Imamu wa Elektroni

Egypt's Dar Al-Ifta

Imamu wa Elektroni

Question

 Ni ipi hukumu ya Kisheria juu ya utumiaji wa kifaa cha Elektroniki katika Swala?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Uislamu kama mfumo na maisha haupingani na mafanikio ya kielimu ni kiasi cha kushirikiana na mafanikio hayo, ikiwa ni kwenda sambamba na utambuzi wa Uislamu wa elimu na Wanachuoni na nafasi zao katika kuijenga dunia na kuiendeleza, pia kumrahisishia mwanadamu katika mambo yote ya maisha yake. Katika ofisi ya Mufti wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri limefikishwa ombi na kupewa nambari 3011 la mwaka 2005 likiwa na swali kuhusu hukumu ya Kisharia ya kutumia kifaa cha elektroniki, katika swali imekuja kuwa kifaa hiki ni ibara ya spika mbili ndogo huzivaa mwenye kuswali masikioni mwake wakati wa kuanza kuswali, kwa kubonyeza tu hizo spika kabla ya kutoa takbira ya kuhirimia Swala anaweza kupangilia rakaa mbili au tatu au nne sawa na idadi ya rakaa za Swala za Faradhi au Sunna, na mwenye kuswali anasikia yafuatayo:
1- Takbira ya kuhirimia Swala (Allahu Akbar) kisha anasikia kifaa kinasoma Suratul-Fatiha, kisha kinampa nafasi mwenye kuswali baada ya hapo inayomwezesha kusoma Suratul-Fatiha mwenyewe.
2- Baada ya kumaliza kusoma Suratul-Fatiha, hicho kifaa kinaanza kusoma Aya zingine za Qur'ani.
3- Baada ya kumaliza kusoma mwenye kuswali atasikia takbira ya kurukuu.
4- Baada ya hapo atasikia “Samiallahu liman Hamidah” kwa ajili ya kuinuka kutoka katika rukuu.
5- Kisha atasikia takbira ya kwenda kwenye sijida ya kwanza, kisha takbira ya kikazi kidogo cha kati ya sijida mbili, kisha atasikia takbira ya sijida ya pili, kisha takbira ya kuinuka ili kuanza rakaa ya pili, au takbira ya kukaa kikazi cha kusoma At-Tahiyyat.
6- Baada ya kumaliza idadi ya rakaa zilizopangiliwa kifaa kinasimama kufanya kazi chenyewe tu.
Sifa za kifaa hiki:
1- Kutoa fursa kwa mwenye kuswali kusikia idadi nyingi za Aya za Qur'ani Tukufu wakati wa Swala tano za kila siku, kisha kinamwezesha kukamilisha Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa uchache mara moja kila baada ya miezi minne au chini ya muda huo sawa na mpangilio wa programu kwenye kifaa hicho.
2- Kupunguza uwezekano wa kusahau katika Swala kwa kiasi kikubwa hasa kwa upande wa watu wazima, kwa sababu kila takbira inakuwa na sauti maalumu anayoizoea mtumiaji baada ya masiku machache.
3- Kifaa kinawapa Waislamu ulimwenguni hasa waliopo katika nchi zisizozungumza lugha ya Kiarabu kuzoea kutamka kwa usahihi na kusoma Qur'ani kwa usahihi na kujifunza pamoja na kufanya mazoezi endelevu ya kusoma Qur'ani Tukufu, kisha ataweza kuhifadhi Aya chache ikiwa itawezekana.
4- Kinawasaidia Waislamu kutamka Qur'ani Tukufu kwa sura salama katika Swala tano za kila siku, pia katika Swala za Sunna na zile za kisimamo cha usiku.
Maelezo Muhimu:
1- Tunapenda kusisitiza kuwa kifaa hiki si mbadala wa Imamu kwa hali yoyote ile, bali chenyewe kimetengenezwa kwa mtu anayeswali peke yake, kama vile sio mbadala kwa sura yoyote ile katika sura za Swala ya pamoja.
2- Tutamueleza mwenye kuswali dalili kwa mtumiaji juu ya wajibu wa kusoma Suratul-Fatiha, na wajibu wa kusoma At-Tahiyyat yeye mwenyewe, na kufuata hatua zote za Kisharia katika Swala.
Likaja jibu kutoka ofisi ya Katibu Mkuu wa Mufti wa Misri kama ifuatavyo:
Hicho kifaa kwa mujibu tulivyosoma kwenye swali husika na uzoefu wetu wa kukitumia, kinafaa kukitumia kwa upande wa Kisharia kwa ujumla, pamoja na kuwa tunapendekeza mambo ya kuboreshwa zaidi ambayo ni:
Kukifanya kisomo kwa mfumo wa msahafu unaofundisha, ambapo msomaji anasoma kisha anaacha nafasi ili mwenye kuswali naye asome baada ya hapo.
Kutumia rikodi za Wasomi wazuri wa Qur'ani kwa upande wa usomaji wa Tajwiid na kusoma kawaida.
Kuongeza maelezo ya Tahiyyat kwa sauti na kumswalia Mtume S.A.W. katika maeneo yake sawa na muundo wa Swala.
Kuweka uwezekano wa kuteua Qur'ani yenye kusikika kuifanyisha kazi kwa kurasa sehemu za robo au vinavyofanana na hivyo ili kwenda sawa na Swala ambazo ni lazima kwa mwenye kuswali kurefusha au kupunguza.
Tunapendelea lau tutaweka baada ya takbira ya kuhirimia Swala maneno ya dua ya ufuguzi wa Swala, na katika rukuu na sujudu kuleta utajo wote na maombi yake.
Kuna maelezo mafupi mengine kwa mtafiti wa kazi za kifaa hiki, nayo ni kusikia mwenye kuswali Qur'ani Tukufu kwa kutumia kifaa hiki - kama ilivyokuja kwenye swali - ukweli ni kuwa kinachotakiwa kwenye Swala ya mtu peke yake ni kusoma na wala sio kusikia, hivyo kusikia kunakuwa katika Swala ya wengi au Swala ya jamaa ya sauti, ambapo Maamuma wanasikia kisomo cha Imamu, ama Swala ya mtu peke yake basi yeye mwenyewe anasoma kwa kusikia yeye mwenyewe, hivyo basi mfumo pendekezwa wa Msahafu unaofundisha ni wenye kufikiwa lengo la Swala ya mtu peke yake inayotakiwa na muulizaji. Naye Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi
Yanayozingatiwa katika swali na jibu ni kuwa kifaa husika hakichukui nafasi ya Imamu kwa hali yoyote ile, bali ni kifaa chenye kusaidia na kuongoza tu, mwenye kuswali peke yake ambaye anakitumia hana zaidi ya malipo ya Swala ya peke yake, ametanguliza maelezo mwenye kuuliza na wala kwenye jibu hakuna kinachofahamika kinyume na hivyo, ama yaliyoenea katika vyombo vya habari na kunukuliwa na watu bila ya kuwa na uhakika au uchunguzi wa kina kuwa ofisi ya Mufti imepitisha matumizi ya kifaa hicho cha elektroniki kwa kuchukua nafasi ya Imamu na nyuma ya kifaa hicho watu wanaweza kuswali na kuzingatiwa iwe hiyo ni Swala ya jamaa au ya pamoja; huo ni uzushi na ni kauli batili, na Mtume S.A.W. amesema: “Inatosha mtu kuwa mwongo kwa kuzungumza kila anachosikia”( ).
Mambo yamebakia kuyafafanua zaidi na kujibu baadhi ya pingamizi ambazo zimekuja katika yale tuliyoyaeleza kuhusu kufaa kutumia hicho kifaa kilichotajwa, na hufupishwa pingamizi hizi kama ifuatayo:
1- Kifaa hiki kinampelekea mwenye kuswali kutokuwa na unyenyekevu kwenye Swala.
2- Kifaa hiki kinampelekea mwenye kuswali kusikiliza tu kisomo cha Qur`ani bila yeye mwenyewe kusoma hata Suratul-Fatihah hasomi, na kwa sababu hii Swala yake haitafaa au kwa maana ya haitasihi kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Hakuna Swala kwa asiyesoma Suratul-Fatiha”( ).
3- Kifaa hiki kinapelekea kutoweka umuhimu wa kuhifadhi Qur'ani.
4- Kifaa hiki pia kitapelekea Waislamu kutoziendea Swala Misikitini.
5- Na asiyehifadhi Qur'ani Mwenyezi Mungu Mtukufu hajamlazimisha kusoma asichohifadhi kwa sababu hili halipo kwenye uwezo wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hailazimishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo}[AL BAQARAH: 286]. Ikiwa hajalazimishwa kusoma asichohifadhi, basi kulazimishwa kwake kisichokuwa cha lazima ni jambo batili( ).
Ama kuhusu kifaa hiki kinapelekea kwa mwenye kuswali kutokuwa na unyenyekevu ndani ya Swala, hatukubaliani na hilo kuwa kifaa hiki kinaondoa unyenyekevu, kwani masuala yanatofautiana kwa kutofautiana watu bali na hali pia, kisha kadhia yetu hapa ni kuathiri kwa Swala au kutoathiri, ama kukosekana kwa unyenyekevu hakuna athari ya kutofaa Swala, kwa sababu huo unyenyekevu si katika nguzo za Swala au sharti la kufaa kwa Swala, kwani Mtume S.A.W. aliswali akiwa amevaa nguo yenye mapambo na akasema: “Hakika nguo hii imenishughulisha kwenye Swala yangu”( ). Pamoja na hilo Mtume S.A.W. hakukatisha Swala yake na wala hakusema kuwa hili linaharibu Swala wala kusema kuwa alirudia Swala, ikiwa tutakubali kuwa kusikiliza kisomo kwenye kifaa hiki na kurudia nyuma yake kunaondoa unyenyekevu, basi hilo halitakuwa dalili ya kuharibika kwa Swala, bali kifaa hiki kinamtenganisha mwenye kuswali na sauti zinazomzunguka ambazo huenda zikamshughulisha kwenye Swala yake, chenyewe kinamfanya mwenye kuswali kuwa na umakini zaidi katika Swala, mwishowe kinampeleke kwenye unyenyekevu unaohitajika.
Ama kuwa kifaa hiki kinamfanya mwenye kuswali anasikiliza tu kisomo cha Qur'ani wala yeye mwenyewe hasomi hata Suratul-Fatihah hivyo Swala yake haikubaliki. Tunasema hivi: Fatwa imesema kisomo katika kifaa hiki ni kama vile kisomo kwenye programu ya msahafu unaofundisha, ambapo kunakuwa na nafasi ya kutosha baada ya kusoma msomaji kwenye kifaa hiki Aya mwenye kuswali atasoma Aya akifuatiza nyuma ya hiki kifaa na kwa mazingira haya mwenye kuswali atasoma Suratul-Fatiha na Aya zingine chache za Qur'ani, basi Swala yake kwa hali hii ni sahihi In Shaa Allah.
Ama kuhusu kifaa hiki kinapelekea kupoteza umuhimu wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu tunasema: Bali chenyewe kinapelekea kuhifadhi Qur'ani kwa njia ya kina zaidi kupitia kuwasikiliza wasomaji wazuri zaidi wa Qur'ani.
Kuhusu kupelekea Waislamu kutoiendea Misikiti kwa ajili ya Swala, chenyewe hakipelekei kabisa Waislamu kutoziendea Swala za jamaa, kwa sababu kuswali na kifaa hiki hakuchukui kabisa nafasi ya Swala ya jamaa, kwani thawabu zake ni sawa na thawabu za mtu mwenye kuswali peke yake ikiwa ataswali peke yake.
Kwa upande wa mtu asiyehifadhi Qur'ani Mwenyezi Mungu Mtukufu hamlazimishi kusoma asichokihifadhi, kwa sababu hilo halipo kwenye uwezo wake. Tunasema kuwa kisomo cha mwenye kuswali kwa upande wa kuwa ni chenye kuhitajika Kisharia, ima kwa sura ya lazima kama vile kusoma Suratul-Fatiha katika kila rakaa, au kwa sura ya usomaji wa Sunna kama vile kusoma Aya chache za Qur'ani baada ya kusoma Suratul-Fatihah katika maeneo ambayo yanahitaji kisomo hiko. Hivyo wajibu na Sunna ni aina mbili: Ya kwanza ni makusudio, ya pili ni hukumu za makusudio, na Sharia inatoa thawabu kwenye njia zinazopelekea utiifu kama ambavyo inatoa thawabu kwenye makusudio( ). Kwa maana hiyo kusikiliza kisomo cha hicho kifaa ni jambo lenye kuhitajika Kisharia kwa sababu ni njia ya kuelekea kwenye kusudio lingine nalo ni kusoma kwa msomaji, wala hakuna katika hilo ulazima kwa mwanadamu kwa kile asicho na uwezo nacho.
Faida ya kifaa hiki kinajitokeza katika kutoa mafundisho kwa asiyejua hukumu na masharti ya Swala kwa wale walioingia kwenye Uislamu hivi karibuni na wala hawawezi kusoma ndani ya Swala, au mtoto mdogo ambaye anataka kujifunza ibada ya Swala, hivyo kifaa hiki kinakuwa ni muongozo kwake.
Imebainika katika hili kupitia yale tuliyoyaeleza kuwa mwenye kuswali peke yake Swala ya lazima au ya Sunna inafaa kwake kusikiliza kisomo kwa kutumia kifaa hiki, na kufuatisha kisomo nyuma ya sauti ya hicho kifaa, na Swala yake inakuwa ni sahihi na inafaa Kisharia, na wala sio makusudio ya hicho kifaa kuchukua nafasi ya Imamu, bali hapa tumeita katika anwani kumsikiliza Imamu wa elektroniki, kwa sababu maudhui huenda watu wakaisikia na wakapeana kwa anwani hii.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

 

 

 

Share this:

Related Fatwas