Mapenzi kwa Mtazamo wa Kiislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Mapenzi kwa Mtazamo wa Kiislamu

Question

 Tunaomba ufafanuzi wa dhana ya mapenzi kama Tabia bora ya Kiislamu.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mapenzi ni hisia za kibinadamu zilizo pevu, humaanisha maisha. Na pia humaanisha ubinadamu au utu, na ni moja ya migawanyiko ya Rehma na athari zake, kwani Mtu mwenye rehma ndiye anayependa na yeyote anayependa humaanisha kuwa yeye ni Mpole, na Mapenzi ni kutoa, na Mapenzi ni ukarimu na mapenzi ni hali ya kipekee.
Kwa hiyo, walisema: anayependa hachukii, na Mapenzi yanapokosekana humaanisha kukosekana kwa huruma au Rehma, na Rehma au Upole unapokosekana basi baada ya hali hiyo usiulize upeo wa ufisadi duniani, na kiwango cha kuenea kwa dhuluma na kiwango cha mporomoko endelevu.
1- Isipokuwa kwamba Mapenzi katika Uislamu yanapindukia kuwa kwake kujisikia na hisia mbalimbali na kuwa ni Faradhi na Wajibu, na Mapenzi yanapindukia zaidi ya maana yake pekee baina ya mwanaume na mwanamke na kuwa na maana pana zaidi inayoyafanya yawe kipimo cha Maisha, na Msingi wa Mwenendo, na Ufunguo wa Maadili. Kwa hiyo Mapenzi katika Maisha kwa vitu vyake na watu wake na misingi yake ni jambo linaloamuliwa ndani ya Qur'ani Tukufu, lakini baada ya kuyabadilisha na kuwa nishati tendaji ya Kheri na Haki na Nguvu na Ujenzi.
2- Na tunanze na yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu Mtukufu na yale asiyoyapenda, nayo katika mkusanyiko wa Aya mbalimbali zinazotuundia Katiba ya Mapenzi ya Kweli yasiyo ya bandia; ambapo wakati huo Mapenzi huchanganyika na matamanio na hamu na huchanganyika wakati huo na masilahi maalumu yanayoshukiwa, wakati ambapo Mapenzi ya Kweli yanaonekana wazi na daima, yanaweza kukusanya matamanio bila ya maovu, na yanaweza kukusanya maslahi bila ya uchoyo, na yanaweza kukusanya lengo bila ya Hiana, hayo ni mapenzi tunayoyatamani.
Na kwa hivyo, Qur'ani Tukufu ndio inayoamua namna ya kuvipenda vitu na wala haivifanyi vitu hivyo kuwa ni dalili ya kheri daima. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu.Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui}. [AL BAQARAH 216].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao}. [AL QASAS 56]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema katika kupenda kwa misingi bora: {Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu}. [AN NUR 22]
Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema katika mambo Anayeyapenda: {Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi.Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike. Wakisha t'ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha}. [AL BAQARAH 222]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Sivyo hivyo, bali anaye timiza ahadi yake na akamchamngu basi Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu}. [AAL IMRAAN 76]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema}. [AL BAQARAH 195]
{Na Manabii wangapi walipigana na pamoja nao Waumini wengi wenye ikhlasi! Hawakufanya woga kwa yaliyo wasibu katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakuwa wanyonge. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanao subiri}. [AAL IMRAAN 146]
{Hao ni wasikilizaji kwa ajili ya kusema uwongo, nani walaji mno vya haramu! Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jipuuze nao. Na ukijipuuza nao, basi wao hawatakudhuru kitu. Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu}. [AL MAIDAH 42]
{Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea}. [AAL IMRAAN 159]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana}. [AS SWAF 4]
Na hizi ndizo sifa nane zilizotajwa na Qur`ani Tukufu kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda Waja wake wawe nazo, Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda pale mja wake anapokosea asilifanye tena kosa hilo hata kama makosa yamejirejea, Yeye anakubali toba ya Mja wake na anasamehe makossa. Na Mtume S.A.W. amesema: "Kila Mwanadamu ni Mkosa, na mbora wa wenye kukosea ni yule anaetubia makosa yake".
Na Toba ni Falsafa kubwa mno ya kutokata tama, na katika Wajibu tuyaweke upya maisha yetu na tuuangalie Mustakbali, na kwamba tusijishughulishe na mzigo wa yaliyopita, na inapokuwa hapana budi, basi tujifunze mafunzo kwa ajili ya maisha yetu ya baadaye, lakini tusisimame katika yaliyopita kwa ajili ya kujivunja moyo na kukata tamaa. Hakika mambo yalivyo, hakati tamaa mja isipokuwa wale waliokufuru. Katika toba kuna kujichunga na inatufundisha kujirekebisha na kuchukua tahadhari kila Siku, na ni katika sifa zinazopendwa basi tuifanye iwe nguzo miongoni mwa nguzo za mapenzi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda pia Wenye kujisafisha nje na ndani yao. Na ikiwa Toba ni njia ya kujisafisha kwa ndani hakika usafi ni katika kujitwaharisha wazi, na Usafi katika Mwili na katika Nguo na Vifaa na Sehemu ni sehemu isiyogawika na ni nguzo kuu katika kuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Waislamu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (yaAlkaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala paamani. Na alipo kuwa akisimama Ibrahim pafanyeni pawe pa kuswalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail:Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanao inama na kusujudu}. [AL BAQARAH 125]
3- Na tuifanye nguzo ya pili kuwa ni Kujisafisha, nayo ni maana inayoweza kubadilika ikawa hatua kadhaa maalumu katika maisha yetu ngazi ya Umma na ngazi ya Jamii na ngazi ya mtu mmoja mmoja.
4- Mmoja wetu anapokuwa na sifa ya kutubu na kuwa msafi basi hakika mambo yalivyo anasifika kwa Uchamungu, nao ni hofu inayotokana na Mapenzi na wala haitokani na woga, kwa hiyo Mchamungu ni yule anayechelea kumkasirisha ampendaye, naye ni yule anayekuwa na woga juu ya anayempenda naye ni yule anayejizuia na kila kinachomuudhi anayempenda na anaharakisha katika kumpenda.
Kama kweli ungelikuwa penzi lake basi ungelimtii,
Kwani Hakika mpenda kwa ampendaye ni mtiifu)
5- Na ikiwa Mchamungu anaanza na nafsi yake basi hakika mtu mwema, wema wake huvuka na kuwafikia wengine, na kwa ajili hiyo, Mwenyezi Mungu amewapenda Watenda wema, na Malipo ya Kitendo cha kuwatendea wema na manufaa wengine ni makubwa na bora zaidi kuliko kitendo kinachoweza kukatishwa, hakika jambo hili lina maana ya mpangilio ulio wazi; ulio wazi kwa Watu, na ulio wazi kwa Ulimwengu mzima, ulio wazi kwa mwingine, na hii ni nguzo ya nne miongoni mwa nguzo za mapenzi.
6- Na ikiwa tutafanya hivyo basi hapana budi kuvumilia na Kudumu na kuendelea kwani "Matendo yapendwayo zaidi na Mwenyezi Mungu ni yale yenye kudumu hata kama yatakuwa madogo". Na uvumilivu ni sifa inayogeuka na kuwa silika iliyotuama moyoni, na Mwenyezi Mungu anawapenda wavumilivu, kwa maana kwamba hampendi aliyezubaa mwenye kigeugeu ambaye huanza kazi kisha huiacha, nayo ni nguzo ya tano ya Mapenzi.
7- Na Uadilifu ni msingi wa ufalme, na kwa hivyo, hakika mambo yalivyo, Mwenyezi Mungu anaupenda Uadilifu na anauamrisha na anatuelekeza kwamba huo Uadilifu ni thamani isiyo na kikomo haibadiliki wala kugeuka kama waonavyo baadhi ya wanao yaabudu masilahi na kumtoa Mwenyezi Mungu katika maisha yao, na kwa hivyo akawa dhalimu, na Mwenyezi Mungu hawapendi madhalimu, bali anawapenda waadilifu. Je, Ukweli huu umekuwa kwa baadhi ya Watu ni jambo la kutazamwa au kuzungumziwa? Inaonekana kwa vitendo vyao kwamba imekuwa hivyo, basi wanalazimika hao kutambua kwamba Mapenzi yatakuwa yameikosa moja kati ya nguzo zake iwapo itaukosa Uadilifu, na hakuna uwepo wa kitu bila ya kuwapo nguzo yake.
8- Atakapowapotosha watu au Mwenyezi Mungu akawa amewaandikia kuwanyima neema ya Mapenzi na wakaingia katika kinyume chake ambacho ni chuki basi tunawajibika kutowafuata. Anasema Mtume S.A.W: Msiwe Wafuasi. Mnasema: Watu wakifanya vyema na sisi tutafanya vyema na ikiwa watadhulumu basi na sisi tutadhulumu, lakini zidhibitini nafsi zenu kwamba watu wanapofanya mema nanyi mfanye mema, na wanapokosea basi nyinyi msidhulumu.
Hakika ya Sifa hizi zinazingatiwa ndizo zinazoeneza kheri na Amani, na zinamwandaa mpiganaji wa Njia ya Mwenyezi Mungu: Jihadi ndogo na Jihadi Kubwa ambaye anataka kuzuia Shari na kuondosha ukandamizaji na Uadui, na wakati huo, hatutampata Mtoa vitisho anayedai kuwa mrekebishaji, au hata Mwovu anayedai kuwa ni Muislamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu}. [AL BAQARAH 204]
{Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi}. [AL BAQARAH 205]
{Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu}. [AL AHZAAB 60]
{Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa}. [AL AHZAAB 61]
Na maana halisi ya neno (Terrorism) Ugaidi ni Irjaafu kwa lugha ya Kiarabu, na mtendaji ni Gaidi, na wingi wake ni Magaidi au Murjifuuna kwa Kiarabu. Na sio ule ugaidi kwa maana ya nguvu, na wala sio kufanya uharibifu duniani na jambo hili kwa mnasaba huo ni upande wa kuiacha huru istilahi hii.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Rejeo ni: Kitabu cha: Sifa za zama za kisasa, cha Mheshemiwa Dkt. Ali Juma, Mufti wa Misri.

 

 

Share this:

Related Fatwas