharibi ni dhidi ya Dini zote, dhidi ya Ufunuo wote, na dhidi ya Imani yote na ni dhidi ya Jumbe zote za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kiasili, Mizizi ya Uangazaji wa Kimagharibi kwa kweli unarejea kwa Francis Bacon katika karne ya kumi na saba, ambaye aliupinga uingiliaji wa Dini katika maarifa kwa sababu Dini inaweka mipaka ya kila aina ya Maarifa. Na Bacon akatoa wito wa kwamba miungu ya Uangazaji ambayo ni (Akili, Elimu na Falsafa) inapaswa kuchukua nafasi ya Mungu na Dini. Na hii ndio sababu tunaweza kusema kuwa Uangazaji wa Kimagharibi, tangu mwanzo – na kama matokeo ya mambo ya kitamaduni ya Magharibi – ilichukua msimamo wa kuipinga Dini, na kwa mwelekeo huo huo, vigogo wa Uangazaji wa Kimagharibi, kama vile Voltaire (1778 AD), Rousseau (1778 AD), Montesquieu (1766 AD), Lessing (1781 AD), na Schlier (1805 AD), na Goethe (1832 AD), Na Kant (mwaka 1804 AD), na mawazo ya Voltaire, kwa mfano, yalitokana na kutukuzwa kwa Akili badala ya utakatifu wa Dini, kulipiga vita kanisa, kuyakana mambo yasiyoonekana, Ufufuo na Malipo, vyote viwili vikiwa vya Akhera, na nafsi sio kitu chochote isipokuwa ni uhai wa mwili, na hakuna ufunuo mtakatifu isipokuwa maumbile. Hiki ndicho chanzo cha Uangazaji na maana yake kwa Wamagharibi.
3 Inaonekana kwa yaliyotangulia kwamba haiwezekani kuihamishia dhana hii ya Kimagharibi katika Ustaarabu wetu wa Kiislamu kwa sababu ya tofauti kubwa na ya kina kati ya Staarabu mbili, na pia kuna tofauti kubwa kati ya sababu za mgogoro na mahitaji ya uamshaji wa maendeleo hapa na pale, na kwamba ni makosa kutumia neno Uangazaji katika jamii zetu za Kiislamu kwa sababu lina mkanganyiko , pia inahitajika kufafanua mkanganyiko uliopo kati ya usekula na sayansi, kwani watu wanachanganya viwili hivi, na wale wanaosimama dhidi ya Usekula huwa wanakuwa kana kwamba wanasimama dhidi ya Sayansi, na hii sio kweli, na Usekula kwa kweli ni suluhisho la Magharibi la Tatizo la Kimagharibi, na kinakusudiwa kuingizwa katika mazingira ya Kiislamu ambayo hayana uhusiano wowote na Tatizo hilo na wala kwa kuwa kwake suluhisho la Kimagharibi.
4 Kwanza kabisa, Uangazaji katika lugha yetu ya Kiarabu ni neno linalomaanisha wakati wa mapambazuko ya asubuhi, na Mungu Mwenyezi anakisifu Kitabu chake kama nuru {Na tumekuteremshia nuru iliyo wazi} [An-Nisa: 174], {Na nuru imekujieni kutoka kwa Mungu na Kitabu kilicho wazi:] [Al-Ma'idah: 15] Na anasema Mtume S.A.W: ((Swala ni nuru). Imehadithiwa na Muslim (H 656), Kwa hiyo muumini kwa Swala hiyo anapata nuru, na ana yeye nuru yake mwenyewe ya Kiislamu, na katika mfumo huu wa Kiislamu kunakuja juhudi za Wanachuoni wakubwa (Mujadiduun) wenye kuleta Upya na mageuzi makubwa kama vile Tahtawi, Al-Afghani, Muhammad Abdu, Saad Zaghloul, Muhammad Husayn Haikal, Taha Hussain, na wengineo, ambao, ikiwa sisi tutaipitia misimamo yao na maandishi yao, tunapata kuwa wako mbali na dhana ya Uangazaji kwa maana yake ya Kimagharibi, na wanazingatia uzingatiaji mkubwa wa maadili ya Ustaarabu wa Kiislamu Ulionyooka.
5 Mwanachuoni Twahtwaawiy, katika kitabu chake cha Fii Takhliis Al-Ebriz, anakanusha kwamba Ustaarabu wa Magharibi unarejea tu katika dalili za Kiakili na sababu za kimaumbile peke yake, na anasema: "Hatuzingatii utoaji wa maamuzi ya uzuri au ubaya Kiakili tu isipokuwa kama hayo yatatajwa ndani ya Sheria. Hii ndio sababu Tahtawi anatofautisha kati ya Elimu ya Kutamaduni kimaendeleo na Falsafa za Magharibi, ambazo, kulingana na yeye, ni "kujazwa jazwa upotoshaji unaopingana na vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu Mtukufu." Kwa hivyo, anazungumzia kutokuamini Mungu na kutokuwa na Dini katika Ustaarabu wa Magharibi, na anashangaa ni kwa jinsi gani zinachanganywa elimu za kiraia na aina hizi za kutokuamini Mungu ((na anasisitiza uboreshaji wa sababu za kimaumbile haizingatiwi isipokuwa ikiamuliwa na Sharia. Na Majukumu ya Kisheria na ya Kisiasa ambayo yamo kwenye mfumo wa Ulimwengu uliowekwa kwa ajili ya kuwajibisha kwa kutumia Akili Sahihi isiyokuwa na makatazo na tatanishi, kwa sababu Sharia na siasa vyote viwili vinajengeka kutokana na hekima inayokubalika kiakili kwetu au kwa njia ya Kiibada ambayo hekima yake anaijua Mwenyezi Mungu Mtukufu, na sisi hatutakiwi kutegemea kile kinachoonwa na akili kuwa ni kizuri au kibaya, isipokuwa Sharia inaposema hivyo. ”Kwa hivyo umbali ulioje wa maneno haya ya Twahtawi na yale ya Waangazaji wa Kimagharibi ambao wanaona kwamba" hakuna mamlaka juu ya Akili isipokuwa Akili "
6 Mojawapo ya maandishi yenye nguvu zaidi ya Twahtwawi kuonesha msimamo wake wa kweli ni kusema kwake: ((Kinachoongoza utakaso wa roho ni sera ya Sharia, na marejeo yake ni Kitabu Kitukufu, ambacho kinakusanya aina za yanayotakiwa miongoni mwa yale yanayokubalika Kiakili na yale ya Kunukuliwa, pamoja na ubainifu wa Sera zinazohitajika katika mfumo wa viumbe, kama vile Sheria ya makatazo yapelekeayo ulinzi wa Dini, Akili, Nasaba, Mali, na Sheria ya kile kinachokidhi hitaji kwa njia ya karibu zaidi ili kufikia kusudio Kila mchezo ambao hauwi katika sera ya Sheria hautoi matokeo mazuri, wala hakuna kuzizingatia nafsi zinazozembea, ambazo zilitumia akili zao kutoa maamuzi ya mawazo walioyapata waliyoyategemea katika kuhalalisha na kuharamisha, na walidhani kwamba walifanikisha lengo lao kwa kuchupa mipaka, kwa hivyo nafsi zinapaswa kufundishwa siasa kwa njia ya Sharia, sio kwa njia za akili tupu, na inajulikana kuwa Sharia haizuii kuleta faida au manufaa kwa watu, wala kuzuia maovu, na wala haipingi ubunifu mpya ambao unabuniwa na wale ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa Akili na akawapa uwezo wa kutengeneza.
7 Na wakati Twahtwawi alipotafsiri sheria zote za Napoleon, hakufanya hivyo ili sheria hizo ziwe Sheria za madai na kutawala katika nchi yetu kama wengine wanavyoieneza. Badala yake, anasema katika utangulizi wa tafsiri yake: ((Agizo kuu la Khedive lilitolewa kuifanya iwe ya Kiarabu ili watu wa nchi hii wajue asili ya falme zingine, na haswa kwa kuwa uhusiano wa kudaiana, na minasaba ya kupeana na kuchukua, inahitaji Misingi kama hiyo ya kutungwa ili wale wanaotangamana nao katika kusuluhisha mambo wapate kuelewa)). Na anasema katika utangulizi wa kutafsiri kanuni za kibiashara: Na kanuni hii ya Biashara inahitajika mno katika wakati huu na hasa kwa kuwa hivi sasa katika Misri yetu mzunguko wa shughuli za kibiashara na watu wa falme za Ulaya umepanuka na uhusiano umeongezeka, kwa hivyo sio vibaya kwa wamiliki wa biashara kujua sheria za biashara za wageni, lakini ni lazima kuzijua sheria hizo kwa wale wanaowekeana mikataba ya kibiashara na wageni hao)) Badala yake, aliupinga mwelekeo wa kuzitumia Sheria za Ulaya na akasisitiza kwamba (kama miamala ya Kifiqhi ingelipangwa na kutumiwa ipasavyo, basi haki isingekiukwa, kwa kuziambatanisha na wakati pamoja na hali husika. Na yeyote anayeangalia vizuri vitabu vya Fiqhi ya Kiislamu, ataona wazi wazi kwamba hazina upungufu wowote wa njia za kuwafaidisha watu wote. Na kwamba upana wa Sharia, pamoja na kuwa kwake na matawi mengi, haikuacha kidogo au kikubwa katika yale Masuala Muhimu, isipokuwa iliyaweka na iliyahuisha kwa njia zote)). Huu ndio Upya na Marekebisho katika mpango wa Twahtwawi, na kama tuonavyo, ni kwamba mpango huu hauhusiani kwa lolote na Uangazaji kwa ile dhana yake ya Kimagharibi.
8 Kuhusu Sheikh Al-Afghaniy: yeye alitoa wito wa kujenga maendeleo ya kisasa juu ya misingi ya Kimashariki, na akaonya dhidi ya kuanzia mahali Wazungu walipoishia, na kukosoa kisasa kwa mtindo wa Magharibi, na hata akaelezea watetezi wa kuanza kutoka mahali Wazungu walipoishia kama safu ya tano kuvunja ukuta wa taifa, na akasikitika sana kwa waigaji wa miji ya Magharibi bila ukuaji wa miji halisi na bila ufahamu, na akusisitiza kuwa ((uzoefu umetufundisha kuwa waigaji kutoka kila taifa, waigaji wa awamu zingine ni njia za maadui … Anawaelezea "huenda kulikuwa na watu binafsi kati yao ambao walisema maneno ya uhuru, uzalendo, utaifa na kadhalika. Wakajiita viongozi wa uhuru ... Miongoni mwao wakabadilisha hali ya majengo na makazi na kubadilisha mwonekano wa chakula , nguo, magodoro, vyombo, na bidhaa zingine ... Kwa hivyo walifukuza utajiri wa nchi yao kwa ajili ya nchi nyingine, Na waliwauwa wataalamu wao, na hii ni sehemu mbaya ya mapitio ya Umma. "
9 Kuhusu Imam Muhammad Abduh: anaelezea ustaarabu wa Magharibi kwa kusema: ((Jiji hili ni jiji la mfalme na sultani, jiji la udanganyifu na unafiki, na mtawala wake mkuu ni Pauni na Lera kwa watu wengine, na Biblia haina uhusiano wowote na hilo)), ni ajabu kwamba Sheikh Muhammad Abdu aliandika kitabu kiitwacho "Uislamu na Ukristo na Sayansi na Uraia." Wakati kitabu hicho kilipochapishwa tena, jina la asili ilibadilishwa na kuwa: "Uislamu kati ya sayansi na ustaarabu." Mchapishaji aliondosha na kubadilisha katika kitabu hicho, na kuweka makala zisizokuwa na uhusiano. Sheikh Muhammad Abdu aliandika kitabu hiki akimjibu Farah Anton katika kitabu cha ((Ibn Rushd)), ambapo Ernest Renan aliiga katika uelewa wake kwa Ibn Rushd na akamchukulia kama "Mwanafalsafa mpenda mali kama msingi wa mafundisho yake ya Maarifa." Sheikh Muhammad Abdu alijibu kwamba Ibn Rushd ni Mwanafalsafa na Muumini. Na alikataa kupitia maandishi ya Ibn Rushd mwenyewe kuwa mwanafalsafa wa kupenda mali au mtu asiyeamini kuwa kuna Mungu.
10 Kuhusu Muhammad Abdu anakosoa ukuhani na mamlaka ya kidini huko Ulaya katika Zama za Kati na kusema: ((Uislamu hautambui mamlaka hayo ya kidini ... ambayo Ulaya wanayaelezea ... Hakuna mamlaka ya kidini katika Uislamu isipokuwa mamlaka ya mawaidha mema, wito wa kutenda mema na kukemea maovu. .. na ni mamlaka ambayo Mwenyezi Mungu amewapa Waislamu wote, wa chini kabisa na wa juu zaidi ... na taifa ndilo linalochukua mamlaka, , na yeye ndiye mmiliki wa haki … Yeye ni mtawala wa kiraia katika mambo yote, na hairuhusiwi kwa mtazamaji sahihi kumchanganya Khalifa kati ya Waislamu na kile Franks wanakiita kitheokrasi, yaani mamlaka ya kimungu. Juu na mmoja wa watu hawa, kwani ni mamlaka ya kiraia iliyotanguliwa na sheria ya Kiislamu … Hakuna mamlaka ya kidini katika Uislamu kwa njia yoyote.
11 Sheikh Muhammed Abdu alizungumzia juu ya ukati na kati katika Uislamu, akisema: ((Uislamu ulionekana, sio tu kiroho, wala msimamo wa mwili, lakini ni ukati na kati ... unatoa haki inayofaa ya silika ya kibinadamu ambayo haipatikani. kwa yeyote ... Uislamu ni dini na sheria, umeweka mipaka, umeweka haki, na hekima ya sheria ya watawala haikamiliki isipokuwa kwa nguvu ya kuweka mipaka, kutekeleza hukumu ya jaji kwa ukweli, na na kuhifadhi utaratibu wa jamii. Uislamu haukumwachia Kaisari kilicho cha Kaisari, kwa hivyo Uislamu ulikuwa ukamilifu wa mtu, na urafiki ndani ya nyumba, na utaratibu kwa mfalme. “Na anasisitiza kwamba” njia ya dini kwa yule anayetaka mageuzi kwa Waislamu. Ni njia ambayo haiwezi kuepukwa, ikiwa inakuja kwa njia za adabu na hekima ambazo hazina asili ya dini, inahitaji kuanzisha kipya ambacho hakina nyenzo yoyote …)) Halafu anauliza: ((Na ikiwa dini inahakikishia uboreshaji wa maadili na matendo mema, na inasababisha roho kutafuta furaha kutoka milango yake, na watu wake wana imani nayo kile wasichokuwa nacho wengine, na iko pamoja nao, na ugumu wa kuwarudisha kwake ni mwepesi kuliko kuleta yale ambayo hawajui, basi kwa nini waache walichonacho na kukielekea kingine? Imam Muhammad Abdu anazungumza wazi juu ya maendeleo ya Kiislamu, Serikali ya Kiislamu, na Ujenzi wake, mawazo yake hayana uhusiano wowote na dhana za Uangazaji wa Magharibi..
12 Kwa habari ya Dk. Taha Hussein: Kitabu chake (On Pre-Islamic Poetry) kilichapishwa takriban miaka hamsini kabla ya kifo chake, na kitabu chake (The future of Culture in Egypt) kilichapishwa takriban miaka arobaini kabla ya kifo chake. sio kuwakilisha mradi wake wa kiakili katika ukomavu wake, bali ni mwanzo tu wa mradi.Na kwa sababu hii, wakati Dkt. Taha Hussein alipochapisha tena vitabu vyake, alichapisha vyote isipokuwa kitabu chake (The future of Culture), na wakati alipofanya mahojiano na katika gazeti la Al-Ahram (1/3/1971) karibu miaka miwili kabla ya kifo chake, na kuulizwa juu ya maoni yake juu ya kitabu hiki, alisema: Hivi ni vitabu vya mwaka 1936 zamani sana, vinataka kusahihishwa ...lazima nivirejee na kurekebisha vitu kadhaa ndani yake na kuongeza. Huu ndio msimamo wa kweli wa Dkt. Taha Hussein, ambaye anapaswa kujitokeza kwa haki yake, na alikuwa na msimamo mkali sana juu ya sheria za Kiislamu wakati alikuwa mjumbe wa Kamati ya Kutunga Katiba mwaka 1953 BK, ambapo anasema - kama ilivyoelezwa katika vikao vya kamati, kikao cha 4/6 / 1953-: "Ni hakika kwamba wengi hawatakubali wakati katiba imewekwa kile Uislamu imeamuru, lakini tunapaswa kuwa waangalifu na kusema: Hakuna sharti ambalo linatuwezesha kuachana na maandishi ya Qur`ani ... Ninataka kusema: Ikiwa kuna maandishi dhahiri ya kidini, basi hekima na wajibu hututaka tusipinge maandishi hayo. Na kuwa wenye busara na waangalifu ili tusidhuru watu kwa hisia zao, dhamiri zao, au dini yao …" Kisha akasema: "Ikiwa serikali inauheshimu Uislamu, lazima iuheshimu kabisa na kwa undani, na imani sio imani katika baadhi ya vitabu na kutokuamini kwa vingine".
13 Kwa upande wa kiongozi Saad Zaghloul na mapinduzi yake, mapinduzi ya mwaka wa 1919, hayakuwa Uangazaji au mapinduzi ya kisekula, bali yalitoka kabisa kwenye vazi la Dini. Mapinduzi haya yalijitoa msikitini na kanisani, na kauli mbiu yake maarufu ilikuwa "Dini ni ya Mungu na nchi ni ya wote" na hii ni kauli mbiu ya Kiislamu kabisa, na wala sio kauli mbiu ya Kisekula. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {…na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu} [AL BAQARAH 193]: Na anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe} [AR RAHMAAN:10]
Na wakati Dola ya Kiislamu lilipoanza iliukubali wingi wa Kidini wa watu. Na alipoulizwa juu ya mapinduzi na kuambiwa: “Wewe ndiye kiongozi wa mwamko huu,” alisema: “Hii ni heshima ambayo siidai … hakika mambo yalivyo, mwamko wenu huu ulianzia tangu enzi za Jamal Al-Din al-Afghani. ”Na Saad Zaghluliy aliandika Makala muhimu kuhusu kitabu cha Sheikh Ali Abdel Razek” Uislamu na Chimbuko la Hukumu “ambapo alisema:” Nimesoma kwa uangalifu kitabu cha Uislamu na Chimbuko la Hukumu ili kujua kiwango cha kampeni mbaya na sahihi dhidi yake, nilishangaa kwanza: ni kwanini Mwanachuoni wa Dini anaandika kwa njia kama hiyo juu ya mada kama hiyo, nimewasoma wataalamu wengi wa Masuala ya Mashariki na wengine, na sijapata yoyote katika hao aliyeushambulia Uislamu kwa maelezo makali kama hayo, kama alivyoandika Sheikh Abdul Raziq ..nimekuja kugundua ya kwamba yeye hajui baadhi ya misingi ya Dini yake, bali machache katika Nadharia zake, iweje yeye adai ya kwamba Uislamu sio Dini ya Kiraia? Wala sio mfumo unaofaa kwa Utawala? Je! Ni sehemu gani ya maisha ambayo haijaainishwa katika Uislamu, ni kuuza, kukodisha, zawadi, au aina yoyote ya miamala? Je! Hakusoma chochote katika haya huko Chuoni Azhar? Au hakusoma kwamba mataifa yalitawaliwa na Misingi ya Kiislamu kwa vipindi virefu tu ambavyo vilikuwa vya enzi bora zaidi, na kwamba mataifa mengi bado yanaendelea kutawaliwa na Misingi hiyo hiyo huku yakiwa salama na yenye utulivu, kwa hivyo, iweje Uislamu usiwe wa Kiraia, na Dini ya kutawalia …)) Huyu ndiye Saad Zaghloul, ambaye hatuwezi kumweka kwenye kapu la Uangazaji kwa maana yake ya Kimagharibi.
14 Kwa upande wa Dkt. Muhammad Hussein Heikal, alikuwa mmoja wa walinganiaji wa kwanza wa Utaifa kwa mtindo wa Kimagharibi, na yeye na Lotfi al-Sayed walikuwa wanapinga Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, lakini mwaka 1930 BC alianza mradi wake wa Kiislamu kwa kuyaandika Maisha ya Muhammad, halafu Al-Farouq Omar, na mwaka wa 1935 alichapisha kitabu chake çha: Katika Nyumba ya Ufunuo. Na kwa ujasiri alikosoa wasifu wake wa kiakili, na katika kukosoa kwake wazo la kuwa na Uzalendo wa Kitaifa kwa maana ya Kimagharibi, na utetezi wake wa wazo la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, anasema: "Wazo la Kiislamu linalotegemea imani ya Mungu mmoja linapingana na kile Ulimwengu wetu unachokitaka hivi sasa ambacho ni utukuzaji wa Utaifa, na kuleta taswira ya mataifa kama sehemu zinazoshindana, upanga unatawala, na sababu za maangamizi kati yao katika kile wanachoshindania, na watu wa Mashariki wameathiriwa na wazo hili la Utaifa, na sisi tumekuwa tukijipatia nguvu kupitia hilo huku tukiwa tunadhani kwamba tunaweza kupambana na Magharibi ambayo imetudhulumu na kutudhalilisha ... Hakika Uzuri wa ustaarabu wa Magharibi umetufanya tusahau kile wazo hili la Utaifa lilichokikusanya miongoni mwa mambo yenye kuangamiza Ustaarabu ambao unaojengeka kwa msingi wake pekee. Kwa hivyo, hatukuwa na njia ya kukwepa kurejea katika historia yetu ambayo tunatafuta ndani yake misingi ya maisha ya kiroho ili tuweze kutoka katika mkwamo wetu dhalilishi, na kuiepuka hatari iliyoivuta fikra hii ya Utaifa wa Kimagharibi, na ikaudumisha uhasama kwa sababu ya maisha ya kimaada" na hapa lazima tugundue kwamba Umma, katika historia yake yote, ndio ulioujenga Ustaarabu, na wala haukujengwa na mifumo hiyo ya kisiasa iliyopo katika historia ya Kiislamu ambayo ilikumbwa na upotoshaji katika nyakati mbalimbali, na ikawa mbali na misingi sahihi ya Uislamu.
15 Kuhusu ustaarabu wa Kiislamu, Dkt. Heikal anasema: "Muhammad aliasisi Dini ya kweli, na akaweka Msingi wa Ustaarabu ambao peke yake unatosha kuleta furaha ya Ulimwengu, na Dini na Ustaarabu ambao Muhammad aliwafikishia watu kwa Wahyi kutoka kwa Mola wake, ni vitu vinavyooana ili kusiwe na mgawanyiko kati yake. Na Historia ya Uislamu imeepukana na migogoro kati ya Mhimili wa Kidini na Mhimili wa Zama, na hiki ndicho kilichouokoa Uislamu, na kuuacha mzozo huu katika mfumo wa fikra za Magharibi na katika mwelekeo wa Historia yake"
16 Dkt. Heikal anaukosoa umagharibishaji kwa ujumla wake, akisema: "Wakati fulani niliwaza, kwanini wenzangu bado wanafikiria kuwa kuhamisha maisha ya kiakili na kiroho ya Magharibi ni njia yetu ya maendeleo na kusonga mbele… Kwa hivyo mimi nilijaribu kuwafikishia watu kwa lugha yangu utamaduni wa kimaadili na kiroho wa Magharibi, ili kwamba sisi sote tuweze kuuchukua kama mwongozo na taa yenye kuangaza. Lakini nilikuja kugundua baada ya hapo kwamba mimi ninapanda mbegu mahali ambapo mbegu hiyo haiwezi kuota, kwa hivyo ardhi hiyo inaimeza mbegu bila ya kuiotesha, na mimi bado ninashirikiana na marafiki zangu juu ya kwamba bado tunahitaji kuhamisha kutoka katika maisha ya akili ya Kimagharibi, kila kitu tunachoweza kukihamisha lakini mimi nimekuwa nikitofautiana nao katika suala la Maisha ya Kiroho, na ninaona kwamba yale yaliyomo Magharibi kuna ambayo hayafai kuhamishwa, kwani Historia yetu ya Kiroho sio Historia ya Magharibi, na Utamaduni wetu wa kiroho sio Utamaduni wake. Magharibi ilishinikizwa kufuata mfumo wa kufikiri wa kikanisa uliopitishwa na Upapa wa Kikristo tangu zama za awali, na Mashariki iliendelea kuwa mbali na ufuasi wa huu mfumo wa kufikiri. Tunawezaje sisi kuuhamisha utamaduni wa Kiroho wa Kimagharibi ya kiroho ili kuiinua kimaendeleo Mashariki hii na wakati ambapo kuna tofauti hii kubwa kati yetu na Magharibi katika Historia na katika Utamaduni wa Kiroho?" Na maisha ya maadili ni Msingi wa uwepo wa kibinadamu kwa mtu binafsi na Mataifa. Kwa hivyo ni jambo lisiloepukika kwamba tutafute katika historia yetu, katika tamaduni zetu, na ndani kabisa ya mioyo yetu na katika awamu mbalimbali za Historia yetu, maisha haya ya kiroho, ambayo kwayo sisi tunafufua kile kilicholala katika akili zetu, na kilichotulizana katika vidonda vyetu na kilichoganda mioyoni mwetu. Historia yetu ya Kiislamu ni mbegu pekee inayokua na kuzaa matunda, ambayo ndani yake kuna maisha yanayozihuisha nafsi zetu, kwa kuzifanyisha kazi na kuzikuza. Na nilipogundua jambo hili, sikuacha kulingania jinsi ya kuhuisha Ustaarabu wetu wa Mashariki .
17 Mifano hii tuliyoitaja ya Viongozi wa Kuinuka kwetu Kisasa tunaweza kubainisha maana ya kweli ya Uangazaji wa hao wanaowasiliana na Wengine na tukanufaika nao bila ya kuwaiga na tukaweza kujenga Mwinuko wa Maendeleo, Upya na Marekebisho kwa kuutumia Msingi wa Ustaarabu wetu Asili wa Kiislamu.
18 Na kwa ajili hiyo hakika sisi kwa kumalizia tunasisitiza – huku tukifuatilia harakati za Maendeleo ya Kiislamu ya Kisasa - kwamba sisi sio kama wanavyoashiria baadhi ya watu mbele ya kuzorota kwa Mpango wa Uangazaji bali sisi tuko mbele ya Mpango Mkubwa wa Uangazaji wa Kiislamu unaoangaza kwa nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Uislamu na Mtume wake S.A.W, na ambao unarejea na hakika mambo yalivyo, huu ni Mradi wa Uangazaji wenye Marejeo yake ya Kimagharibi, mbele ya Mradi Mkubwa wa Uangazaji ambao Marejeo yake ni Uislamu ambao hapana Shaka kwamba unakumbana na changamoto nyingi na majukumu ya Wanachuoni na Waislamu wote na ni jukumu la Taasisi za Kiislamu kuchukua nafasi yake katika Uangazaji wa Kweli na wa Asili, ambao ni Nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka ahadi yake itimie na Qur’ani iukamilishe muda wake uliopangwa
19 Kwa mujibu wa – Dkt. Yahaya Huwaidi haipaswi kutoweka hata mara moja akilini mwetu kama Waislamu kwamba Mielekeo ya Kifikra iliyojitokeza katika zama za Kuibuka kwa Ulaya ingawa ni Mielekeo tunayoweza kunufaika nayo katika Nchi zetu isipokuwa imeambatana na kitu maalumu ambacho kinatuzuia kuzifanya zama hizo za Kuibuka Ulaya kwa Upande wa Kifikra kwa uchache kuwa ni mfano wa kuigwa wa Kuibuka kwetu au kwa Mzinduko Wetu tunaoutarajia. Kwa hiyo kurejea katika zama za Kuinuka kwa Ulaya kuelekea katika Urithi wake wa Kale wa Ugiriki, au kile kinachodaiwa Mizizi ya Fikra ya Kimagharibi, zimeambatana na mwelekeo huu kwa ajili ya kuamini kile kinachodaiwa kama Muujiza wa Kigiriki, na mwelekeo huu uliendelea wazi wazi katika kila kinachotokana na Ustaarabu wa Kimagharibi.
Lakini sisi tunakuta kwamba Ustaarabu wa Kiislamu na katika Staarabu nyingine za Mashariki, kuna yanayothibitisha Kwamba gumzo la Magharibi kuhusu muujiza huo ni tukio linalotiwa chumvi mno. Na vyovyote iwavyo hivi sasa ni wajibu wetu – kwa mujibu wa tamko la Dkt. Huwaidi – kutozungumzia zama za Kuibuka kwa Ulaya isipokuwa na macho yetu yakiwa yamefunguka yanaujua Ustaarabu wetu wa Kiislamu na Kiarabu na Kimashariki, na kwa maneno mengine:
Na Mazungumzo yetu hayapaswi kutoka katika zama hizo za kujihami na kujikinga kwa kiasi kinachopasa kuepukana na kasumba pofu zisizopendwa.
Marejeo ya Msingi ni Dkt. Muhammad Amara, Kitabu cha Fikru Tanwiir baina ya Wasekula na Waislamu, pamoja na kunufaika na jumla ya chambuzi zilizofanywa juu yake, na Wanachuoni wengi Wakubwa Wabobezi walishiriki, na kutokana nao kwa utaratibu wa Majina yao ni Maprofesa wafuatao: Ahmad Fuad Pasha, Taufiq Shaawi, Ali Juma, Mahfudhi Azaam, Sheikh Muhammad Ghazaali, Muhammad Abdul Waahid Twaraabiyah, Muhammad Abduhu Swiyaam, na Utafiti huu kimsingi ni Mhadhara wa Kongamano uliotolewa na kuchapishwa jijini Cairo: Jumuiya ya Kituo cha Kimataifa cha Uthibitishaji na Tafiti mbalimbali na Malezi ya Kiislamu, Mfululizo kuelekea Mzinduko wa Kiislamu (1), 1994 kwa ufupi na upana wake. Profesa Dkt. Yahaya Huwaidi (Mwalimu wa Falsafa katika Kitivo cha Fasihi, Chuo Kikuu cha Cairo), Kitabu chake kiitwacho, Kisa Cha Falsafa ya Kiarabu, Cairo: chapa ya Darul Thaqaafa linnashri Watauzii, mwaka wa 1993, (ukurasa wa 44 hadi 45) kwa ufupi na Kufanyia kazi.

 

 

 

 

 


 

Share this:

Related Fatwas