Ukati kwa Mtazamo wa Maadili ya Kii...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukati kwa Mtazamo wa Maadili ya Kiislamu

Question

 Ni ipi maana ya Ukati katika mfumo wa Maadili ya Kiislamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Hakika Uwastani, Unyoofu, Usimamizi, Uwianifu na Uadilifu ni Msingi miongoni mwa Misingi ya Dini ya Uislamu, na Ubadhirifu, kujikweza, na kupindukia kwa upande mmoja, na ubahili, upungufu na ulegevu kwa upande mwingine si katika mwenendo wa Waumini wanaoshikamana na Maana Sahihi za Kiislamu zinazotokana na Qur'ani Tukufu ambayo Imesema; {Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wastani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume aweni shahidi juu yenu.} [AL BAQARAH 143]
2- Kwa hiyo Njia ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu iko wazi na salama, haina kupindapinda Haina mapindo wala kugubikwa na ugumu wa kutoeleweka. Na mtu mwenye hekima ni yule ambaye ana msimamo katika jambo lake na anamtii Mola wake, na anafuata vyema mienendo yake, na kwa hivyo, haendi kombo kwa kuyavamia aliyokatazwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala haleti madai yoyote ya rai yake Kinyume na Mwenyezi Mungu, na wala hadai kuwa yeye ana ujanja au nguvu, na wala hatumii njia za kutisha ili kuwafanyia vitimbi waja wa Mwenyezi Mungu, wala hawi bendera fuata upepo katika kuziendea fujo na Uadui Na wala haiwajibiki azembee au azidishe katika jambo la Dini yake kwa ajili ya kujikweza au kujionesha kwa watu pamoja na Unafiki.
3- Na katika Hali za Ukati wa Kimaadili katika Uislamu ni mtu kufanya kazi kwa hekima kwa kuitumikia kheri na manufaa kwa wengine. {Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili} [AL BAQARAH 269]. kwani hekima ni Ukati wa Uadilifu, na Kheri ni Fadhila na mwenye hekima ni Mjuzi na Mkweli.
4- Hakika miongoni mwa uwazi wa ukamilifu wa Mfumo wa Uislamu ni kuchunga kwake Ukati adilifu ambao ndani yake hakuna ubadhirifu au Uharibifu (ubahili), hakuna matumizi mabaya au ulegevu (kupindukia) bali hakika mambo yalivyo, hiyo ni Kheri yenye fadhila inayoielezea Kheri na Ukweli katika kila kitu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Sema: Mwombeni Allah au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolotemnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo}. [AL ISRAA 110]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: { Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna na kujifakhirisha (18). Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyo zidi ni sauti ya punda. (19) [LUQMAAN 18-19]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi}. [AL ISRAA 29]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Rejeo: Dkt. Hasan As Sharqawiy, Maadili ya Kiislamu, Cairo, Muasasat Mukhtaar kwa kutangaza na kuchapisha, chapa ya kwanza, 1988. Ku. (15-17, kwa kufupisha)

 

Share this:

Related Fatwas