Kuangalia (Kutazama) Mieleka
Question
Tumepitia barua iliyokuja kutoka / Jopo la utafiti wa mambo ya Kiislamu, ya tarehe 23/06/2013 iliyopewa namba 300 ya mwaka 2013, imekusanya maudhui kutoka idara kuu na kamati zake na kuelekezwa ofisi ya Mufti, hii ni kutokana na maadhimio ya kamati ya utafiti wa kifikhi kwenye kikao chake cha kumi na tano katika mzunguko wake wa arubaini, kilichofanyika siku ya alhamisi tarehe 04/08/1434H sawa na tarehe 13/05/10, kuhusu kitabu kilichopokelewa na Katibu Mkuu wa jopo la utafiti wa mambo ya Kiislamu kutoka ofisi ya Imamu Mkuu na Shaikh Mkuu wa Al-Azhar, kilichowasilishwa na Mwl /Mustafa Muhammad Mustafa – Mwenyekiti wa Jumuiya mpya ya kitaifa ya haki za binadamu na maendeleo ya watu ambapo kinaeleza:
Nimewasilisha ombi kwa Mhe. Waziri pamoja na msaidizi wa kwanza wa Waziri wa mambo ya ndani anayehusu masuala ya haki za binadamu, kuhusiana na tatizo la kuenea kwa idadi kubwa ya watu wanaotazama mchezo wa mieleka huru kwenye maeneo ya umma migahawa na hata majumbani, na yanayopelekea kwenye hilo ikiwa ni pamoja na kuzalika kwa maradhi mapya yanayoharibu amani na usalama wa jamii, ikiwa pia na athari mbaya hasa kwa watoto wadogo, na kuenea kwa uhalifu hasa ndani ya masiku ya hivi karibuni, hivyo basi tunategemea kutoka kwenu kupata Fatwa kwenye jambo hili hatari ikiwa pamoja na athari zake mbaya kwa jamii, na kuonekana kwetu aina mpya ya upingaji chini ya kile kinachoitwa “Mieleka huru”.
Answer
Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Uislamu haujazuia kufanyika michezo ya nguvu bali Waislamu wamekubaliana juu ya kufaa kwake. Imamu Ibn Kudama Al-Maqdasiy mfuasi wa madhehebu ya Imamu Hambaliy amesema ndani ya kitabu cha Al-Mughniy 9/368 chapa ya Dar Ihayaau At-Turaath Al-Arabiy: “Wamekubaliana Waislamu kwa ujumla juu ya kufaa kwa michezo ya mashindano”.
Mwenye kuzingatia atakuta kuwa jumla ya amri za Kisharia zimejengewa na harakati, na harakati ndio nguzo na msingi wa mchezo, kama vile ibada ya Swala pamoja na ibada mbalimbali za Hija, kumtembelea mgonjwa, kutembea kwenda Msikitini, kuhangaika sehemu mbalimbali kutafuta elimu na mfano wa hayo.
Na zaidi ya hayo imepokelewa katika maandiko ya kidini kauli zinazo hamasisha michezo na kusisitiza, na kunufaika na michezo hiyo ikiwa ni pamoja na kupata sifa ya kuwa mtu mwenye nguvu za mwili, kutokana na hilo Mola Mtukufu Anasema: {Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo} [AL ANFAAL: 60], hivyo kujiandaa: Ni kuchukua kitu wakati wa kuhitajika. Na nguvu: Hukubalika kwa kile kitakacholeta nguvu zaidi kwenye vita dhidi ya maadui, na yaliyopokelewa kwenye vitabu vya tafasiri neno nguvu kuwa ni vifaa vya kupambana katika jihadi kama vile wanyama aina ya farasi au mkuki mshale au silaha yeyote ambayo matumizi yake hayakiuki ujumla wa maana ya Aya kwenye nguvu za mwili, kwani tafasiri ya Aya kwa baadhi ya makusudio ya watu ni kwa upande wa tafauti ya aina, hivyo Mwanachuoni Al-AaluusIy amesema katika tafasiri yake 10/24 chapa ya Dar Ihyaau At-Turaath Al-ArabIy: “Kwa maana ya kila kinachoongeza nguvu vitani chochote kiwacho”.
Vile vile Hadithi aliyopokea Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Hurairah R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Muumini mwenye nguvu ni mbora na mwenye kupendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko Muumini dhaifu”. Imamu Al-Kurtuby amesema: “Mwenye nguvu ya mwili na nafsi, mwenye kutekeleza dhamira, ambaye anaweza kuendesha kazi mbalimbali za Ibada kuanzia ibada za hija funga kuamrisha mema na zinginezo ambazo zinaimarisha dini” nukuu kutoka kwa Ibn Allaam ndani ya kitabu cha “Dalilul-Faaliheen” 2/317 chapa ya Dar Al-Maarifah.
Ikiwa mtu kuwa na nguvu ni jambo linalohitajika Kisharia basi na njia ya kupata hizo nguvu pia ni zenye kuhitajika, kwa sababu njia zinahukumu zinazokusudiwa, pindi michezo ya mwili ilivyokuwa ni njia ya kupatia nguvu basi imekuwa ni yenye kuhitajika kwa upande huo.
Imepokelewa kwa Imamu Shafi na Ahmad pamoja na Abu Daud na Ibn Maja pia Ibn Habban na wengine kutoka kwa Mama wa Waumini Bibi Aisha R.A kuwa alikuwa na Mtume S.A.W safarini, alisema tukashindana na nikamshinda kwenye kutembea kwa miguu, pindi nilipozidiwa na unene tulishindana tena kwenye safari nyingine na Mtume S.A.W akanishinda, kisha akasema Mtume S.A.W: “Hii nimekushinda kama ulivyonishinda pale mwanzo”.
Imepokelewa kutoka kwa Imamu BukhariY kutoka kwa Salamah Ibn Al-Akuui R.A amesema: Mtume siku moja alipita kwa watu wa kabila la Aslama wakiwa wanashindana kurusha mkuki. Mtume S.A.W akasema: “Rusheni mikuki enyi watoto wa Mzee Ismail A.S kwani baba yenu Nabii Ismail A.S alikuwa mrushaji mzuri wa mkuki, rusheni na mimi nikiwa na kundi la pili”, anasema Mtume S.A.W akajiunga na kundi lingine na akawaauliza: “Ni kwanini nyinyi hamrushi mikuki?” wakasema: Ni namna gani tunarusha mikuki na Wewe ukiwa nao? Akasema Mtume S.A.W: “Rusheni na mimi nikiwa pamoja na nyinyi nyote”.
Imepokelewa pia kutoka kwa Abu Dawud na wengine kutoka kwa Uqbah Ibn Aamir R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Si katika upuuzi michezo ya aina tatu: Mtu kumfunza nidhamu farasi wake, mtu kucheza na familia yake, na kurusha mkuki, na mwenye kuacha kurusha mkuki baada ya kujifunza kwa utashi wake tu, basi afahamu kuwa hiyo ni neema ameiacha” au amesema: “Aliyoikufuru”.
Imepokelewa katika upande wa Hadithi: “Wafundisheni watoto wenu wa kiume kuogelea na kurusha mkuki” imepokelewa na Ibn Mandah kutoka Hadithi ya Bakri Ibn Abdillah Ibn Rabii Al-Ansary ikiwa imenyanyuliwa daraja mpaka kwa Mtume S.A.W upokezi wake ni dhaifu lakini ina mashahidi wengi kama ilivyokuja kwenye kitabu cha Makasid Al-Hasna cha Haafidh Sakhaawy ukurasa wa 462 chapa ya Dar Al-Kitaab Al-Arabiy.
Imepokelewa kutoka kwa Imamu Al-Baihaqy kutoka kwa Ibn Abbas R.A amesema: “Huenda Omar Ibn Khatwab R.A aliniambia. Njoo nikushinde kwenye maji nani atakuwa na pumzi ndefu zaidi na sisi tukiwa tumevaa nguo za kuhirimia Hija”. Na Hadithi zingine pamoja na athari zinazohusu aina mbalimbali za michezo ya nguvu.
Inaonesha juu ya kufaa kuangalia mfano wa aina hii ya michezo: Hadithi iliyopokelewa na Mashaikh waili – na tamko la Imamu Muslim – kutoka kwa Mama wa Waumini bibi Aisha R.A amesema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu nimemuoa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W akiwa amesimama kwenye mlango wa chumba changu na Wahabeshi wakiwa wanacheza ndani ya Msikiti wa Mtume S.A.W na Mtume akiwa ananifunika kwa kitambaa chake ili niweze kuangalia mchezo wao, kisha akawa anasimama kwa ajili yangu ili niweze kuondoka”, hii ni kukubali kwake Mtume S.A.W kwa Bibi Aisha kuangalia mchezo wa Wahabeshi ili kuburudika.
Ama kuhusu mchezo wa mieleka, umekuwa ni katika mchezo maarufu sana katika mazingira ya Kiarabu kabla ya Uislamu, imepokelewa kuwa vijana wao walikuwa wakishindana kucheza katika maeneo ya wazi nje ya miji na vijiji, wakiwa wanashindana michezo ya kupanda farasi, mieleka, michezo ya kukimbia na kurusha mshale. Angalia kitabu cha Al-Mufadhal fii taarekh Al-Arabu kabla Al-Islamu, kitabu cha Dr. Jawadi Ally 15/294 chapa ya Dar Saaqiy.
Baada ya kuja Uislamu ukatambua michezo hii, kwani yenyewe huimarisha mwili na kuupa nguvu, na hukusanya kati ya michezo ya starehe na ya kipuuzi iliyo halali na manufaa ya mtu na jamii, pamoja na hayo dini imeashiria umuhimu wa kudhibiti nafsi ambapo nguvu wakati mwingine husukuma nafsi kwenye ukiukaji, imepokelewa na Imamu Muslimu kutoka kwa Abi Huraira R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Mtu mwenye nguvu si kwa kufanya mambo kwa haraka bali mtu mwenye nguvu ni yule ambaye huimiliki nafsi yake wakati anapokuwa na hasira”.
Na amepokea Tabraniy katika kitabu cha Mkaarimu Al-Akhlaak ukurasa wa 325 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah kutoka kwa Anas Ibn Maliki R.A kuwa Mtume S.A.W siku moja alipita kwa watu wakiwa wananyanyua mawe, akauliza ni nini hii? Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni mawe tulikuwa wakati wa zama za ujinga tukiyaita: Mawe ya watu wenye nguvu, akasema Mtume S.A.W: “Je niwaambie mtu mwenye nguvu zaidi kwenu? Ni yule mwenye uwezo zaidi yenu ya kumiliki na kudhibiti nafsi yake pale anapokuwa amekasirika”
Imepokelewa katika Sunna kitendo chake na kukubali kwake, kwani Rakanah Ibn Abdu Yazidi alikuwa ni Mkuraishi mwenye nguvu sana, hivyo akaja ili kucheza mieleka na Mtume S.A.W na Mtume akacheza naye, mpaka imepokelewa kuwa aliweza kumuweka chini akiwa hawezi kuizuia nafsi yake kwa chochote. Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhy pamoja na Ibn Is’haka katika kitabu cha Sira.
Na amepokea Khatib katika kitabu cha Al-Muutalifu wal Mukhtalifu kwa upokezi sahihi kutoka kwa Ibn Abbas R.A kuwa Yazidi Ibn Rukana alicheza mieleka na Mtume S.A.W na Mtume akamshinda mara tatu, kila mara mshindi anachukua mbuzi mia moja, ilipofika mara ya tatu akasema: Ewe Muhammad hakuna mtu yeyote aliyewahi kuuweka mgongo wangu ardhini kabla yako, na hakukuwa na mtu ninaye mchukia zaidi kuliko wewe, na mimi ninashuhudia kuwa hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na hakika Wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume S.A.W akasimama na kumrudishia mbuzi wake. Angalia kitabu cha Al-Bidaya wannihaya cha Hafidhi Ibn Kathiir 3/104 chapa ya Dar Al-Fikri, na sherehe Zarkany 6/103 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah.
Amesema Imamu Suhaily katika kitabu ha Rawdhul-Anfu 3/106, 107 chapa ya Dar Ihyaau At-Turath Al-Araby kuwa Kaldah Ibn Asyad Ibn Khalaf – alikuwa ni Muarabu mwenye nguvu sana – mpaka amefikia kutokana na nguvu zake – vile walivyoelezea – kuwa alikuwa anasimama kwenye ngozi ya ng’ombe na kuichana bila yeye kuyumbayumba. Mtume S.A.W alimwita kucheza naye mieleka na akasema: Ikiwa utanishinda basi nitakuamini, ndipo Mtume akacheza naye na kumshinda mara nyingi lakini hakuamini.
Amepokea Imamu Ibn Jarir Tabary katika kitabu cha Taarekh 2/505 chapa ya Dar Turath Beirut kuwa pindi Mtume S.A.W alipotoka kwenda kwenye vita vya Uhudi alimtaka Raafii na Samura wacheze mieleka na ndipo Samura alicheza mieleka na Raafia na Mtume S.A.W akaruhusu na kushuhudiwa mchezo huo na Waislamu wengi.
Amepokea Hakim katika kitabu cha Al-Mustadriku kutoka kwa Abdillah Ibn Omar R.A kuwa Omar Ibn Khattab alikuja na swala ikiwa inakimiwa akiwa na watu watatu mmoja wao ni Abu Jahshi Laithy akasema: Simameni na mswali na Mtume S.A.W wakasimama wawili Abu Jahshi akakataa kusimama, ndipo Omar akamwambia: Swali pamoja na Mtume S.A.W ewe Aba Jahshi, akasema: Si simami mpaka aje mtu mwenye mkono wenye nguvu zaidi ya mimi, na mtu katili zaidi ya mimi anishinde kwenye mieleka, kisha aukanyage uso wangu ardhini kwenye vumbi, akasema Omar: Nikasimama mbele yake na mimi nilikuwa nina mkono wenye nguvu zaidi ya mkono wake, nikacheza naye mieleka na kumshinda kisha nikaukanyaga uso wake kwenye vumbi.
Na amesema Hafidh Ibn Katheer katika kitabu cha Al-Bidaya Wannihaayah 8/102 kuwa Mfalme wa Roma alimpa Khalifa Muawiyah R.A changamoto na mtu wa Kihabeshi anaelezewa kuwa ni mwenye nguvu kwa watu wa Roma, ndipo akaja Muhammad Ibn Hanafiah naye ni Ibn Ally Ibn Abi Talib R.A akamwambia mtu wa Roma: Ima uniweke chini au mimi nikuweke wewe chini, na unipe mkono wako au mimi nikupe mkono wangu, ni yupi kati yetu mwenye uwezo wa kumuinua mwenzake sehemu yake atakuwa amemshinda kinyume na hivyo atakuwa ameshindwa, akasema kumwambia: Unataka nini? Utakaa au nikaye? Akasema Rumiy: bali kaa wewe, ndipo Muhammad Ibn Al-Hanafiah akakaa na kumpa Rumy mkoko wake, ndipo akajitahidi Rumy kwa uwezo wake wote na nguvu zake kumuondoa sehemu yake au kumtikisa ili kumuinua lakini hakuweza kufanya hivyo, wala hakupata njia ya kufanikisha hilo hapo ndipo aliposhindwa Rumy na kuonekana na wale aliyokuwa nao watu wa nchi ya Roma kuwa ameshindwa, kisha Muhammad akasimama na kumwambia Rumy: Kaa chini, akakaa na kumpa mkono wake Muhammad, hakuchukua muda isipokuwa alisimama haraka na kumuinua juu kisha kumtupa kwenye ardhi.
Wametaja Wanachuoni hukumu ya kufaa kucheza mieleka kwa mfumo wa maneno yao kwenye mashindano, miongoni mwa hayo ni pamoja na aliyoyasema Imamu Ibn Juzayy mfuasi wa Imamu Malik katika kitabu chake cha: Al-Kawaanin Al-Fiqhiyah ukurasa wa 276 – 277 kuwa: Mashindano ya kucheza na farasi inafaa, na ikasemwa: Ni yenye kutakiwa, ikiwa mchezo bila zawadi kwa mshindi inafaa moja kwa moja kwenye mchezo wa farasi na mwingine katika wanyama, mchezo wa kueleza jahazi, na kati ya mchezo na ndege, ili kufikia kheri haraka, unafaa mchezo wa mbio na katika kurusha mawe na mieleka, ama ukiwa ni kwa malipo nayo ni rehani basi mchezo una sura tatu: Sura ya kwanza: Kiongozi au mtu mwingine kutoa mali atakayo chukua mshindi jambo hili ilinafaa. Sura ya pili: ni kutoa kila mmoja kati ya washindani wawili mali, mwenye kushinda kati ya wawili hao atachukua mali ya mwenzake na kushikilia vitu vyake hali hii haifai kwa makubaliano ya Wanachuoni, akiwepo mtu wa tatu na akapewa mali ikiwa atashinda na wala hatokuwa na chochote ikiwa atashindwa hali hiyo Ibn Al-Musayyab ameipitisha na Imamu Shafi lakini ameizuia Imamu Malik, hali ya tatu: Mmoja wa washindani kutoa mali, inafaa ikiwa mali hiyo haitorudi kwake na kuchukuliwa na mshinda asiye kuwa yeye au kwa walioshiriki.
Amesema Imamu Al-Imrany katika kitabu chake cha Al-Bayan fii Madhhabu Imamu Shafii 7/422 chapa ya Dar Al-Minhaaj: “Inafaa kucheza mieleka bila ya malipo”.
Akasema Imamu Ibn Kudama Al-Hanbaly katika kitabu cha Al-Mughny 9/368: “Ama mashindano bila ya malipo yanafaa moja kwa moja bila ya kuzuia kitu chochote, kama vile mashindano ya kukimbia, kucheza na majahazi, michezo ya kucheza na ndege, kucheza na tausi, punda, tembo na urushaji wa mkuki, na inafaa mchezo wa mieleka na kuinua mawe ili kumfahamu mtu mwenye nguvu zaidi.
Lakini hata hivyo kuna mkusanyiko wa tahadhari ambazo zinapaswa kujiepusha nazo, na masharti ambayo lazima yafikiwe wakati wa kucheza mieleka – na mfano wake katika michezo mingine – mpaka ikifikiwa hali inayofaa yenye kutajwa, nayo ni:
1-Kusiwe na mchezo wa kamari, kwa kuwekwa sharti la mali kwa pande mbili zenye kucheza mieleka, au kucheza ili watu kuweka vidau na wanao angalia, kwani Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli, uchafu ni katika kazi za shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa} [AL MAIDAH: 90]
2-Usifungamane na kukusudia kupoteza mambo yaliyo wajibu, mfano wa kuchelewesha ibada ya Swala nje ya wakati unaotambuliwa na Sharia, kwa sababu kukusudia hilo ni jambo haramu, na kinachopelekea kwenye haramu basi chenyewe ni haramu. Kitabu cha Kawaaidi Al-Ahkaam cha Imamu Al-Izz Ibn Abdulsalaam 2/218 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Ilmiyah.
3-Kutokuwepo ndani yake madhara kwenye nafsi au kwa kuzalisha ugonvi, kwani imepokewa na Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna kudhuru wala kujidhuru” kwa maana ya mtu asimdhuru ndugu yake wala kuhalalisha madhara kwake, kudhuru ni kuanza kitendo, na kujidhuru ni malipo yake. Kitabu cha Assalaam cha Shaikh San’aany 2/122 chapa ya Dar Al-Hadithi.
4-Isiendane na hali ya kuwa uchi, imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhy kutoka kwa Bahzi Ibn Hakim kutoka kwa baba yake na babu yake R.A amesema: Niliuliza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tupu zetu: Ni zipi zinazofaa kuzionesha na zisizofaa kuonesha? Akasema Mtume S.A.W: “Linda tupu yako isipokuwa kwa mkeo au anayemilikiwa na mkono wako”.
Amepokea Imamu Muslim kutoka kwa Abi Said Al-Khudry R.A kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Mwanamume asiangalie utupu wa mwanamume, wala mwanamke kuangalia utupu wa mwanamke”.
5-Wala kusiwe na kitendo cha kugusa tupu, kwa sababu kipindi cha kuwa ni haramu kuangalia haramu kugusa, kwa sababu kugusa ni zaidi ya kuangalia katika ladha na kuibua matamanio. Angalia kitabu cha Mughany Al-Muhtaaj cha Mwanachuoni Sharbiiny 4/215 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah.
6-Wala usiendane pamoja na vitendo vya uovu na matusi, imepokelewa na Tirmidhy kutoka kwa Ibn Masoud R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Si Muumini Muaibishaji wala Mlaanaji wala Mfanya uovu wala Mkosa haya”.
Amepokea Imamu Bukhari kutoka kwa Ibn Masoud R.A kuwa Mtume S.A.W amesema: “Kumtukana Mwislamu ni ufasiki”.
Udhibiti jumla unaozingatiwa kwenye haya yote ni: “Kutofungamana na yaliyo haramu” ikiwa mchezo utalazimika kuendana na sehemu katika hayo basi mchezo huo utakuwa ni haramu kuucheza, vile vile ni haramu kuuangalia na kuutazama, kwa sababu wakati huo unakuwa ni katika maovu, na kuangalia maovu na yaliyo haramu bila ya kuwepo haja ya Kisharia haifai, kwa sababu kuzoeleka kwake na kurudia kwake huzoesha nafsi haramu na kuathirika kidogo kidogo, kama vile ndani yake kuna aina kukubalika kwa mwenye kufanya yaliyo haramu na kuhamasisha kuendelea na kudharau, kwa hali hiyo mchezo huo unakuwa mlango katika milango ya ushirikiano kwenye dhambi, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Wala msisaidiane kwenye dhimbi na uadui} [AL MAIDAH: 02], na imepokelewa Hadithi na Imamu Muslim kutoka kwa Abi Saidi Al-Khudry R.A kuwa Mtume wa Mwneyezi Mungu amesema: “Mwenye kuona ovu mingoni mwenu basi aliondoe kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi atumie ulimi wake na kama hawezi basi kwa moyo wake na kufanya hivyo ni katika udhaifu wa Imani”. Amesema Shaikh Takiyyu Din Ibn Taimiyah Al-Hambaly katika kitabu cha Al-Fatawa Al-Kubra 1/300 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Ilmiyah – akielezea juu ya Hadithi - :”Ikiwa haikuwezekana hilo na likawezekana kuwa kutoangalia maovu basi na afanye hivyo, ambapo kuangalia maovu pasi na uwepo wa haja wala kutenzwa nguvu ni jambo linalokatazwa”.
Amesema Sayyidy Ahmad Dardiir katika watu wa Malik kwenye Sherhu Al-Kabiir 2/338 chapa ya Dar Ihyaau Turaath Al-Araby: “Kuangalia kilicho haramishwa ni haramu”.
Amesema Mwanachuoni Al-Jubeir katika kitabu chake cha Al-Iknaai cha Shaikh Al-Khatiib Sharbiiny 4/434 chapa ya Dar Al-Fikri: “Kila haramu ni haramu kukiangalia, kwa sababu kuna saidia kwenye maasi”.
Hivi sasa mwenye kuangalia mchezo wa mieleka huru atakuta kuwa haipo mbali na sehemu ya uharibifu uliotajwa hapo mwanzo.
Imekuja katika maamuzi ya tatu kwenye jumla ya maamuzi ya mkutano wa kumi wa jopo la Wanafiqhi wa Kiislamu huko Makka ndani ya mwezi wa mfungo pili kuanzia siku ya mwezi 24 mfungo tano mwaka 1408H sawa na tarehe 17 October 1987 mpaka siku ya Jumatano ya mwezi 28 mfungo tano 1408H sawa na tarehe 21 October 1987 kuhusu maudhui: “Mchezo wa bondia na mieleka pamoja na mieleka ya ng’ombe” yalifikiwa yafuatayo: “Baada ya kuzungumzia mambo haya kwa pande zake tafauti na matokeo ambayo yanayofikiwa kwenye aina hizi ambazo zimenasibishwa kwenye mchezo, na kuwa inaoneshwa kupitia runinga ndani ya nchi za Kiislamu na zinginezo, baada ya kupitia tafiti ambazo ziliwasilishwa kwenye jambo hili kwa amri ya Baraza la Jopo kwenye kikao chake kilichopita kupitia madaktari wenye weledi, na baada ya kupitia takwimu ambazo zilitolewa na baadhi yao kuhusu yale yanayotokea ulimwenguni ikiwa ni matokeo ya uchezaji wa mchezo wa mieleka, na yanayoangaliwa kwenye runinga ikiwa ni baadhi ya matatizo kwenye mieleka huru, Baraza lilifikia maamuzi yafuatayo:
La Kwanza: Mieleka: Baraza la Jopo kwa ujumla wake limekubaliana kuwa mieleka iliyotajwa ambayo imekuwa ikichezwa kwenye ulingo wa mchezo na mashindano ndani ya nchi zetu hii leo ni mchezo haramu katika Sharia ya Kiislamu, kwa sababu unachezwa kwenye msingi wa kuhalalisha maudhi kwa mshindi dhidi ya mwingine maudhi makubwa kwenye mwili wake, wakati mwingine inafikia hali ya upofu au uharibifu mbaya au matatizo kwenye ubongo, au kupelekea uvunjaji mbaya wa kiungo cha mwili au hata kifo, pasina kuhusika mpigaji au muuaji na washabiki wakiwa ni wenye kushangilia na kumuunga mkono mshindi, na kufurahia kero na madhara yaliyomfika aliyeshindwa, na mchezo haramu wenye kupingwa kwa ujumla wake katika hukumu za Uislamu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msijiingize wenyewe kwenye maangamizi} [AL BAQARAH: 195]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msiuwe nafsi zenu hakika Mwenyezi Mungu amekuwa kwenu ni Mwengi wa huruma} [AN-NISAA]: 29. Na kauli ya Mtume S.A.W: “Hakuna kujidhuru wala kudhuru”. Kwa maandiko haya Wanachuoni wa Sharia wameeleza kuwa mwenye kuhalalisha damu yake kwa mwingine akasema kumwambia: Niuwe, ni kuwa haifai kumuuwa, ikiwa atafanya basi anakuwa ni mwenye kuhusika na kustahiki adhabu.
Kutokakana na maelezo hayo Jopo limefikia maamuzi kuwa mchezo huu wa mieleka haifai kuitwa mchezo wa nguvu wala haufai kuchezwa kwa sababu maana na uelewa wa mchezo unasimama kwa msingi wa mazoezi pasina kuleta maudhi na madhara, unapaswa kufutwa katika vipindi vya michezo ya ndani na kushiriki kwenye mchezo huo kwenye mechi za kimataifa, kama vile Baraza limepitisha kuwa haifai kuoneshwa kwenye vipindi vya runinga, lengo ni kutojifunza watoto wadogo vitendo hivi vibaya na kujizoesha kuiga.
La Pili: Mieleka huru: Mieleka huru ambayo unaruhusu kwa wachezaji kufanya maudhi kwa mwingine pamoja na kumdhuru, hivyo Baraza linaona kuna vitendo vinavyofanana sana na mchezo wa bondia uliotajwa pamoja na kutafautiana sura yake, kwa sababu tahadhari zote za Kisharia ambazo zimeelezewa katika mchezo wa bondia zipo katika mchezo wa mieleka huru ambayo huchezwa kwa njia ya wazi, na kuchukua hukumu yake katika uharamu.
Ama aina zingine za mieleka ambayo huchezwa kama mchezo wa mazoezi ya mwili bila ya kuhalalishwa maudhi michezo hiyo inafaa Kisharia, wala Baraza halioni uwepo wa kizuizi. Maamuzi ya Baraza la Fiqhi ya Kiislamu la Makka kwenye kikao chake cha kwanza mpaka cha kumi na saba, maamuzi ya kikao cha kwanza mpaka cha mia na mbili mwaka 1398 – 1424H/ 1977 – 2004 ukurasa wa 216, 217.
Na kwa maamuzi hayo: Ni kuwa ikiwa mieleka huru inakusanya sehemu ya tahadhari za Kisharia kwa sura tuliyoitaja basi haifai kuihudhuria na kuiangalia moja kwa moja, kama vile haifai kuitazama kupitia runinga ikiwa sehemu kubwa inaaminika kuleta uharibifu, kama vile hupelekea kuangalia mchezo huu wa nguvu kuenea kwa utamaduni wa matumizi ya nguvu kwenye mwili wa mwanadamu na uthubutu wa kuleta maudhi na madhara, ikiwa kutakosekana uharibifu wote huu basi mchezo huo utakuwa ni halali.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.