Dia ya Mwanamke

Egypt's Dar Al-Ifta

Dia ya Mwanamke

Question

 Ni ipi Dia ya Mwanamke ni nini? Na yapi Madhehebu ya wanavyuoni katika suala hilo?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Utafiti huu unaelezea malipo ya dia ya mwanamke na maelezo ya Wanachuoni kwenye jambo hili.
Neno Dia kwa upande wa lugha: Ni chanzo cha kitenzi cha amelipa muuwaji dia kwa aliyeuliwa, ni pale anapopewa msimamizi wa marehemu mali ambayo ni badala ya nafsi, kisha mali hiyo ikaitwa dia, ni jina linalotokana na chanzo cha kitenzi chenyewe( ), na katika kamusi: dia ni haki ya muuliwa( ).
Kwa upande wa msamiati: Ni mali anayopewa aliyefanyiwa jinai au msimamizi wake au mrithi kwa sababu ya jinai( ).
Kauli inayotegemewa ni kuwa dia au diya ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, na dalili yetu kwenye hilo ni ifuatayo:
Dalili ya Kwanza:
Ni Hadithi inayotokana na Muadh Ibn jabal R.A amesema: Amesema Mtume S.A.W: “Dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume”( ).
Na yanayotokana na Hadithi hii ni pamoja na yaliyopokelewa miongoni mwa athari za Masahaba na tutazungumzia kuhusu makubaliano ya Masahaba.
Dalili ya Pili:
Makubaliano ya Wanachuoni kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, kauli hii imenukuliwa na Wanachuoni wengi.
Amesema Imamu Shaafi R.A “Sijawahi fahamu kinyume kwa Wanachuoni wa zamani wala wa sasa katika dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume”( )
Na amesema Imamu Ibn Jariir Attwabary katika tafasiri yake: “Dia ya Muumini wa kike haina tafauti kati ya Wanachuoni wote – yasiyozingatiwa kuwa na tafauti – ni nusu ya dia ya Muumini mwanamume”( ).
Akasema Ibn Mundhir: “Na wamekubaliana juu ya kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume”( ).
Amesema Ibn Abdilbarr: “Wamekubaliana Wanachuoni kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, lakini hata hivyo dia yake imekuwa nusu ya dia ya mwanamume ni kwa sababu yeye ana nusu ya mirathi ya mwanamume na ushahidi wa wanawake wawili kwa ushahidi wa mwanamume mmoja”( ).
Na miongoni mwa waliyoelezea pia ni makubaliano ya Wanachuoni ni pamoja na Ibn Qudamah katika kitabu cha Mughny ( )na Qurtwuby katika tafasiri yake ( ).
Makubaliano ya Wanachuoni ni lazima yawe na mapokezi yake ya Aya au Hadithi, kinyume na hivyo lazima kuamini kuwa yamevuliwa kwa makubaliano ya Wanachuoni wote kunukuliwa upokezi huo, ili kulinda dini kujengewa kauli za watengeneza kauli na ufafanuzi wa wajinga.
Katika masuala tunayaelezea katika utafiti huu ni upokezi wa Wanachuoni ima utakuwa ni Andiko nalo ni Hadithi iliyoelezewa katika kitabu cha Baihaqy ya Muadh, au uwianisho kama alivyotaja Ibn Abdulbarr.
Imepokelewa athari kwa Masahaba Watukufu R.A. inayoonesha juu ya hukumu hii, na ufahamu wa Wanachuoni wengi katika Masahaba hukumu hii.
Amepokea Ibn Ab Shaibah katika kitabu chake amesema: Ametuambia Jariir kutoka kwa Mughiira kutoka kwa Ibrahim kutoka kwa Shariih amesema, alinijia Uruwat Al-Barqy akiwa ametoka kwa Omar na kusema kuwa, kujeruhiwa kwa mwanamume na mwanamke ni sawa kwenye jino na maeneo mengine lakini dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume.
Imepokelewa pia: Alituambia Ally Ibn Mus’har kutoka kwa Hishaam kutoka kwa Shaaby kutoka kwa Shariih kuwa Hishaam Ibn Hubair alimuandikia kumuuliza na akamuandikia kumjibu kuwa dia ya mwanamke katika kosa ni nusu ya dia ya mwanamume na Zaidi Ibn Thabiti anasema dia ya mwanamke kwenye kosa ni mfano wa dia ya mwanamume mpaka ifikie theluthi ya dia ama kilichozidia kinabaki katika utaratibu wa nusu( ).
Amepokea Baihaqy katika kitabu chake amesema: Ametueleza Abu Hazim Al-Hafidh alipewa habari na Abul-Fadhli Ibn Khumairawiya naye amepewa habari na Ahmad Ibn Najdah Thana Said Ibn Mansour Thana Hashim kutoka kwa Shaibany na Ibn Aby Laila na Zakaria kutoka kwa Sha’aby kuwa Ally R.A alikuwa anasema: Jeraha la mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume isipokuwa chini ya hapo( ).
Sehemu ya hoja katika hili ni kuwa haikunukuliwa kuwa amepinga yeyote kati yao, ndani yake kuna dalili ya wazi juu ya makubaliano yao, kwa kutokuwepo upingaji au ukanushaji, na kufanya hilo kuwa ni makubaliano ya kunyamazia, nayo ni hoja kwa Jamhuri ya Wanachuoni akiwemo Imamu Shafi na Masahaba wengi, na ni dalili ya mfano wa hivyo imeenea sana na kujirudia kwenye vitabu vya Fiqhi kwa madhehebu yake tafauti.
Amesema Imamu Al-Kasaniy – akiwa anazungumzia dia ya mwanamume na mwanamke –ikiwa ni mwanamke basi dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, kwa makubaliano ya Masahaba R.A. kwani imepokelewa kutoka kwa Omar na Ally pamoja na Ibn Mas’uud na Zaidi Ibn Thabit R.A kuwa wamesema kuhusu dia ya mwanamke kuwa ni nusu ya dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, na wala haikunukuliwa kuwa kuna yeyote aliyewapinga na kuwa hiyo ni makubaliano ya Wanachuoni, na kwa sababu mwanamke katika mirathi yake na utoaji wake ushahidi ni nusu ya mwanamume basi vile vile katika dia yake( ).
Imepokelewa athari nyingine kwa wasiokuwa Masahaba inasema kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, akasema Ibn Abi Shaiba katika kitabu chake:
Ametuambia Al-Masoudy kutoka kwa Hakiim Ibn Atibah vimesema vitabu vya Shariih na Hishaam Ibn Hubairah kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume( ).

Ambayo tumechagua ni madhehebu ya Jamhuri:
Kwani Wanachuoni wa Imamu Abu Hanifa Imamu Maliki Imamu Shaafi na Imamu Hambal wamesema kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume.
Katika kitabu cha Hidaya na sherehe yake ni katika vitabu vya madhehebu ya Abu Hanifa: “Dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, na limepokelewa tamko hili likiwa limeegemezwa kwa Ally na kuinuliwa kwa Mtume S.A.W mfano wa maneno yaliyoegemeshwa ni sawa na yale yaliyoinuliwa ambapo hakuna nafasi ya kuleta muono ndani yake”( ).
Katika sherehe ya kitabu cha Risala cha Ibn Aby Zaidi Al-Qarawany cha Mwanachuoni Ally Ibn Khalaf Al-Maliky: “Ama dia ya mwanamke huru Muislamu ni nusu ya dia ya mwanamume huru Muislamu”( ).
Katika kitabu cha Minhaj miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Imamu Shaafi: “Mwanamke na khunsa (Mwenye tupu mbili) ni nusu ya mwanamume iwe nafsi au jeraha – kwa maana ya dia” akajengea maelezo Sheikh Al-Khatibu As-Sharbiny ndani ya kitabu cha Mughny juu ya hilo na akasema: “Baada ya kumaliza dia kubwa ikaanza kwenye kupunguza, miongoni mwake ni uwanamke kwa maelezo yaliyopokelewa na Baihaqy: “Dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume”( ).
Katika sherehe ya kitabu cha Al-Minhaj – pia – cha Imamu Shamsudeen Ar-Ramly: “Mwanamke huru na mtu Khunsa mwenye maumbile mawili ni nusu ya mwanamume iwe kwa upande wa nafsi au jeraha( ).
Ndani ya kitabu cha Al-Muntaha na sherehe yake ya Bahwaty miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Imamu Hambal: “Dia ya mwanamke kwa sifa yake, kwa maana ya huru Muislamu ni nusu ya dia ya mwanamume, ameyaelezea hayo Ibn Mundhir na Ibn Abdulbarr kwa makubaliano ya Wanachuoni, na katika kitabu cha Amru Ibn Hazmi: Dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, nayo imehusishwa kwa maelezo yaliyopita( ).
Imefahamika kwenye nukuu zilizopita kuwa dalili ya Wanachuoni wa Fiqhi wa madhehebu kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume yamekuja hayo kutoka kwenye nukuu na makubaliano ya Wanachuoni.
Mitazamo ya walio kinyume na makubaliano ya Wanachuoni.
Baadhi ya Wanachuoni wa zamani na wa sasa wamesema kuwa dia ya mwanamke ni kama dia ya mwanamume, ama zamani ameeleza Ibn Qudama ndani ya kitabu cha Mughny kutoka kwa Ibn Ulyyah na Al-Asamm kuwa wamesema: Dia yake ni kama dia ya mwanamume kwa kauli ya Mtume S.A.W: “Kwenye nafsi ya Muumini wa kike ni ngamia mia moja” kisha akamalizia kwenye hilo kwa kusema: “Na hii ni kauli iliyojitenga, inakwenda kinyume na makubaliano ya Masahaba na Sunna ya Mtume S.A.W, ndani ya kitabu cha Amru Ibn Hazmi kinasema: “Dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume” haya ni maelezo maalumu waliyoyataja wote wawili katika kitabu kimoja, hivyo inakuwa kile tulichotaja ni chenye kufasiri yale waliyotaja ( ).
Na inawezekana kusema kuwa kwenda kinyume na Jamhuri ya Wanachuoni kwa Ibn Ulyyah na Al-Asamm hakuzingatiwi, kwani ameeleza Al-Hafidh Ibn Hajar mara nyingi kwenda kwao kinyume na makubaliano ya Jamhuri ya Wanachuoni( ).
Ni muhimu kwetu kuwaelezea hao wawili na tunasema: Al-Asamm ni Abdulrahman Al-Asamm, amesema Imamu An-Nawawy katika kitabu cha Tahdhiib Al-Asmaa wa Lughaat: “Ibn Kaisan ambaye ametajwa mwanzoni mwa kitabu cha mambo ya kukodi kuwa aliibatilisha hukumu ya kukodi, jina lake la kupewa ni Abubakri, na kauli yake Ghazaly katika kitabu cha Wasiitw ni kuwa si wenye kufanyiwa uadui kwenye makubaliano ya Wanachuoni wala kujeruhiwa kuwa kwao kinyume na makubaliano ya Wanachuoni,na kauli hii inakubaliana na kauli ya Ibn Al-Baaqalany na Imamu Al-Haramain kwani wamesema: Hawafanyiwi uadui kwenye makubaliano ya Wanachuoni na kinyume( ).
Katika kitabu cha Al-Bahri Al-Muhitw cha Imam Al-Badr Zarkashy: “Amesema Ustadh Abu Mansour, wamesema watu wa uzushi au bidaa kuwa ni jambo la kuzingatiwa mfanano wa picha, nayo ni kauli ya Al-Asamm, na kwenye hili amesema kuwa kuacha kikao cha mwisho cha suala hakuna madhara ni kama vile kikao cha kwanza tu( ).
Miongoni mwa waliosema juu ya kutohesabiwa kauli ya Al-Asamm kuwa anapingana na makubaliano ya Wanachuoni ni Sheikh Il-Taqa As-Sabaqy katika Fatwa yake – vile vile katika mauzungumzo yake kuhusu hukumu ya kadhi au hakimu…je inavunjwa?( )
Na Ibn Ulayyah: Ni Ibrahim Ibn Ismail Ibn Ulayyah, amesema Ad-Dhahby kuhusu Ulayyah katika kitabu cha Mizan kuwa alisema “Amenidhihaki mwenye kuangamia, alikuwa anafanya mjadala na anasema kwa maadili ya Qur`ani, alifariki mwaka wa 218, akaongeza kusema Al-Hafidh Ibn Hajar kwenye hili katika kitabu cha Lisaanu na akasema: “Ametaja Abu Al-Arab katika kitabu cha Ad-Dhufaa na kunukuliwa kutoka kwa Abil-Hassan Al-Ajaly amesema, amesema Ibrahim Ibn Ulayyah amenidhihaki mshenzi mwenye kulaaniwa, na amesema Ibn Muiin: Hakuna kitu, na akasema Ibn Yunus katika kitabu cha historia ya wageni: Amekuwa na vitabu katika Fiqhi vinavyofanana na mijadala, na akasema Al-Khatib: Alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji na ni miongoni mwa wanaozungumza kwa maadili ya Qur`ani, amesema Shaafi: Ni mtu amepotea amekaa kwenye mlango wa sawaal anapotosha watu, na akasema Ibn Abdilbarr: Ni mtu mwenye kauli nyingi kinyume na makubaliano ya Wanachuoni, na madhehebu yake kwa Ahli Sunna ni kinyume, na wala hakuna kauli yake inayozingatiwa ni kinyume( ).
Amenukuu Imamu Baihaqy katika kitabu cha mambo ya Imani kuwa Imamu Shaafi amemtaja Ibrahimu Ibn Ismail Ibn Ulyyah amesema: Mimi nipo kinyume naye kwa kila kitu, na katika kauli yake Hapana Mola wa haki isipokuwa ni Mwenyezi Mungu si semi kama anavyosema bali mimi nasema Hakuna Mola wa haki isipokuwa ni Mwenyezi Mungu ambaye alizungumza na Nabii Musa nyuma ya pazia, na yeye anasema Hakuna Mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu ambaye ameumba maneno aliyomsikilizisha Nabii Musa nyuma ya pazia( ).
Ama mwenye kusema kuwa Ibn Ulayyah aliyetajwa ni baba wa Ismail Ibn Ulayyah Imamu Mwanachuoni siyo mtoto wa Ibrahimu ambaye wamemjeruhi na kumtuhumu, basi hujibiwa kwa kauli ya Al-Hafidhi Ibn Hajar kutoka kwa Ibrahimu: Ana masuala ya peke yake na alikuwa ni katika Wanafiqhi wa Muutazilah, amefanya makosa mwenye kudhani kuwa aliyenukuliwa kuhusu yeye kuwa ni mtu wa peke yake ni baba yake hapana kwani alikuwa ni katika Wanachuoni wakubwa wa Ahlu Sunna( ).
Kutokana na maelezo yaliyotangulia, kauli ya kuvunja makubaliano ya Wanachuoni kwa Ibn Ulayyah na Al-Asamm ni kauli si sahihi, kutokana na nukuu zilizopita za Wanachuoni, kwani makubaliano ya Wanachuoni yamepitishwa na yatabaki hivyo hakuna mazingatio ya kuwa kinyume Ibn Ualyyah na Al-Asamm.
Waliozungumzia kauli hii ni Wanachuoni wengi wa sasa:( )
Ameelezea Sheikh Muhammad Rashid Ridha katika kufasiri kwake Aya ya kuuwa kwa makosa Suratun-Nisaa: 92 mtazamo wa Wanachuoni katika masuala ya dia mwanamke, ambapo yenyewe ni nusu ya dia ya mwanamume, na ametaja kuwa asili katika hilo ni kuwa manufaa ambayo wanayoyakosa ndugu wa mwanamume kwa kupoteza ndugu yao ni makubwa zaidi kuliko manufaa yanayopotea kwa ndugu wa mwanamke, hivyo amekadiriwa kwa mujibu wa mirathi, kisha akasema: Uwazi wa Aya ni kuwa hakuna tafauti kati ya mwanamke na mwanamume( ).
Amesema Sheikh Mahmoud Shaltut katika kitabu chake cha Al-Islaam Akidatu wa Sharia kwenye mlango wa dia ya mwanamume na mwanamke ni sawa sawa: “Ikiwa ubinadamu wa mwanamke unatokana na ubinadamu wa mwanamume, damu yake inatokana na damu ya mwanamume, na mwanamume anatokana na mwanamke na mwanamke anatokana na mwanamume, na hukumu ya kisasi imekuwa kwa wote wawili pale wanapofanya uadui dhidi ya nafsi, na adhabu ya moto wa jahannamu pamoja na kuishi milele humo motoni, na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na laana yake ndio malipo ya siku ya Akhera ikiwa mwanamke atauwa, kama vile ndio malipo ya siku ya Akhera ikiwa mwanamume ameuwa, basi Aya inayozungumzia kuuwa kwa mwanamke kwa makosa ndio Aya hiyo hiyo inazungumzia kuuwa kwa mwanamume kwa makosa.
Sisi bado tunaendelea kuchukuwa hukumu kwanza kabisa kutoka ndani ya Qur`ani, hivyo neno la Qur`ani katika dia ni la wote halikuhusisha mwanamume sehemu tafauti na mwanamke: {Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe fidia kuwapa jamaa za maiti} [AN NISAA: 92]. Ni wazi kabisa kuwa hakuna tafauti katika wajibu wa kulipa dia kwa kuuwa mwanamume na mwanamke, ndio…..Wanachuoni wametafautiana katika kiwango cha ulipaji wa dia, kwamba ni moja kwa mwanamume na mwanamke au dia kwa upande wa mwanamke ni nusu ya dia anayopaswa kutoa mwanamume? Imamu Raziy ametaja mitazamo miwili ndani ya tafasiri yake na akasema: Madhehebu ya Wanachuoni wengi yanasema kuwa dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, na akasema Al-Asammu na Ibn Ulayyah: Dia ya mwanamke ni sawa na dia ya mwanamume, na hoja ya Wanachuoni wengi kuwa Ally Omar na Ibn Masuud wamepitisha hivyo kuwa mwanamke katika mirathi na kutoa ushahidi ni nusu ya mwanamume katika mambo hayo mawili, vilevile inakuwa ni nusu katika ulipaji wa dia. Na hoja ya Al-Asammu ni kauli yake Mola Mtukufu: {Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya au fidia kuwapa jamaa za maiti} [AN NISAA: 92]. Wakapitisha kuwa Aya hii imeingia ndani yake hukumu ya mwanamume na mwanamke hivyo ikawajibisha hukumu kuwa ni thabiti kwa usawa( ).
Kama vile mtazamo huu umeungwa mkono na Mwanachuoni Sheikh Muhammad Abu Zuhrah katika kitabu chake cha Al-Jariimah wal-Ukuuba fii Fiqhi Al-Islaamiy kwenye mlango wa dia ya mwanamke ambapo amesema baada ya kunukuu maneno ya Ibn Qudama ndani ya kitabu cha Al-Mughny: Haya ndio aliyoyasema mwenye kitabu cha Al-Mughny, na akadai kuna makubaliano ya Wanachuoni, na akasema mwenye kitabu cha badaai katika maana ya haya makubaliano kuwa: Mitazamo ya Masahaba ilitangazwa kati yao na wengine hawakupinga ikawa ni makubaliano ya kunyamazia, wakati ambapo Wanachuoni wengi wamepinga hoja ya makubaliano ya kunyamazia, wakajengea hoja ya mtazamo huo kwa dalili mbili zingine:
Ya Kwanza: Ni kuwa mwanamke katika mirathi anachukuwa nusu ya mirathi ya mwanamume, hivyo inakuwa kwa upande wa mali ni yenye kukadiriwa katika dia nusu ya dia ya mwanamume.
Ya Pili: Ni kuwa dia ya kilichopotea, na kufanya thamani ya kilichopungua kwenye jamii kwa kupotea kwake, na hilo linapelekea dia ya kupotea kwa mwanamke kuwa ni chini ya dia ya mwanamume, kwa sababu manufaa ya mwanamke ni madogo ya manufaa ya mwanamume, na hukadiriwa dia hii inakuwa kwa makadirio ya mirathi nayo ni nusu.
Tunaona kwa mtazamo huu kuwa umeangalia upande wa mali, na wala haujatazama upande wa ubinadamu na upande wa makemeo kwa muhalifu, ukweli ni kuwa kuangalia kiwango cha adhabu ni kunatokana na nguvu pamoja na ukubwa wa jinai kwa muhalifu, kwa maana ya kufanya uadui kwenye nafsi ya mwanadamu, nacho ni kiwango sawa kwa watu wote hakuna tafauti kwa sababu ya tafauti ya jinsia, kwani dia yenyewe ni adhabu kwa muhalifu, na kuwalipa ndugu wa aliyefanyiwa jinai au kufidiwa yeye mwenyewe ikiwa uhalifu huo ni kwenye viungo vya mwili, na kutokana na hilo inapaswa dia ya mwanamke kuwa sawa na dia ya mwanamume ambapo ni adhabu ya kumwaga damu, na kwa vile mwenye kufanya uadui kwa kumuuwa mwanamke ni kama vile mwenye kufanya uadui kwa kumuuwa mwanamume.
Hivyo basi tunayapa nguvu maneno ya Abibakri Al-Asammu, na maandiko ambayo mengi yake ni habari yenye wapokezi wengi na kuunganisha kati ya maelezo hayo ni inawezekana, wala haiwezekani kuipa nguvu habari juu ya habari, na Aya ipo wazi katika ujumla wa hukumu za dia katika uuwaji wa makosa, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Basidi ya au fidia ikabidhiwe kwa ndugu wa maiti} [AN NISAA]. Na Mtume S.A.W amebainisha dia kwa kadhia zote ni “Kutoa ngamia mia moja” .
Amesema pia kwa mtazamo huu Sheikh Muhammad Al-Ghazaliy katika kitabu chake cha As-Sunnatun-Nabawiyah baina Ahlul-Fiqhi wa Ahlul-Hadithi ambapo amesema: “Watu wa Hadithi wamefanya dia ya mwanamke ni nusu ya dia ya mwanamume, na hii ni fikra mbaya na maadili mabaya yamekataliwa na Wanachuoni wahakiki, kwani dia ndani ya Qur`ani ni moja kwa mwanamume na mwanamke, na kudhania kuwa damu ya mwanamke ni rahisi sana na haki yake ni ya kupuuzwa ni dhana ya uwongo inapingana na uwazi wa Qur`ani( ).
Kama vile Sheikh Yusufu Qardhawiy amesema kauli hii ( )na Sheikh Mustafa Zarqa( ).
Hekima ya dia ya mwanamke kuwa nusu ya fidia ya mwanamume.
Muislamu mwenye Imani imara hufuata Sharia ya Mwenyezi Mungu akiwa na yakini na hekima ya Sharia Takatifu, ameifahamu hekima iliyopo au hakuifahamu, lakini pamoja na hayo hakuna ubaya kutafuta kujua hekima iliyopo, kwa sababu kuifahamu hekima kunazidisha uyakini na utulivu, kama vile ndani yake kuna aina ya majibu ya shaka zinazoibuka, na yanayotajwa kwenye maudhui hii:
Kuwa dia ya mwanamke nusu ya dia ya mwanamume ndani yake hakuna maana ya kupunguza hadhi na heshima ya mwanamke au uwezo wake, wala hakuna dharau katika kumfanyia uadui, hilo ni kwa vile dia hailazimishwi yenyewe peke yake isipokuwa pale panapotokea mauaji ya makosa, ama lau ingekuwa kuuwa kwa makusudi basi mwanamume na mwanamke ni sawa sawa kwenye hukumu ya kisasi.
Na dia kwa hali yoyote ile si dia ya mbadala wa uhai wa mtu au ni thamani yake, bali yenyewe ni aina tu ya kufidia kwa ndugu zake kwa kule kumpoteza kwao ndugu yao akiwa ni tegemezi la uzalishaji, kwa mwanamke ni chini kidogo kwa mwanamume, ambapo mwanamume anafanya kazi na anapata pato kwa ajili ya familia yake, kukosekana kwake kuna sababisha hasara kubwa kwa familia yake na ndugu zake ndipo dia kwa upande wake imekuwa ni kubwa zaidi.
Ikiwa patasemwa: Wanawake katika zama hizi wanashiriki kwa nguvu kubwa katika kazi nyingi wakiwa bega kwa bega mwanamume, je dia ya wanawake hawa ni nusu ya dia ya mwanamume au yenyewe ni sawa sawa?
Tunasema: Mfumo wa Uislamu unamzingatia mwanamume kwa kawaida ndio ambaye anayefanya kazi ili kuimarisha kipato cha familia, hivyo ikawa ni sahihi kulipwa dia yake kikamilifu, wakati ambapo mwanamke anatekeleza majukumu mengine yenye umuhimu mkubwa, hivyo hasara ya kumpoteza kwake ni hasara ya kiwango cha chini cha mali, wala hilo halimaanishi kabisa kuwa ndio thamani yake au ndio thamani ya mwanamume,kinachozingatiwa katika utengenezaji Sharia na sheria ni hali jumla ya kawaida, na wala sio hali chache za mmoja mmoja, hakuna shaka kuwa wanaume ndio watendaji zaidi katika masuala ya kazi na kuchuma kuliko wanawake ndani ya jamii za Kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Mustafa Abdulkareem. 6/11/2007

Share this:

Related Fatwas