Hukumu za Kuoga kwa Kutumia Maziwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu za Kuoga kwa Kutumia Maziwa

Question

  Hukumu gani kuoga kwa kutumia Maziwa?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Amemuumba mwanadamu na kumpa jukumu la kuongoza kwenye ardhi ili kuijenga na kuendesha Sharia za Mwenyezi Mungu na kutekeleza hukumu zake, na Mwenyezi Mungu Akaifanya ardhi kuwa ni dhalili ili mwanadamu apate mahitaji yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi} [AL BAQARAH: 29], na kwa maelezo hayo Wanachuoni wote wamesema kuwa asili ya vitu ni halali mpaka iwepo dalili ya kuharamisha( ), na wakasema wengine kuwa asili katika manufaa ni halali na katika madhara ni haramu( ).
Amesema Imamu An-Nasafy katika tafasiri yake: {Yeye ndiye Aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi} maana yake ni kwa ajili yenu na kunufaika nayo katika dunia yenu na Dini yenu, ama la kwanza lipo wazi, na la pili ni la kuangaliwa kwa kina na yaliyomo miongoni mwa maajabu yanayoonesha uwezo wa Mtengenezaji Mwingi wa hekima kwao, na yaliyomo ikiwemo mazingatio ya Siku ya Mwisho, kwa sababu ladha yake inakumbusha thawabu zake na machukizo yake yanakumbusha adhabu zake, wamefanya dalili Al-Karkhy, Abu Bakr Ar-Razy na Muutazila kauli yake: {Aliyekuumbieni} kuwa vitu ambavyo vinafaa kunufaika navyo vimeumbwa kwa asili ni halali( ).
Amesema Shawkany katika tafasiri yake: Amesema Ibn Kaisan: {Aliyekuumbieni} kwa maana, ni kwa ajili yenu, ndani yake kuna dalili kuwa asili katika vitu vilivyoumbwa ni halali, mpaka iwepo dalili inayohamisha asili hii, hakuna tofauti kati ya wanyama na wasiokuwa wanyama miongoni mwa vinavyonufaisha kinyume na dharura, na katika kusisitiza kwa kauli yake: {Vyote} ni dalili yenye nguvu zaidi kwenye hili( ).
Amesema Imamu Al-Mahally katika sherehe yake ya kitabu cha Jam’ii Al-Jawaam’ii baada ya kutaja kauli ya Mola Mtukufu: {Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi} [AL BAQARAH: 29]. Ametaja katika kuelezea neema, wala asitamani isipokuwa chenye kufaa( ).
Eneo la dalili katika Aya ni kuwa asili ya matumizi ya vitu ni halali mpaka pale panapokuwepo dalili inayoonesha kinyume chake, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Amefanya vilivyomo ardhini ni vyenye kuumbwa kwa ajili yetu na kuneemesha kwetu kwa hivyo vitu, na sura ya juu ya neema ni uhalali wa kunufaika na yale yaliyoumbwa kwa ajili yetu, hivyo vinakuwa ni halali kunufaika na vyote vilivyomo ardhini.
Na dalili ya hilo pia ni kauli ya Mola Mtukufu: {Sema: Ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu Alilowatolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao waotu} [AL AA'RAF: 32].
Amesema Imamu Al-Alusy katika tafasiri yake: Aya imechukuliwa dalili kuwa asili katika vinavyoliwa vinavyovaliwa na aina za mapambo ni halali, kwa sababu neno la ishara ya kuuliza ambalo neno “Min” kwa Kiarabu ni alama ya kupinga uharamu wake, na imenukuliwa kutoka kwa Ibn Al-Fars kuwa amesema: Imechukuliwa dalili kwa yule mwenye kuruhusu vazi la Hariri kwa wanaume, kisha akasema: Ukweli ni kuwa kila kisichokuwa na dalili ya uharamu wake katika haya mapambo, basi hakisimamishwi matumizi yake maadamu hakuna ndani yake dhana hiyo kama ilivyoashiriwa hapo mwanzo( ).
Amesema Imamu Ar-Razy: Mwenendo wa Aya hii ni kuwa kila anachojipamba nacho mwanadamu kinapaswa kuwa ni halali, vilevile kila anachotumia kwa manukato lazima kiwe halali, hivyo Aya hii inapelekea kuhalalisha kila manufaa, na hii ndiyo asili inayozingatiwa katika Sharia zote( ).
Katika sahihi mbili Hadithi inayotokana na Saad Ibn Abi Wiqas kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Waislamu wengi kwa Waislamu wenzao ni wenye makosa mwenye kuulizia kitu hakiharamishi kwa muulizaji bali anaharamisha kwa masuala yake”( ), na hii ni wazi katika asili ya vitu ni halali na uharamu ni wenye kuzuka( ).
Hivyo tunasema: Matumizi ya maziwa kwa kuogea au kuyaongezea maji ikiwa makusudio ni masuala ya matibabu au mapambo, basi hakuna kizuizi katika hilo, sura ya kunufaika na Alichoumba Mwenyezi Mungu Mtukufu katika vitu vinavyomzunguka mwanadamu hutofautiana kwa tofauti ya asili ya wanadamu, desturi zao na tamaduni zao, matumizi na manufaa ya vitu hubadilika kwa mabadiliko ya wakati na kuboreka kwa maarifa ya mwanadamu ambapo manufaa yanaweza kurudi kwa kutumia kwake hivi vitu.
Kuonekana kwa faida ambazo huenda akanufaika nazo mwanadamu katika bidhaa za chakula zitokanazo na wanyama na mimea kwa upande wa matibabu jambo si geni na wala si jipya, kwa mfano wa asali pamoja na gharama yake kuwa juu hutumika na Wanachuoni pamoja na madaktari wametoa nasaha kwa kujitibia kwa asali na katika mambo ya nje ya mwili na wala hawajamzungumzia mtumiaji wake kuwa ni matumizi mabaya, katika hayo ni pamoja na yaliyopokelewa kutoka kwa Ibn Umar kuwa alikuwa halalamiki kidonda au chochote isipokuwa alitumia asali hata uvimbe uliojitokeza aliupaka asali, aliulizwa katika hilo akasema: Kwani Mwenyezi Mungu hajasema: {Ndani yake kuna ponyo kwa watu}( ).
Anasema Shawkany katika kusherehesha kauli ya Mtume S.A.W.: “Ponyo katika mambo matatu: Kupiga chuku, au kunywa asali, au kutumia moto, na mimi nawakataza watu wangu kutumia moto”( ), pindi ikitumika asali mwilini kwa ajili ya jipu basi inaua jipu na mapele, pia hurefusha nywele hupendezesha na kung’arisha, na pindi akiitumia kama wanja huondoa kiza cha kuona, na akiitumia kwenye meno, basi hutakatisha meno na kulinda afya yake, nayo ni ajabu katika kulinda mwili wa mtu aliyefariki wala hauozi haraka, pamoja na hayo ni salama yenye madhara machache sana( ).
Vilevile amesema Ibn Muflih katika adabu za Sharia: Ikiwa itapakwa kwenye mwili wenye jipu na nywele basi huua jipu na kurefusha nywele kuzipamba na kung’arisha, na ikitumika kwa wanja, basi huondoa kiza cha kuona na kama itatumika kwenye meno basi hung’arisha meno na kulinda afya yake na afya ya ufidhi( ).
Hivyo kuoga kwa kutumia maziwa kunaingia katika upande wa tiba na kulinda mwili ambapo kumepokelewa Kisharia, na inachukua hukumu ya Sunna au halali au wajibu wakati mwingine.
Wanachuoni wa Imamu Shaafy na Imamu Hanbal wamesema juu ya kufaa kutayamamu mgonjwa kwa kuhofia kutokea kwa athari mbaya( ), kwa sababu anaumiza umbile na kudumisha madhara( ), hivyo kuacha wajibu nao ni kutawadha na kuitumia ruhusa nayo ni kutayamamu kwa lengo la kulinda mazingira ya nje ya mwili, jambo linaloonesha umuhimu unaotolewa na Sharia kwenye uzuri wa nje ya mwili.
Ama kuyamwaga maziwa baada ya kutumika jambo hilo halina ubaya, kwa sababu haidhaniwi kutumika tena baada ya hapo kwa matumizi ya chakula na wala haizingatiwi ni ubadhilifu, kwani ubadhilifu maana yake ni kukiuka makusudio, au kuvuka mpaka( ), na ubadhilifu huenda ikawa ndani yake kuna kukiuka halali na kwenda kwenye haramu, na huenda kukawa kuvuka mipaka katika matumizi( ).
Anasema Imamu Dhahir Ibn Ashur katika tafsiri ya kauli ya Mola Mtukufu: {Na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhilifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya ubadhilifu}[AL A'RAAF: 31]. Katazo la ubadhilifu ni katazo la mwongozo na wala sio katazo la uharamu, hii ni kutokana na kuungana na uhalali unaofuata katika kauli yake Mola Mtukufu: {Sema ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu} mpaka kauli yake {Na vilivyo vizuri katika riziki} kwa kuwa kiwango cha ubadhilifu si chenye kudhibitiwa hivyo hakifungamani na amri, lakini huangaliwa kwa mazingatio ya watu na masilahi yao, na hili linarejea kwenye maana ya usawa unaopatikana katika kauli yake iliyopita Mola Mtukufu: {Sema: Mola Mlezi wangu Ameamrisha uadilifu} hivyo kuacha ubadhilifu ni katika maana ya uadilifu( ).
Ubadhirifu ni kitu cha makadirio watu hutofautiana kwa kutofautiana tamaduni zao na uwezo wao wa mali, hivyo kila kitu kwa hali yake ilivyo.
Uzuri haujakatazwa kwenye Sharia bali umetakiwa, hilo ni pamoja na kauli ya Mtume S.A.W.: “Hakika Mwenyezi Mungu pindi Anapompa neema mja basi anapenda kuona athari ya neema yake kwake”( ),na kauli yake Mtume S.A.W.: “Hakika Mwenyezi Mungu mzuri na anapenda uzuri”( ), na imepokelewa kuwa Mtume S.A.W. siku moja alitoka na akiwa na kitambaa cha kuvaa kichwani thamani yake kilikuwa ni dirhamu elfu moja, na imepokelewa kutoka kwa Zainu Al-Abideen R.A. alikuwa ananunua kitambaa cha kufunga kichwani kwa thamani ya dirhamu hamsini na wala haoni ubaya wowote na anasema: {Sema ni nani anayeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu ambalo amelitoa kwa waja wake} na Abu Hanifa alikuwa akivaa kitambaa cha kufunga kichwani thamani yake ni dirhamu mia nne, na alikuwa anawamrisha watu wake katika hilo, na alikuwa Muhammad Ibn Al-Hassan anavaa nguo ya thamani na anasema: Nina wake zangu hivyo ninavaa mwenyewe ili wasiangalie kwa mwingine( ).
Miongoni mwa maneno ya Imamu Shaafy amesema: Lau mtu atatumia nusu ya mali yake katika uzuri basi sitomzingatia kuwa ni mjinga” athari hizi na zingine zinaonesha umuhimu uliotolewa na watu wema waliotangulia kwenye mandhari ya mavazi na mapambo mazuri ambayo baadhi ya watu hivi sasa wanazingatia ni ubadhirifu wakati ukweli sio hivyo.
Anasema Sheikh Al-Khadimiy katika kitabu cha Bariqat Al-Muhammadia: “Fahamu kuwa ubadhilifu ni upotezaji wa mali na kuitumia pasina faida yoyote iliyozoeleka, kwa sababu kitendo cha hiyari hakifanywi isipokuwa baada ya kufikia faida, lakini hiyo faida ikiwa sio iliyozoeleka husemwa: Kwenye mali kumefanyika ubadhirifu, na katika vyingine viovu (kidini au kidunia halali) kwa kutumia kwake kwa faida iliyozoeleka kidini au kidunia si halali katika Sharia, kama vile kutumia mavazi yaliyo haramu na vyombo vilivyo haramu( ).
Kutumia maziwa kuogea hufikiwa faida iliyozoeleka kwa sababu huenda ikawa ni kwa ajili ya tiba au uzuri, ikiwa ni kwa sababu za tiba basi hakuna lawama kwa mwanadamu ikiwa atafanya jitihada ya kuyapata, kwani kutumia au kuhudumia kuna kuwa kwa mujibu wa haja ya kufikia makusudio, ikiwa kwa ajili ya uzuri, kama vile kuyatumia kwa kuongezea mada za kuogea na kusababisha ngozi kupata uzuri na ulaini pamoja na mng’aro unaopelekea kupambana zaidi na muonekano wa makunyasi na mikato ambapo inawezekana kabisa kuzingatiwa ni katika Sunna ikiwa umeweka nia njema, na wala hili haliwi sehemu yoyote ya ubadhilifu.
Ama matumizi ya maziwa baada ya kutumika kwake kama ilivyoelezwa ikiwa itapatikana njia ya kunufaika nayo kinyume na chakula kwa mwanadamu kwa kutumika kwa ajili ya wanyama au mimea au kuzalishia kitu kwa masharti yake na sifa zake au kwa sura yoyote ya manufaa ya umma au manufaa binafsi basi hilo ni jambo zuri zaidi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

 

Share this:

Related Fatwas